756 Mshinde Shetani kwa Ukweli ili Upatwe na Mungu

1 Wakati wa kazi wa utoaji Wake wa kudumu na msaada kwa binadamu, Mungu anaambia binadamu kuhusu mapenzi Yake na mahitaji Yake yote, na anaonyesha vitendo Vyake, tabia, na kile Anacho na alicho kwa binadamu. Lengo ni kuweza kumtayarisha binadamu ili awe na kimo, na kumruhusu binadamu kupata ukweli mbalimbali kutoka kwa Mungu wakati anaendelea kumfuata Yeye—ukweli ambao ni silaha alizopewa binadamu na Mungu ambazo atatumia kupigana na Shetani. Hivyo akiwa na silaha hizo, binadamu lazima akabiliane na mitihani ya Mungu. Mungu anazo mbinu na njia nyingi za kumjaribu binadamu, lakini kila mojawapo inahitaji “ushirikiano” wa adui wa Mungu: Shetani.

2 Baada ya kumpa binadamu silaha ambazo atatumia kupigana na Shetani, Mungu anamkabidhi binadamu kwa Shetani na kuruhusu Shetani “kujaribu” kimo cha binadamu. Kama binadamu anaweza kufanikiwa dhidi ya uundaji wa vita vya Shetani, kama anaweza kutoroka mizunguko ya Shetani na bado akaishi, basi mwanadamu atakuwa ameupita mtihani. Lakini kama binadamu atashindwa kuondoka kwenye uundaji wa vita vya Shetani, na kujinyenyekeza kwa Shetani, basi hatakuwa ameupita mtihani. Haijalishi ni kipengele kipi cha binadamu ambacho mungu anachunguza, kigezo cha uchunguzi Wake ni kama binadamu atasimama imara katika ushuhuda wake atakaposhambuliwa na Shetani au la, kujua kama amemuacha Mungu au la na akajisalimisha na akajinyenyekeza kwa Shetani baada ya kunaswa na Shetani.

3 Iwapo binadamu anaweza kuokolewa au la yote haya yanategemea kama anaweza kumzidi na kumshinda Shetani, na kama ataweza kupata uhuru au la yanategemea kama anaweza kuinua, yeye binafsi, silaha alizopewa na Mungu ili kushinda utumwa wa Shetani, na kumfanya Shetani kuwacha kabisa tumaini na kumwacha pekee. Kama Shetani ataliacha tumaini na kumwachilia mtu, hii inamaanisha kwamba Shetani hatawahi tena kujaribu kuchukua mtu huyu kutoka kwa Mungu hatawahi tena kumshtaki na kuingilia kati mtu huyu, hatawahi tena kutaka kumtesa au kumshambulia; mtu kama huyu tu ndiye atakuwa kwa kweli amepatwa na Mungu. Huu ndio mchakato mzima ambao Mungu anapata watu.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 755 Ni Wale tu Wanaomshinda Shetani Ndio Wanaookolewa

Inayofuata: 757 Onyo la Ushuhuda wa Ayubu kwa Vizazi vya Baadaye

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp