736 Ni kwa Kumwogopa Mungu tu Ndiyo Maovu Yanaweza Kuepukwa

1 Kwanza kabisa tunajua kwamba tabia ya Mungu ni adhama, ni hasira. Yeye si kondoo ili achinjwe na yeyote; na hata zaidi Yeye si kikaragosi ili adhibitiwe na watu vyovyote vile wanavyotaka. Yeye pia si hewa tupu ili kuamrishwa huku na kule na watu. Kama kweli unasadiki kwamba Mungu yupo, unafaa kuwa na moyo unaomcha Mungu, na unafaa kujua kwamba kiini halisi cha Mungu hakifai kughadhabishwa. Ghadhabu hii inaweza kusababishwa na neno; pengine fikira; pengine aina fulani ya tabia bovu; pengine tabia ya upole tabia inayoweza kuruhusiwa kwenye macho na maadili ya binadamu; au pengine inasababishwa na falsafa, nadharia. Hata hivyo, punde unapomghadhabisha Mungu, fursa yako inapotea na siku zako za mwisho zinakuwa zimewasili. Hili ni jambo baya!

2 Kwanza kabisa tunajua kwamba tabia ya Mungu ni adhama, ni hasira. Yeye si kondoo ili achinjwe na yeyote; na hata zaidi Yeye si kikaragosi ili adhibitiwe na watu vyovyote vile wanavyotaka. Yeye pia si hewa tupu ili kuamrishwa huku na kule na watu. Kama kweli unasadiki kwamba Mungu yupo, unafaa kuwa na moyo unaomcha Mungu, na unafaa kujua kwamba kiini halisi cha Mungu hakifai kughadhabishwa. Kama huelewi kwamba Mungu hawezi kukosewa, basi pengine humchi Mungu, na pengine unamkosea Yeye kila wakati. Kama hujui namna ya kumcha Mungu, basi huwezi kumcha Mungu, na hutaweza kujua namna ya kujiweka kwenye njia ya kutembelea kwa njia ya Mungu—kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Punde unapokuwa na habari, unaweza kuwa na ufahamu kwamba Mungu hawezi kukosewa, kisha utajua ni nini maana ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Umetoholewa kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 735 Njia ya Lazima Kuogopa Mungu na Kujitenga na Maovu

Inayofuata: 737 Mwanadamu Anapaswa Kuwa na Moyo Umwogopao Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp