Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

1001 Kila Kitu Afanyacho Mungu ni cha Haki

1 Ufahamu wa Mungu si kusema hiki au kile kumhusu Mungu kulingana na vile binadamu huvitazama vitu. Hakuna ukweli katika njia ambayo binadamu huvitazama vitu. Lazima uone kiini cha Mungu ni nini, tabia ya Mungu ni gani. Watu hawapaswi kuona kiini cha Mungu kulingana na mambo yaliyo nje ya kile ambacho Mungu amefanya au ameshughulikia. Tabia ya Mungu ni yenye haki. Yeye humtendea kila mtu kwa hali sawa, ambayo haimaanishi kwamba kwa sababu mtu mwenye haki anaweza kustahimili majaribu kwamba hatakiwi kuyapitia, kwamba mtu mwenye haki anatakiwa kuhifadhiwa. Sio hivyo. Ana haki ya kukujaribu. Haya ni maonyesho ya tabia Yake ya haki. Mungu atafanya kile Anachotaka, na Mungu ana haki ya kutofanya jambo hilo kwa njia hii. Ana haki ya kuyashughulikia mambo haya Yeye mwenyewe. Tabia Yake mwenyewe ni yenye haki.

2 Haki kamwe sio adilifu na ya maana, kugawa moja mara mbili, kukufidia wewe kulingana na kiasi cha kazi unayofanya au kukulipa kwa kiasi cha kazi ambayo umeifanya. Hii si haki ya Mungu. Unaamini kwamba kila mtu hufanya sehemu yake, na mgawanyo kulingana na kazi iliyofanywa, na kwamba kila mtu hupokea haki yake kulingana na matokeo ya kazi yake; hii yenyewe ndio haki. Tuseme Mungu angemwangamiza Ayubu baada ya Ayubu kuwa na ushuhuda Wake. Mungu ni mwenye haki hapa, pia. Kwa nini tuseme kwamba Yeye ni mwenye haki? Kusema kwamba Mungu ni mwenye haki katika kufanya hili, kwa nini tuseme jambo kama hili? Haki ni kitu ambacho ikiwa jambo fulani linalingana na dhana za watu, watu husema Mungu ni mwenye haki, ambalo ni rahisi kiasi, lakini ikiwa watu hawaoni kwamba linalingana na dhana zao, ikiwa ni jambo ambalo watu hawawezi kulifahamu, hilo lingehitaji juhudi kubwa ya watu kulieleza hilo kama haki. Kiini cha Mungu ni haki. Ingawa si rahisi kufahamu yale afanyayo Mungu, yote Afanyayo ni yenye haki. Ni kawaida kwamba watu hawafahamu.

3 Unaona kwamba Mungu alipomtoa Petro kwa Shetani, vile Petro alijibu: “Mwanadamu hawezi kuelewa maana ya kile unachofanya, lakini yote ambayo Wewe hufanya yana makusudi yako mema. Kuna haki ndani ya hayo yote. Ninawezaje kukosa kutamka sifa kwa ajili ya matendo Yako ya hekima?” Kila jambo afanyalo Mungu ni haki. Ingawa huwezi kulitambua, hupaswi kufanya hukumu jinsi upendavyo. Likionekana kwako kuwa bila mantiki, au kama una dhana kulihusu, na kisha useme kwamba Mungu si mwenye haki, hili ni la kukosa busara kabisa. Unaona kwamba Petro alipata kwamba mambo mengine hayafahamiki, ilhali alikuwa na hakika kwamba hekima ya Mungu ilikuwa hapa, kwamba makusudi mema ya Mungu yalikuwa katika hilo lote. Mwanadamu hawezi kuelewa kila jambo. Kuna mambo mengi sana yasiyoeleweka. Kujua tabia ya Mungu kwa kweli si jambo rahisi.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kufahamu Tabia Yenye Haki ya Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia:Jinsi ya Kuitemba Njia ya Petro

Inayofuata:Unaitembea Njia ya Paulo Wakati Hufuatilii Ukweli

Maudhui Yanayohusiana

 • Umuhumi wa Maombi

  1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, ku…

 • Furaha Katika Nchi ya Kanaani

  1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu kuingia kati…

 • Upendo wa Kweli

  1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha kutoka kwa ne…

 • Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

  1 Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safar…