316 Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme

Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake.

Tunahudhuria dhifa, tunakula na kunywa maneno Yake.

Sisi tunaaga huzuni, tunaishi maisha mapya.

Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunayafurahia ndani yake.

Kwa kushiriki ukweli, mioyo yetu inang’aa.

Tunayatafakari maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu anatupa nuru.

Kuujua ukweli na kuwekwa huru, mioyo yetu ni tamu kama asali. Chukizo lote limeondoka, tunaishi katika upendo wa Mungu.

Tunapendana, hakuna umbali kati yetu.

Tunauelewa moyo wa Mungu, uhasi umeisha.

Tukiishi ndani ya maneno Yake, tunaona uzuri Wake.

Kwa mwongozo wa Mungu tumechukua njia ya nuru.


Tunaimba sifa kwa Mungu,

tunacheza na kucheza.

Tunasifu maisha yetu mapya, katika ufalme,

wenye furaha katika ufalme wa Mungu.

Mungu ametuokoa kikamilifu,

tumekuwa watu Wake.

Kuinuliwa mbele ya kiti Chake cha enzi ni furaha isiyo na kifani.


Maneno ya Mungu ni yenye thamani na yote ni ukweli kabisa.

Hukumu yake inafichua upotovu wetu.

Sisi ni wenye kiburi, maneno ya Mungu hutupogoa, tumekuja kujijua wenyewe.

Tunapojitafakaria, tuna toba ya kweli.

Kupitia hukumu na kuadibu tunatakaswa.

Tunatupa upotovu wetu, tunakuwa wanadamu wapya,

tukifanya wajibu wetu vizuri na kulipa upendo wa Mungu.

Kila mmoja wetu anafanya sehemu yake, tunajitolea kwa Mungu,

tukisimama imara katika ushuhuda kutimiza mapenzi ya Mungu.

Kila mmoja anatoa mwanga, tukiwa na ushuhuda kwa Mungu.

Upendo safi na aminifu kwa Mungu ni wenye furaha na mtamu.


Tunaimba kwa sauti sifa zetu kwa Mungu,

tunacheza na kucheza.

Tunasifu maisha yetu mapya katika ufalme,

mioyo yetu kweli ni ya furaha.

Ni Mungu aliyetuokoa,

tumekuwa watu wa Mungu.

Kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu

ni furaha isiyo na kifani.


Sisi huunga mioyo na mikono kushuhudia kwa Mungu,

tukieneza injili ya ufalme, tusiogope kamwe ugumu.

Katika majaribu na mateso, tunamtegemea na kumwomba Mungu.

Njia ni yenye mabonde, lakini Mungu hufungua njia.

Tunapojua ukweli wa maneno ya Mungu, mioyo yetu hupata nguvu.

Yanatuhimiza kuzidi kwenda mbele milele.

Tunamshuhudia na kumpa Yeye kila kitu chetu.

Haijalishi mateso ni yapi, tuko tayari sana.

Kwa mwongozo wa maneno ya Mungu, tunamshinda Shetani.

Tunapompenda Mungu kweli, hatuna majuto kabisa.

Tutaliacja kabisa joka kuu jekundu na kuwa askari washindi.

Tutashuhudia daima katika njia yetu ya upendo kwa Mungu.


Tunaimba kwa sauti sifa zetu kwa Mungu,

tunacheza na kucheza.

Tunasifu maisha yetu mapya katika ufalme,

mioyo yetu kweli ni ya furaha.

Ni Mungu aliyetuokoa,

tumekuwa watu wa Mungu.

Kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu

ni furaha isiyo na kifani.

Iliyotangulia: 315 Njia Za Mungu Haziwezi Kueleweka

Inayofuata: 317 Imba na Kucheza katika Sifa kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki