747 Ayubu Aliwezaje Kumwogopa Mungu?

1 Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kumsikia Mungu binafsi akitamka mafundisho yoyote kwake yeye, lakini kwa Mungu moyo wake na yeye mwenyewe vyote vilikuwa vyenye thamani zaidi kuliko wale watu ambao, mbele ya Mungu waliweza tu kuongea kuhusiana na nadharia kuu, ambao waliweza tu kujigamba na kuongea kuhusu kutoa sadaka lakini walikuwa hawajawahi kuwa na maarifa ya kweli ya Mungu na walikuwa hawajawahi kumcha Mungu kwa kweli. Kwa kuwa moyo wa Ayubu ulikuwa safi, na haukufichwa kuonekana na Mungu, na ubinadamu wake ulikuwa wenye uaminifu na ukarimu, na alipenda haki na kile kilichokuwa kizuri. Binadamu kama huyu pekee aliyemiliki moyo kama huo na ubinadamu ndiye aliyeweza kufuata njia ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Binadamu kama huyo angeona ukuu wa Mungu, angeona mamlaka na nguvu Yake, na angeweza kutimiza utiifu kwa ukuu Wake na mipangilio. Binadamu tu kama huyo ndiye angeweza kulisifu jina la Mungu kwa kweli.

2 Hii ni kwa sababu hakuangalia kama Mungu angembariki au Angemletea janga, kwa sababu alijua kwamba kila kitu kinadhibitiwa na mkono wa Mungu, na kwamba binadamu kuwa na wasiwasi ni ishara ya ujinga, kutojua, na kutoweza kufikiria vyema, kuwa na shaka kuhusu ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, na ya kutomcha Mungu. Maarifa ya Ayubu hasa ndiyo ambayo Mungu alitaka. Alikuwa hajapitia kazi ya Mungu wala kuwahi kumsikia Mungu akiongea, au kuuona uso wa Mungu. Kwamba aliweza kuwa na mtazamo kama huo kwa Mungu yalikuwa hasa matokeo ya ubinadamu wake na ufuatiliaji wake binafsi, ubinadamu na ufuatiliaji ambao watu hawana leo. Hivyo, katika enzi hiyo, Mungu alisema, “Hakuna mtu ambaye yuko kama yeye ulimwenguni, mtu aliye mkamilifu na mwaminifu.”

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 746 Matendo ya Haki ya Ayubu Yalimshinda Shetani

Inayofuata: 748 Imani na Utii wa Kweli wa Ayubu kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp