748 Imani na Utii wa Kweli wa Ayubu kwa Mungu

1 Wakati wa maisha yake katika miongo kadhaa iliyopita, Ayubu aliyaona matendo ya Yehova na kupata baraka za Yehova Mungu kwake yeye. Zilikuwa ni baraka zilizomwacha akihisi wasiwasi mkubwa na mwenye wingi wa shukrani, kwani aliamini kwamba alikuwa hajamfanyia chochote Mungu, ilhali alikuwa amepata baraka nyingi na akawa anafurahia neema nyingi. Kwa sababu hii, ndani ya moyo wake mara nyingi aliomba, akitumai angeweza kumlipa Mungu, akitumai kwamba angekuwa na fursa ya Kuwa na ushuhuda wa matendo na ukubwa wa Mungu, na kutumai kwamba Mungu angeweza kuujaribu utiifu wake, na, zaidi, kwamba imani yake ingetakaswa, mpaka pale ambapo utiifu wake na imani yake vyote vingepata idhini ya Mungu.

2 Na wakati Ayubu alipojaribiwa, alisadiki kwamba Mungu alikuwa amesikia maombi yake. Ayubu alifurahia sana fursa hii zaidi ya kitu kingine chochote, na hivyo basi hakuthubutu kuchukulia jambo hili vivi hivi, kwani tamanio kubwa zaidi la maisha yake lingetimia. Kufika kwa fursa hii kulimaanisha kwamba utiifu wake na kumcha Mungu vyote vingeweza kutiwa kwenye majaribu, na kutakaswa. Zaidi, ilimaanisha kwamba Ayubu alikuwa na fursa ya kupata idhini ya Mungu, hivyo kumleta karibu zaidi na Mungu.

3 Wakati wa jaribio, imani kama hiyo na kufuatilia huko kulimruhusu yeye kuwa mtimilifu zaidi, na kupata uelewa mkubwa zaidi wa mapenzi ya Mungu. Ayubu alikuwa mwenye shukrani zaidi kwa baraka na neema za Mungu, katika moyo wake alimwaga sifa kubwa zaidi kwa matendo ya Mungu, na alizidi kumcha Mungu na kumstahi, na kutamani hata zaidi upendo, ukubwa, na utakatifu wa Mungu. Wakati huu, ingawaje Ayubu alikuwa bado yuleyule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu kwenye macho ya Mungu, kuhusiana na yale aliyopitia, imani na maarifa ya Ayubu vyote vilikuwa vimeimarika pakubwa.

4 Imani yake ilikuwa imeongezeka, utiifu wake ulikuwa umeimarika pakubwa, na hali yake ya kumcha Mungu ilikuwa ya kina zaidi. Ingawaje jaribio hili lilibadilisha roho na maisha ya Ayubu, mabadiliko kama hayo hayakumtosheleza Ayubu, wala hayakufanya maendeleo yake ya kwenda mbele kwenda polepole. Wakati huo, akiwa anapiga hesabu kile alichokuwa amepata kutoka kwenye jaribio hilo, na akitilia maanani upungufu wake binafsi, aliomba kimyakimya, akisubiri jaribio linalofuata ambalo lingemsibu yeye, kwa sababu alitamani sana, imani, utiifu, na kumcha Mungu kwake kuweze kuimarishwa kwenye jaribio linalofuata la Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 747 Ayubu Aliwezaje Kumwogopa Mungu?

Inayofuata: 749 Mtazamo wa Ayubu kwa Baraka za Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp