448 Hali ya Kawaida Huleta Ukuaji wa Haraka Maishani

1 Katika kila hatua, hali za watu zinalingana moja kwa moja na kiwango ambacho wameingia na kiasi ambacho wamepata. Wakati hali za watu ni ya kawaida kwa ulinganisho, basi wanaweza kuelewa na kuingia katika ukweli fulani na kuelewa mambo fulani halisi ya kweli kulingana na maneno ya Mungu, na wanaweza kuwatolea na kuwatumikia wengine. Hali za watu wengine si sahihi, na hata ingawa wanawafuata wengine katika kutafuta, na pia wanasoma, kusikiliza, na kuwasiliana, wanaishia kupata kiasi kidogo zaidi kuliko watu wenye hali ya kawaida.

2 Ikiwa daima kutakuwa na uchafu wa kibinadamu, ufunuo wa hali potovu, na uchafuzi wa mawazo na fikira za watu, basi watu lazima wamefunikwa kabisa na ukosefu wa uwazi ndani yao. Je! Hili linakosaje kuathiri kuingia kwa mtu katika ukweli? Ni watu wenye akili timamu pekee ndio wanaoweza kuuelewa ukweli, ni watu wenye mioyo safi pekee ndio wanaoweza kumwona Mungu; ni kwa kuyaondoa mambo yaliyo ndani yako tu ndipo unaweza kuupata ukweli kwa urahisi. Wakati mioyo ya watu iko katika msukosuko, si rahisi kuuelewa ukweli. Ni watu ambao wanaelewa ukweli pekee ndio wanaoweza kuona ndani ya hali zao wenyewe kwa kiasi fulani, na ni kwa kuona ndani ya kiini cha matatizo yake tu ndipo mtu anaweza kuielewa asili yake wenyewe.

3 Ikiwa hali za watu ndani ni sahihi na za kawaida kabisa, basi wana hali ya kweli; hawana uwezekano wa kuteleza au kulalamika wakati mambo yanapowajia. Namna unavyotafuta katika kila hatua na hali ambayo unatafuta ni mambo ambayo huwezi kutojali. Kutojali hatimaye kutaleta shida. Wakati hali yako ni ya kawaida, utatembea katika njia sahihi na kufanya mambo kwa usahihi na utaingia kwa haraka katika maneno ya Mungu. Ni kwa kutafuta maisha kwa njia hii tu ndipo unaweza kukua.

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kuutumia Ukweli Kumaliza Hali Yako Hasi” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 447 Hali ya Kawaida ni Nini?

Inayofuata: 449 Udhihirisho wa Kazi ya Roho Mtakatifu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp