890 Kiini cha Kristo ni Upendo

1 Kwa wanadamu, kiini cha Kristo ni upendo; kwa wale wanaomfuata, ni upendo usio na mpaka. Kama Hangekuwa na upendo au huruma, basi watu wasingekuwa bado wanammfuata. Katika kazi Mungu Anayofanyia binadamu wakati ambapo Yeye ni mwenye mwili, kiini Chake dhahiri na maarufu zaidi ni upendo; ni stahamala isiyo na mwisho. Mnafikiria, “Ikiwa Mungu ananuia kumwangamiza mtu, Atafanya hivyo, na ikiwa Anamchukia mtu, Atamwadhibu, atamlaani, kumhukumu na kumwadibu mtu huyo; Yeye ni mkali sana! Kama Ana hasira kwa watu, watu watatetemeka kwa hofu na hawataweza kusimama mbele Yake.” Lakini, hilo si kweli; hii ni njia moja tu ambayo kwayo tabia ya Mungu huonyeshwa. Mwishowe, azma Yake bado ni wokovu. Upendo Wake unadhihirika kupitia ufichuzi wote wa tabia Yake.

2 Wakati wa kufanya kazi katika mwili, jambo ambalo Mungu hufichua zaidi kwa watu ni upendo. Uvumilivu ni kuwa na huruma kwa sababu ya upendo ndani, na azma Yake bado ni kuwaokoa watu. Mungu anaweza kuwa na huruma juu ya watu kwa sababu Yeye Ana upendo. Kama Mungu angekuwa tu na chuki na hasira, na kutoa tu hukumu na kuadibu, bila upendo wowote ndani ya hayo, basi hali isingekuwa muonavyo sasa na maafa yangewafikia nyinyi watu. Je, Angeweza kuwapa ukweli? Mngekuwa mmelaaniwa baada ya kurudi na kuhukumiwa, ni vipi binadamu huyu bado angekuwepo sasa? Chuki ya Mungu, ghadhabu, na haki yameonyeshwa yote kwa msingi wa kuokoa kundi hili la watu. Upendo na huruma pamoja na subira kubwa mno pia yako ndani ya tabia hizi. Hii chuki ina hisia ya kutokuwa na chaguo lingine, ni kwa pamoja na shaka isiyokuwa na mpaka na kutazamia kwa binadamu!

3 Chuki ya Mungu imelengwa kwa upotovu wa binadamu, imelengwa ukaidi wa binadamu na dhambi; ni ya upande mmoja, na imeimarishwa juu ya msingi wa upendo. Ni wakati tu kuna upendo ndipo chuki huwepo. Chuki ya Mungu kuelekea kwa binadamu ni tofauti na chuki Yake kuelekea kwa Shetani, kwa sababu Mungu anaokoa watu, na Yeye hamwokoi Shetani. Tabia ya Mungu ya haki imeishi kuwa, Yeye siku zote Amekuwa na ghadhabu, haki na hukumu. Hayakuja tu yalipoonyeshwa kwa binadamu. Kwa kweli, bila kujali kama Yeye ni mwenye haki au Mwenye utukufu, au Yeye Huonyesha hasira kali, Yeye huokoa watu na hutekeleza mpango Wake wa usimamizi wote kwa sababu ya upendo. Si kiasi cha upendo Alionao, badala yake Ana asilimia mia moja ya upendo. Kama Angekuwa na upendo wowote chini ya hii, basi binadamu asingeokolewa. Mungu ametoa upendo Wake wote kwa watu.

Umetoholewa kutoka katika “Upendo wa Kweli wa Mungu kwa Wanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 889 Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

Inayofuata: 891 Mungu Huwajali Sana wale Ambao Atawaokoa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp