279 Mungu Aliisifu Toba ya Mfalme wa Ninawi

“Naye Yona akaanza kuingia ndani ya mji huo safari ya siku moja, na akatoa sauti kubwa, na kusema, Imebaki siku arobaini, na Ninawi utashindwa.” Haya ndiyo maneno ambayo Mungu alipitisha moja kwa moja kwake Yona ili aweze kuwaambia Waninawi. Ndiyo pia, kwa kawaida, maneno ambayo Yehova alipenda kusema kwa Waninawi.

1 Wakati mfalme wa Ninawi alipozisikia habari hizi, aliinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua nguo zake, akavalia nguo ya gunia na kukalia jivu. Kisha akatangaza kwamba hakuna mtu kwenye mji huo ambaye angeruhusiwa kuonja chochote, na kuwa hakuna mifugo, wanakondoo na ng’ombe ambao wangekunywa maji na kula nyasi. Binadamu na mifugo kwa pamoja walitakikana kujifunika nguo ya gunia; nao watu wangemsihi Mungu kwa uaminifu. Mfalme pia alitangaza kwamba watu wote wangetupilia mbali njia zao za maovu na kukataa udhalimu ulioko mikononi mwao. Tukifanya uamuzi kutoka kwenye misururu ya vitendo hivi, mfalme wa Ninawi alionyesha toba yake ya dhati. Kupitia misururu hii ya vitendo, mfalme wa Ninawi aliweza kukamilisha kwa kweli kile ambacho kiongozi anafaa kufanya; misururu ya vitendo vyake ndiyo iliyokuwa migumu kwa mfalme yeyote katika historia ya binadamu kutimiza, hatua na pia hatua ambayo hakuna aliyewahi kutimiza. Matendo haya yanaweza kuitwa shughuli isiyo na kifani katika historia ya binadamu; yanastahili kukumbukwa na kuigwa na binadamu.

2 Tangu enzi ya mwanadamu, kila mfalme alikuwa amewaongoza wafuasi wake kukinzana na kumpinga Mungu. Hakuna yule aliyewahi kuwaongoza wafuasi wake kusihi Mungu kutafuta ukombozi kwa ajili ya maovu yao, kupokea msamaha wa Yehova Mungu na kuepuka adhabu kali. Mfalme wa Ninawi, hata hivyo, aliweza kuwaongoza raia wake kumlilia Mungu, kuacha njia zao mbalimbali za maovu na kutupilia mbali udhalimu ulio mikononi mwao. Aidha, aliweza pia kuweka kando kiti chake cha enzi, na badala yake, Yehova Mungu alibadilisha na kughairi na kugeuza hasira Yake, na kuruhusu watu wa mji huu kuishi na kuwalinda dhidi ya kuangamia. Matendo ya mfalme yanaweza kuitwa tu muujiza wa nadra katika historia ya binadamu; yanaweza hata kuitwa kielelezo cha binadamu uliopotoka unaoungama na kutubu dhambi zake mbele ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 278 Hakuna Nguvu Inayoweza Kuzuia Yale Ambayo Mungu Anataka Kufanikisha

Inayofuata: 280 Mungu Ndiye Mkuu wa Pekee wa Majaliwa ya Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp