Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Tabia ya Haki ya Mungu

Kwa vile sasa mmesikiliza ushirika uliopita kuhusu mamlaka ya Mungu, Ninao ujasiri kwamba mmejihami vilivyo na mseto wa maneno kuhusu suala hili. Kiwango unachoweza kukubali, kufahamu, na kuelewa vyote hivi vinategemea na jitihada zipi utakazotumia. Ni tumaini Langu kwamba utaweza kutazamia suala hili kwa dhati; kwa vyovyote vile hufai kulishughulikia shingo upande! Sasa, je, kujua mamlaka ya Mungu ni sawa na kujua Mungu kwa uzima wake? Mtu anaweza kusema kwamba kujua mamlaka ya Mungu ndiyo mwanzo wa kumjua Mungu mwenyewe kwa upekee wake, na mtu anaweza kusema pia kwamba kuyajua mamlaka ya Mungu kunamaanisha kwamba mtu tayari ameingia kwenye lango kuu la kujua hali halisi ya ule upekee wa Mungu Mwenyewe. Ufahamu huu ni sehemu moja ya kumjua Mungu. Sehemu ile nyingine ni nini, hivyo basi? Hii ndiyo mada ambayo Ningependa tuweze kushiriki pamoja leo—tabia ya haki ya Mungu.

Nimeteua sehemu mbili kutoka kwenye Biblia ambazo ningependa tushiriki pamoja kuhusu mada ya leo: Jambo la kwanza linahusu kuangamizwa kwa Sodoma na Mungu, ambalo linaweza kupatikana kwenye Mwanzo 19:1-11 na Mwanzo 19:24-25; jambo la pili linahusu ukombozi wa Ninawi na Mungu, ambalo linaweza kupatikana kwenye kitabu cha Yona 1:1-2, kuongezea sura zile za tatu na nne za kitabu hiki. Ninashuku kwamba nyinyi nyote mnasubiri kusikia kile Nilicho nacho kuhusu sehemu hizi mbili. Kile Ninachosema hakiwezi kwenda kando na mada ya kutaka kumjua Mungu Mwenyewe na kujua hali Yake halisi, lakini ni nini kitakachokuwa zingatio la ushirika wa leo? Je, yupo yeyote kati yenu anayejua? Ni sehemu zipi za ushirika Wangu kuhusu “Mamlaka ya Mungu” ziliweza kuwavutia? Kwa nini Nilisema kwamba yule tu anayemiliki mamlaka na nguvu kama hizo ndiye Mungu mwenyewe? Ni nini Nilichotaka kuelezea kwa kusema hivyo? Ni nini ambacho Nilipenda kukufahamisha kuhusu? Je, mamlaka na nguvu za Mungu ni mtazamo mmoja unaoelezea kuhusu hadhi Yake halisi na inavyoonyeshwa? Je, mamlaka na nguvu hizi ni sehemu ya hali Yake halisi ambayo inathibitisha utambulisho Wake na hadhi? Je, maswali haya yamekufahamisha kile Ninachoenda kusema? Ni nini Ninachotaka uelewe? Fikiria hili kwa makini.

Kwa Kupinga Mungu kwa Ukaidi, Binadamu Anaangamizwa na Hasira za Mungu

Kwanza, hebu tuweze kuangalia mafungu mbalimbali ya maandiko yanayofafanua kuangamizwa kwa Sodoma na Mungu.

Mwa 19:1-11 Na jioni malaika wawili walikuja Sodoma; naye Lutu aliketi katika lango la Sodoma: na baada ya Lutu kuwaona aliinuka kwenda kuwakaribisha; na akasujudu; Naye akasema, Tazama saa hii, bwana zangu, ingieni ndani, nawaomba, ndani ya nyumba ya mtumishi wenu, na mbaki usiku mzima, na msafishe miguu yenu, na mtaamka mapema, na mshike njia zenu. Nao wakasema, La; lakini tutaketi katika uwanja usiku mzima. Na akawaomba sana; na wakamjia na kuingia katika nyumba yake; na akawaandalia karamu, na kupika mikate bila chachu, na wakala. Lakini kabla ya wao kujilaza, watu kutoka mjini, hata wenyeji wa Sodoma, waliizunguka nyumba hiyo, wazee na pia vijana, watu wote kutoka kila sehemu: Na wakamwita Lutu, na kumwambia, Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua. Naye Lutu akatoka mlangoni mahali walipokuwa, na akafunga mlango nyuma yake, Na kusema, nawaomba, ndugu, msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu. Na walisema. Toka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango. Lakini watu wale wakanyosha mbele mkono wao, na kumvuta Lutu katika nyumba walikokuwa, na kuufunga mlango. Na wakawagonga wale watu waliokuwa katika mlango wa nyumba na upofu, wakubwa na wadogo: kiasi kwamba walijichosha kuutafuta mlango.

Mwa 19:24-25 Kisha Yehova alinyesha kwa Sodoma na Gomora kibiriti na moto kutoka Yehova kutoka mbinguni; Na Akaiangusha hiyo miji, na mabonde yote, na wenyeji wote wa miji hiyo, na kile kilichomea kutoka ardhini.

Kutoka kwenye mafungu haya, si vigumu kuona kwamba dhambi ya Sodoma na kupotoka kwake tayari vilikuwa vimefikia kiwango kilichochukiza binadamu na Mungu, na kwamba kwa macho ya Mungu mji ulifaa kuangamizwa. Lakini nini kilichofanyikia mji huu hapo awali kabla haujaangamizwa? Ni msukumo upi tunaoweza kupata kutoka kwenye matukio haya? Je, mtazamo wa Mungu katika matukio haya unatuonyesha nini kuhusu tabia yake? Ili kuelewa hadithi nzima, hebu na tuweze kusoma kwa makini kile kilichorekodiwa katika Maandiko …

Kupotoka kwa Sodoma: Kunakasirisha Binadamu, Kunaghadhibisha Mungu

Kwenye usiku huo, Lutu alipokea wajumbe wawili kutoka kwa Mungu na akawatayarishia karamu. Baada ya chajio, kabla hawajalala, watu kutoka kila pahali kwenye mji walizunguka makazi ya Lutu na kumwita nje Lutu. Maandiko yanawarekodi wakisema, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua.” Ni nani aliyesema maneno haya? Alikuwa akiwaambia kina nani? Haya yalikuwa maneno ya watu wa Sodoma, walipiga mayowe nje ya makazi ya Lutu wakinuia kumwita Lutu. Je, unahisi vipi ukiyasikia maneno haya? Unaghadhibishwa? Je, maneno haya yanakuhuzunisha? Je, unabubujikwa na hasira kali? Je, Huoni kwamba maneno haya yananuka Shetani? Kupitia kwa maneno haya, unaweza kuhisi uovu na giza vilivyomo kwenye mji huu? Je, unaweza kuhisi ukatili na ushamba wa tabia za watu hawa kupitia kwa maneno yao? Je, unaweza kuhisi kina cha kupotoka kwao kupitia kwa tabia yao? Kupitia kwa maudhui ya hotuba yao, si vigumu kuona kwamba asili yao ya dhambi na tabia yao iliyopotoka ilikuwa imefikia kiwango kilichokuwa zaidi ya wao kuidhibiti. Isipokuwa Lutu, kila mtu katika mji huu hakuwa tofauti na Shetani; ule mtazamo tu wa mtu mwingine uliwafanya watu hawa kutaka kudhuru na kuwapotosha wao…. Mambo haya hayampatii tu mtu hisia ya asili potovu na ya kutisha ya mji huu, lakini pia yanamwonyesha harufu ya kifo iliyouzunguka mji huu; yanampa pia mtu hisia za dhambi na umwagikaji wa damu.

Alipojipata uso kwa uso na genge la majambazi waliojaa ukatili, watu waliokuwa wamejaa na maono ya kupotosha nafsi, Lutu aliitikia vipi? Kulingana na Maandiko: “Nawaomba … msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu.” Lutu alimaanisha yafuatayo katika maneno yake: Alikuwa radhi kuwatoa binti zake wawili ili kuwalinda wale wajumbe. Kutokana na akili razini, watu hawa wangekubali masharti ya Lutu na kuwaacha wale wajumbe wawili pekee; kwani hata hivyo, wajumbe hao walikuwa watu wageni kabisa kwao, watu ambao hawakuwa na chochote katu kuhusiana na wao; wajumbe hawa wawili walikuwa hawajawahi kudhuru masilahi yao. Hata hivyo, wakiwa na motisha ya asili yao ya dhambi, hawakuliwachia suala hili hapo. Badala yake, walizidisha tu jitihada zao. Hapa mojawapo ya mabishano yao yanaweza bila shaka kumpatia mtu maono zaidi kuhusu asili ya kweli na potovu ya watu hawa; wakati uo huo yanatujuza na kutufanya tuelewe sababu ya Mungu kutaka kuuangamiza mji huu.

Kwa hivyo walisema nini baadaye? Kama vile Biblia inavyosoma: “Toka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango.” Kwa nini walitaka kuuvunja mlango? Sababu ni kwamba walikuwa na hamu ya kuwaletea madhura wale wajumbe wawili. Wale wajumbe walikuwa wakifanya nini Sodoma? Kusudio lao la kuja hapo lilikuwa ni kumwokoa Lutu na familia yake; hata hivyo, watu wa mji huo walifikiri kimakosa kwamba walikuwa wamekuja kuchukua nyadhifa zao rasmi. Bila ya kuulizia kusudio lao, ilikuwa tu hali ya kujiamulia kufanya mambo kabla ya kujua ukweli wake, iliyoufanya mji huo kutaka kuwadhuru vibaya wajumbe hawa wawili; walitaka kuwadhuru watu wawili ambao hawakuhusiana kwa vyovyote vile na wao. Ni wazi kwamba watu wa mji huu walikuwa wamepoteza kabisa ubinadamu na akili zao razini. Kiwango cha wendawazimu wao na kukosa ustaarabu kwao kilikuwa tayari si tofauti na asili potovu ya Shetani ya kudhuru na kudanganya binadamu.

Walipowaamuru watu hawa watoke kwa Lutu, Lutu alifanya nini? Kutoka kwenye maandishi yanayofuata tunajua kwamba Lutu hakuwakabidhi wajumbe hawa kwa watu hawa. Je, Lutu aliwajua wajumbe hawa wawili wa Mungu? Bila shaka la! Lakini kwa nini aliweza kuwaokoa watu hawa wawili? Je, alijua ni nini walichokuwa wamekuja kufanya? Ingawaje hakujua kuhusu sababu yao ya kuja, alijua kwamba walikuwa ni watumishi wa Mungu, na kwa hivyo aliwapokea. Kwamba aliweza kuwaita watumishi hawa wa Mungu mabwana yaonyesha kwamba Lutu kwa kawaida alikuwa ni mfuasi wa Mungu, tofauti na wale wengine waliokuwa ndani ya Sodoma. Kwa hivyo, wakati wajumbe wa Mungu walipomjia, alihatarisha maisha yake binafsi ili kuwapokea watumishi hao wawili; aidha, aliwatoa binti zake wawili kuwabadilisha na watumishi hao wawili ili kuwalinda watumishi hao. Hiki ndicho kilikuwa kitendo cha haki cha Lutu; vilevile lilikuwa onyesho linaloonekana waziwazi kuhusu asili na hali halisi ya Lutu, na ndiyo pia sababu ya Mungu kuwatuma watumishi Wake ili kumwokoa Lutu. Wakati alipokabiliwa na changamoto, Lutu aliwalinda watumishi hawa wawili bila kujali chochote kingine; alijaribu hata kufanya biashara ya kuwabadilisha binti zake wawili mradi tu watumishi hawa wapate usalama. Mbali na Lutu, kulikuwa na mtu yeyote mwingine ndani ya mji ambaye angefanya jambo kama hili? Kama vile hoja zinavyothibitisha—la! Kwa hivyo, ni wazi kabisa kwamba kila mtu katika Sodoma, isipokuwa Lutu, alikuwa mlengwa wa kuangamizwa pamoja na mlengwa aliyestahili kuangamizwa.

Sodoma Yaangamizwa kwa Kukosea Hasira za Mungu

Wakati watu wa Sodoma walipowaona watu hawa wawili, hawakuuliza sababu ya wao kuja wala hakuna yule aliyeuliza kama walikuwa wamekuja kueneza mapenzi ya Mungu. Kinyume cha mambo, walikusanyika na kuwa umati wa watu na, bila kusubiri ufafanuzi wowote, walikuja kuwakamata watumishi hawa wawili ni kana kwamba walikuwa mbwa koko au mbwa mwitu. Je, Mungu aliyatazama mambo haya wakati yalipokuwa yakifanyika? Mungu alikuwa akifikiria nini katika moyo Wake kuhusiana na tabia hii ya binadamu, aina ya jambo hili? Mungu aliamua kuangamiza mji huu; Asingesita wala kusubiri, wala Asingeendelea kuonyesha subira yake. Siku yake ilikuwa imetimia, na kwa hivyo Aliweza kuweka wazi kazi Aliyopenda kufanya. Hivyo basi, Mwanzo 19:24-25 inasema, “Kisha Yehova alinyesha kwa Sodoma na Gomora kibiriti na moto kutoka Yehova kutoka mbinguni; Na Akaiangusha hiyo miji, na mabonde yote, na wenyeji wote wa miji hiyo, na kile kilichomea kutoka ardhini.” Mistari hii miwili inawaambia watu mbinu ambayo kwayo Mungu aliuangamiza mji huu; pia inawaambia watu kile ambacho Mungu aliangamiza. Kwanza, Biblia inasimulia kwamba Mungu aliunguza mji kwa moto, na kwamba kiwango cha moto kilikuwa tosha kuangamiza watu wote na kila kitu kilichomea kwenye ardhi. Hii ni kusema kwamba, moto ulioangushwa kutoka mbinguni haukuangamiza tu mji; uliangamiza pia watu wote na vitu vilivyo hai ndani yake, vyote bila kuacha chochote nyuma. Baada ya mji kuangamizwa, ardhi ilikuwa tupu bila kitu chochote kilicho hai. Hakukuwa tena na maisha, wala dalili zozote za maisha. Mji ulikuwa umebadilika na kuwa ardhi iliyoharibiwa, mahali patupu palipojaa kimya cha kutisha. Kusingekuwa na matendo maovu zaidi dhidi ya Mungu mahali hapa; kusingekuwa na uchinjaji zaidi au umwagikaji wa damu.

Kwa nini Mungu alitaka kuuchoma mji huu kabisa? Ni nini unachoweza kuona hapa? Je, Mungu angevumilia kumwona mwanadamu na asili, viumbe Vyake mwenyewe, vikiangamia hivi? Kama unaweza kutambua ghadhabu ya Yehova Mungu kutokana na moto ule ambao uliangushwa kutoka mbinguni, basi si vigumu sana kuona kiwango Chake cha hasira kali kutoka kwenye lengo la maangamizo Yake pamoja na kiwango ambacho mji huo uliweza kuangamizwa. Wakati Mungu anadharau mji, Ataweza kutekeleza adhabu Yake juu ya mji huo. Wakati Mungu anachukizwa na mji, Ataweza kutoa maonyo mbalimbali akifahamisha watu kuhusu ghadhabu Yake. Hata hivyo, wakati Mungu anaamua kukomesha na kuangamiza mji—yaani, wakati hasira na adhama Yake vimekosewa—Hataweza kutoa maonyo au adhabu nyingine. Badala yake, Ataweza kuuangamiza moja kwa moja. Ataufanya kutoweka kabisa. Hii ndiyo tabia ya haki ya Mungu.

Baada ya Ukinzani wa Mara kwa Mara wa Sodoma na Ukatili Wao Dhidi Yake, Mungu Anaufuta Kabisa

Mara tu tunapokuwa na ufahamu wa jumla kuhusu tabia ya haki ya Mungu, tunaweza kurejesha umakinifu wetu kwenye mji wa Sodoma—kile ambacho Mungu aliona kuwa mji wa dhambi. Kwa kuelewa hali halisi ya mji huu, tunaweza kuelewa ni kwa nini Mungu alitaka kuuangamiza na ni kwa nini Aliuangamiza kabisa. Kutokana na haya, tunaweza kujua tabia ya haki ya Mungu.

Kutoka katika mtazamo wa binadamu, Sodoma ulikuwa ni mji ulioweza kutosheleza kikamilifu matamanio ya binadamu na maovu ya binadamu. Ulivutia na uliduwaza, kwa muziki na densi usiku baada ya usiku, ufanisi wake uliwasukuma wanaume kufurahia na kuruka kichwa. Maovu yake yalidhuru mioyo ya watu na yakawaduwaza hadi kuzoroteka. Huu ulikuwa mji uliokuwa na roho chafu na roho za Shetani zilicharuka hewani; ulijaa dhambi na mauaji na harufu ya damu iliyovunda. Ulikuwa mji ambao ulitisha watu kabisa, mji ambao mtu angejitoa kwake kwa hofu. Hakuna mtu katika mji huu—awe wa kiume au wa kike, awe mchanga au mzee—aliyetafuta njia ya kweli; hakuna aliyetamani mwangaza au kutaka kuachana na dhambi. Kila mmoja aliishi chini ya udhibiti wa Shetani, upotovu na uwongo. Kila mmoja alikuwa ameupoteza ubinadamu wake; walikuwa wamepoteza hisia zao, na walikuwa wamepoteza shabaha asilia ya kuweko kwa binadamu. Walitenda matendo maovu yasiyohesabika za ukinzani dhidi ya Mungu; walikataa mwongozo wake na kupinga mapenzi Yake. Yalikuwa matendo yao maovu ambayo yaliwapeleka watu hawa, mji na kila kiumbe kilichokuwa ndani ya mji huu, hatua kwa hatua, kwenye njia ya maangamizo.

Ingawaje mafungu haya mawili hayarekodi maelezo yanayofafanua kiwango cha kupotoka cha watu wa Sodoma, badala yake yanarekodi mwenendo wao kwa watumishi wawili wa Mungu kufuatia kuwasili kwao mjini, ukweli mtupu unaweza kufichua kiwango ambacho watu wa Sodoma walikuwa wamepotoka, walijaa maovu na walimpinga Mungu. Kwa mujibu wa haya, ukweli wa mambo na hali halisi ya watu wa mji huu vinafichuliwa pia. Mbali na kutokubali maonyo ya Mungu, hawakuogopa pia adhabu Yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, walifanyia mzaha ghadhabu ya Mungu. Walimpinga Mungu bila sababu. Haijalishi ni nini Alichofanya au ni vipi Alivyokifanya, asili yao ya tamaa ilizidi kuongezeka, na wakampinga Mungu mara kwa mara. Watu wa Sodoma walikuwa wakatili kwa uwepo wa Mungu, kuja Kwake, adhabu Yake, na hata zaidi, maonyo Yake. Hawakuona chochote kingine chenye thamani karibu nao. Waliwapotosha na kuwadhuru watu wote walioweza kupotoshwa na kupata madhara, na wakawatendea watumishi wa Mungu vivyo hivyo. Kuhusiana na matendo yote ya uovu yaliyotendwa na watu hawa wa Sodoma, kuwadhuru watumishi wa Mungu kulikuwa mfano tu wa tone baharini ya kile walichokuwa wakifanya, na asili yao ya uovu uliofichuliwa kwa kweli ulionekana tu kuwa mdogo zaidi kuliko hata tone moja ndani ya bahari kubwa. Kwa hivyo, Mungu alichagua kuwaangamiza kwa moto. Mungu hakutumia gharika, wala Hakutumia zilizala, mtetemeko wa ardhi, sunami au mbinu yoyote nyingine ya kuuangamiza mji huu. Kule kutumia moto na Mungu kuangamiza mji huu kulimaanisha nini? Kulimaanisha uangamizaji kamili wa mji huo; kulimaanisha kwamba mji huu ulitoweka kabisa kutoka ulimwenguni na kutoka katika kuwepo kwake. Hapa, “kuangamiza” hakurejelei tu kule kutoweka kwa umbo na muundo au sura ya nje ya mji huo; kunamaanisha pia kwamba nafsi za watu ndani ya mji huo zilisita kuwepo, baada ya kufutwa kabisa. Kwa ufupi, watu wote, matukio na mambo yote yaliyohusiana na mji huu yaliangamizwa. Kusingekuwa na maisha ya baadaye au roho kuwa mwilini mwao tena; Mungu alikuwa amewafuta kabisa kutoka katika binadamu, uumbaji Wake, mara moja na tena milele. Yale “matumizi ya moto” yalimaanisha kusitisha dhambi, na yalimaanisha mwisho wa dhambi; dhambi hii ingesita kuwepo na kuenea. Yalimaanisha kwamba uovu wa Shetani ulikuwa umepoteza mahali pake pa kunawiri pamoja na eneo la kaburi ambalo liliupatia mji huo mahali pa kukaa na kuishi. Kwenye vita kati ya Mungu na Shetani, matumizi ya moto na Mungu ni alama ya ushindi Wake ambayo Shetani anatajiwa. Kuangamizwa kwa Sodoma ni hatua kubwa ya kuzuia maono ya Shetani ya kupinga Mungu kwa kupotosha na kudanganya binadamu, na vilevile ni ishara ya kudhalilishwa kwa muda kwenye maendeleo ya binadamu ambapo binadamu alikataa mwongozo wa Mungu na akajiachilia kutenda maovu. Aidha, ni rekodi ya ufunuo wa kweli wa tabia ya haki ya Mungu.

Wakati ule moto ambao Mungu alituma kutoka mbinguni ulikuwa umeteketeza kabisa Sodoma hata zaidi ya majivu, ilimaanisha kwamba mji huu ulioitwa “Sodoma” ungesita kuwepo, na vilevile kila kitu ndani ya mji wenyewe. Uliangamizwa kwa ghadhabu ya Mungu; ulitoweka kutokana na hasira na adhama ya Mungu. Kwa sababu ya tabia ya haki ya Mungu Sodoma ilipokea adhabu yake ya haki; kutokana na tabia ya haki ya Mungu, ilipokea mwisho wake wa haki. Mwisho wa kuwepo kwa Sodoma ulitokana na maovu yake, na ulitokana pia na tamanio la Mungu kutowahi kuutazamia mji huu tena, pamoja na watu wote walioishi ndani ya mji huo au maisha yoyote yaliyowahi kukua ndani ya mji huo. “Tamanio la kutowahi kuutazamia mji huo tena” la Mungu ni hasira Yake, pamoja na adhama Yake. Mungu aliuteketeza mji kwa sababu maovu na dhambi zake vilimsababisha Yeye kuhisi ghadhabu, maudhi na chuki katika mji huu na tamanio lake la kutowahi kuuona au watu wowote wa mji huo na viumbe vyote vilivyo hai vilivyokuwa ndani ya mji huo tena. Baada ya mji huo kuacha kuchomeka, huku ukiwa umeacha nyuma jivu pekee, ulikuwa kwa kweli umesita kuwepo mbele ya macho ya Mungu; hata kumbukumbu za Mungu kuuhusu ziliondolewa, zilifutwa. Hii inamaanisha kwamba moto ulioangushwa kutoka mbinguni haukuangamiza tu mji wote wa Sodoma kwa jumla na watu waliokuwa wamejaa dhambi ndani yake, wala kuangamiza tu vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji uliokuwa umepatwa na dosari ya dhambi; hata zaidi, moto huu uliangamiza kumbukumbu za maovu na ukinzani wa binadamu dhidi ya Mungu. Hili ndilo lilikuwa kusudio la Mungu kwa kuuchoma ule mji.

Binadamu ulikuwa umepotoka kupindukia. Watu hawa hawakujua Mungu alikuwa nani au kule walikokuwa wametokea. Kama ungemtaja Mungu, watu hawa wangekushambulia, kukutukana na kukufuru. Hata wakati watumishi wa Mungu walikuwa wamekuja kueneza onyo Lake, watu hawa waliopotoka hawakuweza kuonyesha ishara zozote za toba na hawakuacha mwenendo wao wa maovu, lakini kinyume cha mambo ni kwamba, waliweza bila ya haya, kuwadhuru watumishi wa Mungu. Kile walichoonyesha na kufichua kilikuwa asili na hali yao halisi ya uadui mkubwa kwa Mungu. Tunaweza kuona kwamba ukinzani wa watu hawa waliopotoka dhidi ya Mungu ulikuwa zaidi ya ufunuo wa tabia yao potovu, kama vile tu ilivyokuwa zaidi ya tukio la matusi au kejeli iliyotokana na ukosefu wa ufahamu wa ukweli. Ujinga wala kutojua havikusababisha mwenendo huu wa maovu; haikuwa kwa sababu watu hawa walikuwa wamedanganywa, na bila shaka si kwa sababu walikuwa wamepotoshwa. Mwenendo wao ulikuwa umefikia kiwango cha uhasama wa wazi wa kupinga na kuasi dhidi ya Mungu. Bila shaka, aina hii ya tabia ya binadamu ingempa hasira kali Mungu, na ingesababisha hasira kali kwenye tabia Yake—tabia ambayo haitakiwi kukosewa. Kwa hivyo, Mungu aliachilia kwa njia ya moja kwa moja na kwa uwazi hasira Yake na adhama Yake; huu ni ufunuo wa kweli wa tabia Yake ya haki. Akiwa amekabiliwa na mji uliotiririka na dhambi, Mungu alitamani kuuangamiza kwa njia ya haraka zaidi iliyowezekana; Alipenda kuwaondoa watu waliokuwa ndani yake na uzima wa dhambi zao kwa njia kamilifu zaidi, kuwafanya watu hawa wa mji kusita kuwepo na kukomesha dhambi ndani ya mahali hapa kuongezeka. Njia ya haraka zaidi na kamilifu zaidi ya kufanya hivyo ilikuwa ni kuuteketeza kwa moto. Mtazamo wa Mungu kwa watu wa Sodoma haukuwa ule wa kuwaacha au kutowajali; bali, Alitumia hasira Yake, adhama na mamlaka kuwaadhibu, kuwaweka chini na kuwaangamiza kabisa watu hawa. Mtazamo wake kwao haukuwa tu ule wa kuwaangamiza kimwili bali pia kuwaangamiza kinafsi, ukomeshaji wa milele. Hii ndiyo athari ya kweli ya tamanio la Mungu kwao “kuweza kusita kuwepo.”

Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote

Namna Mungu alivyoshughulikia binadamu wote wa ujinga na kutojua ulitokana kimsingi na huruma na uvumilivu. Hasira yake, kwa upande mwingine, imefichwa kwenye wingi mkubwa mno wa muda na wa mambo; haijulikani kwa binadamu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo. Wakati binadamu anakabiliwa na kazi ya mwisho ya Mungu na hatua ya kuvumilia na kusamehe binadamu—yaani, wakati onyesho la mwisho la Mungu la huruma na onyo Lake la mwisho linapowafikia—kama bado wangali wanatumia mbinu zile kumpinga Mungu na hawafanyi jitihada zozote za kutubu, kurekebisha njia zao au kukubali huruma Yake, Mungu hataweza tena kuwapatia uvumilivu na subira yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, ni katika wakati huu ambapo Mungu atafuta huruma Yake. Kufuatia hili, Atatuma tu hasira Yake. Anaweza kuonyesha hasira Yake kwa njia tofauti, kama vile tu Anavyoweza kutumia mbinu tofauti kuwaadhibu na kuwaangamiza watu.

Matumizi ya Mungu ya moto kuuangamiza mji wa Sodoma ndio mbinu Yake ya haraka zaidi ya kuondoa kabisa binadamu au kitu. Kuwachoma watu wa Sodoma kuliangamiza zaidi ya miili yao ya kimwili; kuliangamiza uzima wa roho zao, nafsi zao na miili yao, na kuhakikisha kwamba watu waliokuwa ndani ya mji wangesita kuwepo kwenye ulimwengu wa anasa na hata ulimwengu usioonekana na mwanadamu. Hii ni njia moja ambayo Mungu hufichua na kuonyesha hasira Yake. Mfano huu wa ufunuo na maonyesho ni dhana moja ya hali halisi ya hasira ya Mungu, kama vile ilivyo kwa kawaida pia ufunuo wa hali halisi ya tabia ya haki ya Mungu. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, Yeye husita kufichua huruma au upole wa upendo wowote, na wala haonyeshi tena uvumilivu au subira Yake; hakuna mtu, kitu au sababu inayoweza kumshawishi kuendelea kuwa na subira, kutoa huruma Yake tena, na kumpa binadamu uvumilivu wake kwa mara nyingine. Badala ya mambo haya, bila kusita hata kwa muda mfupi, Mungu atashusha hasira Yake na adhama, kufanya kile Anachotamani, na Atafanya mambo haya kwa haraka na kwa njia safi kulingana na matamanio Yake binafsi. Hii ndiyo njia ambayo Mungu hushusha hasira na adhama Yake, ambavyo binadamu hatakiwi kukosea, na pia ni maonyesho ya dhana moja ya tabia Yake ya haki. Wakati watu wanashuhudia Mungu akionyesha wasiwasi na upendo kwa binadamu, hawawezi kugundua hasira Yake, kuiona uadhama Yake au kuhisi kutovumilia Kwake kosa. Mambo haya siku zote yamewaongoza watu kusadiki kwamba tabia ya haki ya Mungu ni ile ya huruma, uvumilivu na upendo tu. Hata hivyo, wakati mtu anapoona Mungu akiuangamiza mji au akichukia binadamu, hasira Yake katika kuangamiza binadamu na adhama Yake huruhusu watu kuona kidogo upande ule mwingine wa tabia Yake ya haki. Huku ni kutovumilia kosa kwa Mungu. Tabia ya Mungu isiyovumilia kosa inavuka mawazo ya kiumbe chochote kilichoumbwa, na miongoni mwa viumbe ambavyo havikuumbwa, hakuna kati ya hivyo kinachoweza kuhitilafiana na kingine au kuathiri kingine; lakini hata zaidi, hakiwezi kughushiwa au kuigwa. Kwa hivyo, dhana hii ya tabia ya Mungu ndiyo ambayo binadamu anafaa kujua zaidi. Mungu Mwenyewe Pekee ndiye aliye na aina hii ya tabia, na Mungu Mwenyewe pekee ndiye anayemiliki aina hii ya tabia. Mungu anamiliki aina hii ya tabia kwa sababu Anachukia maovu, giza, maasi na vitendo vya uovu vya Shetani—vya kutosha na kudanganya wanadamu—kwa sababu Anachukia vitendo vyote vya dhambi vinavyompinga Yeye na kwa sababu ya hali Yake halisi takatifu na isiyo na doa. Ni kwa sababu ya haya ndiposa Hataacha viumbe vyovyote kati ya vile vilivyoumba au ambavyo havikuumbwa vimpinge waziwazi au kushindana na Yeye. Hata mtu binafsi ambaye Aliwahi kumwonyesha huruma au kuchagua anahitaji tu kuchochea tabia Yake na kukiuka kanuni Yake ya subira na uvumilivu, na Ataachilia na kufichua tabia Yake ya haki bila ya huruma hata kidogo au kusitasita kokote—tabia isiyovumilia kosa lolote.

Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri

Kwa kuielewa mifano hii ya unenaji wa Mungu, fikira na vitendo vya Mungu, je, unaweza kuielewa tabia ya haki ya Mungu, tabia isiyoweza kukosewa? Mwishowe, hii ni dhana ya tabia ya kipekee kwa Mungu Mwenyewe, bila ya kujali ni kiwango kipi ambacho binadamu anaweza kuelewa. Mungu kutoweza kuvumilia kosa ndicho kiini Chake cha kipekee; hasira ya Mungu ndiyo tabia Yake ya kipekee; adhama ya Mungu ndiyo hali Yake halisi ya kipekee. Kanuni inayoelezea ghadhabu ya Mungu inaonyesha utambulisho na hadhi ambayo Yeye tu ndiye anayemiliki. Mtu hana haja kutaja kwamba ni ishara pia ya hali halisi ya Mungu Mwenyewe wa kipekee. Tabia ya Mungu ndiyo hali Yake halisi ya asili. Haibadiliki kamwe na kupita kwa muda, wala haibadiliki kila wakati mahali panapobadilika. Tabia Yake ya asili ndiyo kiini Chake halisi cha kweli. Haijalishi ni nani anayetekelezea kazi Yake, hali Yake halisi haibadiliki, na wala tabia ya haki Yake pia. Wakati mtu anapomghadhibisha Mungu, kile Anachomshushia ni tabia Yake ya asili; wakati huu kanuni inayoelezea ghadhabu Yake haibadiliki, wala utambulisho na hadhi Yake ya kipekee. Haghadhibishwi kwa sababu ya mabadiliko katika hali Yake halisi au kwa sababu ya tabia Yake kusababisha dalili tofauti, lakini kwa sababu upinzani wa binadamu dhidi Yake huikosea tabia Yake. Uchochezi waziwazi wa binadamu kwa Mungu ni changamoto kubwa katika utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu. Kwa mtazamo wa Mungu, wakati binadamu anapompinga Yeye, binadamu huyo anashindana na Yeye na anampima ghadhabu Yake. Wakati binadamu anapompinga Mungu, wakati binadamu anaposhindana na Mungu, wakati binadamu anapojaribu kila mara ghadhabu ya Mungu—na ndio maana pia dhambi huongezeka—hasira ya Mungu itaweza kufichuka kwa kawaida na kujitokeza yenyewe. Kwa hivyo, maonyesho ya Mungu ya hasira Yake yanaashiria kwamba nguvu zote za maovu zitasita kuwepo; yanaashiria kwamba nguvu zote katili zitaangamizwa. Huu ndio upekee wa tabia ya haki ya Mungu, na ndio upekee wa hasira ya Mungu. Wakati heshima na utakatifu wa Mungu vinapopata changamoto, wakati nguvu za haki zinapata kuzuiliwa na hazionekani na binadamu, Mungu atashusha hasira Yake. Kwa sababu ya hali halisi ya Mungu, nguvu hizo zote ulimwenguni zinazoshindana na Mungu, zinazompinga Yeye na kushindana na Yeye ni za maovu, kupotoka na kutokuwa na dhalimu; zinatoka Kwake na zinamilikiwa na Shetani. Kwa sababu Mungu ni wa haki, wa nuru na mtakatifu bila dosari, vitu vyote viovu, vilivyopotoka na vinavyomilikiwa na Shetani vitatoweka baada ya kuachiliwa kwa hasira ya Mungu.

Ingawaje kumwagwa kwa hasira ya Mungu ni dhana ya maonyesho ya tabia ya haki Yake, hasira ya Mungu kwa vyovyote vile haibagui walengwa wake au haina kanuni. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu si mwepesi wa ghadhabu, wala Hakimbilii kufichua hasira Yake na adhama Yake. Aidha, hasira ya Mungu inadhibitiwa na kupimwa kwa kiwango fulani; hailinganishwi kamwe na namna ambavyo binadamu atakavyowaka kwa hasira kali au kutoa ghadhabu zake. Mazungumzo mengi kati ya binadamu na Mungu yamerekodiwa kwenye Biblia. Maneno ya baadhi ya watu hawa binafsi yalikuwa ya juujuu, yasiyo na ujuzi na yasiyofaa, lakini Mungu hakuwaangusha chini, wala Hakuwashutumu. Hususan, wakati wa majaribio ya Ayubu, je, Yehova Mungu aliwachukuliaje marafiki watatu wa Ayubu na wale wengine baada ya kusikia maneno waliyomzungumzia Ayubu? Je, Aliwashutumu? Je, Aligeuka na kushikwa na hasira kali kwao? Hakufanya kitu kama hicho! Badala yake Alimwambia Ayubu kuwasihi, kuwaombea; Mungu, kwa mkono mwingine, hakuchukua lawama zao na kutia moyoni. Matukio haya yote yanawakilisha mtazamo mkuu ambao Mungu anashughulikia binadamu waliopotoka, na wasiojua. Kwa hivyo, kushushwa kwa hasira ya Mungu si kwa vyovyote vile maonyesho au hali ya kutoa nje hali Yake ya moyo. Hasira ya Mungu si mlipuko mkubwa wa hasira kali kama vile binadamu anavyoielewa. Mungu hawachilii hasira Yake kwa sababu hawezi kuidhibiti hali ya moyo Wake binafsi au kwa sababu ghadhabu Yake imefikia kilele na lazima itolewe. Kinyume cha mambo ni kwamba, hasira Yake ni maonyesho ya tabia ya haki Yake na maonyesho halisi ya tabia ya haki Yake; ni ufunuo wa ishara ya hali Yake halisi takatifu. Mungu ni hasira, asiyevumilia kosa—hivi si kusema kwamba ghadhabu ya Mungu haitofautishi sababu za kufanya hivyo au haifuati kanuni; ni binadamu uliopotoka ambao unafuata mkondo wa kipekee wa kutokuwa na kanuni, mlipuko wa hasira kali bila mpango usiotofautisha hali hii miongoni mwa sababu mbalimbali. Mara tu binadamu anapokuwa na hadhi, mara nyingi atapata ugumu wa kudhibiti hali ya moyo wake, na kwa hivyo atafurahia kutumia nafasi mbalimbali kueleza kutotosheka kwake na kutoa nje hisia zake; mara nyingi atawaka kwa hasira kali bila sababu yoyote, ili kuonyesha uwezo wake na kuwafanya wengine kujua kwamba hadhi yake na utambulisho wake ni tofauti na ule wa watu wa kawaida. Bila shaka, watu waliopotoka wasiokuwa na hadhi yoyote mara kwa mara pia watapoteza udhibiti wao. Ghadhabu yao mara nyingi husababishwa na uharibifu wa manufaa yao ya kibinafsi. Ili kulinda hadhi yake binafsi na heshima, mara kwa mara atatoa nje hisia zake na kufichua asili yake yenye kiburi. Binadamu atalipuka kwa ghadhabu na kutoa nje hisia zake ili kutetea na kushikilia uwepo wa dhambi, na matendo haya ndiyo njia ambayo kwayo binadamu anaonyesha kutotosheka kwake; yamejaa dosari, mifumo na mbinu mbalimbali, kupotoka na maovu ya binadamu, na zaidi ya chochote kingine, yanajaa kwa malengo na matamanio ya binadamu. Wakati haki inaposhindana na maovu, binadamu hataruka juu kwa ghadhabu ili kutetea uwepo wa haki; kinyume ni kwamba, wakati nguvu za haki zinatishwa, zinateswa na kushambuliwa, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutotilia maanani, kukwepa, au kushtuka. Hata hivyo, wakati anapokabiliwa na nguvu za maovu, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutunza, na kunyenyekea mno. Hivyo basi, kutoa nje ghadhabu kwa binadamu ni kimbilio la nguvu za maovu, maonyesho ya mwenendo wa maovu uliokithiri na usiositishwa wa binadamu wa kimwili. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, hata hivyo, nguvu zote za maovu zitasitishwa; dhambi zote za kudhuru binadamu zitasitishwa; nguvu zote katili zinazozuia kazi ya Mungu zitawekwa wazi, zitatenganishwa na kulaaniwa; washirika wote wa Shetani ambao wanampinga Mungu wataadhibiwa, na kuondolewa. Badala yake, kazi ya Mungu itaendelea huru bila vizuizi vyovyote; mpango wa usimamizi wa Mungu utaendelea kuimarika hatua kwa hatua kulingana na utaratibu uliopo; watu walioteuliwa na Mungu watakuwa huru dhidi ya kusumbuliwa na Shetani na kudanganywa; wale wanaomfuata Mungu watafurahia uongozi na ujazo wa Mungu miongoni mwa mazingira yenye utulivu na amani. Hasira ya Mungu ni usalama unaozuia nguvu zote za maovu dhidi ya kuzidishwa na kutapakaa kwa nguvu, na pia ni usalama unaolinda kuwepo na kuenea kwa mambo yote ya haki na mazuri na daima dawamu unayalinda mambo haya dhidi ya kukandamizwa na kuangamizwa.

Unaweza kuona hali halisi ya hasira ya Mungu katika kuangamiza Kwake kwa Sodoma? Je, kuna jambo lolote lililochanganyika kwenye hasira Yake kali? Je, hasira kali ya Mungu ni safi? Ili kutumia maneno ya binadamu, je, hasira kali ya Mungu imetiwa najisi? Je, kunayo hila yoyote katika hasira Yake? Je, kunayo njama yoyote? Je, zipo siri zozote zisizotamkika? Ninaweza kukwambia wazi na kwa makini: Hakuna sehemu ya hasira ya Mungu inayoweza kumwongoza mtu kwa shaka. Ghadhabu yake haina kasoro, ni hasira ambayo haijatiwa najisi na haijasheheni nia au shabaha zozote zingine. Sababu ya ghadhabu Yake ni safi, haina lawama na haipingiki. Ni ufunuo wa kawaida na onyesho la hali Yake halisi ya utakatifu; ni kitu ambacho hakuna kiumbe chochote kinamiliki. Hii ni sehemu ya tabia ya kipekee ya haki ya Mungu, na ni tofauti ya wazi kati ya hali halisi husika ya Muumba na uumbaji Wake.

Haijalishi kama mtu anakuwa na ghadhabu akiwa mbele ya wengine au wakiwa hawako naye, kila mtu anayo nia na kusudi tofauti. Pengine wanajenga heshima zao, au pengine wanatetea masilahi yao binafsi, na kuendeleza taswira yao au kulinda sura yao. Baadhi yao huendeleza hali ya kuzuia ghadhabu yao, huku nao wengine wanakimbilia na wanapandwa na hasira kali kila wanapopenda bila ya hata kiwango kidogo zaidi cha kujizuia. Kwa ufupi, ghadhabu ya binadamu inatokana na tabia yake iliyopotoka. Haijalishi kusudi lake, ni la mwili na ni la asili; halina uhusiano wowote na haki au ukiukaji wa haki kwa sababu hakuna kitu katika asili ya binadamu na hali halisi vinavyolingana na ukweli. Kwa hivyo, hasira ya binadamu wapotovu na hasira ya Mungu vyote havifai kutajwa kwa kiwango sawa. Bila ubaguzi, tabia ya mwanadamu aliyepotoshwa na Shetani huanza na tamanio la kulinda upotovu, na ina msingi katika upotovu; hivyo basi, hasira ya mwanadamu haiwezi kutajwa kwa kiwango sawa na ghadhabu ya Mungu, haijalishi ni bora namna gani kinadharia. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake kali, nguvu za giza zinakaguliwa, mambo ya giza yanaangamizwa, huku mambo ya haki na mazuri yakifurahia utunzaji wa Mungu, ulinzi, na yote yanaruhusiwa kuendelea. Mungu hushusha hasira Yake kwa sababu ya mambo dhalimu, mabaya na ya giza, yanayozuia, yanayotatiza au kuangamiza shughuli na maendeleo ya kawaida ya mambo ya haki na mazuri. Shabaha ya ghadhabu ya Mungu si kusalimisha hadhi na utambulisho Wake binafsi, lakini kusalimisha uwepo wa mambo ya haki, mazuri, ya kupendeza na kuvutia, kusalimisha sheria na mpangilio wa kuwepo kwa kawaida kwa binadamu. Hiki ndicho chanzo asilia cha hasira ya Mungu. Hasira kali ya Mungu ni bora sana, ya kiasili na ufunuo wa kweli wa tabia Yake. Hakuna makusudi yoyote katika hasira Yake kali, wala hakuna udanganyifu au njama yoyote; au hata zaidi, hasira Yake kali haina tamanio lolote, ujanja, mambo ya kijicho, udhalimu, maovu, au kitu kingine ambacho binadamu wote waliopotoka huwa navyo. Kabla ya Mungu kushusha hasira Yake kali, huwa tayari Ametambua hali halisi ya kila suala kwa uwazi na ukamilifu zaidi, na huwa tayari Amepangilia ufafanuzi na hitimisho sahihi na zilizo wazi. Hivyo basi, lengo la Mungu katika kila suala Analofanya ni wazi kabisa, vile ulivyo mtazamo Wake. Yeye si mtu aliyechanganyikiwa; Yeye si kipofu; Yeye si mtu wa kuamua ghafla; Yeye si mzembe; na zaidi, Yeye si mtu asiyefuata kanuni. Hii ndiyo dhana ya kimatendo ya hasira ya Mungu, na ni kwa sababu ya dhana hii ya kimatendo ya hasira ya Mungu ambapo binadamu umefikia uwepo wake wa kawaida. Bila ya hasira ya Mungu, binadamu ungeishia kuishi katika mazingira yasiyo ya kawaida; viumbe vyote vyenye haki, virembo na vizuri vingeangamizwa na kusita kuwepo. Bila ya hasira ya Mungu, sheria na amri za kuwepo kwa viumbe vingekiukwa au hata kupinduliwa kabisa. Tangu uumbwaji wa binadamu, Mungu ametumia bila kusita, tabia Yake ya haki kusalimisha na kuendeleza uwepo wa kawaida wa binadamu. Kwa sababu tabia Yake ya haki inayo hasira na adhama, watu wote waovu, vitu, vifaa na vitu vyote vinavyotatiza na kuharibu uwepo wa kawaida wa binadamu vinaadhibiwa, vinadhibitiwa na kuangamizwa kwa sababu ya hasira Yake. Kwenye milenia mbalimbali zilizopita, Mungu ameendelea kutumia tabia Yake ya haki kuangusha na kuangamiza kila aina za roho chafu na za giza ambazo zinampinga Mungu na kuchukua nafasi ya wasaidizi na watumishi wa Shetani katika kazi ya Mungu ya kusimamia binadamu. Hivyo basi, kazi ya Mungu ya wokovu wa binadamu siku zote imeimarika kulingana na mpango Wake. Hivi ni kusema kwamba kwa sababu ya uwepo wa hasira ya Mungu, sababu za haki zaidi za binadamu hazijawahi kuangamizwa.

Sasa kwa vile unao ufahamu wa hali halisi ya hasira ya Mungu, bila shaka lazima utakuwa na ufahamu bora zaidi wa namna ya kutofautisha maovu ya Shetani!

Ingawa Shetani Anaonekana Mwenye Utu, Haki na Maadili, Ni Mkatili na Mwovu katika Kiini Chake

Shetani hupata umaarufu wake kupitia kwa kuudanganya umma. Mara nyingi hujiweka kama kiongozi na kuchukua wajibu wa kielelezo cha haki. Akisingizia kuwa anasalimisha haki, anaishia kumdhuru binadamu, kudanganya nafsi zao, na kutumia mbinu zote ili kuweza kuteka nyara hisia na fikira za binadamu, kumdanganya na kumchochea. Shabaha yake ni kumfanya binadamu kuidhinisha na kuufuata mwenendo wake wa maovu, kumfanya binadamu kujiunga naye katika kupinga mamlaka na ukuu wa Mungu. Hata hivyo, wakati mtu anapokuwa mwerevu na kutambua njama zake, mipango na sifa zake hizo na hataki kuendelea kudhalilishwa na kudanganywa naye hivyo au kuendelea kuwa mtumwa wa Shetani, au kuadhibiwa na kuangamizwa pamoja na Shetani, Shetani naye hubadilisha sifa zake za awali za utakatifu na kuondoa baraka yake bandia ili kufichua uso wake wa kweli wenye maovu, ubaya, sura mbaya na wa kikatili. Shetani hawezi kupenda jambo lolote isipokuwa kumaliza wale wote wanaokataa kumfuata yeye na wale wanaopinga nguvu zake za giza. Wakati huu Shetani hawezi tena kuvaa sura ya uaminifu, na utulivu; badala yake, sifa zake za kweli za sura mbaya na za kishetani zilizokuwa zimefichwa kwenye mavazi ya kondoo zinafichuliwa. Mara tu njama za Shetani zinapomulikwa, na sifa zake za kweli kufichuliwa, yeye huingia kwenye hisia za hasira kali na kuonyesha ushenzi wake; tamanio lake la kudhuru na kudanganya watu ndipo litazidi zaidi. Hii ni kwa sababu anapandwa na hasira kali kwa kuzindukana kwa binadamu; anataka kuwa na kisasi kingi dhidi ya binadamu kwa maazimio yake ya kutamani kuwa na uhuru na nuru na kutokuwa mateka wa jela yake. Hasira yake kali inanuiwa kutetea maovu yake, na pia ni ufunuo wa kweli wa asili yake ya kishenzi.

Katika kila suala, tabia ya Shetani hufichua asili yake maovu. Kati ya vitendo vyote vya maovu ambavyo Shetani ametekeleza kwa binadamu—kutoka kwa jitihada zake za mapema za kudanganya binadamu ili aweze kumfuata, hadi unyonyaji wake wa binadamu, ambapo anamkokota binadamu hadi kwenye matendo maovu, hadi ulipizaji wa kisasi wa Shetani kwa binadamu baada ya sifa zake za kweli kuweza kufichuliwa na binadamu kuweza kutambua na kumwacha—hakuna hata kimoja kati ya vitendo hivi kinachoshindwa kufichua hali halisi ya uovu wa Shetani; hakuna hata moja inayoshindwa kuthibitisha hoja kwamba Shetani hana uhusiano na mambo mazuri; hakuna hata moja hushindwa kuthibitisha kwamba Shetani ndiye chanzo cha mambo yote maovu. Kila mojawapo ya matendo yake inasalimisha maovu yake, inadumisha maendelezo ya vitendo vyake vya maovu, inaenda kinyume cha haki na mambo mazuri, inaharibu sheria na mpangilio wa uwepo wa kawaida wa binadamu. Wao ni katili kwa Mungu, na ndio wale ambao hasira ya Mungu itaangamiza. Ingawaje Shetani anayo hasira yake kali, hasira yake kali ni mbinu ya kutoa nje asili yake mbovu. Sababu inayomfanya Shetani kukereka na kuwa mkali ni: Kwa sababu njama zake zisizotamkika zimefichuliwa; mipango yake haikwepeki kwa urahisi; malengo yake yasiyo na mipaka na tamanio la kubadilisha Mungu na kujifanya kuwa Mungu, vyote vimekwama na kuzuiliwa; shabaha yake ya kudhibiti binadamu wote imeishia patupu na haiwezi tena kutimizwa. Kuitisha kwa Mungu hasira Yake mara kwa mara ndiko kumesitisha mipango ya Shetani dhidi ya kukamilika na kukatiza kuenea na kusambaa kwa maovu ya Shetani; kwa hivyo, Shetani anaogopa na kuchukia hasira ya Mungu. Kila matumizi ya hasira ya Mungu huwa yanafichua sura halisi ya aibu ya Shetani; na pia kufichua na kuweka kwenye nuru matamanio ya maovu ya Shetani. Wakati uo huo, sababu za hasira kali ya Shetani dhidi ya binadamu zinafichuliwa kabisa. Kule kulipuka kwa hasira kali ya Shetani ni ufunuo wa kweli wa asili yake mbovu, ufichuzi wa njama zake. Bila shaka, kila wakati Shetani anapopandwa na hasira kali, huwa ni dalili ya maangamizo ya mambo maovu; huashiria ulinzi na mwendelezo wa mambo mazuri, na huashiria asili ya hasira ya Mungu—ile ambayo haiwezi kukosewa!

Mtu Hafai Kutegemea Uzoefu na Fikira Ili Kujua Tabia ya Haki ya Mungu

Ukijipata unakabiliwa na hukumu na kuadibiwa na Mungu, je, utasema kwamba neno la Mungu limetiwa najisi? Je, utasema kwamba kunayo hadithi inayoelezea hasira kali ya Mungu, na kwamba hasira Yake kali imetiwa najisi? Je, utamchafulia Mungu jina, ukisema kwamba tabia Yake si ya haki kwa ujumla? Wakati unaposhughulikia kila mojawapo ya vitendo vya Mungu, lazima uwe na hakika kwamba tabia ya haki ya Mungu iko huru dhidi ya vipengele vingine vyovyote, kwamba ni takatifu na haina dosari; vitendo hivi vinajumuisha binadamu kuweza kuangushwa chini, kuadhibiwa na kuangamizwa na Mungu. Bila kuacha, kila kimojawapo cha vitendo vya Mungu kinatekelezwa kulingana na tabia yake ya asili na mpango Wake—hii haijumuishi maarifa ya binadamu, mila na falsafa—na kila kimojawapo cha vitendo vya Mungu ni maonyesho ya tabia Yake na hali halisi, isiyohusiana na chochote kinachomilikiwa na binadamu aliyepotoka. Katika dhana za binadamu, ni upendo, huruma na uvumilivu wa Mungu tu kwa binadamu ndivyo visivyokuwa na dosari, ambavyo havijatiwa najisi na vilivyo vitakatifu. Hata hivyo, hakuna anayejua kwamba ghadhabu ya Mungu na hasira Yake vilevile vyote havijatiwa najisi; aidha, hakuna yule aliyefikiria maswali kama vile: kwa nini Mungu havumilii kosa lolote au kwa nini ghadhabu Yake ni kubwa mno. Kinyume ni kwamba, baadhi ya watu hukosa kuelewa hasira ya Mungu na kudhania kuwa ni hasira kali ya binadamu waliopotoka: wanaelewa ghadhabu ya Mungu kuwa hasira kali ya binadamu waliopotoka; wao hata hudhania kimakosa kwamba hasira kali ya Mungu ni sawa tu na ufunuo wa kiasili wa tabia potovu ya binadamu. Wanasadiki kimakosa kwamba utoaji wa hasira ya Mungu ni sawa tu na ghadhabu ya binadamu waliopotoka, jambo linalotokana na kutoridhika; wanasadiki hata kwamba utoaji wa hasira ya Mungu ni maonyesho ya hali Yake ya moyo. Baada ya kikao hiki cha ushirika, Ninatumai kwamba kila mmoja wenu hatakuwa tena na dhana potovu, fikira au kukisia kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu, na Natumai baada ya kusikiliza maneno Yangu mnaweza kuwa na utambuzi wa kweli wa hasira ya tabia ya haki ya Mungu katika mioyo yenu, kwamba mnaweza kuweka pembeni kuelewa kokote kwa awali kulikofikiriwa vinginevyo kuhusiana na hasira ya Mungu, kwamba mnaweza kubadilisha imani zenu binafsi zilizopotoka na mitazamo ya hali halisi ya hasira ya Mungu. Vilevile, Natumai kwamba mnaweza kuwa na ufafanuzi sahihi wa tabia ya Mungu katika mioyo yenu, kwamba hamtakuwa tena na mashaka yoyote kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu, na kwamba hamtatumia kuwaza kokote kwa binadamu au kufikiria kuhusu tabia ya kweli ya Mungu. Tabia ya haki ya Mungu ni hali halisi ya kweli ya Mungu mwenyewe. Si kitu kilichotungwa au kuandikwa na binadamu. Tabia Yake ni tabia Yake ya haki na haina uhusiano au miunganisho yoyote na uumbaji wowote ule. Mungu Mwenyewe ni Mungu Mwenyewe. Hatawahi kuwa sehemu ya uumbaji, na hata kama Atakuwa mwanachama miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa, tabia Yake ya asili na hali halisi Yake havitabadilika. Hivyo basi, kumjua Mungu si kujua kifaa; si kuchunguza kitu, wala si kuelewa mtu. Kama mwanadamu atatumia dhana au mbinu yake ya kujua kifaa au kuelewa mtu ili kumjua Mungu, basi hutawahi kuweza kutimiza maarifa ya Mungu. Kumjua Mungu hakutegemei uzoefu au kufikiria kwako, na hivyo basi hufai kulazimisha uzoefu wako au kufikiria kwako kwa Mungu. Haijalishi uzoefu au kufikiria kwako ni kwa kipekee namna gani, huko kote bado ni finyu; na hata zaidi, kufikiria kwako hakulingani na hoja, isitoshe hakulingani na ukweli, na pia hakulingani na tabia na hali halisi ya kweli ya Mungu. Hutawahi kufanikiwa kama utategemea kufikiria kwako ili kuelewa hali halisi ya Mungu. Njia ya pekee ni hivi: kukubali yote yanayotoka kwa Mungu, kisha kwa utaratibu uweze kuyapitia na kuyaelewa. Kutakuwa na siku ambayo Mungu atakupa nuru ili uweze kuelewa kwa kweli na kumjua Yeye kwa sababu ya ushirikiano wako na kwa sababu ya hamu yako ya kutaka ukweli. Na kwa haya, hebu na tuhitimishe sehemu hii ya mazungumzo yetu.

Binadamu Hupata Huruma na Uvumilivu wa Mungu Kupitia kwa Toba ya Dhati

Kinachofuata ni hadithi ya biblia ya “Wokovu wa Mungu kwa Ninawi.”

Yona 1:1-2 Sasa neno la Yehova likaja kwa Yona mwana wa Amitai, likisema, Amka, nenda Ninawi, mji mkuu, na uipigie kelele, kwani uovu wao umeenda juu mbele Yangu.

Yona 3 Neno lake Yehova likakuja kwake Yona kwa mara ya pili, likisema, Inuka, nenda Ninawi, mji huo mkuu; na uuhubirie mahubiri ninayokuambia. Kwa hivyo Yona akainuka, na kuenda Ninawi, kulingana na neno la Yehova. Sasa Ninawi ulikuwa mji mkuu wa safari ya siku tatu. Naye Yona akaanza kuingia ndani ya mji huo safari ya siku moja, na akatoa sauti kubwa, na kusema, Imebaki siku arobaini, na Ninawi utashindwa. Basi watu wa hapo Ninawi wakamwamini Mungu, na wakatangaza mfungo, na wakavalia nguo za magunia, kuanzia aliyekuwa mkubwa zaidi kwao mpaka aliyekuwa mdogo zaidi. Kwa kuwa habari ilimfikia mfalme wa Ninawi, na akainuka kutoka kwa kiti chake che enzi, na akaivua nguo yake, na kuvaa nguo ya gunia, na kukaa chini katika majivu. Na akafanya kutangazwe Ninawi kupitia amri yake mfalme na wakubwa wake, ikisema, Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: Ila mwanadamu na mnyama wavikwe kwa nguzo za magunia, na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao. Nani anayejua iwapo Mungu atabadili na kughairi, na kuiacha ghadhabu Yake iliyo kali, ili tusiangamie? Naye Mungu aliona vitendo vyao, kwamba walikuwa wameiacha njia yao ovu; na Mungu akaghairi lile neno ovu, ambalo Alikuwa amesema Angeliwafanyia; na Aakulifanya.

Yona 4 Lakini lilimwudhi Yona mno, naye alikuwa na hasira sana. Na akaomba kwa Yehova, na kusema, Nakuomba, Ee Yehova, hivi sivyo nilivyonena, nilipokuwa bado katika nchi yangu? Kwa hivyo nilitorokea Tarshishi kabla: kwa sababu nilijua kwamba Wewe ni Mungu wa neema, na mwenye huruma, asiyekasirika haraka, na wa rehema kubwa, na Wewe unaghairi maovu. Kwa hivyo sasa, Ee Yehova, chukua, nakusihi, uhai wangu kutoka kwangu; kwa sababu ni heri nikufe kuliko kuishi. Kisha Yehova akasema, Je, unafanya vizuri kukasirika? Hivyo Yona akatoka nje ya mji, na kuketi katika upande wa mashariki wa mji, na huko akajitengenezea kibanda, na akaketi chini yake katika kivuli, mpaka aweze kuona kile kingefanyikia mji huo. Naye Yehova Mungu akatayarisha mtango, na akaufanya ukuje juu yake Yona, ili uweze kuwa kivuli juu ya kichwa chake, na kumwokoa kutoka katika huzuni yake. Kwa hivyo Yona akawa na furaha sana juu ya ule mtango. Lakini Mungu akatayarisha buu siku iliyofuata wakati kulipopambazuka, nalo likaula ule mtango hadi ukanyauka. Na hivyo ikatimia, wakati jua lilipopanda, kwamba Mungu akautayarisha upepo mkali wa mashariki; na jua likapiga kichwa chake Yona, kiasi kwamba alizimia, naye akatamani afe, na akasema, Ni heri mimi nife kuliko niishi. Mungu akasema kwa Yona, Je, unafanya vizuri kukasirika kwa sababu ya mtango? Na yeye akasema, naam, nafanya vizuri kukasirika, hata mpaka kufa. Kisha Yehova akasema, Umeuonea mtango huruma, ambao hujafanyia kazi, wala kuukuza; ambao ulimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini ndani yake ambao hawawezi kutambua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo wengi?

Muhtasari wa Hadithi ya Ninawi

Ingawaje hadithi ya “wokovu wa Mungu wa Ninawi” ni fupi kwa urefu, inaruhusu mtu kuweza kuona kidogo tu ule upande mwingine wa tabia ya haki ya Mungu. Ili kuweza kuelewa haswa upande huo unajumuisha nini, lazima turudi kwenye Maandiko na kuangalia nyuma katika mojawapo ya matendo ya Mungu.

Hebu kwanza tuangalie mwanzo wa hadithi hii: “Sasa neno la Yehova likaja kwa Yona mwana wa Amitai, likisema, Amka, nenda Ninawi, mji mkuu, na uipigie kelele, kwani uovu wao umeenda juu mbele Yangu” (Yona 1:1-2). Katika fungu hili kutoka kwenye Maandiko, tunajua kwamba Yehova Mungu alimwamuru Yona kwenda katika mji wa Ninawi. Kwa nini alimwamuru Yona kwenda katika mji huo? Biblia iko wazi kabisa kuhusu suala hili: Maovu ya watu walio ndani ya mji huo yalikuwa yamefikia macho ya Yehova Mungu, na hivyo basi Alimtuma Yona ili kuwatangazia kile Alichonuia kufanya. Ingawa hakuna kitu kilichorekodiwa kinachotwambia Yona alikuwa nani, jambo hili, bila shaka, halina uhusiano wowote na kumjua Mungu. Hivyo basi, huhitaji kumwelewa mwanamume huyu. Unahitaji kujua tu kile ambacho Mungu alimwamuru Yona kufanya na kwa nini Alifanya kitu hicho.

Onyo la Yehova Mungu Lawafikia Waninawi

Hebu tuendelee hadi kwenye fungu la pili, sura ya tatu ya kitabu cha Yona: “Naye Yona akaanza kuingia ndani ya mji huo safari ya siku moja, na akatoa sauti kubwa, na kusema, Imebaki siku arobaini, na Ninawi utashindwa.” Haya ndiyo maneno ambayo Mungu alipitisha moja kwa moja kwake Yona ili aweze kuwaambia Waninawi. Ndiyo pia, kwa kawaida, maneno ambayo Yehova alipenda kusema kwa Waninawi. Maneno haya yanatwambia kwamba Mungu alianza kukerwa na kuchukia watu wa mji huu kwa sababu ya maovu yao yaliyokuwa yamefika machoni pa Mungu, na hivyo basi, Alipenda kuuangamiza mji huo. Hata hivyo, kabla ya Mungu kuangamiza mji, Aliwatangazia Waninawi, na hapo kwa hapo Akawapa fursa ya kutubu maovu yao na kuanza upya. Fursa hii ingedumu kwa siku arubaini. Kwa maneno mengine, kama watu waliokuwa ndani ya mji huu wasingetubu, na kukubali dhambi au maovu yao wenyewe mbele ya Yehova Mungu ndani ya siku arubaini, Mungu angeangamiza mji huu kama Alivyoangamiza Sodoma. Hivi ndivyo ambavyo Yehova Mungu alipenda kuwaambia watu wa Ninawi. Ni wazi kwamba, hili halikuwa tangazo rahisi. Halikuweza tu kuonyesha hasira ya Yehova Mungu, lakini pia lilionyesha mtazamo Wake kwa wale Waninawi; wakati uo huo tangazo hili rahisi lilitumika kama onyo kali kwa watu waliokuwa wakiishi ndani ya mji huo. Onyo hili liliwaambia kwamba matendo yao maovu yalikuwa yamewafanya kuchukiwa na Yehova Mungu na liliwaambia kwamba matendo yao maovu yangewaletea hivi karibuni fedheha kutokana na maangamizo yao wenyewe; kwa hivyo, maisha ya kila mmoja kule Ninawi yalikuwa karibu kuangamia.

Utofautishaji Mkavu Katika Mwitikio wa Ninawi na Sodoma kwa Onyo la Yehova Mungu

Kupinduliwa kunamaanisha nini? Kwa muktadha wa mazungumzo, kunamaanisha kutoweka. Lakini kwa njia gani? Ni nani angefanya mji mzima kupinduliwa? Haiwezekani kwa binadamu kufanya kitendo kama hicho, bila shaka. Watu hawa hawakuwa wajinga; mara tu waliposikia matangazo haya, walipata wazo hilo. Walijua kwamba yalikuwa yametoka kwa Mungu; walijua kwamba Mungu angetekeleza kazi Yake; walijua kwamba maovu yao yalikuwa yamemkasirisha Yehova Mungu na kumfanya kuwa na hasira kali kwao, ili waweze kuangamizwa pamoja na mji wao. Je, watu wa mji huo walichukulia vipi suala hilo baada ya kusikiliza onyo la Yehova Mungu? Biblia inafafanua kwa maelezo fafanuzi namna ambavyo watu hawa walivyoitikia, kuanzia kwa mfalme wao hadi kwa binadamu wa kawaida. Kama ilivyorekodiwa kwenye Maandiko: “Basi watu wa hapo Ninawi wakamwamini Mungu, na wakatangaza mfungo, na wakavalia nguo za magunia, kuanzia aliyekuwa mkubwa zaidi kwao mpaka aliyekuwa mdogo zaidi. Kwa kuwa habari ilimfikia mfalme wa Ninawi, na akainuka kutoka kwa kiti chake che enzi, na akaivua nguo yake, na kuvaa nguo ya gunia, na kukaa chini katika majivu. Na akafanya kutangazwe Ninawi kupitia amri yake mfalme na wakubwa wake, ikisema, Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: Ila mwanadamu na mnyama wavikwe kwa nguzo za magunia, na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao. …”

Baada ya kusikia tangazo la Yehova Mungu, watu wa Ninawi walionyesha mtazamo uliokuwa kinyume kabisa na ule wa watu wa Sodoma—watu wa Sodoma walimpinga Mungu waziwazi, huku wakiendelea kutoka kwa maovu hadi maovu, lakini baada ya kusikia maneno haya, Waninawi hawakupuuza suala hilo, wala hawakuweza kulipinga; badala yake walimsadiki Mungu na kutangaza kufunga. “Walisadiki” inarejelea nini hapa? Neno lenyewe linapendekeza imani na unyenyekevu. Kama tutatumia tabia halisi ya Waninawi kuelezea neno hili, inamaanisha kwamba walisadiki Mungu anaweza na angeweza kufanya vile Alivyosema, na kwamba walikuwa radhi kutubu. Je, watu wa Ninawi walihisi woga mbele ya janga lililokuwa karibu kutokea? Imani yao ndiyo iliyotia woga katika mioyo yao. Kwa kweli, ni nini tunachoweza kutumia kuthibitisha Imani na woga wa Waninawi? Ni sawa na vile Biblia inavyosema: “na wao wakatangaza kufunga, na wakavalia nguo ya gunia, kuanzia wale walio wakubwa zaidi na hata kwa wale walio wadogo zaidi.” Hivi ni kusema kwamba Waninawi walisadiki kweli, na kwamba kutoka kwenye imani hii woga uliibuka, ambao sasa ulisababisha kufunga na kuvaliwa kwa nguo ya gunia. Hivi ndivyo walivyoonyesha mwanzo wa toba yao. Tofauti kabisa na watu wa Sodoma, Waninawi hawakumpinga Mungu tu, bali walionyesha pia waziwazi toba yao kupitia kwa tabia na matendo yao. Bila shaka, hii haikutumika tu kwa watu wa kawaida wa Ninawi; hata mfalme wao hakubakizwa.

Toba ya Mfalme wa Ninawi Inapata Sifa ya Yehova Mungu

Wakati mfalme wa Ninawi alipozisikia habari hizi, aliinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua nguo zake, akavalia nguo ya gunia na kukalia jivu. Kisha akatangaza kwamba hakuna mtu kwenye mji huo ambaye angeruhusiwa kuonja chochote, na kuwa hakuna mifugo, wanakondoo na ng’ombe ambao wangekunywa maji na kula nyasi. Binadamu na mifugo kwa pamoja walitakikana kujifunika nguo ya gunia; nao watu wangemsihi Mungu kwa uaminifu. Mfalme pia alitangaza kwamba watu wote wangetupilia mbali njia zao za maovu na kukataa udhalimu ulioko mikononi mwao. Tukifanya uamuzi kutoka kwenye misururu ya vitendo hivi, mfalme wa Ninawi alionyesha toba yake ya dhati. Misururu ya vitendo alivyofanya—kutoka kwenye kiti chake cha ufalme, kulitupa joho lake la kifalme, kuvalia nguo ya gunia na kukalia majivu—kulionyesha watu kwamba mfalme wa Ninawi aliweka kando hadhi yake ya kifalme na kuvalia nguo ya gunia pamoja na watu wa kawaida wa nchi. Hii ni kusema kwamba mfalme wa Ninawi hakuweza kushikilia wadhifa wake wa kifalme ili aendelee na njia zake za maovu au udhalimu katika mikono yake baada ya kikao cha tangazo kutoka kwa Yehova Mungu; badala yake, aliweka pembeni mamlaka aliyoyashikilia na kutubu mbele ya Yehova Mungu. Kwenye kipindi hiki cha muda, mfalme wa Ninawi hakuwa akitubu akiwa mfalme; alikuwa amekuja mbele ya Mungu kuungama na kutubu dhambi zake akiwa binadamu wa kawaida wa Mungu. Aidha, aliuambia mji mzima kuungama na kutubu dhambi zao mbele ya Yehova Mungu kwa njia sawa na yeye; vilevile, alikuwa na mpango mahususi wa namna ya kufanya hivyo kama inavyoonekana kwenye Maandiko: “Mtu wala mnyama, wala kundi la ng’ombe, wala kundi la kondoo wasionje chochote: wasikule, wala kunywa maji: … na kulia kwa nguvu kwa Mungu: ndiyo, na wawageuze watu wote kutoka kwa njia ovu, na kutoka kwa vurugu iliyo mikononi mwao.” Kama kiongozi wa mji, mfalme wa Ninawi alimiliki hadhi na nguvu za kimamlaka na angefanya chochote alichopenda. Alipokabiliwa na tangazo la Yehova Mungu, angeweza kupuuza suala hilo au kutubu na kuungama tu dhambi zake pekee; kuhusiana na kama watu wa mji wangechagua kutubu au la, angepuuza suala hili kabisa. Hata hivyo, mfalme wa Ninawi hakufanya hivyo kamwe. Mbali na kuinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, kuvalia nguo ya gunia na kujipaka jivu na kuungama na kutubu dhambi zake mbele ya Yehova Mungu, aliweza pia kuwaamuru watu na mifugo ndani ya mji huo kufanya hivyo. Aliweza hata kuamuru watu “kumlilia Mungu kwa nguvu.” Kupitia misururu hii ya vitendo, mfalme wa Ninawi aliweza kukamilisha kwa kweli kile ambacho kiongozi anafaa kufanya; misururu ya vitendo vyake ndiyo iliyokuwa migumu kwa mfalme yeyote katika historia ya binadamu kutimiza, hatua na pia hatua ambayo hakuna aliyewahi kutimiza. Matendo haya yanaweza kuitwa shughuli isiyo na kifani katika historia ya binadamu; yanastahili kukumbukwa na kuigwa na binadamu. Tangu enzi ya mwanadamu, kila mfalme alikuwa amewaongoza wafuasi wake kukinzana na kumpinga Mungu. Hakuna yule aliyewahi kuwaongoza wafuasi wake kusihi Mungu kutafuta ukombozi kwa ajili ya maovu yao, kupokea msamaha wa Yehova Mungu na kuepuka adhabu kali. Mfalme wa Ninawi, hata hivyo, aliweza kuwaongoza raia wake kumlilia Mungu, kuacha njia zao mbalimbali za maovu na kutupilia mbali udhalimu ulio mikononi mwao. Aidha, aliweza pia kuweka kando kiti chake cha enzi, na badala yake, Yehova Mungu alibadilisha na kughairi na kugeuza hasira Yake, na kuruhusu watu wa mji huu kuishi na kuwalinda dhidi ya kuangamia. Matendo ya mfalme yanaweza kuitwa tu muujiza wa nadra katika historia ya binadamu; yanaweza hata kuitwa kielelezo cha binadamu uliopotoka unaoungama na kutubu dhambi zake mbele ya Mungu.

Mungu Aona Kutubu kwa Dhati katika Vina vya Mioyo ya Waninawi

Baada ya kusikiliza tangazo la Mungu, mfalme wa Ninawi na raia Wake walitekeleza misururu ya vitendo. Je, ni nini asili ya tabia na matendo yao? Kwa maneno mengine, ni nini kiini cha uzima wa mwenendo wao? Kwa nini walifanya kile walichofanya? Katika macho ya Mungu walikuwa wametubu kwa dhati, si tu kwa sababu walikuwa wamemsihi Mungu kwa dhati na kuungama dhambi zao mbele Yake, lakini pia kwa sababu walikuwa wameacha mwenendo wao wenye maovu. Walichukua hatua namna hii kwa sababu baada ya kusikia matamshi ya Mungu, walitishika pakubwa na kusadiki kwamba angefanya vile ambavyo alikuwa amesema. Kwa kufunga, kuvalia nguo ya gunia na kukalia jivu, walipenda kuonyesha namna walivyokuwa radhi kubadilisha njia zao na kujizuia na maovu, kumwomba Yehova Mungu kuzuia hasira Yake, kusihi Yehova Mungu kutupilia mbali uamuzi Wake, pamoja na msiba mkuu ambao ulikuwa karibu kuwasibu. Kupitia uchunguzi wa tabia yao yote, tunaona ya kwamba tayari walielewa kwamba vitendo vyao vya awali vilimchukiza Yehova Mungu na kwamba walielewa sababu iliyomfanya kutaka kuwaangamiza hivi karibuni. Kwa sababu hizi, wote walipenda kutubu kabisa, kugeuka na kuacha njia zao za maovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Kwa maneno mengine, pindi tu walipotambua tangazo la Yehova Mungu, kila mmoja wao alihisi woga katika mioyo yao; hawakuendelea tena na mwenendo wao wa maovu wala kuendelea kutenda vitendo ambavyo Yehova Mungu alichukia. Vilevile, walimsihi Yehova Mungu kusamehe dhambi zao za kale na kutowatendea kulingana na vitendo vyao vya kale. Walikuwa radhi kutowahi kujihusisha tena katika maovu na kutenda kulingana na maagizo ya Yehova Mungu, kama tu wasingewahi kumkasirisha Yehova Mungu. Toba yao ilikuwa ya dhati na ya kweli. Ilitoka kwenye kina cha mioyo yao na haikuwa ya kujidanganya, wala haikuwa ya muda.

Baada ya watu wa Ninawi, kutoka kwa mfalme mwenye mamlaka hadi kwa raia wake, kujua kwamba Yehova Mungu alikuwa amewakasirikia, kila mojawapo ya vitendo vyao, tabia yao nzima, pamoja na kila mojawapo ya uamuzi na machaguo yao vilikuwa wazi na dhahiri mbele ya Mungu. Moyo wa Mungu ulibadilika kulingana na tabia yao. Akili Zake Mungu zilikuwa zinafikiria nini wakati huo? Biblia inaweza kukujibia swali hili. Maneno yafuatayo yalirekodiwa katika maandiko: “Naye Mungu aliona vitendo vyao, kwamba walikuwa wameiacha njia yao ovu; na Mungu akaghairi lile neno ovu, ambalo Alikuwa amesema Angeliwafanyia; na Hakulifanya.” Ingawaje Mungu alibadilisha fikira Yake, hakukuwa na chochote kigumu kuhusu mtazamo wa fikira Yake. Aliweza kubadilika kutoka katika kuonyesha hasira Yake hadi kutuliza hasira Yake, na kisha kuamua kutouleta msiba mkuu katika mji wa Ninawi. Sababu ya uamuzi wa Mungu wa—kuwaokoa Waninawi dhidi ya msiba wao mkuu—ilikuwa ya haraka mno, ni kwa sababu Mungu aliangalia moyo wa kila mmoja wa wale Waninawi. Aliona kwamba katika kina cha mioyo yao waliweza: kuungama na kutubu kwa dhati dhambi zao, imani yao ya dhati kwake Yeye, mtazamo wao wa kina kuhusu vile vitendo vyao vya maovu vilikuwa vimeipa tabia Yake hasira kali, na woga uliotokana na adhabu ya Yehova Mungu iliyokuwa inakaribia. Wakati uo huo, Yehova Mungu aliweza kusikia maombi kutoka kwenye kina cha mioyo yao wakimsihi kusitisha hasira Yake dhidi yao ili waweze kuepuka msiba huu mkuu. Wakati Mungu alipoangalia hoja hizi zote, kwa utaratibu hasira yake ilitoweka. Licha ya vile hasira yake ilivyokuwa kuu hapo awali, alipoona kutubu kwao kwa dhati ndani ya kina cha mioyo ya watu hawa, moyo Wake uliguswa na hili, na kwa hivyo Hakuweza kuvumilia kuwaletea msiba mkuu, na Alisitisha hasira yake kwao. Badala yake Aliendelea kuwaonyesha huruma Yake na uvumilivu kwao na akaendelea kuwaongoza na kuwakimu.

Kama Imani Yako kwa Mungu ni ya Kweli, Utapokea Utunzaji Wake Mara Nyingi

Mungu kubadilisha nia Zake kwa watu wa Ninawi hakukuhusisha kusitasita au kutoeleweka kokote. Badala yake kulikuwa ni mabadiliko kutoka kwa hasira tupu hadi uvumilivu mtupu. Huu ni ufunuo wa kweli wa kiini cha Mungu. Mungu kamwe si wa kusitasita au asiye na uamuzi katika vitendo Vyake; kanuni na makusudio yaliyo katika matendo Yake yote ni wazi na dhahiri, yasiyo na dosari wala doa, yasiyo kabisa na hila ama njama zozote zilizochanganywa ndani. Kwa maneno mengine, kiini cha Mungu hakina giza wala maovu. Mungu alikasirikia Waninawi kwa sababu vitendo vyao viovu vilikuwa vimefikia macho Yake; wakati ule hasira Yake ilitokana na kiini Chake. Hata hivyo, wakati hasira ya Mungu ilitoweka na akatoa uvumilivu Wake kwa watu wa Ninawi kwa mara nyingine tena, kila kitu Alichofichua kilikuwa bado ni kiini Chake. Uzima wa badiliko hili ulitokana na badiliko katika mtazamo wa mwanadamu kwa Mungu. Katika kipindi hiki chote cha muda, tabia ya Mungu isiyokosewa haikubadilika; kiini cha Mungu cha uvumilivu hakikubadilika; kiini cha Mungu cha upendo na huruma hakikubadilika. Wakati watu wanapotekeleza vitendo viovu na kumkosea Mungu atawashushia ghadhabu Yake. Wakati watu wanatubu kwa kweli, moyo wa Mungu utabadilika, na hasira Yake itakoma. Wakati watu wanapoendelea kumpinga Mungu kwa ukaidi, hasira Yake kali haitakoma; hasira Yake itawalemea hatua kwa hatua mpaka watakapoangamizwa. Hiki ndicho kiini cha tabia ya Mungu. Haijalishi kama Mungu anaonyesha hasira au huruma na wema, mwenendo wa binadamu, tabia na mtazamo wake kwa Mungu ndani ya kina cha moyo wake vinaamrisha kile ambacho kinaonyeshwa kupitia kwa ufunuo wa tabia ya Mungu. Kama Mungu anaendelea kumfanya mtu apitie hasira Yake, moyo wa mtu huyu bila shaka humpinga Mungu. Kwa sababu hajawahi kutubu kwa kweli, kuinamisha kichwa chake mbele ya Mungu au kumiliki imani ya kweli kwa Mungu, hajawahi kupata huruma na uvumilivu wa Mungu. Kama mtu hupokea utunzaji wa Mungu mara nyingi na hupokea huruma na uvumilivu Wake mara nyingi, basi mtu huyo bila shaka anaamini Mungu kwa kweli ndani ya moyo wake, na moyo wake haumpingi Mungu. Yeye kwa mara nyingi anatubu kwa kweli mbele ya Mungu; kwa hivyo, hata kama nidhamu ya Mungu mara nyingi humshukia mtu huyu, hasira Yake haitamshukia.

Maelezo haya mafupi yanaruhusu watu kuuona moyo wa Mungu, kuona uhalisi wa kiini Chake, kuona kwamba ghadhabu ya Mungu na mabadiliko katika moyo Wake yana sababu. Licha ya utofautishaji mkavu ambao Mungu alionyesha Alipoghadhabishwa na wakati Alipobadilisha moyo Wake, jambo ambalo linafanya watu kusadiki kwamba utofautishaji mkavu au nafasi kubwa yaonekana kuwepo kati ya vipengele hivi viwili vya kiini cha Mungu—ghadhabu Yake na uvumilivu Wake—mtazamo wa Mungu kwa kule kutubu kwa Waninawi kwa mara nyingine kunaruhusu watu kuweza kuona ule upande mwingine wa tabia halisi ya Mungu. Mabadiliko katika moyo wa Mungu yanaruhusu kwa kweli binadamu kwa mara nyingine kuuona ukweli wa huruma na wema wa Mungu na kuona ufunuo wa kweli wa kiini cha Mungu. Binadamu hawana budi kutambua kwamba rehema ya Mungu na wema si hadithi za uwongo tu, wala si ughushi. Hii ni kwa sababu hisia za Mungu kwa wakati huo zilikuwa kweli; Mabadiliko ya moyo wa Mungu yalikuwa kweli; Mungu kwa kweli aliwapa binadamu kwa mara nyingine tena rehema na uvumilivu Wake.

Toba ya Kweli Ndani ya Mioyo ya Waninawi Inawapa Rehema ya Mungu na Kubadilisha Hatima Zao Wenyewe

Je, kulikuwa na ukinzani wowote kati ya mabadiliko ya moyo wa Mungu na hasira Yake? Bila shaka la! Hii ni kwa sababu uvumilivu wa Mungu wakati ule maalum ulikuwa na sababu yake. Je, sababu yake yaweza kuwa nini? Ni ile iliyotolewa katika Biblia: “Kila mtu aligeuka kutoka kwenye njia yake ovu” na “kuacha vurugu iliyokuwa mikononi mwake.”

Hii “njia ovu” hairejelei kiasi kidogo cha vitendo viovu, lakini inarejelea chanzo cha maovu katika tabia ya watu. “Kugeuka kutoka njia yake ovu” kunamaanisha kwamba wale wanaozungumziwa hawatawahi kutekeleza vitendo hivi tena. Kwa maneno mengine, hawatawahi kutenda kwa njia hii ovu tena; mbinu, chanzo, kusudio, nia na kanuni za vitendo vyao vyote vimebadilika; hawatawahi tena kutumia mbinu na kanuni hizi kuleta nafuu na furaha mioyoni mwao. Kule “kuacha” katika “kuacha vurugu iliyo mikononi mwake” kunamaanisha kuweka chini au kuweka pembeni, kujitenga kabisa na mambo ya kale na kutorudi nyuma tena. Wakati watu wa Ninawi walipoacha vurugu iliyokuwa mikononi mwao, hii ilithibitisha na vilevile iliwakilisha toba yao ya kweli. Mungu huangalia kwa makini sehemu ya nje ya watu na vilevile mioyo yao. Wakati Mungu alipoangalia kwa makini toba ya kweli katika mioyo ya Waninawi bila kuuliza swali na pia kutambua kwamba walikuwa wameacha njia zao ovu na kuacha vurugu iliyokuwa mikononi mwao, Alibadilisha moyo Wake. Hivi ni kusema kwamba mwenendo na tabia ya watu hawa na njia mbalimbali za kufanya mambo, pamoja na ungamo na toba ya dhambi ya kweli zilizokuwa mioyoni mwao, kulisababisha Mungu kubadilisha moyo Wake, kubadilisha nia Zake, kufuta uamuzi Wake na kutowaadhibu wala kuwaangamiza. Kwa hivyo, watu wa Ninawi waliweza kufikia hatima tofauti. Waliyakomboa maisha yao binafsi na wakati uo huo wakapata huruma na uvumilivu wa Mungu, na wakati huo Mungu pia alifuta hasira Yake.

Huruma na Uvumilivu wa Mungu si Nadra—Toba ya Kweli ya Mwanadamu Ndiyo Nadra

Licha ya vile ambavyo Mungu alikuwa na ghadhabu kwa Waninawi, mara tu walipotangaza kufunga na kuvalia nguo ya gunia pamoja na jivu, moyo Wake ulianza kutulia taratibu, na Akaanza kubadilisha moyo Wake. Wakati Alipowatangazia kwamba Angeangamiza mji wao—ule muda kabla ya kuungama na kutubu kwao kwa dhambi zao—Mungu alikuwa angali na ghadhabu na wao. Baada ya wao kupitia mfululizo wa vitendo vya kutubu, ghadhabu ya Mungu kwa watu wa Ninawi ikabadilika kwa utaratibu kuwa huruma na uvumilivu kwao. Hakuna kitu kinachohitilafiana kuhusu ufunuo wenye ulinganifu wa vipengele hivi viwili vya tabia ya Mungu katika tukio lilo hilo. Ni vipi ambavyo mtu anafaa kuelewa na kujua ukosefu huu wa kuhitilafiana? Mungu alionyesha na kufichua viini hivi viwili tofauti kabisa kwa mfululizo wakati watu wa Ninawi walipokuwa wakitubu na Akawaruhusu watu kuona uhalisi na kutokosewa kwa kiini cha Mungu. Mungu alitumia mtazamo Wake kuambia watu yafuatayo: Si kwamba Mungu havumilii watu, au hataki kuwaonyesha huruma; ni kwamba wao hutubu kwa kweli mara nadra kwa Mungu, na ni nadra kwa watu kugeuka kwa kweli kutoka kwa njia zao ovu na kuacha vurugu iliyo mikononi mwao. Kwa maneno mengine, wakati Mungu ameghadhabishwa na binadamu, Anatumaini kwamba binadamu ataweza kutubu kwa kweli na Anatumaini kumwona binadamu akitubu kwa kweli, ambapo Ataendelea kumpa binadamu huruma na uvumilivu Wake kwa ukarimu. Hivi ni kusema kwamba mwenendo mbovu wa mwanadamu ndio husababisha hasira ya Mungu, huku nazo rehema na uvumilivu wa Mungu zikipewa wale wanaomsikiliza Mungu na kutubu kwa kweli mbele Yake, kwa wale wanaoweza kugeuka kutoka kwa njia zao ovu na kuacha vurugu iliyo mikononi mwao. Mtazamo wa Mungu ulifichuliwa waziwazi sana katika jinsi Alivyowatendea Waninawi: Huruma na uvumilivu wa Mungu si vigumu kuvipokea hata kidogo; Anahitaji toba ya kweli ya mtu. Mradi tu watu wageuka kutoka kwa njia zao ovu na kuuacha vurugu iliyo mikononi mwao, Mungu atabadilisha moyo Wake na kubadilisha mtazamo Wake kwao.

Tabia ya Haki ya Muumba ni ya Kweli na Wazi

Wakati Mungu alibadilisha moyo Wake kwa minajili ya watu wa Ninawi, je, huruma na uvumilivu Wake ulikuwa wa bandia? Bila shaka la! Basi mabadiliko kati ya vipengele hivi viwili vya tabia ya Mungu katika suala lili hili yanakuruhusu kuona nini? Tabia ya Mungu ni kamili kabisa; haijagawanywa hata kidogo. Licha ya kama Anaonyesha ghadhabu au huruma na uvumilivu kwa watu, haya yote ni maonyesho ya tabia Yake ya haki. Tabia ya Mungu ni kweli na wazi. Yeye hubadilisha fikira na mitazamo Yake kulingana na maendeleo ya mambo. Mabadiliko ya mtazamo Wake kwa Waninawi yanawaambia binadamu kwamba Anazo fikira na mawazo Yake mwenyewe; Yeye si roboti au sanamu ya udongo, bali Yeye ni Mungu Mwenyewe mwenye uhai. Angeweza kuwa na ghadhabu kwa watu wa Ninawi, sawa tu na vile ambavyo Angeweza kusamehe dhambi zao za kale kulingana na mitazamo yao; Angeweza kuamua kuwaletea Waninawi msiba na Angeweza kubadilisha uamuzi Wake kwa sababu ya kutubu kwao. Watu hupenda kutumia sheria bila kupinda na kutumia sheria kama hizo ili kumwekea mipaka na kumfafanua Mungu, sawa tu na vile watu wanavyopendelea kutumia fomyula ili kujua tabia ya Mungu. Kwa hivyo, kulingana na himaya ya fikira za binadamu, Mungu hafikirii wala Yeye hana mawazo yoyote halisi. Kwa uhalisi, fikira za Mungu zinabadilika siku zote kulingana na mabadiliko katika mambo, na mazingira; huku fikira hizi zikiwa zinabadilika, vipengele tofauti vya kiini cha Mungu vitafichuliwa. Katika kipindi hiki cha mabadiliko, wakati ule Mungu hubadilisha moyo Wake, Yeye hufichulia mwanadamu ukweli wa uwepo wa maisha Yake na kufichua kwamba tabia Yake ya haki ni halisi na wazi. Aidha, Mungu hutumia ufunuo Wake mwenyewe wa kweli kuthibitisha kwa mwanadamu ukweli wa uwepo wa hasira Yake, huruma Yake, wema Wake na uvumilivu Wake. Kiini Chake kitafichuliwa wakati wowote na mahali popote kulingana na maendeleo ya mambo. Anamiliki hasira ya simba na huruma na uvumilivu wa mama. Tabia Yake ya haki hairuhusiwi kushukiwa, kukiukwa, kubadilishwa au kupotoshwa na mtu yeyote. Miongoni mwa masuala yote na mambo yote, tabia ya haki ya Mungu, yaani, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, vyote vinaweza kufichuliwa wakati wowote na mahali popote. Anaonyesha waziwazi vipengele hivi katika kila sehemu ya asili na kuzitekeleza kila wakati kwa uwazi. Tabia ya haki ya Mungu haiwekewi mipaka na muda au nafasi, au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Mungu haionyeshwi bila kufikiri au kufichuliwa kama inavyoongozwa na mipaka ya muda au nafasi. Badala yake, tabia ya haki ya Mungu inaonyeshwa kwa njia huru na kufichuliwa mahali popote na wakati wowote. Unapoona Mungu akibadilisha moyo Wake na kukoma kuonyesha hasira Yake na kujizuia dhidi ya kuuangamiza mji wa Ninawi, je, unaweza kusema kwamba Mungu ni mwenye huruma na upendo tu? Je, unaweza kusema kwamba hasira ya Mungu inajumuisha maneno matupu? Wakati Mungu anapoonyesha hasira kali na kuiondoa huruma Yake, je, unaweza kusema kwamba Hana hisia zozote za upendo wa kweli kwa binadamu? Mungu huonyesha hasira kali kutokana na vitendo viovu vya watu, hasira Yake haina kosa. Moyo wa Mungu unavutiwa na toba ya watu, na ni toba hii ambayo hubadilisha moyo Wake. Kuguswa kwake, mabadiliko katika moyo Wake pamoja na huruma na uvumilivu Wake kwa binadamu, vyote havina kosa kabisa; ni safi, havina kasoro, havina doa na havijachafuliwa. Uvumilivu wa Mungu ni uvumilivu mtupu; Huruma Yake ni huruma tupu. Tabia Yake itafichua hasira, pamoja na huruma na uvumilivu, kulingana na kutubu kwa binadamu na mwenendo wake tofauti. Haijalishi kile ambacho Anafichua na kuonyesha, yote hayo hayana kasoro; yote ni ya moja kwa moja; kiini Chake ni tofauti na chochote kile katika uumbaji. Kanuni za matendo ambazo Mungu huonyesha, fikira na mawazo Yake, au uamuzi wowote maalum, pamoja na kitendo chochote kimoja, vyote havina dosari wala doa. Kama jinsi ambavyo Mungu huamua na jinsi Atendavyo, ndivyo Anavyokamilisha shughuli Zake. Aina hizi za matokeo ni sahihi na hazina dosari kwa sababu chanzo chake hakina dosari na doa lolote. Hasira ya Mungu haina dosari. Vilevile, huruma na uvumilivu wa Mungu, ambazo hazimilikiwi na kiumbe yeyote ni takatifu na hazina kosa, na zinaweza kustahimili fikira na uzoefu.

Baada ya kuelewa hadithi ya Ninawi, je, mnauona upande ule mwingine wa kiini cha tabia ya haki ya Mungu? Je, mnauona upande ule mwingine wa tabia ya haki na ya kipekee ya Mungu? Je, kunaye mtu yeyote miongoni mwa binadamu anayemiliki aina hii ya tabia? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki aina hii ya hasira kama ile ya Mungu? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki huruma na uvumilivu kama ule wa Mungu? Ni nani miongoni mwa viumbe anayeweza kuita hasira nyingi sana na kuamua kuangamiza au kuleta maafa kwa wanadamu? Na ni nani anazo sifa zinazostahili kutoa huruma kuvumilia na kumsamehe binadamu na hivyo basi kubadilisha uamuzi wake wa kuangamiza binadamu? Muumba huonyesha tabia Yake ya haki kupitia mbinu na kanuni Zake za binafsi za kipekee; Hategemei kudhibitiwa au kuzuiliwa na watu, matukio au mambo yoyote. Akiwa na tabia Yake ya kipekee, hakuna mtu anayeweza kubadilisha fikira na mawazo Yake, wala hakuna yule anayeweza kumshawishi Yeye na kubadilisha uamuzi wowote Wake. Uzima wa tabia na fikira za uumbaji upo katika hukumu ya tabia Yake ya haki. Hakuna anayeweza kudhibiti kama atatumia hasira au huruma; ni kiini cha Muumba tu—au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Muumba—kinaweza kuamua hili. Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!

Baada ya kuchambua na kuelewa mabadiliko katika mtazamo wa Mungu kwa watu wa Ninawi, je, unaweza kutumia neno “upekee” kufafanua huruma inayopatikana katika tabia ya haki ya Mungu? Hapo awali tulisema kwamba hasira ya Mungu ni kipengele kimoja cha kiini cha tabia Yake ya haki na ya kipekee. Sasa Nitafafanua vipengele viwili, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, kama tabia Yake ya haki. Tabia ya haki ya Mungu ni takatifu; ni isiyokosewa pamoja na kushukiwa; ni kitu kisichomilikiwa na yeyote miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Ni ya kipekee na maalum kwa Mungu pekee. Hivi ni kusema kwamba hasira ya Mungu ni takatifu na isiyokosewa Vivyo hivyo, kipengele kile kingine cha tabia ya haki ya Mungu—huruma ya Mungu—ni takatifu na haiwezi kukosewa. Hakuna yeyote kati ya viumbe vile vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa, anavyoweza kubadilisha au kuwakilisha Mungu katika vitendo Vyake, wala hakuna yeyote anayeweza kubadilisha au kumwakilisha Yeye katika kuangamiza Sodoma au wokovu wa Ninawi. Haya ndiyo maonyesho ya kweli ya tabia ya haki ya kipekee ya Mungu.

Hisia za Dhati za Muumba kwa Wanadamu

Watu mara nyingi husema kwamba si jambo rahisi kumjua Mungu. Mimi, hata hivyo, nasema kwamba kumjua Mungu si jambo gumu kamwe, kwani Mungu mara kwa mara huruhusu binadamu kushuhudia matendo Yake. Mungu hajawahi kusitisha mazungumzo Yake na mwanadamu; Yeye hajawahi kujificha kutoka kwa binadamu, wala Yeye hajajificha. Fikira Zake, mawazo Yake, maneno Yake na matendo Yake vyote vimefichuliwa kwa mwanadamu. Kwa hivyo, mradi tu mwanadamu angependa kumjua Mungu, anaweza kumwelewa hatimaye na kumjua Yeye kupitia aina zote za mambo na mbinu. Sababu inayomfanya binadamu kufikiria kwa kutojua kwamba Mungu amemwepuka kimakusudi, kwamba Mungu amejificha kimakusudi kutoka kwa binadamu, kwamba Mungu hana nia yoyote ya kumruhusu mwanadamu kuelewa na kumjua Yeye, ni kwamba hajui Mungu ni nani, wala asingependa kujua Mungu; na hata zaidi, hajali kuhusu fikira, matamshi au matendo ya Muumba…. Kusema kweli, kama mtu atatumia tu muda wake wa ziada vizuri katika kuzingatia na kuelewa matamshi au matendo ya Muumba na kuuweka umakinifu mchache kwa fikira za Muumba na sauti ya moyo Wake, haitakuwa vigumu kwa wao kutambua ya kwamba fikira, maneno na matendo ya Muumba, vyote vinaonekana na viko wazi. Vilevile, itachukua jitihada kidogo kutambua kwamba Muumba yuko miongoni mwa binadamu siku zote, kwamba siku zote Anazungumza na binadamu na uumbaji mzima, na kwamba Anatekeleza matendo mapya, kila siku. Hali Yake halisi na tabia vyote vimeelezewa katika mazungumzo Yake na binadamu; fikira na mawazo Yake vyote vinafichuliwa kabisa kwenye matendo Yake haya; Anaandamana na kufuatilia mwanadamu siku zote. Anaongea kimyakimya kwa mwanadamu na uumbaji wote kwa maneno Yake ya kimyakimya: Mimi niko juu ya ulimwengu, na Mimi nimo miongoni mwa uumbaji Wangu. Ninawaangalia, Ninawasubiri; Niko kando yenu…. Mikono yake ni yenye joto na thabiti; nyayo Zake ni nuru; sauti Yake ni laini na yenye neema, umbo Lake linapita na kugeuka, linakumbatia binadamu wote; uso Wake ni mzuri na mtulivu. Hajawahi kuondoka, wala Hajatoweka. Usiku na mchana, Yeye ndiye rafiki wa karibu na wa siku zote wa mwanadamu, ashiyemwacha kamwe. Utunzaji wake wa kujitolea na huba maalum kwa binadamu, pamoja na kujali Kwake kwa kweli na upendo kwa binadamu, vyote vilionyeshwa kwa utaratibu wakati Alipokuwa akiuokoa mji wa Ninawi. Haswa, mabadilishano ya mazungumzo kati ya Yehova Mungu na Yona yaliweza kuweka msingi wa huruma ya Muumba kwa mwanadamu ambaye Yeye Mwenyewe Aliumba. Kupitia kwa maneno haya, unaweza kupata ufahamu wa kina wa hisia za dhati za Mungu kwa binadamu …

Kifungu kifuatacho kimerekodiwa kwenye kitabu cha Yona 4:10-11: “Kisha Yehova akasema, Umeuonea mtango huruma, ambao hujafanyia kazi, wala kuukuza; ambao ulimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini ndani yake ambao hawawezi kutambua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo wengi?” Haya ni maneno halisi ya Yehova Mungu, mazungumzo kati Yake na Yona. Huku mabadilishano ya mazungumzo haya yakiwa mafupi, yamejaa utunzaji wa Muumba kwa mwanadamu na kutotaka Kwake kukata tamaa. Matamshi haya yanaonyesha mtazamo na hisia za kweli ambazo Mungu anashikilia ndani ya moyo Wake kuhusu uumbaji Wake, na kupitia kwa maneno haya yaliyowekwa wazi, ambayo yanasikizwa kwa nadra sana na binadamu, Mungu anakariri nia Zake za kweli kwa binadamu. Mabadilishano ya mazungumzo haya yanawakilisha mtazamo ambao Mungu alishikilia kwa watu wa Ninawi—lakini mtazamo aina hii ni upi? Ni mtazamo Alioshikilia kuhusu watu wa Ninawi kabla na baada ya kutubu kwao. Mungu huchukulia binadamu kwa njia sawa. Ndani ya maneno haya mtu anaweza kupata fikira Zake, pamoja na tabia Yake.

Je, ni fikira zipi za Mungu zinafichuliwa katika maneno haya? Usomaji wa makini unafichua mara moja kwamba Anatumia neno “huruma”; matumizi ya neno hili yanaonyesha mtazamo wa kweli wa Mungu kwa binadamu.

Kwa kiwango cha maana ya juu juu, watu wanaweza kufasiri neno “huruma” kwa njia tofauti: Kwanza, inamaanisha “kupenda na kulinda, kuhisi huruma kuhusu kitu fulani”; pili, inamaanisha “kupenda kwa dhati”; na hatimaye, inamaanisha “kutokuwa radhi kukiumiza kitu fulani na kutoweza kuvumilia kufanya hivyo.” Kwa ufupi, unaashiria yale mahaba na upendo wa dhati, pamoja na kutokuwa radhi kukata tamaa na kumwacha mtu au kitu; unamaanisha huruma ya Mungu na uvumilivu kwa mwanadamu. Ingawaje Mungu alitumia neno linalotamkwa mara nyingi miongoni mwa binadamu, matumizi ya neno hili yanaweka wazi sauti ya moyo wa Mungu na mtazamo Wake kwa mwanadamu.

Huku mji wa Ninawi ukiwa umejaa watu waliopotoka, walio waovu, na wenye udhalimu kama wale wa Sodoma, kutubu kwao kulisababisha Mungu kubadilisha moyo Wake na kuamua kutowaangamiza. Kwa sababu mwitikio wao kwa maneno na maagizo ya Mungu ulionyesha mtazamo uliokuwa na tofauti kavu na ule wa wananchi wa Sodoma, na kwa sababu ya utiifu wao wa dhati kwa Mungu na kutubu kwa uaminifu dhambi zao, pamoja na tabia yao ya kweli na dhati kwa hali zote, Mungu kwa mara nyingine alionyesha huruma Yake ya moyoni naye akaweza kuwapa. Tuzo ya Mungu na huruma Yake kwa binadamu haiwezekani kwa yeyote yule kurudufu; hakuna mtu anayeweza kumiliki huruma au uvumilivu wa Mungu, wala hisia Zake za dhati kwa binadamu. Je, yupo yeyote unayemwona kuwa mwanamume au mwanamke mkuu, au hata mwanamume mkuu zaidi, ambaye angeweza, kutoka katika mtazamo mkuu, akiongea kama mwanamume au mwanamke mkuu au kwenye sehemu ya mamlaka ya juu, kutoa aina hii ya kauli kwa mwanadamu au viumbe? Ni nani miongoni mwa wanadamu anayeweza kujua hali za maisha ya binadamu kama viganja vya mkono wake? Ni nani anayeweza kuvumilia mzigo na jukumu la kuwepo kwa binadamu? Nani aliye na sifa ya kutangaza kuangamizwa kwa mji? Na ni nani aliye na sifa ya kuusamehe mji? Ni nani wanaoweza kusema wanafurahia uumbaji wao binafsi? Muumba Pekee! Muumba pekee ndiye aliye na upole kwa wanadamu hawa. Muumba pekee ndiye anayeonyesha mwanadamu huyu rehema na huba. Muumba pekee ndiye anayeshikilia huba ya kweli, isiyovunjika kwa mwanadamu huyu. Vilevile, Muumba pekee ndiye anayeweza kumpa huruma mwanadamu huyu na kufurahia viumbe vyake vyote. Moyo wake waruka na kuumia kwa kila matendo ya mwanadamu: Ameghadhibishwa, dhikishwa, na kuhuzunishwa juu ya maovu na kupotoka kwa binadamu; Ameshukuru, amefurahia, amekuwa mwenye kusamehe na mwenye kushangilia kutokana na kutubu na kuamini kwa binadamu; kila mojawapo ya fikira na mawazo Yake vyote yapo juu ya na yanazungukia mwanadamu; kile Alicho na anacho vyote vinaonyeshwa kwa uzima au kwa minajili ya mwanadamu; uzima wa hisia Zake vyote vimeingiliana na uwepo wa mwanadamu. Kwa minajili ya mwanadamu, Anasafiri na kuzungukazunguka; kwa utaratibu Anatoa kila sehemu ya maisha Yake; Anajitolea kila dakika na sekunde ya maisha Yake…. Hajawahi kujua namna ya kuyahurumia maisha Yake, ilhali siku zote Amehurumia na kufurahia mwanadamu ambaye Yeye Mwenyewe aliumba…. Anatoa kila kitu Alichonacho kwa binadamu huu…. Yeye anatoa huruma na uvumilivu Wake bila masharti na bila matarajio ya kufidiwa. Anafanya hivi tu ili mwanadamu aweze kuendelea kuwepo mbele ya macho Yake, kupokea toleo Lake la maisha; Anafanya hivi tu ili mwanadamu siku moja aweze kunyenyekea mbele Yake na kutambua kwamba Yeye ni yule anayetosheleza kuwepo kwa binadamu na kuruzuku maisha ya viumbe vyote.

Muumba Aonyesha Hisia Zake za Kweli Kwa Binadamu

Mazungumzo haya kati ya Yehova Mungu na Yona bila shaka ni onyesho la hisia za kweli za Muumba juu ya binadamu. Kwa upande mmoja yanafahamisha watu kuhusu ufahamu wa Muumba wa asili yote yaliyo katika ukuu Wake; kama vile Yehova Mungu alivyosema, “Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini ndani yake ambao hawawezi kutambua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo wengi?” Kwa maneno mengine, ufahamu wa Ninawi na Mungu haukuwa hata karibu na wa laana. Hakujua tu idadi ya viumbe vilivyo hai ndani ya mji (wakiwemo watu na mifugo), bali Alijua pia ni wangapi wasingeweza kutambua kati ya mikono yao ya kulia na kushoto—yaani, ni watoto na vijana wangapi walikuwepo. Hii ni ithibati thabiti ya ufahamu bora kuhusu mwanadamu. Kwa upande mwingine mazungumzo haya yanafahamisha watu kuhusu mtazamo wa Muumba kwa binadamu, ambako ni kusema kwamba uzito wa binadamu katika moyo wa Muumba. Ni vile tu Yehova Mungu alivyosema: “Umeuonea mtango huruma, ambao hujafanyia kazi, wala kuukuza; ambao ulimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu…?” Haya ndiyo maneno ya Yehova Mungu kuhusu lawama kwa Yona lakini yote ni kweli.

Ingawaje Yona alikuwa ameaminiwa kutangaza matamshi ya Yehova Mungu kwa watu wa Ninawi, hakuelewa nia za Yehova Mungu, wala hakuelewa wasiwasi na matarajio Yake kwa watu wa mji huu. Kupitia kwa kemeo hili Mungu alinuia kumwambia kwamba binadamu ulikuwa zao la mikono Yake mwenyewe, na kwamba Mungu alikuwa ametia jitihada za dhati kwa kila mtu; kila mtu alisheheni matumaini ya Mungu; kila mtu alifurahia ruzuku ya maisha ya Mungu; kwa kila mtu, Mungu alikuwa amelipia gharama ya dhati. Kemeo hili lilimfahamisha Yona kwamba Mungu aliufurahia binadamu, kazi ya mikono Yake mwenyewe, kama vile tu ambavyo Yona mwenyewe aliufurahia mtango. Mungu kwa vyovyote vile asingewaacha kwa urahisi kabla ya ule muda wa mwisho unaowezekana; vilevile, kulikuwa na watoto wengi na mifugo isiyo na hatia ndani ya mji. Wakati wa kushughulikia mazao haya machanga na yasiyojua uumbaji wa Mungu, ambayo yasingeweza hata kutofautisha mikono yao ya kulia na ile ya kushoto, Mungu hakuweza kamwe kukomesha maisha yao na kuamua matokeo yao kwa njia ya haraka hivyo. Mungu alitumai kuwaona wakikua; Alitumai kwamba wasingetembea njia ile ile kama wakubwa wao, kwamba wasingeweza kusikia tena onyo la Yehova Mungu, na kwamba wangeshuhudia mambo ya kale ya Ninawi. Na hata zaidi Mungu alitumai kuiona Ninawi baada ya kuweza kutubu, kuuona mustakabali wa Ninawi kufuatia kutubu kwake, na muhimu zaidi, kuiona Ninawi ikiishi katika huruma za Mungu kwa mara nyingine tena. Kwa hivyo, kwa macho ya Mungu, yale mazao ya uumbaji wake ambayo hayangeweza kutofautisha mikono yao ya kulia na kushoto yalikuwa mustakabali wa Ninawi. Wangeweza kubeba na kusimulia hadithi ya kale iliyostahili dharau, kama vile tu ambavyo wangeweza kusimulia wajibu muhimu wa kushuhudia hadithi ya kale ya Ninawi na mustakabali wake kupitia kwa mwongozo wa Yehova Mungu. Katika tangazo hili la hisia Zake za kweli, Yehova Mungu aliwasilisha huruma ya Muumba kuhusu binadamu kwa uzima wake. Lilionyesha binadamu kwamba “ile huruma ya Muumba” si kauli tupu tu, wala si ahadi isiyotimizika; ilikuwa na kanuni, mbinu na majukumu ya kimsingi. Yeye ni kweli na halisi, na hatumii uwongo au utapeli wowote, na kwa njia ii hii huruma Yake inawekewa binadamu katika kila wakati na enzi. Hata hivyo, hadi siku hii, mabadilishano ya mazungumzo ya Muumba na Yona ndiyo kauli moja, na ya kipekee ya matamshi yanayoelezea ni kwa nini Anaonyesha huruma kwa binadamu, jinsi Anavyoonyesha huruma kwa binadamu, ni vipi Alivyo na uvumilivu kwa binadamu na hisia Zake za kweli kuhusu binadamu. Mazungumzo haya ya Yehova Mungu yenye uchache na uwazi yanaonyesha fikira Zake kamili kuhusu binadamu; ni maonyesho ya ukweli ya mtazamo wa moyo Wake kwa binadamu, na ni ushahidi thabiti wa kutoa Kwake kwingi kwa huruma juu ya binadamu. Huruma yake haipewi tu vizazi vya wazee wa binadamu; lakini pia imepewa wanachama wachanga zaidi wa binadamu, kama vile tu ambavyo imekuwa, kuanzia kizazi kimoja hadi kingine. Ingawaje hasira ya Mungu hushushwa mara kwa mara kwenye pembe fulani na enzi fulani za binadamu, huruma ya Mungu haijawahi kusita. Kupitia kwa huruma Yake, Yeye huongoza na kuelekeza kizazi kimoja cha uumbaji Wake hadi kingine, huruzuku na kukifaa kizazi kimoja cha uumbaji hadi kingine, kwa sababu hisia Zake za kweli kwa binadamu hazitawahi kubadilika. Vile tu Yehova Mungu alivyosema: “Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma…?” Siku zote amefurahia uumbaji Wake mwenyewe. Hii ndiyo huruma ya tabia ya haki ya Muumba, na ndio pia upekee usio na kasoro wa Muumba!

Aina Tano za Watu

Kwa sasa, Nitaacha ushirika wetu kuhusu tabia ya haki ya Mungu umalizikie hapo. Kinachofuata Nitaainisha wafuasi wa Mungu katika kategoria mbalimbali, kulingana na ufahamu wao wa Mungu na ufahamu wao na kile wamepitia kuhusiana na tabia ya haki Yake, ili muweze kujua awamu ambayo kwa sasa mnapatikana ndani pamoja na kimo chenu cha sasa. Kuhusiana na maarifa yao ya Mungu na ufahamu wao wa tabia Yake ya haki, awamu na kimo tofauti ambavyo watu huwa navyo vinaweza kugawanywa katika aina tano. Mada hii imeelezewa kwa msingi wa kumjua Mungu wa kipekee na tabia Yake ya haki; kwa hivyo, unaposoma maudhui yafuatayo, unafaa kujaribu kwa makini kuchambua ni kiwango kipi haswa cha ufahamu na maarifa ulichonacho kuhusiana na upekee wa Mungu na tabia Yake ya haki, na kisha utumie hayo kujua ni awamu gani ambayo kwa kweli unapatikana ndani, kimo chako ni kikubwa vipi kwa kweli, na wewe ni aina gani ya mtu kwa kweli.

Aina ya Kwanza: Hatua ya Mtoto Mchanga aliyefungwa kwa Vitambaa

Mtoto mchanga aliyefungwa kwa vitambaa ni nini? Mtoto mchanga aliyefungwa kwa vitambaa ni mtoto mchanga ambaye ndio mwanzo ameingia kwenye ulimwengu huu, amezaliwa. Huu ndio wakati ambao watu wako katika awamu ndogo zaidi na isiyo na ukomavu.

Watu katika awamu hii kimsingi hawamiliki utambuzi au ufahamu wowote wa masuala ya kuamini Mungu. Wamekanganywa na hawajui kila kitu. Watu hawa huenda wamemsadiki Mungu kwa muda mrefu au kwa muda usiokuwa mrefu, lakini hali yao ya kukanganywa na kutojua kimo chao halisi kinawaweka kwenye awamu ya mtoto mchanga aliyefungwa kwa vitambaa. Ufafanuzi wa hakika wa hali hii ya mtoto mchanga aliyefungwa kwa vitambaa ni kama vile: Haijalishi ni muda upi ambao aina hii ya mtu amesadiki Mungu, siku zote atakuwa mpumbavu, atachanganyikiwa na ataonyesha werevu au uamuzi wa kiwango kidogo sana; hajui ni kwa nini anasadiki Mungu, wala hajui Mungu ni nani au Mungu ni nini. Ingawaje anafuata Mungu, hakuna ufafanuzi halisi wa Mungu katika moyo wake, na hawezi kuamua kama yule anayemfuata ni Mungu, sikuambii hata kama kweli anafaa kumsadiki Mungu na kumfuata Yeye. Hizi ndizo hali za kweli za aina hii ya mtu. Fikira za watu hawa zimezingirwa na ukungu, na kama nitasema wazi, imani yao ni ile ya mkanganyo. Siku zote wanakuwa katika hali ya mkanganyiko na utupu; kuwa mpumbavu, kuchanganyikiwa na kuonyesha werevu au uamuzi wa kiwango kidogo sana ndivyo vitu vinavyofanya muhtasari wa hali zao. Hawajawahi kuona wala kuhisi uwepo wa Mungu, na hivyo basi, kuwazungumzia kuhusu kujua Mungu ni sawa tu na kuwafanya kusoma kitabu kilichoandikwa kwa maandiko ya hieroglifu maandiko au ishara zisizofahamika; hawataelewa wala kuyakubali. Kwao, kujua Mungu ni sawa na kusikia kisa cha kifantasia. Huku fikira zao zikiwa zinaweza kuwa na ukungu, kwa hakika wanasadiki kwa dhati kwamba kujua Mungu ni kupoteza muda na jitihada. Huyu ndiye mtu wa aina ya kwanza: mtoto mchanga aliyefungwa kwa vitambaa.

Aina ya Pili: Hatua ya Mtoto Mchanga Anayenyonya

Akilinganishwa na mtoto mchanga aliyefungiwa ndani ya vitambaa, aina hii ya mtu amepiga hatua fulani. Kwa bahati mbaya, bado hawana ufahamu wa Mungu kamwe. Wangali wanakosa ufahamu wazi wa na utambuzi wa Mungu, na hawaelewi vizuri sana ni kwa nini wanafaa kumsadiki Mungu, lakini katika mioyo yao wanalo kusudi lao binafsi na mawazo wazi. Hawajihusishi na suala la kama ni sahihi kumsadiki Mungu. Lengo na kusudi wanalotafuta kupitia kwa imani ya Mungu ni kufurahia neema Yake, kuwa na furaha na amani, kuishi maisha yenye utulivu, kuwa na utunzaji na ulinzi wa Mungu na kuishi katika baraka za Mungu. Hawajali kiwango ambacho wanamjua Mungu; hawana msisimko wa kutafuta kuelewa Mungu, wala hawashughuliki na kile ambacho Mungu anafanya au kile ambacho Angependa kufanya. Wanatafuta tu bila mwelekeo kufurahia neema Yake na kupata baraka Zake nyingi; wanatafuta kupokea baraka mara mia moja kwenye umri wa sasa, na maisha ya baadaye kwenye miaka ijayo. Fikira zao, matumizi na kujitolea kwao, pamoja na kuteseka kwao, vyote vinalo lengo moja: kupokea neema na baraka za Mungu. Hawana shughuli na kitu kingine chochote. Aina hii ya mtu bila shaka ana hakika kwamba Mungu anaweza kuwalinda wakawa salama na kuwapa neema Yake. Mtu anaweza kusema kwamba hawana kivutio chochote katika na hawana mwelekeo sana kuhusiana na kwa nini Mungu angependa kumwokoa binadamu au matokeo ambayo Mungu angependa kupata kutokana na matamshi na kazi Yake. Hawajawahi kutia jitihada za kujua hali halisi ya Mungu na tabia ya haki, wala hawawezi kujipa moyo na kuwa na nia ya kufanya hivyo. Hawahisi kumakinikia katika mambo haya, wala hawapendi kuyajua. Hawapendi hata kuulizia kuhusu kazi ya Mungu, mahitaji ya Mungu kwa binadamu, mapenzi ya Mungu au kitu chochote kingine kinachohusiana na Mungu; wala hawawezi kuwa na msukumo wa kuulizia mambo haya. Hii ni kwa sababu wanasadiki masuala haya hayahusiani na kufurahia kwao kwa neema ya Mungu; wanajali tu Mungu anayeweza kuwapa neema na ambaye ana uhusiano na masilahi yao ya kibinafsi. Hawana haja kamwe na kitu kingine chochote, na kwa hivyo hawawezi kuingia kwenye uhalisi wa ukweli, licha ya miaka mingapi ambayo wamemsadiki Mungu. Bila kuwepo yeyote wa kuwafunza neno la Bwana, mara nyingi ni vigumu kwao kuendelea kupiga hatua katika njia ya imani ya Mungu. Kama hawawezi kufurahia furaha yao na amani ya awali au kufurahia neema ya Mungu, basi wana uwezekano mkubwa wa kujiondoa. Huyu ndiye mtu wa aina ya pili: mtu anayekuwepo kwenye awamu ya mtoto mchanga wa kunyonya.

Aina ya Tatu: Hatua ya Mtoto Mchanga Anayeachishwa Ziwa, au Hatua ya Mtoto Mdogo

Kundi hili la watu humiliki ufahamu fulani wenye uwazi. Watu hawa wanao ufahamu kwamba kufurahia neema ya Mungu hakumaanishi kwamba wao wenyewe wanamiliki uzoefu wa kweli; wanao ufahamu kwamba wasipochoka katika kutafuta furaha na amani, katika kutafuta neema, au kama wanaweza kushuhudia kwa kujadiliana yale yote ambayo wamepitia katika kufurahikia kwao kwa neema ya Mungu au kwa kumsifu Mungu kwa baraka Zake ambazo amewapa, mambo haya hayamaanishi kwamba wanayo maisha, wala hayamaanishi kwamba wanao uhalisi wa ukweli. Tukianzia katika fahamu yao, wanasita kufurahia matumaini yasiyo na mipaka kwamba wataandamana tu na neema ya Mungu; badala yake, wakati wanapofurahia neema ya Mungu, wanapenda wakati uo huo kufanya kitu kwa ajili ya Mungu; wako radhi kutekeleza wajibu wao, kuvumilia ugumu kidogo na uchovu, kuwa na kiasi fulani cha ushirikiano na Mungu. Hata hivyo, kwa sababu kufuatilia kwao katika imani yao katika Mungu kumetiwa najisi sana, kwa sababu nia za kibinafsi na matamanio waliyo nayo ni makali mno, kwa sababu tabia yao ni yenye kiburi kisicho na mipaka, ni vigumu sana kwao kutosheleza tamanio la Mungu au kuwa watiifu kwa Mungu; hivyo basi, wao mara nyingi hawawezi kutambua matamanio yao ya kibinafsi au kuheshimu ahadi zao kwa Mungu. Mara nyingi wanajipata katika hali za kukinzana: Wanapenda sana kutosheleza Mungu hadi kwenye kiwango kikubwa zaidi kinachowezekana, ilhali wanatumia uwezo wao wote kumpinga Yeye; mara nyingi wanaweka nadhiri kwa Mungu lakini kwa haraka sana wanaishia kukwepa nadhiri zao. Hata mara nyingi wanajipata katika hali nyingine kinzani: Wanasadiki kwa dhati katika Mungu ilhali wanamkataa Mungu na kila kitu kinachotokana na Yeye; wanatumai kwa hamu kwamba Mungu atawapa nuru, atawaongoza, atawaruzuku na kuwasaidia, ilhali bado wanatafuta njia yao wenyewe. Wanapenda kuelewa na kujua Mungu, ilhali hawako radhi kuwa na uhusiano wa karibu na Yeye. Badala yake, siku zote wanamwepuka Mungu; mioyo yao haiko wazi kumkaribisha. Huku wakiwa na ufahamu wa juujuu na uzoefu wa maana ya moja kwa moja ya matamshi ya Mungu na ya ukweli, na dhana ya juujuu ya Mungu na ukweli, katika akili iliyofichika bado hawawezi kuthibitisha au kuamua kama Mungu ni ukweli; hawawezi kuthibitisha kama Mungu ni wa haki kwa kweli; wala hawawezi kuamua ule uhalisi wa tabia ya Mungu na hali halisi, sikuambii hata uwepo Wake wa kweli. Imani yao katika Mungu siku zote ina shaka na kutoelewana kwingi, na pia kunazo fikira za maono na dhana mbalimbali. Wanapofurahia neema ya Mungu, wanapitia pia bila kutaka au wanatenda baadhi ya kile wanachosadiki kuwa ukweli unaowezekana, ili kunufaisha imani yao, kukuza kile ambacho wamepitia katika kusadiki Mungu, kuthibitisha ufahamu wao wa kusadiki Mungu, na kutosheleza majisifu yao ya kutembelea njia ya maisha ambayo wao wenyewe wameanzisha na kukamilisha mkondo wa haki wa mwanadamu. Wakati uo huo wanafanya pia mambo haya ili kutosheleza tamanio lao binafsi la kufaidi baraka, ili wawekeane dau ndio waweze kupata baraka kubwa zaidi za binadamu, ili kutimiza maazimio ya maono na matamanio ya kimaisha ya kutopumzika mpaka pale ambapo wamefaidi Mungu. Watu hawa kwa nadra sana wanaweza kupokea nuru ya Mungu, kwani tamanio lao na nia yao ya kufaidi baraka ni muhimu sana kwao. Hawana tamanio la na hawawezi kuvumilia kutupilia mbali hili. Wanaogopa kwamba bila ya tamanio la kufaidi baraka, bila ya maono waliyotamani kwa muda mrefu ya kutopumzika mpaka pale ambapo wamefaidi Mungu, wataweza kukosa motisha ya kusadiki Mungu. Kwa hivyo, hawapendi kukabiliana na uhalisi. Hawapendi kukabiliana na matamshi ya Mungu au kazi ya Mungu. Hawapendi kukabiliana na tabia au hali halisi ya Mungu, sikuambii hata kuzungumzia mada ya kumjua Mungu. Hii ni kwa sababu mara tu Mungu, hali Yake halisi na tabia Yake ya haki vinapobadilisha maono yao, ndoto zao zitatoweka hivyo bila kuonekana; imani yao inayodhaniwa kuwa safi na “sifa njema” zilizokusanywa baada ya miaka ya kazi ngumu zitatoweka zote na kutokuwa na manufaa yoyote; “eneo” lao ambalo wameshinda kupitia kwa jasho na damu yao kwa miaka na mikaka itakuwa karibu kusambaratika. Hii itamaanisha kwamba miaka yao mingi ya kazi ya sulubu na jitihada vyote vimekuwa bure bilashi, kwamba lazima waanze tena kutoka sehemu ya kutokuwa na chochote. Haya ndiyo maumivu magumu zaidi kwao kuvumilia katika mioyo yao, na ni matokeo ambayo wanatamani kwa kiasi cha chini zaidi kuona; hivyo basi siku zote wamefungwa katika aina hii ya kutosonga mbele, na kukataa kurudi nyuma. Huyu ndiye mtu wa aina ya tatu: mtu anayekuwa katika awamu hii ya mtoto mchanga wa kuachishwa ziwa.

Aina tatu za watu waliofafanuliwa hapo juu—kwa maneno mengine, watu wanaopatikana katika awamu hizi tatu—hawamiliki imani yoyote ya kweli katika utambulisho na hadhi ya Mungu au katika tabia Yake halisi, wala hawana utambuzi wowote wazi, wa hakika au thibitisho la mambo haya. Kwa hivyo, ni vigumu sana kwa aina hizi tatu za watu kuingia kwenye uhalisi wa ukweli, na ni vigumu pia kwa wao kupokea huruma, nuru au mwangaza wa Mungu kwa sababu ya namna ambavyo wanasadiki Mungu na mtazamo wao wa kimakosa kwa Mungu unamfanya Yeye kutoweza kutekeleza kazi yoyote ndani ya mioyo yao. Shaka zao, kuelewa kwao vibaya na kufikiria kwao kuhusiana na Mungu kumezidi imani yao na maarifa ya Mungu. Hizi ni aina tatu za watu walio katika hatari kubwa, na ni hatua tatu hatari sana. Wakati mtu anapoendeleza mtazamo wa shaka kwa Mungu, hali halisi ya Mungu, utambulisho wa Mungu, lile suala la kama Mungu ni ukweli na uhalisi wa uwepo Wake na kwamba hawezi kuwa na hakika katika mambo haya, ni vipi ambavyo mtu anaweza kukubali kila kitu kinachotoka kwa Mungu? Mtu anawezaje kukubali hoja kwamba Mungu ni ukweli, njia na uzima? Mtu anawezaje kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu? Mtu anawezaje kukubali wokovu wa Mungu? Ni vipi ambavyo aina hii ya mtu anaweza kupokea mwongozo na ruzuku ya kweli kutoka kwa Mungu? Wale ambao wanapatikana katika awamu hizi tatu wanaweza kumpinga Mungu, kupitisha hukumu kwa Mungu, kukufuru Mungu au kusaliti Mungu wakati wowote. Wanaweza kuacha njia ya kweli na kumtoroka Mungu wakati wowote. Mtu anaweza kusema kwamba watu katika awamu hizi tatu wapo katika kipindi hatari sana, kwani hawajaingia kwenye njia sahihi ya kumsadiki Mungu.

Aina ya Nne: Hatua ya Mtoto Anayekomaa, au Kipindi cha Utoto

Baada ya mtu kuachishwa ziwa—yaani, baada ya wao kufurahia kiwango tosha cha neema, mtu anaanza kuchunguza ni nini maana ya kusadiki Mungu, kutaka kuelewa maswali tofauti, kama vile kwa nini binadamu anaishi, binadamu anafaa kuishi vipi, na kwa nini Mungu hutekeleza kazi Yake kwa binadamu. Wakati ambapo mawazo haya yasiyo wazi na mawazo yaliyokanganyikiwa hujitokeza ndani yao, na kuwepo ndani yao, wanaendelea kupokea kunyunyizwa, na wao wanaweza pia kutekeleza wajibu wao. Kwenye kipindi hiki, hawana tena shaka kuhusiana na ukweli wa uwepo wa Mungu, na wanao ung’amuzi sahihi wa ni nini maana ya kumwamini Mungu. Kwenye msingi huu wao hupata maarifa ya utaratibu kuhusu Mungu, na wanapokea kwa utaratibu baadhi ya majibu ya mawazo yao yasiyo wazi na mawazo yaliyokanganyika kuhusiana na tabia ya Mungu na hali halisi. Kwa mujibu wa mabadiliko yao katika tabia yao pamoja na maarifa yao kuhusu Mungu, watu katika awamu hii huanza kushika njia sahihi na kuingia kwenye kipindi cha mpito. Ni katika awamu hii ambapo watu huanza kuwa na maisha. Vionyeshi wazi vya kumiliki maisha ni uamuzi wa taratibu wa maswali mbalimbali yanayohusiana na kumjua Mungu ambayo watu wanakuwa nayo katika mioyo yao—kutoelewana, mawazo, fikira, na ufafanuzi usio wazi wa Mungu—na si kwamba wao huja kusadiki na kujua uhalisi wa uwepo wa Mungu, lakini pia wao huja kumiliki ufasili wazi wa Mungu na kuwa na nafasi sahihi ya Mungu katika mioyo yao, na kumfuata Mungu kwa kweli kutabadilisha imani yao isiyo dhahiri. Kwenye awamu hii, watu kwa utaratibu wanaanza kujua kutoelewa kwao katika masuala ya Mungu na kutafuta kwao kimakosa na njia za imani. Wanaanza kutamani ukweli, kutamani kupitia hukumu ya Mungu, kurudiwa na nidhamu, kutamani mabadiliko katika tabia yao. Kwa utaratibu wanaanza kuacha aina zote za dhana na fikira kuhusu Mungu kwenye awamu hii; wakati uo huo wanabadilisha na kurekebisha maarifa yasiyo sahihi kuhusu Mungu na kupata baadhi ya maarifa muhimu na sahihi kuhusu Mungu. Ingawaje sehemu ya maarifa inayomilikiwa na watu katika awamu hii si mahususi au sahihi sana, kwa kiwango cha chini zaidi wanaanza kwa utaratibu kuacha dhana zao, maarifa ya kimakosa na kutoelewa mambo kuhusu Mungu; hawaendelezi tena dhana zao binafsi na fikira zao kuhusu Mungu. Wanaanza kujifunza namna ya kuacha—kuacha mambo yanayopatikana miongoni mwa dhana zao binafsi, kutoka kwa maarifa yao na kutoka kwa Shetani; wanaanza kuwa radhi kutii mambo sahihi na mazuri, hata kwa mambo yanayotoka kwenye matamshi ya Mungu na kutii ukweli. Wanaanza pia kujaribu kupitia matamshi ya Mungu, kujua kibinafsi na kutekeleza matamshi Yake, kukubali matamshi Yake kama kanuni za hatua zao na kama msingi wa kubadilisha tabia yao. Kwenye kipindi hiki, watu bila kufahamu wanaikubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, wanakubali bila fahamu matamshi ya Mungu kuwa maisha yao. Huku wakikubali hukumu, kuadibu kwa Mungu, na kukubali matamshi ya Mungu, wanaendelea kuwa na ongezeko la kufahamu na wanaweza kuhisi kwamba Mungu wanayemsadiki ndani ya mioyo yao kweli yupo. Kwa maneno ya Mungu, hali yao wanayopitia na maisha yao, wanazidi kuhisi kwamba Mungu siku zote amesimamia hatima ya binadamu, kumwongoza binadamu na kuruzuku binadamu. Kupitia kwa ushirikiano wao na Mungu, wanaanza kwa utaratibu kuthibitisha uwepo wa Mungu. Kwa hivyo, kabla ya wao kutambua, tayari wameuidhinisha bila kufahamu na kusadiki kwa dhati katika kazi ya Mungu, na wameidhinisha matamshi ya Mungu. Baada ya watu kuidhinisha matamshi ya Mungu, na kuidhinisha kazi ya Mungu, bila kusita wanajikataa, wanakataa dhana zao binafsi, wanakataa maarifa yao binafsi, wanakataa fikira zao binafsi, na wakati uo huo wanatafuta bila kusita ukweli ni nini na mapenzi ya Mungu ni nini. Maarifa ya watu kuhusu Mungu ni ya juujuu sana kwenye kipindi hiki cha maendeleo—hata hawawezi kufafanua wazi maarifa haya kwa kutumia matamshi, wala hawawezi hata kufafanua kimahususi—na wanao ufahamu unaohusu utambuzi; hata hivyo, wakati awamu hii inawekwa sambamba na zile awamu tatu zilizotangulia, maisha ya watu wasiokomaa katika kipindi hiki tayari yameanza kupokea kunyunyizia na ruzuku ya matamshi ya Mungu, na tayari yameanza kuota. Ni sawa na mbegu iliyozikwa ardhini; baada ya kupokea unyevunyevu na virutubisho, lazima itapenyeza kupitia kwenye mchanga; kuota kwake kunawakilisha kuzaliwa kwa maisha mapya. Kuzaliwa huku kwa maisha mapya kunaruhusu mtu kuona vionyeshi vya maisha. Kupitia kwa maisha, watu wataweza kukua. Kwa hivyo, juu ya misingi hii—kwa utaratibu wanaanza kurudi katika njia sahihi ya kusadiki katika Mungu, kuacha dhana zao binafsi, kupata mwongozo wa Mungu—maisha ya watu yataweza kukua bila shaka hatua kwa hatua. Ni katika msingi gani ndipo ukuaji huu unapimwa? Unapimwa kulingana na uzoefu wao na maneno ya Mungu na ufahamu wao wa kweli kuhusu tabia ya haki ya Mungu. Ingawaje wanaona jambo hili likiwa gumu sana katika kutumia maneno yao binafsi ili kufafanua kwa usahihi maarifa yao kuhusu Mungu na hali Yake halisi kwenye kipindi hiki cha ukuaji, kundi hili la watu haliko radhi tena kufuatilia kimsingi furaha kupitia kwa kufurahia neema ya Mungu, au kufuatilia kusudi lao la kusadiki Mungu, ambapo ni kupokea neema Yake. Badala yake, wako radhi kutafuta kuishi kwa neno la Mungu, ili kuwa walengwa wa wokovu wa Mungu. Vilevile, wanamiliki ujasiri na wako tayari kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu. Hii ndiyo alama ya mtu aliye katika awamu ya kukua.

Ingawaje watu katika awamu hii wanayo maarifa fulani kuhusu tabia ya haki ya Mungu, maarifa yao si dhahiri wala bainifu. Huku wakiwa hawawezi kufafanua wazi hali hii, wanahisi kwamba tayari wamefaidi kitu fulani ndani kwa ndani, kwani wamepata kipimo fulani cha maarifa na ufahamu wa tabia ya haki ya Mungu kupitia kwa kuadibu kwa Mungu na hukumu yake; hata hivyo yote haya ni kana kwamba ni ya juujuu, na bado yangali katika awamu ya kimsingi. Kundi hili la watu linao msimamo wa maoni thabiti kuhusiana na neema ya Mungu. Msimamo huu wa maoni unaelezewa kupitia kwenye mabadiliko ya malengo wanayoyatafuta na njia ambayo wanayatafutia. Tayari wameona—katika maneno na kazi ya Mungu, kwenye aina zote za mahitaji Yake ya binadamu na kwenye ufunuo Wake wa binadamu—kwamba kama bado hawatafuatilia ukweli, kama bado hawatafuti kuingia kwenye uhalisia, kama bado hawatafuti kutosheleza na kujua Mungu huku wakipitia maneno Yake, watapoteza umuhimu katika kusadiki Mungu. Wanaona haijalishi ni kiwango kipi ambacho wanafurahia neema ya Mungu, hawawezi kubadilisha tabia yao, kutosheleza Mungu au kumjua Mungu, na kwamba wakiendelea kuishi miongoni mwa neema ya Mungu, hawatawahi kutimiza ukuaji, kupata uzima au kuweza kupokea wokovu. Kwa muhtasari, kama mtu hawezi kupitia maneno ya Mungu kwa njia ya kweli na hawezi kumjua Mungu kupitia kwa maneno Yake, mtu huyo daima dawamu atabakia katika awamu ile ya mtoto mchanga na hatawahi kupiga hatua yoyote mbele kwenye ukuaji wa maisha yake. Kama daima dawamu utakuwepo kwenye hatua ya mtoto mchanga, kama kamwe huingii kwenye uhalisi wa neno la Mungu, kama kamwe huna neno la Mungu kama maisha yako, kama kamwe huna imani na maarifa ya kweli kuhusu Mungu, je, kunao uwezekano wowote kwako wewe kufanywa kuwa kamili na Mungu? Hivyo basi, yeyote anayeingia katika uhalisi wa neno la Mungu, yeyote anayekubali neno la Mungu kuwa maisha yake, yeyote anayeanza kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu, yeyote ambaye tabia yake potovu inaanza kubadilika, na yeyote aliye na moyo unaotamani ukweli, analo tamanio la kumjua Mungu, analo tamanio la kukubali wokovu wa Mungu—watu hawa ndio wale wanaomiliki uzima kwa kweli. Hii kwa kweli ndiyo aina ya nne ya mtu, ile ya mtoto anayekomaa, mtu aliye katika awamu ya utoto.

Aina ya Tano: Hatua ya Maisha Yaliyokomaa, au Hatua ya Mtu Mzima

Baada ya kupitia awamu ya mtoto mchanga hadi ya utoto, awamu hii ya ukuaji uliojaa kupindua kunakojirudia, maisha ya watu tayari yamekuwa thabiti, hatua yao ya kusonga mbele haisiti tena, wala hakuna yeyote anayeweza kuwazuia. Ingawaje njia iliyo mbele ingali na mabonde na misukosuko, si wanyonge tena au wenye woga; hawayumbiyumbi tena huko mbele au kupoteza mwelekeo wao. Misingi yao imekita mizizi kwenye hali halisi ya neno la Mungu. Mioyo yao imevutwa na heshima na ukubwa wa Mungu. Wanatamani kufuata nyayo za Mungu, kujua hali halisi ya Mungu, kujua Mungu kwa uzima Wake.

Watu katika awamu hii tayari wanajua waziwazi ni nani wanayemsadiki, na wanajua waziwazi kwa nini wanafaa kumsadiki Mungu na maana ya maisha yao husika; wanajua pia waziwazi kwamba kila kitu ambacho Mungu huelezea ndicho ukweli. Kwenye miaka yao mingi ya uzoefu, wametambua kwamba bila ya hukumu na kuadibu kwa Mungu, mtu hatawahi kuweza kutosheleza au kumjua Mungu, wala mtu huyo hataweza kuja mbele ya Mungu. Ndani ya mioyo ya watu hawa husika kunalo tamanio thabiti la kujaribiwa na Mungu, ili kuona tabia ya haki ya Mungu huku wakiendelea kujaribiwa, kufikia upendo safi zaidi, na wakati uo huo kuweza kuelewa na kujua Mungu kwa njia ya kweli zaidi. Wale walio katika awamu hii tayari wameaga kwaheri awamu ya mtoto, awamu ya kufurahia neema ya Mungu na kula mkate na kushiba. Hawaweki tena matumaini mengi katika kumfanya Mungu kuvumilia na kuwaonyesha huruma; badala yake, wanao ujasiri wa kupokea na kutumai kupata kuadibu na hukumu isiyosita ya Mungu, ili kuweza kujitenga na tabia yao potovu na hivyo basi kutosheleza Mungu. Maarifa yao kwa Mungu, kufuatilia kwao au shabaha za mwisho za kufuatilia kwao: mambo haya yote yako wazi kabisa katika mioyo yao. Hivyo basi, watu katika awamu ya mtu mzima tayari wameaga kwaheri kabisa awamu ya imani isiyo dhahiri, kwenye awamu ambayo wanategemea neema kupata wokovu, kwenye awamu ya maisha yasiyo komavu yasiyoweza kustahimili majaribio, hadi kwenye awamu ya kutokuwa bainifu, hadi kwenye awamu ya kuyumbayumba, hadi kwenye awamu ya mara kwa mara kutokuwa na njia ya kufuata, hadi kwenye kipindi kisichokuwa thabiti cha kubadilisha kati ya joto na baridi ya ghafla, na hadi kwenye awamu ambapo mtu anafuata Mungu huku ameyafumba macho yake. Aina hii ya mtu hupokea nuru na mwangaza wa Mungu mara kwa mara, na pia mara kwa mara hujihusisha katika ushirikiano na mawasiliano ya kweli na Mungu. Mtu anaweza kusema kwamba watu wanaoishi katika awamu hii tayari wameng’amua sehemu ya mapenzi ya Mungu; wanaweza kupata kanuni za ukweli katika kila kitu wanachofanya; wanajua namna ya kutosheleza tamanio la Mungu. Isitoshe, wamepata pia njia ya kumjua Mungu na wameanza kuwa na ushuhuda wa maarifa yao kwa Mungu. Kwenye mchakato huu wa ukuaji wa utaratibu, wanao ufahamu wa taratibu na maarifa ya mapenzi ya Mungu, ya mapenzi ya Mungu katika kuumba binadamu, ya mapenzi ya Mungu katika kusimamia binadamu; vilevile, kwa utaratibu wanao ufahamu na maarifa ya tabia ya haki ya Mungu kwa mujibu wa hali halisi. Hakuna dhana ya binadamu au kufikiria kunaweza kubadilisha maarifa haya. Huku mtu hawezi kusema kwamba kwenye awamu ya tano maisha ya mtu yamekomaa kabisa au kumwita mtu huyu mwenye haki au mkamilifu, aina hii ya mtu tayari amechukua hatua ya kuelekea kwenye awamu ya ukomavu katika maisha; mtu huyu tayari anaweza kuja mbele ya Mungu, kusimama ana kwa ana na neno la Mungu na kuwa ana kwa ana na Mungu. Kwa sababu mtu wa aina hii tayari amepitia mengi sana yanayohusu neno la Mungu, amepitia majaribio yasiyokadirika na kupitia matukio yasiyokadirika ya nidhamu, hukumu na kuadibu kutoka kwa Mungu, unyenyekevu wake kwa Mungu si wa kutegemea chochote bali ni kamili. Maarifa yao kwa Mungu yamebadilika kutoka kwenye kufichika akilini hadi kwa maarifa wazi na hakika, kutoka kwenye hali ya juujuu hadi kina, kutoka kwenye hali ya kutoeleweka na kutokuwa bainifu hadi hali ya umakinifu na uyakinifu, na wamebadilika kutoka kwenye kutafutatafuta kwa bidii na kutafuta kwa njia iliyo baridi hadi katika hali ya kuwa na maarifa kwa hakika na utoaji ushuhuda wenye mnato. Inaweza kusemekana kwamba watu katika awamu hii wamemiliki uhalisi wa ukweli wa neno la Mungu, kwamba wamepitia kwenye njia ya utimilifu kama vile Petro alivyopita. Huyu ndiye mtu wa aina ya tano, yule anayeishi katika hali ya kuwa mkomavu—awamu ya kuwa mtu mzima.

Desemba 14, 2013

Iliyotangulia: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Inayofuata: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp