718 Kuwa na Imani Katika Mabadiliko ya Tabia

1 Mabadiliko katika tabia hayatokei mara moja—huu ni ukweli. Hiyo ni kwa sababu mabadiliko katika tabia ni aina ya mabadiliko ambayo hupatikana kwa kugundua chanzo cha asili ya mtu iliyo potovu. Wakati wa mchakato huu, labda utaelewa kitu kimoja tu baada ya kupitia mengi, na baada ya hayo tu ndipo utafikia kipengele kimoja ya mabadiliko katika tabia. Au labda baada tu ya kukutana na watu wengi, matukio, mambo, na mazingira tofauti, baada ya kutembea barabara nyingi zilizopinda ndipo utaweza kufanikisha mabadiliko kidogo. Haijalishi ni mabadiliko makubwa kiasi gani, ni ya thamani machoni pa Mungu. Anayathamini na kuyaadhimisha kwa sababu uliteseka sana na kulipa gharama kubwa. Mungu huona ndani ya kina cha mioyo ya wanadamu na Anajua matakwa yako ni yepi. Pia Anajua udhaifu wako ni upi, na hata zaidi Anajua unachohitaji.

2 Katika Biblia, kuna hadithi ya kurudi kwa mwana mpotevu. Kwa nini kuwe na aina hii ya mfano? Ni kwamba mapenzi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu ni ya kweli. Anawapa watu fursa za kutubu na fursa za kubadili, na wakati wa mchakato huu, Anawaelewa watu na Ana ufahamu mkubwa kuhusu udhaifu wao na kiwango cha upotovu wao. Anajua kwamba watajikwaa. Ndiyo maana inasemwa Mungu huona ndani ya vina vya mioyo ya watu. Haijalishi wewe ni dhaifu kiasi gani, mradi huliachi jina la Mungu, mradi humwachi Mungu au njia hii, daima utakuwa na fursa ya kufikia mabadiliko katika tabia. Kwa hiyo, tunapojua mabadiliko katika tabia ni nini, tunapojua ni aina gani ya mchakato tunapaswa kupitia ili tuwe na mabadiliko katika tabia, hatuhitaji kuogopa. Badala yake, tunapaswa kuwa na ujasiri. Kutokana na suala la mabadiliko katika tabia tunaweza kuona kwamba kazi ya Mungu ni ya kweli na ya utendaji, na kwamba Ana uwezo wa kuwaokoa wanadamu kutoka kwa asili yao ya upotovu wa Shetani, kuwapokonya kutoka kwa mikono ya Shetani, na pia Anayo nguvu na hekima ya kuwawezesha kufanikisha mabadiliko katika tabia.

Umetoholewa kutoka katika “Nini Maana ya Mabadiliko Katika Tabia na Njia Kuelekea Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 717 Washahidi wa Mungu Lazima Wawe na Badiliko katika Tabia

Inayofuata: 719 Wale Wanaotii Kazi ya Mungu kwa Kweli Wanaweza Kupatwa na Yeye

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp