808 Petro Alimjua Mungu Vyema Zaidi

1 Petro alikuwa mwaminifu Kwangu kwa miaka mingi, lakini hakunung’unika wala kuwa na moyo wa kulalamika kamwe, na hata Ayubu hakuwa sawa na yeye. Katika enzi zote, watakatifu wote, pia, hawajamfikia hata kidogo. Yeye hakufuatilia kunijua Mimi tu, lakini pia alipata kunijua wakati ambapo Shetani alikuwa anatekeleza njama zake danganyifu. Hii ilisababisha miaka mingi ya huduma iliyoupendeza nafsi Yangu, na kwa sababu hii Shetani hakumnyonya kamwe.

2 Petro alitumia imani ya Ayubu, ilhali yeye pia alifahamu wazi upungufu wake. Ingawa Ayubu alikuwa na imani kubwa, alikosa ufahamu wa masuala katika ulimwengu wa kiroho, na hivyo alisema maneno mengi ambayo hayakulingana na hali halisi; hii inaonyesha kwamba ufahamu wake bado haukuwa wa kina, na haukuwa na uwezo wa kufanywa kuwa kamilifu. Na hivyo, Petro siku zote alitazamia kufahamu roho, na daima alilenga kuchunguza mienendo ya ulimwengu wa kiroho. Kwa sababu hii, hakuwa tu na uwezo wa kutambua matakwa Yangu kiasi, lakini pia alielewa kidogo juu ya njama danganyifu za Shetani, na hivyo ufahamu wake kuhusu Mimi ulikuwa mkubwa zaidi kuliko mwingine wowote katika enzi zote.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 8” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 807 Unapaswa Kumwiga Petro

Inayofuata: 809 Jinsi ya Kuitemba Njia ya Petro

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp