864 Ni Maumivu Magani Makubwa Apitiayo Mungu?
1 Kunao baadhi ya watu ambao huonea huruma hali ya Kristo kwa sababu kunao mstari katika Biblia unaosema: “Mbweha wana mashimo, na ndege wanavyo viota; lakini Mwana wa Adamu hana pahali pa kupumzisha kichwa chake.” Wakati watu wanaposikia haya, wanayatia moyoni na kuamini kwamba haya ndiyo mateso makubwa zaidi ambayo Mungu huvumilia, na mateso makubwa zaidi ambayo Kristo huvumilia. Sasa, tukiangalia katika mtazamo wa ukweli, Mungu haamini kwamba ugumu huu ni mateso. Hajawahi kulia dhidi ya dhuluma hizi kwa ajili ya ugumu wa mwili, na hajawahi kuwalipizia kisasi wanadamu au Kujitoza na chochote. Hata hivyo, Anaposhuhudia kila kitu cha wanadamu, maisha yaliyopotoka na uovu wa wanadamu waliopotoka, Anaposhuhudia kwamba wanadamu wamo katika ung’amuzi wa Shetani na wamefungwa na Shetani na hawawezi kukwepa, kwamba wanaoishi ndani ya dhambi hawajui ukweli ni nini—Hawezi kuvumilia dhambi hizi zote. Chuki Yake kwa binadamu huongezeka siku baada ya siku, lakini lazima Avumilie yote haya. Haya ni mateso makuu ya Mungu.
2 Mungu hawezi kujieleza kikamilifu hata sauti ya moyo Wake au hisia Zake miongoni mwa wafuasi Wake, na hakuna yeyote miongoni mwa wafuasi Wake anayeweza kuelewa kwa kweli mateso Yake. Hakuna yule ambaye hujaribu kuyaelewa au kuutuliza moyo Wake—moyo Wake huvumilia mateso haya siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, mara kwa mara. Unaona nini katika yote haya? Mungu hahitaji chochote kutoka kwa wanadamu kama malipo kwa kile Alichokitoa, lakini kwa sababu ya kiini cha Mungu, Hawezi kuvumilia kamwe uovu, upotovu na dhambi ya wanadamu, lakini Anahisi chukizo na chuki kupindukia, hali ambayo husababisha moyo wa Mungu na mwili Wake kuvumilia mateso yasiyoisha. Je, ungeyaona yote haya? Kuna uwezekano, hakuna yeyote kati yenu ambaye angeyaona kwa sababu hakuna yeyote kati yenu anayeweza kumwelewa Mungu kwa kweli.
Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili