948 Watu wa Siku za Mwisho Hawajawahi Kuona Hasira ya Mungu

1 Inaweza kusemekana kwamba kuanzia wakati wa uumbaji mpaka leo, hakuna kikundi ambacho kimefurahia neema au huruma nyingi za Mungu pamoja na upole wa upendo kama kikundi hiki cha mwisho. Ingawaje, kwenye awamu ya mwisho, Mungu amefanya kazi Yake ya hukumu na kuadibu, na Amefanya kazi Yake kwa adhama na hasira, wakati mwingi Mungu anatumia tu maneno kukamilisha kazi Yake; Anatumia maneno ili kufunza, kunyunyiza na kutosheleza, na kulisha. Hasira ya Mungu, wakati haya yakiendelea, siku zote imefichwa, na mbali na kuipitia tabia ya Mungu yenye hasira kwa maneno Yake, watu wachache sana wamepitia ghadhabu Yake ana kwa ana.

2 Hivi ni kusema, kwamba wakati wa kazi ya hukumu na kuadibu kwa Mungu, ingawaje hasira iliyofichuliwa katika maneno ya Mungu inawaruhusu watu kupitia adhama na kutovumilia kosa kwa Mungu, hasira hii haizidi maneno Yake. Kwa maneno mengine, Mungu hutumia maneno ili kukemea binadamu, kumfichua binadamu, kuhukumu binadamu, kumwadhibu binadamu na hata kumshutumu binadamu—lakini Mungu angali hajawa mwenye wingi wa ghadhabu kwa binadamu, na hata hajaachilia hasira Yake kwa binadamu nje ya maneno yake. Hivyo, rehema na upole wa upendo wa Mungu uliopitiwa na binadamu kwenye enzi hii ni ufunuo wa tabia ya kweli ya Mungu, huku hasira ya Mungu iliyoipitiwa na binadamu ikiwa tu ni athari ya sauti na hisia za matamko Yake. Watu wengi wanachukulia athari hii kimakosa na kuiona kuwa njia ya kweli ya kupitia na maarifa ya kweli ya hasira ya Mungu.

3 Hivyo basi, watu wengi wanasadiki kwamba wameiona huruma ya Mungu na upole wa upendo ndani ya maneno Yake, kwamba wameweza pia kushuhudia kutovumilia Kwake kwa kosa la binadamu, na wengi wao wamekuja hata kutambua huruma na uvumilivu wa Mungu kwake binadamu. Haijalishi tabia ya binadamu ni mbaya kiasi kipi, au upotovu wa tabia yake, Mungu siku zote anavumiliwa. Katika kuvumiliwa, nia Yake ni kusubiria maneno Aliyokuwa Ametamka, jitihada Alizofanya na gharama Aliyolipia ili kutimiza athari iliyo ndani ya wale Anaotaka kupata.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 947 Onyo la Maangamizi ya Mungu ya Sodoma kwa Wanadamu

Inayofuata: 949 Maana ya Ishara ya Ghadhabu ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp