Utangulizi
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kuikaribisha enzi mpya, kubadilisha njia ambayo kwayo Yeye hufanya kazi, na kufanya kazi ya enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili Anene kutoka katika mitazamo tofauti, ili mwanadamu aweze kumwona Mungu kweli, ambaye ni Neno kuonekana katika mwili, na angeweza kuona hekima na ajabu Yake. Kazi kama hiyo inafanywa ili kufikia malengo ya kumshinda mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu na kumuondoa mwanadamu. Hii ndiyo maana halisi ya kutumia Neno kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia kwa Neno, mwanadamu anakuja kuijua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anafaa kuingia ndani. Kupitia kwa Neno, kazi ambayo Mungu anataka kufanya katika Enzi ya Neno inatimizwa kwa ukamilifu. Kupitia kwa Neno, mwanadamu anafichuliwa, anaondolewa, na kujaribiwa. Mwanadamu ameliona Neno, amelisikia Neno, na kuwa na ufahamu wa kuwepo kwa Neno. Kwa sababu hiyo, anaamini katika kuwepo kwa Mungu, katika uweza na hekima ya Mungu, na vilevile katika upendo wa Mungu kwa mwanadamu na hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Ingawa neno “Neno” ni rahisi na la kawaida, Neno kutoka katika kinywa cha Mungu mwenye mwili hutikisa ulimwengu mzima; linabadilisha moyo wa mwanadamu, mawazo, na tabia ya zamani, na jinsi ulimwengu wote ulivyokuwa ukionekana. Katika enzi zote, ni Mungu wa leo tu ndiye Anayefanya kazi kwa njia hii, na ni Yeye Anayezungumza kwa namna hii na kuja kumwokoa mwanadamu hivi. Kuanzia wakati huu na kuendelea, mwanadamu anaishi chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, akichungwa na kuruzukiwa na maneno Yake. Watu wanaishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, kati ya laana na baraka za maneno ya Mungu, na kuna hata watu wengi zaidi ambao wamekuja kuishi chini ya hukumu na kuadibu kwa maneno Yake. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa sababu ya wokovu wa mwanadamu, kwa sababu ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa sababu ya kubadilisha kuonekana kwa asili kwa ulimwengu wa uumbaji wa zamani. Mungu aliuumba ulimwengu kwa kutumia maneno, Anawaongoza watu ulimwenguni kote kutumia maneno, na Anawashinda na kuwaokoa kutumia maneno. Hatimaye, Atatumia maneno kuutamatisha ulimwengu mzima wa zamani, hivyo kuukamilisha mpango Wake mzima wa usimamizi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno
Maneno yangu ndio ukweli usiobadilika milele. Mimi Ndiye mtoaji wa maisha kwa mwanadamu na mwongozo wa pekee kwa wanadamu. Thamani na maana ya maneno Yangu haibainishwi na kama yanakubaliwa au kutambuliwa na mwanadamu, ila ni kwa kiini cha maneno yenyewe. Hata kama hakuna mtu hata mmoja duniani anaweza kupokea maneno Yangu, thamani ya maneno Yangu na usaidizi wake kwa mwanadamu hayapimiki na mwanadamu yeyote. Kwa hivyo, Ninapokumbwa na wanadamu wengi wanaoasi, kukataa au kudharau kabisa maneno Yangu, msimamo Wangu ni huu tu: Acha wakati na ukweli uwe shahidi Wangu na uonyeshe kuwa maneno Yangu ndiyo ukweli, njia na uhai. Wacha vionyeshe kuwa yote Niliyosema ni sawa, na ni yale ambayo mwanadamu anapaswa kuwa nayo, na, zaidi ya hayo, yale ambayo mwanadamu anapaswa kukubali. Nitawajulisha wote wanaonifuata ukweli huu: Wale ambao hawawezi kuyakubali maneno Yangu kikamilifu, wale ambao hawawezi kutenda maneno Yangu, wale ambao hawawezi kupata kusudi katika maneno Yangu, na wale ambao hawawezi kupokea wokovu kwa sababu ya maneno Yangu, ni wale ambao wamehukumiwa na maneno Yangu na, zaidi ya hayo, wamepoteza wokovu Wangu, na fimbo Yangu haitaondoka kamwe miongoni mwao.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu
Haijalishi kama maneno yanayonenwa na Mungu ni ya juu juu au ya kina katika mwonekano wa nje, yote ni ukweli ambao ni wa lazima kwa mwanadamu anapoingia katika uzima; ni chemichemi ya maji ya uzima yanayomwezesha kuishi katika roho na mwili. Yanatosheleza kile ambacho mwanadamu anahitaji ili awe hai; ni kanuni na mfumo wa imani wa kuendesha maisha yake ya kila siku; ni njia, lengo, na mwelekeo ambao ni lazima aupitie ili kupokea wokovu; ni kila ukweli ambao anapaswa awe nao kama kiumbe aliyeumbwa mbele za Mungu; na kila ukweli kuhusu jinsi mwanadamu anavyomtii na kumwabudu Mungu. Ni dhamana ambayo inahakikisha kudumu kwa uwepo wa mwanadamu, ni mkate wa kila siku wa mwanadamu, na pia ni nguzo ya msaada inayowezesha mwanadamu kuwa na nguvu na kusimama. Zimejawa na uhalisi wa ukweli ambao kupitia kwazo mwanadamu aliyeumbwa anaishi ubinadamu wa kawaida, zimejawa na ukweli ambao mwanadamu anatumia kutoka kwenye upotovu na kuepuka mitego ya Shetani, zimejaa mafunzo maonyo, uhamasishaji na faraja isiyokwisha ambayo Muumba anampa binadamu aliyeumbwa. Ni ishara ambayo inawaongoza na kuwaelimisha wanadamu kuelewa yale yote yaliyo chanya, ni dhamana inayohakikisha kuwa wanadamu wataishi kwa kudhihirisha na kumiliki yale yote yaliyo ya haki na mema, kigezo ambacho watu, matukio, na vitu vyote vinapimwa, na pia alama ya usafiri inayowaongoza wanadamu kuuelekea wokovu na njia ya mwanga.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Dibaji
Katika “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima,” Mungu anaonyesha maneno Yake kutoka kwa mtazamo wa Roho. Namna ambavyo Anazungumza haiwezi kufikiwa na wanadamu walioumbwa. Aidha, msamiati na mtindo wa maneno Yake ni mzuri na wa kusisimua, na hakuna mtindo wowote wa maandishi ya binadamu ungechukua nafasi yake. Maneno ambayo Anatumia kumfichua mwanadamu ni sahihi, ni yasiokanushika na falsafa yoyote, nayo huwafanya watu wote kutii. Kama upanga wenye ncha kali, maneno Anayotumia kumhukumu mwanadamu hukata moja kwa moja hadi kwa kina cha nafsi za watu, hata kuwaacha bila mahali pa kujificha. Maneno Anayotumia kuwafariji watu yana huruma na wema wenye upendo, ni kunjufu kama kumbatio la mama mwenye upendo, na huwafanya watu wahisi salama kuliko walivyowahi hapo awali. Sifa moja kubwa zaidi ya matamshi haya ni kwamba, wakati wa hatua hii, Mungu hazungumzi kwa kutumia utambulisho wa Yehova au Yesu Kristo, wala wa Kristo wa siku za mwisho. Badala yake, kwa kutumia utambulisho Wake wa asili—Muumba—Anazungumza kwa na kuwafunza wote wanaomfuata Yeye na ambao bado hawajamfuata Yeye. Ni haki kusema kwamba hii ilikuwa mara ya kwanza tangu uumbaji kwa Mungu kuwahutubia wanadamu wote. Mungu hakuwa amewahi kuzungumza kwa wanadamu walioumbwa kiundani hivyo na kwa utaratibu sana. Bila shaka, hiyo pia ilikuwa mara ya kwanza Alipozungumza mengi hivyo, na kwa muda mrefu sana, kwa wanadamu wote. Ilikuwa ya kipekee kabisa. Na zaidi, matamshi haya yalikuwa maneno halisi ya kwanza yaliyoonyeshwa na Mungu miongoni mwa wanadamu ambapo Aliwafichua watu, akawaongoza, akawahukumu, na kuzungumza nao wazi wazi na kwa hiyo, pia, yalikuwa matamshi ya kwanza ambayo kwayo Mungu aliwaruhusu watu wajue nyayo Zake, mahali Anapokaa, tabia ya Mungu, kile Mungu anacho na alicho, mawazo ya Mungu, na sikitiko Lake kwa wanadamu. Inaweza kusemwa kwamba haya yalikuwa matamshi ya kwanza ambayo Mungu alikuwa amezungumza kwa wanadamu kutoka mbingu ya tatu tangu uumbaji, na mara ya kwanza ambapo Mungu alikuwa ametumia utambulisho Wake wa asili kuonekana na kuonyesha sauti Yake kwa wanadamu katikati ya maneno.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Utangulizi
Njia ya uzima si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kumiliki, wala si kitu ambacho kila mtu anaweza kufikia kwa urahisi. Hii ni kwa sababu uzima unaweza kutoka tu kwa Mungu, ambayo ni kusema, ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayemiliki kiini cha uzima, na ni Mungu Mwenyewe pekee aliye na njia ya uzima. Na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Tangu uumbaji wa dunia, Mungu amefanya kazi kubwa sana inayobeba pamoja nayo uzima uhai wa uzima, Amefanya kazi nyingi ambayo inamletea mwanadamu uzima, na Amelipa gharama kubwa inayomwezesha mwanadamu apate uzima. Hii ni kwa sababu Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ndiye njia ambayo kwayo mwanadamu anaweza kufufuliwa. Mungu kamwe hajawahi kosa kuwepo moyoni mwa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa wanadamu wakati wote. Yeye ndiye nguvu ya kuendesha maisha ya mwanadamu, chanzo cha kuendelea kuishi kwa mwanadamu, na rasilmali kubwa ya kuwepo kwa mwanadamu baada ya kuzaliwa. Yeye huwasababisha watu kuzaliwa upya, na kuwawezesha kuishi kwa ushupavu katika jukumu lao binafsi. Akitegemea uwezo Wake, na nguvu Yake ya uzima isiyozima, mwanadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, huku nguvu ya uzima wa Mungu imekuwa ikitoa utegemezi miongoni mwa binadamu, na Mungu amelipa gharama ambayo hakuna mtu wa kawaida amewahi kulipa. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; hata zaidi ya hayo, zinapita mamlaka yoyote. Uzima Wake ni wa milele, nguvu Zake ni za ajabu, na nguvu Zake za uzima haziwezi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za uzima wa Mungu zipo na hung’aa kwa mwangaza ulio mzuri sana, bila kujali muda au mahali. Mbingu na dunia zinaweza kupitia mabadiliko ya ajabu, lakini uzima wa Mungu ni ule ule daima. Mambo yote yanaweza kupita, lakini uzima wa Mungu bado utakuwepo. Hii ni kwa sababu Mungu ndiye chanzo cha kuwepo kwa vitu vyote, na mzizi unaotegemewa na kila kitu ili kiendelee kuishi. Asili ya maisha ya mwanadamu hutoka kwa Mungu, kuwepo kwa mbingu ni kwa sababu ya Mungu, na kuwepo kwa ardhi kunatokana na nguvu ya uhai wa Mungu. Hakuna kitu kinachomiliki nguvu kinachoweza kuzidi ukuu wa Mungu, na hakuna kitu chenye nguvu kinachoweza kuvunja mipaka ya mamlaka ya Mungu. Kwa njia hii, bila kujali wao ni nani, kila mtu lazima ajiwasilishe kwa utawala wa Mungu, kila mtu lazima aishi chini ya amri za Mungu, na hakuna mtu anayeweza kutoroka kutoka katika utawala Wake.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele
Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta njia ya kweli ya kudumu na ya milele. Ukweli huu ndiyo njia ambayo kwayo binadamu anapata uzima, na ndiyo njia pekee ambayo mwanadamu atamjua Mungu na kukubaliwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maneno, na minyororo ya historia kamwe hawataweza kupata uzima wala kupata njia ya kudumu ya uzima. Hii ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Ukitafuta tu kushikilia yaliyopita, ukisimama tu bila kusonga na kuweka mambo jinsi yalivyo, na usitafute kubadilisha hali iliyopo na kuitupilia mbali historia, hivyo hutakuwa ukimpinga Mungu kila wakati? Hatua za kazi ya Mungu ni zenye nguvu na kuu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—lakini wewe unakaa tu bila kufanya chochote ukisubiri maangamizo, ukikwamilia yale ya zamani na kusubiri vitu vikuangukie miguuni. Kwa njia hii, unaweza kuchukuliwaje kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Unaweza kuonyeshaje kwamba Mungu unayeshikilia ndiye Mungu ambaye ni mpya daima na kamwe si wa zamani? Na maneno ya vitabu vyako vilivyochuchuka yanawezaje kukubeba hadi katika enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi mwako ni maneno tu ambayo yanaweza tu kukupa furaha ya muda mfupi, wala sio ukweli unaoweza kukupa uzima. Maneno ya maandiko unayosoma yanaweza tu kuuimarisha ulimi wako; hayo siyo maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua uzima wa binadamu, sembuse hayo kuwa njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwenye ukamilifu. Je, tofauti hii haikupi sababu ya kutafakari? Je, haikupi umaizi ndani ya siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujipeleka mwenyewe mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Ninakusihi, basi, uache kuota na uangalie ni nani anayefanya kazi sasa—tazama uone ni nani sasa anayetekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu katika siku za mwisho. Kama huwezi, kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele