54 Matamanio ya Moyo Wangu

1

Maisha ya binadamu yasiyo na mipaka,

yaliyojaa upepo, mvua, na mabadiliko.

Miaka iliyotolewa, migumu na yenye ukiwa.

Mawingu ya rangi nyeusi yanashuka chini, yakifanya shimo la giza.

Mfalme wa mapepo anatawala, mwenye ukatili na wa unyama.

Anatawala kama dikteta, anayafunga mawazo.

Anapojaribiwa naye, mwanadamu anapoteza mwelekeo wake.

Akifukuza umaarufu na faida, anapigwa kutoka kichwa hadi mguu.

Akiwa ameumizwa sana, amevuliwa mfano wote wa binadamu.

Aiwa amechoka katika mwili na moyo, amejaa majeraha,

bila nguvu za kupigana, tayari amevunjika moyo.

Hakuna mahali pa kugeuka, katika maumivu na kuchanganyikiwa.

Anataka kupata nchi safi.

Akitafuta kwa bidii, anazurura duniani.

Akifikiri mchana na usiku, moyo umejaa huzuni. Nikiomba kwa haraka,

moyo wangu unatamani. Hatimaye ninakaribisha kurudi kwa Bwana.

2

Kwa kishindo, ngurumo saba zinatoa sauti.

Kristo wa siku za mwisho anashuka duniani.

Nimesikia maneno ya Mungu, nimekuja mbele Zake.

Nafurahia maneno Yake, najua ukweli.

Maneno Yake hunilisha, huniruzuku, huninyunyizia.

Mimi mwenyewe nimehisi upendo wa kweli wa Mungu.

Kupitia majaribu, maumivu na usafishaji,

maisha yanaboreshwa na ukuaji wa kila wakati.

Nikihukumiwa, nauacha upotovu,

na kupata utakaso, wokovu.

Hakutakuwa na machozi, dhiki tena.

Nainama mbele za Mungu, naufunua moyo wangu.

Mungu alinichagua kwa sababu ya upendo Wake;

nashukuru kwa ajili ya wokovu Wake.

Nimelikimbia giza, naishi mbele Zake,

nampa Mungu moyo wangu, nalipiza upendo Wake.

Iliyotangulia: 53 Kumrudia Mungu ni Furaha ya Kweli

Inayofuata: 55 Tuna Bahati Kukutana na Kuja kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp