XV. Maneno Juu ya Kutabiri Uzuri wa Ufalme na hatima ya Wanadamu, na Ahadi na Baraka za Mungu

686. Kazi Yangu inadumu kwa miaka elfu sita tu, na Mimi niliahidi kwamba udhibiti wa yule mwovu juu ya wanadamu wote utakuwa pia si zaidi ya miaka elfu sita. Na kwa hivyo, wakati umeisha. Nami wala Sitaendelea wala kuchelewa tena: Katika siku za mwisho Nitamshinda Shetani, nami Nitaumiliki tena utukufu Wangu wote, na kurudisha nafsi zile zote zilizo Zangu duniani ili nyoyo hizi za dhiki ziweze kutoroka kutoka bahari ya mateso, na hivyo Nitakuwa nimetimiza kazi Yangu nzima duniani. Kutoka siku hii na kuendelea, kamwe Sitawahi kuwa mwili duniani, na kamwe Roho Wangu wa kudhibiti yote Hatafanya kazi tena duniani. Lakini Nitafanya jambo moja duniani: Nitamfanya tena mwanadamu, mwanadamu aliye mtakatifu, na aliye mji Wangu mwaminifu duniani. Lakini ujue kwamba Sitaiangamiza dunia nzima, wala kuangamiza ubinadamu mzima. Nitahifadhi theluthi moja iliyobaki—theluthi moja inayonipenda na imeshindwa kabisa na Mimi, na Nitaifanya theluthi hii iwe yenye kuzaa matunda na kuongezeka duniani kama Israeli walivyofanya chini ya sheria, kuwalisha kwa kondoo wengi mno na mifugo, na utajiri wote wa dunia. Mwanadamu huyu atabaki na Mimi milele, hata hivyo si mwanadamu mchafu wa kusikitisha wa leo, lakini mwanadamu ambaye ni mkusanyiko wa wale wote ambao wamepatwa na Mimi. Mwanadamu wa aina hii hataharibiwa, kusumbuliwa, au kuzungukwa na Shetani, na atakuwa mwanadamu wa pekee anayepatikana duniani baada ya ushindi Wangu juu ya Shetani. Ni wanadamu ambao leo wameshindwa na Mimi na wamepata ahadi Yangu. Na hivyo, wanadamu ambao wameshindwa katika siku za mwisho pia ndio watakaosamehewa na kupata baraka Zangu za milele. Huu utakuwa ushahidi wa pekee wa ushindi Wangu dhidi ya Shetani, na nyara za pekee za vita Vyangu na Shetani. Hizi nyara za vita zimeokolewa nami kutoka utawala wa Shetani, na ni thibitisho la pekee na matunda ya mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita. Wao huja kutoka kila taifa na dhehebu, na kila mahali na nchi ulimwenguni mwote. Ni wa jamii tofauti, na wana lugha mbalimbali, mila na rangi ya ngozi, na huenea katika kila taifa na dhehebu la duniani, na hata kila pembe ya dunia. Hatimaye, watakuja pamoja na kuunda ubinadamu kamili, mkusanyiko wa binadamu usiofikiwa na majeshi ya Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

687. Kwa kuwa maneno Yangu yametimilika, ufalme utaumbwa duniani hatua kwa hatua na mwanadamu atarudishwa kwa ukawaida hatua kwa hatua, na hivyo basi kutaanzishwa duniani ufalme ndani ya moyo Wangu. Katika ufalme, watu wote wa Mungu hupata maisha ya mwanadamu wa kawaida. Msimu wa barafu yenye baridi kali umeenda, umebadilishwa na dunia ya miji ya majira ya chipuko, ambapo majira ya chipuko yanashuhudiwa mwaka mzima. Kamwe, watu hawakumbwi tena na ulimwengu wa mwanadamu wenye huzuni na wenye taabu, na hawavumilii kuishi kwenye baridi kali ya dunia ya mwanadamu. Watu hawapigani na wenzao, mataifa hayaendi vitani dhidi ya wenzao, hakuna tena uharibifu na damu imwagikayo kutokana na uharibifu huo; maeneo yote yamejawa na furaha, na kila mahali pote panafurikwa na joto baina ya wanadamu. Naenda Nikipitia dunia nzima, Nafurahia kutoka juu ya kiti Changu cha enzi, Naishi miongoni mwa nyota. Na malaika wananipa nyimbo mpya na dansi mpya. Udhaifu wao hausababishi machozi kutiririka nyusoni mwao tena. Sisikii tena, mbele Yangu, sauti za malaika wakilia, na hakuna tena anayeninung’unikia kuwa ana shida. Leo hii, nyote mko hai mbele Yangu; kesho nyote mtakua hai ndani ya ufalme Wangu. Je, si hii ndiyo baraka kubwa zaidi ambayo Nimempa mwanadamu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 20

688. Ufalme utakaposhuka duniani kabisa, watu wote watapata tena mfano wao wa asili. Hivyo, Mungu asema, “Nafurahia kutoka juu ya kiti Changu cha enzi, Naishi miongoni mwa nyota. Na malaika wananipa nyimbo mpya na dansi mpya. Udhaifu wao hausababishi machozi kutiririka nyusoni mwao tena. Sisikii tena, mbele Yangu, sauti za malaika wakilia, na hakuna tena anayeninung’unikia kuwa ana shida.” Hili linaonyesha kwamba siku ambayo Mungu atapata utukufu kamili ndiyo siku ambayo mwanadamu atafurahia pumziko lake; watu hawakimbii huku na huko tena kutokana na usumbufu wa Shetani, dunia inaacha kuendelea mbele, na watu wanaishi katika pumziko—kwa kuwa idadi kubwa mno ya nyota angani zinafanywa upya, na jua, mwezi, na nyota, na kadhalika, na milima na mito yote iliyo mbinguni na duniani, vyote vinabadilishwa. Na kwa kuwa mwanadamu amebadilika, na Mungu amebadilika, kwa hiyo, pia, vitu vyote vinabadilika. Hili ndilo lengo la msingi la mpango wa usimamizi wa Mungu, na ule ambao utatimizwa hatimaye.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 20

689. Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, mwanadamu amepata tena utakatifu aliokuwa nao wakati mmoja. Eh, dunia potovu ya zamani! Mwishowe, imeanguka na kutumbukia ndani ya maji machafu na, imezama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope! Ah, ya kwamba binadamu wote Niliouumba hatimaye umerudiwa na uhai tena katika mwanga, kupata msingi wa kuwepo, na kuacha kupambana katika tope! Ah, Mambo mengi ya uumbaji Ninayoyashikilia mikononi Mwangu! Wanawezaje, kukosa kufanywa upya, kupitia maneno Yangu? Wanawezaje, katika mwanga, kukosa kuendeleza kazi zao? Dunia si kimya cha mauti na nyamavu tena, mbingu si ya ukiwa na yenye huzuni tena. Mbingu na nchi, bila kutenganishwa na utupu tena, zimeungana kama kitu kimoja, kamwe kutotenganishwa tena. Katika wakati huu wa shangwe, wakati huu wa nderemo, haki Yangu na utakatifu Wangu umeenea katika kila pembe ya ulimwengu, na binadamu wote wanavisifu bila kikomo. Miji yote ya mbingu inacheka kwa furaha, na falme zote za nchi zinacheza kwa shangwe. Ni nani wakati huu ambaye haonyeshi furaha? Na ni nani wakati huu ambaye halii? Nchi katika hali yake ya asili ni miliki ya mbingu, na mbingu imeungana na nchi. Mwanadamu ni ugwe unaounganisha mbingu na nchi, na kwa sababu ya utakatifu wa mwanadamu, kwa ajili ya kufanywa upya kwa mwanadamu, mbingu haijafichwa tena kutoka kwa nchi, na nchi haiko kimya tena kwa mbingu. Nyuso za binadamu zimezingirwa na tabasamu za shukurani, na nyoyo zao zinadondokwa na utamu usiokuwa na kifani. Mwanadamu hagombani na mwanadamu, wala binadamu kupigana wenyewe kwa wenyewe. Kunao wale ambao, katika mwanga Wangu, hawaishi kwa furaha na wenzao? Kunao wale ambao, katika siku Yangu, hulifedhehesha jina Langu? Watu wote huelekeza macho yao ya heshima Kwangu, na wao hunililia kwa siri katika nyoyo zao. Nimechunguza kila kitendo cha binadamu: Miongoni mwa wanadamu waliotakaswa, hakuna yeyote aliye mkaidi Kwangu, hakuna anayenielekezea hukumu. Binadamu wote umejawa na tabia Yangu. Kila mtu anakuja kunijua, ananijongelea, na ananiabudu. Msimamo wangu ni mmoja katika roho ya mwanadamu, Nimetukuzwa kwa kiwango cha juu zaidi kwa macho ya mwanadamu, na hububujika katika damu ya mishipa yake. Nderemo za furaha katika nyoyo za wanadamu huenea kila sehemu ya uso wa nchi, hewa ni ya kuchangamsha na bichi, ukungu mzito hauitandai ardhi tena, na mwangaza wa jua huvutia.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 18

690. Katika nuru Yangu, watu wanaiona nuru tena. Katika neno Langu, watu wanapata mambo ambayo wanafurahia. Nimekuja kutoka Mashariki, Ninatoka Mashariki. Utukufu Wangu unapoangaza, mataifa yote yanatiwa nuru, vitu vyote vinaletwa kwenye mwanga, hakuna kitu hata kimoja kinachobaki gizani. Katika ufalme, maisha ambayo watu wa Mungu wanaishi pamoja na Mungu ni yenye furaha kupita kiasi. Maji yanacheza kwa furaha katika maisha ya watu yenye baraka, milima inafurahia pamoja na watu katika wingi Wangu. Wanadamu wote wanajitahidi, wakifanya bidii, wakionyesha uaminifu wao katika ufalme Wangu. Katika ufalme, uasi haupo tena, upinzani haupo tena; mbingu na dunia zinategemeana, Mimi na mwanadamu tunakaribiana katika hisia ya kina, katika furaha kuu tamu ya maisha, tukiegemeana…. Wakati huu, Ninayaanza rasmi maisha Yangu mbinguni. Usumbufu wa Shetani haupo tena, na watu wanaingia katika pumziko. Ulimwenguni kote, watu Wangu wateule wanaishi ndani ya utukufu Wangu, wakiwa wamebarikiwa sana, si kama watu wanaoishi kati ya watu, lakini kama watu wanaoishi na Mungu. Binadamu wote wamepitia upotovu wa Shetani, na kuishi maisha ya mateso makubwa. Sasa, mtu anawezaje kutofurahia akiishi katika nuru Yangu? Mtu anawezaje kuuachilia wakati huu mzuri umponyoke? Enyi watu! Imbeni wimbo ulio mioyoni mwenu na mnichezee kwa furaha! Iinueni na mnitolee mioyo yenu ya dhati! Pigeni ngoma zenu na mnichezee kwa furaha! Ninaangaza furaha Yangu ulimwenguni kote! Naufichua uso Wangu mtukufu kwa watu! Nitaita kwa sauti kubwa! Nitaupita ulimwengu wote! Tayari Ninatawala kati ya watu! Ninatukuzwa na watu! Ninapeperuka kwenye mbingu zenye rangi ya samawati na watu wanakwenda wakitembea pamoja nami. Ninatembea kati ya watu na watu Wangu wananizunguka! Mioyo ya watu ni yenye furaha, nyimbo zao zinautikisa ulimwengu, zikiipasua mbingu! Ulimwengu haujafunikwa kwa ukungu tena; hakuna matope tena, hakuna mkusanyiko wa maji machafu tena. Watu watakatifu wa ulimwengu! Mnaonyesha nyuso zenu za kweli chini ya ukaguzi Wangu. Ninyi sio watu mliofunikwa na uchafu, lakini ni watakatifu walio safi kama jiwe la thamani lenye rangi ya kijani kibichi, ninyi nyote ni wapendwa Wangu, ninyi nyote ni furaha Yangu! Vitu vyote vinafufuka! Watakatifu wote wamerejea ili kunitumikia mbinguni, wakiingia katika kumbatio Langu lililo changamfu, hawalii tena, hawana wasiwasi tena, wakijitoa Kwangu, wakirudi nyumbani Kwangu, nao watanipenda bila kukoma katika nchi yao! Wasibadilike kamwe milele! Huzuni iko wapi! Machozi yako wapi! Mwili uko wapi! Dunia inapita, lakini mbingu ni za milele. Ninawaonekania watu wote, na watu wote wananisifu. Maisha haya, uzuri huu, tangu zama za kale hadi mwisho wa dahari, havitabadilika. Haya ndiyo maisha ya ufalme.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Furahini, Enyi Watu Wote!

691. Ufalme unapanuka miongoni mwa binadamu, unachipua miongoni mwa binadamu, unasimama miongoni mwa binadamu; hakuna nguvu inayoweza kuharibu ufalme Wangu. Kwa watu Wangu walio katika ufalme wa leo, nani kati yenu si mwanadamu miongoni mwa wanadamu? Nani kati yenu yu nje ya hali ya ubinadamu? Wakati hatua Yangu ya kwanza mpya itatangazwa kwa wengi; binadamu utaguswa vipi? Mmeona na macho yenu hali ya mwanadamu; hakika bado hamna matumaini ya kudumu milele kwa dunia hii? Sasa Natembea ng’ambo katikati ya watu Wangu, Naishi katikati ya watu Wangu. Leo, walio na pendo la kweli Kwangu, watu kama hawa wamebarikiwa; wamebarikiwa wanaonitii, hakika watabaki katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonijua, hakika watakuwa na mamlaka katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonitafuta, hakika watatoroka vifungo vya Shetani na kufurahia baraka ndani Yangu; wamebarikiwa wanaoweza kujiacha, hakika wataingia katika milki Yangu, na kurithi fadhila ya ufalme Wangu. Wanaokimbia kimbia kwa ajili Yangu Nitawakumbuka, wanaopata gharama kwa ajili Yangu Nitawakumbatia kwa furaha, wanaonitolea sadaka Nitawapa starehe. Wanaopata raha ndani ya maneno Yangu, Nitawabariki; hakika watakuwa nguzo zinazoshikilia mwamba kwa ufalme Wangu, hakika watakuwa na fadhila isiyo na kifani kwa nyumba Yangu, na hakuna anayeweza kulinganishwa nao. Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kuzitafuta ahadi mlizofanyiwa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya katika utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtasimama imara na thabiti katika nchi ya Sinimu. Kupitia katika mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaonyesha utukufu Wangu katika ulimwengu mzima.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 19

692. Hekima Yangu iko kote duniani, na katika ulimwengu mzima. Miongoni mwa vitu vyote, kuna matunda ya hekima Yangu, miongoni mwa watu wote, kumejaa kazi bora zaidi za hekima Yangu; kila kitu ni kama mambo yote katika ufalme Wangu, na watu wote wanakaa kwa mapumziko chini ya mbingu Zangu kama kondoo kwenye uwanja Wangu wa malisho. Nasonga juu ya wanadamu wote na Natazama kila mahali. Hakuna kinachokaa kizee kamwe, na hakuna mtu ambaye yuko kama alivyokuwa. Ninapumzika katika kiti cha enzi, Naegemea juu ya ulimwengu mzima, na Nimeridhika kikamilifu, kwani kila kitu kimerejesha utakatifu wake, na Ninaweza kukaa kwa amani ndani ya Zayuni tena, na watu duniani wanaweza kuishi maisha tulivu na ya kuridhisha chini ya mwongozo Wangu. Watu wote wanasimamia kila kitu mikononi Mwangu, watu wote wamerejesha akili zao za awali na mwonekano wao wa kiasili; hawafunikwi tena na vumbi, lakini, ndani ya ufalme Wangu, ni safi kama lulu, kila mmoja akiwa na uso kama vile wa yule mtakatifu aliye ndani ya moyo wa binadamu, kwani ufalme Wangu umeimarishwa miongoni mwa binadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 16

693. “Nasonga juu ya wanadamu wote na Natazama kila mahali. Hakuna kinachokaa kizee kamwe, na hakuna mtu ambaye yuko kama alivyokuwa. Ninapumzika katika kiti cha enzi, Naegemea juu ya ulimwengu mzima….” Haya ni matokeo ya kazi ya Mungu ya sasa. Wateule wote wa Mungu wanarudi kwa umbo lao la asili, kwa sababu hiyo malaika, ambao wameteseka kwa miaka mingi sana, wanaachiliwa, kama tu asemavyo Mungu, “kila mmoja akiwa na uso kama wa mtakatifu ndani ya moyo wa binadamu.” Kwa sababu malaika hufanya kazi duniani na kumhudumia Mungu duniani, na utukufu wa Mungu husambaa kila mahali ulimwenguni, mbingu inaletwa duniani, na dunia inainuliwa kwenda mbinguni. Kwa hivyo, mwanadamu ni kiungo kinachounganisha mbingu na dunia; mbingu na dunia haziko mbali tena, hazijatengana tena, lakini zimeunganishwa kama kitu kimoja. Kotekote ulimwenguni, Mungu na mwanadamu ndio pekee wanaoishi. Hakuna vumbi wala uchafu, na vitu vyote vinafanywa upya, kama mwanakondoo mdogo anayelala katika ukanda wa mbuga wa kijani kibichi chini ya anga, akifurahia neema yote ya Mungu. Na ni kwa sababu ya ujio wa kijani kibichi ndiposa pumzi ya uhai inaangaza, kwani Mungu anakuja duniani kuishi pamoja na mwanadamu milele yote, kama ilivyosemwa kutoka kinywani mwa Mungu kwamba “Ninaweza kukaa kwa amani ndani ya Zayuni tena.” Hii ni ishara ya kushindwa kwa shetani, ni siku ya pumziko la Mungu, na siku hii itatukuzwa na kutangazwa na watu wote, na itafanyiwa kumbukumbu na watu wote. Wakati ambapo Mungu ametulia juu ya kiti cha enzi pia ndio wakati ambapo Mungu anahitimisha kazi Yake duniani, na ndio wakati ule ambao siri zote za Mungu zinaonyeshwa kwa mwanadamu; Mungu na mwanadamu watakuwa katika upatanifu daima, hawatakuwa mbali tena—haya ni mandhari mazuri ya ufalme!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 16

694. Kwa misingi ya kazi zao na shuhuda zao tofauti, washindi katika ufalme watatumika kama makuhani au wafuasi, na wale wote watakaoshinda taabu watakuwa mwili wa makuhani katika ufalme. Baraza la makuhani litaundwa wakati kazi ya injili ulimwenguni kote itafikia kikomo. Wakati huo ukitimia, yale yanayopaswa kufanywa na mwanadamu yatakuwa jukumu lake ndani ya ufalme wa Mungu, na kuishi kwake pamoja na Mungu katika ufalme. Katika baraza la makuhani, patakuwepo makuhani wakuu na makuhani, na watakaosalia watakuwa wana na watu wa Mungu. Haya yote huamuliwa na ushuhuda wao kwa Mungu wakati wa majaribu; sio nyadhifa zinazopeanwa kwa wazo la ghafla. Wakati hadhi ya mwanadamu itakuwa imeianzishwa, kazi ya Mungu itamalizika, kwa kuwa kila mojawapo imewekwa kulingana na aina yake na kurejeshwa katika hali yake halisia, na hii ndiyo alama ya ukamilisho wa kazi ya Mungu, na haya ndiyo matokeo ya mwisho ya kazi ya Mungu na matendo ya mwanadamu, na ndiko kubainika kwa yale maono ya kazi ya Mungu na ushirikiano wa mwanadamu. Mwishowe, mwanadamu atapata pumziko katika ufalme wa Mungu, na, Mungu pia, atarejea kwenye makazi Yake kupumzika. Haya ndiyo yatakayokuwa matokeo ya miaka 6,000 ya ushirikiano wa mwisho kati ya Mungu na mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

695. Punde tu kazi ya ushindi imekwisha kamilika, mwanadamu ataletwa katika dunia nzuri. Haya maisha, bila shaka, bado yatakuwa duniani, lakini yatakuwa tofauti kabisa na jinsi maisha ya mwanadamu yalivyo leo. Ni maisha ambayo mwanadamu atakuwa nayo baada ya wanadamu kwa ujumla kushindwa, itakuwa mwanzo mpya kwa mwanadamu hapa duniani, na kwa wanadamu kuwa na maisha kama hii ni ushahidi kwamba wanadamu wameingia katika milki jipya na nzuri. Itakuwa mwanzo wa maisha ya mwanadamu na Mungu duniani. Nguzo ya maisha mema kama haya ni lazima iwe hivyo, hivi kwamba baada ya mwanadamu kutakaswa na kushindwa, anajiwasilisha mbele za Muumba. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni awamu ya mwisho ya kazi ya Mungu kabla ya wanadamu kuingia katika hatima ya ajabu. Maisha kama haya ni maisha ya baadaye ya mwanadamu duniani, ni maisha yanayopendeza zaidi duniani, aina ya maisha ambayo mwanadamu ametamania, aina ambayo mwanadamu hajawahi kamwe kutimiza katika historia ya ulimwengu. Ni matukio ya mwisho ya miaka 6,000 ya kazi ya usimamizi, na ndicho wanadamu wanatamani sana, na pia ni ahadi ya Mungu kwa mwanadamu. Lakini ahadi hii haiwezi timika mara moja: Mwanadamu ataingia katika hatima ya mbeleni punde tu kazi ya siku za mwisho zitakapokuwa zimemalizika na yeye amekwisha kushindwa kikamilifu, yaani, punde tu Shetani atakapokuwa ameshindwa kabisa. Mwanadamu atakuwa hana asili ya kutenda dhambi baada ya kusafishwa, kwa sababu Mungu atakuwa amemshinda Shetani, ambayo ina maana kuwa hakutakuwepo na kuvamiwa na vikosi vya uhasama, na hakuna vikosi vya uhasama ambavyo vinaweza kushambulia mwili wa mwanadamu. Na kwa hivyo mwanadamu atakuwa huru, na mtakatifu—yeye atakuwa ameingia ahera.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

696. Wakati mtu anafanikiwa kupata maisha ya ukweli ya mwanadamu duniani na vikosi vizima vya Shetani vimefungwa, mwanadamu ataishi kwa urahisi katika ardhi. Mambo hayatakuwa magumu kama yalivyo sasa: Mahusiano ya binadamu, mahusiano ya kijamii, mahusiano changamani ya kifamilia…., haya ni ya kusumbua, machungu mno! Maisha ya mwanadamu hapa ni duni! Punde tu mwanadamu anaposhindwa, moyo wake na akili yake vitabadilika: atakuwa na moyo unaomcha Mungu na moyo ambao unampenda Mungu. Punde tu wote walio ulimwenguni ambao wanatafuta upendo wa Mungu wanaposhindwa, ambayo ni kusema, punde tu Shetani anaposhindwa, na punde tu Shetani—nguvu zote za giza—zimekwisha fungwa, basi maisha ya mwanadamu duniani yatakuwa yasiyotaabishwa, na ataweza kuishi huru duniani. Kama maisha ya mwanadamu hayana mahusiano ya kimwili, na hayana changamani za mwili, basi itakuwa rahisi mno. Mahusiano ya kimwili ya mwanadamu ni changamani mno, na kwa mwanadamu kuwa na mambo kama hayo ni thibitisho kuwa yeye bado hajajikomboa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kama ungekuwa na uhusiano sawa na kila mmoja wa ndugu na dada, kama ungekuwa na uhusiano sawa na kila mmoja wa wanafamilia wako, basi hungekuwa na wasiwasi, na hungekuwa na haja ya kuhofia kuhusu mtu yeyote. Hakuna kitakachoweza kuwa bora zaidi, na kwa njia hii mwanadamu atapunguziwa nusu ya mateso yake. Kuishi maisha ya kawaida ya binadamu duniani, mwanadamu atakuwa sawa na malaika; ingawa atakuwa bado na mwili, atakuwa sawa na malaika. Hii ni ahadi ya mwisho, ni ahadi ya mwisho ambayo mwanadamu amezawadiwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

697. Wale watakaokamilishwa na Mungu ni wale watakaopokea baraka za Mungu na urithi Wake. Yaani, wanasikia na kuelewa kile Mungu Alicho nacho na Alicho, ili kiwe kile ambacho walicho nacho ndani yao; wanayo maneno yote ya Mungu ndani yao; haijalishi ni vipi nafsi ya Mungu ilivyo, mnaweza kusikia na kuelewa kila kitu Anachokuambia vile kilivyo, na hivyo kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Huyu ndiye aina ya binadamu aliyekamilishwa na Mungu na aliyepatwa na Mungu. Binadamu wa aina hii tu ndiye anayestahili kurithi baraka hizi alizofadhiliwa na Mungu:

1) Kupokea upendo mzima wa Mungu.

2) Kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu katika kila kitu.

3) Kupokea mwongozo wa Mungu, kuishi chini ya mwangaza wa Mungu, na kupatiwa nuru na Mungu.

4) Kuishi kwa kudhihirisha taswira inayopendwa na Mungu hapa ulimwenguni; kumpenda Mungu kwa kweli kama vile Petro alivyofanya, kusulubishwa kwa sababu ya Mungu na kustahili kufa kwa kuufidia upendo wa Mungu; kuwa na utukufu sawa na Petro.

5) Kupendwa, kuheshimiwa, na kuvutiwa na wote ulimwenguni.

6) Kushinda utumwa wote wa kifo na Kuzimu, kutoipatia fursa yoyote kazi ya Shetani, kumilikiwa na Mungu, kuishi ndani ya roho safi na changamfu, na kutokuwa na hisia zozote za uchovu.

7) Kuwa na hisia isiyoelezeka ya msisimko na furaha siku zote katika maisha yako yote, ni kana kwamba ameona kuja kwa siku ya utukufu wa Mungu.

8) Kupokea utukufu pamoja na Mungu, na kuwa na sura inayofanana na watakatifu wapendwa wa Mungu.

9) Kuwa kile ambacho Mungu anapenda zaidi ulimwenguni, yaani, mwana mpendwa wa Mungu.

10) Kubadilisha maumbile na kupaa juu pamoja na Baba kwenye mbingu ya tatu, na kuuzidi mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

698. Wakati mwanadamu ataingia kwenye hatima ya milele, mwanadamu atamwabudu Muumba, na kwa sababu mwanadamu amepata wokovu na kuingia ahera, mwanadamu hawezi kimbiza malengo yoyote, wala, zaidi ya hayo, yeye hatakuwa na haja ya kuhangaika kuwa atazingirwa na Shetani. Kwa wakati huu, mwanadamu atajua nafasi yake, na atatekeleza wajibu wake, na hata kama hataadibiwa au kuhukumiwa, kila mtu atatekeleza jukumu lake. Kwa wakati huo, mwanadamu atakuwa kiumbe katika sura na hadhi pia. Hakutakuwepo tena na tofauti ya juu na chini; kila mtu atatekeleza tu kazi tofauti. Bado mwanadamu ataishi katika hatima ya wanadamu yenye utaratibu na ifaayo, mwanadamu atatekeleza wajibu wake kwa ajili ya kumwabudu Muumba, na wanadamu kama hawa ni wanadamu wa milele. Kwa wakati huo, mwanadamu atakuwa amepata maisha yaliyoangaziwa na Mungu, maisha chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, na maisha pamoja na Mungu. Wanadamu wataishi maisha ya kawaida duniani, na wanadamu wote wataingia katika njia sahihi. Mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 utakuwa umemshinda Shetani kabisa, ambayo ina maana kuwa Mungu atakuwa amerejesha sura ya awali ya mwanadamu kufuatia kuumbwa kwake, na kwa hivyo, nia ya awali ya Mungu itakuwa imetimizwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

699. Maisha ya pumziko ni yale bila vita, bila uchafu, bila udhalimu unaoendelea. Hii ni kusema kwamba hayana unyanyasaji wa Shetani (hapa “Shetani” inamaanisha nguvu za uhasama), upotovu wa Shetani, na pia uvamizi wa nguvu yoyote inayompinga Mungu. Kila kitu kinafuata aina yake na kuabudu Bwana wa uumbaji. Mbingu na dunia ni shwari kabisa. Haya ni maisha matulivu ya binadamu. Mungu aingiapo rahani, hakuna udhalimu wowote utakaoendelea duniani, na hakutakuwa na uvamizi wowote wa nguvu za uhasama. Binadamu pia wataingia ulimwengu mpya; hawatakuwa tena binadamu waliopotoshwa na Shetani, lakini badala yake binadamu ambao wameokolewa baada ya kupotoshwa na Shetani. Siku ya pumziko ya binadamu pia ni siku ya pumziko ya Mungu. Mungu alipoteza pumziko Lake kwa sababu wanadamu hawakuweza kuingia rahani; haikuwa kwamba Hakuweza awali kupumzika. Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo. Mungu kuingia rahani kunamaanisha kwamba Hatafanya tena kazi Yake ya wokovu wa binadamu. Binadamu kuingia rahani kunamaanisha kwamba binadamu wote wataishi ndani ya mwangaza wa Mungu na chini ya baraka Zake; hakutakuwa na upotovu wowote wa Shetani, wala maovu yoyote kutokea. Binadamu wataishi kama kawaida duniani, na wataishi chini ya ulinzi wa Mungu. Mungu na mwanadamu waingiapo rahani pamoja, kutamaanisha kwamba binadamu wameokolewa na kwamba Shetani ameangamizwa, kwamba kazi ya Mungu ndani ya mwanadamu imemalizika kabisa. Mungu hataendelea tena kufanya kazi ndani ya mwanadamu, na mwanadamu hataendelea tena kumilikiwa na Shetani. Kwa hivyo, Mungu hatakuwa shughulini tena, na mwanadamu hatakimbiakimbia tena; Mungu na mwanadamu wataingia rahani wakati huo huo. Mungu atarudia nafasi yake ya awali, na kila mtu atarudia nafasi yake husika. Hizi ndizo hatima ambazo Mungu na mwanadamu wataishi ndani kwa utaratibu huu baada ya mwisho wa usimamizi wote wa Mungu. Mungu ana hatima ya Mungu na mwanadamu ana hatima ya mwanadamu. Apumzikapo, Mungu ataendelea kuwaongoza binadamu wote kwa maisha yao duniani. Akiwa kwa mwangaza wa Mungu, mwanadamu atamwabudu Mungu wa kweli aliye mbinguni. Mungu hataishi tena miongoni mwa binadamu, na mwanadamu pia hataweza kuishi na Mungu katika hitimisho la Mungu. Mungu na mwanadamu hawawezi kuishi ndani ya ulimwengu sawa; badala yake, wote wawili wana njia zao binafsi za kuishi. Mungu ndiye anayeongoza binadamu wote, wakati binadamu wote ni matokeo ya kazi ya Mungu ya usimamizi. Ni binadamu wanaoongozwa; kuhusu kiini, binadamu si sawa na Mungu. Kuingia rahani kunamaanisha kurudi pahali pa awali pa mtu. Kwa hivyo, Mungu aingiapo rahani, kunamaanisha kwamba Mungu amerudi pahali Pake pa awali. Mungu hataishi tena duniani ama kushiriki kwa furaha na mateso ya binadamu wakati yupo miongoni mwa binadamu. Binadamu wanapoingia rahani, kunamaanisha kwamba mwanadamu amekuwa kiumbe halisi; binadamu watamwabudu Mungu wakiwa duniani na kuwa na maisha ya kawaida ya wanadamu. Watu hawatakuwa tena wasiomtii Mungu ama kumpinga Mungu; watarudia maisha asili ya Adamu na Hawa. Haya ndiyo maisha na hatima binafsi ya Mungu na binadamu baada ya kuingia rahani. Kushindwa kwa Shetani ni mwelekeo usioepukika katika vita kati ya Mungu na Shetani. Kwa njia hii, kuingia kwa Mungu rahani baada ya kukamilika kwa kazi Yake ya usimamizi na wokovu kamili wa mwanadamu na kuingia rahani pia kunakuwa mielekeo isiyoepukika. Pahali pa pumziko pa mwanadamu ni duniani, na pahali pa Mungu pa pumziko ni mbinguni. Wakati binadamu wanamwabudu Mungu katika pumziko, wataishi duniani, na wakati Mungu anaongoza sehemu iliyobaki ya binadamu katika pumziko, Atawaongoza kutoka mbinguni, sio kutoka duniani. Mungu bado atakuwa Roho, wakati mwanadamu bado atakuwa mwili. Mungu na mwanadamu wote wawili wana njia zao tofauti za kupumzika. Mungu anapopumzika, Atakuja na kujitokeza miongoni mwa mwanadamu, mwanadamu anapopumzika, ataongozwa na Mungu kutembea mbinguni na pia kufurahia maisha mbinguni.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

700. Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani vitatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Iliyotangulia: XIV. Maneno Juu ya Viwango vya Mungu vya Kuyafafanua Matokeo ya Mwanadamu na juu ya Mwisho wa Mtu wa Kila Aina

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp