427 Mungu Awatuza Mara Mbili Zaidi Wale Wanaoshirikiana Naye

1 Ikiwa unaishi maisha haya ya kiroho kila siku, basi utaweza kumpa Mungu moyo wako zaidi na zaidi, roho yako itakuwa imara zaidi na zaidi, hali yako itakuwa bora zaidi na zaidi, utakuwa na uwezo zaidi wa kutembea katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu, na Mungu atakupa baraka zaidi na zaidi. Lengo la maisha yenu ya kiroho ni kutafuta kwa makusudi na kupata kuwepo kwa Roho Mtakatifu. Sio kuzingatia sheria au kufanya taratibu za dini, bali kutenda kweli pamoja na Mungu na kudhibiti miili yenu. Hiki ndicho mwanadamu anapaswa kufanya, kwa hiyo lazima mtumie juhudi zenu zote ili kufanya hivi.

2 Kadri unavyoshirikiana bora zaidi na kadri unavyojitahidi zaidi, ndivyo utakavyoweza zaidi kugeuza moyo wako kwa Mungu, na ndivyo utakavyozidi kutuliza moyo wako mbele Yake. Mara tu utakapofikia hali fulani, Mungu ataupata moyo wako kabisa. Hakuna atakayeweza kuyumbisha au kuuteka moyo wako, na utakuwa wa Mungu kabisa. Ikiwa unatembea katika njia hii, neno la Mungu litajifichua kwako wakati wote na kukupa nuru kwa kila kitu ambacho huelewei—hii yote inaweza kutimizwa kwa sababu ya ushirikiano wako. Hii ndiyo maana Mungu daima husema, “Wote wanaofanya kazi pamoja na Mimi, Nitawatuza mara mbili.”

Umetoholewa kutoka katika “Maisha ya Kawaida ya Kiroho Huwaongoza Watu Kwenye Njia Sahihi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 426 Unapaswa Kujitahadhari Kutuliza Moyo Wako Mbele za Mungu

Inayofuata: 428 Jinsi ya Kutulia Mbele za Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp