778 Unaweza Kumshuhudia Mungu Mbele ya Joka Kubwa Jekundu?

1 Mimi hufurahia kuwatazama ndege wadogo wakipaa angani. Ingawa hawajaweka azimio lao mbele Yangu, na hawana maneno ya “kunipa” Mimi, wanapata raha katika ulimwengu ambao Nimewapa. Mwanadamu, hata hivyo, haliwezi hili, na uso wake umejaa huzuni—yawezekana kwamba Nina deni lake lisiloweza kulipwa? Kwa nini uso wake daima una michirizi ya machozi? Mimi hustaajabia mayungiyungi yanayochanuka vilimani. Maua na nyasi zinanyooka toka upande mmoja hadi upande mwingine wa miteremko, lakini mayungiyungi yanaongeza mng’aro kwa utukufu Wangu duniani kabla ya kufika kwa majira ya kuchipua—je, mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki? Je, angeweza kunishuhudia duniani kabla ya kurudi Kwangu? Je, angeweza kujitolea kwa ajili ya jina Langu katika nchi ya joka kubwa jekundu?

2 Kazi Yangu kati ya kundi la watu wa siku za mwisho ni shughuli iliyo ya pekee, na hivyo, ili utukufu Wangu uweze kujaza ulimwengu, watu wote wanapitia taabu ya mwisho kwa ajili Yangu Mimi. Je unaelewa mapenzi Yangu? Haya ndiyo matakwa ya mwisho ambayo Nataka kutoka kwa mwanadamu, ambalo ni kusema, Natumai kwamba watu wote wanaweza kutoa ushuhuda wenye nguvu, unaovuma Kwangu mbele ya joka kubwa jekundu, kwamba waweze kujitolea wenyewe Kwangu kwa mara ya mwisho, na kutimiza matakwa Yangu kwa mara nyingine ya mwisho. Je, nyinyi mnaweza kufanya hili kweli? Nyinyi hamkuweza kuuridhisha moyo Wangu katika siku zilizopita—je, mnaweza kuvunja mpangilio huu katika mara ya mwisho? Nawapata watu fursa ya kutafakari, Nawaacha watafakari kwa makini kabla ya kunipa jibu hatimaye. Je, nyinyi mna imani ya kutimiza matakwa Yangu?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 34” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 777 Mungu Huamua Mwisho wa Wanadamu Kutegemeza kwaKama Wanamiliki Ukweli

Inayofuata: 779 Unapaswa Kuyaelewa Mapenzi ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki