456 Beba Kazi ya Roho Mtakatifu Katika Kuingia Kwako
1 Mnapoipokea kazi ya Roho Mtakatifu, mnapaswa kujikita zaidi katika kuingia kwenu, na wakati huo huo, kuona kipi ni kazi ya Roho Mtakatifu na kipi ni kuingia kwenu, vilevile kujumuisha kazi ya Roho Mtakatifu katika kuingia kwenu, ili kwamba muweze kukalishwa Naye vizuri na kuruhusu hulka ya kazi ya Roho Mtakatifu kuletwa pamoja ndani yenu. Wakati mnapitia uzoefu wenu wa kazi ya Roho Mtakatifu, mnamjua Roho Mtakatifu, vilevile nyinyi wenyewe, na katikati ya mateso makali, mnajenga uhusiano wa kawaida pamoja na Mungu, na uhusiano baina yenu na Mungu unakuwa wa karibu siku kwa siku. Baada ya michakato mingi ya kupogolewa na kusafishwa, mnakuza upendo wa kweli kwa Mungu.
2 Hii ndiyo sababu mnapaswa kutambua kwamba mateso, mapigo, na dhiki havitishi; kinachoogopesha ni kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu tu lakini sio kuingia kwenu. Siku inapofika kwamba kazi ya Mungu imemalizika, mtakuwa mmefanya kazi bure; ingawa mmepitia uzoefu wa kazi ya Mungu, hamtakuwa mmemjua Roho Mtakatifu au kuwa na kuingia kwenu wenyewe. Nuru anayopewa mwanadamu na Roho Mtakatifu si ya kudumisha hisia za mwanadamu; ni kufungua njia kwa ajili ya kuingia kwa mwanadamu, vilevile kumruhusu mwanadamu kumjua Roho Mtakatifu, na kuanzia hapo anakuza moyo wa uchaji na ibada kwa Mungu.
Umetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili