811 Ufuatiliaji wa Petro Ulilingana Zaidi na Mapenzi ya Mungu

1 Wakati ambapo alipitia mamia ya majaribio kutoka kwa Mungu, Petro alijichunguza kabisa dhidi ya kila neno la hukumu ya Mungu kwa mwanadamu, kila neno la ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu, na kila neno la madai Yake kwa mwanadamu, na akajitahidi kuelewa maana ya maneno hayo. Alijaribu kwa bidii kutafakari na kukariri kila neno ambalo Yesu alimwambia, na alitimiza matokeo mazuri sana. Kupitia namna hii ya utendaji, aliweza kutimiza kujifahamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na hakuja tu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu, lakini pia alikuja kuelewa kiini, asili, na dosari mbalimbali za mwanadamu. Hii ndiyo maana ya kujifahamu kwa kweli.

2 Kutoka kwa maneno ya Mungu, Petro hakutimiza tu kujifahamu kwa kweli, lakini kutokana na mambo yaliyoonyeshwa katika maneno ya Mungu—tabia ya Mungu yenye haki, kile Anacho na alicho, mapenzi ya Mungu kwa kazi Yake, mahitaji Yake kwa wanadamu—kutoka kwa maneno haya alikuja kumjua Mungu kabisa. Alikuja kujua tabia ya Mungu, na asili yake; alikuja kujua na kuelewa kile Mungu anacho na Alicho, na vilevile uzuri wa Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu. Petro alipitia mamia ya majaribio, lakini hakuteseka bure. Hakuja kujielewa tu kutokana na maneno na kazi ya Mungu, lakini pia alikuja kumjua Mungu.

3 Alizingatia hasa matakwa ya Mungu kwa wanadamu ndani ya maneno Yake. Bila kujali ni katika hali gani mwanadamu anapaswa kumridhisha Mungu ili kukubaliana na mapenzi ya Mungu, Petro aliweza kufanya juhudi kubwa katika vipengele hivi na kupata uwazi kamili; hili lilikuwa la manufaa kubwa sana kwa kuingia kwake mwenyewe. Haijalishi kile ambacho Mungu alizungumzia, maadamu maneno hayo yangeweza kuwa maisha yake na yalikuwa ya ukweli, Petro aliweza kuyaweka ndani ya moyo wake kuyatafakari na kuyathamini mara kwa mara. Baada ya kuyasikia maneno ya Yesu, aliweza kuathiriwa nayo, ambalo linaonyesha kuwa alikuwa akizingatia hasa maneno ya Mungu, na alitimiza matokeo mwishowe kwa kweli. Yaani, aliweza kuyatia maneno ya Mungu katika vitendo kwa uhuru, kutenda kwa usahihi ukweli na kukubaliana na mapenzi ya Mungu, kutenda kikamilifu kwa mujibu wa nia ya Mungu, na kuacha maoni na mawazo yake mwenyewe. Kwa njia hii, Petro aliingia katika ukweli wa maneno ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 810 Petro Daima Alifuatilia Kumjua Mungu

Inayofuata: 812 Petro Alilenga Kumjua Mungu kwa Vitendo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp