19. Situmii Ubora Duni wa Tabia Kama Kisingizio Tena

Na Lin Ran, Mkoa wa Henan

Hapo zamani, kila wakati nilipokabiliwa na shida fulani wakati wa kutekeleza wajibu wangu, au nilifanya kazi yangu vibaya, nilidhani ilikuwa ni kwa sababu ubora wa tabia yangu ulikuwa duni sana. Kama matokeo, mimi mara nyingi niliishi katika hali hasi ya kukaa tu. Mara nyingi ningetumia ubora duni wa tabia yangu kama kisingizio cha kuwaachia watu wengine wajibu niliohisi kuwa mgumu, na nilihisi kuwa hakukuwa na chochote kibaya na hili, kwamba nilikuwa nikifikiria kuhusu kazi ya kanisa nilipowauliza watu wengine wafanye kitu fulani kwa sababu ubora wa tabia yangu ulikuwa duni, na singeweza kukifanya vizuri. Ilikuwa tu kwa sababu ya kusoma maneno ya Mungu ndiyo niliugeuza mtazamo huu mbaya, nikigundua kuwa nilikuwa nikiyatazama mambo kupitia dhana na mawazo yangu mwenyewe. Pia nilijifunza jambo kuhusu tabia yangu mwenyewe potovu.

Siku moja, kiongozi alituma hati ambayo ilihitaji kushughulikiwa kwa haraka. Dada niliyeshirikishwa naye alikuwa akishughulikia kitu kingine, kwa hivyo aliniomba niishughulikie. Nilianza kutoa visingizio haraka: “Ubora wa tabia yangu ni duni sana. Mimi siko bora katika kuandika na kuhariri maandishi. Ingekuwa bora kama ungeishughulikia.” Hivyo, nilikuwa nikisukuma moja kwa moja chochote kigumu kwa mwenzangu. Baadaye, aliniambia, “Tangu tulipokutana, umekuwa ukisema ubora wa tabia yako ni mbaya. Lakini baada ya kuwa na wewe kwa siku chache nimegundua kuwa una uwezo wa kupata matatizo katika kazi. Sidhani kuwa ubora wa tabia yako ni mbaya, lakini kila unapokabiliwa na ugumu wowote katika kutekeleza wajibu wako, kila wakati unasema ubora wa tabia yako ni duni, na wakati mwingine hata unausukuma wajibu wako kwa mtu mwingine. Sijui nia yako ya kuendelea kuzungumza kila wakati juu ya jinsi ubora wako wa tabia ni duni ni ipi—inanionekania kana kwamba unabuni haya tu!” Nilipomsikia akisema haya, sikuwa na la kusema, lakini moyo wangu ulijawa na chuki: “Ninaposema ubora wa tabia yangu ni mbaya, nasema ukweli. Hujui ukweli, na umenielewa visivyo.” Baada ya hapo, nilitafakari kuhusu kwa nini dada huyo alisema hivyo. Sikuwa nasema uongo niliposema kuwa ubora wa tabia yangu ulikuwa duni—angewezaje kusema kuwa nilikuwa na nia? Moyoni mwangu, sikuweza tu kuelewa jambo hilo.

Wakati mmoja, katika mkutano na wafanyikazi wenzangu, niliwaambia ndugu zangu wengine kuhusu mkanganyiko niliokuwa nao. Nilipitia sababu za kwa nini nilidhani ubora wa tabia yangu ulikuwa duni, moja baada ya nyingine: Kwa mfano, nilipiga chapa polepole sana, mtindo wangu wa uandishi haukuwa mzuri sana. Nilipokuwa nikifanya kazi ya maandishi na mwenzangu, alifanya uchapaji na uhariri zaidi, na aliposoma hati, alipata matatizo kwa haraka sana, ilhali mimi nilikuwa nafanya pole pole, na kadhalika. Baada ya kunisikia nikishiriki, kiongozi wetu Ndugu Liu alisema, “Dada, ni kulingana na vitu hivi ndiyo tunapima ikiwa ubora wa tabia wa mtu ni mzuri au mbaya? Je, hili linaambatana na ukweli? Je, linaambatana na mapenzi ya Mungu? Sote tunajua kuwa watu ulimwenguni wanathamini kipaji na ubongo sana. Woote walio wepesi wa akili haraka, wanaojieleza kwa wazi zaidi, na wanaoeweza kushughulikia mambo ya ulimwengu wa nje kwa ustadi ni watu wenye ubora mzuri wa tabia, ilhali wale ambao ni holela katika maongezi, wasiojua na wasio na elimu nzuri wanaonekana kama wasio na ubora wowote wa tabia; hivyo ndivyo wasioamini wanavyoliona. Sisi tunaomwamini Mungu tunapaswa kuangalia mambo kulingana na maneno ya Mungu. Je, tumetafuta mapenzi ya Mungu katika jambo hili? Je, ni kwa msingi upi ambao Mungu hupima ikiwa ubora wa tabia wa watu ni mzuri au mbaya? Na ubora mzuri na mbaya wa tabia ni upi hasa?” Nilikuwa nikitikisa kichwa changu, na Ndugu Liu aliendelea kushiriki: “Hebu tusome kifungu cha mahubiri: 'Ikiwa ubora wa tabia wa mtu fulani ni mzuri au mbaya inahusu hasa jinsi anavyoweza kuelewa vizuri maneno ya Mungu. Kama uwezo wake wa kuelewa ni mzuri, hii inamaanisha kwamba anaposoma maneno ya Mungu, anaweza kubaini maana halisi na kufahamu mapenzi ya Mungu, anaweza kupata ukweli kupitia maneno ya Mungu, na kujua jinsi ya kutenda ili kuhakikisha kuwa anayapendeza mapenzi ya Mungu. Kuwa na uwezo kama huu wa kuelewa kunamaanisha kuwa yeye ni mwenye ubora mzuri wa tabia. Ubora wa tabia sio sawa na kuwa na vipaji, sio sawa na kuwa mwepesi wa akili na mwenye uwezo. Watu wengine huonekana kuwa werevu sana kwa nje lakini wasio stadi kabisa linapokuja suala la kuelewa maneno ya Mungu. Hivyo ndivyo wasioamini wanavyomaanisha wanapozungumza juu ya ubora mzuri wa tabia, lakini maneno kama haya hayana maana katika nyumba ya Mungu. Watu wengine ni wanafunzi wa vyuo vikuu au ni werevu sana, lakini katika nyumba ya Mungu wako taabuni wasiweze kujisaidia, na hawawezi kabisa kuingia katika ukweli. Je, unaweza kusema kuwa ni wenye ubora mzuri wa tabia? Kuna watu wengine wenye masomo duni ambao wamehitimu tu shule ya msingi na hawana kazi muhimu katika ulimwengu wa nje, lakini wamefanikiwa katika kufuatilia ukweli na kuwa wale wanaosifiwa na Mungu. Ni hawa tu ndio watu wenye ubora mzuri wa tabia. Kiwango cha elimu si cha mwanzo na mwisho. Cha muhimu ni ikiwa watu wanaelewa roho’ (Ushirika kutoka kwa Aliye Juu). Kutoka katika ushirika huu tunaona kwamba ikiwa ubora wa tabia ya mtu ni mzuri au mbaya inategemea uwezo wake wa kuelewa maneno ya Mungu. Hiki sicho kile wasioamini wanamaanisha wanaposema mtu ana ubora mzuri wa tabia au ana kipaji na mwerevu. Watu walio na ubora mzuri wa tabia wanaweza kuelewa mapenzi ya Mungu wanapomaliza kusoma maneno Yake, wanaweza kupata njia ya kutenda na kuingia katika ukweli, na wanaweza kutenda kulingana na kile ambacho Mungu anataka. Kwa upande mwingine, kuna wale ambao wanaonekana kuwa watu werevu sana na ni wastadi katika kushughulikia mambo ya ulimwengu wa nje—lakini wanachanganyikiwa mara tu wanapokabiliwa na ukweli wa maneno ya Mungu. Watu kama hao hawawezi kusemwa kuwa wenye ubora mzuri wa tabia. Ni kama tu jinsi watu wengine wenye maarifa, walioelimika wanaonekana kuwa na vipaji na wenye busara kwa nje, lakini hawawezi kuelewa ukweli wa maneno ya Mungu. Wengine wao hata wana mtazamo wa kipuuzi kuhusu mambo. Na kwa hivyo, kuwa mwenye elimu ya juu, mwepesi wa akili, na mwenye uwezo hakuwakilishi ubora mzuri wa tabia, na wala hivi sivyo viwango ambavyo hutumiwa kupima ubora wa tabia wa mtu. Cha muhimu ni ikiwa watu wanaelewa roho, ikiwa wana uwezo wa kuelewa ukweli. Hatuwezi kutegemea dhana na mawazo yetu wenyewe kupima ikiwa ubora wa tabia ya mtu ni mzuri au mbaya!” Baada ya kusikia haya, ghafla nilielewa: Ilitukia kwamba imani zangu zilikuwa tu dhana na mawazo—hazikulingana na ukweli.

Kisha, dada mmoja alipata vifungu viwili vya maneno ya Mungu na akaniomba nivisome. Maneno ya Mungu yanasema: “Wakati mtu anachukulia mambo kwa uzito, anawajibika, ni mwenye kujitolea, na anayefanya kazi kwa bidii, kazi itafanywa vizuri. ... Ushirikiano wa watu ni muhimu sana, mioyo yao ni muhimu sana, na mahali wanapoelekeza mawazo na maoni yao ni muhimu sana. Kuhusu makusudi yao ni yapi na ni kiasi kipi cha juhudi wanaweka katika kutekeleza wajibu wao, Mungu huchunguza na anaweza kuona. Ni muhimu kwamba watu waweke mioyo na nguvu zao zote katika kile wanachofanya. Ushirikiano wao ni muhimu pia. Kujitahidi kutokuwa na majuto juu ya wajibu ambao mtu amekamilisha na juu ya vitendo vya zamani vya mtu, na kufika mahali ambapo mtu hana deni la Mungu—hii ndiyo maana ya kutoa moyo na nguvu zote za mtu” (“Jinsi ya Kusuluhisha Shida ya Kuwa Mvivu na Mzembe Wakati wa Kutekeleza Wajibu Wako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Ikiwa una mtazamo sahihi wa kuukabili ukweli, una mtazamo wa kuukubali ukweli, na uchukue mtazamo wa unyenyekevu, basi hata ikiwa wewe ni mwenye ubora duni wa tabia, Mungu bado atakupa nuru na kukuruhusu upate kitu. Ikiwa wewe ni mwenye ubora mzuri wa tabia lakini daima ni mwenye kiburi, ukifikiria kila wakati kuwa wewe uko sahihi na daima kutokuwa radhi kukubali chochote ambacho wengine wanasema, na unapinga kila wakati, basi Mungu hatafanya kazi ndani yako. Mungu atasema kwamba tabia yako ni mbaya na hustahili kupokea chochote, na hata Mungu atakupokonya kile ulichokuwa nacho. Huku ndiko kunakojulikana kama kufunuliwa” (“Mtu Akitenda Ukweli Tu Ndipo Anaweza Kuwa na Ubinadamu Wa Kawaida” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Dada huyo alisema, “Maneno ya Mungu yanaonyesha kwamba mtazamo wetu wakati tunatekeleza wajibu wetu ni muhimu sana—ni muhimu sana. Kama tuna fikira zinazofaa, kama tunaweza kuitoa mioyo na nguvu zetu zote katika kutekeleza wajibu wetu, Mungu ataona, na atatutendea kulingana na mtazamo wetu kwa wajibu wetu. Hata kama sisi ni wenye ubora duni wa tabia, Mungu bado atatupa nuru na kutuongoza. Kama hatuna fikira sahihi, ikiwa hatuko tayari kulipa gharama na kushirikiana na Mungu, basi hatutakosa tu kutekeleza wajibu wetu vizuri, lakini pia tutakataliwa na Mungu. Tukiwaangalia ndugu walio karibu nasi kupitia katika maneno ya Mungu, tunaona kwamba wengine ni wenye ubora wa kawaida wa tabia lakini wana nia sahihi katika kutekeleza wajibu wao; wanapokabiliwa na ugumu, wanawajibika wenyewe kutafuta ukweli, na kulenga kuingia katika kanuni, na wanazidi kufanikiwa katika kutekeleza wajibu wao. Ilhali kuna ndugu wengine wanaoonekana kwetu kuwa hasa wenye ubora mzuri wa tabia, na walio na ufahamu safi wa maneno ya Mungu, lakini kwa sababu ni wenye majivuno, walioridhika, hawasikilizi ushauri wa watu wengine, na hujichukulia utukufu wa Mungu kila wanapokuwa na mafanikio kidogo katika kutekeleza wajibu wao, hatimaye wanaipoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Wengine hata huivuruga kazi ya kanisa na hunyang'anywa ustahilifu wao wa kutekeleza wajibu wao; katika hali nzito, wao hata hufukuzwa kutoka kanisani. Ukweli huu hutuonyesha kwamba kama ubora wa tabia ya mtu ni mzuri au mbaya hauamui ikiwa atasifiwa na Mungu; kilicho muhimu ni ikiwa anafuatilia ukweli au la.” Kisha, ndugu walitumia uzoefu wao wenyewe kuzungumza kuhusu hatari na matokeo ya kujielezea kulingana na dhana na mawazo yao wenyewe. Hapo tu ndipo niligundua jinsi kutoelewa ukweli kulivyokuwa kujinga; sikuwa nimetafuta ukweli, na badala yake nilikuwa nimejieleza kuwa mwenye ubora duni wa tabia kwa kuishi katika dhana na fikira zangu, kiasi kwamba mara nyingi niliwasukumia watu wengine wajibu mgumu. Sikujaribu kujiboresha, wala sikumtegemea Mungu au kwa kweli kulipa gharama ya kuvunja vizuizi hivi, jambo ambalo hata lilinifanya nisiweze kutekeleza wajibu niliokuwa na uwezo wa kutekeleza. Sikuweza tu kupata mafunzo halisi, au kukua katika ukweli na maisha, lakini hili liliathiri moja kwa moja ufanisi wangu katika kutekeleza wajibu wangu. Nilifikiria juu ya jinsi yule dada niliyefanya naye kazi alivyoweza kupata matatizo kwa haraka. Ingawa hili lilihusika na tabia yake ya asili, la muhimu zaidi lilikuwa kwamba, kwa sababu ya mtazamo wake wa kuwa makini na kuwajibika katika wajibu wake, aliweza kumtegemea Mungu na kupambana na matatizo moja kwa moja alipokumbana nayo. Ni hapo tu ndipo alipopata nuru na mwangaza na Roho Mtakatifu. Mimi, kwa upande mwingine, nilijaribu kukwepa matatizo nilipokumbana nayo, na nikatumia ubora duni wa tabia kama kisingizio cha kujiondoa kwenye wajibu. Sikumtegemea Mungu na kuwajibika mwenyewe kujaribu kutatua tatizo kwa kutafuta ukweli unaofaa, ambayo ilimaanisha sikuweza kuipata kazi ya Roho Mtakatifu. Kutokana na hili, niliona kuwa Mungu yuko na usawa na ni mwenye haki kwa wote. Kupitia kwa ushirika, niligundua pia kuwa Mungu anataka kutoka kwetu kulingana na kile tunachoweza. Sio suala la Yeye kumsukuma mtu afanye jambo asiloweza. Napaswa kujitendea haki mimi mwenyewe; badala ya kuzingatia ubora wa tabia yangu, napaswa kulenga tu kuweka nguvu zangu zote katika kutekeleza wajibu wangu. Napaswa kutafuta na kutafakari kanuni za ukweli, nijifunze kutokana na uwezo wa wengine, nisikilize ushauri wa watu wengine, na kuushirikisha katika kile nilichotenda kwa kweli—na baada ya muda, ningekuwa na uhakika wa kufaidika na kukua.

Baadaye, ukosoaji wa dada huyo ulisikika masikioni mwangu: “Sijui na yako ya kuendelea kila wakati kuzungumza juu ya jinsi ubora wako wa tabia ni duni ni ipi.” Alikuwa sahihi—kila wakati nilikuwa mwepesi wa kusema kuwa ubora wa tabia yangu ni mbaya. Je, ni nia na tabia gani potovu ambazo zilikuwa zikinidhibiti kwa siri?

Siku moja, nilisoma maneno haya kutoka katika ushirika: “Wale ambao huwaambia wengine kila wakati kuwa ni wapotovu, kwamba ni wapumbavu na wajinga, kwamba ni wasio hisia na wasio na akili, wenye ubora duni wa tabia—hawazungumzi kuhusu nia halisi na udanganyifu ulio ndani ya mioyo yao; wao huficha nia hizi mbaya, na kutumia upotovu na ujinga na upumbavu wao wenyewe kama kinga, ngao. Hakuna mtu aliye mjanja kuwaliko watu kama hao, hakuna aliye bora katika kujisingizia, kujifanya ili kuwafanya watu wafikirie kuwa wao ni wazuri, kwamba wanajijua wenyewe, kwamba ni wanyenyekevu, kwamba hawana hila na wako wazi. Haya ni maonyesho kwa wengine; kwa kweli, watu kama hao ni wanafiki wadanganyifu na wajanja ...” (Ushirika kutoka kwa Aliye Juu). Ni wakati tu niliposoma ushirika huu ndipo niligundua kuwa kusema kwangu kila wakati kuhusu ubora wangu duni wa tabia kwa kweli kulielekezwa na asili yangu ya udanganyifu, na kwamba nia mbaya zilikuwa zimefichwa ndani yangu. Kwa mfano, ninapokabiliwa na wajibu ambao sikuwa nimewahi kufanya hapo awali, jambo la kwanza kufanya lingekuwa kuwaambia wale ndugu wengine kuwa ubora watabia yangu ni duni, kwa sababu nilihofu kuwa wangenidharau kama ningeufanya wajibu huo vibaya. Nilifanya hivyo kwa sababu ya heshima na hadhi yangu mwenyewe. Nilifanya hivi ili isiwe kosa langu ikiwa nitaufanya vibaya; sio kwamba sijaweka nguvu zangu zote ndani ya wajibu huo, lakini ni kwamba umezidi ubora wangu wa tabia. Kila nilipokumbana na ugumu wowote katika kutekeleza wajibu wangu, sikuwa tayari kuteseka na kulipa gharama ya kuukabili ana kwa ana. Niliogopa uwajibikaji, pia. Kwa hivyo nilitumia tu ubora duni wa tabia yangu kama kisingizio cha kuusukuma wajibu wangu kwa mtu mwingine, kumfanya afikirie kwamba nilikuwa mwenye busara na ninajitambua. Karibu kila wakati nilipopitia matatizo na nililazimika kulipa gharama au kulazimika kuwajibikiajambo fulani, nilikuwa nikirudi nyuma. Kwa kweli, nilikuwa nikiishi kulingana na falsafa ya uhusiano wa binadamu ya kishetani ya “kaa kimya kwa ajili ya kujilinda na utafute tu kuitoroka lawama.” Lilionekana kama jambo la busara sana—kutumia njia zangu mwenyewe za ujanja kuzuia uwajibikaji—lakini kwa kweli nilikuwa nimekosa fursa nyingi za kutafuta na kuelewa ukweli. Kwa kweli, ubora wa tabia ambao Mungu humpa kila mmoja wetu unafaa kwa kusudi; lakini sikuwa nimeuweka moyo na nguvu zangu zote katika kushirikiana na Mungu kwa msingi wa kile nilichoweza kufanikisha, ili niipate kazi ya Roho Mtakatifu na kuboresha ubora wa tabia yangu; badala yake, kila wakati nilitumia ubora wangu duni wa tabia kama kisingizio cha kutotenda ukweli, ili kujaribu kumhadaa na kumdanganya Mungu. Je, huu sio ujanja, uwovu sana? Na ningewezaje kuongozwa na Mungu hivyo?

Maneno ya Mungu yanasema, “Nawathamini sana wale wasio na shaka kuhusu wengine na pia nawapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Pangu wao ni waaminifu” (“Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Katika mstari unaofuata, ‘Ingawa ubora wangu wa tabia ni duni, nina moyo mwaminifu.’ Watu wengi wanaposikia mstari huu, wanahisi vizuri, sivyo? Jambo hili linahusisha mahitaji ya Mungu kwa watu. Mahitaji yapi? Ikiwa watu wamepungukiwa katika ubora wa tabia, sio mwisho wa dunia, lakini lazima wawe na moyo mwaminifu na, kwa hivyo, wataweza kupokea sifa za Mungu. Haijalishi hali yako ni ipi, lazima uwe mtu mwaminifu, uzungumze kwa uaminifu, utende kwa uaminifu, uweze kutekeleza wajibu wako kwa moyo na akili yako yote, na uwe mwaminifu, na lazima usiikwepe kazi yako, usiwe mjanja au mdanganyifu, usiwe mjanja, usijaribu kuwalaghai wengine, au kuzungumza bila uwazi; lazima uwe mtu anayependa ukweli na anayefuatilia ukweli. … Unasema, ‘Ubora wangu wa tabia uko chini, lakini moyoni mimi ni mwaminifu.’ Wakati wajibu unakuangukia, hata hivyo, unaogopa kuteseka au kuwa unaweza kuwa usipoutimiza vizuri, utalazimika kuuwajibikia, kwa hivyo unatoa visingizio kuukwepa. Je, haya ni maonyesho ya mtu mwaminifu? Ni wazi kuwa siyo. Hivyo basi, mtu mwaminifu anapaswa kutendaje? Anapaswa kukubali na kutii, na kisha kujitolea kabisa katika kutekeleza wajibu wake kadiri ya uwezo wake, akijitahidi kuridhisha mapenzi ya Mungu. Hili linaonyeshwa kwanjia kadhaa. Njia moja ni kwamba unapaswa kukubali wajibu wako kwa uaminifu, kutofikiria kuhusu kitu kingine chochote, na usiwe shingo upande kulihusu. Usipangie kufaidika kwako mwenyewe, Haya ni maonyesho ya uaminifu. Njia nyingine ni kuweka nguvu zako na moyo wako wote katika hilo. Unasema, ‘Hiki ndicho kila kitu ninachoweza kufanya; nitaanza kukifanya chote, na kukikitoa kwa Mungu kabisa.’ Je, si haya ni maonyesho ya uaminifu? Unatoa kila kitu ulicho nacho na kila unachoweza kufanya—haya ni maonyesho ya uaminifu” (“Ni kwa Kuwa Mtu Mwaminifu tu Ndiyo Mtu Anaweza Kuwa na Furaha Kweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinipa njia ya kutenda: Mungu hajali ikiwa ubora wa tabia ya watu ni mzuri au mbaya; kilicho muhimu ni ikiwa wana moyo ambao ni mwaminifu, ikiwa wanaweza kukubali ukweli, na kuuweka katika vitendo. Ingawa ubora wa tabia yangu ni duni, na mimi ni mpole kidogo katika kuelewa ukweli, na wakati mwingine nafuata mafundisho, kama moyo wangu ni mwaminifu, na mimi hufuatilia ukweli kila wakati ili nitatue tabia yangu potovu wakati natimiza wajibu wangu, ikiwa nafanya yote niwezayo kutekeleza yale ambayo Mungu anahitaji, basi nitapokea mwongozo na baraka za Mungu, na hatua kwa hatua nitaweza kuelewa ukweli. Ninapoingia katika ukweli nitaweza kufidia upungufu wangu kuhusu ubora wangu duni wa tabia, na nitakua bora zaidi na zaidi katika kuelewa na kuona mambo. Baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, nilianza kumtegemea Mungu ili niwe bora zaidi nilipotimiza wajibu wangu. Sikuwa navitoa tena vitu ambavyo havikuwa wazi kwangu, ambavyo sikuelewa, kwa watu wengine, lakini nilijaribu sana kutafuta na kuvisuluhisha mwenyewe. Shukrani ziwe kwa Mungu! Nilipotenda kama anavyohitaji Mungu, mimi pia niliweza kuona matatizo katika maandishi—na ingawa kulikuwa na nyakati ambazo masuala kadhaa magumu yalisalia kuwa magumu kwangu, kwa kutafuta kanuni za ukweli pamoja na ndugu, polepole yalionekana wazi kwangu, na nilihisi mwepesi na huru zaidi nilipotekeleza wajibu wangu.

Kwa sababu ya kupitia mazingira niliyowekewa na Mungu, nilipata ufahamu fulani wa upotovu na upungufu wangu, na nikajua jinsi ya kukabiliana na maswala yanayohusiana na ubora wa tabia yangu. Nilipokuwa nikitekeleza wajibu wangu hapo zamani, sikuzingatia kutafuta ukweli, wala sikujaribu kushughulikia tabia yangu potovu. Siku zote niliona mambo kupitia dhana na mawazo yangu mwenyewe, ambayo yalinisababisha kujieleza kinaganaga mara nyingi, na kujaribu kujiondoa katika vitu kwa kusema ubora wa tabia yangu ulikuwa duni. Utendaji wangu wa wajibu ulikuwa umejaa uzembe, niliichelewesha kazi ya kanisa, na nikapata hasara katika maisha yangu mwenyewe. Sasa naelewa kuwa ubora wa tabia wa kila mtu umeshapangiwa kabla na Mungu na ni sehemu ya malengo matukufu ya Mungu. Sipaswi kuwekewa mipaka na ikiwa ubora wa tabia yangu ni mzuri au mbaya. Katika siku zijazo, nitajaribu kutafuta ukweli katika kila jambo, kutenda kwa maadili, na kuwa mtu mwaminifu ili nimridhishe Mungu.

Iliyotangulia: 18. Baada ya Uwongo

Inayofuata: 20. Kwa Nini Nimetembea Njia ya Mafarisayo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

13. Ukombozi wa Moyo

Mwenyezi Mungu anasema, “Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu; kufunuliwa kwa...

20. Kwa Nini Nimetembea Njia ya Mafarisayo

Petro alikamilishwa kwa sababu alimpenda Mungu kweli na kwa sababu alikuwa na hiari na uvumilivu wa kutafuta ukweli. Ingawa niko mbali na hilo, sitaishi kwa namna ya kuchukiza na isiyovutia tena ili kujihifadhi; niko tayari kufanya kumpenda Mungu kuwa lengo langu katika kutafuta na nitatumia juhudi zote na kulipa gharama katika kutimiza wajibu wangu. Kweli nitaubeba mzigo wa majukumu yangu na kutia ukweli katika vitendo wakati ninatimiza wajibu na kuingia katika uhalisi wa kumpenda Mungu.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki