986 Mwili Unaweza Kuharibu Majaliwa Yako

1 Ikiwa watu wanaweza kweli kuiona vizuri njia sahihi ya maisha ya binadamu na vilevile kusudi la usimamizi wa Mungu wa binadamu, wasingeshikilia mategemeo yao ya baadaye na majaliwa yao binafsi kama hazina mioyoni mwao. Kisha wasingetataka tena kuwatumikia wazazi wao, ambao ni wabaya zaidi kuliko nguruwe na mbwa. Wote wanapaswa kuwa na ufahamu wa kina wa kile ambacho wanapaswa kuingia kwacho, na kwa mahususi wanapaswa kutatua kile wanachopaswa kuingia kwacho wakati wa mateso, na vile vile kile wanachopaswa kujiandaa nacho wakati wa majaribu ya moto. Usiwatumikie wazazi wako siku zote (kumaanisha mwili) ambao ni sawa na nguruwe na mbwa na hata ni wabaya zaidi kuliko chungu na wadudu. Kuna haja gani ya kuteseka juu ya hilo, kufikiri sana, na kupiga bongo zako?

2 Mwili si wako, bali upo katika mikono ya Mungu, ambaye kando na kukudhibiti wewe, pia Anamwamuru Shetani. Unaishi chini ya mateso ya mwili, lakini, je, mwili ni wako? Uko chini ya udhibiti wako? Kwa nini upige bongo sana juu ya hilo? Kwa nini usumbuke sana kumsihi Mungu kwa ajili ya mwili wako uliooza ambao umeshahukumiwa zamani sana, kulaaniwa na vilevile kutiwa najisi na roho wachafu? Kuna haja gani ya kuwaweka washirika wa Shetani karibu sana na moyo wako? Huna wasiwasi kwamba mwili unaweza kuuharibu mustakabali wako halisi, matumaini yako mazuri, na hatima ya kweli ya maisha yako?

Umetoholewa kutoka katika “Kusudi la Kuwasimamia Binadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 985 Mwanadamu Hawezi Kuweka Kando Mwili Wake kwa Muda Huu Mfupi?

Inayofuata: 987 Tafuta Kuwa Maonyesho ya Utukufu wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp