162 Kukimbia Kuelekea Njia ya Mwanga
1 Ona uovu wa ulimwengu, Shetani amewapotosha watu kwa ukatili sana. Wakipapasa na kupambana ndani ya maumivu na giza, binadamu wanawezaje kupata njia ing’aayo ya uzima? Kwa bahati nzuri Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli, nimesikia sauti Yake na kumrudia Yeye. Ninashuhudia kuonekana na kazi ya Kristo wa siku za mwisho, lakini napitia kufuatiliwa na kuteswa na serikali ya China. Mara nyingi mimi huomba katika usiku wa giza, maneno ya Mungu hunipa imani na nguvu. Ili kuwaokoa binadamu Mungu huvumilia aibu kubwa, kuteseka pamoja na Kristo ni heshima kubwa sana. Nimebarikiwa kusikia matamko ya Mungu, kumwamini Mungu bila kupata ukweli kungekuwa aibu kubwa. Haijalishi hatari na matatizo ambayo yako mbele, naacha kila kitu ili kumfuata Kristo hadi mwisho.
2 Katika gereza la giza na la kutisha la Kichina, kupitia mateso nilikuwa nilielea kati ya uzima na kifo. Kwa kukata tamaa Maneno ya Mungu yalinipa faraja na kunitia moyo. Kwa kuhisi upendo wa Mungu, nililia machozi mengi. Niliona utunzaji na ulinzi wa Mungu usiokoma, nilijua mamlaka na nguvu za maneno Yake. Gereza la shetani lilikuwa kama kuzimu, nilikuwa maumivuni lakini nilikua karibu na Mungu. Kupitia mateso, dhiki, majaribu, nimeshauona uso wa kishetani wa Chama cha Kikomunisti cha China. Mfalme wa ibilisi yumo mamlakani, anadanganya na kusema uongo, anawashawishi watu kuingia katika uchafu. Kristo wa siku za mwisho ameonekana na kufanya kazi, akiwaletea binadamu mwanga na ukweli. Wale walio na moyo na roho lazima wachague ukweli na haki, hata kama inamaanisha kutoa maisha yao. Kuamini kwa uthabiti kwamba Kristo ni ukweli, njia, uzima, nakimbia kuelekea njia ya mwanga.