Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

1027 Mungu Huvumilia Aibu Kubwa Kuwaokoa Wanadamu

1 Mwanadamu na Mungu kimsingi hawafanani na wanaishi katika dola mbili tofauti. Mwanadamu hawezi kuielewa lugha ya Mungu, sembuse kuyaelewa mawazo ya Mungu. Ni Mungu pekee ndiye Anayemwelewa mwanadamu na haiwezekani kwa mwanadamu kumwelewa Mungu. Kwa hiyo, Mungu ni lazima Awe mwili na awe wa aina sawa na mwanadamu, kuvumilia fedheha na maumivu mengi ili kuwaokoa binadamu, ili waweze kuielewa na kuifahamu kazi ya Mungu. Kwa nini Mungu siku zote Anamwokoa mwanadamu na hajawahi kukata tamaa? Hii si kwa sababu ya upendo Wake kwa mwanadamu? Anamwona binadamu akiharibiwa na Shetani na Hawezi kuvumilia kuacha au kukata tamaa. Kwa hivyo ana mpango wa usimamizi.

2 Kama ingekuwa wanavyofikiri watu na Angewaangamiza binadamu punde tu anaposhikwa na hasira, basi kusingekuwa na haja ya kuteseka kwa njia hii kumwokoa mwanadamu. Na hasa ni kwa sababu ya maumivu yaliyopitiwa na kupata mwili Kwake ndiyo upendo Wake unavumbuliwa kidogokidogo na binadamu na unafahamika kwa watu wote. Kama Mungu asingefanya kazi ya aina hii sasa, watu wangejua tu kwamba kuna Mungu mbinguni na kwamba Anawapenda binadamu. Hali ingekuwa hivi, hiyo ingekuwa mafundisho tu, na watu kamwe wasingeweza kuuona na kuupitia upendo wa Mungu wa kweli.

3 Ni kwa Mungu tu kufanya kazi Yake katika mwili ndipo watu wanaweza kuwa na uelewa wa kweli juu Yake. Ufahamu huu si wa kufikirika au mtupu na wala siyo mafundisho ambayo mtu anayaunga mkono kwa maneno matupu, lakini badala yake ni ufahamu wa kweli sana, kwa sababu upendo ambao Mungu anampatia mwanadamu ni wa manufaa ya kweli. Ni upendo mkubwa kiasi gani ambao Yesu aliwapa watu? Alihudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu waliopotoka kwa kusulubiwa, Alikuja kukamilisha kazi ya ukombozi kwa ajili ya binadamu, hadi aliposulubiwa. Upendo huu hauna mipaka na kazi ambayo Mungu ameifanya ni ya muhimu sana.

Umetoholewa kutoka katika “Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia:Mungu Kupitia Maumivu ya Mwanadamu ni kwa Maana Sana

Inayofuata:Jinsi ya Kufahamu Uenyezi na Utendaji wa Mungu

Maudhui Yanayohusiana

 • Tilia Maanani Majaliwa ya Binadamu

  1 Mungu anawahimiza watu wa makabila yote, nchi zote na hata nyanja: Sikilizeni sauti ya Mungu na kuona kazi Yake; tilia maanani jaala ya binadamu; mf…

 • Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

  1 Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safar…

 • Njia Yote Pamoja na Wewe

  1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga. Maneno Yako ya…

 • Umuhumi wa Maombi

  1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, ku…