167 Nikiwa na Upendo wa Mungu, Sitaogopa

1

Ni nani awatesao na kuwakamata Wakristo na kusababisha maudhi na mateso,

akitarajia bure kutukomesha kufuata nyayo za Kristo?

Ni nani aufunikao mwili wangu kwa majeraha na mavilio na kuniacha nikiwa karibu kufa,

akijaribu sana kuuangamiza mwili wangu na imani yangu?

Na ni nani anayenitishia na kujaribu kunipa rushwa ili niwasaliti ndugu zangu,

akijaribu kunifanya nimsaliti Mungu, niwe Yuda na kupoteza wokovu wa Mungu?

Katika dhiki kubwa sana, maneno mema ya Mungu yanajiruduia masikioni mwangu.

Yanapoza machungu yaliyomo rohoni mwangu na mwilini mwangu.

Ninamwona Mungu kando yangu, Akinipa faraja na kunitia moyo kila mara.

Moyo wangu hauko tena peke yake, nina imani na nguvu ya kuwa shahidi.

2

Ni nani huwatayarisha watoa habari kufuatilia makazi yangu kwa siri

akizuia uhuru wangu wa binafsi kiasi kwamba nazuiliwa kabisa nyumbani?

Nani huja nyumbani kwangu mara kwa mara, akijifanya kuwa ananitembelea tu lakini anatazama kila hatua yangu,

akileta vinasa sauti na kunihoji kuhusu kuhudhuria mikusanyiko na kusoma maneno ya Mungu?

Na ni nani anayenifanya nigutuke ghafla kutoa usingizini kwa hofu,

huku maonyesho ya mateso yangu yakicheza akilini mwangu tena na tena?

Moyo wangu unalia kwa sauti kuwa China kwa kweli ni jela mbaya sana.

Hakuna uhuru, kutiwa kasumba kwa nguvu, na hata kauli zetu ziko chini ya udhibiti wao.

Kudai uhuru wa imani ni uwongo mtupu unaotumiwa na CCP kuficha udanganyifu wake kwa ulimwengu.

Mauaji ya wazi yanaonyesha asili mbovu ya CCP.

Kiitikio

Nina hakika kuwa Kristo ndiye ukweli, njia na uzima.

Bila kujali jinsi CCP inavyoweza kunitesa, nimeazimia kumfuata Kristo hadi mwisho.

Hata kutoa maisha yangu ni ushuhuda ninaopaswa kushuhudia.

Sijui usiku huu usiokuwa na mwisho utadumu kwa muda gani,

lakini nikiwa na upendo wa Mungu wa kuniongoza na neno la Mungu la kunitia moyo, sitaogopa.

Iliyotangulia: 166 Tuweze Kujua Uzuri wa Mungu

Inayofuata: 168 Chaguo Lisilo na Majuto

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp