133 Lazima Tukutane Tena Siku Moja

1

Tunapokuwa pamoja na Mungu, tunacheka na kutabasamu na ni tamu sana.

Unanena na kufanya kazi ya kutunyunyizia na kutuchunga, na unatupa ukweli.

Maneno Yako yamechorwa mioyoni mwetu, tunashiriki mapenzi ya kina sana na Wewe.

Kazi Yako inakaribia tamati, na hivi karibuni Utatuacha.

Sijarudisha fadhila na upendo Wako.

Ee Mungu! Mwenyezi Mungu! Ee Mungu! Mwenyezi Mungu!

Uko karibu kuondoka, kwa hivyo ningekosaje kuhuzunika?

2

Nakumbuka madeni ya zamani, na moyo wangu unaumia kama uliokatwa kwa kisu.

Nimekuumiza sana kwa kuwa hobelahobela na mwasi, na nitajuta milele.

Unaniadibu na kunifundisha nidhamu tena na tena, ukiuamsha moyo wangu usiohisi.

Hukumu na kuadibu vinaondoa upotovu wangu na ninaishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu.

Sasa napata utakaso na wokovu Wako, moyo wangu unakua karibu na Wewe zaidi.

Ee Mungu! Mwenyezi Mungu! Ee Mungu! Mwenyezi Mungu!

Uko karibu kuondoka, na siwezi kusahau hisia hizi za zamani.

3

Unarudi Sayuni na tunatazamia kuwa na Wewe tena.

Ingawa tutakuwa mbali mbali sana, Wewe mbinguni na sisi duniani, lazima tukutane tena siku moja.

Maneno Yako yako pamoja nasi, tunatamani sana upendo Wako.

Tabia Yako ni takatifu na yenye haki, na inastahili sifa.

Lazima tushike maagizo Yako na kukushuhudia milele.

Ee Mungu! Mwenyezi Mungu! Ee Mungu! Mwenyezi Mungu!

Upendo Wako umechorwa mioyoni mwetu na tutakupenda milele.

Iliyotangulia: 132 Kuachana kwa Hisia

Inayofuata: 134 Naomba Niwe na Mungu Milele

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp