623 Tabia ya Aina Hii Inaweza Kufaa kwa Huduma ya Mungu?

1 Kama watu wanaomhudumia Mungu, kila mmoja wenu lazima aweze kulinda maslahi ya kanisa katika kila kitu mnachofanya, badala ya kuzingatia tu masilahi yenu wenyewe. Haikubaliki ninyi kutenda kila mtu peke yake, daima mkidhoofishana. Watu wanaotenda kwa namna hiyo hawafai kumhudumia Mungu! Watu kama hao wana tabia mbaya sana; hawana ubinadamu hata kidogo ndani yao. Wao ni Shetani asilimia mia moja! Wao ni wanyama! Hata sasa, mambo kama haya bado hutokea miongoni mwenu; hata mnafika kiasi cha kushambuliana wakati wa ushirika; mkitafuta visingizio kwa makusudi na kughadhabika sana mnapogombana kuhusu suala fulani lisilo la maana, pasiwe na mtu aliye radhi kujiweka kando, kila mtu akimfichia mwenzake fikira zake za ndani, akimtazama yule mwingine kwa makini na kuwa mwangalifu daima.

2 Je, tabia ya aina hii inafaa katika kumhudumia Mungu? Je, kazi kama hiyo yako inaweza kuwapa ndugu zako chochote? Huwezi tu kuwaongoza watu kwenye njia sahihi ya maisha, lakini kwa kweli unawajaza ndugu zako tabia zako potovu. Je, huwadhuru wengine? Dhamiri yako ni mbaya na ni mbovu kabisa! Huingii katika uhalisi, wala huuweki ukweli katika vitendo. Aidha, unawafichulia wengine asili yako mbaya mno bila aibu. Huna aibu hata kidogo! Umeaminiwa ndugu hawa, lakini unawapeleka kuzimuni. Je, wewe si mtu ambaye dhamiri yake imekuwa mbovu? Huna aibu hata kidogo!

Umetoholewa kutoka katika “Hudumu Jinsi Waisraeli Walivyohudumu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 622 Matokeo ya Huduma ya Shauku kwa Mungu

Inayofuata: 624 Mungu Hawasifu Wale Wanaohudumu Kama Paulo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp