Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

718 Jinsi ya Kufuata Vizuri Hatua ya Mwisho ya Njia

1 Lazima ukumbuke kwamba maneno haya yamezungumzwa sasa: Baadaye, utapitia shida kubwa zaidi na mateso makubwa zaidi! Kukamilishwa si jambo la kawaida au rahisi. Angalau kabisa lazima uwe na imani ya Ayubu au labda hata imani kubwa kuliko yake. Unapaswa kujua kwamba majaribio wakati ujao yatakuwa makubwa zaidi kuliko majaribio ya Ayubu, na kwamba bado unapaswa kupitia kuadibiwa kwa muda mrefu. Je, hili ni jambo rahisi? Ikiwa ubora wako wa tabia hauwezi kuboreshwa, uwezo wako wa kuelewa umepungukiwa, na unajua kidogo sana, basi wakati huo hutakuwa na ushuhuda wowote, lakini utakuwa mpumbavu, kitu cha kuchezewa na Shetani. Ikiwa huwezi kushikilia maono sasa, basi huna msingi wowote hata kidogo, na utaondolewa siku zijazo!

2 Kila sehemu ya barabara si rahisi kutembea, kwa hiyo usichukulie hili kwa urahisi. Chunguza hili kwa uangalifu sasa na ufanye maandalizi ya jinsi ya kutembea hatua ya mwisho kabisa ya njia hii. Hii ndiyo njia ambayo inapaswa kuchukuliwa siku zijazo na watu wote wanapaswa kuichukua. Huwezi kuruhusu ufahamu huu wa sasa uingie katika sikio moja na kutokea kwa hilo lingine, wala usifikiri kwamba kile Ninachosema kwako yote ni kupoteza pumzi. Siku itakuja wakati ambapo utakitumia vizuri—maneno hayawezi kusemwa bure. Huu ndio wakati wa kujitayarisha; ni wakati wa kuandaa njia kwa ajili ya siku zijazo. Unapaswa kuandaa njia ambayo unapaswa kutembea baadaye; unapaswa kuwa na hangaiko na wasiwasi kuhusu jinsi utakavyoweza kusimama imara baadaye na kujiandaa vizuri kwa ajili ya njia yako ya baadaye. Usiwe mlafi na mvivu!

3 Lazima ufanye kila kitu unachoweza kabisa kutumia vizuri muda wako ili upate kila kitu unachohitaji. Nakupa kila kitu ili uweze kuelewa. Kwa kupitia dhiki kubwa zaidi, ufahamu wa kweli ndani ya watu wote utafanikishwa. Hii ni hatua ya kazi. Mara tu unapofahamu kikamilifu maono yaliyoshirikishwa leo na ufanikishe kuwa na kimo halisi, dhiki zozote utakazopitia wakati ujao hazitakushinda—utaweza kuzihimili. Wakati Nimekamilisha hatua hii ya mwisho ya kazi na Nimemaliza kuyatamka maneno ya mwisho, baadaye watu watahitaji kutembea njia yao wenyewe. Hii itatimiza maneno yaliyosemwa awali: Roho Mtakatifu ana agizo kwa kila mmoja, na kazi ya kufanya katika kila mmoja.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi Unavyopaswa Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Mungu Atumai Watu Wote Wapate Njia Ng’avu

Inayofuata:Kutumika kama Foili ni Baraka ya Milele

Maudhui Yanayohusiana

 • Tilia Maanani Majaliwa ya Binadamu

  1 Mungu anawahimiza watu wa makabila yote, nchi zote na hata nyanja: Sikilizeni sauti ya Mungu na kuona kazi Yake; tilia maanani jaala ya binadamu; mf…

 • Ni Muumba Pekee Anayemhurumia Binadamu Huyu

  1 Ni Muumba pekee anayeshiriki na binadamu mapatano ya huruma na upendo yasichovunjika. Ni Yeye pekee Anayetunza viumbe Wake wote, vuimbe Wake wote. K…

 • Furaha Katika Nchi ya Kanaani

  1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu kuingia kati…

 • Upendo wa Kweli

  1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha kutoka kwa ne…