152 Wimbo wa Upendo Mtamu

1

Upendo Wako umefichwa moyoni mwangu,

unaniongoza kuwa karibu na Wewe kwa upendo.

Kwa kuufikiria moyo Wako moyo wangu unakuwa mtamu zaidi,

nakutumikia kwa moyo na akili zangu zote.

Maneno Yako yanauongoza moyo wangu, na hatua zangu za upendo zinakufuata kwa karibu.

Nitatenda kulingana na mapenzi Yako, kukuridhisha kunaufurahisha moyo wangu.

Sasa naishi katika ulimwengu mwingine,

Wewe na mimi tu pamoja.

Hakuna wasiwasi, hakuna kumbukumbu ya uchungu.

Maneno Yako yatakasa upotovu wangu,

na yameujaza moyo wangu.

Nakupenda, ee, nakupenda,

Maneno Yako yamekuwa maisha yangu.

Nina bahati sana kukamilishwa na Wewe

na nitakupenda na kukushuhudia Wewe milele.

Haleluya! Haleluya!

Haleluya! Sifa ziwe kwa Mungu!

2

Kwa upendo tunakwenda pamoja pasiwe na chochote cha kututenganisha, mioyo yetu yote ina furaha.

Naelewa mapenzi Yako na kukutii kabisa,

sitaki kamwe tena kuasi hata kidogo. Nitaishi mbele Yako hata zaidi, nami sitatenganishwa nawe kamwe.

Natafakari kwa kimya juu ya maneno Yako, nathamini kile Ulicho nacho na ulicho.

Maneno Yako yatakasa upotovu wangu,

na yameujaza moyo wangu.

Nakupenda, ee, nakupenda,

Maneno Yako yamekuwa maisha yangu.

Nina bahati sana kukamilishwa na Wewe

na nitakupenda na kukushuhudia Wewe milele.

Haleluya! Haleluya!

Haleluya! Sifa ziwe kwa Mungu!

Haleluya! Haleluya!

Haleluya! Sifa ziwe kwa Mungu!

Iliyotangulia: 151 Kukusanyika katika Sayuni

Inayofuata: 153 Furaha Yetu kwa Wokovu wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp