424 Kumtumainia na Kumtegemea Mungu ni Hekima Kubwa Zaidi

1 Bila kujali mtu anaelewa ukweli kiasi gani, ni kiasi kipi cha wajibu ambacho mtu ametimiza, ni kiasi gani cha uzoefu ambacho mtu amepata wakati wa kutekeleza wajibu huo, jinsi kimo cha mtu kilivyo kikubwa au kidogo, au aina ya mazingira ambayo mtu yuko ndani, jambo moja ambalo hawezi kulikosa ni kwamba katika kila kitu anachofanya, lazima amtegemee Mungu na kumtumainia Mungu. Hii ndiyo aina kubwa zaidi ya hekima. Hata kama mtu amekuja kuelewa ukweli mwingi, je, atafanikiwa iwapo hamtumainii Mungu? Watu wengine, baada ya kumwamini Mungu kwa muda mrefu kidogo, wamekuja kuelewa ukweli kiasi na wamepitia majaribu machache. Huenda wana uzoefu mdogo wa kiutendaji, lakini hawajui jinsi ya kumtegemea Mungu, na hawaelewi jinsi ya kumtumainia Mungu. Je, watu kama hawa wana hekima? Wao ndio watu wapumbavu zaidi, na ni aina ya watu ambao hujiona kuwa mahiri; hawamwogopi Mungu na kuepuka uovu.

2 Kuwa na ufahamu kuhusu maneno halisi na kuongea juu ya mafundisho mengi ya kiroho si sawa na ufahamu wa ukweli, sembuse kuwa sawa na wewe kuelewa kikamilifu mapenzi ya Mungu katika kila hali. Kwa hivyo kuna somo la muhimu sana la kujifunza hapa. Ni kwamba watu wanahitaji kumtegemea Mungu katika mambo yote, na kwamba kwa kumtegemea Mungu katika mambo yote, watu wanaweza kufanikisha imani katika Mungu. Ni kwa kumtegemea Mungu tu ndio watu wanakuwa na njia ya kufuata. Kuna tatizo kubwa hapa, ambalo ni kwamba watu hufanya mambo mengi kwa kutegemea uzoefu wao na sheria ambazo wameelewa, na mawazo fulani ya binadamu. Wanaweza kufikia matokeo bora kabisa kwa shida, ambayo hutokana na kuelewa mapenzi ya Mungu kwa wao kumtegemea Mungu na kumwomba Mungu, na kisha kwa kutumainia kazi na mwongozo wa Mungu. Kwa hivyo Nasema: Hekima kuu zaidi ni kumtegemea Mungu na kumtumainia Mungu katika mambo yote.

Umetoholewa kutoka katika “Waumini Wanahitaji Kwanza Kubaini Mielekeo Mibaya ya Dunia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 423 Hakuna Huduma ya Kweli Bila Ombi la Kweli

Inayofuata: 425 Wale Tu Walio Watulivu Mbele Ya Mungu Ndio Wanaolenga Maisha

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp