746 Matendo ya Haki ya Ayubu Yalimshinda Shetani

1 Wakati Ayubu alipopitia majaribio yake kwa mara ya kwanza, alinyang’anywa mali yake yote na watoto wake wote, lakini hakujisujudia na kusema chochote ambacho kilikuwa dhambi dhidi ya Mungu kutokana na hayo. Alikuwa ameshinda majaribio ya Shetani, na alikuwa ameshinda rasilimali zake zote za dunia na watoto wake, na majaribio ya kupoteza mali yake ya dunia, hivi ni kusema kwamba aliweza kutii Mungu kuchukua na kutwaa kutoka kwake na akatoa shukrani na sifa kwa Mungu kwa sababu ya hayo. Hivyo ndivyo ulivyokuwa mwenendo wa Ayubu wakati wa jaribio la kwanza la Shetani, na huo ndio uliokuwa ushuhuda wa Ayubu wakati wa jaribio la kwanza la Mungu. Kwenye jaribio la pili, Shetani aliunyosha mbele mkono wake ili kumdhuru Ayubu, na ingawaje Ayubu alipitia maumivu yaliyokuwa makubwa zaidi kuliko yale aliyokuwa amepitia awali, bado ushuhuda wake ulikuwa wa kutosha wa kuacha watu wakiwa wameshangazwa. Alitumia ujasiri wake, imani yake, na utiifu kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, kwa mara nyingine tena kumshinda Shetani, na mwenendo wake na ushuhuda wake viliweza kwa mara nyingine tena kuidhinishwa na kupata kibali cha Mungu.

2 Baada ya kupitia majaribio haya mawili, ndani ya Ayubu kulizaliwa uzoefu mwingi, na uzoefu huu ulimfanya yeye kuwa mwenye kimo na uzoefu zaidi, ilimfanya kuwa mwenye nguvu zaidi, na imani kubwa zaidi, na ilimfanya yeye kuwa na ujasiri zaidi kuhusu haki na ustahili wa uadilifu ambao yeye alishikilia kwa dhati. Majaribio ya Yehova Mungu kwa Ayubu yalimpa uelewa wa kina na hisia za wasiwasi wa Mungu kwa binadamu, na kumruhusu yeye kuhisi thamani ya upendo wa Mungu, ambapo vyote vinaelekezwa katika utiliaji maanani kwa na kuhusu upendo wa Mungu na vyote viliweza kuongezwa katika kumcha Mungu. Majaribio ya Yehova Mungu kumwondoa tu Ayubu kutoka Kwake, lakini pia yaliuleta moyo wake karibu na Mungu.

3 Wakati maumivu yale ya mwili yaliyovumiliwa na Ayubu yalifikia kilele, wasiwasi aliouhisi kutoka kwa Yehova Mungu haukumpa chaguo lolote ila kuilaani siku yake ya kuzaliwa. Mwenendo kama huo haukuwa umepangiliwa mapema lakini ulikuwa ni ufunuo wa kiasili wa kutilia maanani na kumpenda Mungu kutoka ndani ya moyo wake, ulikuwa ni ufunuo wa kiasili uliotoka kwenye kutilia maanani na kumpenda Mungu kwake. Hivi ni kusema, kwa sababu alijichukia, na hakuwa na radhi na hakuweza kuvumilia kuona Mungu Akiteswa, hivyo kutilia maanani na upendo wake vilifika hali ya kutojijali.

4 Vitendo vyake vya haki vilimruhusu yeye kumshinda Shetani na kuwa makini katika ushuhuda wake kwa Mungu. Hivyo, pia, matendo yake ya haki yalimfanya kuwa mtimilifu, na kuruhusu thamani ya maisha yake kuimarishwa, kuzidishwa zaidi kuliko awali, na kumfanya yeye kuwa mtu wa kwanza kutoweza kushambuliwa au kujaribiwa zaidi na Shetani. Kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alishtakiwa na kujaribiwa na Shetani; kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alikabidhiwa Shetani; na kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alishinda na kumlemea Shetani, na kuweza kusimama imara katika ushuhuda wake. Kuendelea mbele, Ayubu akawa binadamu wa kwanza ambaye hangewahi tena kukabidhiwa Shetani, kwa kweli alikuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na akaishi kwenye nuru, katika baraka za Mungu bila ya kupelelezwa au kuangamizwa na Shetani.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 745 Ushuhuda wa Ayubu Ulimshinda Shetani

Inayofuata: 747 Ayubu Aliwezaje Kumwogopa Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp