122 Joka Kuu Jekundu Linaanguka Kadiri Watu wa Mungu Wanavyokomaa

1 Wakati ambapo watu wote watakuwa wamefanywa kamili na mataifa yote ya dunia kugeuka kuwa ufalme wa Kristo, basi huo utakuwa wakati ambapo radi saba zitanguruma. Siku ya sasa ni hatua ndefu ya kwenda mbele katika mwelekeo wa hatua hiyo, shambulio limeachiliwa huru kwa muda ujao. Huu ni mpango wa Mungu—hivi karibuni utafanikishwa. Hata hivyo, Mungu tayari amefanikisha yote ambayo Amesema. Hivyo, ni dhahiri kwamba mataifa ya dunia ni makasri tu yaliyo mchangani yanayotetemeka bamvua linapokaribia: Siku ya mwisho iko karibu sana na joka kubwa jekundu litaanguka chini ya neno la Mungu.

2 Ili kuhakikisha kwamba mpango wa Mungu unatekelezwa kwa ufanisi, malaika wa mbinguni wameshuka juu ya dunia, wakifanya kila wanaloweza kumridhisha Mungu. Mungu Mwenyewe mwenye mwili Amejipanga katika uwanja wa vita kupigana na adui. Po pote ambapo Aliyepata mwili huonekana, adui anaangamiziwa mahali hapo. Uchina ni ya kwanza kuangamizwa, kuharibiwa kabisa kwa mkono wa Mungu. Mungu haipi Uchina upande wowote kabisa. Thibitisho la kuendelea kuanguka kwa joka kubwa jekundu linaweza kuonekana katika ukomavu wa watu unaoendelea. Hili linaweza kuonekana wazi na mtu yeyote. Ukomavu wa watu ni ishara ya kifo cha adui. Lakini Mimi binafsi Naenda mahali ambapo joka kuu jekundu limelala likiwa limejizongomeza, Nipigane nalo. Na wakati binadamu wote wanapata kunijua Mimi kutoka ndani ya mwili, na kuweza kuyaona matendo Yangu kutoka ndani ya mwili, wakati huo makazi ya joka kuu jekundu yatageuzwa kuwa jivu na kutoweka yasipatikane tena.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 10” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 121 Kusudi la Kazi ya Mungu Katika Siku za Mwisho

Inayofuata: 123 Mungu Amekamilisha Kundi la Washindi Uchina

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp