28 Tunakusanyika kwa Furaha Kumsifu Mungu

Sifuni na muwe na furaha! Mungu amerudi kama mshindi!

Ni wajibu wetu kumshuhudia Mungu na kumsifu Mungu.

1

Tunakusanyika kwa furaha kumsifu Mungu, na tuna furaha sana.

Tunafuata nyayo za Mungu na kuhudhuria sikukuu.

Tunamsifu Mungu mwenye mwili Aanzapo enzi mpya.

Mungu Mwenyewe anafanya kazi na kunena kati yetu,

Anahukumu udhalimu wote wa mwanadamu

na kufichua upotovu wake.

Uso kwa uso, tunashuhudia kuonekana kwa Mungu.

Tabia Yake yenye rehema, uadhama na haki.

Sifuni na muwe na furaha! Mungu amerudi kama mshindi!

Sifuni na muwe na furaha! Mungu amerudi kama mshindi!

2

Tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunamwomba Mungu,

na tuna nguvu mioyoni mwetu.

Kwa kuelewa ukweli,

tuna njia mpya ya kufuata na tunaangaziwa mioyoni mwetu.

Tunauishi ukweli kumridhisha Mungu na mioyo yetu ina amani.

Tunapitia hukumu ya Mungu na Yeye anatakasa upotovu wetu.

Ni ya kupendeza, tabia Yake ya haki.

Tumeonja upendo wa kweli wa Mungu na kupata wokovu Wake mkuu.

Tumebarikiwa tunapomsifu na tunashuhudia Kwake.

Sifuni na muwe na furaha! Mungu amerudi kama mshindi!

Sifuni na muwe na furaha! Mungu amerudi kama mshindi!

Mungu amemshinda Shetani na amefanyiza kikundi cha washindi.

Joka kubwa jekundu

limeaibishwa na kushindwa kabisa.

Matendo ya Mungu yamefichuliwa kwa wanadamu kikamilifu.

Tunamwona Mungu ni mwenye busara na mweza sana.

Kwa wokovu Wake, Mungu awaonyesha wanadamu neema nyingi, hakika.

Tukishawishika kabisa, tunasujudu katika ibada kwa moyo wote.

Sisi viumbe walioumbwa tutampenda na kumtii milele.

Sifuni na muwe na furaha! Mungu amerudi kama mshindi!

Sifuni na muwe na furaha! Mungu amerudi kama mshindi!

Iliyotangulia: 27 Ni Mwenyezi Mungu Anayetuokoa

Inayofuata: 29 Ufalme wa Mungu Umetimizwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp