824 Akili Anayopaswa Kuwa Nayo Mwanadamu Baada ya Kushindwa

1 Baada ya wanadamu kushindwa na Mungu, sifa ya msingi ya mantiki wanayopaswa kuwa nayo ni kuhakikisha kuwa wasizungumze kwa kiburi. Wanapaswa kuwa na hadhi ya chini, “kama samadi ardhini,” na kunena ukweli fulani; hii itakuwa bora kabisa. Hasa wakati wa kuwa na ushuhuda wa Mungu, ukiweza kusema jambo kutoka moyoni, bila maneno matupu au majivuno na bila uwongo wa kubuni, basi tabia yako itakuwa imebadilika, na haya ndiyo mabadiliko yanayopaswa kutokea mara unaposhindwa na Mungu. Usipoweza kumiliki hata idadi hii ya mantiki, basi huonekani binadamu kwa kweli. Kuanzia sasa na kuendelea, lazima utende kwa tabia nzuri kila wakati, utambue hadhi na nafasi yako, na usirudi tena katika njia zako za zamani.

2 Mfano wa Shetani unajidhihirisha bora kwa kiburi na majivuno ya binadamu. Usipobadilisha kipengele hiki kujihusu, hutawahi kuwa na mfano wa mwanadamu, na daima utakuwa na sura ya Shetani. Kuwa na maarifa tu katika eneo hili hakutatosha kupata mabadiliko kamili; bado utahitaji kuvumilia usafishaji kadhaa. Bila kushughulikiwa na kupogolewa, mwishowe, bado utakuwa hatarini. Ili kuepuka kurudia njia zako za zamani, kwanza lazima utambue kuwa tabia yako bado haijabadilika na kwamba asili yako ya kumsaliti Mungu bado imekita mizizi. Bado uko katika hatari kubwa ya kumsaliti Mungu, na unakabiliwa na uwezekano wa maangamizo kila wakati.

3 Jambo lingine ni kutowahi kuchukua nafasi ya mtu ambaye ni shahidi wa Mungu; unaweza kuzungumza tu juu ya uzoefu wa kibinafsi. Unaweza kuongea kuhusu jinsi Mungu alivyowaokoa, kushiriki juu ya jinsi mlivyoshindwa na Mungu, na kuongea juu ya neema Aliyowapa. Msisahau kamwe kuwa ninyi ndio watu waliopotoshwa zaidi, na ni kupitia kwa Mungu tu ndipo mmeinuliwa. Kwa sababu ninyi ndio mliopotoshwa zaidi na wachafu zaidi, mmeokolewa na Mungu mwenye mwili, naye Amewapa neema kubwa mno. Kwa hivyo hamna chochote cha kujivunia, na mnaweza tu kumsifu na kumshukuru Mungu. Wokovu wenu ni kwa sababu ya neema ya Mungu tu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 823 Ni Kwa Kujua Matendo ya Mungu Tu Ndiyo Mtu Anaweza Kumshuhudia Kweli

Inayofuata: 825 Mungu Amsihi Mwanadamu Amshuhudie Tu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp