42. Dhoruba ya Talaka Yazimwa

Na Lu Xi, Japani

Mnamo mwaka wa 2015, rafiki yangu alinishawishi nianze kumwamini Mwenyezi Mungu. Baada ya kupokea kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, nilikula neno la Mungu kwa shauku, na kwa njia hiyo nikaja kuelewa siri nyingi za ukweli ambazo sikuzijua hapo awali, kama vile: Kazi ya Mungu ya kuokoa wanadamu imegawanywa katika hatua tatu, jinsi ambavyo Mungu hufanya kazi Yake katika kila hatua, uhusiano kati ya hatua tatu za kazi, kupata mwili ni nini, na kwa nini Mungu lazima awe mwili. Hii ilinifanya niwe na hakika zaidi kwamba Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi. Kwa kuwa nilikuwa na mwongozo wa maneno ya Mungu, sikutumia tena muda kutazama runinga kama nilivyofanya hapo zamani, na mume wangu akaniambia: “Imani yako katika Mungu imekufanya usome, hiyo ni bora kuliko kutazama opera za Korea kila siku. Jambo hilo hunifurahisha sana.” Ingawa mume wangu hakuhudhuria mikutano, aliamini siku zote kuwa kuna Mungu kwani mama yake alikuwa muumini—pia aliunga mkono imani yangu katika Mungu. Kwa kawaida, kila nilipopata nuru ya aina fulani kutoka kwa neno la Mungu ningeishiriki na mume wangu, na pia aliidhinisha kuwa na imani. Baadaye, mume wangu alitaka kujua ni kwa nini nilikuwa nikimtaja “Mwenyezi Mungu” wakati ni Bwana Yesu ambaye mama yake alimwamini, na kwa hivyo alienda mtandaoni kutafiti kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu. Lakini bila kutarajia, alichokiona ni kwamba mtandao ulijaa uvumi, ushuhuda wa uwongo na kufuru kwa Mwenyezi Mungu. Alitiwa sumu sana na haya na akaanza kupinga imani yangu katika Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa nilikuwa nimesoma neno la Mwenyezi Mungu na kusikia ushirika na ushuhuda wa kina ndugu, tayari nilikuwa na hakika moyoni mwangu kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli, na nilijua kuwa mambo hayo ambayo yalikuwa mtandaoni yalikuwa uvumi na uwongo tu uliokusudiwa kuwadanganya watu. Hata hivyo, mume wangu alidanganywa na uvumi huo na akashindwa kuelewa hali halisi ya hali hiyo, bila kujali nilivyojaribu kumshawishi na kumpa ushuhuda juu ya kazi ya Mungu katika siku za mwisho, hakuweza kusikiliza.

Baada ya kipindi fulani cha muda, kwa msaada wa Dada Yinghe, ambaye alishiriki tena na tena ushirika na ushuhuda na mume wangu, mwishowe alikubali kuchunguza kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Hata hivyo, mume wangu alishawishiwa na mama yake na alikuwa mwenye kushikilia Bibilia kwa kiasi, kwa hivyo ili kutatua hili tatizo lake, dada wengine walipendekeza kwamba nitazame filamu ya kiinjili iitwayo Fichua Siri Kuhusu Biblia na mume wangu. Hata hivyo, sikumtaka afanye hivyo. Badala yake, nilichukua hatua mimi mwenyewe na nikamtaka atazame filamu iitwayo Kupita Katika Mtego, ambayo inafichua jinsi serikali ya CCP na wapinga Kristo wa ulimwengu wa dini wanavyopinga kazi ya Mungu. Baada ya kuona sehemu fulani tu ya filamu, alisema: “CCP ni serikali ya kukana Mungu, na China ni nchi ya kukana Mungu ambayo imekuwa ikiwatesa waumini kila wakati. Kanisa la Mwenyezi Mungu linachukuliwa hatua kali na serikali ya CCP, na sisi ni mkono tu, ambao hauwezi kushindana na mguu. Itakuwa vipi tukirudi China na kukamatwa? Aidha, mambo ya kila aina yanasemwa mtandaoni, na siwezi kung’amua kilicho kweli na kilicho uongo. Bado nafikiri hufai kuamini katika hili.” Nilimhimiza mume wangu amalizie kutazama filamu hiyo kisha afanye uamuzi wake, lakini hakufanya hivyo. Alipoona kwamba nilisisitiza kuendeleza imani yangu, wakati mmoja alinishambulia kwa hasira, akisema: “Ikiwa unasisitiza juu ya kuamini basi amini, ikiwa unataka kukamatwa basi kamatwa. Lakini ukikamatwa, usiseme kwamba mimi ni mume wako! Hujui kuwa hivi sasa niko chini ya shinikizo kubwa? Nisipoamini, ninaogopa huyu ndiye Mungu wa kweli, lakini nikiamini, kuna mambo hayo yote mtandaoni na nitakuwa katika hatari ya kukamatwa. Kwa hivyo napaswa kumsikiliza nani kwa kweli?” Nilipoona mateso ya mume wangu kutokana na kuzuiwa na uvumi huo uliokuwa mtandaoni, niligundua jinsi uvumi na ushuhuda wa uwongo uliobuniwa na CCP ulivyo wa kudhuru kwa kweli. Sio tu kwamba unazuia watu kukubali njia ya kweli, lakini pia huharibu uhusiano wa kifamilia. Inavyoonekana, watu hawa wanaobuni uvumi na kutoa ushuhuda wa uwongo ni watoto wa ibilisi Shetani, kabisa!

Siku moja, mume wangu alifika nyumbani kutoka kazini na akaona kwamba nilikuwa mkutanoni. Alionyesha huzuni mara moja, kisha akafungua mlango kwa kishindo na kuondoka. Wakati wa chakula cha jioni uliwadia na kupita, lakini bado sikuwa nimemwona akirudi—sikuwa na budi kuanza kuwa na wasiwasi. Mwishowe alirudi nyumbani saa mbili lakini bado alikuwa amekasirika. Nilikuwa nimepanga kumwandalia chakula, lakini akaniambia kwa dharau: “Usijisumbue! Kwa kuwa hunisikizi na unaendeleza imani yako, kuanzia sasa na kuendelea usiingilie mambo yangu. Kuanzia sasa na kuendelea nitawajibika tu gharama zetu za maisha, na chochote nitakachofanya nje ya nyumba hii hakikuhusu! Hata ikiwa nitafanya chochote ambacho kinaweza kusikitisha familia hii, bado hakikuhusu!” Niliposikia haya kutoka kwa mume wangu, nilizidi kufadhaika na nilifikiria zaidi juu ya jambo hilo. Usiku huo niligaagaa na kugeuka kitandani, nisiweze kulala, nikimwomba Mungu kila wakati moyoni mwangu: “Ee Mungu! Mume wangu amedanganywa na uvumi na anajaribu kuzuia imani yangu Kwako, na anasema mambo yasiyo na huruma. Nifanye nini? Tafadhali nionyeshe njia! Sitaki kukuacha.” Asubuhi iliyofuata, nilikumbuka ghafla maneno kadhaa ya Mungu ambayo tulishiriki kuyahusu kwenye mkutano: “Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita. … Wakati Mungu na Shetani wanapigana katika milki ya kiroho, utamridhishaje Mungu, na utasimamaje imara katika ushuhuda wako Kwake? Unapaswa kujua kuwa kila kitu unachokipitia ni majaribu makubwa na ndipo Mungu hukuhitaji kuwa na ushuhuda(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli). Kupitia nuru ya neno la Mungu nilizinduliwa kwa kiasi fulani: Wakati huu nilikuwa nikimtazama mume wangu kila mara, na kuhisi kama kwamba kulikuwa ulaghai na hila nyingi ulimwenguni siku hizi, kwamba kulijaa uwongo na udanganyifu kila mahali. Hasa kwa sababu ya uwongo na taarifa zote za uwongo zilizotoka kwa vyombo vya habari vya CCP. Nilidhani kwamba mtu yeyote aliye na akili kidogo angeweza kufikiria kidogo na kugundua kuwa maneno haya ya matandaoni yanayomshambulia, kuhukumu na kumlaani Mwenyezi Mungu ni uwongo na upumbavu, kwamba hafai kudanganywa na kukanganywa nao. Lakini kwa bahati mbaya, mume wangu aliamini uvumi aliosikia mtandaoni, na nilihisi kweli kwamba hakufaa kufanya hivyo. Wakati huo singetafuta sababu kuu nje. Ni Mungu aliyekuwa akinijaribu, Akitumia hali hii kujaribu kuona kama imani yangu Kwake ni ya kweli, kuona ikiwa ninaweza kushikilia njia ya kweli kwa uthabiti huku nikishambuliwa na Shetani, na ikiwa ninaweza kutoa ushuhuda kwa Mungu huku nikiwa katikati ya jaribio hili au la. Nilipogundua mapenzi ya Mungu, ukungu uliokuwa umefunika moyo na akili yangu uliondoka, na moyo wangu ukachangamka kidogo.

Siku iliyofuata tulipokuwa tukila kiamsha kinywa, mume wangu alikuwa bado alionekana kusononeka na hakuzungumza nami, lakini kwa kuwa nilikuwa na mwongozo wa maneno ya Mungu, sikuwa na wasiwasi wala hofu kama siku iliyopita. Nilimwambia kwa utulivu: “Naamini katika Mungu na sijawahi kufanya kitu chochote kusikitisha familia hii. Ikiwa unataka kufanya hivyo, basi ni wewe uko radhi kuwa mpotovu, si kwa sababu ya imani yangu katika Mungu.” Mume wangu aliposikia nikisema hivi, aligeuza sauti ikawa laini, akasema: “Si nilisema mambo hayo kwa sababu hukunisikiliza na uliendelea kuendeleza imani yako?” Baadaye hakusema lolote lingine, na dhoruba ikapita. Shukrani kwa Mungu! Ni maneno ya Mungu ambayo yalinipa nguvu ya kushinda majaribu ya Shetani!

Lakini jambo zuri halidumu milele. Mwezi mmoja baadaye mume wangu alikuwa akiingia tena mtandaoni na kusoma uvumi huo. Siku moja aliporudi nyumbani kutoka kazini aliona kwamba nilikuwa nimekaa kwenye kompyuta, ana akaanza kunisemea kwa sauti kubwa: “Nadhani umerukwa na akili! Nimefikiria tena: Uache imani yako mara moja au tutengue ndoa. Nimefikiria pia juu ya suala la watoto wetu wawili; unaweza kuwachukua wote wawili, lakini nakisia kwamba hutaweza kukaa Japani, kwa hivyo warudishe watoto wetu huko Shanghai! Nitakupa chumba chetu huko Shanghai, na kila mwezi nitakupa yeni 100,000 ya kuwasaidia wa watoto. Na ikiwa huwataki watoto basi hiyo ni sawa pia, chochote utakachochagua! Hata nimechunguza kesi za talaka. Tunachohitaji kufanya ni kwenda kwenye ofisi ya wadi na kutia saini mapatano ya talaka, basi niambie tu msimamo wako!” Baada ya kumsikia akisema hayo yote, moyo wangu ulikuwa ukipiga kwa nguvu na nilihisi kama kichwa changu kilikuwa kimejaa. Nilikaa tu hapo nikashindwa kusema chochote, na hata nilisahau kuomba kwa Mungu. Nilichoweza kufikiria tu ni, tukitengua ndoa, itakuwa vipi kwa watoto? Wangenifuata, lakini sikuwa na pesa! Kama hawangenifuata, ingesikitisha sana kama hawangekuwa na mama! Na kisha kulikuwa na wazazi wangu, marafiki na jamaa wengine, wangefikiria nini juu yangu? Kuwa ughaibuni kulikuwa jambo zuri kiasili, lakini tukitengua ndoa basi wazazi wangu wangewezaje kupata heshima yao mbele ya wengine…. Kwa hivyo, sikumpa majibu mume wangu; nilimwambia tu kwamba lazima nifikirie. Nilikwenda chumbani kwangu na kuanza kulia sana. Kadiri nilivyozidi kufikiri juu ya maisha yangu baada ya talaka ndivyo nilivyozidi kuhisi maumivu. Sikulala kabisa usiku huo, na machozi yangu yalilowesha foronya yangu. Siku iliyofuata, mume wangu aliondoka kwenda kazini bila kusema neno, na wakati huo tu ndipo nikaja mbele ya Mungu katika ombi, nikimwomba Anipe nguvu zaidi ili niweze kushinda udhaifu wa mwili. Kwa kuwa nilipata matatizo na shida na sikujua la kufanya, niliwaambia ndugu wengine juu ya kile kilichotokea. Wote walinitia moyo na kunifariji, wakisema kwamba hili lilikuwa moja ya majaribu ya Shetani ambalo nilikuwa nikipitia, na wakanisaidia kujifunza jinsi ya kumtegemea Mungu. Walisema singepoteza imani yangu au kumuelewa Mungu visivyo. Walishiriki pia uzoefu na ushuhuda wa ndugu wengine na mimi, na kushiriki juu ya jinsi ambavyo Mungu ndiye anayewaokoa wanadamu, kwamba Shetani pekee ndiye hutuumiza, kutufanya tuteseke, na kuharibu uhusiano wetu na watu wengine. Walinisomea pia kifungu kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu: “Wakati watu bado hawajaokolewa, maisha yao mara nyingi yanaingiliwa kati na hata kudhibitiwa na, Shetani. Kwa maneno mengine, watu ambao hawajaokolewa ni wafungwa wa Shetani, hawana uhuru, hawajaachiliwa na Shetani, hawajafuzu wala kustahili kumwabudu Mungu, na wanafuatiliwa kwa karibu na kushambuliwa kwa ukali na Shetani. Watu kama hawa hawana furaha ya kuzungumzia, hawana haki ya uwepo wa kawaida wa kuzungumzia, na zaidi hawana heshima ya kuzungumzia. Ni pale tu unaposimama imara na kupigana na Shetani, kwa kutumia imani yako katika Mungu na utiifu kwake, pamoja na kumcha Mungu kama silaha ambazo utatumia kupigana vita vya maisha na mauti dhidi ya Shetani, kiasi cha kwamba utamshinda kabisa Shetani na kumsababisha kukata tamaa na kuwa mwoga kila anapokuona wewe, ili aache kabisa mashambulizi na mashtaka yake dhidi yako—hapo tu ndipo utakapookolewa na kuwa huru(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II). Neno la Mungu lilinifanya nigundue kuwa kila wakati ambapo sikutenda imani yangu katika Mungu, nilikuwa nikitawaliwa kabisa na Shetani, kwamba nilikuwa mtumwa na kitu cha Shetani cha kuchezea. Baada ya kupata imani yangu, nilitoka nje ya kambi ya Shetani na nikarudi mbele ya uwepo wa Mungu; kwa sababu nilimwacha Shetani, hakuwa tayari kushindwa, kwa hivyo alimtumia mume wangu kushambulia udhaifu wangu. Alitumia talaka kunilazimisha nimsaliti Mungu na kurudi kwenye utawala wake. Kwa kweli huu ulikuwa ujanja wa Shetani. Nilikuwa na wasiwasi juu ya kuwamudu watoto baada ya talaka, jinsi ambavyo watu kutoka makazi yangu ya kudumu wangenifikiria, na jinsi ambavyo wazazi wangu wangepata heshima mbele ya majirani zao. Mawazo haya yote yalitokana na vurugu ya Shetani, na kama ningedhibitiwa na mawazo haya basi ningedhibitiwa na Shetani, mwishowe yangenipelekea kujitenga na Mungu au hata kumkataa, na kurudi tena kwenye kambi ya Shetani. Imani yangu na ibada yangu kwa Muumba ni mambo ya kusaidia kabisa, ni sheria ya mbinguni na kanuni ya dunia, na hakuna mwanadamu aliye ana haki ya kuyaingilia, lakini Shetani hujaribu kila kitu ili kunidhibiti, kunisukuma mimi kumsaliti Mungu. Kwa kweli Shetani ni mwenye kustahili dharau na mwenye chuki sana! Wakati huo, nilijua kwamba sikuwa na imani ya kukabiliana na majaribu ya Shetani peke yangu, lakini nilikuwa tayari kumtegemea Mungu na kutegemea mwongozo wa neno la Mungu ili kuchukua njia iliyokuwa mbele yangu, na niliazimia kusimama upande wa Mungu na kumshuhudia Mungu; singesalimu amri kwa shetani asilani. Haya yaliponijia akilini, moyo wangu uliokuwa na wahaka ulipata nafasi ya hakika na mateso yangu yalipungua.

Baadaye, ndugu wengine walishiriki tena neno la Mungu nami: “Bila ruhusa ya Mungu, ni vigumu sana kwa Shetani kugusa hata tone la maji au chembechembe ya mchanga kwenye ardhi; bila ruhusa ya Mungu, Shetani hana hata hiari ya kusongea mchwa wanaojiendea zao kwenye ardhi, sikwambii hata mwanadamu, aliyeumbwa na Mungu. Kwenye macho ya Mungu, Shetani ni duni zaidi ya yungiyungi kwenye mlima, hadi kwenye ndege wanaopaa hewani, hadi kwenye samaki walio baharini, hadi kwenye funza kwenye juu ya nchi. Wajibu wake miongoni mwa viumbe vyote ni kuhudumia viumbe vyote, na kufanyia kazi mwanadamu, na kuhudumia kazi ya Mungu na mpango Wake wa usimamizi. Licha ya vile anavyoonea wenzake kijicho katika asili yake, na vile ambavyo hali yake halisi ya maovu ilivyo, kitu ambacho Shetani anaweza kufanya tu ni kuweza kukubaliana kwa wajibu kuhusiana na kazi yake: kuwa mwenye huduma kwa Mungu, na kuwa mjalizo kwa Mungu. Hiki ndicho kiini na nafasi ya Shetani. Hali yake halisi haijaungana na maisha, haijaungana na nguvu, haijaungana na mamlaka; ni kitu cha kuchezea tu kwenye mikono ya Mungu, mtambo tu kwenye huduma ya Mungu!(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I). Kutoka kwa neno la Mungu nilikuja kugundua kuwa mamlaka ya Mungu ni ya juu, Mungu hutawala mbingu na dunia na vitu vyote, na kila kitu chetu kiko mikononi Mwake. Talaka yangu na familia yangu pia ziko mikononi mwa Mungu, na bila idhini ya Mungu hakuna kitu ambacho Shetani anaweza kufanya. Ikiwa ningepata talaka au la ilikuwa chini ya ukuu na utabiri wa Mungu—haikuwa mume wangu ambaye alikuwa na mwisho wa kusema, kwa hivyo nilikuwa tayari kujisalimisha kwa ukuu na mipango ya Mungu. Nilifikiri juu ya makafiri ambao hupata talaka. Wengine hufanya hivyo kwa ajili ya pesa, wengine hufanya hivyo kwa sababu wenzi wao wana uhusiano nje ya ndoa, na wengine hufanya kwa sababu uhusiano wao unavunjika tu…. Mume wangu alitaka kunitaliki kwa sababu nilichagua kuamini katika Mungu na kuchukua njia sahihi ya maisha, kufuatilia ukweli na kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Hili ni jambo la heshima, si la aibu! Wakati huo huo nilikumbuka maneno haya kutoka kwa Mungu: “Imani ni kama daraja moja la gogo la mti, wale ambao hushikilia maisha kwa unyonge watakuwa na ugumu katika kulivuka, lakini wale ambao wako tayari kujitolea wenyewe wanaweza kulivuka bila wasiwasi. Kama mtu ana mawazo ya uoga na ya kuogofya, wao wanadanganywa na Shetani. Ina hofu kwamba tutavuka daraja la imani ili kuingia katika Mungu. Shetani hubuni kila njia iwezekanayo kututumia mawazo yake, tunapaswa daima kuomba kwamba nuru ya Mungu itatuangazia sisi, na ni lazima daima tumtumainie Mungu kututakasa kutoka kwa sumu ya shetani. Daima tutakuwa tukitenda katika roho zetu kuja karibu na Mungu. Tutamruhusu Mungu kuwa na utawala juu ya asili yetu yote(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 6). Maneno ya Mungu kwa mara nyingine yalinipa imani na nguvu, njia ya kufuata, na pia ujasiri wa kumkabili mume wangu. Hiyo ni kweli—kitu pekee ambacho ningeweza kufanya ni kutahadhari. Bila kujali kile ambacho njia yangu ya mustakabali ingekuwa nacho, hakuwezi kuwa na makosa katika kuchukua njia ya imani!

Baada ya mume wangu kurudi nyumbani jioni hiyo, nilimwambia waziwazi: “Hutaki nimwamini Mwenyezi Mungu, lakini kwangu jambo hilo haliwezekani. Kama unataka kutaliki basi tutaifanya kwa njia yako!” Mume wangu alipigwa na bumbuwazi kidogo baada ya kusikia haya, na akawa bila chaguo lingine, alisema: “Inavyoonekana siwezi kukudhibiti tena! Kuna kila aina ya vitu mtandaoni—nisipokudhibiti, basi siku moja kitu kikitokea kwako nitakiwajibikia. Natumia talaka hii kama njia ya kukutishia tu, lakini bado huachi imani yako katika Mungu. Kitu kikikufika kwa sababu ya imani yako, mama yako atajua, kwa hivyo usinilaumu.” Kuanzia wakati huo, hakujali tena juu ya imani yangu katik Mungu; uhusiano wetu ulipata afueni kimuujiza na hakuzungumza tena juu ya kutaliki. Hivi ndivyo dhoruba ya talaka iliyosababishwa na uvumi wa CCP ulivyozimwa.

Baadaye kuna wakati mmoja ambapo mimi na binti yangu mdogo tulishikwa na mafua. Wakati huo kulikuwa kunanyesha kidogo, lakini binti yangu mkubwa alihitaji kwenda kufanya mazoezi, kwa hivyo sikuwa na budi kumpeleka, huku nikivuta mwili wangu uliokuwa umechoka pamoja na binti yangu mdogo. Baada ya mume wangu kupata juu ya haya, alisema: “Umefanya kazi kwa bidii leo. Lu Xi, nimeyaona mabadiliko kwako hivi karibuni. Umekuwa mwenye upendo zaidi kwa watoto na mwenye bidii sana.” Niliposikia maneno haya kutoka kwa mume wangu, nilimshukuru Mwenyezi Mungu ndani ya moyo wangu kwa sababu nilijua kuwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo yalikuwa yamenibadilisha. Nikiwa na maneno ya Mungu kama msingi wangu, nina mwelekeo maishani mwangu, najua ubinadamu sahihi ni nini na tabia potovu ni nini. Unaweza kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu sahihi kwa kuishi tu kulingana na neno la Mungu. Kwa hivyo, siruhusu tena hasira yangu ilipuke kwa watoto wangu bila kufikiria, na tena siishi maisha kwa ajili tu ya starehe. Polepole, nilikuja kugundua kuwa mume wangu pia alikuwa amebadilika. Hapo zamani alikuwa daima akihisi kuwa yeye ndiye aliyekuwa sahihi, lakini sasa anaposhughulikia maswala mengine yeye huomba maoni yangu. Hata amewapa marafiki wake ushuhuda wa mamlaka na ukuu wa Mungu. Ninapoona mambo haya, moyo wangu unajaa shukrani. Ee Mungu, Wewe ni mwenye uweza kwa kweli! Maneno Yako ni nishati yetu ya uhai, na bila kujali jinsi nguvu ya Shetani ilivyo ya shari au ya hasira, mradi tuwe na maneno Yako ya kutuongoza tutaweza kushinda majaribu yote ya Shetani, na kuishi kwa amani chini ya utunzaji na ulinzi Wako.

Namshukuru Mungu kwa kunipangia haya yote, na kwa kuniruhusu nipitie neno Lake na kuelewa ukweli mwingi. Kwa sababu ya kupitia aina hizi za hali nimeona kuwa kwa kweli Shetani ni mwenye kustahili dharau, kwamba anafikiria kila njia inayowezekana ya kuwafanya watu wamwache Mungu na kuwa mawindo yake ili awale. Wakati huo huo nimeona pia kwamba Mungu hutawala vitu vyote na hupanga kila kitu; bila ruhusa ya Mungu, haijalishi Shetani atakavyozidi kuwa na hasira. Hataweza kufanya chochote, hataweza kukamilisha kitu chochote—hataweza hata kugusa unywele mmoja kwenye vichwa vyetu. Mradi tuwe na imani, na kutegemea neno la Mungu kuishi, basi tutaweza kushinda ushawishi mwovu wa Shetani, tumeshuhudia Mungu na kumletea Mungu utukufu! Ukweli pia unathibitisha kuwa uvumi na ushuhuda wa uwongo ambao upo mtandaoni hauwezi kuthibitika. Ukweli na wakati vitathibitisha kila kitu, na mwishowe uvumi huu utakumbukwa katika historia kwa aibu ya milele, kama tu vile “Ukanaji Mungu,” “Nadharia ya Darwin ya mageuzi” na “Ukomunisti.” Utakuwa alama ya aibu ya milele kwa CCP. Kondoo wa Mungu wataisikia sauti ya Mungu, bila kujali vizuizi vya Shetani ni vikubwa kiasi gani, wale wote ambao wanamwamini Mungu kwa kweli na wanapenda ukweli, wataweza kuacha udanganyifu na vifungo vya uvumi, kuja mbele za Mungu na kupatwa na Mungu. Hii ni kwa sababu hili ni jambo ambalo Mungu anataka kulitimiza—hakuna nguvu za Shetani zinazoweza kuzuia!

Iliyotangulia: 41. Kesi ya Zhaoyuan ya Mnamo Mei 28 Lasababisha Upeo wa Tatizo la Familia

Inayofuata: 43. Kupotea na Kurejea Tena

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

9. Upendo wa Aina Tofauti

Na Chengxin, BrazilNafasi ya bahati mnamo mwaka wa 2011 iliniruhusu nije Brazili kutoka China. Nilipokuwa nimewasili tu, nilizidiwa na...

12. Fumbo la Utatu Linafichuliwa

Na Jingmo, MalaysiaNilikuwa na bahati katika mwaka wa 1997 kukubali injili ya Bwana Yesu na nilipobatizwa, mchungaji aliomba na kunibatiza...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp