139 Ee Mungu, Wajua Jinsi Ninavyokutamani Sana?

1

Nakutamani Wewe moyoni mwangu, nangojea kurudi Kwako.

Bila kuuona uso Wako, moyo wangu umejaa wasiwasi.

Usiku mrefu, wenye giza sana, nitauona lini mwanga?

Nangojea kwa hamu kukuona tena siku moja karibuni.

Ee Mungu! Unajua nangojea kurudi Kwako.

Nakuomba Usiniache, siwezi kuwa bila Wewe!

2

Nikisikia sauti Yako, moyo wangu unafurahia.

Nahudhuria karamu na Wewe, nafurahia maneno Yako.

Naamua kwa kimya kutoa vyote nilivyo navyo.

Nayaeneza na kuyashuhudia maneno Yako niyaridhishe mapenzi Yako tu.

Ee Mungu! Mei Naomba Uungojee upendo wangu.

Natoa moyo na akili ili nikuridhishe, siwezi kuwa bila Wewe!

3

Nipitiapo hukumu Yako, kuna uchungu na huzuni.

Ingawa mwili ni dhaifu, sijakusahau.

Nauchukia mwili, na namchukia Shetani hata zaidi.

Nafurahia kukubali hukumu kujiweka huru kutoka kwa Shetani siku moja hivi karibuni.

Siwezi kukubali kufa bila kuridhisha tamanio la moyo Wako.

Nitakapoweza kuona tabasamu Lako, nitahisi kutosheka!

4

Maneno Yako kama rafiki hunipa imani na nguvu.

Sitakuwa hasi tena, nakupenda sana.

Nimepitia mateso mengi sana katika majaribu, upotovu wangu umetakaswa.

Haijalishi ni shida ngapi ninazokabili, nitakupenda na kukushuhudia.

Natarajia kuwa mtu mpya, kupata idhini Yako.

Kukupa Wewe upendo safi, kamwe kutokuwa mbali na Wewe!

Iliyotangulia: 138 Popote Uendapo Nitaambatana na Wewe

Inayofuata: 140 Ee Mungu, Nakukosa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp