889 Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

1 Tangu Yeye amuumbe mwanadamu, Yeye anamwongoza; kwa sababu Yeye humwokoa mwanadamu, atamwokoa mwanadamu kwelikweli, na atampata kikamilifu; kwa kuwa Yeye humwongoza mwanadamu, atamleta kwenye hatima inayofaa; na kwa kuwa Yeye alimuumba mwanadamu na humsimamia mwanadamu, ni sharti Achukue jukumu la hatima ya mwanadamu na matarajio yake. Ni hii ndio kazi ambayo hufanywa na Muumba. Ingawa kazi ya ushindi inatimizwa kwa kutakasa matarajio ya mwanadamu, hatimaye ni lazima mwanadamu aletwe kwenye hatima ifaayo aliyotengenezewa na Mungu kwa ajili yake. Ni kwa sababu hasa kuwa Mungu hufanya kazi katika mwanadamu ndiyo maana mwanadamu ana hatima na hatima yake ni ya uhakika.

2 Kitu ambacho mwanadamu hutumainia na kufuata ni tamaa za harakati ya hamu ya kimwili iliyo badhirifu, badala ya hatima ya mwanadamu anayotazamiwa. Kile ambacho Mungu amemwandalia mwanadamu, wakati huo huo, ni baraka na ahadi alizoandaliwa mwanadamu mara baada ya kutakaswa, ambayo Mungu alimtayarishia mwanadamu baada ya kuumba ulimwengu, na ambayo haitiwi doa na uchaguzi, dhana, mawazo au mwili wa mwanadamu. Hatima hii haitayarishwi kwa ajili ya mtu fulani, lakini ni mahali pa kupumzikia pa wanadamu wote. Na kwa hivyo, hii hatima ni hatima inayofaa zaidi kwa wanadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 888 Upendo wa Mungu kwa Wanadamu Hauna Mipaka

Inayofuata: 890 Kiini cha Kristo ni Upendo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp