B. Maneno Juu ya Kukifichua Asili ya Shetani ya Wanadamu Wapotovu na Kiini na Asili Yao

81. Chanzo cha upinzani wa mwanadamu na uasi dhidi ya Mungu ni kupotoshwa kwake na Shetani. Kwa sababu amepotoshwa na Shetani, dhamiri ya mwanadamu imekuwa bila hisia, yeye ni mwovu, mawazo yake yamepotoka, na ana mtazamo duni. Kabla ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu kawaida alimfuata Mungu na alitii maneno Yake baada ya kuyasikia. Alikuwa kawaida mwenye akili timamu na dhamiri, na wa ubinadamu wa kawaida. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hali yake ya awali, dhamiri, na ubinadamu vilidhoofika sana na viliharibiwa na shetani. Hivyo, yeye amepoteza utii wake na upendo kwa Mungu. Akili ya mwanadamu imekuwa potovu, tabia yake imekuwa sawa na ile ya mnyama, na uasi wake kwa Mungu kabisa umekuwa wa mara kwa mara na wa kuhuzunisha zaidi. Hata hivyo mwanadamu bado hajui wala kutambua hili, na kwa upofu anapinga na kuasi. Ufunuo wa tabia ya mwanadamu ni udhihirisho wa hisia zake, utambuzi na dhamiri, na kwa sababu hisia yake na utambuzi si timamu, na dhamiri yake imezidi kuwa ndogo zaidi, hivyo tabia yake ni ya uasi dhidi ya Mungu. Kama hisia ya mwanadamu na utambuzi hauwezi kubadilika, basi mabadiliko katika tabia yake hayawezekani, sawa na kuwa baada ya moyo wa Mungu. Kama hisia ya mwanadamu sio timamu, basi hawezi kumhudumia Mungu na hafai kutumiwa na Mungu. “Hisia za Kawaida” inaashiria kutii na kuwa mwaminifu kwa Mungu, kuwa mwenye imani kamili kwa Mungu, na kwa kuwa na dhamiri kwa Mungu. Inamaanisha kuwa na moyo mmoja na akili kwa Mungu, na si kwa kumpinga Mungu kwa makusudi. Wale ambao ni wa akili potovu hawako hivi. Tangu mwanadamu aharibiwe na Shetani, ametunga dhana kuhusu Mungu, na yeye hajakuwa na uaminifu au kumtamani Mungu, pia hana dhamiri kwa Mungu. Mwanadamu kwa makusudi anapinga na huweka hukumu juu ya Mungu, na, zaidi ya hapo, anatupa shutuma Kwake nyuma Yake. Mwanadamu anajua vizuri kuwa Yeye ni Mungu, lakini bado humhukumu nyuma ya mgongo wake, hana nia ya kumtii, na hufanya madai ya kipofu na maombi kwa Mungu. Watu wa aina hii—watu walio na akili potovu—hawana uwezo wa kujua tabia zao za kudharauliwa au ya kujuta uasi wao. Kama watu wana uwezo wa kujijua wenyewe, basi wao wamerudisha kiasi kidogo cha akili zao; Zaidi ya vile watu wanavyomuasi Mungu lakini hawajui wenyewe, ndivyo walivyo zaidi wenye akili isiyo timamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

82. Baada ya miaka elfu kadhaa ya upotovu, mwanadamu amekuwa asiyehisi na mpumbavu, pepo anayempinga Mungu, kwa kiasi kwamba uasi wa mwanadamu kwa Mungu umeandikwa katika vitabu vya historia, na hata mwanadamu mwenyewe hana uwezo wa kutoa ripoti kamili ya tabia zake za uasi wake—kwa kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na amehadaiwa na Shetani kiasi kwamba hajui ni wapi pa kugeukia. Hata wa leo, mwanadamu bado anamsaliti Mungu: Wakati mwanadamu anamwona Mungu, anamsaliti, na wakati yeye hawezi kumwona Mungu, bado anamsaliti. Kuna hata wale ambao, baada ya kushuhudia laana ya Mungu na ghadhabu ya Mungu, bado wanamsaliti. Na hivyo Nasema kwamba hisia ya mwanadamu imepoteza kazi yake ya awali, na kwamba dhamiri ya mwanadamu, pia, imepoteza kazi yake ya awali. Mwanadamu Ninayemtazamia ni mnyama katika mavazi ya binadamu, yeye ni nyoka mwenye sumu, haijalishi jinsi anavyojaribu kuonekana mwenye kuhurumiwa machoni Pangu, Sitawahi kamwe kuwa na huruma kwake, kwa kuwa mwanadamu hana ufahamu wa kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe, tofauti kati ya ukweli na yasiyo ya kweli. Hisia ya mwanadamu ni usiohisi chochote, ilhali bado anataka apate baraka; ubinadamu wake si wa kuheshimika lakini bado anataka kumiliki ukuu wa mfalme. Ataweza kuwa mfalme wa nani, na hisia kama hiyo? Jinsi gani yeye na ubinadamu kama huo ataweza kukaa kwenye kiti cha enzi? Mwanadamu kwa kweli hana aibu! Yeye ni mdhalili wa kujivuna tu! Kwa wale kati yenu mnaotaka kupokea baraka, Ninawashauri kwanza mtafute kioo na kuangalia picha zenu mbaya—je, una kile kinachohitajika kuwa mfalme? Je, una uso wa mwanadamu ambaye anaweza kupata baraka? Hakujawa mabadiliko hata madogo katika tabia yako na wewe hujaweka ukweli wowote katika vitendo, ilhali bado unatamani kuona siku ifuatayo ikiwa ya ajabu. Unajihadaa mwenyewe! Kwa sababu ya kuzaliwa katika nchi ya uchafu vile, mwanadamu ameangamizwa kabisa na jamii, amekuwa akishawishiwa na maadili ya kikabaila, na amefundisha katika “taasisi za elimu ya juu.” Fikra zilizo nyuma kimaendeleo, maadili potovu, mtazamo mbaya juu ya maisha, falsafa za kudharauliwa za kuishi, uwepo usio na thamani, na hali potovu za maisha na desturi—mambo yote haya yameuingilia moyo wa mwanadamu, na kudhoofisha na kushambuliwa dhamiri yake pakubwa. Matokeo yake, mwanadamu kamwe yuko mbali kutoka kwa Mungu, na kila mara anampinga. Tabia ya mwanadamu inakuwa matata zaidi kila siku, na hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari yake atatoa chochote kwa ajili ya Mungu, hakuna hata mmoja ambaye kwa hiari atamtii Mungu, wala, zaidi ya hayo, mwanadamu mmoja ambaye kwa hiari yake atatafuta uso wa Mungu. Badala yake, chini ya umiliki wa shetani, mwanadamu hafanyi kitu ila kukimbiza anasa, kujitoa mwenyewe kwa upotovu wa mwili katika nchi ya matope. Hata wanaposikia ukweli, wale wanaoishi gizani hawafikiri kuuweka katika vitendo, na wala kuelekea kumtafuta Mungu hata kama wameuona mwonekano Wake. Jinsi gani wanadamu wapotovu kiasi hiki wawe na nafasi yoyote ya wokovu? Jinsi gani wanadamu waovu kiasi hiki kuishi katika mwanga?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

83. Chanzo cha ufunuo wa upotovu wa tabia ya mwanadamu ni dhamiri yake iliyofifia, asili yake mbovu na akili yake isiyo timamu; kama dhamiri ya mwanadamu na hisia vinaweza kurudi kawaida, basi atafaa kwa matumizi mbele ya Mungu. Ni kwa sababu tu kuwa dhamiri ya mwanadamu daima imekuwa isiyosikia, akili ya mwanadamu haijawahi kuwa timamu, na inazidi kuwa hafifu ndio mwanadamu amezidisha uasi wake kwa Mungu, hata akampiga Yesu misumari juu ya msalaba na kumkataa Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho kuingia katika nyumba yake, na analaani mwili wa Mungu, na anaona mwili wa Mungu kuwa wa hali ya chini. Kama mwanadamu angekuwa na ubinadamu kidogo, hangekuwa mkatili kiasi hicho katika utendeaji wake wa mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na akili hata kidogo tu, hangekuwa hivyo katika utendeaji wake wa mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na dhamiri hata kidogo, hangekuwa mwenye “shukrani” kwa Mungu mwenye mwili kwa njia hii. Mwanadamu anaishi katika enzi ya Mungu kuwa katika mwili, lakini yeye hawezi kumshukuru Mungu kwa kumpatia nafasi nzuri kiasi hicho, na badala yake analaani kuja kwa Mungu, au kupuuza kabisa ukweli wa Mungu aliyepata mwili, na inaonekana anapinga hali hii na anachoshwa nayo. Haijalishi jinsi mwanadamu anachukua kuja kwa Mungu, Mungu, kwa ufupi, daima ameendeleza kazi yake kwa uvumilivu—hata kama mwanadamu hajawahi kumkaribisha, na bila kujua yeye hufanya maombi kwa Mungu. Tabia ya mwanadamu imekuwa mbaya zaidi, akili yake imekuwa hafifu zaidi, na dhamiri yake imekanyagwa kabisa na yule muovu na kwa muda mrefu imekoma kuwa dhamiri ya awali ya mwanadamu. Mwanadamu hajakosa tu shukrani kwa Mungu mwenye mwili kwa kukabidhi maisha na neema nyingi juu ya wanadamu, bali pia anachukia Mungu kwa kumpatia ukweli; ni kwa sababu mwanadamu hana haja ya kujua ukweli hata kidogo ndio maana anamchukia Mungu. Haitoshi kwamba mwanadamu hawezi kuutoa uhai wake kwa ajili ya Mungu mwenye mwili tu, lakini pia anajaribu kutoa neema kutoka kwa Mungu, na anafanya madai kwa Mungu yaliyo mara kadhaa kubwa kuliko kile mwanadamu ametoa kwa Mungu. Watu wa dhamiri na hisia kama hizo hufikiria kwamba hili si jambo kubwa, na bado wanaamini kuwa wao wamefanya mengi sana kwa ajili ya Mungu, na kwamba Mungu amewapa kidogo sana. Kuna watu ambao wamenipa bakuli la maji na kisha kunyosha mikono yao na kudai kwamba nilipie bakuli mbili za maziwa, au kunipa chumba kwa usiku mmoja lakini walijaribu kunilipisha mara nyingi zaidi katika ada ya makazi. Ukiwa na ubinadamu kama huo, na dhamiri ya aina hii, ni jinsi gani bado mnatarajia kupata uzima? Nyinyi ni fukara wa kudharauliwa mlioje!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

84. Nisipoangazia uovu uliomo ndani ya mioyo yenu, basi kila mmoja wenu atajitwika taji kichwani na kujipa utukufu wote. Asili zenu za majivuno na kiburi huwaelekeza kusaliti dhamiri zenu wenyewe, kuasi na kumpinga Kristo, na kufichua uovu wenu, hivyo basi kuleta kwenye mwangaza fikra zenu, mawazo, tamaa nyingi na macho yaliyojaa ulafi. Ilhali mnaendelea kukiri kwamba mtajitolea maisha yenu kwa ajili ya kazi ya Kristo, na mnakariri tena na tena mambo ya kweli yaliyosemwa na Kristo zamani zile. Hii ndiyo “imani” yenu. Hii ndiyo “imani yenu isiyokuwa na doa”. Kwa muda huu wote, Nimemweka mwanadamu katika nidhamu ya hali ya juu. Iwapo uaminifu wako unakuja na nia na masharti, basi ni heri Nisijihusishe na huo mnaoita uaminifu wenu hata kidogo, kwa maana Ninachukia wale hunidanganya kupitia kwa nia zao na kunanihadaa na masharti. Natamani tu mwanadamu awe mwaminifu kabisa Kwangu, na afanye mambo yote kwa ajili ya, na kudhibitisha neno hilo moja: imani. Ninachukizwa na matumizi yenu ya maneno matamu ili Unifurahishe Mimi. Kwa maana daima Mimi napenda mtende pia kwa ukweli mtupu na uwazi na hivyo Ningependa pia mfanye matendo yenu Kwangu kwa imani ya kweli. Inapofika katika swala la imani, watu wengi hufikiri kwamba wanamfuata Mungu kwa sababu wako na imani, la sivyo hawangevumilia mateso hayo. Basi Nakuuliza hivi: Ni kwa nini humheshimu Mungu ilhali unaamini kuwepo Kwake? Ni kwa nini, basi, haumchi Mungu moyoni mwako iwapo unaamini kuwa Mungu Yupo? Unakubali kuwa Kristo ni kupata mwili kwa Mungu, basi ni kwa nini uwe na dharau Kwake? Kwa nini unatenda bila heshima Kwake? Ni kwa nini unamhukumu wazi wazi? Ni kwa nini siku zote unachunguza Yeye anakoenda? Mbona usijisalimishe katika mipango Yake? Ni kwa nini hutendi kulingana na neno Lake? Ni kwa nini unamhadaa na kumpokonya matoleo Yake? Ni kwa nini unazungumza katika nafasi ya Kristo? Ni kwa nini unatoa hukumu ya kubaini iwapo kazi Yake na neno Lake ni ya kweli? Mbona unathubutu kumkufuru Yeye kisiri? Ni mambo haya na mengine ndiyo yanayounda imani yenu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

85. Mkitumia fikira zenu wenyewe kumpima na kumwekea Mungu mipaka, kana kwamba Mungu ni sanamu ya udongo isiyobadilika, na mkimwekea Mungu mipaka kabisa katika vigezo vya Biblia na kumweka katika mawanda ya kazi yenye mipaka, basi hii inathibitisha kwamba mmemshutumu Mungu. Kwa sababu Wayahudi katika Agano la Kale walimchukulia Mungu kuwa sanamu yenye umbo lisilobadilika waliloshikilia mioyoni mwao, kana kwamba Mungu angeweza tu kuitwa Masihi, na Yeye aliyeitwa Masihi pekee ndiye Angeweza kuwa Mungu, na kwa sababu binadamu walimtumikia na kumwabudu Mungu kana kwamba Alikuwa sanamu ya udongo (isiyo na uhai), walimsulubisha Yesu wa wakati huo msalabani, wakimhukumu kifo—hivyo Yesu asiye na hatia Alihukumiwa kifo. Mungu hakuwa na kosa lolote, mwanadamu alikataa kumsamehe, naye alisisitiza kumhukumu afe na basi Yesu akasulubishwa. Kila wakati mwanadamu huamini kuwa Mungu habadiliki na humfafanua kwa msingi wa kitabu kimoja tu, Biblia, kana kwamba mwanadamu ana ufahamu wa kina kuhusu usimamizi wa Mungu, kana kwamba mwanadamu anavyo vitu vyote atendavyo Mungu katika kiganja cha mkono wake. Wanadamu ni wapumbavu kupita kiasi, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha kutia chumvi sana wanapoelezea jambo. Bila kujali jinsi kiwango chako cha ufahamu kumhusu Mungu kilivyo, bado Nasema kwamba humfahamu Mungu, kwamba wewe ni mtu ambaye humpinga Mungu zaidi, na kwamba umemshutumu Mungu, kwa sababu huna uwezo kabisa wa kuiheshimu kazi ya Mungu na kutembea katika njia ya kufanywa kamilifu na Mungu. Kwa nini Mungu hatosheki kamwe na matendo ya mwanadamu? Kwa sababu mwanadamu hamjui Mungu, kwa sababu ana fikira nyingi sana, na kwa sababu maarifa yake kuhusu Mungu hayaafikiani na uhalisi hata kidogo, lakini badala yake hurudia tu mada ile ile bila mabadiliko na hutumia mwelekeo ule ule katika kila hali. Na hiyo, kwa kuwa Amekuja duniani leo, Mungu anasulubishwa kwa mara nyingine na mwanadamu. Wanadamu dhalimu! Kuwafumba watu macho na kula njama, kupokonyana na kunyang’anya mmoja kutoka kwa mwingine, kung’ang’ania umaarufu na mali, kuuana—haya yote yataisha lini? Licha ya mamia ya maelfu ya maneno ambayo Mungu amezungumza, hakuna hata mmoja ambaye ameacha kufanya upumbavu. Watu hutenda kwa ajili ya familia zao, watoto wao, kazi zao, matarajio yao ya baadaye, cheo, majivuno, na pesa, kwa sababu ya chakula, mavazi, na mwili. Lakini kuna yeyote ambaye matendo yake kwa kweli ni kwa ajili ya Mungu? Hata miongoni mwa wale ambao wanatenda kwa ajili ya Mungu, kunao wachache tu wanaomfahamu Mungu. Ni watu wangapi ambao hawatendi kwa ajili ya maslahi yao? Ni wangapi wasiowakandamiza na kuwatenga wengine ili kulinda vyeo vyao wenyewe? Na hivyo, Mungu amehukumiwa kifo mara nyingi kwa nguvu, na mahakimu wakatili wengi mno wamemhukumu Mungu na kumsulubisha msalabani tena. Wangapi wanaweza kuitwa wenye haki kwa sababu wanatenda mambo kwa ajili ya Mungu kwa kweli?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Waovu Hakika Wataadhibiwa

86. Je, si watu wengi humpinga Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofautitofauti ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye majivuno na wadekezi katika asili yao, na wanatazama kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza masomo ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo zee kudhibitisha kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele ya Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wadogo wasiojua na wasio na habari ya kutosha jinsi na wanajaribu kuonyesha walivyo werevu? Kwa maarifa haba ya Biblia, wanajaribu kupotosha “wasomi”; wa dunia, kwa mafundisho duni ya dini ili kuwafunza watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya ihusu mchakato wao wanavyofikiria, na kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kuona kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Watu hawa hawana mantiki yoyote hata kidogo! Kwa kweli, maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo wanavyokuwa wagumu wa kuhukumu kazi Yake. Zaidi ya hayo, wanazungumzia tu machache kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu leo, lakini si wepesi wa kuhukumu. Kadri watu wanavyojua machache kumhusu Mungu, ndivyo wanavyozidi kuwa wenye majivuno na wenye kujiamini sana, na ndivyo wanavyozidi kutangaza nafsi ya Mungu kwa utundu—ilhali wanazungumzia tu nadharia, na wala hawapeani ushahidi wowote halisi. Watu kama hawa hawana thamani yoyote kabisa. Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru—je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, zaidi ya hayo, wale wasiojua, wenye majivuno ya asili na wasioweza kutawalwa? Hata ikiwa siku itakuja ambapo watu hawa watakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, bado Mungu hatawavumilia. Hawadharau tu wale wanaofanya kazi ya Mungu, bali pia wanamkufuru Mungu Mwenyewe. Watu kama hawa jasiri pasi na hadhari hawatasamehewa, katika enzi hii ama enzi itakayokuja na wataangamia kuzimuni milele! Watu kama hawa wasio na heshima, wenye kujifurahisha, wanajifanya kuwa wanamwamini Mungu, na kadiri wanavyozidi kufanya vile, ndivyo wanavyozidi kukosea amri za utawala wa Mungu. Je, si hao mafidhuli ambao kiasili hawazuiliki, na hawajawahi kumtii yeyote, wote hupitia njia hii? Je, si wao humpinga Mungu siku baada ya siku, Yeye ambaye daima huwa mpya na wala hazeeki?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

87. Fahamuni kuwa mnapinga kazi ya Mungu, ama mnatumia dhana zenu kupima kazi ya leo, kwa sababu hamjui kanuni za kazi ya Mungu, na kwa sababu hamchukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa makini kutosha. Upinzani wenu kwa Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kumetokana na dhana zenu na upumbavu wenu wa kiasili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sawa, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kiasili ya kutotii. Baada ya kupata imani yao katika Mungu, watu wengine hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, ilhali wanathubutu kuzungumza hadharani wakitathmini haki na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na pia wanawakemea mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; ubinadamu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote. Je, si siku itawadia ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumwagiza Mungu jinsi atakavyofanya kazi. Je, ni kwa namna gani watu hawa wasio na busara watamjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati anapomtafuta na anapokuwa na uzoefu naye; si katika kumkosoa kwa ghafla ndipo anapokuja kumjua Mungu kwa kupitia kutiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kadiri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao Kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, ubinadamu wako wa zamani, na utu wako, tabia na maadili ndiyo “mtaji” ambao unampingia Mungu, na kadri unavyokuwa mpotovu, ama ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale waliomilikiwa na dhana kali na wenye tabia ya unafiki wamo hata zaidi katika uadui wa Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo. Ikiwa dhana zako hazitarekebishwa, basi daima zitakuwa kinyume na Mungu; daima hutalingana na Mungu, na daima utakuwa mbali na Yeye.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

88. Wowote wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu ni wale wanaompinga Mungu, na hata zaidi ya hayo ni wale waliofahamu madhumuni ya kazi ya Mungu lakini bado hawatafuti kumridhisha Mungu. Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza? Wale wanaojiheshimu mbele ya Mungu ni wanadamu wa chini kabisa, ilhali wanaojinyenyekeza ndio wa heshima zaidi. Na wale wanaojifikiria kujua kazi ya Mungu na kutangaza neno la Mungu kwa wengine kwa kishindo na tarumbeta nyingi wakati macho yao yako Kwake—hawa ndio wajinga zaidi kati ya wanadamu. Wanadamu kama hao ni wale wasio na ushahidi wa Mungu, na wale walio na kiburi na majivuno. Wale wanaoamini kwamba wana ufahamu mdogo wa Mungu licha ya uzoefu wao halisi na ufahamu wa vitendo ni wale Anaowapenda zaidi. Ni wanadamu kama hawa ndio walio na ushahidi wa kweli na wanaweza kweli kukamilishwa na Mungu. Wale wasioelewa mapenzi ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale wanaoelewa mapenzi ya Mungu lakini bado hawauweki ukweli katika vitendo ni wapinzani wa Mungu; wale wanaokula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado wanaenda dhidi ya kiini cha maneno ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale walio na dhana za Mungu mwenye mwili na wanaasi makusudi ni wapinzani wa Mungu; wale wanaomhukumu Mungu ni wapinzani wa Mungu; na yeyote asiyeweza kumjua Mungu na kumshuhudia ni mpinzani wa Mungu. Kwa hivyo sikiliza ushawishi Wangu: Kama kweli una imani ya kutembea njia hii, basi zidi kuifuata. Iwapo huwezi kuepuka upinzani kwa Mungu, basi ni bora kwenda zako kabla hujachelewa. Vinginevyo, inaashiria mabaya badala ya mazuri, kwani asili yenu ni potovu sana. Huna uaminifu ama utii hata kidogo, ama moyo ulio na kiu ya haki na ukweli. Na wala huna upendo hata kidogo kwa Mungu. Inaweza kusemwa kuwa hali yako mbele ya Mungu imesambaratika kabisa. Huwezi kushika unachopaswa wala kusema unachopaswa. Huwezi kuweka katika vitendo kile ambacho unapaswa, na huwezi kutekeleza kazi unayopaswa. Huna uaminifu, dhamiri, utii ama azimio unalopasa. Hujavumilia mateso unayopaswa kuwa umevumilia, na huna imani unayopaswa kuwa nayo. Huna sifa yoyote kabisa; una heshima binafsi ya kuendelea kuishi? Nakuhimiza kwamba ni bora kufunga macho kwa mapumziko ya milele, hivyo kumtoa Mungu katika kujishughulisha nawe na kuvumilia mateso kwa ajili yako. Unaamini katika Mungu lakini bado hujui mapenzi Yake; unakula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado huwezi kukidhi mahitaji Yake. Unaamini katika Mungu lakini bado humjui, na kuishi ingawa huna lengo la kujaribu kufikia. Huna maadili na huna madhumuni. Unaishi kama mwanadamu lakini huna dhamiri, uadilifu wowote wala hata uaminifu kidogo. Unafikiriwaje kuwa wanadamu? Unaamini katika Mungu lakini unamdanganya. Zaidi ya hayo, unachukua pesa za Mungu na kula sadaka Yake, na bado, mwishowe, huonyeshi fikira kwa hisia za Mungu ama dhamiri kwa Mungu. Huwezi hata kukidhi mahitaji ya Mungu ya chini zaidi. Kwa hivyo unawezaje kufikiriwa kuwa mwanadamu? Chakula unachokula na hewa unayopumua vimetoka kwa Mungu, unafurahia neema Yake, na bado mwishowe, huna hata ufahamu mdogo wa Mungu. Kinyume na hayo, umekuwa mtu asiye na maana anayempinga Mungu. Si basi wewe ni mnyama asiye bora kuliko mbwa? Kuna mnyama yeyote aliye mkatili kukuliko wewe?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu

89. Tatizo kubwa zaidi la mwanadamu ni kwamba anaweza kupenda tu vitu ambavyo hawezi kuviona au kuvigusa, vitu ambavyo ni vya siri kubwa na vya kushangaza, na kwamba haviwezi kufikiriwa na mwanadamu na haviwezi kufikiwa na mwanadamu. Kadiri vitu hivi vinavyokuwa si halisi, kadiri vinavyochambuliwa na mwanadamu, ambaye anavifuata bila kujali kitu chochote, na hujaribu kuvipata. Kadiri vinavyokuwa si halisi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kuvichunguza na kuvichambua zaidi, hata kwenda kwa kiwango cha kufanya mawazo yake ya kina kuyahusu. Kinyume chake, jinsi vitu vinavyokuwa halisi zaidi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kuvipuuza; huviangalia kwa dharau, na hata huvitweza. Huu hasa si mtazamo weni juu ya kazi halisi Ninayoifanya leo? Kadiri mambo hayo yanavyokuwa halisi, ndivyo unavyozidi kuyadharau. Wala hutengi muda kwa ajili ya kuyachunguza, bali unayapuuza; unayadharau mambo haya halisi yenye kiwango cha chini, yenye matakwa ya moja kwa moja, na hata unakuwa na fikira nyingi kuhusu Mungu huyu ambaye ni halisi sana, na huwezi tu kuukubali uhalisi na ukawaida Wake. Kwa njia hii, huamini katika hali isiyo dhahiri? Una imani thabiti katika Mungu asiye dhahiri wa wakati uliopita, na wala hupendi kumjua Mungu wa kweli wa leo. Hii si kwa sababu Mungu wa jana na Mungu wa leo wanatoka katika enzi tofauti? Si pia kwa sababu Mungu wa jana ni Mungu wa mbinguni aliyeinuliwa, wakati Mungu wa leo ni mwanadamu mdogo wa duniani? Aidha, si pia kwa sababu Mungu anayeabudiwa na mwanadamu ni yule aliyetokana na dhana zake, wakati Mungu wa leo ni mwili halisi uliotengenezwa duniani? Hata hivyo, si kwa sababu Mungu wa leo ni halisi sana kiasi kwamba mwanadamu hamfuatilii? Maana kile ambacho Mungu wa leo anamtaka mwanadamu afanye ni kile ambacho mwanadamu hayupo radhi kabisa kukifanya, na ambacho kinamfanya ahisi aibu. Huku sio kufanya mambo yawe magumu kwa mwanadamu? Je, hili halionyeshi makovu yake hapa? Kwa namna hii, wengi wao ambao hawafuati uhalisi wanakuwa maadui wa Mungu mwenye mwili, wanakuwa wapinga Kristo. Huu si ukweli dhahiri? Hapo zamani, wakati Mungu alikuwa hajawa mwili, inawezekana ulikuwa mtu wa dini, au msahilina. Baada ya Mungu kuwa mwili, wasahilina wengi kama hao waligeuka bila kujua na kuwa wapinga Kristo. Unajua ni nini kinachoendelea hapa? Katika imani yako kwa Mungu, hujikiti katika uhalisi au kuufuatilia ukweli, bali unashikilia sana uongo—je, si hiki ndicho chanzo wazi cha uadui wako na Mungu mwenye mwili?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

90. Kabla ya kuwasiliana na Kristo, unaweza kuamini kwamba tabia yako imebadilishwa kabisa, kwamba wewe ni mfuasi mwaminifu wa Kristo, na kwamba wewe unastahili kupokea baraka za Kristo zaidi. Pia kwamba, kwa kuwa umesafiri njia nyingi, umefanya kazi nyingi, na kuleta matunda mengi, hivyo ni lazima utakuwa mtu anayepata taji mwishowe. Hata hivyo kuna ukweli ambao huenda hujui: Tabia potovu na uasi na upinzani wa mwanadamu huonekana wazi mara tu anapomwona Kristo, na uasi na upinzani unaoonekana wakati huu kwa hakika na kamilifu kuliko wakati mwingine wote. Ni kwa sababu Kristo ni Mwana wa Adamu—Mwana wa Adamu aliye na ubinadamu wa kawaida—kwamba mwanadamu hamwogopi wala kumheshimu. Ni kwa sababu Mungu anaishi katika mwili ndio maana uasi wa mwanadamu hufichuliwa kikamilifu na kwa uwazi sana. Kwa hivyo Nasema kwamba kuja kwake Kristo kumechimbua uasi wote wa wanadamu na kutupa asili ya mwanadamu katika afueni ya ghafla. Huku kunaitwa “kumvuta chui mkubwa kutoka mlimani” na “kumvuta mbwa mwitu kutoka pangoni pake.” Je, unathubutu kusema kwamba wewe ni mwaminifu kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe huonyesha utiifu kamili kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe si muasi? Wengine watasema: Kila wakati ambao Mungu ananiweka katika mazingira mapya, mimi daima hutii na silalamiki na aidha siweki fikra zozote juu ya Mungu. Wengine watasema: Kazi zozote nilizopewa na Mungu mimi hufanya kadri ya uwezo wangu na kamwe mimi si mvivu. Kama ndivyo hali, Nawauliza hivi: Je, mnaweza kulingana na Kristo wakati mnaishi pamoja naye? Na ni kwa muda gani nyinyi mnaweza kulingana na Yeye? Siku moja? Siku mbili? Saa moja? Saa mbili? Imani yenu inaweza kuwa ya kustahili sifa, lakini hamna uthabiti wa kutosha. Wakati unaishi na Kristo kwa kweli, kujidai kwako na kujigamba kwako kutawekwa wazi kwa maneno na matendo yako kidogo kidogo, na hivyo ndivyo tamaa yako ya kupindukia, na akili yako isiyotii na kutoridhika kwako kutafichuka kwa kawaida. Mwishowe, kiburi chako kitakuwa kikubwa zaidi, hadi wakati wewe utazozana sana na Kristo kama maji na moto, na basi asili yako itawekwa wazi kabisa. Wakati huo, fikra zako haziwezi kufichika tena, malalamiko yako, pia, yataonekana kwa ghafla, na ubinadamu wako duni utakuwa wazi kabisa. Hata hivyo, hata wakati huo, utaendelea kukana uasi wako mwenyewe, ukiamini kwamba badala yake kwamba Kristo kama huyu si rahisi kukubaliwa na mwanadamu, ni mwingi wa madai kwa binadamu, na ungetii kikamilifu kwake kama Yeye angekuwa tu Kristo mwenye huruma zaidi. Mnaamini kwamba daima kuna sababu ya haki ya uasi wenu, na kwamba nyinyi mnamwasi tu baada ya Kristo amewafikisha hatua fulani. Kamwe hamjawahi kufikiri kwamba mmekosa kumchukulia Kristo kama Mungu na katika nia ya kumtii. Badala yake, wewe kwa ukaidi unasisitiza Kristo afanye kazi Yake kulingana na matakwa yako, na punde ambapo kuna jambo lolote ambamo Hafanyi hivyo, basi unaamini kwamba Yeye si Mungu bali ni mwanadamu. Je, si kuna wengi kati yenu ambao wameridhika na Yeye katika hali hii? Ni nani huyo mnayemwamini hata hivyo? Na ni jinsi gani mnatafuta?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

91. Kila mara mnataka kumwona Kristo, lakini Nawasihi msijipandishe hadhi hivyo; kila mtu anaweza kumwona Kristo, lakini Nasema hakuna ambaye ni wa kufaa kumwona Kristo. Kwa sababu asili ya binadamu imejazwa na uovu, kiburi, na uasi, wakati unapomwona Kristo, asili yako itakuharibu na itakuhukumu hadi kufa. Ushirika wako na ndugu (au dada) huenda usionyeshe mengi kukuhusu wewe, lakini si rahisi hivyo unaposhiriki na Kristo. Wakati wowote, fikira zako zinaweza kukita mizizi, kiburi chako kianze kuchipuka, na uasi wako kuzaa mitini. Unawezaje kufaa kushiriki na Kristo na ubinadamu kama huo? Je, kweli unaweza kumchukua Yeye kama Mungu kila wakati wa kila siku? Je, kweli utakuwa na hali halisi ya utiifu kwa Mungu? Mnamuabudu Mungu mkubwa ndani ya mioyo yenu kama Yehova wakati mnamchukua Kristo anayeonekana kama mwanadamu. Hisia zenu ni duni mno na ubinadamu wenu ni wa hali ya chini! Hamwezi kumfikiria Kristo kama Mungu milele; ni mara chache tu, mnapotaka, ndio mnamshika na kumwabudu kama Mungu. Hii ndiyo sababu Ninasema nyinyi si waumini wa Mungu, ila kikundi cha washirika ambao wanaopigana dhidi ya Kristo. Hata watu ambao huonyesha wema kwa wengine hulipwa, lakini Kristo, ambaye amefanya kazi ya namna hiyo kati yenu, hajapokea upendo wa Mungu au fidia na utii wake. Je, hili si ni jambo la kusikitisha moyo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

92. Inaweza kuwa kwamba katika miaka yako yote ya imani katika Mungu, kamwe hujamlaani mtu yeyote wala kufanya tendo mbaya, lakini katika ushirika wako na Kristo, huwezi kusema ukweli, kutenda kwa uaminifu, au kutii neno la Kristo; basi, Ninasema kwamba wewe ndiye mtu mwovu zaidi na mwenye nia mbaya zaidi duniani. Unaweza kuwa mkunjufu na mwaminifu mno kwa jamaa zako, marafiki, mke (au mume), wanao na mabinti, na wazazi, na kamwe huwatumii wengine vibaya, lakini kama huwezi kulingana na kupatana na Kristo, basi hata ukitumia vitu vyako vyote kuwasaidia majirani zako au kulinda vizuri baba yako, mama, na wanakaya, Ningesema kwamba wewe bado ni mwovu, na zaidi ya hayo aliyejaa hila za ujanja. Usifikiri, kwamba wewe unalingana na Kristo kwa sababu tu unapatana na wengine au unafanya baadhi ya matendo mema. Je, unafikiri kwamba nia yako ya huruma inaweza kupata baraka kutoka Mbinguni kwa ujanja? Je, unafikiri kwamba matendo machache mema yanaweza kubadilishwa na utii wako? Hakuna hata mmoja wenu anaweza kukubali kushughulikiwa na kupogolewa, na wote wanaona vigumu kukubali ubinadamu wa kawaida wa Kristo, hata hivyo siku zote mnatangaza utiifu wenu kwa Mungu. Imani kama yenu italeta adhabu ya kufaa. Wacheni kujihusisha katika ndoto za ajabu na kutaka kumwona Kristo, kwa maana nyinyi ni wadogo sana katika kimo, kiasi kwamba nyinyi hata hamstahili kumwona. Wakati umeuwacha kabisa uasi wako na unaweza kupatana na Kristo, wakati huo Mungu Atakuonekania kwa kawaida. Iwapo utaenda kumwona Mungu kabla ya kupogolewa au kupitia hukumu, basi bila shaka utakuwa mpinzani wa Mungu na utakuwa katika njia ya kuangamizwa. Asili ya mwanadamu kwa kawaida ina uhasama kwa Mungu, kwa kuwa watu wote wamepotoshwa kabisa na shetani. Hakuna kizuri kinachoweza kupatikana kwa mtu kujaribu kushirikiana na Mungu kutokana na upotovu wake. vitendo na maneno yake kwa hakika vitafichua upotovu wake kila wakati; na katika kushirikiana na Mungu, uasi wake utafichuka katika vipengele vyote. Binadamu, kwa kutojua anakuja anampinga Kristo, kumdanganya Kristo, na kumtelekeza Kristo; hili litakapofanyika, mwanadamu atakuwa katika hali ya hatari zaidi na, hili likiendelea, atapata adhabu.

Baadhi ya watu wanaweza kuamini kwamba, kama kushirikiana na Mungu ni hatari sana, basi huenda likawa jambo la busara zaidi kukaa mbali na Mungu. Ni nini watu kama hawa wanaweza kupokea? Je, wanaweza kuwa waaminifu kwa Mungu? Hakika, kushirikiana na Mungu ni kugumu sana, lakini hiyo hasa ni kwa sababu mwanadamu amepotoka na si kwa sababu Mungu hawezi kushiriki naye. Ingekuwa bora kwenu kuweka juhudi zaidi kwa ukweli wa kuzijua nafsi zenu. Mbona hamjapata fadhili kwa Mungu? Kwa nini tabia zenu ni chukizo sana Kwake? Kwa nini maneno yenu yanachochea chuki Yake? Punde ambapo mmeonyesha uaminifu kidogo, nyinyi mnajisifu wenyewe, na mnadai malipo kwa ajili ya mchango mdogo; nyinyi huwadharau wengine wakati nyinyi mnaonyesha utiifu kidogo, na kumdharau Mungu baada ya kufanya kazi ndogo. Mnataka utajiri, zawadi na pongezi kwa ajili ya kumpokea Mungu. Nyoyo zenu huumwa wakati mnatoa sarafu moja au mbili; wakati mnatoa kumi, mnataka kubarikiwa na kutendewa kwa heshima. Ubinadamu kama wenu kweli ni wa kukera kuzungumziwa au kusikizwa. Kuna chochote kinachostahili sifa katika maneno na matendo yenu? Wale ambao wanatekeleza wajibu wao na wale wasiofanya; wale ambao huongoza na wale ambao hufuata; wale wanaompokea Mungu na wale wasiompokea; wale wanaotoa na wale wasiotoa; wale wanaohubiri na wale ambao hupokea neno, na kadhalika; watu wote kama hawa hujisifu wenyewe. Je, hamuoni hili likiwa la kuchekesha? Mkijua vyema kwamba mnamwamini Mungu, hata hivyo ninyi hamwezi kulingana na Mungu. Kweli mnajua vyema kwamba hamstahili hata kidogo. Je, hamhisi kuwa hisia yenu imepunguka kiasi kwamba hamwezi tena kujizuia? Na hisia kama hii, mnastahili vipi kushirikiana na Mungu? Je, kufikia hapa nyinyi hamjionei hofu? Tabia yenu tayari imepunguka kiasi kwamba hamwezi kulingana na Mungu. Hali ikiwa hivi, je, imani yenu si ya kuchekesha? Imani yenu si ya kipuuzi? Ni jinsi gani utashughulikia maisha yako ya baadaye? Ni jinsi gani utachagua njia ya kutembelea?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

93. Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa wanaitwa wanaotafuta mamlaka. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni. Mioyo yao imejaa umaarufu, mali na utukufu. Hawaamini kamwe kuwa mtu wa kawaida tu anaweza kuwashinda wengi vile, kwamba mtu asiye wa kutambulika kwa macho tu anaweza kukamilisha watu. Hawaamini kuwa hawa watu wasio na sifa, walio kwenye vumbi na vilima vya samadi ni watu waliochaguliwa na Mungu. Wanaamini kuwa kama watu wale wangekuwa vyombo vya wokovu Wake Mungu, basi mbingu na ardhi zitageuzwa juu na chini na watu wote watacheka kupindukia. Wanaamini kuwa iwapo Mungu atawachagua watu wasio na sifa yoyote wafanywe viumbe kamili, basi wao walio na sifa watakuwa Mungu Mwenyewe. Maoni yao yamechafuliwa na kutoamini; hakika, mbali na kutoamini, wao ni wanyama wasio na maana. Kwa maana wao wanathamini tu nyadhifa, hadhi kuu na mamlaka; wanachokithamini sana ni makundi makuu na madhehebu makuu. Hawana heshima hata kidogo kwa wale wanaoongozwa na Kristo; wao ni wasaliti tu waliomgeuka Kristo, kuugeuka ukweli na uhai.

Unachopendezwa nacho sio unyenyekevu wa Kristo, ila ni wale wachungaji wa uongo wenye umaarufu. Hupendi maarifa au kupendeza kwa Kristo, bali unapenda wale watukutu wanaojihusisha na ulimwengu mchafu. Unauchekelea uchungu wa Kristo asiyekuwa na pahali pa kulaza kichwa Chake, na badala yake unatamani maiti zinazokamata sadaka na kuishi katika uasherati. Hauko tayari kupokea mateso pamoja na Kristo, lakini unakimbilia mikononi mwa wapinzani wa Kristo hata ingawa wanakupa nyama za mwili pekee, barua na udhibiti pekee. Hata sasa, moyo wako bado unawaendea wao, sifa zao, hadhi zao, na ushawishi wao. Ilhali unazidi kuchukua mtazamo ambapo unaona kazi ya Kristo kuwa ngumu sana kukubali na huko tayari kuikubali. Hii ndiyo maana Ninasema hauna imani ya kumkubali Kristo. Sababu iliyokufanya Umfuate mpaka leo hii ni kuwa hukuwa na chaguo jingine. Moyoni mwako milele mna picha nyingi refu; huwezi kusahau kila neno lao na matendo yao, au maneno yao ya ushawishi na mikono. Wao ni, katika moyo wenu, wakuu milele na tena mashujaa milele. Lakini hivi sivyo ilivyo na Kristo wa leo hii. Yeye moyoni mwako kamwe Hana umuhimu na kamwe Hastahili heshima. Kwa maana Yeye ni wa kawaida sana, mwenye ushawishi mdogo zaidi na Yuko mbali na ukuu.

Kwa vyovyote vile, Ninasema kuwa wote wale wasioenzi ukweli ni wasioamini na waasi wa ukweli. Watu kama hawa hawatawahi kuipokea idhini ya Kristo. Umeweza sasa kutambua kiasi cha kutoamini kilicho ndani yako? Na kiasi gani cha usaliti kwa Kristo? Kwa hivyo Nakuhimiza hivi; Kwa maana umeichagua njia ya ukweli, basi huna budi ila kujitolea na moyo wote; usiwe na kuchanganyikiwa au wa kusitasita. Unafaa kufahamu kuwa Mungu si wa ulimwengu huu au wa mtu yeyote, bali ni wa wale wote wanaoamini katika Mungu kwa kweli, wote wale wanaomwabudu, na wote wale waliojitolea na wanaoamini katika Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

94. Wengi wa watu wanaomfuata Mungu wanashughulika tu na jinsi watakavyopata baraka nyingi na kuepuka majanga. Panapotajwa kazi na usimamizi wa Mungu, wanakaa kimya na kupoteza matamanio yao yote. Wanaamini kuwa kujua maswali ya kuchosha kama hayo hakutakuza maisha yao au kuwa na faida yoyote, na kwa hivyo hata kama wamezisikia habari kuhusu usimamizi wa Mungu, wanazichukulia kikawaida. Na hawazichukulii kama kitu cha thamani kukipokea, na hata kukikubali kama sehemu ya maisha yao. Watu kama hao wana nia sahili sana katika kumfuata Mungu, na nia hiyo ni kupokea Baraka. Watu kama hao hawawezi kujishughulisha kuzingatia kitu chochote kingine ambacho hakihusiani na nia hii moja kwa moja. Kwao, kuamini kwa Mungu ili kupata baraka ndilo lengo halali na la thamani kwa imani yao. Hawaathiriwi na kitu chochote ambacho hakiwezi kutekeleza lengo hili. Hivyo ndivyo ilivyo na watu wengi wanaomfuata Mungu leo. Nia yao na motisha huonekana kuwa halali, kwa sababu wakati huo huo wa kumwamini Mungu, wanatumia rasilmali kwa ajili ya Mungu, wanajitolea kwa Mungu, na kutekeleza wajibu wao. Wanauacha ujana wao, wanajinyima kwa familia na kazi zao, na hata hukaa miaka mingi wakijishughulisha mbali na nyumbani kwao. Kwa ajili ya lengo lao kuu, wanabadili matamanio yao, wanabadili mtazamo wao wa nje wa maisha, hata kubadili njia wanayoitafuta, ila bado hawawezi kubadili nia ya imani yao kwa Mungu. Wanajishughulisha na usimamizi wa matamanio yao wenyewe; haijalishi njia iko mbali vipi, na ugumu na vikwazo vilivyo njiani, wanashikilia msimamo wao bila uoga hadi kifo. Ni nguvu zipi zinazowafanya wawe wa kujitolea kwa njia hii? Ni dhamiri yao? Ni sifa zao kubwa na nzuri? Ni kujitolea kwao kupigana na nguvu za maovu hadi mwisho? Ni imani yao wanayomshuhudia Mungu kwayo bila kutaka malipo? Ni utiifu wao ambao kwao wanajitolea kuacha kila kitu ili kutimiza mapenzi ya Mungu? Au ni roho yao ya kujitolea ambayo kwayo wanajinyima kila mara mahitaji badhirifu ya kibinafsi? Kwa watu ambao hawajawahi kujua kazi ya usimamizi wa Mungu kutoa zaidi, kwa hakika, ni muujiza wa ajabu! Hivi sasa, acha tusijadiliane kuhusu kiasi ambacho hawa watu wametoa. Tabia yao, hata hivyo, inastahili sana sisi kuichambua. Mbali na manufaa ambayo yanahusiana nao, je, kuna uwezekano wa kuweko kwa sababu nyingine ya wale hawajawahi kumfahamu Mungu kujitolea zaidi Kwake? Kwa hili, tunagundua tatizo ambalo halikutambuliwa hapo awali: Uhusiano wa mwanadamu na Mungu ni ule wa mahitaji ya kibinafsi yaliyo wazi. Ni uhusiano baina ya mpokeaji na mpaji wa baraka. Kwa kuiweka wazi, ni kama ule uhusiano baina ya mwajiriwa na mwajiri. Mwajiriwa hufanya kazi ili tu kupokea malipo yanayotolewa na mwajiri. Katika uhusiano kama huu, hakuna upendo, ila maafikiano tu, hakuna kupenda au kupendwa, ni fadhila na huruma tu; hakuna maelewano, ila hasira iliyofichwa na udanganyifu; hakuna mapenzi, ila ufa usioweza kuzibika. Mambo yanapofikia hapa, nani anaweza kubadilisha mwelekeo kama huu? Na ni watu wangapi ambao wanaweza kufahamu kwa kweli jinsi uhusiano huu ulivyokosa matumaini? Naamini kuwa watu wanapojitosa wenyewe kwenye raha ya kubarikiwa, hakuna anayeweza kukisia jinsi uhusiano na Mungu ulivyo wa aibu na usiopendeza.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

95. Jambo la kusikitisha mno kuhusu imani ya wanadamu kwa Mungu ni kuwa wanadamu wanatekeleza usimamizi wao wenyewe katikati ya kazi ya Mungu na hawasikilizi usimamizi wa Mungu. Udhaifu mkubwa wa mwanadamu unaegemea katika jinsi, wakati huo huo anatafuta kujitoa kwa Mungu na kumwabudu, mwanadamu anaunda hatima yake kamilifu na kuhesabu jinsi ya kupokea baraka kubwa zaidi na hatima iliyo bora zaidi. Hata kama watu watafahamu jinsi walivyo wa kuhurumiwa, wenye chuki na walivyo ovyo, ni wangapi hapo ambao wanaweza kuachana na ukamilifu na matumaini yao? Na ni nani anayeweza kusimamisha hatua zake na kuacha kujifikiria yeye mwenyewe? Mungu Anawahitaji wale watakaojihusisha kwa karibu Naye kukamilisha usimamizi Wake. Anawahitaji wale ambao watatoa mawazo yao na mwili kwa ajili ya kazi Yake ya usimamizi ili kujitoa Kwake; Hawahitaji wale watakaoinua mikono yao na kuomba kutoka Kwake kila siku, na hata wale wanaotoa kidogo na kusubiri kulipwa kwa hilo tendo la kutoa. Mungu Anawadharau wale wanaotoa michango kidogo na kuridhika. Anawachukia wenye roho katili ambao hukataa kazi ya usimamizi Wake na hutaka tu kuongea kuhusu kwenda mbinguni na kupata baraka. Anachukia hata zaidi na wale ambao hufaidika na fursa inayowezeshwa na kazi Anayoifanya katika kuokoa wanadamu. Hii ni kwa sababu hawa watu hawajawahi kushughulishwa na Anachotarajia kupata Mungu kutokana na kazi Yake ya usimamizi. Wanashughulishwa tu na jinsi wanavyoweza kutumia hiyo fursa iliyowezeshwa na kazi ya Mungu ili kupata baraka. Hawajali roho Yake Mungu, kwa kuwa wanajishughulisha na mustakabali na hatima yao. Wale ambao wanakataa kazi ya usimamizi wa Mungu na hawana hata tamanio dogo katika jinsi Mungu Anavyowaokoa wanadamu na mapenzi Yake, wote wanafanya wapendavyo kando na kazi ya usimamizi wa Mungu. Tabia yao haikumbukwi na Mungu, na haikubaliwi na Mungu, na hata haiangaliwi kwa fadhila ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

96. Matendo Yangu ni mengi zaidi kwa kuhesabiwa kuliko chembechembe za changarawe kwenye ufuo na hekima Yangu kubwa zaidi kuliko ile ya watoto wote wa kiume wa Suleimani, ilhali binadamu wanafikiria kwamba Mimi ni daktari tu asiye na mengi kumhusu na mwalimu wa binadamu asiyejulikana! Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze tu kupata uponyaji? Ni wangapi wanaoniamini Mimi hili tu niweze kutumia nguvu Zangu kupunga roho chafu kutoka kwenye miili yao? Na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili tu waweze kupokea amani na furaha kutoka Kwangu? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili kuhitaji kutoka Kwangu utajiri mwingi zaidi wa dunia, na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuishi maisha hayo kwa usalama na kuwa salama salimini katika maisha yajayo? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuepuka tu mateso ya kuzimu na kupokea baraka za mbinguni? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili wapate tulizo lakini hawatafuti kupata chochote kutoka kwa ulimwengu ujao? Niliposhushia hasira Zangu binadamu na kuchukua furaha na amani yote aliyokuwa nayo mwanzo, binadamu akaanza kuwa na shaka. Nilipomkabidhi binadamu mateso ya kuzimu na kuchukua tena baraka za mbinguni, aibu ya binadamu iligeuka na kuwa hasira. Wakati binadamu aliponiomba Mimi kumponya, bado Sikumsikiza na aidha nilimchukia pakubwa, binadamu alienda mbali sana na Mimi na akatafuta njia za dawa ovu na uchawi. Nilipochukua kila kitu ambacho binadamu walitaka kutoka Kwangu, walitoweka bila kuonekana tena. Kwa hivyo, Ninasema kwamba mwnadamu ana imani Kwangu kwa sababu Nampa neema nyingi kupindukia, na mambo yapo mengi sana ya kupata.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?

97. Unatumai kwamba imani yako kwa Mungu haitakuwa na changamoto ama dhiki, ama mateso yoyote. Unafuata vile vitu ambavyo havina maana, na huambatanishi faida yoyote kwa maisha, badala yake kuweka mawazo ya fujo kabla ya ukweli. Huna maana! Unaishi kama nguruwe—kuna tofauti gani kati yako, nguruwe na mbwa? Je, hao wasiofuata ukweli na badala yake wanafuata mapenzi ya kimwili, si wote ni wanyama? Hao waliokufa na bila roho si wafu wanaotembea? Maneno mangapi yamenenwa kati yenu? Je, kazi kidogo imefanywa kati yenu? Ni kiasi gani nimetoa kati yenu? Na mbona hujapata chochote? Una nini cha kulalamikia? Je, si ni kweli kuwa hujapata chochote kwa sababu unapenda mwili sana? Na ni kwa sababu mawazo yako ni ya fujo sana? Je, si kwa sababu wewe ni mpumbavu sana? Kama huna uwezo wa kupata baraka hizi, unaweza kumlaumu Mungu kwa kutokukuokoa? Unachofuata ni cha kukuwezesha kupata amani baada ya kumwamini Mungu—watoto wako wawe huru kutokana na magonjwa, ili mme wako apate kazi nzuri, ili mwana wako apate mke mwema, binti wako apate mme anayeheshimika, ili ndume na farasi wako walime shamba vizuri, kwa mwaka wa hali ya anga nzuri kwa mimea yako. Hili ndilo unalolitafuta. Harakati yako ni kuishi kwa starehe, ili ajali isipate familia yako, ili upepo ukupite, ili uso wako usiguswe na changarawe, ili mazao ya familia yako yasipate mafuriko, ili usiguswe na majanga yoyote, kuishi katika mikono ya Mungu, kuishi kwenye kiota chenye joto. Mwoga kama wewe, anafuata mwili kila wakati—je, una moyo, una roho? Si wewe ni mnyama? Nakupa njia ya ukweli bila kukuuliza chochote, ilhali hauifuati. Je, wewe ni wale wamwaminio Mungu? Nahifadhi uhai wa ukweli wa binadamu juu yako, ila hauufuati. Je, una tofauti kati ya nguruwe na mbwa? Nguruwe hawafuati maisha ya binadamu, hawafuati kutakaswa, na hawaelewi maana ya maisha. Kila siku wanapokula na kushiba, wanalala. Nimekupa njia ya ukweli, ila hujaipata: Wewe u mkono mtupu. Je, unakubali kuendelea na maisha haya, maisha ya nguruwe? Umuhimu wa watu hao kuwa hai ni nini? Maisha yako ni ya kudharauliwa na kutoheshimika, unaishi huku ukiwa na uchafu na uzinzi, na hufuati lengo lolote; je, si maisha yako ni ya kutoheshimika kwa yote? Je, una ujasiri wa kumtazamia Mungu? Ukiendelea kuwa na uzoefu wa haya, je, si utakosa kupata chochote? Umepewa njia ya ukweli, lakini kama utaipata ama hapana inategemea na kutafuta kwako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

98. Katika uzoefu wa watu katika maisha yao, mara nyingi wao hufikiria, nimetoa familia yangu na ajira yangu kwa Mungu, na Amenipa nini? Lazima niongezee na kuthibitisha haya—je, nimepokea baraka zozote hivi majuzi? Nimetoa mengi sana wakati huu, nimekimbia na kukimbia na kuteseka sana—je, Mungu amenipa ahadi zozote baada ya haya? Je, Amekumbuka matendo yangu mazuri? Mwisho wangu utakuwa vipi? Ninaweza kuzipokea baraka za Mungu? … Kila mtu kila wakati hufanya hesabu kama hizi ndani ya moyo wake, na yeye hutoa madai yake kwa Mungu yanayoonyesha motisha yake, malengo na mawazo ya mabadilishano. Hii ni kusema, ndani ya moyo wake mwanadamu siku zote humweka Mungu majaribuni, siku zote anaunda njama kumhusu Mungu, akijitetea kwa Mungu kila wakati kwa sababu ya mwisho wake binafsi na kujaribu kumfanya Mungu atoe kauli, aweze kuona kama Mungu anaweza kumpa kile anachotaka au la. Wakati huohuo akimfuata Mungu, binadamu hamchukulii Mungu kama Mungu. Siku zote mwanadamu amejaribu kufanya mipango na Mungu, akitoa madai bila kusita kwake Yeye na hata akimsukuma Yeye katika kila hatua, akijaribu kupiga hatua ya maili licha ya kupewa inchi moja. Wakati huohuo akijaribu kufanya mabadilishano na Mungu, binadamu pia anabishana na Yeye, na wapo hata watu ambao, wakati majaribu yanawapata au wanapojipata katika hali ya kuteketea, mara nyingi wanakuwa wanyonge, wananyamaza na kuzembea katika kazi yao, na wanajaa malalamiko kumhusu Mungu. Tangu wakati ambapo mwanadamu alianza kumwamini Mungu, amemchukulia Mungu kama alama ya pembe inayoonyesha wingi wa neema, kisu cha Kijeshi cha Uswisi, na amejichukulia yeye mwenyewe kuwa mdaiwa mkubwa zaidi wa Mungu, ni kana kwamba kujaribu kupata baraka na ahadi kutoka kwa Mungu ni haki na jukumu lake la asili, huku jukumu la Mungu likiwa ni kumlinda na kumtunza mwananadamu na kumruzuku. Huu ndio ufahamu wa kimsingi wa “imani katika Mungu” wa wale wote wanaomwamini Mungu, na ufahamu wao wa kina zaidi wa dhana ya imani katika Mungu. Kutoka katika kiini cha asili ya mwanadamu hadi katika ufuatiliaji wake wa kibinafsi, hakuna kitu chochote kinachohusiana na kumcha Mungu. Nia ya mwanadamu katika kumwamini Mungu huenda isiwe na uhusiano na kumwabudu Mungu. Hivi ni kusema kwamba, mwanadamu hajawahi kufikiria wala kuelewa kwamba imani katika Mungu inahitaji kumcha Mungu, na kumwabudu Mungu. Kwa mujibu wa haya yote, kiini cha mwanadamu kiko wazi. Kiini hiki ni kipi? Ni kwamba moyo wa mwanadamu ni mwovu, unaficha udanganyifu na ujanja, haupendi mambo ya kutopendelea na haki na kile kilicho chanya, nao ni wenye kustahili dharau na ulafi. Moyo wa mwanadamu umemfungia Mungu nje sana, hajampa Mungu moyo wake kabisa. Mungu hajawahi kuona moyo wa kweli wa mwanadamu, wala hajawahi kuabudiwa na mwanadamu. Haijalishi jinsi gharama ambayo Mungu amelipia ilivyo kubwa, au ni kiasi kipi cha kazi Anachofanya, au ni kiwango kipi Anachompa mwanadamu, mwanadamu anabakia yule asiyeona hayo yote, na hajali kuyahusu. Mwanadamu hajawahi kumpa Mungu moyo wake, anataka tu kuujali moyo wake yeye mwenyewe, kufanya uamuzi wake mwenyewe—sababu ikiwa kwamba mwanadamu hataki kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, au kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, wala hataki kumwabudu Mungu kama Mungu. Hivyo ndivyo hali ya mwanadamu ilivyo leo.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

99. Wakati wowote hatima inatajwa, muichukulie kwa uzito maalumu; nyinyi nyote ni mahususi hasa kuhusu jambo hili. Baadhi ya watu hawawezi kusubiri kumsujudia Mungu ili hatimaye kuwa na hatima nzuri. Naweza kutambua hamu yenu, ambayo haihitaji kuonyeshwa katika maneno. Kabisa hamtaki miili yenu ianguke katika maafa, na hata zaidi, hamtaki kushuka katika adhabu ya muda mrefu hapo baadaye. Mnatarajia tu kujiruhusu muishi kwa uhuru zaidi kidogo, kwa urahisi zaidi kidogo. Na hivyo unahisi mwenye wasiwasi hasa wakati wowote hatima inatajwa, ukiwa na hofu kubwa kwa undani kwamba, usipokuwa mwangalifu vya kutosha, unaweza kumkosea Mungu na hivyo upate adhabu unayostahili. Hamjasita kufanya maafikiano kwa ajili ya hatima zenu, na wengi wenu ambao wakati mmoja walikuwa wa kuzunguka na wapuuzi hata kwa ghafla wamegeuka hususa wapole na wa dhati; unyofu wenu hata una mzizimo. Pasipo kutilia maanani, nyinyi nyote mna mioyo “minyoofu”, na kutoka mwanzo hadi mwisho mmejifungua wazi Kwangu bila kuficha siri zozote katika mioyo yenu, yawe lawama, udanganyifu, au ibada. Kwa jumla, “mmekiri” kwa uwazi Kwangu yale mambo muhimu katika pahali pa siri yenye kina kwenu. Mambo kama yalivyo, Sijawahi kuepuka mambo kama haya, kwa sababu yamekuwa ya kawaida Kwangu. Afadhali muingie katika bahari la moto kwa hatima yenu ya mwisho kuliko kupoteza mlia mmoja wa nywele ili kupata kibali cha Mungu. Sio kwamba Ninakuwa wa kulazimishia imani kwenu; ni kwamba mioyo yenu ya ibada ni pungufu hasa kwa kukabiliana na kila kitu Ninachofanya. Hamuwezi kuelewa Ninachomaanisha, hivyo basi acheni Niwatolee maelezo rahisi: Mnachohitaji si ukweli na maisha; si kanuni za jinsi ya kutenda, na hasa siyo kazi Yangu yenye kujitahidi. Yote mnayohitaji ni yale ambayo mnamiliki katika mwili—mali, hadhi, familia, ndoa, nk. Ninyi mnatupilia mbali kabisa maneno na kazi Yangu, hivyo Naweza kujumlisha imani yako kwa neno moja: shingo upande. Mtafanya lolote ili kutimiza mambo ambayo bila shaka mmejitolea, lakini Nimegundua kwamba hampuuzi kila kitu kwa ajili ya mambo ya imani yenu katika Mungu. Badala yake, nyinyi ni waaminifu tu kiasi, na kiasi. Hiyo ndiyo sababu Nasema kwamba wale wanaokosa moyo wa usafi mkubwa ni washinde katika imani yao katika Mungu. Fikiria kwa uangalifu—je, kunao wengi washinde miongoni mwenu?

Mnapaswa kujua kwamba mafanikio katika kumwamini Mungu yanatimizwa kwa sababu ya matendo ya watu wenyewe; wakati watu hawafanikiwi lakini badala yake wanashindwa, hiyo pia ni kwa sababu ya matendo yao wenyewe, sio matokeo ya vipengele vingine. Ninaamini kwamba mngefanya kitu chochote kitachukua ili kupata kitu kufanyika ambacho ni kigumu zaidi na kinachohitaji mateso zaidi kuliko kumwamini Mungu, na kwamba mngekichukulia kwa makini sana. Hamngetaka hata kufanya makosa yoyote; hizi ni aina za juhudi zisizolegea ambazo nyote mmeweka katika maisha yenu wenyewe. Nyinyi hata mna uwezo wa kunidanganya Mimi katika mwili chini ya hali ambazo hamuwezi kudanganya yeyote wa familia yenu wenyewe. Hii ni tabia yenu thabiti na kanuni ambayo mnatumia katika maisha yenu. Je, si bado mnaendeleza picha ya uongo ili kunidanganya Mimi, kwa ajili ya hatima yenu, na kuwa na hatima nzuri na ya furaha? Nafahamu kwamba ibada yenu na unyofu wenu ni wa muda tu; je, matamanio yenu na gharama mnayolipa ni ya sasa tu na si ya baadaye? Mnataka tu kutumia nguvu moja ya mwisho ili kupata hatima nzuri. Azma yenu ni kubadilisha tu; siyo ili msiwe wenye deni kwa ukweli, na ni hasa msinilipe kwa ajili ya gharama Niliyolipa. Kwa neno, mko tu tayari kutumia ujanja wenu, lakini hamtaki kuipigania. Je, si haya ni matakwa yenu ya dhati? Sio lazima mjifiche, na hata zaidi, sio lazima mpige mbongo zenu juu ya hatima yenu hadi pale ambapo hamuwezi kula au kulala. Je, si ni kweli kwamba matokeo yenu yatakuwa yameamuliwa mwishowe?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Juu ya Hatima

100. Mmekuwa wafuasi Wangu kwa miaka mingi sana, lakini hamjawahi kunionesha hata chembe ya uaminifu. Badala yake mmekuwa mkizunguka kwa watu mnaowapenda na vitu vinavyowapendeza sana, na kuviweka karibu na mioyo yenu na havijawahi kuachwa, wakati wowote, mahali popote. Mnapokuwa na hamu ama shauku na kitu chochote kile Mnachokipenda, siku zote mnakuwa ni wakati ambapo mnanifuata, au hata wakati mnaposikiliza maneno Yangu. Hivyo nasema, mnatumia uaminifu ninaowataka muonyeshe, kuwa badala yake waaminifu na kufurahia “vipenzi” wenu. Ingawa mnaweza kutoa sadaka ya kitu kimoja au vitu viwili kwa ajili Yangu, hakuwakilishi vitu vyenu vyote, na haionyeshi kwamba ni Kwangu ambako uaminifu wako uko kwa kweli. Mnajiweka wenyewe katika shughuli ambazo mnazipenda: Wengine ni waaminifu kwa watoto, wengine kwa waume, wake, utajiri, kazi, wenye vyeo, umaarufu, au wanawake. Kwa maana kile ambacho mnakuwa waaminifu kwacho, hujawahi kuhisi kuchoshwa au kukerwa nacho, badala yake, mnatamani kuwa na kiasi kikubwa zaidi na ubora wa vitu ambavyo ninyi mu waaminifu kwavyo na hamjawahi kukata tamaa. Mimi mwenyewe na maneno Yangu daima hutupwa pembeni katika masuala ya vitu mnavyovipenda. Na hamna namna isipokuwa kuyaweka mwisho; wengi hata wanaondoka sehemu ya mwisho kwa ajili ya kuwa waaminifu kwa kitu ambacho hawajakigundua bado. Hawajawahi kuniweka mioyoni mwao kwa kiwango chochote kile. Pengine mtafikiri kwamba ninahitaji mambo mengi sana kutoka kwenu au Ninawahukumu kimakosa, lakini je, mmeshawahi kufikiri kuhusu ukweli huu kwamba mnapotumia muda kwa furaha pamoja na familia yenu, hujawahi kuwa mwaminifu kwangu hata mara moja? Wakati kama huu, hii haiwaumizi? Mioyo yenu inapojawa na furaha kwa kupokea malipo kwa kazi zenu, haiwavunji moyo kwamba hamjajitweka kwa ukweli wa kutosha? Ni lini mmewahi kulia kwa kukosa idhinisho langu? Mnaitesa akili yenu na kupata maumivu makubwa kwa ajili ya watoto wenu, lakini bado hamjaridhika, bado mnaamini kwamba hamjaweka jitihada za kutosha kwao, kwamba hamjatumia nguvu zenu zote. Lakini Kwangu, mmekuwa ajizi na wa kutojali, mkiniweka tu katika kumbukumbu zenu na wala Sidumu ndani ya mioyo yenu. Kujitolea Kwangu na jitihada zangu daima hupita bila nyinyi kuzihisi, na wala hamjawahi kuweka jitihada ili muweze kuelewa. Nyinyi hutafakari kidogo tu na kuamini kwamba hiyo itatosha. “Uaminifu” wa aina hii sio ule ambao Nimekuwa nikiutazamia, bali ni ule ambao umekuwa machukizo Kwangu kwa muda mrefu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

101. Kama sasa Ningeweka utajiri mbele yenu na kuwaambia kuwa mchague kwa uhuru, huku Nikijua kwamba[a] sitawahukumu, basi wengi wangechagua utajiri na kuacha ukweli. Wazuri miongoni mwenu wangeacha utajiri na kuchagua ukweli shingo upande, ilhali wale ambao wako katikati wangekumbatia utajiri kwa mkono mmoja na kwa mkono mwingine kuukumbatia ukweli. Kwa njia hii, je, rangi zenu halisi si zingejidhihirisha? Unapochagua ukweli kwa kulinganisha na kitu chochote ambacho u mwaminifu kwacho, wote mtafanya maamuzi kama hayo, na tabia yenu itabakia kuwa ile ile. Si ndivyo ilivyo? Je, hakuna watu wengi miongoni mwenu waliobadilika badilika katika kuchagua baina ya wema na ubaya? Katika mashindano kati ya mazuri na mabaya, nyeusi na nyeupe, mna uhakika na uchaguzi mlioufanya kati ya familia na Mungu, watoto na Mungu, amani na vurugu, utajiri na umasikini, hadhi na kuwa mtu wa kawaida, kusaidiwa na kutupiliwa mbali, na kadhalika. Kati ya familia yenye amani na familia iliyovunjika, nyinyi huchagua ya kwanza bila kusita; kati ya utajiri na wajibu, safari hii pia mnachagua ya kwanza, bila kuwa na nia ya kurudi ufuoni[b] kati ya starehe na umasikini, tena mlichagua ya kwanza; kati ya watoto, mke, mume na Mimi, mnachagua za kwanza; na kati ya dhana na ukweli, kwa mara nyingine tena mlichagua ya kwanza. Nikikabiliwa na kila namna ya matendo yenu maovu, karibu sana Nimepoteza imani Yangu kwenu. Ninashangazwa sana na kwamba mioyo yenu inapinga kulainishwa. Miaka mingi ya kujitolea na jitihada Yangu imeniletea kuvunjika moyo tu nanyi kupoteza imani Nami. Hata hivyo, matumaini Yangu juu yenu yanakua kila siku inayopita, kwa kuwa siku Yangu tayari imekwisha kuwekwa wazi kwa kila mtu. Lakini, bado mnaendelea kuyafuata yale ambayo ni ya giza na maovu, na mnakataa kulegeza mshiko wenu. Kwa kufanya hivyo, mtapata matokeo gani? Mmewahi kutafakari kwa makini kuhusu hili? Kama mngetakiwa kuchagua tena, msimamo wenu ungekuwa upi? Bado lingekuwa ni chaguo la kwanza? Je, yale ambayo mngenipatia bado yangekuwa maudhi na huzuni ya majuto? Je, mioyo yenu bado ingekuwa migumu? Je bado mngekuwa hamjui cha kufanya ili kuufariji moyo Wangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

102. Kila siku, fikira na matendo ya kila mmoja yanachunguzwa na Yeye na, katika wakati uo huo, wamo katika matayarisho ya siku zao zinazofuata. Hii ni njia ambayo lazima kila mtu aliye hai aipitie na ambayo Nimeamulia kabla kila mmoja. Hakuna anayeweza kuepuka hili na hakuna atakayepata upendeleo. Nimezungumza maneno yasiyohesabika na zaidi ya yote Nimefanya kazi kubwa mno. Kila siku, Ninatazama vile kila mwanadamu kiasili anafanya yote ambayo anafaa kufanya kulingana na asili yake na vile inavyoendelea. Bila kujua, wengi tayari wamo katika “njia sahihi”, ambayo Niliiweka kwa ufunuo wa mwanadamu wa kila aina. Tayari Nimemweka kila aina ya mwanadamu katika mazingira tofauti tofauti, na katika sehemu zao, kila mmoja amekuwa akionyesha tabia zake za asili. Hakuna mtu wa kuwafunga, hakuna mtu wa kuwatongoza. Wako huru katika nafsi yao yote na lile wanalolieleza linakuja kwa wepesi. Kuna kitu kimoja tu ambacho huwaweka katika nidhamu, na hayo ni maneno Yangu. Kwa hivyo watu wengine huyasoma maneno Yangu shingo upande, bila kuyatenda kamwe, wakifanya hivyo ili kuepuka kifo tu. Kwa upande mwingine, wanadamu wengine huona ugumu kuvumilia siku bila maneno Yangu kuwaelekeza na kuwapa, kwa hivyo wao hushikilia maneno Yangu kiasili wakati wote. Muda unavyopita, wao basi hugundua siri ya maisha ya mwanadamu, hatima ya mwanadamu na thamani ya kuwa na utu. Mwanadamu si zaidi ya haya katika uwepo wa maneno Yangu, na Mimi huruhusu tu mambo yachukue mkondo wake. Sifanyi chochote kinachomlazimisha mwanadamu kuishi kulingana na maneno Yangu kama msingi wa kuwepo kwake. Na kwa hivyo wale wasiokuwa na dhamiri au thamani katika kuwepo kwao hutazama kwa kimya mambo yanavyoenda kisha wanayatupa maneno Yangu kando kwa ujasiri na kufanya vile wanavyopenda. Wanaanza kuchoshwa na ukweli na mambo yote yatokayo Kwangu. Isitoshe, wao huchoka kukaa katika nyumba Yangu. Wanadamu hawa hukaa katika nyumba Yangu kwa ufupi tu kwa ajili ya hatima zao na kuepuka adhabu, hata kama wanafanya huduma. Lakini nia zao huwa hazibadiliki, wala matendo yao. Hii huendeleza zaidi hamu zao za Baraka, hamu za njia moja kwenda katika ufalme ambako wanaweza kubakia milele, na pia njia ya kuingia mbingu ya milele. Jinsi wanavyotamani zaidi siku Yangu ije hivi karibuni, ndivyo wanavyohisi zaidi kuwa ukweli umekuwa kizingiti, kizuizi njiani mwao. Wanangoja kwa hamu kuingia katika ufalme ili wafurahie daima baraka za ufalme wa mbinguni, bila kutaka kuufuata ukweli ama kukubali hukumu na kuadibu, na zaidi ya yote, bila kuhitaji kuishi kwa utumishi katika nyumba Yangu na kufanya vile Ninavyoamuru. Wanadamu hawa hawaingii katika nyumba Yangu kuukamilisha moyo unaotaka kujua ukweli wala kufanya kazi pamoja na uongozi Wangu. Lengo lao tu ni wawe miongoni mwa wale ambao hawataangamizwa katika enzi inayofuata. Kwa hivyo nyoyo zao hazijawahi kuujua ukweli wala kujua jinsi ya kuukubali ukweli. Hii ndiyo sababu wanadamu wa aina hii hawajawahi kutia vitendoni ukweli au kujua undani wa ufisadi wao, ilhali wameishi katika nyumba yangu kama “wajakazi” mpaka mwisho. Wanangoja “kwa uvumilivu” kuja kwa siku Yangu, na hawachoki wanaporushwa huku na kule na hali ya kazi Yangu. Haijalishi bidii zao ni kubwa namna gani au ni gharama gani wamelipa, hakuna atakayeona kuwa wameteseka kwa ajili ya ukweli ama kujitoa kwa ajili Yangu. Katika mioyo yao, wanangoja kwa hamu siku ambayo Nitakomesha enzi nzee, na zaidi ya hayo, wanangoja kwa hamu kujua jinsi nguvu na mamlaka Yangu ni kuu. Kile hawajawahi kimbilia kufanya ni kujibadilisha na kufuata ukweli. Wanapenda kile kinachonichosha na kuchoshwa na kile ninachopenda. Wanangoja kwa hamu kile Ninachokuwa na kinyongo nacho lakini wakati uo huo wanaogopa kupoteza kile Ninachochukia. Wanaishi katika dunia hii yenye maovu ila hawajawahi kuwa na chuki nayo na wana hofu sana kuwa Nitaiangamiza dunia hii. Nia walizo nazo zinakanganya: Wanapendezwa na dunia hii Ninayochukia, na kwa wakati uo huo wanangoja kwa hamu Niiharibu dunia hii hivi karibuni. Kwa njia hii, wataepuka mateso ya uharibifu na wabadilishwe kuwa watawala wa enzi mpya kabla hawajapotoshwa kutoka katika njia ya kweli. Hii ni kwa sababu hawapendi ukweli na wanahofia kila kitu kitokacho Kwangu. Huenda ikawa watakuwa “watu watiifu” kwa muda mfupi kwa minajili ya kutopoteza baraka, lakini fikira zao za kungoja baraka kwa hamu na woga wao wa kuangamia na kuingia katika ziwa la moto haziwezi kukingwa kuonekana. Siku Yangu inapokaribia, hamu zao zinazidi kuimarika. Na vile janga lilivyo kubwa, ndivyo wanavyopoteza tumaini wasijue watakapoanzia ili kunifanya Nifurahi na kuzuia wasipoteze baraka ambazo wamezingoja kwa muda mrefu. Pindi mkono Wangu unapoanza kazi yake, wanadamu hawa wana hamu kuchukua hatua kuhudumu kama watangulizi. Wanafikiri tu kusonga kwa nguvu mpaka mstari wa mbele wa majeshi, wakiwa na woga mwingi kuwa Sitawaona. Wanafanya na kusema kile wanachodhani ni ukweli, bila kujua kuwa vitendo na matendo yao hayajawahi na umuhimu kwa ukweli, na kuwa hutatiza na kuingilia tu mipango Yangu. Hata ingawa wanaweza kuwa wameweka juhudi nyingi na wanaweza kuwa wa kweli katika ridhaa na nia zao kustahimili ugumu, kila wanachokifanya hakihusiani na Mimi, kwa maana Sijaona hata mara moja kwamba matendo yao yametoka kwa nia njema, na zaidi ya hayo, Sijawaona kama wameweka kitu chochote kwenye madhabahu Yangu. Hayo ndiyo matendo yao mbele Yangu kwa miaka hii mingi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu

103. Watu wengi huyashika maneno ya Mungu kuyasoma siku baada ya siku, kiasi kwamba wanaviweka akilini vifungu vyote maarufu humo kama vitu vyao vyenye thamani zaidi, na zaidi kuyahubiri maneno ya Mungu kila mahali, wakiwatolea na kuwasaidia wengine kwa njia ya maneno Yake. Wanafikiri kuwa kufanya hivi ni kuwa na ushuhuda kwa Mungu, kuwa na ushuhuda kwa maneno Yake, kwamba kufanya hivi ni kufuata njia ya Mungu; wanafikiri kuwa kufanya hivi ni kuishi kulingana na maneno ya Mungu, kwamba kufanya hivi ni kuleta maneno Yake katika maisha yao halisi, kuwa kufanya hivi kutawawezesha kupokea pongezi ya Mungu, na kuokolewa na kukamilika. Lakini, hata wanapohubiri maneno ya Mungu, hawazingatii maneno ya Mungu katika matendo, ama kujaribu kujileta sambamba na yale yanayofichuliwa katika maneno ya Mungu. Badala yake, wanayatumia maneno ya Mungu kupata upendo na imani ya wengine kwa hila, kuingia katika usimamizi wao wenyewe, na kubadhiri na kuiba sifa za Mungu. Wanatarajia, kwa ubatili, kutumia nafasi waliyopata kwa kueneza maneno ya Mungu ili kupewa kazi ya Mungu na pongezi Yake. Miaka mingapi imepita, lakini hao watu hawajaweza tu kupata pongezi ya Mungu katika hatua ya kuyahubiri maneno ya Mungu, na hawajaweza tu kugundua njia ambayo wanafaa kufuata katika hatua ya kushuhudia maneno ya Mungu, na hawajajisaidia tu ama kujipatia wenyewe katika hatua ya kuwapa na kuwasaidia wengine kwa njia ya maneno ya Mungu, na hawajaweza tu kumjua Mungu, ama kuamsha ndani yao uchaji wa kweli wa Mungu, katika hatua ya kufanya haya yote; kwa upande mwingine, kutoelewa kwao kuhusu Mungu kunakuwa hata wenye kina zaidi, kutokuwa na imani kwao kwa Mungu kunazidi kuwa na mashaka, na mawazo yao kumhusu yanatiwa chumvi zaidi. Wakijazwa na kuongozwa na mawazo yao kuhusu maneno ya Mungu, wanaonekana kuwa katika haki yao kamili, kana kwamba wanapitia ujuzi wao bila juhudi, kana kwamba wamepata kusudi lao katika maisha, wito wao, na kana kwamba wameshinda maisha mapya na kuokolewa, kana kwamba, maneno ya Mungu yakibiringika kutoka kwenye ulimi kwa kukariri, wameupata ukweli, kushika nia za Mungu, na kugundua njia ya kumjua Mungu, kana kwamba, katika wakati wa kuhubiri maneno ya Mungu, wanakuja kila wakati uso kwa uso na Mungu, pia, wana “sukumwa” kila wakati mpaka kiwango cha kilio, na kila wakati kuongozwa na “Mungu” katika maneno ya Mungu, wanaonekana kushika bila kukoma wasiwasi Wake wenye ari na nia njema, na wakati uo huo kushika wokovu wa Mungu kwa mwanadamu na usimamizi Wake, kuja kujua kiini Chake, na kuelewa tabia Yake ya haki. Msingi huu ukizingatiwa, wanaoneka kuamini hata zaidi katika uwepo wa Mungu, kujua zaidi hali ya utukufu Wake, na kuhisi hata kwa kina zaidi ukuu Wake na kuvuka mipaka Kwake. Wakiwa wameinuka katika ufahamu wao wa kijuujuu wa maneno ya Mungu, itaonekana kuwa imani yao imekua, kuamua kwao kupitia mateso kumetiwa nguvu, na maarifa yao kwa Mungu yamekuwa na kina. Ila hawajui kwamba, hadi watakapopitia maneno ya Mungu kwa kweli, maarifa yao yote kuhusu Mungu na mawazo yao kumhusu Yeye yanatoka kwa mawazo yao wenyewe ya kufikiri kwa ubunifu na kukisia. Imani yao haiwezi kusimama jaribio lolote kutoka kwa Mungu, wanachoita kiroho na kimo haviwezi kusimama chini ya majaribu ya Mungu na ukaguzi, uamuzi wao ni ngome tu iliyojengwa juu ya changarawe, na wanachoita maarifa juu ya Mungu pia sio zaidi ya ubunifu wa mawazo yao. Kwa hakika, watu hawa, ambao, ilivyokuwa, wameweka juhudi kubwa katika maneno ya Mungu, hawajawahi kutambua imani ya kweli ni nini, kujiwasilisha kwa kweli ni nini, kujali kwa kweli ni nini, ama maarifa ya kweli ya Mungu ni nini. Wanachukua nadharia, mawazo, maarifa, zawadi, utamaduni, ushirikina na hata tabia nzuri za binadamu, na kuyafanya kuwa “mtaji na silaha” za kumwamini Mungu na ufuataji wao wa Mungu, hata kuyafanya kuwa misingi ya imani yao kwa Mungu na katika kumfuata Yeye. Wakati uo huo, pia wanachukua uwekezaji msingi huu na silaha na kuyafanya kuwa hirizi ya uchawi kwa kumjua Mungu, ya kukutana na kubishana na ukaguzi wa Mungu, majaribu, kuadibu, na hukumu. Mwishowe, wanachopata bado hakijumlishi chochote zaidi ya hitimisho kumhusu Mungu zinazoegemea hisia za kidini, katika kabaila za ushirikina, na kwa yote yaliyo ya kimapenzi, ya kustaajabisha, na yenye ugumu kuelewa, na njia yao ya kujua na kumweleza Mungu imepigwa muhuri katika muundo sawa na wa wale watu wanaoamini katika Mbingu iliyo Juu pekee, ama Mtu Mzee aliye Mawinguni, wakati ukweli wa Mungu, kiini Chake, tabia Zake, miliki Zake na asili, na kadhalika, yote yanayomhusu Mungu wa kweli Mwenyewe, ni vitu ambavyo kuvijua kumekosa mshiko, havina uhusiano kabisa na viko mbali kabisa. Katika njia hii, ingawa wanaishi chini ya upaji na ustawishaji wa maneno ya Mungu, hawawezi hata hivyo kutembea kwa kweli katika njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu. Sababu ya hakika ya hii ni kwamba hawajawahi kupata kujuana na Mungu, wala hawajawahi kuwa na mawasiliano ya kweli ama ushirika Naye, kwa hivyo haiwezekani kufikia maelewano ya pamoja na Mungu, ama kuamsha ndani mwao imani halisi katika, kufuata, ama ibada ya Mungu. Kwamba wanafaa kuyahusisha maneno ya Mungu, kwamba wanafaa kumhusisha Mungu—mwelekeo huu na tabia imewahukumu kurudi mkono mtupu kutoka kwa jitihada zao, imewahukumu katika maisha yote wasiweze kutembea katika njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu. Lengo wanalolengea, na mwelekeo wanaoelekea, inamaanisha kuwa ni maadui wa Mungu milele, na kwamba hata milele hawatawahi kuweza kupokea wokovu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Dibaji

104. Katika miaka mingi ya kazi Yangu, mwanadamu amepokea vitu vingi na kujinyima vitu vingi, lakini bado Nasema kuwa mwanadamu haniamini kikamilifu. Kwa maana mwanadamu anakubali kijuujuu tu kuwa Mimi ni Mungu lakini hakubaliani na ukweli Ninaounena, sembuse kuuweka ukweli katika matendo Ninavyohitaji kwake. Hiyo ni kusema, mwanadamu anakubali tu uwepo wa Mungu, lakini sio ule wa ukweli; mwanadamu hukubali tu uwepo wa Mungu, lakini sio wa uzima; mwanadamu anakubali tu jina la Mungu, lakini sio kiini Chake. Kutokana na ari yake, mwanadamu amekuwa chukizo mbele Zangu. Kwa kuwa mwanadamu anatumia tu maneno yanayofurahisha masikio kunihadaa, na hakuna anayeniabudu kwa moyo wa kweli. Maneno yenu yanabeba majaribu ya ibilisi. Na maneno yenu ni yenye kiburi kupindukia, ni vile tu kama yamesemwa na malaika mkuu. Zaidi ya hayo, matendo yenu yamechakaa; tamaa zenu zisizo na kiasi na nia zenu zenye tamaa ni za kukera zikisikizwa. Nyote mmegeuka nondo katika nyumba Yangu, vyombo vya kukataliwa na chukizo. Kwa maana hapana kati yenu ambao ni wapenda ukweli, bali ni wanadamu wanaopenda baraka tu, walio na matamanio ya kupaa mbinguni, na ya kumwona Kristo anapoonyesha nguvu Zake duniani. Lakini mmewahi kuwaza jinsi mwanadamu kama ninyi, aliyepotoka sana, na asiyejua kabisa Mungu ni nini, angestahili kumfuata Mungu? Mnawezaje kupaa mbinguni? Mnawezaje kustahili kuuona uzuri wa ukuu usio na kifani? Vinywa vyenu vimejaa maneno ya uongo na uchafu, usaliti na kiburi. Kamwe hamjawahi kunena maneno ya ukweli Kwangu, wala maneno matakatifu, wala maneno ya kunitii baada ya kulipitia neno Langu. Hatimaye, hii imani yenu ni ya aina gani? Nyoyo zenu zimejaa tamaa na mali, mawazo yenu yamejaa mali ya kilimwengu. Kila siku, mnafanya hesabu jinsi mtakavyofaidika kutoka Kwangu, mkihesabu kiasi cha mali na vitu vya kidunia mlivyopata kutoka Kwangu. Kila siku, mnangoja baraka zaidi ziwashukie ili muweze kufurahia, hata zaidi na vyema zaidi, vitu zaidi vya raha. Vile vilivyo katika mawazo yenu kila wakati si Mimi, wala ukweli utokao Kwangu, bali ni mume (mke), mwanao, bintiyo au mlacho na kuvaa, na vile mtakavyoburudika na starehe nzuri zaidi. Hata mlishindilie tumbo lenu kwa vyakula hadi pomoni, je, si nyinyi bado ni zaidi ya maiti tu? Hata wakati ambapo, kwa nje, mnavalia mavazi ya kupendeza sana, si nyinyi bado ni maiti inayotembea isiyo na uhai? Mnafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya tumbo lenu mpaka mnapotokwa na mvi, ilhali hakuna aliye tayari kuutoa unywele mmoja kwa ajili ya kazi Yangu. Mnasafiri kila mara, mnafanya kazi na kupiga bongo kwa ajili ya miili yenu, na kwa sababu ya watoto wenu, ilhali hakuna yeyote anayeshughulika wala kufikiria kuhusu mapenzi Yangu. Ni nini ambacho bado mnatarajia kufaidi kutoka Kwangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa

105. Nimeeleza maneno mengi sana, na pia nimeeleza mapenzi Yangu na tabia, lakini hata hivyo, bado watu hawana uwezo wa kunijua Mimi na kuniamini. Au, inaweza kusemwa, bado hawana uwezo wa kunitii. Wale wanaoishi katika Biblia, wale wanaoishi katika sheria, wale wanaoishi juu ya msalaba, wale ambao wanaishi kwa mujibu wa mafundisho, wale wanaoishi miongoni mwa kazi Ninayofanya leo—yupi kati yao analingana na Mimi? Ninyi mnafikiria tu kupokea baraka na tuzo, na hamjawahi kamwe kufikiria jinsi ya kulingana na Mimi, au jinsi ya kujizuia wenyewe kutoka katika uadui na Mimi. Nimeaibishwa sana na nyinyi, kwa kuwa Nimewapa mengi sana, ilhali Mimi Nimepokea kidogo sana kutoka kwenu. Udanganyifu wenu, kiburi chenu, tamaa yenu, tamaa yenu yenye fujo, usaliti wenu, kuasi—lipi kati ya haya linaweza kujificha kutoka kwa macho Yangu? Ninyi mnanitendea hobela hobela, mnanidanganya Mimi, mnanitusi, mnanibembeleza, mnanilazimisha na kupata sadaka kutoka Kwangu kwa nguvu—ni jinsi gani tabia ya kudhuru kama hii itaepuka ghadhabu Yangu? Udhalimu wenu ni thibitisho la uadui wako Kwangu, na ni thibitisho la uwiano wenu na Mimi. Kila mmoja wenu anaamini mwenyewe akilingana na Mimi, lakini ikiwa ni hivyo, basi ni kwa nani ushahidi huu dhahiri unatumika? Mnaamini wenyewe kwamba mnao ukweli wa juu sana na uaminifu Kwangu. Mnafikiri kwamba nyinyi ni wema sana, wenye huruma sana, na mmetoa sana Kwangu. Mnafikiri kwamba mmefanya vya kutosha kwa ajili Yangu. Bado hamjawahi kulinganisha imani hizi dhidi ya tabia zenu wenyewe? Nasema mmejaa mengi ya kiburi, tamaa nyingi, wingi wa uzembe; hila mnayotumia kunidanganya ni janja sana, na mna mengi ya nia ya kudharau na mbinu ya kudharau. Uaminifu wenu pia ni mdogo, bidii yenu pia ni ndogo, na dhamiri yako hata haipo zaidi. Kuna mabaya mengi sana katika nyoyo zenu, na hakuna mtu anayeepuka kuathiriwa na hila yenu, hata Mimi mwenyewe. Mnanifungia nje kwa ajili ya watoto wenu, au waume wenu, au kwa ajili ya hifadhi zenu wenyewe. Badala ya kunijali, mnajali familia zenu, watoto wenu, hali yenu, maisha yenu ya baadaye, na kujitosheleza wenyewe. Ni lini mmewahi kuniwaza Mimi mnapozungumza au kutenda? Wakati hali ya hewa ni baridi, mawazo yenu hurejea kwa watoto wenu, waume wenu, wake wenu, au wazazi wenu. Wakati hali ya hewa ni ya joto, hata Siwezi kupata nafasi katika mawazo yenu pia. Unapotekeleza wajibu wako, wewe huwaza tu kuhusu maslahi yako mwenyewe, ya usalama wako mwenyewe binafsi, ya watu wa familia yako. Ni nini umewahi kufanya kwa ajili Yangu? Ni lini umeweza kuwaza kunihusu Mimi? Ni lini umewahi kujitoa mwenyewe, kwa gharama yoyote, kwa ajili Yangu na kazi Yangu? Uko wapi ushahidi wa uwiano wako na Mimi? Uko wapi ukweli wa uaminifu wako kwa ajili Yangu? Uko wapi ukweli wa utiifu wako Kwangu? Ni lini mujibu wako hujakuwa kwa sababu ya kupokea baraka Zangu? Mnanilaghai na kunidanganya Mimi, mnacheza na ukweli na kuficha kuwepo kwa kweli, na kuisaliti dutu ya ukweli, na mnajiweka wenyewe kwa uadui kama huu na Mimi. Basi, ni nini kinawangoja katika siku za usoni? Ninyi mnatafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, na kutafuta tu imani zisizo yakini ilhali ninyi hulingani na Kristo. Si uovu wenu utapata adhabu kama ile wanayostahili waovu? Wakati uo huo, mtagundua kuwa hakuna mtu yeyote asiyelingana na Kristo atakayeepuka siku ya ghadhabu, na mtagundua ni aina gani ya adhabu italetwa juu ya wale walio katika uadui na Kristo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

106. Katika kutafuta kwenu, mna dhana, matumaini, na siku za baadaye nyingi sana za kibinafsi. Kazi ya sasa ni ili kushughulikia tamaa yenu ya hadhi na tamaa zenu badhirifu. Matumaini, hadhi, na dhana yote ni mifano bora kabisa ya tabia ya kishetani. Sababu ambayo vitu hivi vipo katika mioyo ya watu ni kwa sababu hasa sumu ya Shetani daima inaharibu fikira za watu, na daima watu hawawezi kuondoa vishawishi hivi vya Shetani. Wanaishi katikati ya dhambi ilhali hawaiamini kuwa dhambi, na bado wao huwaza: “Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima Atupe baraka na kupanga kila kitu kwa ajili yetu ipasavyo. Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima tuwe wa cheo cha juu kuliko wengine, na lazima tuwe na hadhi zaidi na maisha zaidi ya baadaye kuliko mtu mwingine yeyote. Kwa kuwa tunaamini katika Mungu, lazima Atupe baraka bila kikomo. Vinginevyo, hakungeitwa kuamini katika Mungu.” Kwa miaka mingi, mawazo ambayo watu wametegemea kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao yamekuwa yakiharibu mioyo yao hadi kiwango ambapo wamekuwa wadanganyifu, waoga, na wenye kustahili dharau. Hawakosi tu ushupavu na uamuzi, lakini pia wamekuwa walafi, wenye kiburi, na wa kudhamiria. Kabisa wanakosa uamuzi wowote upitao sana ubinafsi, na hata zaidi, hawana ujasiri hata kidogo wa kuondoa shutuma za ushawishi huu wa giza. Fikira na maisha ya watu ni mabovu sana kiasi kwamba mitazamo yao juu ya kuamini katika Mungu bado ni miovu kwa namna isiyovumilika, na hata watu wanaponena kuhusu mitazamo yao juu ya imani katika Mungu haivumiliki kabisa kusikia. Watu wote ni waoga, wasiojimudu, wenye kustahili dharau, na dhaifu. Hawahisi maudhi kwa nguvu za giza, na hawahisi upendo kwa nuru na ukweli; badala yake, wanafanya kila wanaloweza kuvifukuza. Je, si fikira na mitazamo yenu ya sasa iko hivi tu? “Kwa kuwa ninaamini katika Mungu ninapaswa tu kumiminiwa baraka na inapaswa kuhakikishwa kwamba hadhi yangu kamwe haitelezi na kwamba inabaki kuwa juu kuliko ile ya wasioamini.” Hamjakuwa mkihodhi mtazamo wa aina hiyo ndani yenu kwa mwaka mmoja au miaka miwili tu, lakini kwa miaka mingi. Kufikiria kwenu kwa kibiashara kumekua sana. Ingawa mmewasili kwenye hatua hii leo, bado hamjaacha hadhi lakini mnapambana bila kukoma kuuliza kuihusu, na mnaichunguza kila siku, kwa hofu kubwa kwamba siku moja hadhi yenu itapotea na jina lenu litaharibiwa. Watu hawajawahi kuweka kando tamaa yao ya starehe. … Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii, ndivyo utakavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo watakavyozalimika kupitia usafishaji mkubwa. Watu kama hao hawana thamani kabisa! Lazima wshughulikiwe na wahukumiwe vya kutosha ili waachane na mambo haya kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii uzima hawawezi kubadilishwa, na wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na uingiaji, lakini badala yake unalenga tamaa badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kumkaribia Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?

107. Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Ninachunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani. Ninaangalia kila pembe ya ulimwengu, na Ninaona kuwa milima yote imefunikwa na ukungu, kwamba maji yameganda kwa ajili ya baridi, na kwamba, kwa sababu ya kuja kwa mwanga, watu wanatazama Mashariki ili wapate kuona kitu kilicho na thamani zaidi—ilhali mwanadamu bado hana uwezo wa kutambua njia ya wazi kwenye ukungu huo. Kwa sababu dunia nzima imefunikwa kwa ukungu, Ninapotazama kutoka mawinguni, kuwepo Kwangu hakujawahi kutambuliwa na mwanadamu; mwanadamu anatafuta kitu fulani duniani, anaonekana akichakura, anayo nia, inaonekana, ya kusubiri kurudi Kwangu—ilhali yeye hajui siku Yangu, na anaweza tu kutegemea mara kwa mara mwanga unaong’aa mashariki. Miongoni mwa watu wote, Ninatafuta wale wanaoupendeza moyo Wangu kwa kweli. Natembea miongoni mwa watu wote, na kuishi miongoni mwa watu wote, lakini mwanadamu yuko salama salimini duniani, na kwa hivyo hakuna wanaopendeza nafsi Yangu kwa kweli. Watu hawajui jinsi ya kuyajali mapenzi Yangu, hawawezi kuona matendo Yangu, na hawawezi kutembea katika mwanga na kumulikwa na mwanga huo. Hata ingawa mwanadamu daima anayathamini maneno Yangu, yeye hana uwezo wa kuona katika mikakati ya udanganyifu ya Shetani; kwa kuwa kimo cha mwanadamu ni kidogo sana, hana uwezo wa kufanya vile ambavyo moyo wake unatamani. Mwanadamu hajawahi kunipenda kwa dhati. Ninapompandisha, yeye hujiona asiyefaa, lakini hili halimfanyi awe na ari ya kuniridhisha. Yeye hushikilia tu nafasi Niliyompa mikononi mwake na kukichunguza; bila hisia yoyote kwa uzuri Wangu, yeye anasisitiza badala yake kujijaza na baraka za kituo chake. Je, huu sio upungufu wa mwanadamu? Milima inaposonga, je, inaweza kubadili mkondo kwa ajili ya kituo chako? Maji yanaposonga, je, yanaweza kukoma kabla ya kufikia kituo cha mwanadamu? Je, mbingu na dunia zinaweza kubadilishwa na kituo cha mwanadamu? Wakati mmoja Nilikuwa mwenye huruma kwa mwanadamu, mara kwa mara—ilhali hakuna anayependa kwa dhati wala kuthamini haya, waliyasikiliza tu kama hadithi, au waliisoma tu kama tamthilia. Je, maneno Yangu hayauguzi moyo wa mwanadamu? Je, matamshi Yangu kwa kweli hayaleti mabadiliko yoyote? Inawezekana kuwa hakuna anayeamini katika kuwepo Kwangu? Mwanadamu hajipendi mwenyewe; badala yake, anaungana na Shetani ili kunivamia Mimi, na kumtumia Shetani kama “chombo” cha kunitumikia Mimi. Nitapenyeza katika mipango yote ya Shetani, na kuwazuia watu wote wa duniani dhidi ya kukubali uongo wa Shetani, ili wasije wakaniasi Mimi kwa ajili ya kuwepo kwa Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 22

108. Watu wengi walio nyuma Yangu wanatamani baraka ya cheo, wana ulafi wa chakula, wanapenda kulala na kuushughulikia mwili kwa makini, kila mara wakiogopa kwamba hakuna njia ya kuondoka ndani ya mwili. Hawaifanyi kazi yao ya kawaida kanisani, lakini wanalitumia kanisa vibaya, au wanawaonya ndugu zao kwa maneno Yangu, wanasimama juu na kuwatawala wengine. Watu hawa huendelea kusema kwamba wanafanya mapenzi ya Mungu, wao husema kila mara kwamba ni marafiki wema wa Mungu—huu si upuuzi? Ikiwa una motisha iliyo sahihi, lakini huwezi kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, basi wewe unakuwa mpumbavu; lakini ikiwa motisha yako si sahihi, na bado unasema kwamba unamhudumia Mungu, basi wewe ni mtu anayempinga Mungu, na unastahili kuadhibiwa na Mungu! Sina huruma kwa watu wa aina hiyo! Wao ni doezi katika nyumba ya Mungu, na kila mara wao hutamani raha za mwili, na hawazingatii mambo ambayo Mungu anayapenda; kila mara wao hutafuta mambo yaliyo mazuri kwao, wala hawatilii maanani mapenzi ya Mungu, mambo yote wanayoyafanya hayaongozwi na Roho wa Mungu, kila mara wao hufanya hila dhidi ya ndugu zao na kuwadanganya, na kuwa ndumakuwili, kama mbweha ndani ya shamba la mizabibu, akiiba mizabibu kila mara na kulikanyaga na kuliharibu shamba la mizabibu. Je, watu wa aina hiyo wanaweza kuwa marafiki wema wa Mungu? Je, unastahili kupokea baraka za Mungu? Wewe huwajibiki kuhusu maisha yako na kanisa, unastahili kupokea agizo la Mungu? Ni nani anayeweza kuthubutu kumwamini mtu kama wewe? Unapohudumu kwa njia hii, je, Mungu anaweza kuthubutu kukuaminia kazi kubwa zaidi? Je, si wewe unachelewesha mambo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

109. Hawajali kama yeye ni Mungu au mwanadamu, na wao huzungumza juu ya masharti yao tu, na kutafuta kuridhisha tamaa zao wenyewe tu. Mnaponipikia, mnadai malipo ya huduma, wakati mnakimbia kwa ajili Yangu, mnadai pesa za mkimbiaji, mkinifanyia kazi mnadai ada ya kazi, mkifua nguo Zangu, mnadai ada ya kufua, wakati mnatoa kwa ajili ya kanisa mnadai malipo ya kurudisha nguvu, mkizungumza, mnadai malipo ya msemaji, mkipeana vitabu mnadai ada ya usambazaji, na wakati mnaandika mnadai malipo ya kuandika. Wale Nimehusiana nao hata hudai malipo kutoka Kwangu, na wale waliotumwa nyumbani hudai fidia kwa uharibifu wa majina yao; wale ambao hawajaoa au kuolewa hudai mahari, au fidia kwa ujana wao waliopoteza, wale wanaochinja kuku wanadai ada ya uchinjaji, wale wanaokaanga chakula wanadai ada ya kukaanga, na wale ambao hupika supu wanadai malipo pia…. Huu ndio ubinadamu wenu mkuu na wenye majivuno, na haya ndiyo matendo yanayoamrishwa na dhamiri yenu yenye joto. Hisia zenu ziko wapi? Ubinadamu wenu uko wapi? Wacha Niwaambie! Mkiendelea hivi Nitakoma kufanya kazi miongoni mwenu. Sitafanya kazi miongoni mwa wanyama waliovalia mavazi ya binadamu, Sitateseka hivyo kwa ajili ya kundi la watu ambao nyuso zao nzuri zimeficha nyoyo za uhasama, Sitavumilia kwa ajili ya kundi la wanyama ambao hawana uwezekano hata kidogo wa kuokolewa. Siku Nitakayowapa mgongo ndiyo siku mtakayokufa, ndiyo siku ambayo giza litakuja juu yenu, na ni siku mtakayoachwa na mwanga. Hebu Niwaambie! Sitakuwa mwema kamwe kwa kundi kama lenu, kundi ambalo liko chini ya hata wanyama! Kuna mipaka katika maneno na matendo Yangu, na vile ubinadamu wenu na dhamiri zilivyo, Sitafanya kazi zaidi, kwani mmekosa dhamiri, umenisababishia maumivu mengi sana, na tabia yenu ya kudharauliwa inanichukiza Mimi sana. Watu wanaokosa utu na dhamira kamwe hawatakuwa na nafasi ya wokovu; Mimi kamwe Sitawaokoa watu kama hao wasio na utu wala shukurani. Siku Yangu itakapofika, Nitanyesha mvua ya moto Wangu mkali milele juu ya wana waasi walioiamsha hasira na ghadhabu yangu kali hapo awali, Nitalazimisha adhabu yangu milele juu ya wanyama wale ambao wakati mmoja waliupa lugha chafu Kwangu na wakaniacha, Nitawachoma wakati wote kwa moto wa hasira Yangu wana wa uasi waliokula na kuishi pamoja Nami lakini hawakuniamini, na wakanitukana na kunisaliti. Nitawatia wote walionikasirisha kwa adhabu Yangu, Nitanyesha ghadhabu Yangu kwa ukamilifu juu ya wanyama hao waliotamani wakati mmoja kusimama kando Yangu kama visawe Vyangu ilhali hawakuniabudu wala kunitii, fimbo Ninayotumia kumgonga mwanadamu itaanguka juu ya wanyama hao waliofurahia utunzaji Wangu na siri Nilizonena, na waliojaribu kuchukua starehe ya mali ya dunia kutoka Kwangu. Sitamsamehe mtu yeyote anayejaribu kuchukua nafasi Yangu; Sitamsamehe yeyote anayejaribu kupokonya chakula na nguo kutoka Kwangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

110. Kile mnachoona leo ni upanga tu mkali wa kinywa Changu. Bado hamjakiona kiboko kilicho katika mkono Wangu au moto Ninaotumia kumchoma binadamu, na ndiyo maana bado mna kiburi na msio na kadiri mbele Yangu. Ndiyo maana bado mnapigana na Mimi katika nyumba Yangu, huku mkipinga kwa ulimi wa mwanadamu kile ambacho Nimenena na kinywa Changu. Binadamu haniogopi Mimi. Akiwa bado katika uhasama na Mimi hadi leo, bado haniogopi kamwe. Mnao ulimi na meno ya wale wasio na haki vinywani mwenu. Maneno na matendo yenu ni kama yale ya yule nyoka aliyemshawishi Hawa na kumfanya kutenda dhambi. Mnadai nyinyi kwa nyinyi kulipiza kisasi, na mnashindana mbele Yangu kwa ajili ya nafasi, umaarufu, na faida kwa ajili yenu wenyewe, ilhali hamjui kwamba Natazama maneno na matendo yenu kwa siri. Kabla hata ya nyinyi kuja mbele Yangu, Nimejua vina vya nyoyo zenu kabisa. Siku zote binadamu hutamani kutoroka kutoka mfumbato Wangu na kuepuka uangalizi wa macho Yangu, lakini Sijawahi kuepuka maneno au matamshi yake. Badala yake, kwa kusudio kuu huwa Nayaruhusu maneno na matendo hayo yaingie katika macho Yangu, ili Niweze kuadibu udhalimu wake na kuhukumu uasi wake. Kwa hiyo, maneno na matendo fiche ya binadamu siku zote yanawekwa mbele ya kiti Changu cha hukumu, na hukumu Yangu haijawahi kumtoka binadamu, kwa sababu uasi wake ni mwingi mno. Kazi Yangu ni kuteketeza na kusafisha maneno na matendo yote ya binadamu yaliyotamkwa na kufanywa mbele ya Roho Wangu. Kwa njia hiyo, baada ya Mimi kuondoka ulimwenguni, binadamu wataweza bado kuendeleza utiifu Kwangu, na bado watanihudumia kama vile watumishi Wangu watakatifu wanavyofanya katika kazi Yangu, wakiruhusu kazi Yangu hapa ulimwenguni iendelee mpaka siku itakapokamilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

111. Nawathamini sana wale wasio na shaka kuhusu wengine na pia nawapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Pangu wao ni waaminifu. Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine. Mnakisia iwapo Mungu anaweza kuwa kama mwanadamu: mwenye dhambi isiyosameheka, mwenye tabia ndogondogo, anayependelea na asiye na mantiki, aliyekosa hisia ya haki, mwenye mbinu ovu, mdanganyifu na mjanja, na pia anayefurahishwa na uovu na giza, na kadhalika. Si sababu ambayo mwanadamu ana mawazo kama haya kwamba hana hata ufahamu mdogo wa Mungu? Imani kama hii ni sawa na dhambi! Zaidi ya hayo, kuna hata wale wanaoamini kwamba Sifurahishwi na yeyote isipokuwa wale wanaojirairai na kujipendekeza, na kwamba wale wasio na ujuzi huu hawatakaribishwa na watapoteza nafasi yao katika nyumba ya Mungu. Je, haya ndiyo maarifa ambayo mmepata kwa miaka hii yote mingi? Ni haya ndiyo mliyoyapata? Na ufahamu wenu kunihusu hauko kwa kutoelewa kama huku tu; mbaya hata zaidi ni kukufuru kwenu Roho wa Mungu na kuitukana Mbingu. Hii ndiyo maana Ninasema kwamba imani kama yenu itawasababisha tu kupotea mbali na Mimi na kukuwa na upinzani mkubwa dhidi Yangu. Kwa miaka mingi ya kazi, mmeona ukweli mwingi, lakini mnajua kile masikio Yangu yamesikia? Ni wangapi kati yenu walio tayari kukubali ukweli? Nyote mnaamini kwamba mko tayari kulipa gharama ya ukweli, lakini ni wangapi walioteseka kweli kwa ajili ya ukweli? Yote yaliyo ndani ya mioyo yenu ni uovu, na hivyo mnaamini kwamba yeyote, bila kujali ni nani, ni mjanja na asiye mwaminifu. Hata mnaamini kwamba Mungu mwenye mwili angekuwa bila moyo wa ukarimu na upendo wema kama tu binadamu wa kawaida. Zaidi ya hayo, mnaamini kwamba tabia ya adabu na asili yenye huruma na ukarimu ziko kwa Mungu wa mbinguni pekee. Na mnaamini kwamba mtakatifu kama huyu hayuko, na kwamba giza na uovu tu ndio unaotawala duniani, ilhali Mungu ni kitu ambacho mwanadamu huwekea matumaini yake ya mazuri na mema, na mtu maarufu aliyebuniwa na mwanadamu. Ndani ya akili zenu, Mungu aliye mbinguni ni mnyoofu sana, mwenye haki, na mkubwa, anayestahili ibada na upendezewaji, lakini Mungu huyu aliye duniani ni mbadala tu na chombo cha Mungu aliye mbinguni. Mnaamini Mungu huyu hawezi kuwa sawa na Mungu wa mbinguni, na hata zaidi hawezi kutajwa kwa pumzi moja na Yeye. Ifikapo kwa ukubwa na heshima ya Mungu, ni mali ya utukufu wa Mungu aliye mbinguni, lakini ifikapo kwa tabia na upotovu wa mwanadamu, vinahusishwa na Mungu aliye duniani. Mungu aliye mbinguni daima ni mkuu, ilhali Mungu wa duniani daima ni asiye na maana, mdhaifu na asiyejimudu. Mungu aliye mbinguni haathiriwi na hisia, kwa haki tu, ilhali Mungu aliye duniani ana motisha za kibinafsi tu na Hana haki na mantiki yoyote. Mungu aliye mbinguni hana udanganyifu hata kidogo na daima ni mwaminifu, ilhali Mungu wa duniani daima ana upande mdanganyifu. Mungu aliye mbinguni anampenda sana mwanadamu, ilhali Mungu wa duniani anamjali mwanadamu isivyotosha, hata kumpuuza kabisa. Ufahamu huu usio sahihi umewekwa kwa muda mrefu kwa mioyo yenu na unaweza pia kuendelezwa mbele katika siku za usoni. Mnachukulia matendo yote ya Kristo kwa msimamo wa wadhalimu na kuhukumu kazi Yake yote na utambulisho Wake na kiini Chake kwa mtazamo wa waovu. Mmefanya kosa kubwa sana na kufanya kile ambacho hakijawahi kufanywa na wale kabla yenu. Yaani, mnamtumikia tu Mungu mkuu aliye mbinguni na taji juu ya kichwa Chake na hammshughulikii kamwe Mungu mnayemchukulia kuwa asiye na maana kabisa kiasi cha kutoonekana kwenu. Hii siyo dhambi yenu? Huu sio mfano halisi wa kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu? Mnamwabudu sana Mungu aliye mbinguni. Mnapenda sana sura zilizo kuu na kuheshimu wanaojulikana kwa ajili ya umbuji wao. Mnaamrishwa kwa furaha na Mungu Anayejaza mikono yenu na utajiri, na mnatamani sana Mungu Anayeweza kutimiza tamaa zenu zote. Yule tu msiyemwabudu ni Mungu huyu asiye mkuu; Chombo chenu tu cha chuki ni ushirikiano na huyu Mungu ambaye hakuna mwanadamu anayeweza kumchukulia kuwa mkuu. Kitu pekee ambacho hamko tayari kufanya ni kumtumikia huyu Mungu ambaye hajawahi kuwapa senti hata moja, na Yule tu msiyemtamani ni huyu Mungu asiyependeza. Mungu kama huyu hawezi kuwawezesha kupanua upeo wenu wa macho, kuhisi kana kwamba mmepata hazina, sembuse kutimiza mnachotaka. Mbona, basi, mnamfuata? Je, mmefikiria kuhusu maswali kama haya? Kile ufanyacho hakimkosei huyu Kristo tu; cha muhimu hata zaidi, kinakosea Mungu aliye mbinguni. Nadhani kwamba, haya siyo madhumuni ya imani yenu kwa Mungu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

112. Wengi wanaona afadhali washutumiwe hadi kuzimu kuliko kuongea na kutenda kwa uaminifu. Si ajabu kwamba Nina matendo mengine kwa wale ambao si waaminifu. Bila shaka, Ninaelewa ugumu mkuu mnaokumbana nao kwa kuwa binadamu waaminifu. Nyinyi wote ni werevu sana na stadi katika kupima uungwana wa mtu kwa kipimio chenu wenyewe; kwa hiyo kazi Yangu inakuwa rahisi zaidi. Na kwa sababu nyinyi mnaficha siri katika mioyo yenu, basi, Nitawatumeni, mmoja baada ya mwingine, katika janga kupitia ili “mfundishwe” kupitia moto, ili baadaye mtajitolea kabisa katika kuamini maneno Yangu. Hatimaye, Nitapokonya maneno “Mungu ni Mungu wa uaminifu,” kutoka kwa vinywa vyenu na kisha ndipo mtakapojigamba na kujitanua kifua na kulalama, “Ujanja ndio moyo wa binadamu!” Hali za akili zenu zitakuwa zipi wakati huu? Ninafikiri hamtajisahau sana na majivuno kama mlivyo sasa. Na sembuse hamtakuwa “wa maana sana kiasi cha kutoeleweka” kama mlivyo sasa. Baadhi hutenda kwa ustaarabu na huonekana hasa “wenye tabia nzuri” mbele ya Mungu, na bado wanakuwa waasi na wasiozuiliwa mbele ya Roho Mtakatifu. Je, mnaweza kumhesabu binadamu kama huyu miongoni mwa safu ya waaminifu? Kama wewe ni mnafiki na mmoja ambaye ni stadi katika kutangamana, basi Nasema kwamba bila shaka wewe ni mmoja ambaye humchezea Mungu. Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu

113. Ninaelewa kabisa udanganyifu ulio ndani ya mioyo yenu; wengi wenu hunifuata kutokana na udadisi na mmekuja kunitafuta kutokana na utupu. Wakati matakwa yenu ya tatu yanavunjwavunjwa—kwa ajili ya maisha ya amani na yenye furaha—udadisi wenu pia unatapanywa. Udanganyifu ulio ndani ya mioyo ya kila mmoja wenu wote hufunuliwa kupitia maneno na matendo yenu. Kusema kweli, nyinyi mnataka tu kujua kunihusu, hamwogopi; hamjali matamshi yenu, na mnazuia tabia zenu hata mara chache zaidi. Basi imani yenu iko vipi kwa kweli? Je, ni ya kweli? Mnatumia tu maneno Yangu kuondoa wasiwasi wenu na kupunguza uchoshi wenu, ili kujaza nafasi zilizobaki tupu katika maisha yako. Ni nani miongoni mwenu ambaye ameyatia katika vitendo? Nani ana imani ya kweli? Mnaendelea kupiga kelele kwamba Mungu ni Mungu ambaye huona ndani kabisa ya mioyo ya watu, lakini ni vipi Mungu mnayepiga kelele kuhusu mioyoni mwenu analingana na Mimi? Kwa kuwa mnapiga kelele kwa njia hii, basi kwa nini mnatenda kwa njia ile? Inawezea kuwa kwamba huu ndio upendo mnaotaka kunilipizia nao? Hakuna kiasi kidogo cha upendo kwenye midomo yenu, lakini ziko wapi dhabihu zenu, na matendo yenu mema? Isingalikua maneno yenu kuyafikia masikio Yangu, Ningaliwezaje kuwachukia sana? Ikiwa kweli mliniaminia, mngewezaje kuangukia hali kama hii ya dhiki? Mnazo sura za huzuni kwenye nyuso zenu kana kwamba mko kuzimu mkishtakiwa. Hamna uhai wowote, na mnanena kuhusu sauti yenu ya ndani kwa udhaifu; mmejawa hata na malalamiko na laana. Mlipoteza imani katika yale Nifanyayo zamani na hata imani yenu ya asili imepotea, basi mnawezaje kufuata mpaka mwisho? Mnawezaje kuokolewa kwa njia hii?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno kwa Vijana na kwa Wazee

114. Ingawaje binadamu anamsadiki Mungu, moyo wa binadamu haupo na Mungu, na hajui chochote kuhusu namna ya kumpenda Mungu, wala hataki kumpenda Mungu, kwani moyo wake haujawahi kusonga karibu na Mungu na siku zote anamuepuka Mungu. Kutokana na haya, moyo wa binadamu umekuwa mbali sana na Mungu. Kwa hivyo, moyo wake uko wapi? Kwa hakika, moyo wa binadamu haujaenda popote: Badala ya kuupatia moyo huo Mungu, au kuufichua kwa Mungu ili Aweze kuuona, amejiekea yeye mwenyewe. Hiyo ni licha ya ukweli kwamba baadhi mara nyingi wanamwomba Mungu na kusema, “Ee Bwana, utazame moyo wangu—unajua yote ninayofikiria,” na baadhi hata huapa kumruhusu Mungu kuwafikiria, kwamba waweze kuadhibiwa kama watavunja kiapo chao. Ingawaje binadamu anamruhusu Mungu kuangalia ndani ya moyo wake, hii haimanishi kwamba anaweza kutii mipango na mipangilio ya Mungu, wala kwamba ameacha hatima na matarajio yake na mambo yake yote katika udhibiti wa Mungu. Hivyo, licha ya viapo unavyotoa kwa Mungu au mwelekeo kwake Yeye, kwa macho ya Mungu moyo wako ungali umefungwa kwake Yeye, kwani unamruhusu Mungu tu kuangalia kwenye moyo wako lakini humruhusu Yeye kuudhibiti. Kwa maneno mengine, hujampa Mungu moyo wako kamwe, na unazungumza tu maneno yanayosikika kuwa matamu ili Mungu asikie; nia zako mbalimbali za kijanja, huku, unajificha kutoka kwa Mungu, unajificha usionekane na Mungu, pamoja na maajabu, njama, na mipango yako, na unashikilia matarajio na hatima yako mikononi mwako, ukiwa na hofu kubwa kwamba huenda yakachukuliwa na Mungu. Hivyo, Mungu hatazamii uaminifu wa binadamu kwake Yeye. Ingawaje Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, na Anaweza kuona kile ambacho binadamu anafikiria na anataka kufanya moyoni mwake, na Anaweza kuona ni mambo yapi yamewekwa ndani ya moyo wake, moyo wa binadamu haumilikiwi na Mungu, hajautoa ili udhibitiwe na Mungu. Hivi ni kusema, Mungu anayo haki ya kuangalia, lakini Hana haki ya kuudhibiti moyo huo. Kwenye nadharia za kibinafsi za binadamu, binadamu hataki wala hanuii kujiacha kwenye huruma za Mwenyezi Mungu. Binadamu hajajifungia tu kutoka kwa Mungu, bali kunao hata watu wanaofikiria njia za kusetiri mioyo yao, kwa kutumia mazungumzo matamu na sifa za kinafiki ili kuunda hali ya uongo na kupata uaminifu wa Mungu, na kuficha uso wao wa kweli dhidi ya kuonekana na Mungu. Nia yao ya kutomruhusu Mungu kuona ni kutoruhusu Mungu kuelewa namna walivyo kwa kweli. Hawataki kuitoa mioyo yao kwa Mungu lakini wanajihifadhia wao wenyewe. Maandishi madogo ya haya ni kwamba kile ambacho binadamu anafanya na kile ambacho anataka kimepangiliwa chote, kikapigiwa hesabu, na kuamuliwa na binadamu mwenyewe; haihitaji kushiriki au kuingilia kati kwa Mungu, na isitoshe hahitaji mipango na mipangilio ya Mungu. Hivyo, iwapo ni kuhusiana na amri za Mungu, agizo Lake, au mahitaji ambayo Mungu anamwekea binadamu, uamuzi wa binadamu unatokana na nia na maslahi yake mwenyewe, katika mazingira na hali yake mwenyewe ya wakati huo. Siku zote binadamu anatumia maarifa na maono ambayo amezoeana nayo, na akili zake binafsi ili kuamua na kuchagua njia anayofaa kutembelea na haruhusu uingiliaji kati au udhibiti wa Mungu. Huu ndio moyo wa binadamu ambao Mungu anaona.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

115. Watu wengi wangependa kunipenda kwa kweli, lakini kwa sababu mioyo yao si yao wenyewe, hawawezi kujidhibiti wenyewe; watu wengi hunipenda kwa kweli katika majaribio Ninayotoa, lakini hawana uwezo wa kuelewa kwamba Mimi kwa kweli Nipo, na wananipenda tu katikati ya utupu; na si kwa sababu ya kuwepo Kwangu halisi; watu wengi, baada ya kuweka nyoyo zao mbele Zangu, hawazijali, na hivyo nyoyo zao zinanyakuliwa na Shetani wakati wowote anapopata nafasi, na baada yake huniacha; watu wengi hunipenda kwa dhati Ninapotoa maneno Yangu, lakini hawathamini maneno Yangu katika roho zao, badala yake wakiyatumia kwa kawaida kama mali ya umma na kuyatupa yalipotoka wakati wowote wanapotaka. Mwanadamu hunitafuta akiwa na maumivu, na hunitazamia akiwa na majaribu. Wakati kuna amani yeye hunifurahia, wakati wa hatari yeye hunikana, wakati ana kazi nyingi yeye hunisahau, na asipokuwa na kitu cha kufanya yeye hufanya vitu kwa namna isiyo ya dhati—lakini kamwe hakuna yeyote ambaye amenipenda katika maisha yake yote. Ningependa mwanadamu awe mwenye bidii mbele Zangu: Mimi Simuombi chochote, ila tu watu wote wanichukulie kwa umakini, kwamba, badala ya kunirairai, waniruhusu kurudisha uaminifu wa mwanadamu. Nuru Yangu, mwangaza na gharama ya juhudi Zangu huenea kwa watu wote, ilhali hivyo pia ukweli halisi wa kila tendo la mwanadamu huenea kwa watu wote, kama ufanyavyo wao kunidanganya. Ni kama kwamba viungo vya udanganyifu wa mwanadamu vimekuwa naye tangu tumboni mwa mamake, kama kwamba amekuwa na mbinu hizi maalum za kuhadaa tangu kuzaliwa kwake. Kuzidisha, hajawahi kufichua siri yake; hakuna mwanadamu aliyewahi kutambua chanzo cha ujuzi huu wa udanganyifu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu anaishi katika udanganyifu bila kujua, na ni kana kwamba yeye hujisamehe mwenyewe, kana kwamba ni mipango ya Mungu na sio yeye kunidanganya. Je, hiki sicho chanzo halisi cha mwanadamu kunidanganya? Je, huu sio mpango wake wa ujanja? Sijawahi kuchanganywa na ushawishi na hila za mwanadamu, kwa maana Mimi Nilishatambua kiini chake muda mrefu uliopita. Nani anayejua kiasi cha uchafu ulio katika damu yake, na kiasi gani cha sumu ya Shetani kimo ndani ya mafupa yake? Mwanadamu anapata uzoefu wa sumu hii kila uchao, hata anakosa busara ya kufahamu maafa ya Shetani na hivyo hana nia ya kutambua “sanaa ya uwepo wa afya.”

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 21

116. Wanadamu wote ni viumbe wasio na ufahamu kujihusu, na hawezi kujijua mwenyewe, yeye hata hivyo anajua kila mwanadamu mwingine kama kiganja cha mkono wake, kana kwamba watu wengine wote wamepitia ukaguzi wake na kupokea kibali chake kabla waseme au kufanya chochote, na hivyo ionekane kama yeye amewapima kikamilifu wengine wote mpaka katika hali yao ya kisaikolojia. Binadamu wote wako namna hii. Mwanadamu ameingia katika Enzi ya Ufalme leo hii, lakini asili yake bado haijabadilika. Yeye bado anafanya kama Ninavyofanya akiwa mbele Yangu, lakini nyuma Yangu anaanza kufanya “shughuli” zake mwenyewe za kipekee. Hata hivyo, mara hiyo inapokamilika na anarudi mbele Yangu tena, yeye huwa kama mwanadamu tofauti, akiwa na hali ya utulivu safihi, hali yake ni shwari, na mpigo wa moyo wake ni mtulivu. Je, si hili ndilo hasa hufanya mwanadamu kudharauliwa? Ni watu wangapi huvaa sura mbili tofauti kabisa, moja mbele Yangu na nyingine nyuma Yangu? Wangapi kati yao ni kama wanakondoo wachanga mbele Yangu lakini nyuma Yangu hugeuka na kuwa chui wabaya wenye milia wakali kinyama, na kisha kugeuka ndege wadogo wakirukaruka huku na kule kwa furaha milimani? Ni wangapi huonyesha lengo na uamuzi mbele Yangu? Ni wangapi huja mbele Zangu, kutafuta maneno Yangu kwa kiu na hamu lakini, nyuma Yangu, kukerwa nayo na kuyaacha, kana kwamba maneno Yangu ni mzigo unaosumbua? Mara nyingi, Nikiona jamii ya binadamu ikipotoshwa na adui Yangu, Mimi Nimeacha kuweka matumaini Yangu katika mwanadamu. Mara nyingi, Nikiona mwanadamu akija mbele Zangu kwa machozi akiomba msamaha, lakini kwa sababu ya kutojiheshimu kwake, utundu wake usiorekebika, Nimefunga macho Yangu kwa vitendo vyake kwa hasira, hata wakati moyo wake ni wa kweli na nia yake ni ya dhati. Mara nyingi, Naona mwanadamu akiwa na uwezo wa kuwa na imani ya kushirikiana na Mimi, ambaye, wakati ako mbele Yangu, anaonekana kuwa katika kumbatio Langu, akionja joto lake. Mara nyingi, kwa kuona upole, uchangamfu, na uzuri wa watu Wangu Niliowachagua, katika Moyo wangu Mimi daima Nimekuwa na furaha kwa sababu ya mambo haya. Binadamu hawajui jinsi ya kufurahia baraka Nilizowaamulia kabla katika mikono Yangu, kwa sababu wao hawajui ni nini hasa maana ya baraka au mateso. Kwa sababu hii, wanadamu wako mbali na kweli katika jitihada zao za kunitafuta. Kama hakungekuwa na kesho, ni yupi kati yenu mliosimama mbele Yangu atakuwa safi kama theluji na asiye na lawama kama jiwe la thamani? Hakika upendo wako Kwangu si kitu ambacho kinaweza kubadilishwa kwa mlo wenye ladha, au suti yenye ufahari, au ofisi ya juu na mishahara mikubwa? Au inaweza kubadilishwa na upendo ambao wengine wako nao kwako? Hakika, kupitia majaribu hakutawafukuza wanadamu waache upendo wao Kwangu? Hakika, mateso na dhiki hayatasababisha mwanadamu alalamike dhidi ya kile Nimepanga? Hakuna mwanadamu aliyewahi kweli kufahamu upanga ulio katika kinywa Changu: Yeye anajua maana yake ya juu bila kufahamu undani wake. Kama wanadamu wangeweza kweli kuona ukali wa upanga Wangu, wangekimbia kwa hofu hadi ndani ya mashimo kama panya. Kwa sababu ya kutokuwa kwao na hisia, wanadamu hawaelewi kitu chochote cha maana halisi ya maneno Yangu, na hivyo wao hawana kidokezo kuhusu jinsi maneno Yangu ni yenye kuogofya, au kiasi gani asili yao imefichuliwa, na ni kiasi gani cha upotovu wao umepokea hukumu, ndani ya maneno hayo. Kwa sababu hii, kulingana na mawazo yao yasiyo kamili kuhusu maneno Yangu, watu wengi wamechukua msimamo vuguvugu na usio wa kuwajibika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 15

117. Katika enzi zote, wengi wametoweka duniani kwa taabu, na kusita, na wengi wamekuja duniani kwa matumaini na imani. Nimeandaa kuja kwa wengi, na pia Nimewaondoa wengi. Watu wengi wamepitia mikono Yangu. Roho nyingi zimetupwa Kuzimu, wengi wameishi katika mwili, na wengi wamekufa na wamezaliwa upya duniani. Hata hivyo kamwe hakuna yeyote kati yao aliyepata nafasi ya kufurahia baraka za ufalme leo. Mimi nimewapa wanadamu mengi sana, lakini wamepata kidogo, lakini kwa sababu mashambulizi ya jeshi la Shetani imewafanya wasiweze kufurahia utajiri Wangu wote. Amekuwa tu na bahati nzuri ya kuangalia juu, lakini hajawahi kuwa na uwezo wa kujifurahisha kikamilifu. Mwanadamu hajawahi gundua nyumba ya hazina mwilini mwake ili kupokea utajiri wa mbinguni, kwa hivyo amepoteza baraka ambazo Nimempa. Je, si roho ya mwanadamu ndio haswa uwezo wa kumuunganisha na Roho Wangu? Mbona mwanadamu hajawahi Kunihusisha na roho yake? Mbona ananikaribia kimwili na asiweze kunikaribia kiroho? Je, sura Yangu ya kweli ni ya kimwili? Mbona mwanadamu hatambui kiini Changu? Kuna uwezekano kuwa hakujawahi kuonekana ishara yoyote Yangu ndani ya roho ya mwanadamu? Je, Nimetoweka kabisa katika roho ya mwanadamu? Ikiwa mwanadamu hataingia katika ulimwengu wa kiroho, atawezaje kufahamu nia Zangu? Je, kuna chochote machoni mwa mwanadamu ambacho kinaweza penyeza moja kwa moja mpaka ulimwengu wa kiroho? Ni mara nyingi Nimemwita mwanadamu kwa Roho Wangu, lakini matendo yake huwa ni kama amechomwa kisu na Mimi, anahusiana nami kwa umbali, katika hofu kubwa kuwa Nitamwongoza kwenda ulimwengu mwingine. Kwa mara nyingi Nimepeleleza ndani ya moyo wa mwanadamu, lakini anabaki bila ufahamu kabisa, akiwa na hofu kubwa kabisa kuwa Nitaingia nyumbani mwake na kuchukua fursa hiyo kumnyang’anya mali yake yote. Kwa hivyo, ananifungia nje, kuniacha bila chochote ila mlango uliofungwa na kukazwa na kuniacha nje kwenye baridi. Ni mara nyingi mwanadamu ameanguka na Nimemwokoa, lakini baada ya kuamka ananiacha mara moja, bila kuguswa na upendo Wangu, mwanadamu kunipiga macho ya hadhari; Sijawahi pasha joto moyo wa mwanadamu. Mwanadamu ni kiumbe kikatili kisichokuwa na hisia. Hata kama amepashwa joto na kumbatio Langu, kamwe hajawahi guswa na jambo hili. Mwanadamu ni kama kiumbe katili cha mlimani. Hajawahi thamini upendo Wangu wa binadamu. Hana nia ya kunikaribia, akipendelea kukaa katika milima, ambapo anavumilia tishio la wanyama pori—lakini bado hana nia ya kuchukua makao ndani Yangu. Simshawishi mwanadamu yeyote: Ninafanya tu kazi Yangu. Siku itawadia ambapo mwanadamu ataogelea kuja upande Wangu kutoka katikati ya bahari kuu, ili aweze kufurahia mali yote ya dunia na kuacha hatari ya kumezwa na bahari.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 20

118. Imani yenu ni ya kupendeza sana; mnasema kwamba mko tayari kutumia maisha yenu yote kwa ajili ya kazi Yangu, na kwamba mko tayari kutoa maisha yenu kwa ajili ya kazi hiyo, lakini tabia zenu hazijabadilika sana. Mnazungumza tu kwa kiburi, licha ya ukweli kwamba tabia yenu halisi ni mbovu sana. Ni kana kwamba ndimi na midomo ya watu iko mbinguni lakini miguu yao iko chini duniani, na kwa sababu hiyo, maneno na matendo yao na sifa zao bado ni mbovu na zisizoheshimika. Sifa zenu zimeharibiwa, tabia yenu imepotoka, njia yenu ya kuzungumza ni duni, na maisha yenu ni yenye kustahili dharau; hata ubinadamu wenu wote umezama katika hali duni ya chini kabisa. Ninyi ni wenye mawazo finyu kuhusu wengine, na ninyi hubishana kuhusu kila jambo dogo. Ninyi hugombana kuhusu heshima na hadhi zenu wenyewe, hadi kufikia kiwango ambapo mko tayari kushuka kuzimuni na kuingia kwenye ziwa la moto. Maneno na matendo yenu ya sasa yanatosha Mimi kubaini kwamba ninyi ni wenye dhambi. Mitazamo yenu kwa kazi Yangu inatosha Mimi kubaini kuwa ninyi ni wadhalimu, na tabia zenu zote zinatosha kuonyesha kwamba ninyi ni watu wachafu mliojaa machukizo. Maonyesho yenu na kile mnachofichua vinatosha kusema kwamba ninyi ni watu ambao mmekunywa damu ya roho wachafu hadi mkatosheka. Kuingia katika ufalme kunapotajwa, hamfichui hisia zenu. Je, mnaamini ya kwamba jinsi mlivyo sasa inatosha kwa ninyi kupita katika lango la kuingia katika ufalme Wangu wa mbinguni? Je, mnaamini ya kwamba mnaweza kuingia katika nchi takatifu ya kazi na maneno Yangu, bila maneno na matendo yenu wenyewe kujaribiwa na Mimi kwanza? Ni nani anayeweza kunihadaa? Tabia na mazungumzo yenu yenye kustahili dharau na yaliyo duni yanaweza kuepukaje macho Yangu? Maisha yenu yamebainiwa na Mimi kuwa maisha ya kunywa damu na kula nyama ya roho hao wachafu kwa sababu ninyi huwaiga mbele Yangu kila siku. Mbele Yangu, tabia yenu imekuwa mbaya hasa, kwa hiyo Ninawezaje kukosa kuwaona kuwa wenye kuchukiza? Maneno yenu yana uchafu wa roho wachafu: Mnabembeleza, kuficha na kujipendekeza kama tu wale wanaoshiriki katika uchawi na kama wale walio wadanganyifu na wanaokunywa damu ya wadhalimu. Maonyesho yote ya mwanadamu ni dhalimu mno, kwa hivyo watu wote wanaweza kuwekwaje katika nchi takatifu ambako wenye haki wako? Je, unafikiri kwamba hiyo tabia yako yenye kustahili dharau inaweza kukubainisha kama mtakatifu ikilinganishwa na wale wadhalimu? Ulimi wako ulio kama wa nyoka hatimaye utauangamiza huu mwili wako ambao huleta uharibifu na kutekeleza machukizo, na hiyo mikono yako iliyojaa damu ya roho wachafu pia hatimaye itaipeleka roho yako jahannamu. Basi, kwa nini huipokei kwa furaha nyingi fursa hii ili uitakase mikono yako iliyojaa uchafu? Na kwa nini huchukui fursa hii kwa manufaa yako uukate huo ulimi wako unaozungumza maneno ya kudhulumu? Je, inawezekana kwamba uko tayari kuteseka katika moto wa jahannamu kwa ajili ya mikono, ulimi na midomo yako? Mimi huuchunga moyo wa kila mtu kwa macho yote mawili, kwa sababu muda mrefu kabla Niwaumbe wanadamu, Nilikuwa nimeifumbata mioyo yao mikononi Mwangu. Nilikuwa nimeibaini mioyo ya watu kitambo, kwa hiyo mawazo yao yangeyaepukaje macho Yangu? Muda utakosaje kuwa umewaishia wa kuepuka kuchomwa na Roho Wangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!

119. Midomo yako ni mikarimu zaidi kuliko njiwa, lakini moyo wako ni mwovu zaidi kuliko yule nyoka wa zamani. Midomo yako ni ya kupendeza hata kama wanawake wa Lebanoni, lakini moyo wako si mwema zaidi kuliko yao, na hakika hauwezi kulinganishwa na uzuri wa Wakanaani. Moyo wako ni mdanganyifu mno! Vitu Ninavyochukia ni midomo na mioyo ya wadhalimu tu, na matakwa Yangu kwa watu si ya juu zaidi ya yale Ninayotarajia kutoka kwa watakatifu hata kidogo; ni kwamba tu Natiwa kinyaa kwa ajili ya matendo maovu ya wadhalimu, nami Natumai kwamba waweze kutupilia mbali uchafu wao na kutoroka kutoka katika hatari waliyomo sasa ili waweze kusimama kutoka kwa hao wadhalimu na wawe watakatifu na kuishi na wale ambao ni wenye haki. Ninyi mko katika hali sawa na Yangu, lakini mmejaa uchafu; hamna hata mfano kidogo zaidi wa asili wa wanadamu walioumbwa hapo mwanzo. Aidha, kwa sababu kila siku mnaiiga mifano ya hao roho wachafu, mkifanya kile wanachofanya na kusema kile wanachosema, kila sehemu yenu—hata ndimi na midomo yenu—imelowezwa katika maji yao machafu, kiasi kwamba mmejaa madoa kama hayo kabisa, na hakuna sehemu yenu hata moja inayoweza kutumika kwa ajili ya kazi Yangu. Ni jambo la kusikitisha sana! Mnaishi katika dunia ya farasi na ng’ombe kabisa, lakini kwa kweli hamhisi kufadhaishwa; mmejaa furaha na mnaishi kwa uhuru na bila matatizo. Mnaogelea huku na kule katika maji hayo machafu, lakini kwa kweli hamtambui ya kwamba mmeingia katika hatari kama hiyo. Kila siku, mnaandamana na roho wachafu na kuingiliana na “kinyesi.” Maisha yenu ni ya kishenzi sana, ilhali hujui kweli kwamba haupo katika ulimwengu wa wanadamu kabisa na kwamba hujidhibiti. Je, hujui kwamba maisha yako yalikandamizwa na roho hao wachafu zamani, au kwamba tabia yako ilishachafuliwa na maji machafu zamani? Je, unafikiri kwamba unaishi katika paradiso ya duniani, na kwamba uko katikati ya furaha? Je, hujui kwamba umeishi maisha pamoja na roho wachafu, na kwamba umeishi pamoja kwa amani na kila kitu ambacho wamekuandalia? Jinsi unavyoishi inawezaje kuwa na maana yoyote? Maisha yako yanawezaje kuwa na thamani yoyote? Umekuwa ukikimbia huku na kule kwa ajili ya wazazi wako, wazazi wa roho wachafu, lakini hujui kweli kuwa wale wanaokutega ni hao wazazi wa roho wachafu waliokuzaa na kukukela. Aidha, huna habari kwamba kweli ni wao ndio waliokupa uchafu wako wote; kile unachojua tu ni kwamba wanaweza kukuletea “furaha”, hawakuadibu, wala hawakuhukumu, na hususani hawakulaani. Hawajawahi kukulipukia kwa hasira, lakini wanakutendea kwa upendo na fadhila. Maneno yao huusitawisha moyo wako na kukuvutia sana kiasi kwamba unakanganyikiwa, na bila kutambua, unafyonzwa na unakuwa tayari kuwahudumia, ukigeuka kuwa njia yao ya kutoka na kuwa mtumishi wao. Huna malalamiko hata kidogo, bali uko tayari kuwafanyia kazi kama mbwa, kama farasi; unadanganywa na wao. Kwa sababu hii, huna majibu yoyote kabisa kwa kazi Ninayoifanya. Si ajabu kwamba kila wakati wewe hutaka kuponyoka kutoka Kwangu kwa siri, na si ajabu kwamba kila wakati wewe hutaka kutumia maneno matamu kupata kibali kutoka Kwangu kwa njia danganyifu. Kama inavyotokea, tayari ulikuwa na mpango mwingine, na mpangilio mwingine. Unaweza kuona matendo Yangu kidogo kama mwenye Uweza, lakini huna ufahamu hata kidogo kuhusu hukumu na kuadibu Kwangu. Hujui kuadibu Kwangu kulianza lini; unajua tu jinsi ya kunidanganya—lakini hujui kwamba Sitastahimili ukiukaji wowote kutoka kwa mwanadamu. Kwa kuwa tayari umeweka uamuzi wako kunitumikia Mimi, sitakuacha uende. Mimi ni Mungu anayechukia uovu, na Mimi ni Mungu ambaye ana wivu kwa mwanadamu. Kwa kuwa tayari umewekelea maneno yako juu ya madhabahu, Sitakuvumilia wewe kuhudumia mabwana wawili. Je, ulifikiri ungepata upendo mwingine baada ya kuweka maneno yako juu ya madhabahu Yangu, baada ya kuyaweka mbele ya macho Yangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo? Je, ulidhani kwamba ungeweza kuweka nadhiri kikawaida, kula kiapo Kwangu Mimi na ulimi wako? Je, ungewezaje kula kiapo kwa kiti Changu cha enzi, Aliye Juu Zaidi? Je, ulifikiri kwamba viapo vyako vilikuwa tayari vimekufa? Nawaambia, hata kama miili yenu ikifa, viapo vyenu haviwezi kufa. Hatimaye, Nitawahukumu kwa msingi wa viapo vyenu. Lakini mnadhani kwamba mnaweza kuweka maneno yenu mbele Yangu ili kunivumilia Mimi na kwamba mioyo yenu inaweza kuwatumikia pepo wachafu na pepo wabaya. Je, hasira Yangu ingewezaje kuwavumilia hao watu mithili ya mbwa na nguruwe wanaonidanganya? Lazima Nitekeleze amri Zangu za kiutawala, na kuwapokonya kutoka kwa mikono ya pepo wachafu wale wote wenye fukuto, “wacha Mungu” ambao wanaamini katika Mimi “kunitumikia” Mimi kwa njia ya mpango, kuwa ng’ombe Wangu, kuwa farasi Wangu na kudhibitiwa na Mimi. Nitakufanya ushike uamuzi wako wa awali na kunitumikia Mimi tena. Siwezi kuvumilia kiumbe yeyote kunidanganya Mimi. Je, ulifikiria kwamba ungeweza kufanya maombi tu kiutukutu na kudanganya kiutukutu mbele Yangu? Je, ulifikiri kwamba Mimi sikuwa nimesikia au kuona maneno na matendo yako? Je, maneno yako na matendo yako yangekosaje kuwa katika mtazamo Wangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!

120. Nimekuwa miongoni mwenu, Nimeshirikiana nanyi kwa majira kadhaa ya kuchipua na kwa majira kadhaa ya kupukutika, Nimeishi kati yenu kwa muda mrefu—ni kiasi gani cha tabia yenu ya kudharaulika kimeponyoka mbele ya macho Yangu? Maneno yenu hayo ya dhati daima yarudisha mwangwi ndani ya masikio Yangu; mamilioni na mamilioni ya matarajio yenu yamewekwa juu ya madhabahu Yangu—hayawezi hata kuhesabiwa. Lakini kwa kujitolea kwako na kile mnachokitumia, hakuna hata kidogo. Hakuna hata tone dogo la uaminifu wenu kwenye madhabahu Yangu. Yako wapi matunda ya imani yenu Kwangu? Mmepokea neema isiyo na mwisho kutoka Kwangu na mmeona mafumbo yasiyo na mwisho kutoka mbinguni, na Nimewaonyesha hata miale ya mbinguni lakini Sijawahi kuwa na moyo wa kuwachoma, na ni kiasi gani mmenipa Mimi kama malipo? Je, mko radhi kunipa Mimi kiasi gani? Kama umeshikilia chakula Nilichokupa, unageuka na kunitolea Mimi, hata ukisema kuwa ni kitu ambacho umepata kama malipo kwa jasho la kazi yako ngumu, kwamba unatoa yote uliyo nayo Kwangu. Je, unawezaje kukosa kujua kwamba “michango” yako Kwangu ni vitu vyote vilivyoibwa kutoka kwa madhabahu Yangu? Na sasa unavitoa Kwangu—si wewe unanidanganya Mimi? Unawezaje kukosa kujua kuwa vitu Ninavyovifurahia leo ni matoleo yote juu ya madhabahu Yangu, na sicho kile ulichokichuma kama malipo ya kazi yako ngumu halafu ukanitolea Mimi? Kwa kweli mnathubutu kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa hiyo ni kwa jinsi gani Ninaweza kuwasamehe? Ninawezaje kuvumilia hili zaidi? Nimewapa kila kitu. Nimewafungulia kila kitu, Nikakimu mahitaji yenu, na kuyafungua macho yenu, lakini bado mnanidanganya Mimi kwa njia hii, mkipuuza dhamiri yenu. Bila ubinafsi Nimewapa kila kitu, ili kwamba hata kama mnateseka, mmepata kutoka Kwangu kila kitu Nilichokileta kutoka mbinguni. Lakini hamna kujitolea kamwe, na hata kama mna mchango mdogo, mnalipa deni baada ya hapo. Je, si mchango wako utakuwa bure? Kile ambacho umenipa si chochote isipokuwa chembe moja ya mchanga, lakini kile ulichouliza kutoka Kwangu ni tani moja ya dhahabu. Je, si wewe unakuwa muhali? Ninafanya kazi miongoni mwenu. Hakuna kabisa dalili ya asilimia kumi ambayo Ninapaswa kupata, sembuse dhabihu za ziada. Zaidi ya hayo, asilimia kumi inayochangwa na wale ambao ni wacha Mungu inachukuliwa na wale waovu. Je, si nyinyi wote mmetawanyika kutoka Kwangu? Je, si nyinyi nyote mna uhasama na Mimi? Je, si nyinyi nyote mnaharibu madhabahu Yangu? Je, mtu wa aina hii anawezaje kuonekana kama hazina machoni Pangu? Je, si yeye ni nguruwe, mbwa ambao Ninawachukia? Ningewezaje kurejelea uovu wenu kama hazina?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!

121. Kuna njia nyingi zaidi ya ufahamu wenu, maneno mengi msiyoelewa. Ninyi ni wapumbavu sana. Nazijua hali zenu na upungufu wenu vema. Kwa hivyo, ingawa kuna maneno mengi ambayo hamtaweza kuyaelewa, bado Ninataka kuwaambia ukweli huu wote ambao hamjawahi kuuchukua—kwa kuwa kila mara Ninahofu iwapo, katika hali yenu ya sasa, mtaweza kusimama na kutoa ushuhuda Kwangu. Sio kwamba Nawadhalilisha. Nyote mmekuwa wanyama ambao hawajapitia mafunzo Yangu ya rasmi, na hili ni jambo ambalo linaleta shauku kuhusu kiasi cha utukufu ulio ndani yenu. Ingawa Nimetumia nguvu nyingi kushughulika juu yenu, inaonekana kuwa vipengele vizuri ndani yenu havipo kabisa, ilhali dalili za uovu zinaweza kuhesabika kwa vidole na zinatumika tu kama shuhuda za kumwaibisha Shetani. Takriban kila kitu kingine ndani yenu ni sumu ya Shetani. Mnaonekana Kwangu ni kama ambao mmepita kiwango cha kuokolewa. Kama mambo yalivyo, Naziangalia baadhi ya maonyesho na mienendo yenu, na hatimaye, Najua vimo vyenu halisi. Hiyo ndiyo maana Nina wasiwasi kwa sababu yenu: Akiachwa kuishi maisha peke yake, je, mwanadamu atapata kuwa bora ikilinganishwa na hali ilivyo sasa? Je, hamna wasiwasi kuhusu hali zenu za kitoto? Mnaweza hakika kuwa kama watu wateule wa Uyahudi, kuwa waaminifu Kwangu pekee Yangu katika kila hali? Kile mnachodhihirisha sio mchezo wa watoto ambao wametangatanga kutoka wazazi wao, bali ni unyama unaoonekana katika wanyama ambao wako mbali na mjeledi wa mchungaji wao. Mnapaswa kujua hali yenu halisi, ambayo pia ni udhaifu mlio nao nyote, ambao ni ugonjwa mlio nao nyote. Kwa hivyo ombi Langu la pekee kwenu ni kwamba muwe na ushahidi Kwangu. Msije katika hali yoyote kuyaruhusu maradhi ya zamani kuchipuka tena. Jambo la muhimu zaidi ni kutoa ushuhuda. Hicho ndicho kiini cha kazi Yangu. Mnafaa kuyakubali maneno Yangu jinsi Maria alivyokubali ufunuo wa Yehova uliomjia kupitia kwenye ndoto, kuamini na kisha kutii. Hili pekee ndilo linakubalika kama kuwa mtakatifu. Kwa maana ni ninyi ndio mnasikia neno Langu zaidi, na ambao wamebarikiwa zaidi na Mimi. Ninawapa mali Yangu yote ya thamani, kuwakabidhi kila Nilicho nacho. Hali yenu na ile ya Wayahudi, hata hivyo, ni tofauti kabisa, ni kama nchi mbili tofauti. Lakini mkilinganishwa nao, mnapokea baraka nyingi zaidi yao. Huku wao wakisubiri kwa hamu ili kujitokeza Kwangu, muda mwingi Nimekuwa na ninyi, kutumia utajiri Wangu kwa pamoja. Kwa ulinganisho, ni nini kinachowapa haki ya kunifokea na kuzozana na Mimi na kudai sehemu za mali Yangu? Hampati vya kutosha? Ninawapa vingi sana, lakini Mnachonipa ni huzuni wa kuvunja moyo na dhiki na chuki isiyokomeshwa na kutoridhika. Mnakuwa wazushi sana, ilhali bado mnaiamsha huruma Yangu. Kwa hivyo sina la kufanya ila kuizima chuki Yangu yote na kunena kupinga Kwangu kwenu tena na tena. Katika hii miaka elfu kadhaa ya kazi Yangu, Sikuwa Nimewahi kuleta pingamizi kwa mwanadamu awali kwa kuwa Nilikuwa Nimegundua kwamba katika historia ya kukua kwa mwanadamu, wale waongo zaidi miongoni mwenu ndio wanaofahamika zaidi. Wao ni kama urithi wa thamani ambao umeachiwa wewe na “babu” maarufu wa zama za kale. Jinsi gani Ninavyochukia wale nguruwe na mbwa ambao wana upungufu wa ubinadamu. Hamna hisia kabisa! Tabia zenu ni zenye uovu sana! Mioyo yenu ni migumu mno! Iwapo Ningepeleka haya maneno Yangu na hii kazi Yangu kwa Wayahudi, Ningekuwa nimeshapata utukufu muda mrefu uliopita. Lakini sio hivyo miongoni mwenu. Miongoni mwenu kuna tu kutojali kwa kikatili, madharau yenu, na visingizio vyenu. Hamna hisia na hamna thamani yoyote kabisa!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufahamu Wako Kumhusu Mungu Ni Upi?

122. Tafakarini kuhusu siku za nyuma: Ni lini macho Yangu yamekuwa na hasira, na sauti Yangu kuwa kali, kwenu? Ni wakati upi Nimegombana nanyi? Ni wakati upi Nimewakaripia bila mantiki? Ni wakati upi Nimewakemea usoni mwenu? Je, si ni kwa ajili ya kazi Yangu ndio kwamba Mimi namwomba Baba Yangu kuwaweka mbali na majaribu? Kwa nini mnanitendea Mimi hivi? Je, Nimewahi kutumia mamlaka Yangu kuipiga miili yenu? Kwa nini mnanilipa Mimi kwa njia hii? Baada ya ninyi kuwa moto na baridi Kwangu, nyinyi si moto wala baridi, na kisha mnajaribu kunirairai Mimi na kuficha mambo kutoka Kwangu, na vinywa vyenu vimejaa mate ya wasio haki. Je, mnafikiri kuwa ndimi zenu zinaweza kumdanganya Roho Wangu? Je, mnafikiri kwamba ndimi zenu zinaweza kuepuka ghadhabu Yangu? Je, mnafikiri kuwa ndimi zenu zinaweza kupitisha hukumu kwa matendo Yangu, Yehova, jinsi zinavyopenda? Je, Mimi ni Mungu ambaye mwanadamu hupishia hukumu? Ningewezaje kuruhusu buu dogo linikufuru hivyo? Ningewezaje kudai wana wa uasi kuwa miongoni mwa baraka Zangu za milele? Maneno na matendo yenu kwa muda mrefu yamewafichua na kuwahukumu. Wakati Nilieneza mbingu na kuumba vitu vyote, Sikuruhusu kiumbe yeyote kushiriki atakavyo, sembuse kuruhusu jambo lolote kuvuruga kazi Yangu na usimamizi Wangu, vile linavyopenda. Sikuvumilia mtu au kitu chochote; Ningewezaje kuwaacha walio wakatili na wa kinyama Kwangu? Ningewezaje kuwasamehe wale ambao wanaasi dhidi ya maneno Yangu? Ningewezaje kuwaacha wanaoniasi? Je, majaliwa ya mwanadamu hayako katika mikono Yangu, Mwenyezi? Ningeuchukua vipi udhalimu wako na uasi kama vitu vitakatifu? Jinsi gani dhambi zako zingenajisi utakatifu Wangu? Mimi sijanajisika na uchafu wa wasio haki, wala kufurahia sadaka ya wasio haki. Kama ungekuwa mwaminifu Kwangu, Yehova, je, ungeweza kujichukulia sadaka kutoka katika madhabahu Yangu? Je, ungeweza kutumia ulimi wako wa sumu kukufuru jina Langu takatifu? Ungeweza kuliasi neno Langu kwa njia hii? Je, ungeweza kuuchukua utukufu Wangu na jina langu takatifu kama chombo ambacho kwalo unamtumikia Shetani, yule mwovu? Maisha Yangu yametolewa kwa ajili ya furaha ya watakatifu. Ningewezaje kukuruhusu ucheze na maisha Yangu jinsi utakavyo, na kuyatumia kama chombo kwa ajili ya migogoro kati yenu? Mngewezaje kuwa wakatili sana, na watovu sana katika njia ya wenye wema, katika jinsi mlivyo Kwangu? Je, hamjui kwamba tayari Nimeandika matendo yenu maovu katika neno hili la maisha? Jinsi gani mngeweza kuepuka siku ya ghadhabu Ninapoadibu Misri? Ningewezaje kuwaruhusu kunipinga na kuniasi kwa njia hii, mara kwa mara? Nawaambia wazi, siku itakapokuja, basi kuadibu kwenu kutakuwa kusikovumilika zaidi kuliko ile ya Misri! Mnawezaje kuitoroka siku ya ghadhabu Yangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

123. Mwanadamu anashindwa kumpata Mungu sio kwa sababu Mungu ana hisia, au kwa sababu Mungu hataki kupatikana na mwanadamu, bali ni kwa sababu mwanadamu hataki kumpata Mungu, na kwa sababu mwanadamu hana haraka kumtafuta Mungu. Jinsi gani mmoja wa wale ambao kweli wanamtafuta Mungu alaaniwe na Mungu? Ni jinsi gani mwenye akili timamu na dhamiri nzuri anaweza laaniwa na Mungu? Ni vipi yule anayemwabudu kwa kweli na kumhudumia Mungu ataangamizwa na moto wa ghadhabu yake? Ni jinsi gani mwanadamu aliye na furaha ya kumtii Mungu kutupwa nje ya nyumba ya Mungu kwa mateke? Jinsi gani mwanadamu ambaye hawezi kumpenda Mungu vya kutosha aishi katika adhabu ya Mungu? Jinsi gani mwanadamu ambaye ana furaha ya kuacha kila kitu kwa ajili ya Mungu kuachwa bila chochote? Mwanadamu hana nia ya kumfuata Mungu, hana nia ya kutumia mali yake kwa Mungu, hana nia ya kutoa juhudi za milele kwa Mungu, na badala yake anasema kwamba Mungu amepita kiasi, kwamba mengi kuhusu Mungu yanakinzana na dhana za mwanadamu. Na ubinadamu kama huu, hata kama mngekuwa wakarimu katika juhudi zenu bado hamngeweza kupata kibali cha Mungu, bila kutaja kuwa hamumtafuti Mungu. Je, hamjui kwamba ninyi ni bidhaa mbovu za binadamu? Je, hamjui kwamba hakuna ubinadamu ulio mnyenyekevu zaidi kuliko wenu? Je, hamjui “cheo” chenu ni kipi? Wale ambao kweli wanampenda Mungu wanawaita baba wa mbweha, mama wa mbweha, mwanambweha, na mjukuu wa mbweha; nyinyi ni vizazi vya mbweha, watu wa mbweha, na mnapaswa kujua utambulisho wenu na kamwe msiwahi kuusahau. Msidhani kwamba nyinyi ni kiumbe mkubwa zaidi: Nyinyi ni kundi mojawapo la wasio-wanadamu wabaya zaidi miongoni mwa wanadamu. Je, hamjui lolote kuhusu haya? Je, mnajua ni kiasi gani cha hatari Nimechukua kwa kufanya kazi miongoni mwenu? Kama akili yenu haiwezi kurudi kawaida, na dhamiri yenu haiwezi kufanya kazi kwa kawaida, basi kamwe hamtawahi kuwa huru kutokana na jina “mbwa mwitu”, kamwe hamtaitoroka siku ya laana, kamwe hamtaitoroka siku ya adhabu yenu. Mlizaliwa mkiwa duni, kitu kisicho na thamani yoyote. Kwa hivyo nyinyi ni kundi la mbwa mwitu wenye njaa, rundo la uchafu na takataka, na, tofauti na nyinyi, Mimi Sifanyi kazi kwenu ili nipate chochote, lakini kwa sababu ya haja ya kazi. Mkiendelea kuwa waasi kwa njia hii, basi Nitakomesha kazi Yangu, na kamwe sitafanya kazi kwenu tena; badala yake, Nitahamisha Kazi yangu kwa kundi lingine linalonipendeza, na kwa njia hii kuondoka kwenu milele, kwa sababu Mimi sina nia ya kuwaangalia walio katika uadui na Mimi. Hivyo basi, je, mnataka kulingana na Mimi, au katika uadui dhidi Yangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

124. Unapoitembea njia ya leo, ufuatiliaji unaofaa zaidi ni wa aina gani? Katika ufuatiliaji wako, unapaswa kujiona kama mtu wa aina gani? Unafaa kujua jinsi unavyopaswa kukabili yote yanayokukumba leo, yawe majaribu ama taabu, ama kuadibu na laana isiyo ya huruma. Unapaswa kuyazingatia kwa uangalifu katika hali zote. Mbona Nasema hili? Nasema hili kwa sababu yanayokukumba leo hata hivyo ni majaribu mafupi yanayotokea tena na tena; huenda huyaoni kuwa yanayosumbua sana kiakili, na hivyo unayaacha mambo yaende mrama, na huyachukulii kuwa rasilmali ya thamani katika ufuatiliaji wa maendeleo. Wewe ni asiyejali kweli! Sana kiasi kwamba unaifikiria rasilmali kana kwamba ni wingu linaloelea machoni pako, na huyathamini haya mapigo makali yanayokuja mara kwa mara—mapigo ambayo ni ya muda mfupi na yanayoonekana kuwa dhaifu kwako—ila unayatazama kwa utulivu, usiyafikirie kwa dhati na kuyachukulia tu kama mapigo ya mara moja. Wewe ni mfidhuli sana! Kwa mashambulio haya makali, mashambulio yaliyo kama dhoruba na yanayokuja mara kwa mara unaonyesha kupuuza kwa dharau; wakati mwingine hata unatabasamu bila hisia, ukifichua jinsi usivyojali—kwani hujawahi kujiwazia mbona unashinda ukipitia “misiba” kama hii. Je, Namtendea mwanadamu bila haki kwa kiasi kikubwa? Je, Natafuta makosa kwako? Ingawa shida zako za akili huenda zisiwe nzito jinsi Nilivyoeleza, kupitia utulivu wako wa nje, tangu zamani umebuni taswira nzuri sana ya dunia yako ya ndani. Hakuna maana ya Mimi kukuambia kwamba jambo la pekee lililofichika katika vina vya moyo wako ni matusi yasiyo adilifu na athari dhaifu ya huzuni ambayo wengine hawayaoni. Kwa sababu unahisi kwamba si haki hata kidogo kupitia majaribu kama haya, unatoa matusi; majaribu hayo hukufanya uhisi ukiwa wa dunia, na kwa sababu ya hili, unajawa na ghamu. Badala ya kutazama nidhamu na mapigo haya yanayorudiwa kama ulinzi bora kabisa, unayaona kuwa uchokozi wa Mbinguni usio na sababu, ama vinginevyo kama adhabu inayokufaa. Wewe ni mpumbavu sana! Unazifungia nyakati nzuri gizani bila huruma; mara kwa mara unaona nidhamu na mapigo mazuri kuwa mashambulio kutoka kwa adui zako. Huwezi kubadilika kulingana na mazingira yako sembuse kutaka kufanya hivyo kwani huna hiari ya kupata chochote kutoka kwa kuadibu huku kunakorudiwa na unakoona kuwa katili. Hufanyi juhudi yoyote kutafuta au kuchunguza, na, unajikabidhi tu kwa yale majaaliwayako, kwenda pahali popote itakapokuelekeza. Yanayoonekana kwako kuwa marudio makali hayajaubadili moyo wako wala hayajatwaa udhibiti wa moyo wako; badala yake, yanakuchoma moyoni. Unaona “kuadibu huku katili” kuwa adui wako katika maisha haya tu na hujapata chochote. Wewe unajidai sana! Ni mara chache ambapo unaamini kwamba unapitia majaribu kama haya kwa sababu wewe ni duni sana; badala yake, unajiona aliye na bahati mbaya sana, na kusema kwamba Mimi daima hutafuta makosa kwako. Kufikia leo, kwa kweli una kiasi kipi cha maarifa ya kile Ninachosema na kufanya? Usifikiri kwamba una kipaji cha asili, uliye chini kidogo ya mbingu lakini juu sana ya dunia. Wewe si mwerevu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote—na hata inaweza kusemwa kwamba wewe ni mpumbavu zaidi kuliko watu wowote duniani walio na mantiki, kwani unajiona sana kuwa bora, na hujawahi kujiona kuwa mtu wa chini; inaonekana kwamba unayachunguza matendo Yangu kwa utondoti kabisa. Kwa kweli, wewe ni mtu ambaye kimsingi hana mantiki, kwa kuwa hufahamu kabisa Nitakachofanya sembuse kutambua Ninachofanya sasa. Kwa hivyo Nasema kwamba wewe hata hulingani na mkulima mzee anayefanya kazi kwa bidii shambani, mkulima ambaye hafahamu maisha ya binadamu hata kidogo na bado anategemeabaraka za Mbinguni wakati anapolima shamba. Huyafikirii maisha yako hata kidogo, hujui chochote chenye sifa sembuse kujijua. Wewe “una hadhi ya juu” sana!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wasiojifunza na Wanaosalia Wajinga: Je, Wao Sio Wanyama?

125. Wengine wanajivika mapambo mazuri, lakini ya juujuu: Kina dada wanajivika mapambo mazuri kama maua, na kina ndugu wanavalia kama wana wa wafalme ama wambuji wadogo matajiri. Wanajali tu kuhusu vitu vya nje, kama vitu wanavyokula na kuvalia; ndani yao, wao ni mafukara na hawamfahamu Mungu hata kidogo. Hili lina maana gani? Na kisha kuna wengine wanaovalia kama waombaji maskini—kweli wanaonekana kama watumwa wa Asia Mashariki! Je, kweli hamwelewi Ninachotaka kutoka kwenu? Shirikini kwa karibu: Mmepata nini kweli? Mmemwamini Mungu kwa miaka hii yote, lakini mmevuna hili tu—je, hamna aibu? Je, hamwoni haya? Mmekuwa mkifuatilia kwenye njia ya kweli kwa miaka hii yote, lakini leo kimo chenu bado ni cha chini kuliko cha jurawa! Watazame mabibi wadogo walio miongoni mwenu, warembo kama picha mkiwa mmevalia mavazi na vipodozi vyenu, mkijilinganisha kati yenu—na ni nini mnacholinganisha? Starehe zenu? Matakwa yenu? Je, mnadhani kwamba Nimekuja kuandikisha waonyesha mitindo? Hamna aibu! Maisha yenu yako wapi? Je, kile mnachokifuatilia si tamaa zilizopita kiasi tu? Unadhani kuwa wewe ni mrembo sana, lakini ingawa umevalia kila aina ya umaridadi, kwa kweli wewe si buu anayegaagaa, aliyezaliwa katika rundo la kinyesi? Leo, huna bahati ya kufurahia baraka hizi za mbinguni kwa ajili ya uso wako mrembo, ila kwa sababu Mungu anafanya jambo la kipekee kwa kukuinua. Je, bado huelewi ulikotoka? Maisha yanapotajwa, unafunga mdomo wako na husemi chochote, na unakimya kama sanamu, lakini bado una ujasiri wa kuvalia vizuri! Bado unataka kupaka uso wako rangi nyekundu na poda! Na watazame wambuji walio miongoni mwenu, wanaume waliopotoka wanaoshinda siku kutwa wakitembea huku na kule polepole, wakaidi, na wenye sura tepetevu usoni pao. Je, hivi ndivyo mtu anapaswa kutenda? Je, kila mmoja kati yenu, awe mwamamume ama mwanamke, anazingatia nini siku nzima? Je, mnajua mnamtegemea nani kujilisha? Tazama mavazi yako, tazama kile ulichovuna mikononi mwako, sugua kitambi chako—umefaidika nini kutoka kwa gharama ya damu na jasho ambayo umelipa katika miaka hii yote ya imani? Bado unafikiri kwenda kutalii sehemu maarufu, bado unafikiri kupamba mwili wako unukao—ufuatiliaji usio na maana! Unaombwa uwe mtu wa kawaida, lakini sasa wewe si mtu asiye wa kawaida tu, wewe ni mpotovu. Mtu kama wewe anawezaje kuwa na ujasiri wa kuja mbele Zangu? Ukiwa na ubinadamu kama huu, ukionyesha uzuri wako na kuringa kwa ajili ya mwili wako, ukiishi daima ndani ya tamaa za mwili—je, wewe si mzao wa mashetani wachafu na pepo waovu? Sitamruhusu shetani mchafu kama huyu aendelee kuishi kwa muda mrefu! Na usifikiri kwamba Sijui kile unachofikiri moyoni mwako. Unaweza kudhibiti vikali tamaa na mwili wako, lakini Nawezaje kukosa kujua fikira zilizo moyoni mwako? Nawezaje kukosa kujua tamaa zote za macho yako? Je, ninyi mabibi wadogo hamjirembeshi sana ili kuonyesha miili yenu? Wanaume wana faida gani kwenu? Je, kweli wanaweza kuwaokoa kutoka katika bahari ya mateso? Na kwa wambuji miongoni mwenu, nyote huvalia ili kujifanya muonekane waungwana na wa heshima, lakini, je, hii si hila iliyokusudiwa kuvuta macho kwa sura zenu changamfu? Mnafanya hili kwa sababu ya nani? Wanawake wana faida gani kwenu? Je, wao si chanzo cha dhambi yenu? Enyi wanaume na wanawake, Nimewaambia maneno mengi sana, lakini mmetii machache tu. Masikio yenu hayataki kusikia, macho yenu yamefifia, na mioyo yenu ni migumu kiasi kwamba kuna tamaa tu katika miili yenu, kiasi kwamba mmetegwa nayo, msiweze kutoroka. Ni nani anayetaka kuwakaribia ninyi mabuu, ninyi mnaojifurukuta katika uchafu na masizi? Msisahau kwamba ninyi tu ni wale Niliowatoa kutoka katika rundo la kinyesi, kwamba mwanzoni hamkuwa na ubinadamu wa kawaida. Ninachotaka kutoka kwenu ni ule ubinadamu wa kawaida ambao hamkuwa nao mwanzoni, si kwamba muonyeshe tamaa zenu ama muachilie miili yenu iliyooza, ambayo imeelekezwa na ibilisi kwa miaka mingi sana. Mnapojivisha nguo hivyo, je, hamwogopi kwamba mtategwa kwa kina zaidi? Je, hamjui kwamba mwanzoni mlikuwa wenye dhambi? Je, hamjui kwamba miili yenu imejaa tamaa sana kiasi kwamba hata inavuja kutoka kwa mavazi yenu, ikifichua hali zenu kama mashetani wabaya na wachafu kukithiri? Je, si kweli kwamba mnajua hili vyema zaidi kuliko yeyote mwingine? Mioyo yenu, macho yenu, midomo yenu—je, si vyote vimenajisiwa na mashetani wachafu? Je, hizi sehemu zenu si chafu? Je, unadhani kwamba alimradi hutendi, basi wewe ndiwe mtakatifu kabisa? Je, unadhani kwamba kuvalia mavazi mazuri kunaweza kuficha nafsi zenu duni? Hilo haliwezekani! Nawashauri muwe wenye uhalisi zaidi: Msiwe wadanganyifu na bandia, na msijigambe. Mnaonyeshana tamaa zenu, lakini yote mtakayopata kama malipo ni mateso ya milele na kurudiwa kikatili! Mna haja gani ya kupepeseana macho yenu na kujiingiza katika mapenzi? Je, hiki ndicho kipimo cha uaminifu wenu, kiasi cha uadilifu wenu? Nawachukia kabisa wale miongoni mwenu wanaojihusisha katika uganga na uchawi; Nawachukia sana wale wanaume na wanawake wadogo miongoni mwenu wanaopenda miili yao wenyewe. Ni vyema mjizuie, kwa sababu sasa mnahitajika kuwa na ubinadamu wa kawaida, na hamruhusiwi kuonyesha tamaa zenu—lakini mnachukua kila fursa muwezayo, kwani miili yenu imejaa sana, na tamaa zenu ni kubwa mno!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (7)

126. Wale wanaofikiria tu miili yao na wanaofurahia faraja, wale wanaoonekana kuamini lakini wasioamini kwa kweli; wale wanaojihusisha katika uganga na uchawi; wale ambao ni wazinzi, walio duni kabisa; wale wanaoiba sadaka za Yehova na mali Yake; wale wanaopenda hongo; wale walio na njozi za kupaa mbinguni; wale ambao ni wenye majivuno na fidhuli, wanaojitahidi tu kwa sababu ya umaarufu na utajiri wa kibinafsi; wale wanaoeneza maneno ya safihi; wale wanaomkufuru Mungu Mwenyewe; wale wanaotoa tu hukumu dhidi ya Mungu Mwenyewe na kumkashifu; wale wanaounda vikundi na kutafuta kujitegemea; wale wanaojitukuza juu ya Mungu, wale wanaume na wanawake wadogo, wa makamo na wakubwa ambao ni wapuuzi na wametegwa katika uasherati; wale wanaume na wanawake wanaofurahia umaarufu na utajiri wa kibinafsi na wanafuatilia hadhi ya kibinafsi miongoni mwa mengine; wale watu wasiotubu walionaswa katika dhambi—je, si wote hawawezi kuokolewa? Uasherati, kutenda dhambi, uganga, uchawi, matusi na maneno ya safihi yote yamejaa kwenu; na ukweli na maneno ya uzima yanakanyagwa miongoni mwenu, na lugha takatifu inachafuliwa miongoni mwenu. Ninyi Mataifa, mliojaa uchafu na uasi! Matokeo yenu ya mwisho yatakuwa yapi? Je, wale wanaopenda mwili, wanaotenda uchawi wa mwili, na waliotegwa katika dhambi ya uasherati wanawezaje kuwa na ujasiri wa kuendelea kuishi! Je, hujui kwamba watu kama ninyi ni mabuu wasioweza kuokolewa? Ni nini kinachowapa haki ya kudai hili na lile? Hadi leo, hakujakuwa na mabadiliko hata kidogo katika wale wasiopenda ukweli na wanapenda tu mwili—watu kama hawa wanawezaje kuokolewa? Wale wasiopenda njia ya uzima, wasiomtukuza Mungu ama kumshuhudia, wanaopanga njama kwa ajili ya hadhi yao wenyewe, wanaojisifu sana—je, si bado wao wako vivyo hivyo, hadi leo? Kuna thamani gani katika kuwaokoa? Iwapo unaweza kuokolewa hakutegemei ukubwa wako ama ni miaka mingapi umekuwa ukifanya kazi, sembuse sifa ambazo umeongeza. Badala yake, kunategemea iwapo ufuatiliaji wako umezaa matunda. Unapaswa kujua kwamba wale waliookolewa ni “miti” inayozaa matunda, siyo miti iliyo na majani yaliyositawi sana na maua mengi lakini ambayo hayazai matunda. Hata kama umeshinda miaka mingi ukizurura mitaani, hilo lina maana gani? Ushuhuda wako uko wapi? Uchaji wako wa Mungu ni kidogo sana kuliko upendo wako kwako mwenyewe na hamu zako zenye tamaa—je, si mtu kama huyu ni mpotovu? Anawezaje kuwa kielelezo na mfano wa wokovu? Asili yako ni isiyorekebishika, wewe ni mwasi sana, huwezi kuokolewa! Je, si watu kama hawa ni wale watakaoondolewa? Je, si wakati ambapo kazi Yangu inakamilika ni wakati wa kufika kwa siku yako ya mwisho? Nimefanya kazi nyingi sana na kuzungumza maneno mengi sana miongoni mwenu—kweli mmeyasikiliza kiasi kipi? Mmewahi kutii kiasi kipi? Kazi Yangu ikamilikapo, huo utakuwa wakati ambapo unakoma kunipinga, wakati ambapo unakoma kusimama dhidi Yangu. Nifanyapo kazi, mnanipinga bila kukoma; kamwe hamyatii maneno Yangu. Nafanya kazi Yangu na wewe unafanya “kazi” yako mwenyewe, ukitengeneza ufalme wako mdogo. Ninyi ni kundi la mbweha na mbwa tu, mnaofanya kila kitu kunipinga! Mnajaribu kila wakati kuwakumbatia wale wanaowapa upendo wao wa dhati—uchaji wenu uko wapi? Kila kitu mfanyacho ni kidanganyifu! Hamna utii wala uchaji, na kila kitu mfanyacho ni kidanganyifu na cha kukufuru! Je, watu kama hawa wanaweza kuokolewa? Wanadamu ambao ni waasherati na wakware daima hutaka kuwavutia makahaba wenye ubembe kwao kwa ajili ya raha zao wenyewe. Sitawaokoa mashetani wa kisherati kama hawa hata kidogo. Nawachukia ninyi mashetani wachafu, na ukware na ubembe wenu utawatumbukiza kuzimuni. Mna nini cha kusema kujihusu? Ninyi mashetani wachafu na pepo waovu ni wa kutia kinyaa! Mnachukiza! Watu ovyo kama ninyi mnawezaje kuokolewa? Je, wale waliotegwa katika dhambi wanaweza kuokolewa bado? Leo, ukweli huu, njia hii, na uzima huu hauwavutii; badala yake mnavutiwa na utendaji dhambi, fedha, hadhi, umaarufu na faida; mnavutiwa na raha za mwili; sura nzuri za wanaume na uzuri wa wanawake. Ni nini kinachowastahiki kuingia katika ufalme Wangu? Sura yenu hata ni ya juu zaidi kuliko ya Mungu, hadhi yenu hata ni ya juu kuliko ya Mungu sembuse fahari yenu kubwa miongoni mwa wanadamu—mmekuwa sanamu ambayo watu wanaabudu. Je, hujageuka kuwa malaika mkuu? Wakati matokeo ya watu yanafichuliwa, ambao pia ndio wakati kazi ya wokovu itakaribia kuisha, wengi kati yenu mtakuwa maiti msioweza kuokolewa na lazima muondolewe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (7)

127. Inaweza kusemwa kwamba wanadamu ni wanyonge wasio na thamani kwa sababu hawajithamini. Kama hata hawajipendi, bali hujikandamiza, hili halionyeshi kwamba hawana thamani? Wanadamu ni kama mwanamke mwovu ambaye hujihadaa na ambaye hujitoa kwa wengine kwa hiari kuingiliwa bila heshima. Lakini hata hivyo, bado hawajui vile walivyo duni. Wao hufurahia kuwatumikia wengine, au kuzungumza na wengine, kujiweka chini ya utawala wa wengine; huu kweli si uchafu wa wanadamu? Ingawa Sijapitia maisha miongoni mwa wanadamu, kwa vile Sijapitia kweli maisha ya binadamu, Nina ufahamu kamili wa kila mwendo, kila hatua, kila neno, na kila kitendo cha mwanadamu. Naweza hata kuwaweka wanadamu wazi mpaka waaibike kabisa, kiasi cha kutoweza tena kuthubutu kuonyesha hila zao na kutoweza tena kuthubutu kujiachilia kwa tamaa zao. Kama konokono ambaye hurudi ndani ya kombe lake, hawathubutu tena kuonyesha hali zao mbaya. Kwa sababu wanadamu hawajijui, dosari yao kubwa sana ni kuonyesha kwa hiari haiba yao mbele ya wengine, wakionyesha sura yao mbaya; Hiki ni kitu ambacho Mungu hukichukia zaidi. Kwa sababu mahusiano kati ya watu si ya kawaida, na hakuna mahusiano ya kawaida ya mtu mmoja na mwingine kati ya watu, sembuse uhusiano wa kawaida kati yao na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 14

128. Mpaka watu wawe wamepitia kazi ya Mungu na kupata ukweli, ni asili ya Shetani inayotwaa madaraka na kuwatawala kwa ndani. Ni nini, hasa, kilicho ndani ya asili hiyo? Kwa mfano, kwa nini wewe ni mchoyo? Kwa nini wewe hulinda nafasi yako mwenyewe? Kwa nini una hisia kali sana namna hiyo? Kwa nini unafurahia hivyo vitu visivyo vya haki? Kwa nini unapenda maovu hayo? Msingi wa kupenda kwako vitu hivi ni upi? Mambo haya hutoka wapi? Kwa nini unafurahia sana kuyakubali? Kufikia sasa, nyote mmekuja kuelewa kwamba sababu kuu ya mambo haya yote ni kwamba sumu ya Shetani iko ndani yenu. Kuhusu sumu ya Shetani ni nini, inaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa maneno. Kwa mfano, ukiwauliza baadhi ya watenda maovu kwa nini walitenda jinsi walivyotenda, watajibu, “Kwa sababu kila mwamba ngoma huvutia upande wake.” Msemo huu mmoja unaonyesha asili ya shida. Mantiki ya Shetani imekuwa maisha ya watu. Wanaweza kutenda mambo kwa ajili ya madhumuni fulani au mengine, lakini wanajifanyia tu. Kila mtu hudhani kwamba kwa kuwa ni kila mwamba ngoma huvutia upande wake, watu wanafaa kuishi kwa sababu yake mwenyewe tu, na kufanya kila awezalo kupata wadhifa mzuri kwa ajili ya chakula na mavayi mazuri. “Kila mwamba ngoma huvutia upande wake”—haya ndiyo maisha na falsafa ya mwanadamu, na pia inawakilisha asili ya binadamu. Maneno haya ya Shetani ni sumu ya Shetani hasa, na watu wanapopoiweka moyoni, inakuwa asili yao. Asili ya Shetani hufunuliwa kupitia maneno haya; yanamwakilisha yeye kabisa. Sumu hii inakuwa maisha ya watu pamoja na msingi wa kuwepo kwao; na wanadamu waliopotoshwa wametawaliwa kwa uthabiti na sumu hii kwa maelfu ya miaka. Kila kitu ambacho Shetani hufanya ni kwa ajili yake. Anatamani kumpita Mungu, kujiondoa Kwake na kushika mamlaka mwenyewe, na kumiliki vitu vyote ambavyo Mungu ameumba; kwa hivyo, asili ya mwanadamu ni asili ya Shetani. Kwa kweli, wito wa watu wengi unaweza kuwakilisha na kuakisi asili yao. Haijalishi jinsi watu hujaribu kuificha, katika kila kitu wafanyacho na kila kitu wasemacho, hawawezi kuificha asili yao. Kuna wengine ambao huwa hawasemi ukweli kamwe na wanajua sana kujifanya, lakini punde tu wengine wanapoingiliana nao kwa muda, asili yao ya udanganyifu na wao kutokuwa waaminifu kabisa kutagunduliwa. Muda utafichua yote. Baada ya kuwajua kwa muda, asili yao itagunduliwa. Mwishowe, wengine hufikia hitimisho hili: Mtu huyo kamwe hasemi neno lolote la ukweli na ni mdanganyifu. Kauli hii ni ukweli wa asili ya mtu wa aina hiyo; ni ushahidi na kielezo cha asili yake; falsafa yake ya maisha ni kutomwambia yeyote ukweli, na pia kutomwamini mtu yeyote. Asili ya kishetani ya mwanadamu ina kiwango kikubwa cha falsafa. Wakati mwingine wewe mwenyewe huna hata habari ya hilo na hulielewi, ilhali kila muda wa maisha yako unategemea hilo. Isitoshe, unafikiri kuwa falsafa hii ni sahihi sana, yenye mantiki na isiyo na kosa. Falsafa ya Shetani imekuwa ukweli wa watu, na wanaishi kulingana na falsafa ya Shetani kabisa, bila kumpinga hata kidogo. Kwa hivyo, kila mara wanaonyesha asili yao ya kishetani. mwanadamu daima hufichua asili ya Shetani, na katika vipengele vyote, wanaishi daima kulingana na falsafa ya ya kishetani. Asili ya Shetani ni maisha ya mwanadamu.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

129. Asili ya mwanadamu ni tofauti kabisa na kiini Changu, kwa sababu asili potovu ya mwanadamu hutoka kwa Shetani kabisa; asili ya mwanadamu imetengenezwa na kupotoshwa na Shetani. Yaani, mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa uovu na ubaya wake. Mwanadamu hakui katika ulimwengu wa ukweli au mazingira matakatifu, sembuse mwanadamu kuishi katika nuru. Kwa hiyo, haiwezekani kwa mtu yeyote kuwa na ukweli ndani ya asili yake tangu wakati wa kuzaliwa, sembuse mtu kuweza kuzaliwa na kiini kinachomwogopa na kumtii Mungu. Badala yake, watu wana asili ambayo humpinga na kumwasi Mungu, na haipendi ukweli. Asili hii ndilo tatizo Ninalotaka kujadili—usaliti.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

130. Tabia ambayo haiwezi kunitii kabisa ni usaliti. Mwenendo ambao hauwezi kuwa mwaminifu Kwangu ni usaliti. Kunidanganya na kutumia uongo kunilaghai ni usaliti. Kujawa na dhana na kuzieneza kila mahali ni usaliti. Kutozilinda shuhuda na maslahi Yangu ni usaliti. Kubuni tabasamu wakati mtu ameniacha moyoni mwake ni usaliti. Tabia hizi ni mambo yote ambayo daima mna uwezo wa kuyafanya, na pia ni za kawaida kati yenu. Hakuna mmoja wenu anayeweza kufikiri kwamba hilo ni tatizo, lakini Mimi sifikirii hivyo. Siwezi kuchukulia kunisaliti kama jambo dogo, na zaidi ya hayo siwezi kulipuuza. Sasa, Nafanyapo kazi miongoni mwenu, mnakuwa wenye tabia ya aina hii—ijapo siku ile ambapo hakutakuwa na mtu wa kuwalinda, hamtakuwa kama wezi waliojitangaza kuwa wafalme? Wakati hili linafanyika na mnasababisha janga kubwa, nani atakuwa hapa kuvisafisha vitu tena na kuondoa uchafu? Mnaweza kufikiri kwamba baadhi ya vitendo vya usaliti ni kitu cha mara moja tu badala ya tabia ya kuendelea, na hakipaswi kutajwa kwa uzito hivi, kikiwasababisha kuadhirika. Kama kweli mnaamini hivyo, basi mnakosa wepesi wa kuhisi. Kadiri mtu anavyofikiri hivi, ndivyo anavyokuwa kielelezo na umboasili wa uasi. Asili ya mtu ni maisha yake, ni kanuni ambayo anaitegemea ili kuendelea kuishi, na anashindwa kuibadilisha. Jinsi ilivyo hali ya usaliti—kama unaweza kufanya kitu ili kumsaliti ndugu au rafiki, hii inathibitisha kwamba ni sehemu ya maisha yako na hali ambayo ulizaliwa nayo. Hiki ni kitu ambacho hakuna mtu anaweza kukikana.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (1)

131. Mtu yeyote anaweza kutumia maneno na vitendo vyake wenyewe kuwakilisha tabia yake halisi. Sura hii ya kweli bila shaka ni asili yake. Kama wewe ni mtu anayeongea bila kuwa dhahiri, basi una asili mbovu. Kama asili yako ni yenye hila sana, basi namna ambayo unafanya mambo ni janja na laghai sana, nawe unafanya iwe rahisi sana kwa watu kulaghaiwa nawe. Kama asili yako ni mbovu sana, huenda maneno yako ni mazuri kusikiliza, lakini vitendo vyako haviwezi kuficha njia zako mbovu. Kama asili yako ni vivu sana, basi kila kitu unachosema vyote vinalenga kukwepa lawama na wajibu wa uzembe na uvivu wako, na vitendo vyako vitakuwa vya polepole sana na vizembe, na vizuri sana katika kuuficha ukweli. Kama asili yako ni yenye uwezo wa kuhisi maono ya wengine sana, basi maneno yako yatakuwa yenye busara na hatua zako pia zitalingana sana na ukweli. Kama asili yako ni aminifu sana, basi maneno yako lazima yawe ya dhati na namna ambayo unafanya mambo lazima iwe yenye kuhusika na mambo halisi, bila mengi ya kufanya bwana wako asikuamini. Kama asili yako ni yenye tamaa sana au ni yenye tamaa ya fedha, basi moyo wako mara nyingi utajazwa na mambo haya na utafanya baadhi ya mambo yaliyopotoka bila kukusudia, mambo maovu ambayo hufanya iwe vigumu kwa watu kusahau na zaidi ya hayo yatawaudhi. Kama Nilivyosema, kama una asili ya usaliti basi ni kujinasua kutoka kwake kwa nadra sana. Msiamini kuwa hivyo ndivyo ilivyo kwamba hamna asili ya usaliti kwa sababu hamjamkosea mtu yeyote. Kama hivyo ndivyo unavyofikiri basi unachukiza sana. Maneno ambayo Nimenena kila wakati yamewalenga watu wote, sio tu mtu mmoja au aina ya mtu. Kwa sababu tu hujanisaliti Mimi kwa jambo moja haithibitishi kwamba huwezi kunisaliti katika jambo moja haiashirii kwamba huwezi kunisaliti Mimi katika jambo jingine. Kwa kutafuta ukweli, baadhi ya watu hupoteza imani yao katika kuutafuta ukweli wakati wa kipingamizi katika ndoa zao. Baadhi ya watu huwacha wajibu wao wa kuwa waaminifu Kwangu wakati wa kuvunjika kwa familia. Baadhi ya watu huniacha kwa ajili ya kutafuta wakati wa furaha na msisimko. Baadhi ya watu afadhali waanguke katika korongo lenye giza kuliko kuishi katika mwanga na kupata furaha ya kazi ya Roho Mtakatifu. Baadhi ya watu hupuuza ushauri wa marafiki kwa ajili ya kuridhisha tamaa zao kwa ajili ya mali, na hata sasa hawawezi kuyakubali uovu wao na kugeuza mkondo. Baadhi ya watu wanaishi tu kwa muda chini ya jina Langu ili wapate ulinzi Wangu, wakati wengine hujitolea tu kidogo tu Kwangu kwa kulazimishwa kwa sababu wameyashikilia maisha na wanahofu kifo. Si vitendo hivi na vingine viovu na zaidi ya hayo visivyofaa tabia tu ambazo watu wamenisaliti kwa muda mrefu ndani ya mioyo yao? Bila shaka, Najua usaliti wa watu haukuwa umepangwa mapema, lakini ni ufunuo wa kimaumbile wa asili zao. Hakuna mtu anayetaka kunisaliti, na zaidi ya hayo hakuna mtu aliye na furaha kwa sababu amefanya kitu kunisaliti. Kinyume chake, wanatetemeka kwa hofu, sivyo? Hivyo mnafikiri kuhusu jinsi mnavyoweza kuzikomboa saliti hizi, na jinsi mnavyoweza kubadili hali ya sasa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (1)

132. Mlitengwa kutoka kwa matope na kwa vyovyote vile, mlichaguliwa kutoka kwa mashapo, wachafu na mliochukiwa na Mungu. Mlikuwa wa Shetani na wakati mmoja mlikanyagwa na kuchafuliwa na yeye. Hii ndiyo maana inasemwa kuwa mlitengwa kutoka kwa matope, na nyinyi si watakatifu, lakini badala yake nyinyi ni vitu visivyo binadamu ambavyo Shetani kwa muda mrefu alikuwa amevifanya vipumbavu. Haya ndiyo maelezo sahihi zaidi yenu. Lazima mtambue kuwa nyinyi ni uchafu unaopatikana katika maji yaliyotuama na matope, kinyume na ushikaji unaofaa kama samaki na uduvi, kwa maana hakuna starehe inayoweza kupatikana kutoka kwenu. Kuzungumza waziwazi, nyinyi ni wanyama wa chini sana wa tabaka la chini zaidi, wanyama wabaya zaidi kuliko nguruwe na mbwa. Kusema kweli, kuwahutubia kwa istilahi kama hizo si chuku au kutia chumvi, lakini ni njia ya kurahisisha suala hilo. Kuwahutubia kwa istilahi kama hizo kwa kweli ni njia ya kuwapa heshima. Utambuzi wenu, hotuba, mwenendo kama watu, na vitu yote katika maisha yenu—ikiwa ni pamoja na hali yenu katika matope—vinatosha kuthibitisha kwamba utambulisho wenu ni “wa kipekee.”

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utambulisho wa Asili wa Mwanadamu na Thamani Yake: Je, Viko Namna Gani?

133. Mwanadamu si kitu kingine ila ni adui Yangu. Mwanadamu ni yule mwovu anayenipinga na kuniasi. Mwanadamu si mwingine ila kizazi cha yule mwovu aliyelaaniwa na Mimi. Mwanadamu si mwingine ila ukoo wa malaika mkuu ambaye alinisaliti Mimi. Mwanadamu si mwingine ila mrithi wa shetani ambaye, akiwa amekataliwa kwa dharau na Mimi kitambo, amekuwa adui Wangu asiyeweza kupatanishwa tangu wakati huo. Anga iliyo juu ya jamii ya binadamu ni nzito sana, ni yenye giza na huzuni, bila hata dalili ya uwazi, na ulimwengu wa mwanadamu uko katika giza totoro, kiasi kwamba anayeishi ndani yake hawezi hata kuona mkono wake mwenyewe wakati anapounyosha mbele yake au jua anapoinua kichwa chake. Barabara chini ya miguu yake, ni matope na imejaa mashimo makubwa, ni mipindopindo na ya minyongo; nchi yote imejaa maiti. Pembe za giza zimejaa mabaki ya wafu. Na katika pembe zenye baridi na giza magenge ya mapepo yameshika makazi. Na kila mahali katika dunia ya binadamu, mapepo yanakuja na kwenda katika magenge. Kizazi cha wanyama wa aina yote, waliojawa na uchafu, wanapigana mkono kwa mkono katika mapambano ya kikatili, sauti ambayo huleta hofu moyoni. Nyakati kama hizo, katika dunia kama hiyo, “paradiso ya kidunia” ya aina hii, ni wapi ambako mwanadamu huenda kutafuta bahati ya maisha? Ni wapi ambako mtu ataenda kupata hatima ya maisha yake? Mwanadamu, akiwa amekanyagwa chini ya miguu ya Shetani kwa muda mrefu, amekuwa tangu mwazo mwigizaji akitenda kwa mfano wa Shetani—hata zaidi, kuwa na mwili wake, wakitumika kama shahidi wa kushuhudia kwa Shetani, kwa uwazi. Aina hii ya jamii ya binadamu, aina hii ya watu wachafu walioharibika tabia, na watoto wa aina hii wa familia hii ya binadamu potovu, inawezaje kuwa na ushuhuda kwa Mungu? Utukufu Wangu unatoka wapi? Mtu anaweza kuanza wapi kuongea juu ya shahidi Wangu? Kwa adui ambaye, baada ya kupotosha mwanadamu, anasimama dhidi Yangu, tayari amemchukua mwanadamu—mwanadamu ambaye niliumba kitambo sana na ambaye alikuwa amejawa na utukufu Wangu kuishi kulingana na Mimi—na kumchafua. Amepokonya utukufu Wangu, na yote ambayo imetia moyoni mwa mwanadamu ni sumu iliyojawa na ubaya wa Shetani, na maji ya matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maana ya Kuwa Mtu Halisi

134. Miaka yenu mingi ya matendo mbele Yangu imenipa jibu ambalo Sijawahi kupata hapo awali. Na swali la jibu hili ni: “Mtazamo wa mwanadamu mbele ya ukweli na Mungu wa ukweli ni upi?” Juhudi ambazo Nimemwagia mwanadamu ni dhihirisho la kiini Changu cha kumpenda mwandamu, na vitendo na matendo ya mwanadamu mbele Yangu pia yamedhihirisha kiini cha mwanadamu cha kuchukia ukweli na kunipinga Mimi. Katika wakati wote Mimi hujali wale wote ambao wamenifuata, lakini hakuna wakati ambao wale wanaonifuata wameweza kupokea neno Langu; hawana uwezo kabisa wa kukubali hata maoni yanayotoka Kwangu. Hili ndilo hunihuzunisha zaidi ya yote. Hakuna anayeweza kunielewa na, zaidi ya hayo, hakuna anayeweza kunikubali, hata ingawa mtazamo Wangu ni wa kweli na maneno Yangu ni ya upole. Wote wanafanya kazi Niliyowaaminia kuifanya kulingana na fikira zao; hawatafuti nia Zangu, wala kuuliza maombi Yangu. Bado wanadai kuwa Wananihudumia kwa uaminifu, wakati huu wote wakiwa wananiasi. Wengi wanaamini kuwa ukweli usiokubalika nao au ukweli ambao hawawezi kutia vitendoni sio ukweli. Kwa watu kama hawa, ukweli Wangu unakuwa kitu cha kukataliwa na kutupiliwa kando. Kwa wakati uo huo Ninakuwa mmoja anayetambuliwa na mwanadamu kwa neno tu kama Mungu, lakini pia kuchukuliwa kama mtu wa nje ambaye sio ukweli, njia na uhai. Hakuna anyejua ukweli huu: Maneno yangu ndio ukweli usiobadilika milele. Mimi Ndiye msambazaji wa binadamu na kiongozi wa pekee wa mwanadamu. Thamani na maana ya maneno Yangu haibainishwi na kama yanakubaliwa au kutambuliwa na mwanadamu, ila ni kwa kiini cha maneno yenyewe. Hata kama hakuna mtu hata mmoja duniani anaweza kupokea maneno Yangu, thamani ya maneno Yangu na usaidizi wake kwa mwanadamu hayapimiki na mwanadamu yeyote. Kwa hivyo, Ninapokumbwa na wanadamu wengi wanaoasi, kukataa au kudharau kabisa maneno Yangu, msimamo Wangu ni huu tu: Wacha wakati na ukweli uwe shahidi Wangu na uonyeshe kuwa maneno Yangu ndiyo ukweli, njia na uhai. Wacha vionyeshe kuwa yote Niliyosema ni ya ukweli, na kuwa ni yale ambayo mwanadamu lazima apewe, na, zaidi ya yote, yale ambayo mwanadamu anafaa akubali. Nitawaruhusu wote wanaonifuata wajue ukweli huu: Wote wasioyakubali maneno Yangu kikamilifu, wale wasioyaweka maneno Yangu katika vitendo, wale wasiopata sababu ndani ya maneno Yangu, na wale wasiopata wokovu kwa sababu ya maneno Yangu, ni wale ambao wamehukumiwa na maneno Yangu na, zaidi ya hayo, wamepoteza wokovu Wangu, na fimbo Yangu haitaondoka kamwe miongoni mwao.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu

Tanbihi:

a. Matini ya asili haina kauli “kuelewa kwamba.”

b. Kurudi ufuoni: nahau ya Kichina, ikiwa na maana kwamba “mtu kuacha njia zake za uovu.”

Iliyotangulia: A. Maneno Juu ya Kufichua Jinsi Shetani Huwapotosha Wanadamu

Inayofuata: C. Maneno Juu ya Kufichua Mawazo, Uzushi na Uongo wa Kidini wa Wanadamu Wapotovu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp