Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Utakatifu wa Mungu (II)

Leo, kaka na dada, hebu tuimbe wimbo. Tafuta mmoja ambao mnapenda na ambao mmeimba mara nyingi kabla. (Tungependa kuimba wimbo wa neno la Mungu “Upendo Safi Bila dosari.”)

1  “Upendo” unarejelea hisia ambayo ni safi na bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kujali. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna mashaka, hakuna udanganyifu, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna mabadilishano na hakuna chochote kichafu. Iwapo una upendo, basi hautadanganya, kulalamika, kusaliti, kuasi, kushurutisha, au kutafuta kupata kitu au kupata malipo fulani.

2  “Upendo” unarejelea hisia ambayo ni safi na bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kujali. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna mashaka, hakuna udanganyifu, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna umbali na hakuna chochote kichafu. Iwapo una upendo, basi utajitolea na kuvumilia magumu kwa furaha, na utalingana na Mimi, utaacha kila kitu ulicho nacho kwaajili Yangu, utaacha vyote ulivyo navyo kwa sababu ya Mungu: familia yako, siku zako za baadaye, ujana wako, na ndoa yako. Vinginevyo, upendo wenu haungekuwa upendo hata kidogo, lakini badala yake udanganyifu na usaliti!

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Huu ulikuwa wimbo mzuri kuchagua. Mnapenda kuimba wimbo huu? Mnahisi nini baada ya kuimba wimbo huu? Mnaweza kuhisi upendo wa aina hii ndani yenu? (Bado.) Ni maneno yapi ya wimbo huu yanayokugusa kwa kina zaidi? (Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, hakuna mabadilishano, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna uchaguzi na hakuna chochote kichafu. Lakini ndani yangu bado naona uchafu mwingi, na sehemu zangu nyingi ambazo hujaribu kufanya mabadilishano na Mungu. Kwa kweli sijafikia aina ya upendo ulio safi na usiokuwa na dosari.) Ikiwa hujafikia upendo safi, usio na dosari, basi kiwango cha upendo wako ni kipi? (Niko tu katika hatua ambapo niko tayari kutafuta, katika hatua ambapo nina hamu.) Kulingana na kimo chako mwenyewe na kutumia maneno yako mwenyewe kutoka kwa uzoefu wako mwenyewe, umefikia kiwango kipi? Je, una udanganyifu? Je, una madai ndani ya moyo wako? Kuna vitu unavyotaka na kutamani kutoka kwa Mungu? (Ndiyo, kuna hivi vitu vilivyo na doa.) Vinajitokeza katika hali gani? (Wakati hali ambayo Mungu amenipangia hailingani na fikira zangu ya vile inapaswa kuwa, ama wakati matakwa yangu hayajatimizwa: katika nyakati kama hizi, Ninafunua aina hii ya tabia potovu.) Ninyi ndugu mnaotoka Taiwani, je, ninyi huimba wimbo huu mara kwa mara pia? Je, mnaweza kuzungumza kidogo juu ya jinsi mnavyoelewa “upendo safi bila dosari”? Kwa nini Mungu anafafanua upendo kwa njia hii? (Ninaupenda wimbo huu sana kwa sababu ninaweza kuona kutoka kwenye wimbo huu kwamba upendo huu ni upendo kamili. Hata hivyo, bado nina mwendo mrefu kabisa wa kufikia kiwango hicho, na bado niko mbali sana kufikia upendo wa kweli. Kuna vitu ambavyo kwavyo nimeweza kupiga hatua na kushirikiana kupitia nguvu ambayo maneno Yake hunipa na kwa njia ya maombi. Hata hivyo, ninapokabiliwa na majaribu au ufichuzi fulani, mimi huhisi kwamba sina mustakabali au majaliwa, kwamba sina hatima. Wakati kama huo, mimi huhisi dhaifu sana, na suala hili hunisumbua mara nyingi.) Je, ni nini unachozungumzia hasa unaposema “mustakabali na majaliwa”? Je, kuna kitu maalum unachorejelea? Je, ni picha au kitu ulichodhania, au mustakabali na hatima yako ni vitu unavyoweza kuona kweli? Je, ni kitu halisi? Nataka kila mmoja wenu afikirie juu ya jambo hilo: Je, wasiwasi mlio nao kuhusu mustakabali na majaliwa yenu yanarejelea nini? (Ni kuweza kuokolewa ili niweze kuishi.) Ninyi ndugu wengine, ninyi pia zungumzieni kidogo juu ya ufahamu wenu wa “upendo safi bila dosari.” (Mtu anapokuwa nao, hakuna uchafu unaotokana na nafsi yake mwenyewe na hadhibitiwi na mustakabali wake au majaliwa yake. Licha ya vile Mungu anamtunza, anaweza kutii kikamilifu kazi ya Mungu na mipango Yake na kumfuata Yeye hadi mwisho kabisa. Upendo wa aina hii tu kwa Mungu ndio upendo safi na usio na dosari. Katika kujipima dhidi yake, nimegundua kwamba, ingawa ninaonekana kuwa nilijitumia au kutupa kando vitu kadhaa katika miaka michache iliyopita ya kumwamini Mungu, sijaweza kweli kumpa Yeye moyo wangu. Wakati Mungu ananifunua, nahisi kwamba siwezi kuokolewa, na nasalia katika hali hasi. Najiona nikifanya wajibu wangu, lakini wakati huo huo najaribu kufanya mipango na Mungu, siwezi kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, na hatima yangu, siku zangu za baadaye, na kudura yangu yote daima yako kwa akili yangu.) Inaonekana kwamba mmepata ufahamu kiasi wa wimbo huu, na mmefanya uhusiano fulani kati ya wimbo huo na matukio yenu halisi. Hata hivyo, mna viwango tofauti vya kukubali kila kirai katika wimbo “Upendo Safi bila Dosari.” Watu wengine hufikiri kwamba ni juu ya utayari, watu wengine wanatafuta kuweka kando siku zao za baadaye, watu wengine wanatafuta kuweka kando familia zao, watu wengine hawatafuti kupokea chochote. Bado wengine wanajihitaji kuwa bila udanganyifu, bila malalamiko, na kutoasi dhidi ya Mungu. Kwa nini Mungu angetaka kupendekeza aina hii ya upendo na kuhitaji kwamba watu wampende namna hii? Hii ni aina ya upendo ambao watu wanaweza kuufikia? Hiyo ni kusema, watu wanaweza kupenda namna hii? Watu wanaweza kuona kwamba hawawezi, kwa sababu hawamiliki kamwe upendo wa aina hii. Wakati hawaumiliki, na kimsingi hawajui kuhusu upendo, Mungu anazungumza maneno haya, ambayo ni mageni kwao. Kwa sababu watu wanaishi katika dunia hii, wanaishi katika tabia yao potovu, iwapo watu wangekuwa na aina hii ya upendo ama iwapo mtu angeweza kumiliki aina hii ya upendo, bila kuwa na maombi na madai, kuwa radhi kujitoa wenyewe na kuwa radhi kustahimili mateso na kuacha vyote vilivyo vyao, mtu anayemiliki aina hii ya upendo angewezaje kuonekana katika macho ya watu wengine? Si angekuwa mtu mkamilifu? (Ndiyo.) Je, mtu mkamilifu kama huyo yupo katika dunia hii? Mtu wa aina hii hayupo kabisa katika dunia hii. Hili ni bila shaka. Hivyo, watu wengine—kupitia uzoefu wao—wanatumia juhudi nyingi kuwa kama kile ambacho maneno haya yalielezea. Wanajishughulikia, wanajizuia, na hata mara kwa mara wanajiacha: Wanastahimili mateso na wanaacha mawazo potofu waliyoshikilia. Wanaacha njia ambazo wamekuwa waasi kwa Mungu, wanaacha tamaa zao na matakwa. Lakini mwishowe bado hawawezi kufikia mahitaji hayo. Kwa nini hayo yanafanyika? Mungu anasema mambo haya ili kutoa kiwango cha watu kufuata, ili watu wajue kiwango wanachodaiwa na Mungu. Lakini Mungu amewahi kusema kwamba watu lazima wafikie hiki mara moja? Je, Mungu amewahi kusema ni katika wakati upi watu wanapaswa kufikia hilo? (La.) Je, Mungu amewahi kusema kwamba watu lazima wampende namna hii? Je, kifungu hiki kinasema hivi? La, hakisemi hivi. Mungu anawaambia watu tu kuhusu “upendo” Aliokuwa akirejelea. Kuhusiana na watu kuweza kumpenda Mungu namna hii na kumtendea Mungu namna hii, mahitaji ya Mungu ni yapi? Si muhimu kuyafikia mara moja, ama papo hapo kwa sababu watu hawawezi kufanya hivyo. Mmewahi kufikiria kuhusu masharti ambayo watu wanapaswa kutimiza ili kupenda namna hii? Iwapo watu wangeyasoma maneno haya mara nyingi watakuwa na upendo huu polepole? (La.) Masharti ni yapi basi? Kwanza, watu wanawezaje kuwa huru kutokana na mashaka kumhusu Mungu? (Ni watu waaminifu tu wanaoweza kufikia jambo hilo.) Je, kuwa huru kutokana na udanganyifu? (Pia wanapaswa kuwa watu waaminifu.) Je, kuwa mmoja asiyetaka kufanya mipango na Mungu? Huyo pia lazima awe mtu mwaminifu, vipi kuhusu, kutokuwa na ujanja? Kunarejelea nini kusema hakuna chaguo katika upendo? Yote yanarejelea kuwa mtu mwaminifu? Kuna maelezo mengi hapo; je, inathibitisha nini kwamba Mungu anaweza kuzungumza na kufafanua aina hii ya upendo kwa njia hii? Tunaweza kusema kwamba Mungu anamiliki upendo wa aina hii? (Ndiyo.) Je, mnaona wapi hili? (Katika upendo ambao Mungu anao kwa mwanadamu.) Je, upendo wa Mungu kwa mwanadamu una masharti? Je, kuna vizuizi ama umbali kati ya Mungu na mwanadamu? Je, Mungu ana tuhuma uu ya mwanadamu? (La.) Mungu humwangalia mwanadamu na kumwelewa mwanadamu; kwa kweli Anamwelewa mwanadamu. Je, Mungu ni mdanganyifu kwa mwanadamu? (La.) Kwa kuwa Mungu anaongea kikamilifu kuhusu upendo huu, moyo Wake ama kiini Chake vinaweza kuwa kamilifu sana? (Ndiyo.) Bila shaka vinaweza; wakati uzoefu wa watu umefikia kiwango fulani, wanaweza kuhisi jambo hili. Je, watu wamewahi kufafanua upendo kwa njia hii? Mwanadamu amefafanua upendo katika hali gani? Mwanadamu anazungumza vipi kuhusu upendo? Si ni kupeana ama kutoa? (Ndiyo.) Ufafanuzi wa mwanadamu wa upendo ni rahisi, na hauna kiini.

Ufafanuzi wa Mungu wa upendo na namna Mungu anazungumza kuhusu upendo inahusiana na kipengele cha kiini Chake, lakini ni kipengele kipi cha kiini Chake? Wakati uliopita tulishiriki kuhusu mada muhimu sana, ni mada ambayo watu wamezungumzia mara nyingi awali, na ni neno ambalo linatajwa mara nyingi katika kipindi cha kumwamini Mungu, lakini ni neno linalojulikana na pia ni geni kwa watu. Lakini kwa nini hivyo? Ni neno linalotoka kwa lugha za mwanadamu; hata hivyo, miongoni mwa mwanadamu ufafanuzi wake ni tofauti na usioeleweka. Neno hili ni nini? (Utakatifu.) Utakatifu: hiyo ndiyo ilikuwa mada ya wakati wa mwisho tuliposhiriki. Tulishiriki kiasi kuhusu mada hii. Kupitia katika ushirika wetu wa wakati uliopita, je, kila mtu alipata ufahamu mpya kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu? Mnafikiri uelewa mpya ulikuwa nini? Yaani, nini katika uelewa huo ama maneno hayo yaliwafanya kuhisi kwamba uelewa wenu wa utakatifu wa Mungu ulikuwa tofauti ama uliobadilishwa na kile Nilichoshiriki kuhusu utakatifu wa Mungu? Je, iliacha maono? (Mungu anasema Anachohisi katika moyo Wake; ni safi. Hiki ni kipengele kimoja cha utakatifu.) (Kuna utakatifu wakati Mungu ana ghadhabu kwa mwanadamu, hakuna dosari.) (Kuhusu utakatifu wa Mungu, naelewa kwamba kuna ghadhabu ya Mungu na huruma ya Mungu katika tabia Yake ya haki. Hili liliacha mtazamo wenye nguvu kwangu. Katika ushirika wetu wa wakati uliopita, ilitajwa pia kuwa tabia ya Mungu yenye haki ni ya kipekee—sikuelewa jambo hili zamani. Ni baada tu ya kusikia kile ambacho Mungu alikuwa ameshiriki ndipo nilielewa kuwa ghadhabu ya Mungu ni tofauti na hasira ya mwanadamu. Ghadhabu ya Mungu ni kitu chanya na ina kanuni; hiyo hutumwa kwa sababu ya kiini cha asili cha Mungu. Mungu huona kitu kibaya, na hivyo Anaachilia ghadhabu Yake. Hiki ni kitu kisichomilikiwa na kiumbe yeyote aliyeumbwa.) Mada yetu leo ni utakatifu wa Mungu. Watu wote wamesikia na kujifunza kitu kuhusu tabia ya haki ya Mungu. Aidha, watu wengi mara nyingi huzungumza juu ya utakatifu wa Mungu na tabia ya Mungu yenye haki kwa pamoja; wao husema kuwa tabia ya Mungu yenye haki ni takatifu. Neno “takatifu” hakika si geni kwa mtu yeyote—ni neno linalotumiwa mara nyingi. Lakini kwa kuzingatia maana zilizo ndani ya neno hilo, ni maonyesho gani ya utakatifu wa Mungu ambayo watu wanaweza kuona? Ni nini Mungu amefichua ambacho watu wanaweza kutambua? Ninahofia kwamba hiki ni kitu ambacho hakuna anayejua. Tabia ya Mungu ni ya haki, lakini basi ukichukua tabia ya haki ya Mungu na useme kuwa ni takatifu, hiyo inaonekana isiyo dhahiri kiasi, ya kuchanganya wazo; mbona hivi? Unasema tabia ya Mungu ni ya haki, ama unasema tabia Yake ya haki ni takatifu, hivyo katika mioyo yenu mnauainisha utakatifu wa Mungu vipi? Mnauelewa vipi? Hivyo ni kusema, ni nini kuhusu kile ambacho Mungu amefichua, ama kile Anacho na alicho ambacho watu wanaweza kutambua kama kitakatifu? Umefikiria hili hapo awali? Kile Nilichoona ni kwamba watu mara nyingi husema maneno yanayotumika sana ama wana virai ambavyo vimesemwa mara kwa mara, lakini hawajui wanachosema. Hivi tu ni vile kila mtu anavyosema, na wanasema hivi mara nyingi, hivyo inakuwa kirai kilichowekwa. Hata hivyo, iwapo wangechunguza na kutafiti kwa kina maelezo, wangepata kwamba hawajui maana halisi ni nini ama inachorejelea. Kama tu neno “takatifu,” hakuna anayejua kabisa ni kipengele kipi cha kiini cha Mungu kinarejelewa kuhusiana na utakatifu Wake ambao wanaongea kuhusu, na hakuna anayejua kupatanisha neno “takatifu” na Mungu. Watu wamechanganyikiwa mioyoni mwao, na utambuzi wao wa utakatifu wa Mungu ni usio dhahiri na wazi. Kuhusu jinsi Mungu ni mtakatifu hakuna aliye wazi kabisa. Leo tutashiriki kuhusu mada ya kupatanisha neno “takatifu” na Mungu ili watu waweze kuona maudhui ya kweli ya kiini cha utakatifu wa Mungu, na hili litazuia watu wengine kulitumia neno hilo kimazoea ovyo ovyo na kusema vitu kwa nasibu wakati hawajui maana yake, ama kama wako sawa na sahihi. Watu daima wamekuwa wakizungumza namna hii; wewe umefanya, yeye pia na hivyo imekuwa tabia ya usemi. Bila kukusudia inaharibu neno kama hilo.

Kuhusu neno “takatifu,” juujuu linaonekana rahisi sana kuelewa, siyo? Kwa kiwango cha chini kabisa watu wanaamini neno “takatifu” linamaanisha nadhifu, isiyo na doa, tukufu, na safi. Kuna watu wengine pia ambao huhusisha “utakatifu” na “upendo,” ambayo ni sahihi; hii ni sehemu yake. Upendo wa Mungu ni sehemu ya kiini Chake, lakini si kiini chote. Hata hivyo, katika mitazamo ya watu, wanaona neno na kulishirikisha na vitu ambavyo wao wenyewe wanaviona kuwa nadhifu na safi, ama na vitu ambavyo wao binafsi wanafikiri havina doa wala havina dosari. Kwa mfano, watu wengine walisema kwamba ua la yungiyungi ni safi, na kwamba linatoa maua bila dosari kutoka kwa maji machafu. Hivyo watu wakaanza kutumia neno “takatifu” kwa ua la yungiyungi. Watu wengine walichukulia hadithi za mapenzi zilizobuniwa na wengine kuwa takatifu, ama wangewaona wahusika wakuu wanaostahili kuwa watakatifu. Zaidi, wengine walifikiria watu kutoka kwenye Biblia, ama wengine walioandikwa katika vitabu vya kiroho—kama watakatifu, mitume, au wengine ambao walimfuata Mungu awali Alipokuwa akifanya kazi Yake—kama waliokuwa na uzoefu wa kiroho ambao ulikuwa takatifu. Haya yote ni mambo yaliyofikiriwa na watu na hizi ni dhana zinazoshikiliwa na watu. Mbona watu wanashikilia dhana kama hizi? Sababu ni rahisi sana: Ni kwa sababu watu wanaishi miongoni mwa tabia potovu na wanaishi katika dunia ya uovu na uchafu. Kila kitu wanachoona, kila kitu wanachogusa, kila kitu wanachopitia ni uovu wa Shetani na upotovu wa Shetani na pia kufanya mipango, kupigana wenyewe kwa wenyewe, na vita vinavyotokea miongoni mwa watu walio chini ya ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, hata wakati Mungu anafanya kazi Yake kwa watu, na hata wakati Anazungumza nao na kufichua tabia na kiini Chake hawawezi kuona ama kujua utakatifu na kiini cha Mungu ni nini. Watu mara nyingi husema kwamba Mungu ni mtakatifu, lakini hawana uelewa wowote wa kweli; wao husema tu maneno matupu. Kwa sababu watu wanaishi miongoni mwa uchafu na upotovu na wanamilikiwa na Shetani, na hawaoni mwangaza, hawajui chochote kuhusu masuala mema na zaidi, hawajui ukweli. Kwa hivyo, hakuna anayejua maana ya utakatifu. Baada ya kusema hayo, je, kuna vitu vitakatifu ama watu watakatifu miongoni mwa binadamu hawa wapotovu? Tunaweza kusema kwa uhakika La, hakuna, kwa sababu kiini cha Mungu tu ndicho kitakatifu.

Kuhusu utakatifu wa kiini cha Mungu, wakati uliopita tulishiriki kidogo kuuhusu na huo ulikuwa msukumo wa maarifa ya watu ya utakatifu wa Mungu, lakini hautoshi. Hauwezi kutosha kusaidia watu kujua kikamilifu utakatifu wa Mungu, wala hautoshi kuwasaidia kuelewa kwamba utakatifu wa Mungu ni wa kipekee. Zaidi, hautoshi kuruhusu watu kuelewa kipengele cha maana ya ukweli ya utakatifu kwani imejumuishwa kabisa kwa Mungu. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba tuendelee na ushirika wetu katika mada hii. Hapo nyuma ushirika wetu ulijadili mada tatu, kwa hivyo sasa tunapaswa kujadili mada ya nne, na tutaanza kusoma maandiko.

Majaribu ya Shetani

Mat 4:1-4 Baada ya hapo Yesu akaongozwa mwituni na Roho kwa minajili ya kujaribiwa na ibilisi. Na baada ya Yeye kufunga kwa siku arobaini mchana na usiku, Alihisi njaa. Na aliyemjaribu alipokuja Kwake, alimwambia, Iwapo Wewe ni Mwana wa Mungu, yaamrishe mawe haya yabadilike kuwa mikate. Lakini Akamjibu na kusema, imeandikwa, Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.

Haya ndiyo maneno ambayo ibilisi kwanza alijaribu kumjaribu Bwana Yesu. Ni nini maudhui ya aliyoyasema ibilisi? (“Iwapo Wewe ni Mwana wa Mungu, yaamrishe mawe haya yabadilike kuwa mikate.”) Maneno haya ambayo ibilisi alizungumza ni rahisi kiasi, lakini kuna tatizo na kiini chake? Ibilisi alisema, “Iwapo Wewe ni Mwana wa Mungu,” lakini katika moyo wake, alijua au hakujua kwamba Yesu alikuwa Mwana wa Mungu? Alijua au hakujua kwamba Alikuwa Kristo? (Alijua.) Basi kwa nini alisema “Iwapo Wewe ni”? (Alikuwa akijaribu kumjaribu Mungu.) Lakini ni nini madhumuni ya kufanya hivyo? Alisema, “Iwapo Wewe ni Mwana wa Mungu.” Katika moyo wake alijua kwamba Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu, alijua haya vizuri sana moyoni mwake, lakini licha ya kujua haya, je, alinyenyekea Kwake na kumwabudu Yeye? (La.) Alitaka kufanya nini? Alitaka kutumia mbinu hii na maneno haya kumghadhabisha Bwana Yesu, na kisha kumhadaa Atende kulingana na makusudi yake. Je, si hii ndiyo iliyokuwa maana ya maneno ya ibilisi? Katika moyo wa Shetani, alijua wazi kwamba huyu alikuwa Bwana Yesu Kristo, lakini alisema maneno haya hata hivyo. Je, si hii ni asili ya Shetani? Asili ya Shetani ni nini? (Kuwa mjanja, mwovu na kutokuwa na Heshima kwa Mungu.) Ni matokeo gani yangetokana na kutomcha Mungu? Je, si kwamba alitaka kumshambulia Mungu? Alitaka kutumia mbinu hii kumshambulia Mungu, na hivyo alisema: “Iwapo Wewe ni Mwana wa Mungu, yaamrishe mawe haya yabadilike kuwa mikate”; je, si hii ni nia ovu ya Shetani? Alikuwa anajaribu kufanya nini kweli? Lengo lake ni wazi sana: Alikuwa anajaribu kutumia mbinu hii kukanusha nafasi na utambulisho wa Bwana Yesu Kristo. Alichomaanisha na maneno hayo ni, “Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Usipofanya hivyo, basi wewe siwe Mwana wa Mungu na Hufanyi kazi hii.” Hii ni sahihi? Alitaka kutumia mbinu hii kumshambulia Mungu, alitaka kuvunja na kuharibu kazi ya Mungu; huu ndio uovu wa Shetani. Uovu wake ni maonyesho ya kiasili ya asili yake. Ingawaje alijua Bwana Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu, kupata mwili kwenyewe kwa Mungu Mwenyewe, hangeweza kuacha kufanya kitu kama hiki, kumfuata Mungu nyuma na kuendelea kumshambulia na kujaribu sana kuvuruga na kuharibu kazi ya Mungu.

Sasa, hebu tuchambue kirai hiki alichonena Shetani: “Yaamrishe mawe haya yabadilike kuwa mikate” Kubadili mawe yawe mikate—hili linamaanisha chochote? Iwapo kuna chakula, kwa nini usile? Kwa nini ni muhimu kubadili mawe yawe mikate? Kuna maana hapa? Ingawa alikuwa amefunga wakati huo, kwa hakika Bwana Yesu alikuwa na chakula cha kula? (Alikuwa nacho.) Kwa hivyo, hapa, tunaona upumbavu wa matumizi ya Shetani ya kirai hiki. Kwa ujanja na uovu wake wote, tunaona upumbavu na upuuzi wake. Shetani anafanya idadi fulani ya mambo. Unaona asili yake yenye kudhuru na unaona akiharibu kazi ya Mungu, na wa kuchukiza na kuudhi sana. Lakini kwa upande mwingine, unapata asili ya kitoto na ujinga nyuma ya maneno na vitendo vyake? Huu ni ufunuo kuhusu asili ya Shetani; ana asili ya aina hii na atafanya kitu kama hiki. Kwa wanadamu, kirai hiki ni cha upuuzi na cha kuchekesha. Lakini maneno kama hayo kwa hakika yanaweza kutamkwa na Shetani. Tunaweza kusema kwamba ni asiyejua? Mjinga? Uovu wa Shetani uko kila mahali na daima unafichuliwa. Na Bwana Yesu anamjibuje? (“Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.”) Maneno haya yana nguvu yoyote? (Yanayo.) Mbona tunasema kwamba yana nguvu? Hii ni kwa sababu maneno haya ni ukweli. Sasa, mtu anaishi kwa mkate tu? Bwana Yesu alifunga kwa siku arubanini usiku na mchana. Alikufa kwa njaa? Hakufa kwa njaa, kwa hivyo Shetani alimkaribia, akimwambia abadili mawe yawe chakula kwa kusema kitu kama hiki: “Ukiyabadili mawe yawe chakula, Hutakuwa basi na vitu vya kula? Si basi Hutalazimika kufunga, Hutalazimika kuwa na njaa?” Lakini Bwana Yesu alisema, “Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee,” inayomaanisha kwamba, ingawa mwanadamu anaishi katika mwili, kile kinachouruhusu mwili wake kuishi na kupumua si chakula, ila maneno yote yaliyotamkwa na kinywa cha Mungu. Katika upande mmoja, maneno haya ni ukweli; yanawapa watu imani, yakiwafanya wahisi kwamba wanaweza kumtegemea Mungu na kwamba Yeye ni ukweli. Kwa upande mwingine, kuna kipengele cha vitendo katika maneno haya? Si Bwana Yesu bado amesimama pale na bado Yu hai baada ya kufunga kwa siku arubaini mchana na usiku? Je, huu si mfano? Hajala chakula chochote kwa siku arubaini mchana na usiku. Bado yuko hai. Huu ni ushahidi wa nguvu unaothibitisha ukweli wa maneno Yake. Maneno haya ni rahisi, lakini kwa Bwana Yesu, je, Aliyazungumza tu wakati ambapo Shetani alimjaribu, au yalikuwa tayari pamoja na Yeye? Kuliweka kwa njia nyingine, Mungu ni ukweli, Mungu ni uhai, lakini je, ukweli na uhai wa Mungu uliongezwa kwa kuchelewa? Je, ulitokana na uzoefu? La, ni ya asili ndani ya Mungu, Ambayo inamaanisha ukweli na uhai vipo ndani ya kiini cha Mungu. Licha ya kile kinachomfanyikia, Anachofichua ni ukweli. Ukweli huu, kirai hiki—iwapo maudhui yake ni mapana ama finyu—kinaweza kumwacha mwanadamu aishi, kimpe uhai; kinaweza kumwezesha mwanadamu kupata, ndani yake, ukweli, uwazi kuhusu njia ya maisha ya binadamu, na kumwezesha kuwa na imani kwa Mungu. Kwa maneno mengine, chanzo cha matumizi ya Mungu ya kifungu hiki ni chanya. Kwa hivyo tunaweza kusema jambo hili chanya ni takatifu? (Ndiyo.) Maneno ya Shetani yanatokana na asili ya Shetani. Shetani anafichua asili yake ovu, asili yake yenye kijicho, kila mahali, daima. Sasa, ufunuo huu, Shetani anaufanya kiasili? Kuna yeyote anayemchochea? Kuna yeyote anayemsaidia? Kuna yeyote anayemshurutisha? La. Ufunuo huu wote, yeye anautoa kwa hiari yake mwenyewe. Hii ni asili ovu ya Shetani. Licha ya kile Mungu anafanya na jinsi Anavyokifanya, Shetani yuko nyuma Yake. Kiini na sura ya ukweli ya vitu hivi ambavyo Shetani anasema na kufanya ni kiini cha Shetani—kiini ovu, kiini chenye nia mbaya. Sasa, tukiendelea kusoma, Shetani anasema nini kingine? Tuendelee kusoma hapa chini.

Mat 4:5-7 Kisha Ibilisi akamchukua hadi katika mji mtakatifu, na kumweka juu ya kinara cha hekalu, Naye akamwambia, Ikiwa Wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jirushe chini: kwa kuwa imeandikwa, Atawaamuru malaika Wake wakuchunge: na watakubeba mikononi mwao, usije ukaukwaa mguu wako kwenye jiwe wakati wowote. Yesu akamwambia, Imeandikwa tena, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

Hebu kwanza tuone maneno ambayo Shetani alizungumza hapa. Shetani alisema “Ikiwa Wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jirushe chini,” na kisha akadondoa kutoka kwenye maandiko, “Atawaamuru malaika Wake wakuchunge: na watakubeba mikononi mwao, usije ukaukwaa mguu wako kwenye jiwe wakati wowote.” Unahisi vipi unaposikia maneno ya Shetani? Si ni ya kitoto sana? Ni ya kitoto, upuuzi na kuchukiza. Mbona Nasema hivi? Daima Shetani hufanya kitu kijinga, anaamini kwamba ni mwerevu sana; na mara nyingi hutaja maandiko—hata neno la Mungu—anajaribu kuyabadili maneno haya dhidi ya Mungu kumshambulia na kumjaribu. Lengo lake la kufanya hivi ni kuharibu mpango wa kazi ya Mungu. Je, unaweza kuona chochote katika maneno haya yaliyonenwa na Shetani? (Shetani huwa na nia mbaya) Katika kila ambacho Shetani hufanya, kila mara yeye hutafuta kuwajaribu binadamu. Shetani hazungumzi kwa njia inayoeleweka kirahisi, bali kwa njia isiyo wazi akitumia majaribu, ulaghai na ushawishi. Shetani anachukulia kumjaribu kwake Mungu kana kwamba Yeye alikuwa binadamu wa kawaida, akiamini kwamba Mungu pia ni asiyejua, mjinga, na asiyeweza kutofautisha kwa wazi vitu vilivyo. Shetani anafikiri kwamba Mungu na pia mwanadamu hawataona hadi kwa kiini chake na kwamba Mungu na mwanadamu wote hawataona udanganyifu wake na nia zake mbaya. Si hapa ndipo Shetani anapata ujinga wake? Zaidi, Shetani anataja maandiko wazi; anafikiria kwamba kufanya hivyo kunamfanya kuaminika, na kwamba hutaweza kuona dosari zozote kwa haya ama kuepuka kudanganywa na haya. Si hapa ndipo Shetani anakuwa mjinga na kama mtoto? Hii ni kama wakati watu wengine wanaeneza injili na kuwa na ushuhuda kwa Mungu, si wasioamini watasema kitu kama alichosema Shetani? Mmesikia watu wakisema kitu kama hiki? Ni jinsi gani unahisi kuchukizwa unaposikia vitu kama hivyo? Je, unahisi kuchukizwa? (Ndiyo.) Unapohisi kuchukizwa, pia unahisi kutiwa kinyaa na kukirihishwa? Unapokuwa na hisia hizi unaweza kutambua kwamba Shetani na tabia potovu ambayo Shetani anamfanyia mwanadamu ni ovu? Katika mioyo yenu mmewahi kuwa na utambuzi kama, “Maneno ya Shetani yanaleta mashambulizi na majaribu, maneno yake ni ya kijinga, ya kuchekesha, ya kitoto, na ya kuchukiza. Hata hivyo, katika matamshi ya Mungu na vitendo vya Mungu, Hangetumia mbinu kama hizi kuzungumza ama kufanya kazi Yake, na Hajawahi kufanya hivyo”? Bila shaka, katika hali hii watu wana tu kiasi kidogo cha kuhisi kuendelea na hawana utambuzi wa utakatifu wa Mungu, sivyo? Na kimo chenu cha sasa, mnahisi tu hivi: “Kila kitu Mungu anasema ni ukweli, ni cha manufaa kwetu, na lazima tukikubali”; bila kujali iwapo unaweza kukubali hili au la, bila ubaguzi unasema kwamba maneno ya Mungu ni ukweli na kwamba Mungu ni ukweli, lakini hujui kwamba ukweli ni utakatifu wenyewe na kwamba Mungu ni mtakatifu.

Hivyo, jibu la Yesu kwa maneno haya ya Shetani lilikuwa lipi? Yesu alimwambia: “Imeandikwa tena, Usimjaribu Bwana Mungu wako.” Kuna ukweli katika maneno haya ambayo Yesu alisema? Bila shaka, kuna ukweli ndani yake. Juujuu inaonekana maneno haya ni amri ya watu kufuata, ni kirai rahisi, lakini hata hivyo, mwanadamu na Shetani wamekiuka maneno haya mara nyingi. Hivyo, Bwana alimwambia Shetani, “Usimjaribu Bwana Mungu wako,” kwa sababu hiki ndicho kile Shetani alifanya mara nyingi na alifanya kila juhudi kufanya hivyo, unaweza hata kusema kwamba Shetani alifanya hivyo bila haya. Ni asili ya msingi ya Shetani kutomcha Mungu na kutomheshimu Mungu kwa moyo wake. Hata wakati Shetani alikuwa kando ya Mungu na angeweza kumwona, Shetani hakuweza kuacha kumjaribu Mungu. Kwa hivyo, Bwana Yesu alimwambia Shetani, “Usimjaribu Bwana Mungu wako.” Hiki ni kirai ambacho Mungu amemwambia Shetani mara nyingi. Si kutumia kirai hiki kunafaa hata leo? (Ndiyo, kwani pia sisi humjaribu Mungu mara nyingi.) Kwa nini watu hufanya hivyo mara nyingi? Je, ni kwa sababu watu wamejawa na tabia potovu ya kishetani? (Ndiyo.) Kwa hivyo kile ambacho Shetani alisema hapa juu ni kitu ambacho watu husema mara nyingi? Na katika hali gani? Mtu anaweza kusema kwamba watu wamekuwa wakisema mambo kama haya licha ya wakati na mahali. Hii inadhihirisha kwamba tabia ya watu ni sawa kabisa na tabia potovu ya Shetani. Bwana Yesu alisema maneno rahisi, ambayo yanawakilisha ukweli na ambayo watu wanahitaji. Hata hivyo, katika hali hii Bwana Yesu alikuwa akibishana na Shetani? Je, kulikuwa na jambo lolote la kupingana katika kile Alichomwambie Shetani? (La.) Bwana Yesu aliyachukulia vipi majaribu ya Shetani kwa moyo Wake? Je, Alihisi kuchukizwa na kutiwa kinyaa? Bwana Yesu alihisi kutiwa kinyaa na kuchukizwa lakini Hakugombana na Shetani, wala hata chini zaidi Hakuzungumza kuhusu kanuni zozote kubwa. Kwa nini hivyo? (Kwa sababu Shetani daima yuko hivyo, hawezi kubadilika.) Tunaweza kusema kwamba Shetani hana akili? (Ndiyo, tunaweza.) Je, Shetani anaweza kutambua kwamba Mungu ni ukweli? Shetani hatawahi kutambua kwamba Mungu ni ukweli na hatawahi kukubali kwamba Mungu ni ukweli; hii ni asili yake. Zaidi, kuna kitu kingine kuhusu asili ya Shetani kinachotia kinyaa, ni nini? Katika majaribio yake ya kumjaribu Bwana Yesu, Shetani alifikiri kwamba, hata kama alimjaribu Mungu na hangefaulu, bado angejaribu jambo hili tu. Hata kama angeadhibiwa, angeifanya tu. Hata kama hangepata chochote chema kutoka kwa kufanya hivyo, angeifanya tu, na kuendelea na kusimama dhidi ya Mungu hadi mwisho kabisa. Hii ni asili ya aina gani? Si huo ni uovu? Yule anayekasirika sana wakati Mungu anatajwa, yule anayekuwa na hasira wakati Mungu anatajwa, je, amemwona Mungu? Je, anamjua Mungu? Hajui Mungu ni nani, hamwamini, na Mungu hajaongea naye. Mungu hajawahi kumsumbua, kwa hivyo kwa nini awe na hasira? Tunaweza kusema kwamba mtu huyu ni mwovu? Mitindo ya kidunia, kula, kunywa, na kutafuta raha, na kufuata watu mashuhuri—hakuna chochote kati ya vitu hivi kitakachomsumbua mwanadamu kama huyo. Hata hivyo, “Mungu” akitajwa tu au ukweli wa maneno ya Mungu, yeye anashikwa na hasira ghafla. Je, si huku kunajumuisha kuwa na asili ya uovu? Hili linatosha kuthibitisha kwamba hii ni asili ya uovu ya mwanadamu. Sasa, mkijizungumzia, kuna wakati ambapo ukweli unatajwa, ama wakati majaribio ya Mungu kwa mwanadamu yanatajwa ama wakati maneno ya Mungu ya hukumu dhidi ya mwanadamu yanatajwa, na mnahisi kusumbuliwa, kutiwa kinyaa, na hamtaki kusikia kuyahusu? Mioyo yenu inaweza kufikiri: Si watu wote walisema kwamba Mungu ni ukweli? Baadhi ya maneno haya si ukweli, haya bila shaka ni maneno tu ya Mungu ya maonyo kwa mwanadamu! Watu wengine hata wanaweza kuhisi kuchukizwa mioyoni mwao: Haya yanatajwa kila siku, majaribio Yake kwetu daima yanatajwa kama hukumu Yake; haya yote yataisha lini? Tutapokea lini hatima njema? Haijulikani hasira hii isiyo na sababu inatoka wapi. Hii ni asili ya aina gani? (Asili ovu.) Inasababishwa na asili ovu ya Shetani. Na kwa Mungu kuhusu asili ovu ya Shetani na tabia potovu ya mwanadamu, Hagombani kamwe wala kubishana na watu, na kamwe Halalamiki wakati watu wanatenda kutokana na ujinga. Hamtamwona Mungu akiwa na mitazamo sawa kuhusu vitu ambavyo watu wanavyo, na zaidi hamtamwona Akitumia maoni ya wanadamu, maarifa yao, sayansi yao ama filosofia yao ama fikira za mwanadamu kushughulikia vitu, Badala yake, kila kitu anachofanya Mungu na kila kitu Anachofichua kinahusiana na ukweli. Yaani, kila neno Alilolisema na kila hatua Aliyoichukua inahusiana na ukweli. Ukweli huu sio tu ndoto isiyo na msingi; ukweli huu na maneno haya yanaelezwa na Mungu kwa sababu ya kiini cha Mungu na uhai Wake. Kwa sababu maneno haya na kiini cha kila kitu ambacho Mungu amefanya ni ukweli, tunaweza kusema kwamba kiini cha Mungu ni kitakatifu. Kwa maneno mengine, kila kitu ambacho Mungu anasema na kufanya kinaleta uzima na mwangaza kwa watu, kinawaruhusu watu kuona vitu vizuri na uhalisi wa vitu hivyo vizuri, na inaelekeza njia kwa ajili ya wanadamu ili waweze kutembea katika njia sahihi. Vitu hivi vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha Mungu na vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha utakatifu Wake. Mmekiona, siyo? Tutaendelea kuyasoma maandiko.

Mat 4:8-11 Tena, Ibilisi akampeleka hadi kwenye mlima mrefu sana, na kumwonyesha falme zote za dunia, na fahari yao; Na akamwambia, Hivi vyote nitakupa Wewe, Ukianguka chini na kuniabudu. Kisha Yesu akamwambia, Ondoka uende zako, Shetani; kwa kuwa imeandikwa, Muabudu Bwana Mungu wako, na ni Yeye peke Yake ndiye utakayemtumikia. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.

Shetani, ibilisi, baada ya kushindwa katika hila zake mbili za awali, alijaribu nyingine tena: Alionyesha falme zote duniani na utukufu wa falme hizi kwa Bwana Yesu na kumwambia amwabudu ibilisi. Unaona nini kuhusu sura za ukweli za ibilisi kutoka kwa hali hii? Si Shetani ibilisi hana haya kabisa? (Ndiyo.) Anaweza kukosa haya namna gani? Kila kitu kiliumbwa na Mungu, lakini Shetani anakigeuza na kumwonyesha Mungu akisema, “Angalia utajiri na utukufu wa falme hizi zote. Hivi vyote nitakupa, ukianguka chini na kuniabudu.” Je, si hili ni mabadiliko ya jukumu? Si Shetani hana haya? Mungu aliumba kila kitu, lakini, je, ilikuwa ni kwa ajili ya kufurahia Kwake? Mungu alimpa mwanadamu kila kitu, lakini Shetani alitaka kunyakua vyote na baadaye akasema, “Niabudu! Niabudu na nitakupa Wewe haya yote.” Huu ni uso usiopendeza wa Shetani; hana haya kabisa! Shetani hata hajui maana ya neno “haya,” na huu ni mfano mwingine tu wa uovu wake. Hata hajui haya ni nini. Shetani anajua vyema kwamba Mungu aliumba kila kitu na kwamba Anavisimamia na Anavitawala. Kila kitu ni cha Mungu, si cha mwanadamu, sembuse Shetani, lakini Shetani ibilisi bila haya alisema kwamba angempa Mungu kila kitu. Si tena Shetani anafanya kitu cha ujinga na kisicho na aibu? Mungu anamchukia Shetani hata zaidi sasa, sivyo? Lakini licha ya kile Shetani alijaribu kufanya, Bwana Yesu alikiamini? Bwana Yesu alisema nini? (“Muabudu Bwana Mungu wako na umtumikie Yeye pekee.”) Je, kirai hiki kina maana ya utendaji? (Ndiyo.) Maana gani ya utendaji? Tunaona uovu na kutokuwa na aibu kwa Shetani katika matamshi yake. Kwa hivyo iwapo mwanadamu angemwabudu Shetani, hitimisho lingekuwa nini? Angepokea utajiri na utukufu wa falme zote? (La.) Angepokea nini? Je, wanadamu wangekuwa wasio na haya na wa kuchekwa kama tu Shetani? (Ndiyo.) Watakuwa hawana tofauti kabisa na Shetani. Kwa hivyo, Bwana Yesu alisema maneno haya ambayo ni muhimu kwa kila mwanadamu: “Muabudu Bwana Mungu wako, na ni Yeye peke Yake ndiye utakayemtumikia,” hii ina maana kwamba isipokuwa Bwana, isipokuwa Mungu Mwenyewe, ukimhudumia mwingine, ukimwabudu Shetani ibilisi, basi utagaagaa katika uchafu sawa na Shetani. Kisha utashiriki kutokuwa na haya na uovu wa Shetani, na kama tu Shetani ungemjaribu Mungu na kumshambulia Mungu. Na basi mwisho wako ungekuwa upi? Ungechukiwa na Mungu, kuangushwa na Mungu na kuangamizwa na Mungu. Baada ya Shetani kumjaribu Bwana Mungu mara kadhaa bila mafanikio, alijaribu tena? Shetani hakujaribu tena na kisha akaondoka. Hii inathibitisha nini? Inathibitisha kwamba asili ovu ya Shetani, kuonea kijicho kwake, na ujinga na upuuzi wake vyote havistahili kutajwa mbele ya Mungu. Bwana Yesu alimshinda Shetani kwa sentensi tatu tu, na baadaye akatoroka na mkia wake katikati ya miguu yake, akiaibika sana asiweze kuonyesha uso wake tena, na hakumjaribu Bwana Yesu tena. Kwa sababu Bwana Yesu alikuwa amelishinda jaribio hili la Shetani, Angeweza kuendelea kwa urahisi kazi ambayo Alipaswa kufanya na kuanza kazi zilizokuwa mbele Yake. Je, yote aliyoyasema Bwana Yesu na kufanya katika hali hii yanabeba maana fulani ya vitendo kwa kila mtu yakitumika sasa? (Ndiyo.) Ni aina gani ya utendaji? Je, kumshinda Shetani ni kitu rahisi kufanya? Je, ni lazima watu wawe na uelewa wazi wa asili ovu ya Shetani? Je, ni lazima watu wawe na uelewa sahihi wa vishawishi vya Shetani? (Ndiyo.) Unapopitia vishawishi vya Shetani katika maisha yako, na iwapo unaweza kuona hadi kwa asili ovu ya Shetani, utaweza kumshinda? Iwapo unajua kuhusu ujinga na upuuzi wa Shetani, bado unaweza kusimama kando ya Shetani na kumshambulia Mungu? Ikiwa unaelewa jinsi kuwa na kijicho na kutokuwa na aibu kwa Shetani vinafichuliwa kupitia kwako—iwapo unatambua wazi na kujua mambo haya—bado ungemshambulia na kumjaribu Mungu kwa njia hii? (La, hatungeweza.) Utafanya nini? (Tutaasi dhidi ya Shetani na kumwacha.) Hili ni jambo rahisi kufanya? Hili si rahisi, kufanya hivi, watu wanalazimika kuomba mara nyingi, ni lazima wajiweke mbele ya Mungu na wajichunguze. Na lazima waache kufundisha nidhamu kwa Mungu na hukumu Yake na kuadibu Kwake viwajie. Ni kwa njia hii tu ndiyo watu wataweza kujinasua polepole kutoka kwa udanganyifu na udhibiti wa Shetani.

Tunaweza kuweka pamoja mambo yanayojumuisha kiini cha Shetani kutoka kwa mambo haya ambayo amesema. Kwanza, kiini cha Shetani kwa ujumla kinaweza kusemwa kuwa ni kiovu, ambacho ni kinyume na utakatifu wa Mungu. Kwa nini Nasema kiini cha Shetani ni kiovu? Mtu anapaswa kuangalia matokeo ya kile Shetani anafanyia watu ili kuona haya. Shetani anampotosha na kumdhibiti mwanadamu, na mwanadamu anatenda chini ya tabia potovu ya Shetani, na anaishi katika dunia ya watu waliopotoshwa na Shetani. Binadamu wanamilikiwa na kusimilishwa na Shetani bila kujua; mwanadamu hivyo ana tabia potovu ya Shetani, ambayo ni asili ya Shetani. Kutoka kwa yote Shetani amesema na kufanya, umeona kiburi chake? Umeona udanganyifu na ubaya wake? Kiburi cha Shetani kimsingi kinaonekana vipi? Je, Shetani daima anataka kuchukua nafasi ya Mungu? Shetani daima anataka kuharibu kazi ya Mungu na nafasi ya Mungu na kujichukulia kuwa yake ili watu wamuunge mkono na kumwabudu Shetani; hii ni asili ya kiburi ya Shetani. Wakati Shetani anawapotosha watu, je, anawaambia moja kwa moja kile wanachopaswa kufanya? Wakati Shetani anamjaribu Mungu, je, anajitokeza na kusema, “Nakujaribu, nitakushambulia”? Hakika hafanyi hivyo. Ni mbinu gani hivyo Shetani anatumia? Anashawishi, anajaribu, anashambulia, na anaweka mitego yake, na hata kwa kutaja maandiko, Shetani anazungumza na kutenda kwa njia mbalimbali ili kutimiza dhamira na nia zake mbaya. Baada ya Shetani kufanya hivi, ni nini kinachoweza kuonekana kutoka kile kilichojitokeza kwa mwanadamu? Je, si watu wana kiburi? Mwanadamu ameteseka kutoka kwa upotovu wa Shetani kwa maelfu ya miaka na hivyo mwanadamu amekuwa mwenye kiburi, mdanganyifu, mwenye kijicho, na asiyefikiri. Haya mambo yote yameletwa kutokana na asili ya Shetani. Kwa sababu asili ya Shetani ni ovu, amempa mwanadamu asili hii ovu na kumletea mwanadamu tabia hii potovu. Kwa hivyo, mwanadamu anaishi chini ya tabia potovu ya kishetani na, kama Shetani, mwanadamu anaenda kinyume na Mungu, anamshambulia Mungu, na kumjaribu Yeye hadi kwa kiwango ambacho mwanadamu hamwabudu Mungu na hamheshimu katika moyo wake.

Njia Tano Ambazo Shetani Humptosha Mwanadamu

Kuhusu utakatifu wa Mungu, hata kama inaweza kuwa mada inayojulikana, ni mada ambayo, inapozungumziwa, inaweza kuwa dhahania kiasi kwa watu wengine na inaweza kuwa ya kina na isiyofikiwa. Lakini hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Nitawasaidia kuelewa maana ya utakatifu wa Mungu. Ili kumwelewa mtu fulani ni mtu wa aina gani, angalia kile anachofanya na matokeo ya vitendo vyake, na kisha utaweza kuona kiini cha mtu huyo. Inaweza kusemwa hivyo? (Ndiyo.) Basi, hebu tushiriki kuhusu utakatifu wa Mungu kutoka kwa mtazamo huu kwanza. Kwa maneno mengine kiini cha Shetani ni kiovu, na kwa hivyo vitendo vya Shetani kwa mwanadamu vimekuwa kumpotosha bila kikomo. Shetani ni mwovu, kwa hivyo watu ambao amewapotosha hakika ni waovu, siyo? Kuna yeyote anayeweza kusema, “Shetani ni mwovu, pengine mtu ambaye amempotosha ni mtakatifu”? Ni mzaha, sivyo? Je, hata inawezekana? (La.) Shetani ni mwovu, na ndani ya uovu wake kuna upande muhimu na pia wa vitendo. Haya si mazungumzo matupu tu. Hatujaribu kusema uwongo juu ya Shetani; tunashiriki tu kuhusu ukweli na uhalisi. Hii inaweza kuumiza watu wengine ama sehemu fulani ya watu, lakini hakuna nia mbaya hapa; pengine mtasikia haya leo na kuhisi kutostareheka kiasi, lakini siku fulani hivi punde, wakati mnaweza kumtambua, mtajichukia, na mtahisi kwamba kile tulichozungumzia leo ni cha manufaa kwenu na chenye thamani. Kiini cha Shetani ni kiovu, kwa hivyo matokeo ya vitendo vya Shetani bila shaka ni maovu, ama kwa kiwango cha chini kabisa, yanahusiana na uovu wake, je, tunaweza kusema hayo? (Ndiyo.) Kwa hivyo, je Shetani anampotosha mwanadamu vipi? Kuhusu uovu anaoufanya Shetani duniani na miongoni mwa binadamu, ni vitu vipi ambavyo vinaonekana na kuhisiwa na watu? Je, mmewahi kuyafikiria haya awali? Pengine hamkuyafikiria sana, kwa hivyo wacha Nitaje hoja kadhaa muhimu. Kila mtu anajua kuhusu nadharia ya mageuko ambayo Shetani anapendekeza, siyo? Je, si hii ni sehemu ya maarifa yanayosomwa na mwanadamu? (Ndiyo.) Hivyo, Shetani kwanza anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu, na huwafunza maarifa na mbinu zake mwenyewe. Kisha anatumia sayansi kuwapotosha wanadamu, akiamsha mvuto wao kwa maarifa, sayansi, na vitu vya ajabu, ama kwa vitu ambavyo watu wanataka kuchunguza. Vitu vifuatavyo vinavyotumiwa na Shetani kumpotosha mwanadamu ni desturi ya kitamaduni na ushirikina, na baada ya vitu hivyo, anatumia mienendo ya kijamii. Hivi vyote ni vitu ambavyo watu wanapatana navyo katika maisha yao ya kila siku na hivi vyote vinahusiana na vitu vilivyo karibu na watu, vitu wanavyoona, wanavyosikia, wanavyogusa na wanavyopitia. Mtu anaweza kusema kwamba vinamzunguka kila mtu, haviwezi kutorokwa na kuepukika. Wanadamu hawana njia ya kuepuka kuathiriwa, kuambukizwa, kudhibitiwa, na kufungwa na vitu hivi; hawana nguvu za kuvisukumia mbali.

a. Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Maarifa Kumpotosha Mwanadamu

Kwanza tutazungumza kuhusu maarifa. Je, si kila mtu angechukulia maarifa kuwa kitu chema? Ama kwa kiwango cha chini kabisa, watu wanafikiri kwamba kidokezo cha neno “maarifa” ni chema badala ya hasi. Kwa hivyo mbona tunataja hapa kwamba Shetani anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu? Je, nadharia ya mageuko ni kipengele cha maarifa? Je, sheria za kisayansi za Newton ni sehemu ya maarifa? Je, nguvu ya mvutano wa dunia ni sehemu ya maarifa, sivyo? (Ndiyo.) Hivyo mbona maarifa yametajwa miongoni mwa maudhui anayoyatumia Shetani kumpotosha mwanadamu? Maoni yenu hapa ni yapi? Je, maarifa yana hata chembe cha ukweli ndani yake? (La.) Kwa hivyo ni nini kiini cha maarifa? Je, maarifa ambayo mwanadamu anajifunza yanategemea msingi upi? Je, yanategemea nadharia ya mageuko? Je, maarifa ambayo mwanadamu ameyapata kupitia uchunguzi na majumuisho yana msingi wa kumkana Mungu? Je, kuna sehemu yoyote ya maarifa haya ambayo yana uhusiano na Mungu? Je, yanahusiana na kumwabudu Mungu? Yanahusiana na ukweli? (La.) Hivyo Shetani anatumiaje maarifa kumpotosha mwanadamu? Nimetoka tu kusema kwamba hakuna sehemu yoyote ya maarifa haya inayohusiana na kumwabudu Mungu ama na ukweli. Watu wengine wanayafikiria hivi: “Yanaweza kutokuwa na chochote kuhusiana na ukweli, lakini hayawapotoshi watu.” Mnafikiri nini kuhusu haya? Je, ulifundishwa na maarifa kwamba furaha ya watu ilitegemea kile walichokitengeneza kwa mikono yao wenyewe? Je, maarifa yaliwahi kukufunza kwamba hatima ya mwanadamu ilikuwa mikononi mwake? (Ndiyo.) Haya ni mazungumzo ya aina gani? (Ni mazungumzo ya kishetani.) Bila shaka! Ni mazungumzo ya kishetani! Maarifa ni mada tata sana kuijadili. Unaweza kuiweka kwa urahisi kwamba eneo la maarifa ni maarifa tu. Hili ni eneo la maarifa linalofunzwa kwa msingi wa kutomwabudu Mungu na kutokuwa na uelewa kwamba Mungu aliumba mambo yote. Watu wanaposoma aina hii ya maarifa, hawaoni Mungu anatawala mambo yote, hawaoni Mungu anaongoza ama anasimamia mambo yote. Badala yake, wanayofanya tu ni kutafiti na kuchunguza, bila kikomo kwa sehemu hiyo ya maarifa, na kutafuta majibu kwa msingi wa maarifa. Hata hivyo, iwapo watu hawamwamini Mungu na badala yake wanatafiti tu, kamwe hawatapata majibu ya kweli, siyo? Maarifa yanakupa tu riziki, yanakupa tu kazi, yanakupa tu mapato ili usiwe na njaa, lakini kamwe hayawezi kukufanya umwabudu Mungu, na hayatakuweka mbali na maovu. Kadiri watu wanavyosoma maarifa, ndivyo watakavyotamani zaidi kuasi dhidi ya Mungu, kumchunguza Mungu zaidi, kumjaribu Mungu, na kwenda kinyume na Mungu. Hivyo sasa, tunaona yapi ambayo maarifa yanawafunza watu? Yote ni falsafa ya Shetani. Je, falsafa na kanuni za kuishi zinazosambazwa na shetani miongoni mwa wanadamu wapotovu zina uhusiano wowote na ukweli? Hazina uhusiano wowote na ukweli na, kwa kweli, ni kinyume cha ukweli. Watu mara nyingi husema, “Maisha ni mwendo” na “Mwanadamu ni chuma, mchele ni chuma, mwanadamu huhisi anataabika kwa njaa asipokula mlo”; misemo hii ni nini? Ni uwongo, na kuisikia kunasababisha hisia ya kuchukiza. Pengine kila mtu anajua kuhusu jinsi Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu. Kwa yanayoitwa maarifa ya mwanadamu, Shetani amejaza kidogo falsafa yake ya kuishi na kufikiria kwake. Na wakati Shetani anafanya haya, Shetani anamruhusu mwanadamu kutumia kufikiria kwake, filosofia, na mtazamo wake ili mwanadamu aweze kukana uwepo wa Mungu, kukana utawala wa Mungu juu ya mambo yote na utawala juu ya hatima ya mwanadamu. Kwa hivyo, masomo ya mwanadamu yanapoendelea, na anapata maarifa zaidi, anahisi uwepo wa Mungu kuwa usio yakini, na anaweza hata kuhisi kwamba Mungu hayupo. Kwa sababu Shetani ameingiza mawazo, mitazamo na dhana fulani ndani ya mwanadamu, mara tu Shetani anapoingiza sumu hii ndani ya mwanadamu, je, si mwanadamu amehadaiwa na kupotoshwa na Shetani? Kwa hivyo mnaweza kusema watu wa siku hizi wanaishi kwa kufuata nini? Je, hawaishi kwa kufuata maarifa na mawazo yaliyoingizwa na Shetani? Na mambo yaliyofichwa ndani ya maarifa na mawazo haya—je, si hayo falsafa na sumu ya Shetani? Mwanadamu huishi kwa kufuata falsafa na sumu ya Shetani. Na ni nini kilicho katika msingi wa wanadamu kupotoshwa na Shetani? Shetani anataka kumfanya mwanadamu amkane, kumpinga, na kwenda dhidi ya Mungu jinsi anavyofanya yeye; hili ndilo lengo la Shetani kumpotosha mwanadamu, na pia ndiyo njia ambayo kwayo Shetani humpotosha mwanadamu.

Kwanza tutazungumzia kipengele cha juujuu zaidi cha mada hii. Je, sarufi na maneno katika masomo ya lugha yaliweza kuwapotosha watu? Je, maneno yanaweza kuwapotosha watu? Maneno hayawapotoshi watu; na ni chombo kinachowaruhusu watu kuongea na chombo ambacho watu wanatumia kuwasiliana na Mungu. Zaidi ya hayo, lugha na maneno ni jinsi ambavyo Mungu anawasiliana na watu sasa, ni vyombo, ni vya umuhimu. Moja ongeza moja ni mbili, na mbili zidisha kwa mbili ni nne; haya ni maarifa, siyo? Lakini yanaweza kukupotosha? Hii ni akili ya kawaida na kanuni kwa hivyo haiwezi kupotosha watu. Kwa hivyo ni maarifa gani yanayopotosha watu? Ni maarifa ambayo yamechanganywa mitazamo na fikira za Shetani, Shetani anataka kujaza mitazamo na fikira hizi ndani ya binadamu kupitia maarifa. Kwa mfano, katika insha, hakuna chochote kibaya na maneno yaliyoandikwa, lakini shida inaweza kuwa mitazamo na nia ya mwandishi alipoandika insha hiyo na pia maudhui ya fikira zake. Haya ni mambo ya kiroho—na yanaweza kuwapotosha watu. Kwa mfano, iwapo ungekuwa ukitazama kipindi kwenye runinga, ni mambo yapi ndani yake yangeweza kubadili mtazamo wako? Je, yale yaliyosemwa na wasanii, maneno yenyewe, yangeweza kuwapotosha watu? (La.) Ni mambo yapi ambayo yangeweza kuwapotosha watu? Yangekuwa mawazo ya msingi na yaliyomo katika onyesho, ambayo yangewakilisha maoni ya mwendeshaji, na habari iliyobebwa katika maoni haya inaweza kushawishi mioyo na akili za watu. Siyo? Sasa mnajua Narejelea nini katika mjadala Wangu wa Shetani kutumia maarifa kuwapotosha watu. Hutaelewa visivyo, siyo? Hivyo unaposoma riwaya ama insha tena, unaweza kutathmini iwapo fikira zilizoelezwa katika insha hiyo zinampotosha ama hazimpotoshi mwanadamu ama kuchangia kwa binadamu? (Tunaweza kufanya hivyo kidogo.) Hiki ni kitu ambacho lazima kisomwe na kupitiwa polepole, si kitu kinachoeleweka kwa urahisi mara moja. Kwa mfano, unapotafiti ama kusoma sehemu ya maarifa, baadhi ya vipengele vyema vya maarifa hayo vinaweza kukusaidia kuelewa mambo fulani ya kawaida kuhusu eneo hilo, na kile ambacho watu wanapaswa kuepukana nacho. Chukua mfano wa “umeme,”—huu ni uwanja wa maarifa, siyo? Je, hutakuwa mjinga iwapo hujui kwamba kwamba umeme unaweza kuwatetemesha na kuwaumiza watu? Lakini utakapoelewa sehemu hii ya maarifa, hutakuwa na uzembe kuhusu kugusa kitu cha umeme na utajua jinsi ya kutumia umeme. Haya yote ni mambo mema. Je, sasa unaelewa kile ambacho tumekuwa tukijadili kuhusiana na jinsi maarifa yanavyowapotosha watu? Kuna aina nyingi za maarifa ambazo zinasomwa duniani na lazima mchukue wakati wenu kuzitofautisha wenyewe.

b. Jinsi ambavyo Shetani Hutumia Sayansi Kumpotosha Mwanadamu

Sayansi ni nini? Si sayansi imewekwa kwa hadhi ya juu na kuchukuliwa kuwa muhimu katika akili za karibu kila mtu? Sayansi inapotajwa, si watu wanahisi, “Hiki ni kitu ambacho watu wa kawaida hawawezi kuelewa, hii ni mada ambayo tu watafiti wa kisayansi ama wataalam wanaweza kugusia. Haina uhusiano wowote na sisi watu wa kawaida”? Je, ina uhusiano lakini? (Ndiyo.) Shetani anatumiaje sayansi kuwapotosha watu? Hatutazungumza kuhusu mambo mengine isipokuwa mambo ambayo watu mara nyingi wanapatana nayo katika maisha yao binafsi. Je, umesikia kuhusu vinasaba? Nyote mnalijua neno hili, sivyo? Je, vinasaba viligunduliwa kupitia sayansi? Vinasaba vinamaanisha nini hasa kwa watu? Je, havifanyi watu kuhisi kwamba mwili ni kitu cha ajabu? Wakati watu wanajulishwa kwa mada hii, si kutakuwa na watu—hasa wenye kutaka kujua—ambao watataka kujua zaidi ama kutaka maelezo zaidi? Hawa watu wanaotaka kujua wataweka nguvu zao zote kwenye mada hii na wakati hawana shughuli watatafuta maelezo kwenye vitabu na Intaneti kujifunza maelezo zaidi kuihusu. Sayansi ni nini? Kuongea waziwazi, sayansi ni fikira na nadharia ya vitu ambavyo mwanadamu anataka kujua, vitu visivyojulikana, na ambavyo hawajaambiwa na Mungu; sayansi ni fikira na nadharia za siri ambazo mwanadamu anataka kuchunguza. Wigo wa sayansi ni upi? Unaweza kusema kwamba ni mpana sana; mwanadamu hutafiti na kujifunza kila kitu ambacho anavutiwa nacho. Sayansi inahusiana na kutafiti maelezo na sheria za vitu hivi na kuweka mbele nadharia zenye kukubalika ambazo zinawafanya watu wafikirie: “Wanasayansi hawa ni wakubwa mno! Wanajua mengi na wana maarifa mengi kuelewa mambo haya!” Wanavutiwa sana na watu hao, sivyo? Watu wanaotafiti sayansi, wana mitazamo ya aina gani? Je, hawataki kutafiti ulimwengu, kutafiti mambo ya ajabu katika eneo lao linalowavutia? Je, matokeo ya mwisho wa haya ni nini? Katika baadhi ya sayansi, watu wanafikia mahitimisho yao kwa kubahatisha, na katika nyingine watu wanategemea uzoefu wa kibinadamu kufikia mahitimisho yao. Bado katika nyanja zingine ya sayansi, watu hufikia mahitimisho yao kutokana na uchunguzi wa kihistoria na usuli. Sivyo? Hivyo, sayansi inawafanyia nini watu? Kile sayansi inafanya ni kwamba inawaruhusu tu watu kuona vyombo katika ulimwengu wa maumbile na tu kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu; haimruhusu mwanadamu kuona sheria ambazo Mungu anatumia kutawala mambo yote. Mwanadamu anaonekana kupata majibu kutoka kwa sayansi, lakini majibu hayo yanachanganya na yanaleta tu ridhaa ya muda mfupi, ridhaa ambayo inawekea moyo wa mwanadamu mipaka kwa ulimwengu yakinifu. Mwanadamu anahisi kwamba amepata majibu kutoka kwenye sayansi, kwa hivyo licha ya suala litakaloibuka, yeye anatumia mitazamo yake ya kisayansi kama msingi wa kuthibitisha na kukubali suala hilo. Moyo wa mwanadamu unashawishiwa na sayansi na unamilikiwa nayo kiasi kwamba mwanadamu hana tena hamu ya kumjua Mungu, kumwabudu Mungu, na kuamini kwamba mambo yote yanatoka kwa Mungu na mwanadamu anapaswa kumwangalia kupata majibu. Hii si ukweli? Kadiri ambavyo mtu anaamini sayansi, anakuwa mjinga zaidi, akiamini kwamba kila kitu kina suluhisho la kisayansi, kwamba utafiti unaweza kutatua chochote. Hamtafuti Mungu na haamini kwamba Yupo. Kuna hata baadhi ya waumini wa muda mrefu wa Mungu ambao punde wanapopatwa na tatizo lolote, watatumia kompyuta kuangalia mambo na kutafuta majibu; wanapekua kila aina ya nyenzo, kwa kutumia mitazamo ya kisayansi kujaribu kutatua tatizo. Hawaamini kwamba maneno ya Mungu ni ukweli, hawaamini kwamba maneno ya Mungu yanaweza kutatua matatizo yote ya binadamu, hawaoni matatizo ya binadamu yaliyo mengi kutoka katika mtazamo wa ukweli. Haijalishi ni shida gani wanayokumbana nayo, hawamwombi Mungu kamwe au kutafuta suluhu kwa kutafuta ukweli katika maneno ya Mungu. Katika mambo mengi, wanapendelea kuamini kwamba maarifa yanaweza kutatua tatizo; kwao, sayansi ndiyo jibu kamili. Mungu hayupo kabisa katika mioyo ya watu kama hao. Wao ni wasioamini, na maoni yao kuhusu imani katika Mungu si tofauti na yale ya wasomi na wanasayansi wengi mashuhuri, ambao sikuzote hujaribu kumchunguza Mungu kwa kutumia mbinu za kisayansi. Kwa mfano, kuna wataalam wengi wa kidini walioenda kwenye mlima ambako safina ilisimama, na hivyo walithibitisha kuwepo kwa safina. Lakini katika kuonekana kwa safina hawaoni uwepo wa Mungu. Wanaamini hadithi na historia tu; haya ni matokeo ya utafiti wao wa kisayansi na utafiti wa dunia yakinifu. Ukitafiti vitu yakinifu, viwe maikrobaiolojia, falaki, ama jiografia, hutawahi kupata matokeo yanayoamua kwamba Mungu yupo ama kwamba Ana mamlaka juu ya vitu vyote, Kwa hivyo sayansi humfanyia nini mwanadamu? Si inamweka mbali na Mungu? Si hii inawaruhusu watu kumtafiti Mungu? Je, haimweki mwanadamu mbali na Mungu? Je, haiwasababishi watu wamsome Mungu? Je, haiwafanyi watu kuwa na shaka zaidi kuhusu uwepo wa Mungu na ukuu wake, na hivyo kumkana na kumsaliti Mungu? Haya ndiyo matokeo. Kwa hiyo Shetani anapotumia sayansi kumpotosha mwanadamu, Shetani anajaribu kufikia lengo gani? Anataka kutumia mahitimisho ya kisayansi kuwahadaa watu na kuwafanya wakose hisia, na kutumia majibu yenye utata kushikilia mioyo ya watu ili wasimtafute au kuuamini uwepo wa Mungu. Kwa hivyo hii ndiyo maana Ninasema kwamba sayansi ni mojawapo ya njia ambazo kwazo Shetani hupotosha watu.

c. Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu

Je, kuna mambo mengi yanayochukuliwa kuwa sehemu ya desturi ya kitamaduni? (Ndiyo.) Hii desturi ya kitamaduni inamaanisha nini? Wengine wanasema inapitishwa kutoka kwa mababu, hiki ni kipengele kimoja. Kutoka mwanzo, familia, vikundi vya makabila, na hata jamii ya binadamu imepitisha njia yao ya maisha, ama mila, misemo, na kanuni, ambazo zimeingizwa kwenye fikira za watu. Watu wanayachukulia kuwa yasiyoweza kutengwa na maisha yao. Wanayachukua mambo haya na kuyachukulia kuwa kanuni na maisha ya kuzingatiwa, na hata kamwe hawataki kuyabadilisha ama kuyaacha mambo haya kwa sababu yalipitishwa kutoka kwa mababu. Kuna vipengele vingine vya desturi ya kitamaduni, kama kile kilichopitishwa na Confucius ama Mencius, na mambo waliyofunzwa watu na Utao ama Uconfucius. Je, hili si kweli? Ni vitu gani vinavyojumuishwa katika desturi ya kitamaduni? Je, inajumuisha sikukuu ambazo watu wanasherehekea? Kwa mfano: Tamasha la Majira ya machipuko, Tamasha la Taa, Siku ya Kufagia Kaburi, Tamasha la Mashua ya Joka, pamoja na Tamasha ya Zimwi na Tamasha ya Katikati ya Majira ya Kupukutika kwa Majani. Baadhi za familia hata husherehekea siku ambazo wazee wanahitimu umri fulani, ama wakati watoto wanahitimu umri wa mwezi mmoja au siku mia moja. Na kadhalika. Hizi zote ni sikukuu za kitamaduni. Je, hakuna desturi ya kitamaduni katika sikukuu hizi? Ni nini kiini cha desturi ya kitamaduni? Je, ina uhusiano wowote na kumwabudu Mungu? Je, ina uhusiano wowote na kuwaambia watu kuweka ukweli katika vitendo? Je, kuna sikukuu zozote za watu kumtolea Mungu dhabihu, kwenda kwenye madhabahu ya Mungu na kupokea mafundisho Yake? Kuna sikukuu kama hizi? (La.) Watu hufanya nini katika sikukuu hizi zote? Katika nyakati za sasa zinaonekana kuwa hafla za kula, kunywa, na kujiburudisha. Ni nini chanzo cha desturi ya kitamaduni? Desturi ya kitamaduni imetoka kwa nani? Imetoka kwa Shetani. Katika usuli wa hizi sikukuu za kitamaduni, Shetani anaingiza mambo ndani ya mwanadamu, haya ni mambo gani? Kuhakikisha kwamba watu wanakumbuka mababu zao, je, hili ni mojawapo ya mambo haya? Kwa mfano, wakati wa Tamasha la Kufagia Kaburi watu husafisha makaburi na kutoa sadaka kwa mababu zao, hivyo watu hawatasahau mababu zao. Pia, Shetani anahakikisha kwamba watu wanakumbuka kuwa wazalendo, kama katika Tamasha la Mashua ya Joka. Je, Tamasha la Katikati ya Majira ya Kupukutika kwa Majani? (Kupatana kwa familia.) Ni nini usuli wa kupatana kwa familia? Sababu zake ni nini? Ni kuwasiliana na kuunganika kihisia. Bila shaka, iwapo ni kusherehekea Mkesha wa Mwaka Mpya wa Mwezi ama Tamasha la Taa, kuna njia nyingi za kuelezea sababu za usuli. Haijalishi jinsi mtu anaelezea sababu iliyo nyuma yazo, kila moja ni njia ya Shetani ya kuingiza filosofia yake na kufikiria kwake kwa watu, ili waweze kupotea kutoka kwa Mungu na wasijue kwamba kuna Mungu, na kwamba watoe sadaka ama kwa mababu zao au Shetani, ama kwamba ni udhuru wa kula, kunywa na kujifurahisha kwa ajili ya matamanio ya mwili. Kila moja ya sikukuu hizi inapoadhimishwa, fikira na mitazamo ya Shetani yanapandwa kwa kina ndani ya akili za watu na hata hawajui. Wakati watu wanafikia umri wa kati ama zaidi, fikira na mitazamo hii ya Shetani tayari yamekita mizizi ndani sana ya mioyo yao. Zaidi ya hayo, watu wanafanya juhudi zao kabisa kueneza fikira hizi, ziwe sahihi ama si sahihi, kwa kizazi kifuatacho bila wasiwasi pasipo kuchagua. Sivyo? (Ndiyo.) Ni jinsi gani desturi hii ya kitamaduni na sikukuu hizi zinawapotosha watu? Je, unajua? (Watu wanawekewa mipaka na kufungwa na kanuni za hizi desturi kana kwamba hawana muda ama nguvu kumtafuta Mungu.) Hiki ni kipengele kimoja. Kwa mfano, kila mtu anasherehekea wakati wa Mwaka Mpya wa Mwezi, usingesherehekea, hungehisi huzuni? Je, kuna miiko yoyote ambayo unapaswa kushikilia? Hungehisi, “Sikusherehekea Mwaka Mpya. Siku hii ya Mwaka Mpya wa Mwezi ilikuwa mbaya sana; mwaka huu wote utakuwa mbaya”? Si ungehisi kutokuwa na utulivu na kuogopa kiasi? Kuna hata watu wengine ambao hawajatoa sadaka kwa mababu zao kwa miaka mingi na ghafla wamekuwa na ndoto ambapo mtu aliyekufa anawaomba pesa, watahisi nini ndani yao? “Inahuzunisha kwamba huyu mtu aliyekufa anahitaji pesa ya kutumia! Nitawachomea baadhi ya pesa za makaratasi, na kama sitafanya hivyo hakika haitakuwa sawa. Sisi tunaoishi huenda tukaingia kwenye matatizo ikiwa sitachoma pesa za karatasi, ni nani anayeweza kusema ni lini janga litatokea?” Daima watakuwa na wingu hili dogo la hofu na wasiwasi katika mioyo yao. Ni nani anayewapa wasiwasi? Shetani huleta wasiwasi. Si hii ndiyo njia moja ambayo Shetani anampotosha mwanadamu? Anatumia mbinu na udhuru mbalimbali ili kukudhibiti, kukutishia, kukufunga, hadi kiasi kwamba unachanganyikiwa na kumkubali na kumnyenyekea; hivi ndivyo Shetani anampotosha mwanadamu. Nyakati nyingi ambapo watu ni wanyonge ama hawaelewi vyema hali ilivyo, wanaweza bila kutaka, kufanya kitu kwa njia iliyochanganyikiwa, yaani, wanaanguka chini ya mshiko wa Shetani bila kujua na wanaweza kufanya kitu bila kujua na wasijue wanafanya nini. Hii ni njia ambayo Shetani anampotosha mwanadamu. Hata kuna watu wachache sasa ambao wanasita kuachana na desturi za kitamaduni ambazo zimekita mizizi, ambao hawawezi kuziacha kabisa. Ni hasa wakati ni wanyonge na wasioweza kujizuia ndipo wanataka kusherehekea sikukuu za aina hizi na wanataka kukutana na Shetani na kumridhisha Shetani tena, ili kuifariji mioyo yao. Ni nini usuli wa desturi hizi za kitamaduni? Je, mkono mweusi wa Shetani unavuta nyuzi nyuma ya pazia? Je, asili ovu ya Shetani inatawala na kudhibiti vitu? Je, Shetani anadhibiti hivi vitu vyote? (Ndiyo.) Wakati watu wanaishi katika desturi ya kitamaduni na kusherehekea sikukuu za kitamaduni za aina hizi, tunaweza kusema kwamba haya ni mazingira ambapo wanadanganywa na kupotoshwa na Shetani, na zaidi ya hayo kwamba wana furaha kupumbazwa na kupotoshwa na Shetani? (Ndiyo.) Hiki ni kitu ambacho nyinyi nyote mnakiri, ambacho nyote mnakijua.

d. Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Ushirikina Kumpotosha Mwanadamu

Mnalijua neno “ushirikina,” siyo? Kuna usawa unaopatana kati ya ushirikina na desturi ya kitamaduni, lakini hatutazungumza kuhusu huo leo, badala yake Nitajadili unaokabiliwa mara nyingi: uganga, uaguzi, kuchoma ubani, na kuabudu Buddha. Watu wengine wanafanya uganga, wengine wanaabudu Buddha na kuchoma ubani, ilhali wengine wanabashiriwa ama wanaambiwa bahati zao kwa kumruhusu mtu kusoma vipengele vya nyuso zao. Wangapi kati yenu wameambiwa bahati zao ama wamesomwa uso? Hiki ni kitu ambacho watu wengi wanataka, siyo? (Ndiyo.) Mbona hivyo? Watu wanapata faida ya aina gani kutoka kwa uaguzi na uganga? Wanapata ridhaa ya aina gani kutoka kwa hayo? (Udadisi.) Je, ni udadisi tu? Hiyo si lazima iwe hivyo, jinsi nionavyo Mimi. Lengo la ubashiri na upigaji ramli ni nini? Kwa nini ufanyiwe? Si kwa ajili ya kuona siku za baadaye? Watu wengine wanasomwa nyuso zao ili kutabiri siku za baadaye, wengine wanafanya hivyo ili kuona iwapo watakuwa na bahati nzuri au la. Wengine wanafanya hivyo ili kuona vipi ndoa zao zitakuwa, na bado wengine wanafanya hivyo kuona bahati itakayoletwa na mwaka ulio mbele. Watu wengine wanasomwa nyuso zao kuona matarajio yao na yale ya wana na binti zao yatakuwa vipi, na wanabiashara wengine wanafanya hivyo kuona watatengeneza pesa ngapi ili waweze kupata mwongozo kwa kile wanachopaswa kufanya. Je, ni kuridhisha udadisi tu? Wakati watu wanasomwa nyuso zao ama kufanya vitu vya aina hii, ni kwa faida ya siku zao za binafsi za baadaye na wanaamini kwamba haya yote yanahusiana kwa karibu na hatima zao. Je, kuna yoyote katika mambo haya yaliyo ya manufaa? (La.) Mbona si ya manufaa? Je, si kitu kizuri kujua kidogo kuhusu mambo hayo? Hii inakusaidia kujua wakati shida inaweza kutokea, ili uweze kuiepuka kama ulikuwa unajua kuihusu awali, siyo? Kupigiwa ramli kunaweza kukuruhusu kuongozwa kuhusiana nako, ili mwaka ulio mbele uweze kuwa mzuri na unaweza kuwa tajiri ukifanya biashara. Je, hii ni ya manufaa? Liwe ni la manufaa au la halituhusu, na ushirika wetu leo hautahusisha mada hii. Shetani anatumiaje ushirikina kumpotosha mwanadamu? Watu wote wanataka kujua majaliwa yao, hivyo Shetani anatumia udadisi wao kuwashawishi. Watu wanashiriki katika ubashiri, upigaji ramli na kusoma uso ili kujua kile kitakachowafanyikia katika siku zijazo na ni njia ya aina gani iliyoko mbele yao. Hata hivyo, mwishowe, ni mikononi mwa nani kuna hatima na matarajio ambayo watu wana wasiwasi navyo sana? (Vipo mikononi mwa Mungu.) Vitu hivi vyote vimo katika mikono ya Mungu. Kwa kutumia mbinu hizi, Shetani anataka watu wajue nini? Shetani anataka kutumia kusoma uso na uaguzi ili kuwaambia watu kwamba anajua bahati zao zilizo mbeleni, na Shetani anataka kuwaambia watu kwamba anajua vitu hivi na anavidhibiti. Shetani anataka kutumia fursa hii na kutumia mbinu hizi kudhibiti watu, ili kwamba watu waweke imani yenye upofu ndani yake na kutii kila neno lake. Kwa mfano, ukisomwa uso, mwaguzi akifunga macho yake na kukwambia kila kitu ambacho kimekufanyikia katika miongo michache iliyopita kwa uwazi kamili, ungehisi vipi ndani yako? Ghafla ungehisi, “Yuko sahihi sana! Sijawahi kumwambia yeyote maisha yangu ya nyuma, alijuaje kuyahusu? Nimependezwa sana na huyu mwaguzi!” Haitakuwa vigumu sana kwa Shetani kujua maisha yako ya nyuma, siyo? Mungu amekuongoza hadi leo, na Shetani pia amewapotosha watu wakati huo wote na amekufuata. Kupita kwa miongo kwako si chochote kwa Shetani na si vigumu kwake kujua vitu hivi. Wakati unajua kwamba alichosema Shetani ni sahihi, si unampa moyo wako? Siku zako za baadaye na bahati yako, si unategemea udhibiti wake? Papo hapo, moyo wako utahisi heshima ama ustahi kwake, na kwa watu wengine, nafsi zao pengine tayari zimenyakuliwa naye. Na utamwuliza mwaguzi mara moja: “Napaswa kufanya nini baada ya hapa? Napaswa kuepukana na nini mwaka ujao? Ni vitu gani ambavyo sipaswi kufanya?” Na kisha atasema hupaswi kwenda pale, hupaswi kufanya hili, usivae nguo za rangi fulani, hupaswi kwenda pahali kama hapo na hapo unapaswa kufanya mambo fulani zaidi…. Si utatia vyote anavyosema moyoni mara moja? Ungevikariri haraka kuliko neno la Mungu. Mbona ungevikariri haraka hivyo? Kwa sababu ungetaka kumtegemea Shetani kwa sababu ya bahati njema. Si hapa ndipo anaunyakua moyo wako? Wakati maneno yake yanakuwa ukweli kama alivyotabiri, si ungependa kurejea kwake na kujua ni bahati gani mwaka unaokuja utaleta? (Ndiyo.) Utafanya chochote Shetani anakwambia ufanye na utaepukana na vitu anakwambia uepukane navyo, si unatii vyote anavyosema? Utajipata katika kumbatio lake haraka sana, upotoshwe, na kudhibitiwa naye. Hii inafanyika kwa sababu unaamini anachosema ni ukweli na kwa sababu unaamini kwamba anajua kuhusu maisha yako ya nyuma, maisha yako ya sasa, na vitu ambavyo siku za badaye zitaleta. Hii ni mbinu Shetani anatumia kudhibiti watu. Lakini kwa kweli, ni nani aliye katika udhibiti? Ni Mungu Mwenyewe, si Shetani. Shetani anatumia tu hila zake hapa kudanganya watu wajinga, kuwadanganya watu wanaoona tu ulimwengu yakinifu ili waumini na kumtegemea. Kisha, wataanguka katika mshiko wa Shetani na kutii kila neno lake. Lakini, je, Shetani hupunguza jitihada watu wanapotaka kumwamini na kumfuata Mungu? Shetani hapunguzi jitihada. Katika hali hii, je, Shetaniwatu wanaanguka kweli katika mshiko wa Shetani? (Ndiyo.) Je, tunaweza kusema kwamba tabia ya Shetani hapa haina haya hata kidogo? (Ndiyo.) Kwa nini tuseme hivyo? Hizi ni mbinu za ulaghai na zinadanganya. Shetani hana haya na anawadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti kila kitu chao na kuwadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti hatima zao. Hii inawafanya watu wajinga kuja kumtii kabisa na anawadanganya na sentensi moja ama mbili tu na katika kuchanganyikiwa kwao, watu wanasujudu mbele yake. Hivyo, Shetani anatumia mbinu za aina gani, anasema nini kukufanya umwamini? Kwa mfano, pengine hujamwambia Shetani idadi ya watu katika familia yako, lakini anaweza kusema kuna watu wangapi katika familia yako, na umri wa wazazi wako na watoto wako. Iwapo ulikuwa na tuhuma na shaka zako mwanzoni, hutahisi kwamba anaaminika zaidi kidogo baada ya kusikia hayo? Shetani kisha anaweza kusema jinsi kazi imekuwa ngumu kwako hivi karibuni, kwamba wakubwa wako hawakupi utambuzi unaostahili na daima wanafanya kazi dhidi yako na kadhalika. Baada ya kuyasikia hayo, ungefikiri, “Hiyo ni sahihi kabisa! Mambo yamekuwa hayaendi vizuri kazini.” Hivyo ungemwamini Shetani zaidi kidogo. Kisha angesema kitu kingine kukudanganya, kukufanya umwamini hata zaidi. Kidogo kidogo, utajipata huwezi kupinga ama kuwa na tuhuma kwake tena. Shetani anatumia tu hila chache zisizo na maana, hata ndogo zisizojalisha, kukufadhaisha. Unapofadhaishwa, hutaweza kupata njia zako, hutajua kile cha kufanya, na utaanza kufuata kile Shetani anasema. Hii ni mbinu ya “ah nzuri sana” anayotumia Shetani kumpotosha mwanadamu pahali unapoingia katika mtego wake bila kujua na unashawishiwa naye. Shetani anakwambia mambo machache ambayo watu wanafikiria kuwa mambo mazuri, na kisha anakwambia kile cha kufanya na kile cha kuepuka. Hivi ndivyo unavyodanganywa bila kujua. Punde unapoingia mtegoni mwake, mambo yatakwendea mrama; daima utakuwa ukifikiria kile alichosema Shetani na kile alichokwambia ufanye, na bila kujua utamilikiwa naye. Mbona hivi? Ni kwa sababu wanadamu hawana ukweli na hivyo hawawezi kusimama dhidi ya majaribu na ushawishi wa Shetani. Wanapokabiliwa na uovu, udanganyifu, usaliti, na kijicho cha Shetani, wanadamu ni wajinga sana, ni wachanga na wanyonge, siyo? Si hii ni mojawapo ya njia ambayo Shetani anampotosha mwanadamu? (Ndiyo.) Mwanadamu anadanganywa na kulaghaiwa bila kujua, kidogo kidogo, kupitia mbinu mbalimbali za Shetani, kwa sababu hawana uwezo wa kutofautisha kati ya mema na hasi. Hawana kimo hiki, na uwezo wa kumshinda Shetani.

e. Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Mienendo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu

Mienendo ya kijamii ilianza lini? Je, ni kitu kipya? Mtu anaweza kusema kwamba mienendo ya kijamii ilianza wakati Shetani alipoanza kuwapotosha watu. Mienendo ya kijamii inajumuisha nini? (Mtindo wa mavazi na vipodozi.) Hiki ni kitu ambacho watu mara nyingi wanakutana nacho. Mtindo wa mavazi, mtindo wa kisasa na mienendo, hiki ni kipengele kidogo. Kuna kingine zaidi? Je, misemo maarufu ambayo watu wanapenda kusema inahesabika pia? Je, pia mitindo ya maisha ambayo watu wanataka inahesabika? Je, nyota wa muziki, watu mashuhuri, majarida, na riwaya ambazo watu hupenda zinahesabika? (Ndiyo.) Katika akili zenu, ni kipengele kipi cha mienendo hii kinaweza kumpotosha mwanadamu? Ni mienendo ipi inawavutia sana? Watu wengine husema: “Sisi sote tumefikia umri fulani, tuko katika miaka ya, hamsini, sitini, sabini ama themanini ambapo hatuwezi kufaa katika mienendo hii na haituvutii tena.” Je, hii ni sahihi? Wengine husema: “Hatufuati watu mashuhuri, hicho ni kitu ambacho vijana walio katika umri wa ishirini wanafanya; pia hatuvai nguo za mitindo ya kisasa, hicho ni kitu ambacho watu wanaojali sura wanafanya.” Kwa hivyo ni ipi kati ya hii inaweza kuwapotosha? (Misemo maarufu.) Je, hii misemo maarufu inaweza kuwapotosha watu? Huu ni msemo mmoja, na mnaweza kuona iwapo unawapotosha watu au la, “Pesa inaifanya dunia izunguke”; huu ni mtindo? Ikilinganishwa na mitindo ya mavazi na chakula mliyotaja, sihuu ni mbaya zaidi? “Pesa inaifanya dunia izunguke” ni falsafa ya Shetani, na inaenea miongoni mwa wanadamu wote, katika kila jamii ya binadamu. Mnaweza kusema kwamba ni mwenendo kwa sababu umewekwa ndani ya moyo wa kila mtu. Tangu mwanzo kabisa, watu hawakuukubali msemo huu, lakini kisha waliukubali kimyakimyabila kusema walipokutana na maisha halisi, na wakaanza kuhisi kwamba maneno haya kweli yalikuwa ya kweli. Je, huu si mchakato wa Shetani kumpotosha mwanadamu? Pengine watu hawaelewi msemo huu kwa kiwango sawa, lakini kila mtu ana kiwango tofauti cha tafsiri na utambuzi wa msemo huu kutokana na mambo ambayo yamefanyika karibu nao na uzoefu wao binafsi, siyo? Licha ya kiwango cha uzoefu mtu alionao katika msemo huu, ni nini athari mbaya ambayo inaweza kuwa nayo katika moyo wa mtu? Kitu fulani kinafichuliwa kupitia tabia ya binadamu katika dunia hii, ikiwemo kila mmoja wenu. Kitu hiki ni kipi? Ni kuabudu pesa. Je, ni vigumu kuondoa kitu hiki kutoka kwenye moyo wa mtu? Ni vigumu sana! Inaonekana kwamba upotoshaji wa Shetani kwa mwanadamu ni wa kina sana! Shetani hutumia pesa kuwajaribu watu, na kuwapotosha ili waabudu pesa na kuabudu vitu vya kimwili. Na ibada hii ya pesa inadhihirika vipi ndani ya watu? Je, mnahisi kwamba hamwezi kuishi katika dunia hii bila pesa yoyote, kwamba hata siku moja bila pesa haiwezi kuishika kabisa? Hadhi ya watu inatokana na kiasi cha pesa walizo nazo na pia heshima yao. Migongo ya maskini imekunjwa kwa aibu, ilhali matajiri wanafurahia hadhi zao za juu. Wanatenda kwa njia ya kujigamba na wana majivuno, wakiongea kwa sauti kubwa na kuishi kwa kiburi. Msemo na mwenendo huu unaleta nini kwa watu? Si watu wengi wanaona kupata pesa kunastahili gharama yoyote? Si watu wengi hupoteza utu na uadilifu wao wakitafuta pesa zaidi? Si watu wengi hupoteza fursa ya kufanya wajibu wao na kumfuata Mungu kwa sababu ya pesa? Je, kupoteza nafasi ya kupata ukweli na kuokolewa si ndiyo hasara iliyo kubwa zaidi kwa watu? Si Shetani ni mbaya kutumia mbinu hii na msemo huu kumpotosha mwanadamu kwa kiwango kama hicho? Si hii ni hila yenye kijicho? Unaposonga kutoka kuukataa huu msemo maarufu hadi mwishowe kuukubali kama ukweli, moyo wako unaanguka kabisa chini ya mshiko wa Shetani, na hivyo unakuja kuishi naye bila kujua. Msemo huu umekuathiri kwa kiwango kipi? Unaweza kujua njia ya ukweli, na unaweza kuujua ukweli, lakini huna nguvu ya kuufuatilia. Unaweza kujua kwa hakika kwamba maneno ya Mungu ni ukweli, lakini hauko radhi kulipa gharama au kuteseka ili kupata ukweli. Badala yake, kwako, ni afadhali utoe siku zako za baadaye na kudura yako kwenda kinyume na Mungu hadi mwisho kabisa. Licha ya kile Mungu anasema, licha ya kile Mungu anafanya, licha ya kiasi unachogundua kwamba upendo wa Mungu kwako ni wa kina na mkubwa, bado ungeendelea kwa njia hiyo kwa ukaidi na kulipa gharama ya msemo huu. Yaani, msemo huu tayari umeyadanganya na kuyadhibiti mawazo yako, tayari umeitawala tabia yako, na unaona afadhali utawale majaliwa yako kuliko uweke kando ufuatiliaji wako wa mali. Kwamba watu wanaweza kutenda namna hiyo, kwamba wanaweza kudhibitiwa na kuongozwa na maneno ya Shetani—si hili linamaanisha kwamba wamedanganywa na kupotoshwa na Shetani? Je, falsafa na mawazo ya Shetani, na tabia ya Shetani, havijakita mizizi ndani ya moyo wako? Unapofuatilia mali bila kufikiri na kuacha ufuatiliaji wa ukweli, je, Shetani hajafanikiwa katika lengo lake la kukudanganya wewe? Hii ndiyo hali halisi hasa. Kwa hivyo, je, unaweza kuhisi wakati unapodanganywa na kupotoshwa na Shetani? Huwezi. Kama huwezi kumwona Shetani akiwa amesimama mbele yako, au kuhisi kwamba ni Shetani anayetenda kisirisiri, je, utaweza kuuona uovu wa Shetani? Je, utaweza kujua jinsi Shetani huwapotosha binadamu? Shetani humpotosha mwanadamu wakati wote na pahali pote. Shetani anaifanya isiwezekane kwa mwanadamu kujilinda dhidi ya upotovu huu na anamfanya mwanadamu awe mnyonge kwake. Shetani anakufanya ukubali fikira zake, mitazamo yake na mambo maovu yanayotoka kwake katika hali ambazo hujui na huna utambuzi wa kile kinachokufanyikia. Watu wanakubali kikamilifu vitu hivi na hawavibagui. Wanapenda sana vitu hivi na kuvishikilia kama hazina, wanaviacha vitu hivi viwatawale na kuwachezea; hivi ndivyo wanavyoishi watu chini ya mamlaka ya Shetani, na wanamwabudu Shetani bila kujua, na upotoshaji wa Shetani kwa mwanadamu unazidi kuwa wa kina.

Shetani hutumia mbinu hizi nyingi kumpotosha mwanadamu. Mwanadamu ana maarifa na baadhi ya nadharia za kisayansi, mwanadamu anaishi na ushawishi wa desturi ya kitamaduni, na kila mtu ni mrithi na msambazaji wa desturi ya kitamaduni. Mwanadamu ataendeleza desturi ya kitamaduni aliyopewa kutoka kwa Shetani na pia kutenda pamoja na mienendo ya kijamii ambayo Shetani anawapa wanadamu. Binadamu hawezi kutengana na Shetani, kushiriki na kile ambacho Shetani anafanya wakati wote, kukubali uovu, udanganyifu, kijicho na kiburi chake. Mwanadamu alipomiliki tabia hizi za Shetani, je, amekuwa na furaha ama huzuni kuishi miongoni mwa binadamu hawa wapotovu? (Huzuni.) Mbona unasema hivyo? (Kwa sababu binadamu amefungwa na anadhibitiwa na vitu hivi vipotovu, anaishi dhambini na amegubikwa na mapambano makali.) Watu wengine huvaa miwani, wakionekana kuwa werevu; wanaweza kuzungumza kwa heshima sana, kwa ufasaha na mantiki, na kwa sababu wamepitia vitu vingi sana, wanaweza kuwa wenye uzoefu sana na wastaarabu. Wanaweza kuzungumza kwa undani kuhusu masuala makubwa na madogo; wanaweza pia kutathmini uhalisi na mantiki ya vitu. Wengine wanaweza kuangalia tabia na kuonekana kwa watu hawa, na vile vile tabia, ubinadamu, mwenendo, na kadhalika, na wasione kosa lolote katika haya. Watu kama hao wanaweza hasa kuzoea mitindo ya sasa ya kijamii. Ingawa mtu huyu anaweza kuwa mzee, kamwe hayuko nyuma ya nyakati na kamwe si mzee sana kufunzwa. kijuujuu, hakuna anayeweza kupata dosari kwake, lakini ndani amepotoshwa na Shetani kabisa na kikamilifu. Kijuujuu hakuna chochote kibaya, yeye ni mpole, ni muungwana, anayo maarifa na maadili fulani; ana uadilifu na vitu anavyojua vinalingana na vile wanavyojua vijana. Hata hivyo, kuhusu asili na kiini chake, mtu huyu ni mfano kamili na unaoishi wa Shetani, ana usawa kabisa na Shetani. Hili ni “tunda” la upotovu wa Shetani kwa mwanadamu. Kile Nilichosema kinaweza kuwaumiza, lakini chote ni ukweli. Maarifa ambayo mwanadamu anasoma, sayansi anayoelewa, na mbinu anazochagua kuingiliana na mienendo ya jamii, bila ubaguzi, ni vyombo vya upotovu wa Shetani. Huu ni ukweli kabisa. Kwa hivyo, mwanadamu anaishi miongoni mwa tabia ambayo imepotoshwa kabisa na Shetani na mwanadamu hana njia ya kujua utakatifu wa Mungu ni nini na kiini cha Mungu ni nini. Hii ni kwa sababu kijuujuu mtu hawezi kupata dosari kwa njia ambazo Shetani anampotosha mwanadamu; hakuna anayeweza kuamua kutoka kwa tabia ya mtu kwamba kuna chochote kibaya. Kila mtu anaendelea na kazi yake kwa kawaida na kuishi maisha ya kawaida; wanasoma vitabu na magazeti kwa kawaida, wanasoma na kuzungumza kwa kawaida. Watu wengine wamejifunza maadili machache na ni wazuri katika kuzungumza, ni wenye kuelewa na ni wazuri, ni wenye kusaidia wengine, na hawajihusishi katika ugomvi wa mambo madogo madogo au kuwadhulumu watu wengine. Hata hivyo, tabia yao iliyopotoka ya kishetani imekita mizizi ndani yao; kiini hiki hakiwezi kubadilishwa kwa kutegemea juhudi za nje. Mwanadamu hana uwezo wa kujua utakatifu wa Mungu kwa sababu ya kiini hiki, na licha ya kiini cha utakatifu wa Mungu kuwekwa wazi kwa mwanadamu, mwanadamu hakichukulii kwa umakini. Hii ni kwa sababu Shetani tayari amemiliki kabisa hisia, fikira, mitazamo, na mawazo ya mwanadamu kupitia njia mbalimbali. Huu umiliki na upotovu si wa muda mfupi ama wa hapa na pale; upo kila mahali na kila wakati. Hivyo, watu wengi mno ambao wamemwamini Mungu kwa miaka mitatu au minne au hata miaka sita na saba, bado wanachukulia mawazo, fikira na falsafa hivi za uovu ambazo Shetani aliweka ndani yao kama vitu vya thamani, na hawawezi kuviachilia. Kwa sababu mwanadamu ameukubali uovu, kiburi, na mambo kutoka kwa asili ya kijicho ya Shetani, bila kuepukika kwa mahusiano ya ana kwa ana ya mwanadamu mara nyingi kuna migogoro, mara nyingi kuna magombano na kutokuwa na uwiano, mambo ambayo yameumbwa kwa sababu ya asili ya kiburi ya Shetani. Iwapo Shetani angempa mwanadamu vitu vyema—kwa mfano, iwapo Uconfucius na Utao wa desturi ya kitamaduni ambayo mwanadamu alikubali ilichukuliwa kuwa vitu vizuri—watu wa aina sawa wanapaswa kuweza kupatana na wengine baada ya kukubali vitu hivyo. Hivyo mbona kuna mgawanyiko mkubwa kati ya watu waliokubali vitu sawa? Mbona hivyo? Ni kwa sababu viti hivi vimetoka kwa Shetani na Shetani husababisha mgawanyiko miongoni mwa watu. Vitu ambavyo Shetani hutoa, bila kujali jinsi vinavyoonekana kuwa vya heshima na vikubwa kwa juujuu, vinamletea mwanadamu na vinaleta katika maisha ya mwanadamu kiburi pekee, na si chochote ila udanganyifu wa asili ovu ya Shetani. Sivyo? Mtu ambaye anaweza kuficha uhalisia wake, ambaye anamiliki maarifa mengi ama aliye na malezi mazuri bado angekuwa na wakati mgumu kuficha tabia yake potovu ya kishetani. Hiyo ni kusema, haijalishi mtu huyu atajificha kwa njia ngapi, kama ulimfikiri kuwa mtakatifu, ama kama ulifikiri ni mkamilifu, ama kama ulifikiri ni malaika, haijalishi ulifikiri ni mtu safi vipi, maisha yake yangekuwaje nyuma ya pazia? Utaona asili ipi katika ufunuo wa tabia yake? Bila shaka ungeona asili ovu ya Shetani. Je, mtu anaweza kusema hivyo? (Ndiyo.) Kwa mfano, tuseme mnamjua mtu wa karibu nanyi ambaye mlifikiria kuwa mtu mzuri, ama ulimfikiria kuwa mtu bora, pengine mtu uliyemwabudu kama Mungu. Kwa kimo chako cha sasa, unawafikiria vipi? Kwanza, unaangalia iwapo mtu wa aina hii anao ama hana ubinadamu, iwapo ni mwaminifu, iwapo ana upendo wa kweli kwa watu, iwapo maneno na vitendo vyao vinafaidi na kusaidia wengine. (La.) Huo unaoitwa wema, upendo na uzuri unaofichuliwa hapa, ni nini kweli? Yote ni uongo, yote ni sura ya kinafiki. Hii sura ya kinafiki ya nyuma ya pazia ina madhumuni maovu ya chinichini: Ni ya kumfanya mtu huyo apendwe na kuabudiwa kama Mungu. Je, mnaona jambo hili kwa dhahiri? (Ndiyo.)

Mbinu ambazo Shetani anazitumia ili kuwapotosha watu zinaleta nini kwa wanadamu? Je, kuna chochote kilicho chanya kuzihusu? Kwanza, mwanadamu anaweza kutofautisha kati ya mema na mabaya? Je, unaweza kusema kwamba katika dunia hii, iwe ni mtu mashuhuri au mtu mkubwa, au jarida fulani ama toleo fulani, je, wanatumia viwango sahihi kupima iwapo kitu fulani ni chema ama kiovu, na kizuri ama kibaya? Je, tathmini zao za matukio na watu ni za haki? Kuna ukweli ndani ya tathmini hizi? Je, ulimwengu huu, ubinadamu huu, unatathmini mambo chanya na hasi kulingana na kiwango cha ukweli? (La.) Mbona watu hawana uwezo huo? Watu wamesoma maarifa mengi na wanajua mengi kuhusu sayansi, uwezo wao si mkubwa vya kutosha? Mbona hawawezi kutofautisha kati ya vitu vyema na hasi? Mbona hivi? (Kwa sababu watu hawana ukweli; sayansi na maarifa si ukweli.) Kila kitu ambacho Shetani huletea kwa wanadamu ni uovu na upotovu na hakina ukweli, uhai, na njia. Na uovu na upotovu ambao Shetani anamletea mwanadamu, unaweza kusema kwamba Shetani ana upendo? Unaweza kusema kwamba mwanadamu ana upendo? Watu wengine wanaweza kusema: “Haupo sahihi, kuna watu wengi duniani kote wanaosaidia maskini na watu wasio na makazi. Si hao ni watu wazuri? Pia kuna mashirika ya hisani ambayo hufanya kazi nzuri; je, si kazi yote wanayofanya ni kazi nzuri?” Utasema nini kuhusu hayo? Shetani anatumia mbinu na nadharia mbalimbali kumpotosha mwanadamu; huu upotovu wa mwanadamu ni dhana isiyo dhahiri? La, siyo dhahiri. Shetani pia anafanya vitu vingine vya utendaji, na pia anakuza mtazamo au nadharia katika dunia hii na katika jamii. Katika kila nasaba na katika kila kipindi cha historia, anakuza nadharia na kuingiza baadhi ya fikira ndani ya wanadamu. Fikira na nadharia hizi polepole zinakita mizizi katika mioyo ya watu, na kisha watu wanaanza kuishi kwa nadharia na fikira hizi. Punde wanapoishi kulingana na mambo haya, si wanakuwa Shetani bila kujua? Je, si watu wako kitu kimoja na Shetani? Wakati watu wamekuwa kitu kimoja na Shetani, ni nini mtazamo wao kwa Mungu mwishowe? Si ni mtazamo sawa ambao Shetani anao kwa Mungu? Hakuna anayethubutu kukubali haya, siyo? Ni ya kutisha sana! Mbona Nasema kwamba asili ya Shetani ni ovu? Hii inaamuliwa na kuchambuliwa kulingana na kile Shetani amefanya na vitu ambavyo Shetani amefichua; si bila ustahili kusema kwamba Shetani ni mwovu. Iwapo Ningesema tu kwamba Shetani ni mwovu, mngefikiri nini? Mngefikiri, “Bila shaka Shetani ni mwovu.” Hivyo nitakuuliza: “Ni kipengele kipi cha Shetani ni ovu?” Ukisema: “Shetani kumpinga Mungu ni uovu,” bado hutakuwa ukizungumza kwa uwazi. Sasa tumesema mambo maalum kwa njia hii; je, mna uelewa kuhusu maudhui maalum ya kiini cha uovu wa Shetani? (Ndiyo.) Ikiwa unaweza kuona waziwazi asili ovu ya Shetani, basi utaona hali zako mwenyewe. Je, kuna uhusiano wowote kati ya vitu hivi viwili? Je, hili ni jambo lenye manufaa kwako au la? (Ni lenye manufaa.) Ninaposhiriki kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu, ni muhimu Niwe na ushirika kuhusu kiini kiovu cha Shetani. Maoni yako kuhusu hilo ni yapi? (Ndiyo, ni muhimu.) Kwa nini? (Uovu wa Shetani unauweka mbali utakatifu wa Mungu.) Je, hivyo ndivyo ilivyo? Hii ni sahihi kwa kiasi fulani, ikichukuliwa kwamba bila uovu wa Shetani, watu hawangejua kwamba Mungu ni mtakatifu; ni sahihi kusema hivi. Hata hivyo, ukisema kwamba utakatifu wa Mungu upo tu kwa sababu ya tofauti yake na uovu wa Shetani, hii ni sahihi? Hii namna ya kujua ukweli kwa majadiliano si sahihi. Utakatifu wa Mungu ni kiini cha asili cha Mungu; hata ingawa Mungu anaufichua kupitia matendo Yake, hili bado ni onyesho asili la kiini cha Mungu na ni kiini cha asili cha Mungu; daima kimekuwepo na ni cha kiasili na ya asili kwa Mungu Mwenyewe, ingawa mwanadamu hawezi kukiona. Hii ni kwa sababu mwanadamu anaishi katikati ya tabia potovu ya Shetani na chini ya ushawishi wa Shetani, na hawajui kuhusu utakatifu, sembuse maudhui maalum ya utakatifu wa Mungu. Hivyo, ni muhimu kweli kwamba tushiriki kwanza kuhusu kiini kiovu cha Shetani? (Ndiyo, ni muhimu.) Watu wengine wanaweza kuonyesha baadhi ya shaka kama, “Unashiriki kuhusu Mungu Mwenyewe, mbona Unazungumza daima kuhusu jinsi Shetani anawapotosha watu na jinsi asili ya Shetani ni ovu?” Sasa umeyaweka mapumzikoni mashaka haya, siyo? Wakati watu wana utambuzi wa uovu wa Shetani na wakati wana ufafanuzi sahihi wa uovu, wakati watu wanaweza kuona wazi maudhui maalum na udhihirisho wa uovu, chanzo na kiini cha uovu—wakati utakatifu wa Mungu unajadiliwa sasa—basi watu watautambua kwa uwazi, ama kuufahamu wazi kama utakatifu wa Mungu, kama utakatifu wa kweli. Nisipojadili uovu wa Shetani, watu wengine wataamini kimakosa kwamba kitu fulani ambacho watu wanafanya katika jamii ama miongoni mwa watu—ama kitu fulani katika dunia hii—kinaweza kuhusiana na utakatifu. Si mtazamo huu ni wa kimakosa? (Ndiyo.)

Hivi, Nimeshiriki kuhusu kiini cha Shetani. Mmefikia uelewa upi wa utakatifu wa Mungu kupitia uzoefu wenu wa miaka ya hivi karibuni, kutokana na nyinyi kuona neno la Mungu na kutokana na kupitia kazi Yake? Endelea, na uuzungumzie. Si lazima utumie maneno yanayofurahisha sikio, zungumza tu kutoka kwa uzoefu wako mwenyewe, je, utakatifu wa Mungu ni upendo Wake tu? Ni upendo wa Mungu tu tunaoelezea kama utakatifu? Huo utakuwa wa upande mmoja sana, siyo? Mbali na upendo wa Mungu, kuna vipengele vingine vya kiini cha Mungu? Je, mmeviona? (Ndiyo. Mungu anachukia tamasha na sikukuu, mila, na ushirikina; huu pia ni utakatifu wa Mungu.) Mungu ni mtakatifu kwa hivyo Anachukia vitu, inamaanisha hivyo? Katika mizizi ya hayo, ni nini utakatifu wa Mungu? Utakatifu wa Mungu hauna maudhui makubwa, ni kwamba tu Anachukia vitu? Katika akili zenu mnafikiria, “Kwa sababu Mungu anachukia vitu hivi viovu, hivyo mtu anaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu”? Si huu ni uvumi hapa? Si hii ni aina ya dhana na hukumu? Ni nini mwiko mkubwa zaidi inapokuja kwa kuelewa kiini cha Mungu? (Ni wakati tunaacha ukweli nyuma na kuzungumza kuhusu mafundisho ya kidini.) Huu ndio mwiko mkubwa sana kufanya. Kitu kingine? (Uvumi na ubunifu.) Hizi pia ni miiko mikali sana. Kwa nini uvumi na ubunifu hazifai? Je, mambo ambayo unakisia na kufikiria ni mambo ambayo unaweza kuona kweli? Je, ni kiini halisi cha Mungu? (Hapana.) Ni nini kingine ambacho ni mwiko? Je, ni mwiko kuhesabu tu kifungu cha maneno yanayosikika kuwa mazuri kuelezea kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Si huku ni kujigamba na upuuzi? Hukumu na uvumi ni upuuzi, kama tu kuchukua maneno yanayosikika kuwa mazuri. Sifa tupu pia ni upuuzi, siyo? Je, Mungu anafurahia kusikiliza watu wakisema upuuzi wa aina hii? (La, hafurahii.) Anahisi kutostareheka kusikia huu upuuzi! Mungu anaongoza na kuokoa kundi la watu, na baada ya kundi hili la watu kusikia maneno Yake hawaelewi Anachomaanisha. Mtu anaweza kuuliza: “Mungu ni mwema?” na wangejibu, “Mwema!” “Mwema vipi?” “Mwema sana sana!” “Mungu anampenda mwanadamu?” “Ndiyo!” “Kiasi gani? Unaweza kuuelezea?” “Sana sana zaidi! Ni wa kina zaidi kuliko bahari, wa juu zaidi kuliko anga!” Si huu ni upuuzi? Je, si huu upuuzi ni sawa na kile mlichotoka kusema kuhusu, “Mungu anachukia tabia potovu ya Shetani, hivyo Mungu ni mtakatifu”? (Ndiyo.) Si kile mlichotoka kusema ni upuuzi? Mengi ya haya mambo ya upuuzi yanayosemwa yanatoka wapi? Mambo ya upuuzi yanayosemwa kimsingi yanatoka kwa kutowajibika kwa watu na kutomheshimu Mungu. Tunaweza kusema hayo? Hukuwa na uelewa wowote lakini bado uliongea upuuzi, si huku ni kutowajibika? Si ni kutomheshimu Mungu? Umesoma kiasi kidogo cha maarifa, umeelewa kiasi kidogo cha hoja, na kiasi kidogo cha mantiki, ambayo umetumia na, zaidi, umefanya hivyo ukimjua Mungu. Unafikiri Mungu anahisi kutostareheka kuyasikia hayo? Mnawezaje kumjua Mungu mkitumia mbinu hizi? Je, si hayo yanasikika kuwa ya kufedhehesha? Kwa hivyo, inapokuja kwa maarifa ya Mungu, mtu lazima awe makini sana; mahali unapomjua Mungu, zungumza tu kuhusu hayo. Zungumza kwa uaminifu na kivitendo na usipambe maneno yako na pongezi za kawaida na usitumie sifa isiyostahilika; Mungu haihitaji na kitu kama hiki kinatoka kwa Shetani. Tabia ya Shetani ni ya kiburi na Shetani anapenda kupewa sifa isiyostahilika na kusikia maneno mazuri. Shetani ataridhishwa na kufurahia iwapo watu watataja maneno yote mazuri ambayo wamejifunza na kutumia maneno haya kwa Shetani. Lakini Mungu hahitaji hii; Mungu hahitaji kuvishwa kilemba cha ukoka ama sifa isiyostahilika na Hahitaji kwamba watu wazungumze upuuzi na kumsifu kwa upofu. Mungu anachukizwa sana na hata Hatasikiza sifa ambayo haiko sambamba na ukweli. Hivyo, wakati watu wengine wanamsifu Mungu kwa upofu na kile wanachosema hakilingani na kile kiko katika mioyo yao na wanapofanya viapo kwa upofu na kumwomba ovyo ovyo, Mungu hasikilizi hata kidogo. Lazima uwajibike kwa kile unachosema. Ikiwa hujui jambo, sema tu; ikiwa unajua jambo, onyesha hivyo kwa njia ya kitendo. Hivyo, kuhusiana na utakatifu wa Mungu unajumuisha nini hasa na kwa kweli, je, mna ufahamu wa kweli kuhusu hilo? (Nilipoonyesha uasi, nilipofanya makosa, nilipokea hukumu na kuadibu kwa Mungu, na hapo niliona utakatifu wa Mungu. Na nilipokabiliana na mazingira ambayo hayakukubaliana na matarajio yangu, niliomba kuhusu mambo haya na kutafuta nia za Mungu na Mungu aliponipa nuru na kuniongoza na maneno Yake, niliona utakatifu wa Mungu.) Haya yametoka kwa uzoefu wako mwenyewe. (Kutoka kwa yale ambayo Mungu amezungumza kuyahusu, nimeona kile ambacho mwanadamu amekuwa baada ya kupotoshwa na kudhuriwa na Shetani. Hata hivyo, Mungu ametoa yote kutuokoa na kutokana na haya naona utakatifu wa Mungu.) Hii ni njia ya kivitendo ya kuzungumza; ni maarifa ya kweli. Je, kuna njia zozote tofauti za kuelewa hili? (Naona uovu wa Shetani kutoka kwenye maneno aliyoyasema ili kumlaghai Hawa kutenda dhambi na ushawishi wake kwa Bwana Yesu. Kutoka kwa maneno ambayo kwayo Mungu aliwaambia Adamu na Hawa kile walichoweza na wasichoweza kula, naona kwamba maneno ya Mungu ni wazi na safi na kwamba ni ya kuaminiwa; kutoka kwa haya naona utakatifu wa Mungu.) Kwa kile mmesikia watu hawa wakisema, mnasema Amina zaidi kwa maneno ya nani? Ushirika wa nani ulikuwa karibu zaidi na ushirika wa mada yetu ya leo, ni ya nani ilikuwa ya kweli zaidi? Ushirika wa dada wa mwisho ulikuwa vipi? (Mzuri.) Unasema Amina kwa kile alichosema, ni nini alichosema kilichokuwa sahihi kwenye lengo? (Katika maneno ambayo ndugu alizungumza hivi karibuni, nilisikia kwamba neno la Mungu linaeleweka kwa urahisi na ni wazi sana, si kama maneno ya Shetani yasiyo ya moja kwa moja. Niliona utakatifu wa Mungu kwa haya.) Hii ni sehemu ya hayo. Ilikuwa sahihi? (Ndiyo.) Vizuri sana. Naona kwamba mmepata kitu katika shirika hizi mbili za hivi karibuni, lakini lazima nyinyi mwendelee kufanya kazi kwa bidii. Ni lazima mfanye kazi kwa sababu kuelewa kiini cha Mungu ni somo kubwa sana; si kitu ambacho mtu anaweza kuelewa mara moja ama anaweza kuzungumza wazi kwa maneno machache tu.

Kila kipengele cha tabia potovu ya Kishetani ya watu, maarifa, filosofia, fikira na mitazamo ya watu, na vipengele binafsi vinawazuia pakubwa kujua kiini cha Mungu; hivyo mnapozisikia mada hizi, mada zingine zinaweza kuwa mbali kwenu kufikia, mada zingine pengine hamtaelewa, ilhali mada zingine pengine kimsingi hamtalingana nazo na hali halisi. Licha ya hayo, Nimesikia kuhusu uelewa wenu wa utakatifu wa Mungu na Najua kwamba katika mioyo yenu mmeanza kukubali kile Nilichosema na kushiriki kuhusu utakatifu wa Mungu. Najua kwamba katika mioyo yenu hamu yenu ya kuelewa kiini cha utakatifu wa Mungu imeanza kuchipuka. Lakini ni nini kinachonifanya kuwa na furaha zaidi ni kwamba wengine wenu tayari wanaweza kutumia maneno rahisi sana kuelezea maarifa yenu ya utakatifu wa Mungu. Ingawa hiki ni kitu rahisi kusema na Nimekisema awali, katika mioyo ya wengi wenu hii bado haijakubaliwa ama kuweka alama. Hata hivyo, wengine wenu wameweka maneno haya moyoni na ni vizuri kabisa na huu ni mwanzo mzuri sana. Natumai kwamba kwa mada ambazo mnafikiri kuwa za maana sana—ama kwa mada ambazo ziko mbali kwenu kufikia—mtaendelea kutafakari, na kufanya ushirika zaidi na zaidi. Kwa yale masuala ambayo yako mbali kwenu kufikia kutakuwa na mtu wa kuwapa mwongozo zaidi. Mkishiriki katika ushirika zaidi kuhusu maeneo ambayo mnaweza kufikia sasa, Roho Mtakatifu atafanya kazi Yake na mtakuwa na uelewa mkubwa zaidi. Kuelewa kiini cha Mungu na kujua kiini cha Mungu kuna umuhimu mkubwa zaidi kwa kuingia kwa watu katika maisha. Natumai kwamba hamtapuuza haya ama kuyaona kama mchezo, kwa sababu kumjua Mungu ndio msingi wa imani ya mwanadamu na pia muhimu kwa mwanadamu kufuatilia ukweli na kupata wokovu. Iwapo watu wanamwamini Mungu lakini hawamjui, iwapo wanaishi tu miongoni mwa baadhi ya barua na mafundisho ya kidini, haitawahi kuwezekana wao kufikia wokovu hata kama wanatenda na kuishi kulingana na maana ya juujuu ya ukweli. Hiyo ni kusema, iwapo unamwamini Mungu lakini humjui, basi imani yako ni bure na haina chochote. Unaelewa, sivyo? (Ndiyo, tunaelewa.) Ushirika wetu utaishia hapa kwa leo.

Januari 4, 2014

Iliyotangulia: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Inayofuata: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp