944 Mungu Aendeleza Kuwepo kwa Mwanadamu kwa Tabia Yake ya Haki
1 Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake kali, nguvu za giza zinakaguliwa, mambo ya giza yanaangamizwa, huku mambo ya haki na mazuri yakifurahia utunzaji wa Mungu, ulinzi, na yote yanaruhusiwa kuendelea. Mungu hushusha hasira Yake kwa sababu ya mambo dhalimu, mabaya na ya giza, yanayozuia, yanayotatiza au kuangamiza shughuli na maendeleo ya kawaida ya mambo ya haki na mazuri. Shabaha ya ghadhabu ya Mungu si kusalimisha hadhi na utambulisho Wake binafsi, lakini kusalimisha uwepo wa mambo ya haki, mazuri, ya kupendeza na kuvutia, kusalimisha sheria na mpangilio wa kuwepo kwa kawaida kwa binadamu. Hiki ndicho chanzo asilia cha hasira ya Mungu. Hasira kali ya Mungu ni bora sana, ya kiasili na ufunuo wa kweli wa tabia Yake. Hakuna makusudi yoyote katika hasira Yake kali, wala hakuna udanganyifu au njama yoyote; au hata zaidi, hasira Yake kali haina tamanio lolote, ujanja, mambo ya kijicho, udhalimu, maovu, au kitu kingine ambacho binadamu wote waliopotoka huwa navyo.
2 Kabla ya Mungu kushusha hasira Yake kali, huwa tayari Ametambua hali halisi ya kila suala kwa uwazi na ukamilifu zaidi, na huwa tayari Amepangilia ufafanuzi na hitimisho sahihi na zilizo wazi. Hivyo basi, lengo la Mungu katika kila suala Analofanya ni wazi kabisa, vile ulivyo mtazamo Wake. Yeye si mtu aliyechanganyikiwa; Yeye si kipofu; Yeye si mtu wa kuamua ghafla; Yeye si mzembe; na zaidi, Yeye si mtu asiyefuata kanuni. Hii ndiyo dhana ya kimatendo ya hasira ya Mungu, na ni kwa sababu ya dhana hii ya kimatendo ya hasira ya Mungu ambapo binadamu umefikia uwepo wake wa kawaida. Bila ya hasira ya Mungu, binadamu ungeishia kuishi katika mazingira yasiyo ya kawaida; viumbe vyote vyenye haki, virembo na vizuri vingeangamizwa na kusita kuwepo. Bila ya hasira ya Mungu, sheria na amri za kuwepo kwa viumbe vingekiukwa au hata kupinduliwa kabisa.
3 Tangu uumbwaji wa binadamu, Mungu ametumia bila kusita, tabia Yake ya haki kusalimisha na kuendeleza uwepo wa kawaida wa binadamu. Kwa sababu tabia Yake ya haki inayo hasira na adhama, watu wote waovu, vitu, vifaa na vitu vyote vinavyotatiza na kuharibu uwepo wa kawaida wa binadamu vinaadhibiwa, vinadhibitiwa na kuangamizwa kwa sababu ya hasira Yake. Kwenye milenia mbalimbali zilizopita, Mungu ameendelea kutumia tabia Yake ya haki kuangusha na kuangamiza kila aina za roho chafu na za giza ambazo zinampinga Mungu na kuchukua nafasi ya wasaidizi na watumishi wa Shetani katika kazi ya Mungu ya kusimamia binadamu. Hivyo basi, kazi ya Mungu ya wokovu wa binadamu siku zote imeimarika kulingana na mpango Wake. Hivi ni kusema kwamba kwa sababu ya uwepo wa hasira ya Mungu, sababu za haki zaidi za binadamu hazijawahi kuangamizwa.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili