221 Kutakaswa na Maneno ya Mungu

1 Nilimwamini Bwana kwa miaka mingi na nilikuwa na mwenendo mzuri, na nilidhani nilikuwa nimebadilika. Nilifanya kazi kidogo kisha nikaomba baraka za Mungu, na nilidhani jambo hili lilistahili kabisa. Nilihubiri maarifa ya teolojia na nadharia pekee, na nilidhani nilikuwa na ukweli. Ni wakati nilipohukumiwa na kuadibiwa na maneno ya Mungu tu ndipo nilipata uvumbuzi. Sikuwa na ufahamu hata mdogo kuhusu ukweli na maisha vilikuwa nini. Yote niliyotaka ilikuwa kupata baraka za ufalme wa mbinguni kama malipo ya kufanya kazi, kuteseka na kulipa gharama. Sikuwahi kuyaweka katika vitendo au kuyapitia maneno ya Bwana, lakini bado nilitaka kupata sifa za Bwana. Lakini sasa nagundua kuwa fikira na mawazo yangu yalikuwa yamenipofusha. Isingekuwa hukumu na wokovu wa Mungu, ningekuwa bado ninaishi gizani.

2 Maneno yote ya Mwenyezi Mungu ni ukweli. Yanapenya kabisa katika kina cha moyo wangu. Hukumu na ufunuo wa Mungu, yote ni ukweli, hakuna mahali pa kuficha uso wangu kwa aibu. Asili yangu ni ya tamaa na ubinafsi, nilimwamini Bwana kwa ajili ya tuzo tu. Nilizungumza juu ya jinsi nilivyompenda Bwana lakini moyo wangu ulipenda ulimwengu na starehe za mwili. Ingawa nilionekana kutenda vyema, moyo wangu ulikuwa umejaa tabia za kishetani. Nilifanya kazi na kuhubiri kwa sababu tu ya hadhi na sikuwa na ucha Mungu hata kidogo. Kila neno na tendo langu lilikuwa utendaji wa ibada za dini, na hayakuhusiana na ukweli. Nilikuwa mpotovu sana, ningewezaje kustahili kuingia katika ufalme wa mbinguni bila kuhukumiwa na kutakaswa? Nagundua sasa kuwa hukumu na kuadibu kwa Mungu ni wokovu Wake kwangu.

3 Mungu hutawala juu ya kila kitu na hupanga mazingira yote, kuna mengi ya kujifunza kila siku. Natuliza moyo wangu mbele za Mungu na kusoma maneno Yake, nikiishi kila siku mbele ya Mungu. Ninapofanya wajibu wangu na kutenda maneno ya Mungu, naona kwamba nimekosa mengi sana. Ninapotafakari juu ya upotovu wangu, naona kuwa siishi kwa kudhibitisha ubinadamu wa kawaida. Kwa njia ya kupitia hukumu, majaribio, upogoaji na ushughulikiaji, naona upendo wa Mungu. Natumia maneno ya Mungu katika maisha halisi, natafuta ukweli katika vitu vyote. Katika uzoefu wangu wa vitendo naona kuwa kila neno la Mungu ni ukweli. Kwa kutenda kufuatana na maneno ya Mungu, tabia zangu potovu zinasafishwa polepole. Kwa kumwogopa Mungu na kuepukana na uovu mwishowe napata sifa za Mungu.

Iliyotangulia: 220 Hukumu ya Mungu Huniokoa Kutokana na Dhambi

Inayofuata: 222 Rehema ya Mungu Ilinihuisha Tena

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki