267 Hukumu ya Mungu Iliufanya Moyo Wangu Umpendao Mungu Uwe Safi Zaidi

1 Ee Mungu! Mwili wangu ni mkaidi, na unaniadibu na kunihukumu mimi. Nafurahi katika adabu Yako na hukumu, na hata kama Hunitaki mimi, katika hukumu Yako mimi ninaona tabia Yako takatifu na tabia Yako ya haki. Unaponihukumu, ili wengine wapate kuiona hali Yako ya haki katika hukumu Yako, ninaridhika.

2 Ninatamani tu kwamba tabia Yako ionekane ili, tabia Yako ya haki iweze kuonekana na viumbe wote, na kwamba niweze kukupenda kwa usafi zaidi kupitia hukumu Yako na nifikie mfanano wa yule mwenye haki. Hukumu hii Yako ni nzuri, kwa maana hivyo ndivyo mapenzi Yako ya neema yalivyo.

3 Najua kwamba bado kuna mengi ndani yangu yaliyo ya uasi, na kwamba mimi bado sifai kuja mbele Yako. Ningependa unihukumu hata zaidi, iwe ni kupitia mazingira ya uhasama au mateso makubwa; haijalishi ni nini Utakayofanya, kwangu ni ya thamani. Upendo Wako ni mkuu, na mimi niko tayari kujiweka katika huruma Yako bila malalamiko hata kidogo.

Iliyotangulia: 266 Upendo Wa Petro Kwa Mungu

Inayofuata: 268 Niko Tayari Kutii Kazi ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp