Kuingia Katika Uzima (IV)
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 483)
Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watiifu kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini. Imani kama hii ni kujidanganya, kujihakikishia, na kujishukuru. Kama imani yako haijajengwa katika msingi wa utii kwa Mungu, basi hatimaye utaadhibiwa kwa kumpinga Mungu. Wale wote ambao hawatafuti utii kwa Mungu kwa imani yao wanampinga Mungu. Mungu anaomba kwamba watu watafute ukweli, kwamba wawe na kiu ya neno la Mungu, na wanakula na kunywa maneno ya Mungu, na kuyaweka katika matendo, ili waweze kupata utii kwa Mungu. Kama motisha zako ni hizo kweli, basi Mungu atakuinua juu hakika, na hakika Atakuwa mwenye neema kwako. Hakuna anayeweza kutilia shaka hili, na hakuna anayeweza kulibadilisha. Ikiwa motisha zako sio kwa ajili ya utii kwa Mungu, na una malengo mengine, basi yote ambayo unasema na kufanya—maombi yako mbele ya Mungu, na hata kila tendo lako—litakuwa linampinga Mungu. Unaweza kuwa unaongea kwa upole na mwenye tabia ya upole, kila tendo lako na yale unayoyaonyesha yanaweza kuonekana ni sahihi, unaweza kuonekana kuwa mtu anayetii, lakini linapofikia suala la motisha zako na mitazamo yako juu ya imani kwa Mungu, kila kitu unachofanya kipo kinyume cha Mungu, na ni uovu. Watu wanaoonekana watii kama kondoo, lakini mioyo yao inahifadhi nia mbovu, ni mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo, wanamkosea Mungu moja kwa moja, na Mungu hatamwacha hata mmoja. Roho Mtakatifu atamfichua kila mmoja wao, ili wote waweze kuona kwamba kila mmoja wa hao ambao ni wanafiki hakika watachukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu. Usiwe na shaka: Mungu atamshughulikia na kumkomesha kila mmoja.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 484)
Kama huwezi kukubali nuru mpya ya Mungu, na huwezi kuelewa yote ambayo Mungu anayafanya leo, na huyafuati, au unayatilia shaka, unayahukumu, au unayachunguza na kuyachambua, basi huna akili ya kuweza kumtii Mungu. Kama, nuru ya hapa na sasa inatokea, na bado unathamini nuru ya jana na kuipinga kazi mpya ya Mungu, basi wewe si chochote zaidi ya mtu mpumbavu—wewe ni mmoja wa wale wanaompinga Mungu kwa makusudi. Jambo muhimu katika kumtii Mungu ni kuitambua nuru mpya, na kuweza kuikubali na kuiweka katika vitendo. Huu pekee ndio utii wa kweli. Wale ambao hawana hiari ya kuwa na kiu ya Mungu hawana uwezo wa kuwa na akili ya kumtii Mungu, na wanaweza tu kumpinga Mungu kama matokeo ya kuridhika kwao na jinsi hali ilivyo. Kwamba mtu hawezi kumtii Mungu ni kwa sababu amefungwa na kitu kilichotangulia kabla. Mambo ambayo yalikuja kabla yamewapatia watu kila namna ya dhana na njozi za uongo kuhusu Mungu ambazo zimekuwa ndiyo taswira ya Mungu akilini mwao. Hivyo, kile wanachoamini ni dhana zao wenyewe, na viwango vya mawazo yao wenyewe. Ikiwa utampima Mungu ambaye anafanya kazi halisi leo dhidi ya Mungu wa mawazo yako mwenyewe basi imani yako inatoka kwa Shetani, na ni kulingana na mapendeleo yako mwenyewe—na Mungu hataki imani kama hii. Bila kujali sifa zao ni za juu sana kiasi gani, na bila kujali kujitoa kwao—hata kama wamejitoa jitihada za maisha yao yote katika kazi Yake, na wamejitoa mhanga—Mungu hakubali imani yoyote kama hii. Anawaonyesha tu neema kidogo, na kuwaacha waifurahie kwa muda. Watu kama hawa hawawezi kuuweka ukweli katika vitendo, Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yao, na badala yake Mungu atamwondoa kila mmoja wao. Bila kujali ama ni wazee au vijana, wale ambao hawamtii Mungu katika imani yao na wana motisha mbaya, ni wale ambao wanapinga na kuingilia, na watu kama hao bila kuhoji wataondolewa na Mungu. Wale ambao hawana utii kwa Mungu hata kidogo, ambao wanalitambua tu jina la Mungu, na wana ufahamu kiasi juu ya mapenzi na wema wa Mungu lakini hawaenendi sawa na hatua za Roho Mtakatifu na hawatii kazi na maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu—watu kama hao wanaishi katikati ya neema ya Mungu, na hawatachukuliwa na kukamilishwa na Mungu. Mungu huwakamilisha watu kupitia utii wao, kupitia kula kwao, kunywa na kufurahia maneno ya Mungu, na kupitia mateso na usafishaji maishani mwao. Ni kupitia tu imani kama hii ndipo tabia za watu zinaweza kubadilika, baada ya hapo tu ndipo wanaweza kuwa na maarifa ya kweli kuhusu Mungu. Kutoridhika na kuishi katikati ya neema za Mungu, kuwa na kiu ya ukweli, na kutafuta ukweli, na kunuia kuchumwa na Mungu—hii ndio maana ya kumtii Mungu katika hali ya utambuzi; hii ndiyo aina ya imani ambayo Mungu anataka. Watu ambao hawafanyi kitu zaidi ya kufurahia neema za Mungu hawawezi kukamilishwa, au kubadilishwa, na utii wao, uchaji Mungu, na upendo na ustahimilivu vyote hivyo ni vya juujuu tu. Wale ambao wanafurahia tu neema za Mungu hawawezi kumfahamu Mungu kweli, na hata pale wanapomjua Mungu, maarifa yao ni ya juujuu, na wanasema mambo kama vile Mungu anampenda mwanadamu, au Mungu ni mwenye huruma kwa mwanadamu. Hii haiwakilishi maisha ya mwanadamu, na haionyeshi kwamba kweli watu wanamjua Mungu. Ikiwa, maneno ya Mungu yatakapowasafisha, au majaribu yake yatakapowajia, watu hawataweza kumtii Mungu—ikiwa, badala yake, watakuwa watu wa mashaka na kuanguka chini—basi hawana utii hata kidogo. Ndani yao, kuna kanuni na masharti mengi kuhusu imani kwa Mungu, uzoefu wa zamani ambao ni matokeo ya miaka mingi ya imani, au mafundisho mbalimbali kutoka kwenye Biblia. Je, watu kama hawa wanaweza kumwamini Mungu? Watu hawa wamejawa na mambo ya wanadamu—wanawezaje kumtii Mungu? Wote wanatii kulingana na mapendeleo yao binafsi—je, Mungu anaweza kutamani utii kama huu? Huku sio kumtii Mungu bali ni kufungamanishwa na mafundisho, ni kujiridhisha na kujifariji mwenyewe. Ikiwa unasema kwamba huu ni utii kwa Mungu, je, hivi hutakuwa unamkufuru Yeye? Wewe ni Farao wa Misri, unafanya uovu, unajishughulisha katika kazi ya kumpinga Mungu—je, Mungu anaweza kutaka kazi kama hii? Ni bora ungefanya haraka ukatubu na kuweza kujitambua kiasi fulani. Ikiwa sivyo, ni bora uende nyumbani: hivyo itakuwa imekusaidia sana kuliko huduma yako kwa Mungu, hutaingilia wala kusumbua, utakuwa umeijua sehemu yako, na kuishi vizuri—na hiyo haitakuwa bora zaidi? Kwa namna hiyo utakuwa umeepuka kumpinga Mungu na kuweza kuadhibiwa!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 485)
Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa nyuma wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; hii ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi. Hivyo, bila utii moyoni mwake, mwanadamu ataona vigumu kufuata nyayo za Mungu. Mungu hafuati kanuni zozote, wala hachukulii hatua yoyote ya kazi Yake kama isiyobadilika. Badala yake, kazi Anayofanya daima ni mpya zaidi na daima ni juu zaidi. Kazi Yake inazidi kuwa ya utendaji kwa kila hatua, sambamba zaidi na matendo halisi ya mwanadamu. Baada tu ya mwanadamu kuwa na uzoefu wa aina hii ya kazi ndipo anaweza kufikia mabadiliko ya mwisho ya tabia yake. Maarifa ya mwanadamu ya maisha yanakua hata juu zaidi, na vivyo hivyo kazi ya Mungu pia inakuwa juu zaidi. Mwanadamu anaweza kufikia ukamilifu kwa njia hii tu na kufaa kwa matumizi ya Mungu. Kwa upande mmoja, Mungu anafanya kazi hivi ili kupinga na kubadilisha fikira za mwanadamu, na kwa upande mwingine, kumwongoza mwanadamu katika hali ya juu zaidi na kweli zaidi, hadi katika ulimwengu wa juu zaidi wa imani katika Mungu, ili mwishowe, mapenzi ya Mungu yaweze kufanyika. Wote walio na asili isiyotii wanaopinga kwa kusudi wataachwa nyuma na hatua hii ya kazi ya Mungu ya haraka na yenye kusonga mbele kwa nguvu; wale tu walio na moyo mtiifu na wako tayari kuwa wanyonge wataendelea hadi mwisho wa njia. Katika kazi kama hii, nyote mnapaswa kujua jinsi ya kutii na kuweka kando fikira zenu. Mnapaswa kuwa waangalifu katika kila hatua mnayochukua. Kama wewe ni mzembe, hakika utakuwa mmoja wa wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na yule anayemkatiza Mungu katika kazi Yake. Kabla ya kufanyiwa hatua hii ya kazi, kanuni na sheria za mwanadamu za zamani zilikuwa nyingi sana hadi akawa na msisimko zaidi, na mwishowe, akawa mwenye majivuno na kujisahau. Hivi vyote ni vikwazo vinavyomzuia mwanadamu kuikubali kazi mpya ya Mungu; vinakuwa pingamizi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Iwapo mwanadamu hana utii katika moyo wake wala tamaa ya ukweli, basi atakuwa hatarini. Ukitii tu kazi na maneno yaliyo rahisi, na huwezi kukubali yoyote yaliyo na ugumu zaidi, basi wewe ni yule anayeendelea na njia za zamani na hawezi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 486)
Kazi inayofanywa na Mungu ni tofauti kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Ukionyesha utii mkubwa katika awamu moja, lakini katika awamu ifuatayo uonyeshe utii mdogo ama usionyeshe wowote, basi Mungu atakuacha. Ukienda sambamba na Mungu anapopaa hatua hii, basi lazima uendelee kuwa sambamba Anapopaa ifuatayo. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu ambaye ni mtiifu kwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu unamwamini Mungu, lazima ubakie daima katika utii wako. Huwezi tu kutii unapotaka na kutotii usipotaka. Namna hii ya utii haikubaliki na Mungu. Kama huwezi kwenda sambamba na kazi mpya Ninayoshiriki na uendelee kuyashikilia maneno ya zamani, basi kutakuaje na ukuaji katika maisha yako? Kazi ya Mungu ni kukuruzuku kupitia neno Lake. Unapotii na kulikubali neno Lake, basi Roho Mtakatifu hakika atafanya kazi ndani yako. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa njia Ninayozungumza kabisa. Fanya Nilivyosema, na Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako mara moja. Natoa mwangaza mpya ili muweze kuona na kuwaleta kwa mwangaza wa wakati wa sasa. Unapotembea katika mwangaza huu, Roho Mtakatifu ataanza kazi ndani yako mara moja. Kuna wengine wanaoweza kuwa wakaidi na kusema, “Sitafanya tu Usemavyo.” Basi Nakwambia kwamba sasa umefika mwisho wa njia umenyauka na huna maisha zaidi. Hivyo, kwa kupitia mabadiliko ya tabia yako, ni muhimu kabisa kwenda sambamba na mwangaza wa sasa. Roho Mtakatifu hafanyi kazi tu kwa baadhi ya wanadamu wanaotumiwa na Mungu, lakini hata zaidi kanisani. Anaweza kuwa akifanya kazi kwa yeyote. Anaweza kufanya kazi ndani yako sasa, na baada ya wewe kuwa na uzoefu nayo, Anaweza kufanya kazi ndani ya mtu mwingine ajaye. Fanya hima ufuate; unapozidi kufuata mwangaza wa sasa, ndivyo maisha yako yanaweza ku kua. Haijalishi yeye ni mwanadamu wa aina gani, alimradi Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yake, kuwa na hakika kufuata. Chukua uzoefu wake kupitia wako mwenyewe, na utapokea mambo ya juu hata zaidi. Kwa kufanya hivyo utaona ukuaji haraka zaidi. Hii ni njia ya ukamilifu kwa mwanadamu na njia ambayo maisha hukua. Njia ya ukamilifu inafikiwa kupitia utii wako wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hujui ni kupitia kwa mtu wa aina gani ndiyo Mungu Atafanya kazi kukukamilisha, wala kupitia mtu yupi, tukio, ama jambo ndiyo Atakuwezesha kuingia katika umiliki na kupata ufahamu fulani. Ukiweza kutembea kwenye njia hii sawa, hii inaonyesha kwamba kuna matumaini makubwa kwako kukamilishwa na Mungu. Kama huwezi kufanya hivyo, inaonyesha kwamba maisha yako ya baadaye ni ya dhalili na giza. Mara unapoenda kwenye njia iliyo sahihi, utapata ufunuo katika mambo yote. Bila kujali yale ambayo Roho Mtakatifu atafichua kwa wengine, ukiendelea kupitia mambo wewe mwenyewe kwa msingi wa maarifa yao, basi uzoefu huu utakuwa sehemu ya maisha yako, na utaweza kuwakimu wengine kwa sababu ya huu uzoefu. Wale wanaowakimu wengine kwa kuyarudia maneno ni wale wasio na uzoefu wowote; lazima ujifunze kupata, kupitia mwangaza na nuru ya wengine, njia ya kutenda kabla ya kuzungumza kuhusu uzoefu na maarifa yako halisi. Hii itakuwa ya manufaa zaidi kwa maisha yako binafsi. Unapaswa kuwa na uzoefu kwa njia hii, kutii yote yatokayo kwa Mungu. Unapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu katika vitu vyote na kujifunza masomo katika vitu vyote, ili maisha yako yaweze kukua. Vitendo vya aina hii huleta ukuaji wa haraka zaidi.
Roho Mtakatifu anakupa nuru kupitia uzoefu wa vitendo vyako na kukukamilisha kupitia imani yako. Uko tayari kweli kukamilishwa? Kama kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu, basi utakuwa na ujasiri kuweka kando mwili wako, na utaweza kutekeleza maneno ya Mungu na kutokuwa mtu anayekaa tu ama mnyonge. Utaweza kutii yote yatokayo kwa Mungu, na vitendo vyako vyote, viwe vimefanywa hadharani au faraghani, vitastahiki kwa Mungu. Kama wewe ni mtu mwaminifu, na unatenda ukweli katika mambo yote, basi utakamilishwa. Wale wanadamu wadanganyifu wanaotenda njia moja mbele ya wengine na nyingine nyuma yao hawako tayari kukamilishwa. Wote ni wana wa maangamizo na uharibifu; wao si wa Mungu lakini ni wa Shetani. Hao si aina ya wanadamu waliochaguliwa na Mungu! Kama vitendo na tabia yako haviwezi kustahiki mbele ya Mungu ama kufikiriwa na Roho wa Mungu, hii ni thibitisho kwamba wewe una shida. Ukikubali tu hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kuweka umuhimu katika mabadiliko ya tabia yako ndipo utafika kwenye njia ya kukamilishwa. Ikiwa kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu na kufanya mapenzi ya Mungu, basi unapaswa kutii kazi yote ya Mungu na kutotoa neno lolote la kulalamika, wala hupaswi kutathmini ama kuhukumu kazi ya Mungu utakavyo. Haya ni masharti ya msingi kabisa ya kukamilishwa na Mungu. Mahitaji ya lazima kwa wale wanaotaka kukamilishwa na Mungu ni haya: fanya mambo yote kwa moyo unaompenda Mungu. Inamaanisha nini “kufanya mambo kwa moyo unaompenda Mungu”? Inamaanisha kwamba vitendo na tabia yako yote inaweza kuletwa mbele ya Mungu. Kwa sababu una nia sawa, iwapo vitendo vyako ni sawa ama vibaya, huogopi vikionyeshwa kwa Mungu ama kwa ndugu zako; unathubutu kuapa mbele ya Mungu. Lazime uonyeshe kila nia, fikra, na wazo lako mbele ya Mungu ili ayachunguze; ukitenda na kuingia kwa njia hii, basi maendeleo katika maisha yako yatakuwa mepesi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 487)
Kwa sababu unamwamini Mungu, basi lazima uweke imani ndani ya maneno yote ya Mungu na ndani ya kazi Yake yote. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu unamwamini Mungu, ni lazima umtii. Kama huwezi kufanya hivi, basi haijalishi iwapo unamwamini Mungu. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini. Mtu kama huyu anawezaje kutii kazi na maneno ya Mungu ambayo hayafuati fikira za mwanadamu? Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu? Hata wale walio tu na moyo nusu wa utii hawawezi kutembea hadi mwisho, sembuse hawa wadhalimu wasio na utii hata kidogo kwa mioyo yao. Kazi ya Mungu haipatwi virahisi na mwanadamu. Hata mwanadamu akitumia nguvu yake yote, ataweza kupata kipande tu na kufikia ukamilifu mwishowe. Na vipi basi kuhusu watoto wa malaika mkuu wanaotaka kuharibu kazi ya Mungu? Je, hawana hata matumaini madogo zaidi ya kupatwa na Mungu? Madhumuni Yangu katika kufanya kazi ya ushindi si tu kushinda kwa sababu ya ushindi, lakini kushinda ili kufichua haki na udhalimu, kupata ushahidi kwa ajili ya adhabu ya mwanadamu, kulaani waovu, na hata zaidi, kushinda kwa sababu ya kuwakamilisha wale walio radhi kutii. Mwishowe, wote watatengwa kulingana na aina, na mawazo ya wale wote waliokamilishwa yatajazwa na utii. Hii ndiyo kazi itakayokamilishwa mwishowe. Lakini waliojawa na uasi wataadhibiwa, kutumwa kuchomeka motoni na milele kulaaniwa. Wakati huo utakapofika, wale “mashujaa wakubwa wasioshindwa” wa awali watakuwa “waoga wanyonge na wasio na maana” wa chini zaidi na wanaoepukwa zaidi. Hii tu ndiyo inaweza kuonyesha kila kipengele cha haki ya Mungu na kufichua tabia Yake ambayo hairuhusu kosa lolote. Hili tu ndilo linaloweza kutuliza chuki iliyo moyoni Mwangu. Je, hamkubali kwamba hili ni la busara sana?
Sio wote walio na uzoefu wa kazi ya Roho Mtakatifu wanaweza kupata uzima, na sio wote katika mkondo huu wanaweza kupata uzima. Uzima sio mali ya kawaida inayoshirikisha binadamu wote, na mabadiliko ya tabia ni kitu ambacho hakifikiwi na wote kwa urahisi. Kujisalimisha kwa kazi ya Mungu lazima kugusike na kuishi kwa kudhihirishwa. Kujisalimisha kwa kiwango cha juu juu hakuwezi kupokea idhini ya Mungu, na kutii tu vipengele vya juujuu vya neno la Mungu bila kutaka mgeuzo wa tabia ya mtu, hakutaweza kuufurahisha moyo wa Mungu. Utiifu kwa Mungu na kujinyenyekeza kwa kazi ya Mungu ni kitu kimoja. Wale wanaomtii Mungu tu lakini hawatii kazi Yake hawawezi kudhaniwa kuwa watiifu, sembuse wale wasiotii kwa kweli na kwa nje hao ni wa kujipendekeza. Wale ambao kweli wanajinyenyekeza kwa Mungu wote wanaweza kufaidika kutokana na kazi na kupata ufahamu wa tabia na kazi ya Mungu. Wanadamu kama hawa tu ndio kweli wanajinyenyekeza kwa Mungu. Wanadamu kama hawa wanaweza kupata maarifa mapya kutokana na kazi mpya na kuwa na uzoefu wa mabadiliko mapya kutoka hayo. Wanadamu kama hawa tu ndio wana idhini ya Mungu; mwanadamu wa aina hii tu ndiye amekamilishwa, ndiye amepitia mabadiliko ya tabia yake. Wale wanaopokea idhini ya Mungu ni wale wanaojisalimisha kwa Mungu kwa furaha, na pia kwa neno na kazi Yake. Mwanadamu wa aina hii tu ndiye yuko sahihi; mwanadamu wa aina hii tu ndiye kweli anamtamani Mungu, na anamtafuta Mungu kwa dhati. Na kwa wale wanaozungumzia tu imani yao kwa Mungu kwa vinywa vyao lakini kwa hakika wanamlaani, ni wanadamu waliovaa barakoa, walio na sumu ya nyoka, ni wanadamu wasaliti zaidi. Siku moja hawa waovu watavuliwa barakoa zao mbovu. Je, hiyo si kazi inayofanywa leo? Wanadamu waovu daima watakuwa waovu na hawataepuka kamwe siku ya adhabu. Wanadamu wazuri daima watakuwa wazuri na watafichuliwa kazi itakapoisha. Hakuna hata mmoja wa waovu atakayedhaniwa kuwa wenye haki, wala yeyote mwenye haki atakayedhaniwa kuwa mwovu. Je, Ningemruhusu yeyote ashtakiwe kimakosa?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 488)
Maisha yako yanapoendelea, lazima daima uwe na kiingilio kipya na ufahamu mpya na wa juu zaidi, unaokua kwa kina na kila hatua. Hiki ndicho wanadamu wote wanapaswa kuingia ndani. Kupitia kuwasiliana, kusikiliza ujumbe, kusoma neno la Mungu, ama kushughulikia suala, utapata ufahamu mpya na kupata nuru upya. Huishi ndani ya kanuni za zamani na nyakati za zamani. Unaishi daima ndani ya mwangaza mpya, na hupotei mbali na neno la Mungu. Huku ndiko kunaitwa kwenda katika njia sahihi. Kulipa tu gharama ya juu juu hakutakubalika. Siku baada ya siku, neno la Mungu linaingia katika ulimwengu wa juu zaidi na mambo mapya yanajitokeza kila siku. Ni muhimu pia kwa mwanadamu kuingia upya kila siku. Mungu anavyozungumza, ndivyo Anavyotimiza yote ambayo Amezungumza; kama huwezi kwenda sambamba, basi unabaki nyuma. Lazima uende kwa kina zaidi katika maombi yako; kula na kunywa neno la Mungu hakuwezi kuwa kuna kosa mfululizo. Imarisha nuru na mwangaza unayopokea, ufunuo unaopokea, na dhana zako na fikira zako lazima zipungue hatua kwa hatua. Lazima pia uimarishe hekima yako, na chochote unachopitia, lazima uwe na mawazo yako kukihusu na uwe na mtazamo wako. Kwa kuelewa mambo fulani katika roho, lazima upate ufahamu wa mambo ya nje na kuelewa kiini cha suala lolote. Kama hujajiandaa na mambo haya, utawezaje kuliongoza kanisa? Iwapo unazungumzia tu barua na mafundisho ya dini bila uhalisi wowote na bila njia ya kutenda, unaweza tu kuendelea kwa muda mfupi. Inaweza kukubalika kidogo kwa waumini wapya, lakini baada ya muda, wakati waumini wapya wanapata tajriba halisi, basi hutaweza tena kuwakimu. Basi unafaa vipi kwa matumizi ya Mungu? Bila kupata nuru upya, huwezi kufanya kazi. Walio bila nuru upya ni wale wasiojua jinsi ya kuwa na uzoefu, na wanadamu kama hao kamwe hawapati maarifa mapya ama tajriba. Na katika suala la kuleta maisha, hawawezi kamwe kufanya jukumu lao la kusambaza uhai, wala hawawezi kufaa kwa ajili ya matumizi na Mungu. Mwanadamu kama huyu ni dhaifu na hana maana. Kwa kweli, wanadamu kama hawa hawawezi kufanya jukumu lao kabisa kwa kazi na wote hawana faida. Wanashindwa kufanya jukumu lao na pia kwa kweli wanaweka mzigo mwingi usiohitajika juu ya kanisa. Nawahimiza hawa “wanaume wazee” kuharakisha na kuondoka kanisani ili wengine wasilazimishwe kuwaona tena. Wanadamu kama hawa hawaelewi kazi mpya lakini wamejawa na fikira zisizokoma. Hawafanyi chochote kanisani; badala yake, wanachochea na kusambaza uhasi kila pahali, hata kushiriki katika kila namna ya utovu wa nidhamu na vurugu kanisani, na hivyo kuwarusha wale wasiobagua katika vurugu na machafuko. Haya ibilisi wanaoishi, hawa mapepo mabaya wanapaswa kuondoka kanisani haraka iwezekanavyo, kanisa lisije likaharibiwa kwa sababu yako. Labda huogopi kazi ya leo, lakini huogopi adhabu ya haki ya kesho? Kuna idadi kubwa ya watu kanisani ambao ni vimelea, na pia kuna idadi kubwa ya mbwa mwitu wanaotafuta kuvuruga kazi ya kawaida ya Mungu. Vitu hivi vyote ni mapepo yaliyotumwa na Ibilisi, ni mbwa mwitu wakali wanaotafuta kuwala kondoo wasiojua. Iwapo wanadamu kama hawa hawatafukuzwa, basi wanakuwa vimelea kwa kanisa na nondo wanaokula sadaka. Hawa mabuu wenye kudharauliwa wajinga, duni, na wenye kuchukiza wataadhibiwa siku moja karibuni!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 489)
Kuwa na ujuzi wa utendaji na kuwa na uwezo wa kuona wazi kazi ya Mungu—yote haya yanaonekana katika maneno Yake. Ni katika maneno ya Mungu tu ndio unaweza kupata nuru, hivyo unapaswa kujitayarisha na maneno Yake zaidi. Gawa ufahamu wako kutoka kwa maneno ya Mungu katika ushirika, na kupitia katika ushirika wako wengine wanaweza kupata nuru na unaweza kuwaongoza watu kwenye njia—njia hii ni ya utendaji. Kabla ya Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili yenu, kila mmoja wenu lazima kwanza ajitayarishe na maneno Yake. Hiki ni kitu ambacho kila mtu anapaswa kufanya—ni kipaumbele cha haraka. Kitu cha kwanza cha kufanya ni kuwa na uwezo wa kula na kunywa maneno Yake. Kwa mambo ambayo huwezi kufanya, tafuta njia ya kutenda kutoka kwa maneno Yake, na angalia katika maneno Yake masuala yoyote ambayo hujui au matatizo yoyote uliyo nayo. Yafanye maneno ya Mungu yawe ruzuku yako, na uyaruhusu yaweze kukusaidia katika kutatua shida na matatizo yako ya vitendo; pia yaruhusu maneno Yake yawe msaada wako katika maisha. Mambo haya yanahitaji jitihada kwa upande wako. Katika kula na kunywa neno la Mungu, lazima ufanikishe matokeo; lazima uweze kuutuliza moyo wako mbele Yake, na kutenda kulingana na maneno Yake unapokabili masuala. Wakati hujakutana na masuala yoyote, kula na kunywa tu. Wakati mwingine unaweza kuomba na kutafakari juu ya upendo wa Mungu, kuwa na ushirika juu ya ufahamu wako wa maneno Yake, na kuwasiliana juu ya kupata nuru na kupata mwanga unaoupitia ndani yako mwenyewe na majibu ambayo umekuwa nayo unapoyasoma matamko haya. Aidha, unaweza kuwapa watu suluhisho. Hili pekee ndilo la utendaji. Lengo la kufanya hili ni kuyaruhusu maneno ya Mungu kuwa utoaji wako wa vitendo.
Kitika kipindi cha siku moja, unatumia saa ngapi kwa hakika mbele ya Mungu? Ni kiasi gani cha siku yako kinachotolewa kwa Mungu? Ni kiasi gani kinachopewa kwa mwili? Moyo wa mtu kuelekea daima kwa Mungu ndiyo hatua ya kwanza kwenye njia sahihi ya kufanywa mkamilifu na Mungu. Unaweza kuutoa moyo wako na mwili na upendo wako wote wa kweli kwa Mungu, uyaweke mbele Zake, kuwa mtiifu kabisa Kwake, na kufikiria kabisa mapenzi Yake. Si kwa ajili ya mwili, si kwa ajili ya familia, wala si kwa ajili ya matamanio yako mwenyewe, bali ni kwa ajili ya maslahi ya nyumba ya Mungu. Katika kila kitu unaweza kuchukua neno la Mungu kama kanuni, kama msingi. Hivyo, malengo yako na mtazamo wako yote yatakuwa mahali sahihi, na utakuwa mtu ambaye anapata sifa za Mungu mbele Zake. Wale ambao Mungu hupenda ni watu ambao ni kamili kabisa, watu ambao wamejitolea kwake na hakuna mwingine. Wale ambao Yeye huwachukia ni watu ambao wako shingo upande kumhusu, na ambao wanaasi dhidi Yake. Anawachukia wale wanaomwamini na daima wanataka kumfurahia, lakini hawawezi kujitumia kabisa kwa ajili Yake. Anawachukia wale wanaosema wanampenda lakini wanaomuasi mioyoni mwao. Anawachukia wale wanaotumia maneno matamu ili wafanye udanganyifu. Wale ambao hawajitolei kwa kweli kwa Mungu au hawana utiifu wa kweli Kwake ni watu wasio waaminifu; wao kwa kawaida ni wenye kiburi sana. Wale ambao hawawezi kuwa watiifu kwa kweli mbele ya Mungu wa kawaida, wa vitendo hata ni wenye kiburi zaidi, na hasa wao ni uzao mtiifu wa malaika mkuu. Wale ambao kwa kweli hujitumia wenyewe kwa ajili ya Mungu huweka nafsi zao zote mbele Yake. Wao hutii kwa kweli matamshi Yake yote, na wana uwezo wa kuweka maneno Yake katika matendo. Wao hufanya maneno ya Mungu kuwa msingi wa kuwepo kwao, na wanaweza kutafuta kwa kweli sehemu za matendo katika neno la Mungu. Huyu ni mtu ambaye kwa kweli anaishi mbele ya Mungu. Ikiwa unachofanya ni cha manufaa kwa maisha yako, na kwa njia ya kula na kunywa maneno Yake, unaweza kukidhi mahitaji yako ya ndani na upungufu ili tabia yako ya maisha inabadilishwa, basi hii itatimiza mapenzi ya Mungu. Ikiwa unatenda kulingana na mahitaji ya Mungu, ikiwa huuridhishi mwili lakini unaridhisha mapenzi Yake, huku ni kuingia katika uhalisi wa maneno Yake. Wakati unazungumza juu ya kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu kwa kweli zaidi, kunamaanisha unaweza kutekeleza wajibu wako na kukidhi mahitaji ya Mungu. Aina hizi tu za vitendo ndizo zinazoweza kuitwa kuingia katika uhalisi wa maneno Yake. Ikiwa una uwezo wa kuingia katika uhalisi huu, basi una ukweli. Huu ndio mwanzo wa kuingia katika uhalisi; lazima kwanza ufanye mazoezi haya na ni baada tu ya hayo ndio utakuwa na uwezo wa kuingia katika hali halisi za kina zaidi. Fikiria jinsi ya kushika amri na jinsi ya kuwa mwaminifu mbele ya Mungu. Usifikiri kila muda kuhusu wakati utakapoweza kuingia katika ufalme—ikiwa tabia yako haibadiliki, chochote unachokifikiria kitakuwa bure! Ili kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu, lazima kwanza uweze kufanya mawazo yako na fikira zote ziwe kwa ajili ya Mungu—hili ni hitaji la msingi zaidi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli Ni Wale Wanaoweza Kutii Utendaji Wake Kabisa
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 490)
Kuna watu wengi ambao sasa wako katikati ya majaribio; hawaelewi kazi ya Mungu. Lakini Nakwambia—ikiwa huielewi, ni vyema usiihukumu. Labda kutakuwa na siku moja wakati ukweli utajulikana na kisha utaujua. Kutohukumu kutakuwa na manufaa kwako, lakini huwezi kusubiri tu bila kuonyesha hisia. Lazima utafute kuingia ndani kwa matendo—huyu tu ndiye mtu anayeingia kwa vitendo. Kwa sababu ya uasi wao, watu daima wanaendeleza mawazo kuhusu Mungu wa vitendo. Hii inahitaji watu wote kujifunza jinsi ya kuwa watiifu kwa sababu Mungu wa vitendo ni jaribio kubwa kwa wanadamu. Ikiwa huwezi kusimama imara, basi kila kitu kimekamilika; kama huna ufahamu wa utendaji wa Mungu wa vitendo, huwezi kukamilishwa na Mungu. Hatua muhimu katika ikiwa watu wanaweza kufanywa kuwa kamili au sio ni kuelewa uzoefu wa Mungu. Uzoefu wa Mungu mwenye mwili aliyekuja duniani ni jaribio kwa kila mtu. Ikiwa unaweza kusimama imara katika kipengele hiki basi wewe ni mtu anayemjua Mungu, na wewe ni mtu anayempenda kwa kweli. Ikiwa huwezi kusimama imara katika kipengele hiki, ikiwa unamwamini tu Roho na huwezi kuwa na imani kwa utendaji wa Mungu, basi bila kujali jinsi imani yako ilivyo kubwa kwa Mungu, haina maana. Ikiwa huwezi kumwamini Mungu anayeonekana, unaweza kuamini Roho wa Mungu? Je, hujaribu kumdanganya Mungu? Wewe si mtiifu kwa Mungu anayeonekana na Anayeshikika, kwa hivyo unaweza kumtii Roho? Roho haishikiki na haionekani, kwa hiyo wakati unasema kwamba unatii Roho wa Mungu, je, huzungumzi tu upuuzi? Cha msingi katika kushika amri ni kuwa na ufahamu wa Mungu wa vitendo. Mara tu ukiwa na ufahamu wa Mungu wa vitendo, utakuwa na uwezo wa kushika amri. Kuna vipengele viwili katika kuzishika: Kimoja ni kushikilia kiini kiini cha Roho Wake, na mbele ya Roho, kuwa na uwezo wa kukubali uchunguzi wa Roho; kingine ni kuwa na uwezo wa kuwa na ufahamu wa kweli wa mwili wenye mwili, na kufikia utii wa kweli. Ikiwa ni mbele ya mwili au mbele ya Roho, moyo wa kumtii na kumcha Mungu lazima udumishwe daima. Ni mtu wa aina hii pekee ndiye anayestahiki kukamilishwa. Ikiwa una ufahamu wa utendaji wa Mungu wa vitendo—yaani, kama umesimama imara katika jaribio hili—kisha hakuna kitu kitakuwa kikubwa sana kwako.
Watu wengine husema, “Amri ni rahisi kushika. Unahitaji tu kuja mbele ya Mungu, kusema kwa uwazi na kwa dhati bila kutumia mikono, na huku ni kushika amri.” Je, hiyo ni sawa? Kwa hivyo, ukifanya mambo machache bila Mungu kujua ambayo yanampinga, je, hilo linahesabika kama kushika amri? Lazima uwe na ufahamu wa kina kuhusu kushika amri kunajumuisha nini. Linahusiana na ikiwa una ufahamu wa kweli wa utandaji wa Mungu au la; ikiwa una uelewa wa kutenda, na hujikwai na kuanguka katika jaribio hili, hili linahesabika kama wewe kuwa na ushahidi wa nguvu. Kuwa na ushahidi mkuu kwa Mungu hasa kunahusiana na ikiwa una ufahamu wa Mungu wa vitendo au la, na ikiwa unaweza au huwezi kutii mbele ya mtu huyu ambaye ni wa kawaida na kutii mpaka hata kifo. Ikiwa unamshuhudia Mungu kwa kweli kupitia utii huu, hiyo inamaanisha kuwa umepatwa na Mungu. Kuwa na uwezo wa kutii mpaka kifo, na kuwa bila malalamiko mbele Yake, kutohukumu, kutokashifu, kutokuwa na mawazo, na kutokuwa na makusudi mengine—kwa njia hii Mungu atapata utukufu. Utiifu mbele ya mtu wa kawaida ambaye anadharauliwa na mwanadamu na kuwa na uwezo wa kutii mpaka kifo bila mawazo yoyote—huu ni ushuhuda wa kweli. Uhakika ambao Mungu anataka watu waingie ndani ni kwamba unaweza kutii maneno Yake, unaweza kuweka maneno Yake katika matendo, kuweza kuinama mbele ya Mungu wa vitendo na kujua upotovu wako mwenyewe, kuweza kufungua moyo wako mbele Yake, na mwishowe kupatwa na Yeye kupitia maneno haya Yake. Mungu hupata utukufu wakati maneno haya yanakushinda na kukufanya uwe mtiifu kikamilifu Kwake; kwa njia hii Anamwaibisha Shetani na kukamilisha kazi Yake. Wakati huna mawazo yoyote ya utendaji wa Mungu mwenye mwili, yaani, unaposimama imara katika jaribio hili, basi wewe huwa na ushuhuda mzuri. Ikiwa kuna siku ambayo uko na uelewa mkamilifu juu ya Mungu wa matendo na unaweza kutii mpaka kifo kama Petro, utapatwa na Mungu, na kukamilishwa na Yeye. Kile ambacho Mungu hufanya ambacho hakilingani na mawazo yako ni jaribio kwako. Ikiwa kingelingana na mawazo yako, hakingekuhitaji kuteseka au kusafishwa. Ni kwa sababu kazi Yake ni ya vitendo sana na kwamba hailingani na mawazo yako ndiyo inakuhitaji kuyaachilia mawazo yako. Hii ndiyo sababu ni jaribio kwako. Ni kwa sababu ya utendaji wa Mungu ndiyo maana watu wote wako katikati ya majaribio; kazi Yake ni ya vitendo, siyo ya kawaida. Kwa kuelewa kikamilifu maneno Yake ya vitendo, matamshi Yake ya vitendo bila mawazo yoyote, na kuwa na uwezo wa kumpenda kwa kweli zaidi ndivyo kazi Yake ilivyo ya vitendo zaidi, utapatwa na Yeye. Kundi la watu ambao Mungu atapata ni wale wanaomjua Mungu, yaani, ambao wanajua utendaji Wake, na hata zaidi ni wale wanaoweza kutii kazi ya vitendo ya Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli Ni Wale Wanaoweza Kutii Utendaji Wake Kabisa
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 491)
Wakati wa Mungu akiwa ndani ya mwili, utii Anaohitaji kwa watu sio ule ambao watu wanafikiri—kutohukumu au kutopinga. Badala yake, Anahitaji kwamba watu wafanye maneno Yake kuwa kanuni yao ya maisha na msingi wa kuendelea kuishi kwao, kwamba wanaweka kikamilifu kiini cha maneno Yake katika matendo, na kwamba wanayaridhisha kabisa mapenzi Yake. Kipengele kimoja cha kuhitaji watu kumtii Mungu mwenye mwili kinahusu kuweka maneno Yake katika matendo, huku kipengele kingine kinarejelea kuwa na uwezo wa kutii ukawaida na utendaji Wake. Haya yote mawili lazima yawe bila shaka. Wale ambao wanaweza kutimiza vipengele hivi viwili ni wale wote ambao wana moyo wa upendo wa kweli kwa Mungu. Wote ni watu ambao wamepatwa na Mungu, na wote wanampenda Mungu kama wanavyopenda maisha yao wenyewe. Mungu mwenye mwili ana ubinadamu wa kawaida na wa utendaji katika kazi Yake. Kwa njia hii, gamba Lake la nje la ubinadamu wa kawaida na wa utendaji linakuwa jaribio kubwa kwa watu; linakuwa tatizo lao kubwa. Hata hivyo, ukawaida na utendaji wa Mungu hauwezi kuepukwa. Alijaribu kila kitu ili kupata suluhisho lakini hatimaye hakuweza kujiondoa Mwenyewe kutoka kwenye gamba la nje la ubinadamu Wake wa kawaida kwa sababu, hata hivyo, Yeye ni Mungu aliyekuwa mwili, si Mungu wa Roho aliye mbinguni. Yeye si Mungu ambaye watu hawawezi kumuona, lakini Mungu aliyevaa gamba la kiumbe mmoja. Katika hili, kujiondoa Mwenyewe kutoka katika gamba la ubinadamu Wake wa kawaida bila shaka hakuwezi kuwa rahisi. Kwa hivyo bila kujali chochote, bado Yeye hufanya kazi ambayo Yeye hutaka kufanya kutoka kwa mtazamo wa mwili. Kazi hii ni maonyesho ya Mungu wa kawaida na wa matendo, kwa hivyo inawezekanaje kuwa sawa kwa watu kutotii? Ni nini duniani ambacho watu wanaweza kufanya kuhusu matendo ya Mungu? Anafanya chochote Anachotaka kufanya; chochote Anachofurahia kiko jinsi kilivyo. Ikiwa watu hawatii, wanaweza kuwa na mpango gani mwingine thabiti? Hadi sasa, bado ni utiifu tu ambao unaweza kuwaokoa watu; hakuna mawazo mengine ya ujanja. Ikiwa Mungu anataka kuwajaribu watu, wanaweza kufanya nini kuhusu hilo? Lakini yote haya si wazo la Mungu wa mbinguni; ni wazo la Mungu mwenye mwili. Anataka kufanya hili, hivyo hakuna mtu anayeweza kulibadilisha. Mungu aliye mbinguni haingilii kati kile Anachofanya, kwa hivyo watu hawapaswi kumtii hata zaidi? Ingawa Yeye ni wa matendo na wa kawaida, Yeye ni Mungu aliyekuwa mwili kikamilifu. Kulingana na mawazo Yake mwenyewe, Anafanya chochote Anachotaka. Mungu aliye mbinguni Amemkabidhi Yeye kazi zote; lazima utii chochote Anachofanya. Ingawa Ana ubinadamu na Yeye ni wa kawaida sana, yote haya ni yale ambayo Amepanga kwa makusudi, kwa hivyo watu wanaweza kumtazamaje, macho wazi kwa kutokubali? Anataka kuwa wa kawaida, kwa hivyo Yeye ni wa kawaida. Anataka kuishi ndani ya ubinadamu, hivyo Anaishi ndani ya ubinadamu. Anataka kuishi ndani ya uungu, hivyo anaishi ndani ya uungu. Watu wanaweza kuona hilo jinsi wanavyotaka. Mungu daima Atakuwa Mungu na watu daima watakuwa watu. Kiini Chake hakiwezi kukataliwa kwa sababu ya maelezo madogo, wala Hawezi kusukumwa nje ya “nafsi” ya Mungu kwa sababu ya kitu kidogo. Watu wana uhuru wa binadamu, na Mungu ana hadhi ya Mungu; haya hayaingiliani. Je, watu hawawezi kumpa Mungu uhuru kidogo? Je, hawawezi kumvumilia Mungu kuwa wa kawaida zaidi? Usiwe makini sana na Mungu! Kila mtu anapaswa kuwa na uvumilivu kwa kila mmoja; basi si kila kitu kitakuwa kimesuluhishwa? Je, bado kungekuwa na kufarakana kokote? Ikiwa mtu hawezi kuvumilia kitu kidogo kama hicho, anawezaje hata kufikiria kuwa mtu mkarimu, mwanadamu wa kweli? Siye Mungu anayewapa wanadamu wakati mgumu, lakini ni wanadamu wanaompa Mungu wakati mgumu. Daima wanashughulikia vitu kwa kufanya kitu kidogo kionekane kikubwa—kwa kweli wao hufanya kitu kisicho cha maana kuwa kizito, na hiyo si lazima! Wakati Mungu anafanya kazi katika ubinadamu wa kawaida na wa matendo, kile Anachofanya si kazi ya wanadamu, bali ni kazi ya Mungu. Hata hivyo, watu hawaoni kiini cha kazi Yake—daima wanaona gamba la nje la ubinadamu Wake. Hawajaona kazi kubwa kama hiyo, lakini wanasisitiza kuona ubinadamu wa kawaida wa Mungu na hawaachilii wazo hili. Je, hii inawezaje kuitwa kumtii Mungu? Mungu mbinguni sasa “amegeuka kuwa” Mungu duniani, na Mungu duniani sasa ni Mungu wa mbinguni. Haijalishi kama sura Yao ya nje ni sawa au jinsi kazi Yao ilivyo. Kwa ujumla, Yeye anayefanya kazi ya Mungu mwenyewe ni Mungu Mwenyewe. Lazima utii bila kujali ikiwa unataka au la—hiki si kitu ambacho unapata kuchagua! Mungu lazima atiiwe na watu, na watu lazima wamtii kabisa Mungu bila ya kujifanya hata kidogo.
Kikundi cha watu ambao Mungu mwenye mwili Anataka kuwapata leo ni wale wanaokubali mapenzi Yake. Watu wanahitaji tu kutii kazi Yake, sio daima kujishughulisha na mawazo ya Mungu aliye mbinguni, waishi ndani ya hali isiyo dhahiri, au kufanya mambo kuwa magumu kwa Mungu mwenye mwili. Wale ambao wanaweza kumtii ni wale wanaoyasikia kabisa maneno Yake na kutii mipango Yake. Watu hawa hawajali kamwe jinsi Mungu mbinguni alivyo kwa kweli au ni kazi ya aina gani Mungu wa mbinguni Anafanya sasa kwa wanadamu, lakini wao humpa Mungu aliye duniani mioyo yao kabisa na kuweka nafsi zao zote mbele Yake. Kamwe hawazingatii usalama wao wenyewe, wala hawalalamiki kamwe juu ya ukawaida na utendaji wa Mungu katika mwili. Wale wanaomtii Mungu katika mwili wanaweza kukamilishwa na Yeye. Wale wanaomwamini Mungu mbinguni hawatapata kitu. Hii ni kwa sababu si Mungu mbinguni, lakini ni Mungu hapa duniani ndiye Anayetoa ahadi na baraka juu ya watu. Watu hawapaswi daima kumtukuza Mungu aliye mbinguni na kumwona Mungu duniani kama mtu wa wastani. Hii si haki. Mungu mbinguni ni mkuu na wa ajabu na mwenye hekima ya ajabu, lakini hii haipo kabisa. Mungu duniani ni wa wastani sana na asiye na maana; Yeye pia ni wa kawaida sana. Hana mawazo ya ajabu au vitendo vya kimiujiza. Anatenda tu na kuongea kwa njia ya kawaida na ya matendo. Ingawa Hazungumzi kwa njia ya ngurumo au kuita upepo na mvua, Yeye kwa kweli ni mwili wa Mungu aliye mbinguni, na kwa kweli ni Mungu anayeishi kati ya wanadamu. Watu hawapaswi kumtukuza yule wanayeweza kumwelewa na ambaye analingana na mawazo yao wenyewe kama Mungu, au kumwona Yeye ambaye hawawezi kumkubali na kabisa hawawezi kufikiria kama wa chini. Yote haya ni uasi wa watu; yote ni chanzo cha upinzani wa wanadamu kwa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli Ni Wale Wanaoweza Kutii Utendaji Wake Kabisa
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 492)
Watu wakitegemea tu hisia za dhamiri zao, hawawezi kuhisi kupendeza kwa Mungu; wakitegemea tu dhamiri zao, upendo wao kwa Mungu utakuwa dhaifu. Ukizungumza tu kuhusu kulipa neema na upendo wa Mungu, hutakuwa na msukumo wowote katika upendo wako Kwake; kumpenda Yeye kwa kutegemea hisia za dhamiri yako ni mtazamo baridi. Ni kwa nini Nasema kwamba ni mtazamo baridi? Hili ni suala la utendaji. Huu ni upendo wa aina gani? Huku si kujaribu kumdanganya Mungu na kufanya kitu kwa namna isiyo ya dhati tu kwa ajili Yake? Watu wengi sana huamini kwamba hakuna tuzo la kumpenda Mungu, na mtu ataadhibiwa hata hivyo kwa kutompenda Yeye, kwa hiyo kwa jumla kutotenda dhambi tu kunatosha. Kwa hiyo kumpenda Mungu na kulipa upendo Wake kwa kutegemeza hisia za dhamiri ya mtu ni mtazamo baridi, na si upendo kwa Mungu unaokuja kwa hiari kutoka moyoni mwa mtu. Upendo kwa Mungu unapaswa kuwa hisia halisi kutoka katika kina cha moyo wa mtu. Watu wengine husema: “Mimi mwenyewe niko radhi kumfuatilia Mungu na kumfuata Yeye. Sasa Mungu anataka kuniacha lakini bado nataka kumfuata Yeye. Iwapo Ananitaka au la, bado nitampenda Yeye, na mwishowe lazima nimpate Yeye. Ninatoa moyo wangu kwa Mungu, na haijalishi kile Yeye hufanya, nitamfuata Yeye kwa maisha yangu yote. Lolote litokealo, lazima nimpende Mungu na lazima nimpate Yeye; sitapumzika mpaka nimpate Yeye.” Una aina hii ya nia?
Njia ya kuamini katika Mungu ni njia ya kumpenda Yeye. Ikiwa unaamini katika Yeye lazima umpende Yeye; kwa hali yoyote, kumpenda Yeye hakuhusu tu kulipa upendo Wake au kumpenda kwa kutegemea hisia za dhamiri—ni pendo safi kwa Mungu. Kuna nyakati ambazo watu hutegemea tu dhamiri zao na hawawezi kuhisi upendo wa Mungu. Kwa nini kila mara Nilisema: “Roho wa Mungu asisimue roho zetu”? Kwa nini Sikuzungumzia kusisimua dhamiri za watu kumpenda Mungu? Ni kwa sababu dhamiri za watu haziwezi kuhisi kupendeza kwa Mungu. Ikiwa hujaridhishwa na maneno hayo, huenda ukatumia dhamiri yako kuhisi upendo Wake, na utakuwa na msukumo fulani wakati huo lakini baadaye utatoweka. Ukitumia tu dhamiri yako kuhisi kupendeza kwa Mungu, una msukumo unapoomba, lakini baadaye unaondoka tu, unatoweka. Hilo linahusu nini? Ukitumia tu dhamiri yako hutaweza kuamsha upendo wako kwa Mungu; unapohisi kweli kupendeza Kwake ndani ya moyo wako roho yako itasisimuliwa na Yeye, na ni wakati huo tu ndio dhamiri yako itaweza kufanya kazi yake ya asili. Hiyo ni kusema kwamba watu wakishasisimuliwa na Mungu katika roho zao na wakati roho zao zimepata maarifa na himizo, yaani, baada ya wao kupata uzoefu, ndipo tu wataweza kumpenda Mungu kwa kufaa na dhamiri zao. Kumpenda Mungu na dhamiri yako si vibaya—hiki ni kiwango cha chini sana cha kumpenda Mungu. Njia ya wanadamu ya upendo ya kufanya haki kwa shida tu kwa neema ya Mungu bila shaka haiwezi kuchochea kuingia kwao kiutendaji. Watu wanapopata baadhi ya kazi ya Roho Mtakatifu, yaani, wanapoona na kuonja upendo wa Mungu katika uzoefu wao wa vitendo, wakiwa na maarifa fulani ya Mungu na kuona kweli kwamba Mungu anastahili sana upendo wa wanadamu na jinsi Alivyo mzuri, ni wakati huo tu ndio watu wanaweza kumpenda Mungu kwa uhalisi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 493)
Watu wanapowasiliana na Mungu na mioyo yao, mioyo yao inapoweza kumgeukia Yeye kikamilifu, hii ni hatua ya kwanza ya upendo wa wanadamu kwa Mungu. Ikiwa unataka kumpenda Mungu, lazima kwanza uweze kugeuza moyo wako Kwake. Kugeuza moyo wako kwa Mungu ni nini? Ni wakati ambapo kila kitu unachofuatilia ndani ya moyo wako ni kwa ajili ya kumpenda na kumpata Mungu, na hii inaonyesha kwamba umeugeuza moyo wako kikamilifu kwa Mungu. Bali na Mungu na maneno Yake, hakuna takriban kitu chochote kingine ndani ya moyo wako (familia, mali, mume, mke, watoto au vitu vingine). Hata kama vipo, haviwezi kuumiliki moyo wako, na hufikirii juu ya matazamio yako ya baadaye lakini unafuatilia tu kumpenda Mungu. Wakati huo utakuwa umegeuza moyo wako kwa Mungu kabisa. Ikiwa bado unajitengenezea mipango ndani ya moyo wako na kila mara unafuatilia manufaa yako binafsi, na kila mara unafikiri: “Ni lini ninaweza kumwomba Mungu ombi ndogo? Familia yangu itakuwa tajiri lini? Ninawezaje kupata mavazi kadhaa mazuri? …” Ikiwa unaishi katika hali hiyo inaonyesha kwamba moyo wako haujamgeukia Mungu kwa ukamilifu. Ikiwa una maneno ya Mungu tu moyoni mwako na unaweza kumwomba Mungu na kuwa karibu naye nyakati zote, kana kwamba Yeye yu karibu sana nawe, kana kwamba Mungu yu ndani yako nawe u ndani Yake, ikiwa uko katika hali ya aina hiyo, inamaanisha kwamba moyo wako umekuwa katika uwepo wa Mungu. Ukimwomba Mungu na kula na kunywa maneno Yake kila siku, unafikiria kila mara kuhusu kazi ya kanisa, ukifikiria juu ya mapenzi ya Mungu, ukitumia moyo wako kumpenda Yeye kwa uhalisi na kuridhisha moyo Wake, basi moyo wako utakuwa wa Mungu. Ikiwa moyo wako unamilikiwa na vitu vingine vingi, basi bado unamilikiwa na Shetani na haujamrudia Mungu kweli. Wakati moyo wa mtu umemrudia Mungu kweli, atakuwa na upendo halisi, wa hiari Kwake na ataweza kufikiria kazi ya Mungu. Ingawa bado atakuwa na hali za kipumbavu na zisizo na akili, ataweza kuwa na fikira kwa ajili ya maslahi ya nyumba ya Mungu, ya kazi Yake, na ya mabadiliko katika tabia yake. Moyo wake utakuwa sahihi kabisa. Watu wengine kila mara hupeperusha bendera ya kanisa haijalishi wanachofanya; kweli ni kwamba hii ni kwa manufaa yao. Mtu wa aina hiyo hana aina nzuri ya nia. Yeye ni mhalifu na mdanganyifu na mambo mengi sana anayofanya ni ya kutafuta manufaa yake mwenyewe. Mtu wa aina hiyo hafuatilii kumpenda Mungu; moyo wake bado ni wa Shetani na hauwezi kumgeukia Mungu. Mungu hana njia ya kumpata mtu wa aina hiyo.
Hatua ya kwanza ya kumpenda Mungu kweli na kupatwa na Yeye ni kuurudisha moyo wako kwa ukamilifu kwa Mungu. Katika kila jambo ufanyalo, jichunguze na uulize: “Ninafanya hiki kulingana na moyo wa upendo kwa Mungu? Kuna nia yoyote ya kibinafsi ndani yake? Lengo langu halisi la kufanya hili ni lipi?” Ikiwa unataka kumpa Mungu moyo wako lazima kwanza uuhini moyo wako, uachane na nia zako zote, na ufikie kiwango cha kuwa wa Mungu kwa ukamilifu. Hii ni njia ya kufanya mazoezi ya kumpa Mungu moyo wako. Kuuhini moyo wa mtu kunahusu nini? Ni kuachana na tamaa za kupita kiasi za mwili wa mtu, kutotamani baraka za cheo au kutamani starehe, kufanya kila kitu kumridhisha Mungu, na kwamba moyo wa mtu unaweza kuwa Wake kwa ukamilifu, sio kwa ajili ya mtu mwenyewe. Hivyo ndivyo ilivyo.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 494)
Upendo halisi kwa Mungu hutoka ndani ya kina cha moyo; ni upendo uliopo tu kwa msingi wa wanadamu kumfahamu Mungu. Moyo wa mtu unapomgeukia Mungu kwa ukamilifu basi ana upendo kwa Mungu, lakini upendo huo sio lazima uwe takatifu na sio lazima uwe kamili. Hii ni kwa sababu kuna umbali fulani kati ya moyo wa mtu kumgeukia Mungu kwa ukamilifu na mtu huyo kuwa na ufahamu halisi wa Mungu na kuabudu kihalisi Kwake. Njia ya mtu kutimiza upendo wa kweli kwa Mungu na kujua tabia ya Mungu ni kuurudisha moyo wake kwa Mungu. Baada ya kutoa moyo wao wa kweli kwa Mungu, wataanza kuingia katika uzoefu wa maisha, na hivyo tabia yao itaanza kubadilika, upendo wao kwa Mungu utakua polepole, na ufahamu wao wa Mungu utaongezeka pia polepole. Kwa hivyo kuurudisha moyo wa mtu kwa Mungu ni sharti la mwanzo la kuingia katika njia sahihi ya uzoefu wa maisha. Watu wanapoweka mioyo yao mbele ya Mungu, wao huwa tu na moyo wa kumtamani Yeye lakini sio wa kumpenda Yeye, kwa sababu hawana ufahamu kumhusu Yeye. Hata ingawa katika hali hii wana upendo fulani Kwake, si wa hiari na si halisi. Hii ni kwa sababu chochote kitokacho kwa mwili wa mwanadamu ni athari ya kihisia na hakitoki kwa ufahamu halisi. Ni msukumo wa muda mfupi tu na hakiwezi kuwa ibada ya kudumu. Watu wasipokuwa na ufahamu wa Mungu wanaweza tu kumpenda Yeye kulingana na upendeleo wao wenyewe na fikira zao binafsi; aina hiyo ya upendo haiwezi kuitwa upendo wa hiari, wala haiwezi kuitwa upendo halisi. Moyo wa mtu ukimrudia Mungu kwa uhalisi, anaweza kufikiria juu ya maslahi ya Mungu katika kila kitu, lakini ikiwa hana ufahamu wowote wa Mungu, hana uwezo wa kuwa na upendo wa hiari kwa uhalisi. Yote anayoweza kufanya ni kutimiza kazi fulani za kanisa na kutekeleza wajibu wake mdogo, lakini hauna msingi. Mtu wa aina hiyo ana tabia ambayo ni ngumu kubadilisha; wao wote ni watu ambao ama hawaufuatilii ukweli, au hawauelewi. Hata mtu akiurudisha kabisa moyo wake kwa Mungu haimaanishi kwamba moyo wake wa upendo kwa Mungu ni safi kabisa, kwa sababu wale walio na Mungu ndani ya mioyo yao sio lazima kwamba wanao upendo ndani ya mioyo yao kwa Mungu. Hili linahusu utofautishaji kati ya mtu anayefuatilia au asiyefuatilia ufahamu wa Mungu. Mara tu mtu anapokuwa na ufahamu wa Yeye, inaonyesha kwamba moyo wake umemrudia Mungu kwa ukamilifu, inaonyesha kwamba upendo wake halisi kwa Mungu ndani ya moyo wake ni wa hiari. Mtu wa aina hiyo pekee ndiye ana Mungu ndani ya moyo wake. Kugeuza moyo wa mtu kwa Mungu ni sharti la mwanzo la yeye kuingia katika njia sahihi, la kumfahamu Mungu, na la kutimiza upendo wa Mungu. Siyo alama ya kukamilisha wajibu wake ya kumpenda Mungu, wala siyo alama ya kuwa na upendo halisi Kwake. Njia ya pekee ya mtu kutimiza upendo halisi kwa Mungu ni kuurudisha moyo wake kwa Mungu, ambacho pia ni kitu cha kwanza mmoja wa uumbaji Wake anapaswa kufanya. Wale wanaompenda Mungu wote ni watu wanaotafuta uzima, yaani, watu wanaofuatilia ukweli na watu wanaomtaka Mungu kweli; wote wana nuru ya Roho Mtakatifu na wamesisimuliwa n na Yeye. Wote wanaweza kuongozwa na Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 495)
Mnapotaka kumpenda na kumjua Mungu leo, kwa upande mmoja ni lazima mstahimili mateso, usafishaji, na kwa ule upande mwingine, ni lazima mgharamike. Hakuna funzo lililo kubwa kuliko lile la kumpenda Mungu, na inaweza kusemwa kuwa funzo ambalo watu hujifunza katika maisha yao yote ya imani ni jinsi ya kumpenda Mungu. Hii ni kusema, kama unamwamini Mungu ni lazima umpende Mungu. Ikiwa unamwamini tu Mungu lakini humpendi, hujapata ufahamu wa Mungu, na hujawahi kumpenda Mungu kwa upendo wa kweli utokao moyoni mwako, basi imani yako kwa Mungu ni bure; kama katika imani yako kwa Mungu humpendi Mungu, basi unaishi bure, na maisha yako yote ndiyo ya duni zaidi kwa maisha yote. Ikiwa katika maisha yako yote hujawahi kumpenda au kumtosheleza Mungu, basi kuna haja gani ya kuishi? Kuna haja gani ya imani yako kwa Mungu? Huku si kuharibu nguvu? Hii ni kusema, kama watu wanataka kuamini na kumpenda Mungu, ni sharti wagharamike. Badala ya kujaribu kuenenda kwa namna fulani kwa nje tu, wanapaswa watafute utambuzi wa kweli kutoka ndani ya mioyo yao. Ikiwa unapenda sana kuimba na kucheza lakini huwezi kuonyesha ukweli katika vitendo, unaweza kusemekana kwamba unampenda Mungu? Kumpenda Mungu kunahitaji utafutaji wa mapenzi ya Mungu katika mambo yote, na kwamba ujisaili wewe mwenyewe kwa kina jambo lolote likikutokea, kujaribu kujua mapenzi ya Mungu na kujaribu kuona mapenzi ya Mungu ni yapi katika suala hili, Anataka ufanikishe nini, na ni jinsi gani utayajali mapenzi Yake? Kwa mfano: jambo fulani linafanyika linalokutaka uvumilie hali ngumu, wakati huo unapaswa ufahamu ni nini mapenzi ya Mungu, na ni jinsi gani unapaswa kuyajali mapenzi ya Mungu. Usijiridhishe mwenyewe: Jiweke kando kwanza. Hakuna kitu kilicho duni kuliko mwili. Ni lazima udhamirie kumridhisha Mungu, na ni lazima utekeleze wajibu wako. Katika mawazo kama hayo, Mungu atakupa nuru ya kipekee katika jambo hili, na moyo wako pia utapata faraja. Jambo lolote likikutendekea, liwe dogo au kubwa, ni sharti kwanza ujiweke pembeni na kuuona mwili kama kitu duni zaidi kuliko vitu vyote. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo unavyochukua uhuru zaidi; ukiuridhisha mara hii, wakati mwingine utataka zaidi. Hili linapoendelea, watu wanapata kuupenda mwili hata zaidi. Mwili mara zote una tamaa kupita kiasi, mara zote mwili unakutaka uuridhishe, na kwamba uutosheleze kwa ndani, iwe ni katika chakula unachokula, unachokivaa, au kuwa na hasira katika matendo yako, au kuushawishi udhaifu na uzembe wako… Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo tamaa yake inaongezeka, na jinsi mwili unavyopotoka zaidi, hadi kufikia kiwango ambacho miili ya watu inahodhi dhana nzito, na kutomtii Mungu, na kujiinua, na kuanza kuishuku kazi ya Mungu. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo udhaifu wa mwili unavyokuwa mkubwa; daima utahisi kuwa hakuna anayekuonea huruma kwa udhaifu wako, daima utaamini kuwa Mungu amezidi sana, na utasema: Mungu anawezaje kuwa mkali namna hii? Ni kwa nini Hawezi kuwapa watu nafasi? Watu wakiudekeza sana mwili, na kuupenda kupindukia, basi wanajiangamiza wao wenyewe. Ikiwa unampenda Mungu kwa dhati, na huuridhishi mwili, basi utaona kuwa kila anachokifanya Mungu ni chenye haki sana, na kizuri sana, na kwamba laana Yake kwa uasi wako na hukumu ya udhalimu wako ni haki. Zitakuwepo nyakati ambapo Mungu atakurudi na kukufundisha nidhamu, na kuanzisha mazingira ya kukukasirisha, na kukushurutisha uje mbele Zake—na daima utahisi kuwa anachokifanya Mungu ni cha ajabu. Hivyo utahisi kana kwamba hakuna uchungu mwingi, na kwamba Mungu anapendeza. Ukifuata udhaifu wa mwili, na kusema kwamba Mungu amezidi, basi daima utahisi uchungu na daima utahuzunika, na utakosa uwazi kuhusu kazi yote ya Mungu na itaonekana kana kwamba Mungu hana huruma kwa udhaifu wa mwanadamu, na Hatambui shida za mwanadamu. Hivyo utajihisi mnyonge na mpweke, kana kwamba umekumbwa na dhuluma kubwa, na wakati huo utaanza kulalama. Kadiri unavyoutosheleza udhaifu wa mwili, ndivyo unavyohisi kuwa Mungu anazidi, hadi inakuwa mbaya kiasi kwamba unaikana kazi ya Mungu, na kuanza kumpinga Mungu na kujaa uasi. Hivyo unafaa kuuasi mwili na usiutosheleze: “Mume wangu(mke), watoto, matarajio, ndoa, familia—hakuna hata moja kati ya haya ambalo ni la thamani! Moyoni mwangu mna Mungu pekee na nitajaribu kumridhisha Mungu kadiri ya uwezo wangu, na si kuuridhisha mwili.” Lazima uwe na azimio hili. Daima ukiwa na azimio hili, basi ukiuweka ukweli katika vitendo, na kujiweka kando, utaweza kufanya hivyo kwa juhudi kidogo. Inasemekana kuwa kulikuwepo na mkulima aliyeona nyoka barabarani aliyekuwa ameganda. Huyu mkulima alimchukua yule nyoka na kumweka kifuani mwake, na baada ya yule nyoka kuamka alimuuma yule mkulima hadi akafa. Miili ya wanadamu ni kama yule nyoka: asili yake ni kuyadhuru maisha yao—na ikipata mbinu yake kikamilifu, maisha yako yanapotea. Mwili ni wa Shetani. Kuna tamaa kupita kiasi ndani yake, hujithamini wenyewe, unafurahia faraja, na kushangilia burudani, kujiachilia katika uvivu na uzembe, na baada ya kuuridhisha kwa kiwango fulani mwishowe utakuangamiza. Hivi ni kusema, ukiuridhisha sasa, wakati mwingine utakuomba zaidi. Daima mwili una tamaa na matakwa kupita kiasi, na unajinufaisha kutokana na wewe kuutosheleza mwili na kukufanya uufurahie hata zaidi na kuishi katika starehe zake—na ikiwa hutaushinda, mwishowe utajiangamiza mwenyewe. Iwapo utapata uzima mbele za Mungu, na namna hatima yako itakavyokuwa, inategemea uasi wako dhidi ya mwili utakuwa wa namna gani. Mungu amekuokoa, na kukuteua na kukuamulia kabla, bado ikiwa leo hauko radhi kumridhisha, hauko radhi kuuweka ukweli katika vitendo, hauko radhi kuuasi mwili wako kwa moyo umpendao Mungu kwa dhati, hatimaye utajiangamiza mwenyewe, na kwa hivyo utapitia mateso mengi. Ikiwa mara zote unautosheleza mwili, Shetani atakumeza hatua kwa hatua, na kukuacha bila uzima, au upako wa Roho, hadi siku itafika ambayo ndani utakuwa giza. Ukiishi katika giza, utakuwa umetekwa nyara na Shetani, hutakuwa na Mungu tena moyoni mwako, na wakati ule utaukataa uwepo wa Mungu na kumwacha. Kwa hivyo, ikiwa watu wanataka kumpenda Mungu, ni lazima walipe gharama ya uchungu na kupitia shida. Hakuna haja ya hamasa za nje na shida, kusoma zaidi na kuzungukazunguka zaidi; badala yake, wanafaa kuweka kando vitu vilivyomo ndani yao: mawazo kupita kiasi, maslahi ya kibinafsi, na masuala yao binafsi, fikira, na nia. Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 496)
Ushughulikiaji wa Mungu juu ya tabia za nje za watu ni sehemu moja ya kazi Yake; kwa mfano, kushughulikia ubinadamu wa watu wa nje, usiokuwa wa kawaida, au maisha na tabia zao, njia na desturi zao, na vilevile vitendo vyao vya nje, na hamasa zao. Lakini Anapowataka watu wauweke ukweli katika vitendo na wabadilishe tabia zao, kimsingi kinachoshughulikiwa hapa ni motisha na mawazo yaliyo ndani yao. Kushughulikia tabia zako za nje tu si kugumu; ni sawa na kukukataza kula vitu uvipendavyo, jambo ambalo ni rahisi. Kinachogusia fikira zilizo ndani yako, hata hivyo, si rahisi kukiachia. Inawahitaji wauasi mwili wao, na kulipa gharama, na kuteseka mbele za Mungu. Hii ndiyo hali hasa katika nia za watu. Tangu watu waanze kumwamini Mungu, wamekuwa na nia ambazo si sahihi. Wakati ambapo huweki ukweli katika vitendo, unahisi kuwa motisha zako ni sahihi, lakini jambo likikutokea, utaona kuwa kuna motisha nyingi ndani zisizo sahihi. Hivyo, Mungu akiwafanya watu kuwa wakamilifu, Anawafanya kugundua kuwa kuna dhana nyingi ndani yao ambazo zinawazuia kumfahamu Mungu. Ukitambua kuwa motisha zako zina makosa, kama unaweza kuacha kutenda kulingana na motisha na dhana zako, na unaweza kuwa na ushuhuda wa Mungu na kusimama imara katika msimamo wako kwa kila lifanyikalo kwako, hili linathibitisha kuwa umeuasi mwili wako. Ukiasi dhidi ya mwili wako, bila shaka kutakuwa na vita ndani yako. Shetani atajaribu kufanya watu kuifuata, atajaribu kuwafanya wafuate dhana za kimwili na kutekeleza maslahi ya kimwili—ila maneno ya Mungu yatawapa nuru watu na kuwaangazia kwa ndani, na wakati huu itakuwa juu yako ikiwa utamfuata Mungu au utamfuata Shetani. Mungu anawataka watu kuweka ukweli katika matendo kimsingi kushughulikia mambo yaliyo ndani yao, kushughulikiwa fikira zao, na dhana zao ambazo haziufuati moyo wa Mungu. Roho Mtakatifu huwagusa watu ndani ya mioyo yao, na kuwapa nuru na mwangaza. Kwa hivyo katika tukio lolote katika vita: Kila wakati watu wanapoweka ukweli katika vitendo, au kuweka mapenzi ya Mungu katika vitendo, huwa kuna vita vikali, na japokuwa mambo yanaweza kuonekana shwari katika miili yao, ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona—na ni baada tu ya hivi vita vikali, baada ya kutafakari kwa kina, ndipo ushindi au kushindwa kunaweza kuamuliwa. Mtu anashindwa kujua ama acheke au alie. Kwa sababu motisha nyingi ndani ya watu zina makosa, ama kwa sababu kazi kubwa ya Mungu inakinzana na dhana zao, watu wakiuweka ukweli katika vitendo vita vikali huzuka kisirisiri. Baada ya kuuweka huu ukweli katika vitendo, kisirisiri watu watakuwa wamemwaga machozi mengi sana ya huzuni kabla ya kuamua kumridhisha Mungu. Ni kwa sababu ya vita hivi watu huvumilia shida na usafishaji; huku ni kuteseka kwa kweli. Vita vikikukabili, kama unaweza kusimama kweli upande wa Mungu, utaweza kumridhisha Mungu. Katika harakati ya kutenda ukweli, hakuepukiki kwamba mtu atateseka kwa ndani; ikiwa, wanapoweka ukweli katika vitendo, kila kitu ndani yao kingekuwa sawa, basi wasingehitaji kufanywa wakamilifu na Mungu, na kusingekuwa na vita, na hawangeteseka. Ni kwa sababu kuna mambo mengi ndani ya watu ndipo hawafai kutumiwa na Mungu, na tabia nyingi za uasi wa mwili, ndipo watu wanapaswa kujifunza funzo la kuasi dhidi ya mwili kwa kina zaidi. Huku ndiko Mungu anaita kuteseka ambako Alimtaka mwanadamu kushiriki Naye. Ukikumbana na shida, fanya hima na umwombe Mungu: Ee Mungu! Ninataka kukuridhisha, ninataka kustahimili mateso ya mwisho ili kuuridhisha moyo Wako, na bila kujali kuwa vikwazo ninavyokumbana navyo ni vikubwa kiasi gani, bado ni sharti nikuridhishe. Hata ikiwa ni kuyatoa maisha yangu yote, bado ni sharti nikuridhishe! Ukiomba na hili azimio utaweza kusimama imara katika ushuhuda wako. Kila wawekapo ukweli katika vitendo, kila wapitiapo usafishaji, kila wanapojaribiwa, na kila wakati kazi ya Mungu inapowashukia, watu wanapitia mateso makubwa. Haya yote ni mtihani wa watu, na kwa hivyo ndani yao wote mna vita. Hii ndiyo gharama hasa wanayolipa. Kusoma zaidi neno la Mungu na kuzungukazunguka zaidi, kwa namna fulani ni gharama. Ndiyo watu wanapaswa kufanya, ndio wajibu wao, na jukumu ambalo ni sharti walitimize, lakini ni lazima watu waweke kando yale yanayofaa kuwekwa kando. Ikiwa hamwezi, basi haijalishi mateso yako yatakuwa makubwa kiasi gani, na utazunguka kiasi gani, yote yatakuwa bure! Hivi ni kusema, ni mabadiliko ndani yako tu yanaweza kuamua iwapo mateso yako ya nje yana thamani. Tabia yako ya ndani ikibadilika na ikiwa umeweka ukweli katika vitendo, basi mateso yako yote ya nje yatapata kibali cha Mungu; ikiwa hakujakuwa na mabadiliko katika tabia yako ya ndani, basi haijalishi unateseka kiasi gani au unazungukazunguka kiasi gani nje, hakutakuwa na kibali kutoka kwa Mungu—na mateso ambayo hayajaidhinishwa na Mungu ni bure! Hivyo, kama gharama ambayo umelipa imedhinishwa na Mungu inaamuliwa na kama umekuwa na mabadiliko ndani yako au la, na kama unatia ukweli katika vitendo na kuasi dhidi ya motisha na dhana zako mwenyewe ili kupata ridhaa ya mapenzi ya Mungu, ufahamu wa Mungu, na uaminifu kwa Mungu. Haijalishi unazungukazunguka kiasi gani, ikiwa hujawahi kujua kuasi dhidi ya motisha zako, unatafuta tu matendo na hamasa za nje, na usitilie maanani maisha yako, basi taabu zako zitakuwa zimepita bure. Ikiwa una kitu unachotaka kusema katika mazingira fulani, ila kwa ndani unahisi kwamba kukisema si sawa, kwamba kukisema hakuna faida kwa ndugu na dada zako, na kinaweza kuwadhuru, basi na usikiseme, uchague kuumia kwa ndani, kwa kuwa haya maneno hayawezi kuridhisha mapenzi ya Mungu. Wakati huu, kutakuwa na vita ndani yako, lakini utakuwa tayari kuumia na kuviacha uvipendavyo, utakuwa radhi kustahimili haya mateso ili kumridhisha Mungu na ingawa utaumia kwa ndani, hutautosheleza mwili, na moyo wa Mungu utakuwa umeridhishwa, hivyo utafarijika kwa ndani. Kwa hakika huku ni kulipa gharama, na ndiyo gharama inayotakiwa na Mungu. Ukitenda kwa njia hii, kwa hakika Mungu atakubariki; ikiwa huwezi kulifanikisha hili, basi haijalishi unaelewa kiasi gani, au unaweza kunena vyema kiasi gani, yote haya hayatafaa kitu! Katika njia ya kumpenda Mungu, ikiwa unaweza kusimama upande wa Mungu anapopigana na Shetani, na usimgeukie Shetani, basi utakuwa umefanikisha mapenzi ya Mungu, na utakuwa umesimama imara katika ushuhuda wako.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 497)
Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita. Kwa mfano, ikiwa unawabagua ndugu na dada zako, utakuwa na maneno ambayo unataka kusema—maneno unayohisi huenda yasimpendeze Mungu—lakini usipoyasema, utahisi kutoridhika ndani, na kwa wakati huu vita vitazuka ndani yako: “Niseme au nisiseme?” Hivi ndivyo vita. Kwa hivyo, katika kila jambo unalopitia kuna vita, na wakati kuna vita ndani yako, kutokana na ushirikiano wako na kuteseka kwako, Mungu anafanya kazi ndani yako. Hatimaye unaweza kuliweka kando jambo lenyewe na ghadhabu yako inazimika. Hiyo ndiyo athari ya ushirika wako na Mungu. Kila kitu wafanyacho watu kinawahitaji kulipa gharama fulani katika juhudi zao. Bila taabu ya kweli, hawawezi kumridhisha Mungu, hata hawakaribii kumridhisha Mungu, na wanarusha tu maneno matupu! Je, haya maneno matupu yaweza kumridhisha Mungu? Wakati Mungu na Shetani wanapigana katika milki ya kiroho, utamridhishaje Mungu, na utasimamaje imara katika ushuhuda wako Kwake? Unapaswa kujua kuwa kila kitu unachokipitia ni majaribu makubwa na ndipo Mungu hukuhitaji kuwa na ushuhuda. Kwa nje yataonekana kama mambo madogo; lakini haya mambo yakitendeka huonyesha kama unampenda Mungu au la. Ikiwa unampenda, utaweza kusimama imara katika ushuhuda wako Kwake, na ikiwa hujaweka upendo Wake katika vitendo, hili linaonyesha kuwa wewe si Mtu ambaye anapenda kuuweka ukweli katika vitendo, kwamba huna ukweli, huna uzima, kuwa wewe ni makapi! Mambo huwatokea watu wakati Mungu anawataka wasimame imara katika ushuhuda wao Kwake. Hakuna kubwa lililokutendekea kwa sasa, na huna ushuhuda mkubwa, lakini kila chembe ya maisha yako ya kila siku inahusiana na ushuhuda kwa Mungu. Ikiwa utawavutia ndugu na dada zako, wanafamilia, na kila aliye karibu nawe; ikiwa siku moja wasioamini watakuja na wavutiwe na yote unenayo na utendayo, na kuona kuwa yote afanyayo Mungu ni ya ajabu, basi utakuwa umekuwa na ushuhuda. Ijapokuwa huna ufahamu na wewe si mwerevu sasa, kupitia kwa kufanywa mkamilifu na Mungu, unaweza kumridhisha na kuzingatia mapenzi Yake, ukiwaoshyesha wengine kazi kubwa Aliyofanya miongoni mwa watu wenye ubora duni wa tabia. Watu wanapokuja kumjua Mungu na kuwa washindi mbele ya Shetani, waaminifu kwa Mungu kwa kiwango kikubwa, basi hakuna aliye na uthabiti kuliko hili kundi la watu, na huu ndio ushuhuda mkubwa zaidi. Ijapokuwa huwezi kufanya kazi kubwa, unaweza kumridhisha Mungu. Wengine hawawezi kuyaacha mawazo yao, ila wewe unaweza; wengine hawawezi kuwa na ushuhuda kwa Mungu wakati wa mapito yao ya kweli, ila unaweza kutumia hadhi na matendo yako ya kweli kulipia mapenzi ya Mungu na kuwa na ushuhuda mkubwa Kwake. Hili ndilo huhesabika kama mapenzi ya kweli kwa Mungu. Ikiwa huliwezi hili, basi hutoi ushuhuda miongoni mwa jamaa zako, miongoni mwa ndugu zako, miongoni mwa dada zako, au mbele ya walimwengu. Ikiwa huwezi kuwa na ushuhuda mbele ya Shetani, Shetani atakucheka, atakuchukulia kama mzaha, mwanasesere, mara kwa mara atakuchezea na kukughadhibisha. Majaribu mengi yatakupata siku za usoni—lakini ikiwa leo unampenda Mungu kwa moyo wa dhati, na ikiwa haijalishi ukubwa wa majaribu yaliyo mbele, bila kujali unachokipitia, unaweza kusimama imara katika ushuhuda wako, na kuweza kumridhisha Mungu, basi moyo wako utafarijiwa, na utakuwa jasiri hata majaribu utakayokabiliana nayo siku za usoni yawe makubwa kiasi gani. Hamwezi kuona ni nini kitatendeka siku za usoni; mnaweza tu kuridhisha Mungu katika hali ya leo. Hamwezi kufanya kazi yoyote kubwa, na unafaa kulenga kumridhisha Mungu kwa kuyapitia maneno yake katika maisha halisi, na kuwa na ushuhuda thabiti na mzito ambao unamtia aibu Shetani. Japo mwili wako hautaridhishwa na utateseka, utakuwa umemridhisha Mungu na kumletea aibu Shetani. Ikiwa daima unatenda hivi, Mungu atakufungulia njia mbele yako. Na siku moja, jaribio kubwa likija, wengine wataanguka chini, ila utaweza kuendelea kusimama imara: kwa sababu ya gharama uliyolipa, Mungu atakulinda ili usimame imara na usianguke. Kwa kawaida, ikiwa unaweza kuweka ukweli katika vitendo na kumridhisha Mungu kwa moyo ambao unampenda kweli, kwa hakika Mungu atakulinda wakati wa majaribu ya siku zijazo. Japokuwa wewe ni mpumbavu na mwenye kimo cha chini na usiye mwerevu, Mungu hatakubagua. Inategemea iwapo motisha zako ni za haki. Unaweza kumridhisha Mungu leo, iwapo uko makini na masuala madogo, unamridhisha Mungu kwa mambo yote, una moyo unaompenda Mungu kwa dhati, unampa Mungu moyo wa dhati, na japokuwa kuna baadhi ya mambo ambayo huwezi kuelewa, unaweza kwenda mbele za Mungu kurekebisha motisha zako, na kuyafuata mapenzi ya Mungu, na kufanya kila lipaswalo kumridhisha Mungu. Pengine ndugu na dada zako wataachana nawe, lakini moyo wako utakuwa unamridhisha Mungu, na hutatamani raha za mwili. Ikiwa daima unatenda kwa namna hii, utalindwa majaribu yakikusibu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 498)
Majaribu haya yanailenga hali gani ya ndani ya watu? Yanalenga tabia ya uasi ndani ya watu ambayo haiwezi kumridhisha Mungu. Kuna mengi ambayo ni machafu ndani ya watu, na mengi ambayo ni ya unafiki, na kwa hivyo Mungu anawatia katika majaribu ili kuwasafisha. Lakini, ikiwa leo unaweza kumridhisha Mungu, basi majaribu ya siku zijazo yatakuwa ukamilifu kwako. Ikiwa leo, huwezi kumridhisha Mungu, basi majaribu ya siku za usoni yatakushawishi, na utaanguka bila kujua, na wakati huo hutaweza kujisaidia mwenyewe, kwani huendani na kazi ya Mungu, na huna kimo halisi. Na kwa hivyo, kama unataka kuweza kusimama imara katika siku za usoni, kumridhisha vyema Mungu, na kumfuata hadi mwisho, unapaswa kujenga msingi thabiti leo, unafaa kumridhisha Mungu kwa kutia ukweli katika vitendo kwa kila jambo, na kuzingatia mapenzi Yake. Iwapo daima unatenda kwa namna hii, kutakuwa na msingi ndani yako, na Mungu atahamasisha ndani yako moyo unaompenda, na Atakupa imani. Siku moja ambapo majaribu yatakuwa yamekukumba kwa kweli, ijapo utaumia, na kuhisi umedhulumiwa kwa kiwango fulani, na kuwa na huzuni kubwa, kana kwamba ulikuwa umekufa—ila mapenzi yako kwa Mungu hayatabadilika, na yataongezeka zaidi. Hizo ni baraka za Mungu. Ikiwa unaweza kumkubali Mungu na yote asemayo na atendayo leo kwa moyo mtiifu, basi kwa hakika utabarikiwa na Mungu, na kwa hivyo utakuwa mtu aliyebarikiwa na Mungu, na anayepokea ahadi Yake. Ikiwa leo hutendi, siku ambayo majaribu yatakukumba utakosa imani au moyo wenye mapenzi, na wakati huo jaribu litakuwa kishawishi; utatoswa ndani ya kishawishi cha Shetani na hutapata namna ya kuponyoka. Leo, unaweza kusimama imara jaribio dogo likikukabili, ila huenda usiweze kusimama imara siku ambayo jaribio kubwa litakukumba. Baadhi ya watu hujivuna, na kufikiri kwamba wako karibu na ukamilifu. Ikiwa huzami zaidi wakati huo, na kuridhika, basi utakuwa hatarini. Leo, Mungu hafanyi kazi ya majaribu makubwa, kwa kuonekana, kila kitu kiko salama, ila Mungu atakapokujaribu, utagundua kuwa umepungukiwa sana, kwani kimo chako ni kidogo mno, na huna uwezo wa kustahimili majaribu mazito. Ukisalia jinsi ulivyo na uko katika hali ya inesha, basi, majaribu yatakapokuja, utaanguka. Mara nyingi inafaa mtazame udogo wa kimo chenu; mtapiga hatua kwa njia hii tu. Ikiwa unauona udogo wa ukomavu wako wakati wa majaribu tu, kwamba kimo chako ni dhaifu, kwamba kuna kidogo sana ndani yako ambacho ni halisi, na kwamba hutoshi kwa mapenzi ya Mungu—na kama utagundua haya wakati wa majaribu tu, utakuwa umechelewa mno.
Ikiwa hujui tabia ya Mungu, bila shaka utaanguka wakati wa majaribu, kwa kuwa hufahamu jinsi Mungu anavyowafanya watu kuwa wakamilifu, na ni kwa njia gani Huwafanya wakamilifu, na majaribu ya Mungu yakikushukia na yasilingane na mawazo yako, utashindwa kusimama imara. Upendo wa kweli wa Mungu ni tabia Yake kamili, na tabia kamili ya Mungu inapoonyeshwa kwa watu, hili linauletea mwili wako nini? Tabia ya haki ya Mungu inapoonyeshwa kwa watu, bila shaka miili yao iapata uchungu mkubwa zaidi. Iwapo hutapata haya maumivu, basi huwezi kufanywa mkamilifu na Mungu, wala huwezi kumpa Mungu mapenzi ya kweli. Mungu akikufanya mkamilifu kwa hakika atakuonyesha tabia Yake kamili. Tangu uumbaji hadi leo, Mungu hajawahi kumwonyesha mwanadamu tabia Yake kamili—ila katika siku za mwisho Anaifichua kwa hili kundi la watu ambao Aliwateua awali na kuwachagua, na kwa kuwafanya watu wakamilifu, Anaiweka wazi tabia Yake, na kupitia kwayo Analifanya kamili kundi la watu. Huo ndio upendo wa kweli wa Mungu kwa watu. Kuyapitia mapenzi ya kweli ya Mungu kunawapasa watu wastahimili uchungu mkali, na kulipa gharama kubwa. Ni baada tu ya hili ndipo watapatikana na Mungu na waweze kutoa tena mapenzi ya kweli kwa Mungu, na ni hapo tu ndipo Moyo wa Mungu utaridhishwa. Ikiwa watu wanataka wafanywe wakamilifu na Mungu, na kama wanataka kufanya na mapenzi Yake, na kumpa Mungu mapenzi yao ya dhati kikamilifu, ni sharti wapitie mateso mengi na maumivu makali kutokana na hali hizo, kupata uchungu mkali kuliko mauti, hatimaye watashurutishwa kuirejesha mioyo yao ya kweli kwa Mungu. Ikiwa mtu anampenda Mungu kwa dhati au la, itafichuliwa wakati wa shida na usafishaji. Mungu hutakasa mapenzi ya watu, na hili vilevile hupatikana tu ndani ya shida na usafishaji.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 499)
Kiini cha imani ya watu wengi katika Mungu ni imani za kidini: Hawana uwezo wa kumpenda Mungu na wanaweza kumfuata Mungu tu kama roboti, bila kuweza kumtamani Mungu, ama kumwabudu. Wanamfuata tu kimyakimya. Watu wengi wanamwamini Mungu, lakini wapo wachache sana ambao humpenda Mungu; “wanamheshimu” tu Mungu kwa sababu wanaogopa majanga, au hata wanamstahi Mungu kwa sababu ni Mwenye nguvu na aliye juu—lakini katika kumheshimu na kuvutiwa kwao hakuna upendo au kutamani kwa kweli. Katika matukio wanayoyapitia wanataka chembe za ukweli, au hata miujiza fulani isiyokuwa na maana. Watu wengi hufuata tu, wanapitia njia mbaya ili tu kupokea baraka; hawataki ukweli, wala kumtii Mungu kwa kweli ili kupokea baraka za Mungu. Maisha ya imani kwa Mungu ya watu wote hayana maana, hayana thamani, na katika imani yao mna fikira na kazi zao za kibinafsi; hawaamini katika Mungu ili kumpenda Mungu, lakini kwa ajili ya kutaka kubarikiwa. Watu wengi hutenda jinsi wapendavyo, hufanya wanachokitaka, na kutojali anachopenda Mungu, au kama wanachokifanya ni kulingana na mapenzi ya Mungu. Watu kama hao hawawezi kupata imani ya kweli, sembuse upendo wa Mungu. Kiini cha Mungu sio tu kwa mwanadamu kuamini; vilevile ni, kwa mwanadamu kupenda. Lakini wengi wa wale wanaomwamini Mungu hawana uwezo wa kugundua hii “siri.” Watu hawathubutu kumpenda Mungu, wala hawajaribu kumpenda Yeye. Hawajawahi kugundua kuwa kuna mengi sana ya kupendeza kuhusu Mungu, hawajawahi kugundua kwamba Mungu ni Mungu anayempenda mwanadamu, na kwamba ni Mungu ambaye mwanadamu anapaswa kumpenda. Upendo wa Mungu umeonyeshwa katika kazi Yake: ni baada tu ya kupitia kazi Yake ndipo wanaweza wakagundua upendo Wake, ni katika matukio wanayopitia ya hakika tu ambapo wanaweza kufahamu upendo wa Mungu, na bila kuupitia katika maisha halisi, hakuna anayeweza kugundua kupendeza kwa Mungu. Kuna mengi ya kupendeza kumhusu Mungu, lakini bila ya kujihusisha na Yeye kwa hakika watu wengi hawana uwezo wa kuyagundua. Hivi ni kusema, kama Mungu asingefanyika mwili, watu wasingekuwa na uwezo wa kujihusisha na Yeye, na kama wasingekuwa na uwezo wa kujihusisha na Yeye, pia wasingeweza kupitia Kazi Yake—na kwa hivyo upendo wao kwa Mungu ungetiwa doa la uongo mwingi na mawazo. Upendo wa Mungu ulio mbinguni si halisi kama upendo wa Mungu ulio ulimwenguni, kwa kuwa ufahamu wa watu kuhusu Mungu aliye mbinguni umejengwa katika mawazo yao, bali si kwa yale ambayo wameyaona kwa macho yao, na yale ambayo wameyapitia wao wenyewe. Mungu anapokuja ulimwenguni, watu wanaweza kuyaona matendo Yake halisi na upendo wake, na wanaweza kuona kila kitu katika matendo na tabia Zake za kawaida, ambayo ni mara elfu halisi kuliko ufahamu wa Mungu aliye mbinguni. Bila kujali ni vipi ambavyo watu wanampenda Mungu aliye mbinguni, hakuna kitu halisi kuhusu huu upendo, na umejaa mawazo ya kibinadamu. Haijalishi udogo wa upendo wao kwa Mungu aliye duniani, huu upendo ni halisi; hata kama ni kidogo, ungali ni halisi. Mungu huwafanya watu kumjua kupitia kazi halisi, na kupitia ufahamu huu Anapata upendo wao. Ni kama Petro: kama hangeishi na Yesu, haingewezekana yeye kumwabudu Yesu. Aidha, huu uaminifu ulijengwa kwenye uhusiano wake na Yesu. Ili kumfanya mwanadamu ampende, Mungu amekuja miongoni mwa wanadamu na kuishi na wanadamu, na yote Anayomfanya mwanadamu kuona na kupitia ni uhalisi wa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 500)
Mungu hutumia uhalisi na ujio wa ukweli kuwafanya watu kuwa wakamilifu; maneno ya Mungu hutimiza sehemu ya kuwafanya watu kuwa wakamilifu, na hii ni kazi ya uelekezaji na kufungua njia. Hivi ni kusema, katika maneno ya Mungu lazima utafute njia ya matendo, na lazima utafute ufahamu wa maono. Kwa kuyaelewa haya mambo, mwanadamu atakuwa na njia na maono anapotenda, na kuweza kupata nuru kupitia maneno ya Mungu, ataweza kuelewa kuwa haya mambo hutoka kwa Mungu, na kuweza kutambua mengi. Baada ya kuelewa, lazima aingie katika uhalisia mara moja, na kutumia maneno ya Mungu kumridhisha Mungu katika maisha yake halisi. Mungu atakuelekeza katika mambo yote, na Atakupa njia ya matendo, na kukufanya uhisi kuwa Mungu anapendeza sana, na kukufanya uone kuwa kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako ni kwa ajili ya kukufanya uwe mkamilifu. Ukitaka kuona upendo wa Mungu, ukitaka kwa kweli kupitia katika upendo wa Mungu, hivyo ni lazima uzame katika uhalisi, ni lazima uzame katika maisha halisi, na kuona kwamba kila kitu afanyacho Mungu ni upendo, na wokovu, na kwamba watu waweze kuacha kile ambacho si safi, na kwa ajili ya kusafisha mambo ndani yao ambayo hayana uwezo wa kuridhisha mapenzi ya Mungu. Mungu hutumia maneno kumkimu mwanadamu na wakati huo huo kutengeneza mazingira katika maisha halisi ambayo huwaruhusu watu kupitia, na kama watu watakula na kunywa maneno mengi ya Mungu, basi wanapoyaweka katika vitendo, wanaweza kutatua matatizo yote katika maisha yao kwa kutumia maneno mengi ya Mungu. Hivi ni kusema, lazima uwe na maneno ya Mungu ili kuzama katika uhalisi; kama huli na hunywi maneno ya Mungu, na huna kazi ya Mungu, basi hutakuwa na njia katika maisha halisi. Kama hujawahi kushiriki maneno ya Mungu, basi utashangaa wakati mambo yatakapokutokea. Unajua tu kwamba unapaswa kumpenda Mungu, lakini huwezi kutofautisha chochote, na huna njia ya vitendo; umevurugika na kuchanganyikiwa, na mara nyingine unaamini kuwa kwa kuuridhisha mwili unamridhisha Mungu—yote ambayo ni matokeo ya kutokula na kunywa maneno ya Mungu. Hivi ni kusema, kama huna usaidizi wa maneno ya Mungu, na kutapatapa tu katika uhalisi, basi kimsingi huna uwezo wa kupata njia ya vitendo. Watu kama hawa hawaelewi maana ya kumwamini Mungu, au hata kuelewa kumpenda Mungu kunamaanisha nini. Ikiwa, kwa kutumia nuru na uelekezaji wa maneno ya Mungu, unaomba mara kwa mara, na kuchunguza, na kutafuta, ambayo kwayo unagundua kile unachofaa kuweka katika vitendo, kutafuta fursa ya Kazi ya Roho Mtakatifu, unashirikiana na Mungu kwa kweli, na huvurugiki na kuchanganyikiwa, basi utakuwa na njia katika maisha halisi, na kumridhisha Mungu kwa kweli. Ukimridhisha Mungu, ndani yako kutakuwa na uelekezaji wa Mungu, na hasa kubarikiwa na Mungu, ambako kutakupa hisia za furaha: utahisi hasa umeheshimika kwa kuwa umemridhisha Mungu, na utahisi umeng'aa kwa ndani, na katika moyo wako utakuwa wazi na mwenye amani, dhamiri yako itafarijiwa na haitakuwa na shutuma, utahisi furaha ndani yako uwaonapo ndugu na dada zako. Hii ndio maana ya kufurahia upendo wa Mungu, na kwa kweli huku ndiko kumfurahia Mungu. Furaha ya watu kutokana na upendo wa Mungu inapatikana kwa kupitia matukio: kwa kupitia matatizo, na kupitia uwekaji ukweli katika vitendo, wanapata baraka za Mungu. Kama unasema tu Mungu anakupenda, kuwa Mungu amelipa gharama kubwa kwa watu, kuwa Mungu ameongea maneno mengi kwa uvumilivu na huruma, na Huokoa watu kila mara, utamkaji wako wa maneno haya ni upande mmoja tu wa kumfurahia Mungu. Ilhali, raha kubwa zaidi—kufurahia halisi—kungekuwa ni kwa watu kuweka ukweli katika vitendo katika maisha yako halisi, ambapo baadaye watakuwa na amani na kuwa wazi moyoni mwao, watahisi wakiwa wamesisimka, ndani yao, na kuwa Mungu anapendeza sana. Utahisi kuwa gharama uliyoilipa inafaa sana. Baada ya kulipa gharama kubwa katika juhudi zako, utang'aa hasa ndani yako: utahisi kuwa unafurahia upendo wa Mungu kwa kweli, na kuelewa kuwa Mungu amefanya Kazi ya kuwaokoa watu, kuwa kuwasafisha watu ni kwa ajili ya kuwatakasa, na kuwa Mungu anawajaribu watu ili kupima kama wanampenda kwa kweli. Kama utaweka ukweli katika vitendo kwa njia hii, basi hatua kwa hatua utakuza ufahamu wazi zaidi wa kazi ya Mungu, na wakati huo utakuwa unahisi kuwa maneno ya Mungu mbele yako yatakuwa wazi kabisa. Kama unaweza kuelewa waziwazi ukweli mwingi, utahisi kuwa maswala yote ni rahisi kuweka katika vitendo, kuwa utashinda swala hili, na kushinda jaribio hilo, na utaona kuwa hakuna chochote kigumu kwako, ambacho kitakufanya kuwa mtu huru na aliyekombolewa. Kufikia hapa utakuwa ukifurahia upendo wa Mungu, na upendo wa Mungu wa kweli utakuwa umekushukia. Mungu hubariki wale ambao wana maono, ambao wana ukweli, ambao wana ufahamu, na ambao wanampenda kwa kweli. Watu wakitaka kuuona upendo wa Mungu, lazima waweke ukweli katika vitendo katika maisha halisi, lazima wawe tayari kuvumilia mateso na kuacha hicho wanachokipenda na kumridhisha Mungu, mbali na machozi kwenye macho yao, lazima waweze kuuridhisha moyo wa Mungu. Kwa njia hii, kwa hakika Mungu atakubariki, na ukivumilia matatizo kama haya, yatafuatiwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kupitia kwa maisha halisi, na kutokana na kupitia maneno ya Mungu, watu wanaweza kuona upendo wa Mungu, na wanaweza kumpenda Mungu kwa ukweli ikiwa tu wameuonja upendo wa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 501)
Kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyokuwa na ukweli; kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyokuwa na upendo wa Mungu; na kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyobarikiwa na Mungu. Kama utatenda kwa njia hii kila mara, upendo wa Mungu kwako utakuwezesha kuona polepole, jinsi tu ambavyo Petro alivyokuja kumjua Mungu: Petro alisema kuwa si kuwa Mungu ana busara ya kuumba mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo pekee, lakini, aidha, kuwa Ana busara ya kufanya kazi halisi ndani ya watu. Petro alisema kuwa Mungu hastahili tu upendo wa watu kwa sababu ya uumbaji Wake wa mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo, lakini, vilevile, kwa sababu ya uwezo Wake wa kuumba mwanadamu, kumwokoa, kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na kutoa upendo wake kwa mwanadamu. Petro alimwambia Yesu: “Je, Hustahili upendo wa watu zaidi ya kuumba mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo? Kuna mengi ndani Yako ambayo yanapendeka, unatenda na kuendelea katika maisha halisi, Roho Wako ananigusa ndani, unanifundisha nidhamu, unanikemea—haya mambo yanastahili zaidi upendo wa watu.” Kama unataka kuona na kupitia upendo wa Mungu, basi lazima uzuru na kutafuta katika maisha halisi, na uwe tayari kuweka kando mwili wako. Lazima ufanye azimio hili: kuwa mtu mwenye uamuzi, ambaye anaweza kumridhisha Mungu katika mambo yote, bila ya kuzembea, au kutamani kuufurahisha mwili, kutoishi kwa ajili ya mwili lakini kuishi kwa ajili ya Mungu. Kunaweza kuwa na nyakati ambazo hukumridhisha Mungu. Hii ni kwa sababu huelewi mapenzi ya Mungu; wakati ujao, hata kama itahitaji juhudi zaidi, lazima umridhishe Mungu, na lazima usiuridhishe mwili. Unapopitia kwa njia hii, utakuja kumjua Mungu. Utaona kuwa Mungu angeweza kuumba mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo, na Amekuwa mwili ili watu wamwone kwa uhakika, na kujihusisha na Yeye, kuwa ana uwezo wa kuishi miongoni mwa wanadamu, kuwa Roho Wake aweza kufanya watu kuwa wakamilifu katika maisha halisi, kuwawezesha kuona upendo na uzoefu wa nidhamu Yake, kurudi Kwake, na baraka Zake. Kama huwa unapitia kwa njia hii, katika maisha halisi hutatenganishwa na Mungu, na kama siku moja uhusiano wako na Mungu utaacha kuwa wa kawaida, utaweza kupatwa na aibu, na kuweza kuhisi huzuni. Unapokuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, hutatamani kamwe kutaka kumuacha, na siku moja Mungu akisema Atakuacha, utaogopa, na kusema kuwa ni heri ufe kuliko kuachwa na Mungu. Punde tu unapokuwa na hisia hizi, utahisi kuwa hakuna uwezo wa kumwacha Mungu, na kwa njia hii utakuwa na msingi, na utafurahia upendo wa Mungu wa kweli.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 502)
Mara nyingi watu husema kuwa wamemfanya Mungu kuwa maisha yao, lakini bado wangali kupitia hatua hii. Wanasema tu kuwa Mungu ndiye maisha yao, kuwa Anawaongoza kila siku, kuwa wanakula na kunywa maneno Yake kila siku, na kuwa wanamwomba kila siku, na hivyo Amekuwa ndiye maisha yao. Ufahamu wa wanaosema hili ni wa juu juu. Ndani ya watu wengi hakuna msingi; maneno ya Mungu yamepandwa ndani yao, lakini bado hayajaota, au hata kuzaa tunda lolote. Hadi leo, umepitia uzoefu wa kiwango gani? Ni saa hii, baada ya Mungu kukulazimisha kuja umbali huu, ndio unahisi kuwa huwezi kumuacha Mungu. Siku moja ukishakuwa na uzoefu hadi kiwango fulani, Mungu akitaka kukuacha, hutaweza kufanya hivyo. Daima utahisi kuwa huwezi kuishi bila Mungu ndani yako; waweza kuwa bila mume, mke, au watoto, bila familia, bila mama au baba, bila kufurahia kwa mwili, lakini huwezi kuishi bila Mungu. Kuwa bila Mungu itakuwa kama kupoteza uhai wako, hutaweza kuishi bila Mungu. Unapopitia hadi kiwango hiki, utakuwa umefanikisha imani yako kwa Mungu, na kwa njia hii Mungu atakuwa maisha yako, atakuwa msingi wa kuishi kwako, na hutaweza tena kumuacha Mungu. Unapokuwa umepitia hadi kiwango hiki, utakuwa umefurahia upendo wa Mungu kwelikweli, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa karibu mno, Mungu atakuwa maisha yako, upendo wako, na wakati huo utaomba kwa Mungu na kusema: “Ee Mungu! Siwezi kukuacha, wewe ndiwe maisha yangu, naweza kuishi bila vitu vingine vyote—lakini bila Wewe siwezi kuendelea kuishi.” Hiki ni kimo halisi cha watu; ni maisha halisi. Watu wengine wamelazimika kufika walipo siku ya leo: lazima waendelee wapende wasipende, na daima huhisi kuwa wako katika hali ngumu. Lazima ugundue kuwa Mungu yupo maishani mwako, kiasi kwamba kama Mungu angeondolewa kutoka katika moyo wako ingekuwa kama kupoteza uhai wako; Mungu lazima awe maisha yako, na lazima uwe huwezi kumwacha. Kwa njia hii utakuwa umekutana na Mungu, na kwa wakati huu, unapompenda Mungu, utampenda Mungu kwa kweli, na utakuwa upendo wa kipekee, upendo safi. Siku moja, matukio unayopitia yatakapokuwa kwamba maisha yako yamefikia kiwango fulani, unapomwomba Mungu, na kula na kunywa maneno ya Mungu, hutaweza kumwacha Mungu ndani, wala hutaweza kumsahau hata kama unataka. Mungu atakuwa maisha yako, waweza kuusahau ulimwengu, waweza kumsahau mkeo, mmeo, au watoto, lakini itakuwia vigumu kumsahau Mungu—hilo haliwezekani, haya ndiyo maisha yako halisi, na upendo wako wa ukweli kwa Mungu. Upendo wa watu kwa Mungu ufikiapo kiwango fulani, upendo wao kwa kitu kingine chochote huwezi kulinganishwa na upendo wao kwa Mungu; upendo wao kwa Mungu unapewa kipaumbele. Kwa njia hii wanaweza kuacha vitu vingine vyote, na wawe tayari kukubali kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Unapopata pendo kutoka kwa Mungu ambalo linazidi mengine yote, utaishi katika uhalisi, na katika upendo wa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 503)
Punde tu Mungu anapokuwa uzima katika watu, wanakuwa hawana uwezo wa kumwacha Mungu. Je, hili sio tukio la Mungu? Hakuna ushuhuda mkubwa kuliko huu! Mungu amefanya kazi hadi kiwango fulani; Amewataka watu kutoa huduma, na kuadibiwa, au kufa, na watu hawajarudi nyuma, ambalo linaonyesha kuwa watu hawa wameshindwa na Mungu. Watu ambao wana ukweli ni wale ambao, katika matukio wanayopitia ya kweli, wanaweza kusimama imara katika ushuhuda wao, kusimama imara katika nafasi zao, kusimama katika upande wa Mungu, bila kurudi nyuma, na ambao wanaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na watu wanaompenda Mungu, wale ambao, mambo yakishawatokea, wanaweza kumtii Mungu kabisa, na wanaweza kumtii Mungu hadi kifo. Matendo na ufunuo wako katika maisha halisi ndio ushuhuda wa Mungu, ni kuishi kwa kudhihirisha maisha ya mwanadamu na ushuhuda wa Mungu, na huku ni kufurahia upendo wa Mungu; unapopitia hadi kiwango hiki, matukio unayopitia yatakuwa yamekuwa na athari. Watu ambao wameuona upendo wa Mungu kwa kweli ni wale ambao wanaishi kwa kudhihirisha kwa kweli, ambao kila matendo yao yanapongezwa na wengine. Mavazi na kuonekana kwenu kwa nje hakupendezi, lakini wanaoishi kwa kudhihirisha maisha ya utiifu wa hali ya juu, ambao wanawasiliana kwa karibu maneno ya Mungu na huelekezwa na Mungu, na kupata nuru kutoka kwa Mungu, ambao huweza kuongea mapenzi ya Mungu katika maneno yao, na wanawasiliana kwa karibu uhalisi, ambao huelewa zaidi kuhusu kuhudumu katika Roho, wanaongea kwa wazi, ambao ni wenye heshima na kuaminika, ambao hawakabiliki na wana tabia nzuri, ambao wanaweza kutii mipango ya Mungu na kusimama imara katika ushuhuda wakati mambo yanapowatokea, ambao wana utulivu bila kujali wanachokumbana nacho. Watu wengine wangali wachanga, lakini wanatenda kama mtu mzima; wamekomaa, wana ukweli, wanapendwa na wengine—na hawa ndio watu ambao wana ushuhuda, na ndio udhihirisho wa Mungu. Ni sawa na kusema, wanapopitia mambo na kufikia kiwango fulani, ndani yao watakuwa na ufahamu juu ya Mungu, tabia zao za ndani zitakuwa zimeimarika. Watu wengi hawaweki ukweli katika vitendo na wengi hawasimami imara kwa ushuhuda wao. Ndani ya watu kama hao hakuna upendo wa Mungu, au ushuhuda kwa Mungu, na hawa ndio watu ambao wanachukiwa sana na Mungu. Wanasoma maneno ya Mungu katika mikutano, lakini wanachoishi kwa kudhihirisha ni Shetani, na huku ni kumfedhehesha Mungu, kumkashifu Mungu na kumkufuru Mungu. Ndani ya watu kama hawa, hakuna dalili ya upendo wa Mungu, na hawana kazi ya Roho Mtakatifu hata kidogo. Kwa hivyo maneno na matendo ya watu yanamwakilisha shetani. Kama moyo wako uko na amani na Mungu kila wakati, na huwa uko makini kwa watu na vitu vinavyokuzunguka, na kinachoendelea katika mazingira yako, na unafahamu mzigo wa Mungu, na kila mara una moyo unaomheshimu Mungu, basi Mungu atakupa nuru ndani yako. Kanisani kuna watu ambao ni “wasimamizi”, wanatazama makosa ya wengine, kisha kunakili na kuwa kama wao. Hawana uwezo wa kutofautisha, hawachukii dhambi, hawachukii au kughadhibishwa na vitu vya Shetani. Watu kama hao wamejawa na vitu vya Shetani, na hatimaye wataachwa na Mungu kabisa. Wale ambao wana maono kama msingi wao, na ambao huandama maendeleo, ni wale ambao mioyo yao daima inamheshimu Mungu, ambao ni wa wastani katika maneno na vitendo vyao, ambao wasingetaka kumpinga Mungu, kumkasirisha Mungu, au Kazi ya Mungu kwao isiwe na thamani, au shida walizozipitia ziwe bure, au yale yote ambayo wameweka katika vitendo yapite bure. Ni watu ambao wako tayari kutoa juhudi zaidi na upendo wa Mungu katika njia iliyo mbele.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 504)
Watu wakimwamini Mungu, na kupitia maneno ya Mungu, kwa moyo unaomheshimu Mungu, basi ndani ya watu hao kunaweza kuonekana wokovu wa Mungu, na upendo wa Mungu. Watu hawa wana uwezo wa kumshuhudia Mungu, wanaishi kwa kudhihirisha ukweli, na kile wanachokikiri ni kweli, kile Mungu Alicho, na tabia ya Mungu, na wanaishi Kati ya upendo wa Mungu na wameona upendo wa Mungu. Watu wakitaka kumpenda Mungu, lazima wauonje upendo wa Mungu, na kuuona upendo wa Mungu; hapo tu ndipo wanaweza kupata kuamshiwa moyo ndani yao ambao unampenda Mungu, moyo ambao uko tayari kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu kwa heshima. Mungu hawafanyi watu kumpenda kupitia maneno na sura, au kwa mawazo yao, na Hawalazimishi watu kumpenda. Badala yake, Anawafanya wampende kwa hiari yao, na huwafanya kuyaona mapenzi Yake katika kazi Yake na matamshi, ambapo baadaye wanakuwa na upendo wa Mungu. Ni kwa njia hii tu ndio watu wanaweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Watu hawampendi Mungu kwa sababu wameombwa na wengine kufanya vile, wala si msukumo wa hisia wa muda mfupi. Wanampenda Mungu kwa sababu wameuona upendo wake, na wameona kuwa kuna mengi kumhusu ambayo yanastahili upendo wao, kwa sababu wameona wokovu wa Mungu, busara, na matendo ya ajabu—na kutokana na hayo, wanamsifu Mungu kwa kweli, na kumtamani kwa kweli, na wanaamshiwa msisimko ndani yao kwamba hawawezi kuishi bila kumpata Mungu. Sababu ya wale ambao humshuhudia Mungu wanaweza kumtolea ushuhuda wa kufana ni kwa kuwa ushuhuda wao umekitwa kwenye msingi wa ufahamu wa kweli pamoja na matamanio ya kweli kwa Mungu, si kutokana na msukumo wa hisia, lakini kulingana na ufahamu wa Mungu na tabia Zake. Kwa sababu wamepata kumjua Mungu, wanahisi kwamba lazima wamshuhudie Mungu, na kuwafanya wale wote wamtamanio Mungu wamjue Mungu, na kufahamu upendo wa Mungu, na uhalisi Wake. Sawa na mapenzi ya watu kwa Mungu, ushuhuda wao ni wa hiari, ni halisi, na una umuhimu halisi na thamani. Si baridi, au tupu na usiokuwa na maana. Sababu ya wale tu wanaompenda Mungu kweli kuwa na thamani na maana katika maisha yao, na kuamini katika Mungu tu, ni kwa sababu watu hawa wanaishi katika mwangaza wa Mungu, na wanaweza kuishi kwa ajili ya kazi ya Mungu na usimamizi Wake; hawaishi gizani, bali wanaishi katika mwangaza; hawaishi maisha yasiokuwa na maana, ila wanaishi maisha ambayo yamebarikiwa na Mungu. Ni wale tu ambao wanampenda Mungu wanaweza kumshuhudia Mungu, ndio tu mashahidi wa Mungu, ndio tu wamebarikiwa na Mungu, na ndio tu wanaweza kupokea ahadi za Mungu. Wanaompenda Mungu ni wandani wa Mungu, ndio watu ambao wamependwa na Mungu, na wanaweza kufurahia baraka pamoja na Mungu. Ni watu hawa tu ambao wataishi milele, na ni wao tu wataishi milele katika utunzaji na ulinzi wa Mungu. Mungu yuko kwa ajili ya kupendwa na watu, na anastahili upendo wa watu wote, lakini si watu wote ambao wanaweza kumpenda Mungu, na si watu wote wanaweza kumshuhudia Mungu na kushiriki mamlaka pamoja na Mungu. Kwa sababu wanaweza kumshuhudia Mungu, na kutoa juhudi zao zote kwa kazi ya Mungu, wanaompenda Mungu kwa kweli wanaweza kutembea mahala popote chini ya mbingu bila ya mtu yeyote kujaribu kuwapinga, na wanaweza kushika mamlaka na kutawala watu wote wa Mungu. Hawa watu wanakusanyika pamoja kutoka pembe zote za dunia, wanazungumza lugha tofauti na ni wa rangi tofauti, lakini kuishi kwao kuna maana sawa, wote wana moyo unaompenda Mungu, wote wana ushuhuda sawa, na wana maazimio sawa, na mapenzi sawa. Wale ambao wanampenda Mungu wanaweza kutembea ulimwenguni kote wakiwa huru, wanaomshuhudia Mungu wanaweza kusafiri duniani kote. Watu hawa wamependwa wa Mungu, wamebarikiwa na Mungu, na wataishi milele katika mwangaza Wake.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 505)
Unampenda Mungu kiasi gani hasa leo? Na unajua kiasi gani hasa kuhusu yote ambayo Mungu amefanya ndani yako? Haya ni mambo unayopaswa kujifunza. Mungu anapowasili duniani, yote ambayo Amefanya ndani ya mwanadamu na kumkubalia mwanadamu kuona ni ili mwanadamu atampenda na kumjua Yeye kweli. Kwamba mwanadamu anaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu na ameweza kufikia umbali huu ni, kuhusiana na jambo moja, kwa sababu ya upendo wa Mungu, na kuhusiana na jambo lingine, ni kwa sababu ya wokovu wa Mungu; zaidi ya hayo, ni kwa sababu ya kazi ya hukumu na kuadibu ambayo Mungu ametekeleza ndani ya mwanadamu. Kama hamna hukumu, kuadibu, na majaribio ya Mungu, na kama Mungu hajawafanya mteseke, basi, kusema ukweli, ninyi hammpendi Mungu kweli. Kadri kazi ya Mungu ilivyo kuu zaidi ndani ya mwanadamu, na kadri mateso ya mwanadamu yalivyo makuu zaidi, ndivyo inavyoweza kuonyesha zaidi hasa vile kazi ya Mungu ilivyo ya maana, na ndivyo moyo wa mwanadamu unavyoweza kumpenda Mungu kweli zaidi. Unajifunzaje jinsi ya kumpenda Mungu? Bila mateso makali na usafishaji, bila majaribio ya kuumiza—na kama, zaidi ya hayo, yote ambayo Mungu alimpa mwanadamu ingekuwa neema, upendo, na rehema—je, ungeweza kufikia upendo wa kweli kwa Mungu? Kwa upande mmoja, wakati wa majaribio ya Mungu mwanadamu huja kujua kasoro zake, na huona kwamba yeye ni mdogo, wa kudharauliwa, na duni, kwamba hana chochote, na si kitu; kwa upande mwingine, wakati wa majaribio Yake Mungu humuumbia mwanadamu mazingira tofauti yanayomfanya mwanadamu aweze zaidi kupitia kupendeza kwa Mungu. Ingawa maumivu ni makubwa, na wakati mwingine yasiyoshindika—na hata hufikia kiwango cha huzuni ya kuseta—baada ya kuyapitia, mwanadamu huona vile kazi ya Mungu ndani yake ni ya kupendeza, na ni juu ya msingi huu tu ndiyo ndani ya mwanadamu huzaliwa upendo wa kweli kwa Mungu. Leo mwanadamu huona kwamba na neema, upendo na rehema ya Mungu pekee, hana uwezo wa kujijua mwenyewe kweli, sembuse kuweza kujua kiini cha mwanadamu. Ni kupitia tu usafishaji na hukumu ya Mungu, ni wakati tu wa usafishaji kama huo ndiyo mwanadamu anaweza kujua kasoro zake, na kujua kwamba hana chochote. Hivyo, upendo wa mwanadamu kwa Mungu umejengwa juu ya msingi wa usafishaji na hukumu ya Mungu. Kama wewe hufurahia tu neema ya Mungu, na maisha ya familia yenye amani au baraka yakinifu, basi hujampata Mungu, na imani yako kwa Mungu haiwezi kuchukuliwa kama iliyofaulu. Mungu tayari ametekeleza hatua moja ya kazi ya neema katika mwili, na tayari amempa mwanadamu baraka yakinifu—lakini mwanadamu hawezi kufanywa mkamilifu na neema, upendo, na rehema pekee. Katika uzoefu wa mwanadamu yeye hukabiliwa na baadhi ya upendo wa Mungu, na huuona upendo na rehema ya Mungu, lakini baada ya kupitia kwa kipindi fulani cha wakati, yeye huona kwamba neema ya Mungu na upendo na rehema Yake hayawezi kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na hayana uwezo wa kufichua kile ambacho ni potovu ndani ya mwanadamu, wala hayawezi kumwondolea mwanadamu tabia yake potovu, au kufanya kuwa kamilifu upendo na imani yake. Kazi ya Mungu ya neema ilikuwa kazi ya kipindi kimoja, na mwanadamu hawezi kutegemea kufurahia neema ya Mungu ili kumjua Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 506)
Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani, wao hukanwa na ulimwengu, maisha yao ya nyumbani yamesumbuliwa, wao si wapendwa wa Mungu, na matazamio yao ni matupu. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu! Mungu ana hamu ya mwanadamu kumpenda Yeye, lakini kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo kuteseka kwa mwanadamu huwa kwingi zaidi, na kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo majaribio ya mwanadamu huwa makubwa zaidi. Ikiwa unampenda Yeye, basi kila aina ya mateso yatakufika—na ikiwa humpendi, basi labda kila kitu kitaendelea kwa urahisi kwako, na kila kitu kinachokuzunguka kitakuwa kitulivu kwako. Unapompenda Mungu, utahisi kwamba mengi kandokando yako hayawezi kushindikana, na kwa sababu kimo chako ni kidogo sana utasafishwa; aidha, huwezi kumridhisha Mungu, na daima utahisi kwamba mapenzi ya Mungu ni ya juu sana, kwamba hayawezi kufikiwa na mwanadamu. Kwa sababu ya haya yote utasafishwa—kwa sababu kuna udhaifu mwingi ndani yako, na mengi yasiyoweza kuridhisha mapenzi ya Mungu, utasafishwa ndani. Lakini lazima muone kwa dhahiri kwamba utakaso hutimizwa tu kupitia usafishaji. Hivyo, katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana. Unapojaribiwa na Shetani, unapaswa kusema: “Moyo wangu ni wa Mungu, na Mungu tayari amenipata. Siwezi kukuridhisha wewe—lazima nitoe kila kitu changu ili kumridhisha Mungu.” Kadri unavyomridhisha Mungu, ndivyo Mungu hukubariki zaidi, na ndivyo nguvu za upendo wako kwa Mungu huwa kuu zaidi; kwa hiyo, vilevile, utakuwa na imani na azimio, na utahisi kwamba hakuna kilicho na thamani zaidi au cha maana kuliko kutumia maisha ukimpenda Mungu. Inaweza kusemwa kwamba mwanadamu anatakiwa tu kumpenda Mungu ili kuishi bila huzuni. Ingawa kuna nyakati ambazo mwili wako ni dhaifu na unazongwa na matatizo mengi ya kweli, katika nyakati hizi utamtegemea Mungu kweli, na ndani ya roho yako utafarijiwa, na utahisi hakika, na kwamba una kitu cha kutegemea. Kwa njia hii, utaweza kushinda hali nyingi, na kwa hiyo hutalalamika kuhusu Mungu kwa sababu ya uchungu unaopitia; utataka kuimba, kucheza, na kuomba, kukusanyika na kuwasiliana kwa karibu, kumfikiria Mungu, na utahisi kwamba watu wote, mambo, na vitu vilivyo kandokando yako ambavyo vimepangwa na Mungu vinafaa. Kama humpendi Mungu, yote ambayo unategemea yatakuwa yenye kero kwako, hakuna kitakachokuwa cha kufurahisha machoni mwako; ndani ya roho yako hutakuwa huru bali wa kudhulumiwa, moyo wako daima utalalamika kuhusu Mungu, na daima utahisi kwamba unapitia mateso mengi sana, na kwamba ni udhalimu sana. Kama hufuatilii kwa ajili ya furaha, bali ili umridhishe Mungu na kutoshtakiwa na Shetani, basi ukimbizaji kama huo utakupa nguvu nyingi za kumpenda Mungu. Mwanadamu anaweza kutekeleza yote yanayonenwa na Mungu, na yote ayafanyayo yanaweza kumridhisha Mungu—hii ndiyo maana ya kuwa na hakika. Kufuatilia ridhaa ya Mungu ni kuutumia upendo wa Mungu kutia maneno Yake katika vitendo; pasipo kutia maanani wakati—hata kama wengine hawana nguvu—ndani yako bado kuna moyo unaompenda Mungu, ambao unamtamani Mungu sana, na humkosa Mungu. Hiki ni kimo halisi. Jinsi ambavyo kimo chako ni kikubwa hasa hutegemea jinsi upendo wako kwa Mungu ulivyo mkuu, kama unaweza kusimama imara wakati unajaribiwa, kama wewe ni mdhaifu hali fulani inapokujia, na kama unaweza kusimama imara wakati ambapo ndugu zako wanakukataa; majilio ya ukweli yataonyesha hasa upendo wako kwa Mungu ukoje. Inaweza kuonekana kutoka kwa kazi nyingi ya Mungu kwamba Mungu kweli anampenda mwanadamu, ni hasa tu macho ya roho ya mwanadamu bado hayajafunguliwa kabisa, na hawezi kufahamu kazi nyingi ya Mungu, na mapenzi ya Mungu, na vitu vingi ambavyo ni vya kupendeza kuhusu Mungu; mwanadamu ana upendo kidogo sana wa kweli kwa Mungu. Umemwamini Mungu katika wakati huu wote, na leo Mungu amezuia njia zote za kutoroka. Kusema kwa kweli, huna chaguo lingine ila kuifuata njia sahihi, njia sahihi ambayo umeelekezwa kwayo kwa hukumu kali na wokovu mkubwa kabisa wa Mungu. Ni baada tu ya kupitia taabu na usafishaji ndiyo mwanadamu hujua kwamba Mungu ni wa kupendeza. Baada ya kupitia mpaka leo, inaweza kusemwa kwamba mwanadamu amekuja kujua sehemu ya kupendeza kwa Mungu—lakini hili bado halitoshi, kwa sababu mwanadamu amepungukiwa sana. Lazima apate uzoefu zaidi wa kazi ya Mungu ya ajabu, na zaidi ya usafishaji wote wa mateso uliowekwa na Mungu. Ni wakati huo tu ndiyo tabia ya maisha ya mwanadamu itaweza kubadilishwa.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 507)
Nyote mko katikati ya majaribu na usafishaji. Mnapaswa kumpendaje Mungu wakati wa usafishaji? Baada ya kupitia usafishaji, watu wanaweza kumtolea Mungu sifa ya kweli, na katika usafishaji, wanaweza kuona kwamba wamepungukiwa sana. Kadiri usafishaji wako ulivyo mkubwa, ndivyo unaweza zaidi kukana mwili; kadiri usafishaji wao ulivyo mkubwa, ndivyo zaidi ulivyo upendo wa watu kwa Mungu, Hili ndilo mnapaswa kuelewa. Je, kwa nini ni lazima watu wasafishwe? Linalenga kutimiza matokeo gani? Je, umuhimu wa kazi ya Mungu ya usafishaji kwa mwanadamu ni gani? Ukimtafuta Mungu kwa kweli, basi baada ya kupitia usafishaji Wake hadi kiwango fulani utahisi kwamba ni mzuri sana, na ni wa umuhimu mkubwa kabisa. Je, mwanadamu anapaswa kumpenda Mungu jinsi gani wakati wa usafishaji? Kwa kutumia azimio la kumpenda Mungu kukubali usafishaji Wake: Wakati wa usafishaji, unateseka ndani, kana kwamba kisu kinasokotwa moyoni mwako, ilhali uko tayari kumridhisha Mungu kwa kutumia moyo wako, ambao unampenda, na hauko tayari kuutunza mwili. Hii ndiyo maana ya kutenda upendo wa Mungu. Unaumia ndani, na mateso yako yamefikia kiwango fulani, lakini bado uko tayari kuja mbele ya Mungu na kuomba ukisema: “Ee Mungu! Siwezi kukuacha. Ingawa kuna giza ndani yangu, ningependa kukuridhisha; Unaujua moyo wangu, na ningependa kwamba Uwekeze zaidi ya upendo Wako ndani yangu.” Huu ndio utendaji wakati wa usafishaji. Ukitumia upendo wa Mungu kama msingi, usafishaji unaweza kukuleta karibu zaidi na Mungu na kukufanya mwandani zaidi wa Mungu. Kwa kuwa unamwamini Mungu, ni lazima uukabidhi moyo wako mbele ya Mungu. Ukiutoa moyo wako na kuuweka mbele ya Mungu, basi wakati wa usafishaji, haitawezekana wewe kumkana Mungu, au kumwacha Mungu. Kwa njia hii, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa karibu hata zaidi, na wa kawaida hata zaidi, na mawasiliano yako na Mungu yatakuwa ya mara kwa mara zaidi. Ikiwa wewe daima hutenda kwa jinsi hii, basi utashinda wakati zaidi katika mwanga wa Mungu, na wakati zaidi chini ya mwongozo wa maneno Yake, kutakuwa pia na mabadiliko zaidi na zaidi katika tabia yako, na ufahamu wako utaongezeka kila siku. Siku itakapokuja na majaribu ya Mungu yakufike kwa ghafla, hutaweza tu kusimama kando ya Mungu, bali pia utaweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Wakati huo, utakuwa kama Ayubu, na Petro. Baada ya kuwa na ushuhuda kwa Mungu, utampenda kwa kweli, na utamtolea maisha yako kwa furaha; utakuwa shahidi wa Mungu, na yule ambaye ni mpendwa wa Mungu. Upendo ambao umepitia usafishaji ni wa nguvu, na sio dhaifu. Haijalishi ni lini au vipi Mungu anakufanya upatwe na majaribu Yake, unaweza kutojali ikiwa unaishi au unaangamia, kuachana na kila kitu kwa furaha kwa ajili ya Mungu, na kuvumilia chochote kwa furaha kwa ajili ya Mungu—na hivyo upendo wako utakuwa safi, na imani yako halisi. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu anayependwa na Mungu kwa kweli, na ambaye amefanywa kamili na Mungu kwa kweli.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kuwa na Upendo wa Kweli
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 508)
Watu wakijipata chini ya ushawishi wa Shetani, basi hawana upendo kwa Mungu ndani yao, na maono, upendo na azimio yao ya awali yamepotea. Watu walikuwa wakihisi kwamba walifaa kuteseka kwa ajili ya Mungu, lakini leo wanafikiri kwamba ni aibu na hawakosi malalamiko. Hii ni kazi ya Shetani; inaonyesha kwamba mwanadamu amemilikiwa na Shetani. Ukikabiliwa na hali hii ni sharti uombe, na uibadilishe haraka uwezavyo—hii itakulinda dhidi ya mashambulizi ya Shetani. Ni wakati wa usafishaji mkali ambapo mwanadamu anaweza kujipata chini ya ushawishi wa Shetani kwa urahisi zaidi—kwa hivyo ni jinsi gani unapaswa kumpenda Mungu wakati wa usafishaji kama huu? Unapaswa kuyaita mapenzi yako, kuuweka moyo wako mbele ya Mungu na kutenga muda wako wa mwisho Kwake. Haijalishi jinsi gani Mungu hukusafisha, unafaa kuwa na uwezo wa kutia ukweli katika vitendo kutimiza mapenzi ya Mungu, na unafaa kujitolea kumtafuta Mungu na kutafuta mawasiliano. Nyakati kama hizi, zaidi unavyokaa tu, ndivyo utakuwa mtu hasi zaidi, na ndivyo itakuwa rahisi zaidi kwako kurudi nyuma. Wakati ambapo inakulazimu kutenda kazi yako, ingawa huitendi vyema, unafanya kila unachoweza, na unaifanya kwa kutumia tu upendo wako wa Mungu; bila kujali kile ambacho wengine husema—ikiwa wanasema umetenda vyema, au kwamba umetenda vibaya—motisha zako ni sahihi, na wewe sio wa kujidai, kwani unatenda kwa niaba ya Mungu. Wengine wanapokuelewa vibaya, unaweza kumwomba Mungu na kusema: “Ee Mungu! Siombi kwamba wengine wanivumilie au kunitendea vyema, wala kwamba wanielewe au kunikubali. Naomba tu kwamba niweze kukupenda moyoni mwangu, kwamba niwe na utulivu moyoni mwangu, na kwamba dhamiri yangu ni safi. Siombi kwamba wengine wanisifu, au kuniheshimu, ninatafuta tu kukuridhisha kutoka moyoni mwangu, ninatenda wajibu wangu kwa kufanya kila ninachoweza, na ingawa mimi ni mpumbavu na mjinga, na mwenye ubora wa tabia duni, na kipofu, najua kwamba Unapendeza, na niko tayari kukutolea kila ninacho.” Punde tu unapoomba kwa jinsi hii, upendo wako kwa Mungu huibuka, na unahisi utulivu zaidi moyoni mwako. Hili ndilo linalomaanishwa na kutenda upendo wa Mungu. Unavyopata uzoefu, utashindwa mara mbili na kufaulu mara moja, au pia ushindwe mara tano na kufaulu mara mbili, na unavyopata uzoefu kwa jinsi hii, ni katikati ya kushindwa tu ndipo utaweza kuona uzuri wa Mungu na kugundua kinachokosa ndani yako. Unapopitia hali kama hizi tena, unafaa kujitahadharisha, kutuliza mwendo wako, na kuomba mara nyingi zaidi. Polepole utakuza uwezo wa kushinda katika hali kama hizi. Hilo linapofanyika, maombi yako yamekuwa yenye matokeo yanayotarajiwa. Unapoona umefanikiwa wakati huu, utafurahishwa ndani yako, na unapoomba utaweza kumhisi Mungu, na kuhisi kwamba uwepo wa Roho Mtakatifu haujakutoka—na ni hapo tu ndipo utajua jinsi Mungu hufanya kazi ndani yako. Kutenda kwa njia hii kutakupa njia inayoelekea katika uzoefu. Usipoutia ukweli katika vitendo, basi utakuwa bila uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako. Lakini ukiutia ukweli katika vitendo unapokumbana na mambo jinsi yalivyo, basi, ingawa unaumia ndani, Roho Mtakatifu atakuwa nawe baadaye, utaweza kuhisi uwepo wa Mungu unapoomba, utakuwa na nguvu ya kutenda maneno ya Mungu, na wakati wa mawasiliano na ndugu zako, hakutakuwa na chochote kinachosumbua dhamiri yako, na utahisi amani, na kwa jinsi hii, utaweza kufunua yale ambayo umefanya. Bila kujali yale ambayo wengine husema, utaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, hutazuiliwa na wengine, hutashindwa na lolote—na katika hili, utaonyesha kwamba kutenda kwako maneno ya Mungu kumekuwa kwa matokeo yanayotarajiwa.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kuwa na Upendo wa Kweli
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 509)
Kadiri usafishaji wa Mungu ulivyo mkubwa, ndivyo mioyo ya watu inaweza kumpenda Mungu zaidi. Mateso ndani ya mioyo yao ni ya manufaa kwa maisha yao, wanaweza zaidi kuwa na amani mbele ya Mungu, uhusiano wao na Mungu ni wa karibu zaidi, na wanaweza kuona vizuri zaidi upendo wa juu kabisa wa Mungu na wokovu Wake wa juu kabisa. Petro alipitia usafishaji mamia ya mara, na Ayubu alipitia majaribio kadhaa. Ikiwa mngependa kufanywa kamili na Mungu, nyinyi pia sharti mpitie usafishaji mamia ya mara; ni ikiwa tu mtapitia mchakato huu, na mtegemee hatua hii, ndiyo mnaweza kuridhisha mapenzi ya Mungu, na kufanywa kamili na Mungu. Usafishaji ndio njia bora zaidi ambayo Mungu hutumia kuwafanya watu kamili; usafishaji na majaribio makali pekee ndiyo yanaweza kusababisha kuonekana upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo ya watu. Bila taabu, watu hukosa upendo wa kweli kwa Mungu; ikiwa hawajaribiwi ndani, na hawapitii usafishaji kwa kweli, basi mioyo yao daima itakuwa ikielea kwa nje. Baada ya kusafishwa hadi kiwango fulani, utayaona mapungufu na matatizo yako mwenyewe, utaona kiasi ambacho unakosa na kwamba huwezi kuzishinda zile shida nyingi unazokabiliwa nazo, na utaona jinsi kutotii kwako kulivyo kukubwa. Ni katika majaribu pekee ndipo watu wataweza kujua kwa kweli hali zao halisi, na majaribu huwafanya watu waweze kufanywa kamili vyema.
Katika maisha yake, Petro alipitia usafishaji mamia ya mara na alipitia majaribu mengi ya uchungu. Usafishaji huu ukawa msingi wa upendo wake mkubwa kabisa kwa Mungu na ukawa uzoefu muhimu zaidi katika maisha yake yote. Kwamba aliweza kuwa na upendo mkubwa kabisa wa Mungu ilikuwa, kwa namna moja, kwa sababu ya uamuzi wake kumpenda Mungu; la muhimu zaidi, hata hivyo, ilikuwa kwa sababu ya usafishaji na mateso aliyopitia. Mateso haya yakawa mwongozo wake katika njia ya kumpenda Mungu, na yakawa jambo lililokumbukwa zaidi kwake. Ikiwa watu hawapitii uchungu wa usafishaji wanapompenda Mungu, basi upendo wao umejaa uchafu na mapendeleo yao wenyewe; upendo kama huu umejaa mawazo ya Shetani, na hauwezi hata kabisa kuridhisha mapenzi ya Mungu. Kuwa na azimio la kumpenda Mungu sio sawa na kumpenda Mungu kwa kweli. Hata ingawa yote wanayofikiria mioyoni mwao ni kwa ajili ya kumpenda Mungu, na kumridhisha Mungu, kana kwamba fikira zao hazina mawazo yoyote ya kibinadamu, kana kwamba zote ni kwa ajili ya Mungu, fikira zao zinapoletwa mbele ya Mungu, fikira kama hizi hazisifiwi wala kubarikiwa na Mungu. Hata wakati watu wameelewa kikamilifu ukweli wote—wakati wamekuja kuujua wote—hili haliwezi kusemwa kuwa ishara ya kumpenda Mungu, haiwezi kusemwa kwamba watu hawa hakika wanampenda Mungu. Licha ya kuelewa ukweli mwingi bila kupitia usafishaji, watu hawana uwezo wa kutia ukweli huu katika vitendo; ni wakati wa usafishaji tu ndipo watu wanaweza kuelewa maana halisi ya ukweli huu, hapo tu ndipo watu wanaweza kufahamu kwa kweli maana yao ya ndani. Wakati huo, wanapojaribu tena, wanaweza kutia ukweli katika vitendo kwa njia ya kufaa, na kulingana na mapenzi ya Mungu; wakati huo, mawazo yao ya kibinadamu yanapunguzwa, upotovu wao wa kibinadamu unapunguzwa, na hisia zao za kibinadamu zinapunguzwa; ni wakati huo tu ndipo utendaji wao ni onyesho la ukweli la upendo wa Mungu. Athari ya ukweli wa upendo wa Mungu haitimizwi kupitia ufahamu wa kusemwa au kuwa tayari kiakili, wala haiwezi kutimizwa kwa kueleweka tu. Inahitaji kwamba watu walipe gharama, na kwamba wapitie uchungu mwingi wakati wa usafishaji, na hapo tu ndipo upendo wao utakuwa safi, na wa kuupendeza moyo wa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kuwa na Upendo wa Kweli
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 510)
Anapokabiliwa na hali ya mwanadamu na mtazamo wake kwa Mungu, Mungu amefanya kazi mpya, Akimruhusu mwanadamu kuwa na ufahamu Wake na utiifu Kwake, na upendo pia na ushahidi. Hivyo, mwanadamu lazima apitie usafishaji wa Mungu kwake, na pia hukumu, ushughulikiaji na upogoaji Wake kwake, ambazo pasi nazo mwanadamu hangewahi kumjua Mungu, na hangewahi kuwa na uwezo wa kumpenda kwa kweli na kuwa na ushuhuda Kwake. Usafishaji wa Mungu kwa mwanadamu sio tu kwa ajili ya athari inayoegemea upande mmoja, bali kwa ajili ya athari inayogusia pande nyingi. Ni kwa jinsi hii tu ndiyo Mungu hufanya kazi ya usafishaji kwa wale ambao wako tayari kutafuta ukweli, ili upendo na uamuzi wao ufanywe timilifu na Mungu. Kwa wale walio tayari kuutafuta ukweli na wanaomtamani Mungu, hakuna kilicho cha maana zaidi, au cha usaidizi zaidi, kuliko usafishaji kama huu. Tabia ya Mungu haijulikani wala kueleweka kwa urahisi sana na mwanadamu, kwani Mungu, hatimaye, ni Mungu. Mwishowe, haiwezekani kwa Mungu kuwa na tabia sawa na mwanadamu, na hivyo si rahisi kwa mwanadamu kujua tabia Yake. Ukweli haumilikiwi kwa asili na mwanadamu, na hauleweki kwa urahisi na wale ambao wamepotoshwa na Shetani; mwanadamu hana ukweli na hana azimio la kutia ukweli katika vitendo, na asipoteseka, na asisafishwe au kuhukumiwa, basi uamuzi wake hautawahi kufanywa timilifu. Kwa watu wote, usafishaji ni wa kutesa sana na ni mgumu sana kukubali—ilhali ni katika usafishaji ndipo Mungu huweka wazi tabia Yake ya haki kwa mwanadamu, na Huweka hadharani mahitaji Yake kwa mwanadamu, na Hutoa nuru zaidi, na upogoaji na ushughulikiaji halisi zaidi; kwa kulinganisha mambo ya hakika na ukweli, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa zaidi kujihusu na ukweli, na Humpa mwanadamu ufahamu mkubwa zaidi wa mapenzi ya Mungu, hivyo kumruhusu mwanadamu kuwa na upendo wa kweli zaidi na safi zaidi wa Mungu. Haya ndiyo malengo ya Mungu katika kutekeleza usafishaji. Kazi yote Afanyayo Mungu kwa mwanadamu ina malengo yake na maana yake; Mungu hafanyi kazi isiyo na maana, wala Hafanyi kazi isiyo na manufaa kwa mwanadamu. Usafishaji haumaanishi kuondoa watu kutoka mbele ya Mungu, wala haumaanishi kuwaangamiza katika kuzimu. Unamaanisha kubadilisha tabia ya mwanadamu wakati wa usafishaji, kubadilisha motisha zake, mitazamo yake ya kale, kubadilisha upendo wake kwa Mungu, na kubadilisha maisha yake yote. Usafishaji ni jaribio la kweli la mwanadamu, na aina ya mafunzo halisi na ni wakati wa usafishaji tu ndipo upendo wake unaweza kutimiza wajibu wake wa asili.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kuwa na Upendo wa Kweli
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 511)
Kama unamwamini Mungu, basi ni lazima umtii Mungu, uweke ukweli katika vitendo na utimize wajibu wako wote. Zaidi ya hayo, ni lazima uelewe mambo unayopaswa kupitia. Ikiwa unapitia tu kushughulikiwa, kufundishwa nidhamu na kuhukumiwa, kama wewe unaweza tu kumfurahia Mungu lakini usalie usiyeweza kuhisi wakati Mungu anakufundisha nidhamu au kukushughulikia—hili halikubaliki. Labda katika wakati huu wa usafishaji, unaweza kushikilia msimamo wako, bali hili bado halitoshi; ni lazima bado uendelee kusonga mbele. Funzo la kumpenda Mungu halikomi kamwe na halina mwisho. Watu huona kumwamini Mungu kama jambo lililo rahisi mno, lakini mara tu wanapopata uzoefu kiasi wa vitendo, wao kisha hutambua kwamba imani katika Mungu si rahisi kama watu wanavyofikiria. Wakati Mungu anafanya kazi ili kumsafisha mwanadamu, mwanadamu huteseka. Kadiri usafishaji wa mtu ulivyo mkubwa, ndivyo upendo wake kwa Mungu utakavyokuwa mkubwa zaidi na ndivyo nguvu za Mungu zitakavyofichuliwa zaidi kwake. Kinyume chake, kadiri mtu apokeavyo usafishaji mdogo zaidi, ndivyo upendo wake kwa Mungu utakavyokuwa kwa kiwango kidogo zaidi, na ndivyo nguvu za Mungu zitakavyofichuliwa kwake kwa kiwango kidogo zaidi. Kadiri usafishaji na uchungu wa mtu kama huyo ulivyo mkubwa na kadiri anavyopitia mateso mengi zaidi, ndivyo upendo wake kwa Mungu utakavyokuwa, ndivyo imani yake kwa Mungu itakavyokuwa ya kweli zaidi, na ndivyo maarifa yake ya Mungu yatakavyokuwa ya kina zaidi. Katika matukio unayopitia, utawaona watu wanaoteseka sana wanapokuwa wakisafishwa, wanaoshughulikiwa na kufundishwa nidhamu sana, na utaona kwamba ni watu hao ndio walio na upendo mkubwa kwa Mungu na maarifa ya kina na elekevu ya Mungu. Wale ambao hawajapitia kushughulikiwa wanayo maarifa ya juu juu tu, na wao wanaweza tu kusema: “Mungu ni mzuri sana, Yeye huwapa watu neema ili waweze kumfurahia Yeye.” Kama watu wamepitia kushughulikiwa na kufundishwa nidhamu, basi hao wanaweza kuzungumza kuhusu maarifa ya kweli ya Mungu. Hivyo kazi ya Mungu katika mwanadamu ilivyo ya ajabu zaidi, ndivyo ilivyo ya thamani zaidi na ni muhimu zaidi. Kadiri inavyokosa kupenyeza kwako zaidi na kadiri isivyolingana na mawazo yako, ndivyo kazi ya Mungu inavyoweza kukushinda, kukupata, na kukufanya mkamilifu. Umuhimu wa kazi ya Mungu ni mkubwa ulioje! Kama Mungu hangemsafisha mwanadamu kwa njia hii, kama Hangefanya kazi kulingana na njia hii, basi kazi Yake haingekuwa na ufanisi na ingekuwa isiyo na maana. Ilisemwa hapo awali kwamba Mungu angelichagua na kulipata kundi hili na kuwakamilisha katika siku za mwisho; hili lina umuhimu mkubwa sana. Kadiri kazi Anayofanya ndani yenu ilivyo kuu, ndivyo upendo wenu kwa Mungu ulivyo mkubwa na safi. Kadiri kazi ya Mungu ilivyo kuu zaidi, ndivyo mwanadamu anavyoweza kuelewa kitu kuhusu hekima Yake na ndivyo maarifa ya mwanadamu Kwake yalivyo ya kina zaidi. Katika siku za mwisho, miaka elfu sita ya mpango wa Mungu wa usimamizi itafika kikomo. Je, kweli inaweza kufika mwisho kwa urahisi? Baada ya Yeye kuwashinda wanadamu, je, kazi Yake itakuwa imefika mwisho? Je, inaweza kuwa rahisi vile? Watu kweli hufikiria kwamba ni rahisi hivi, lakini kile ambacho Mungu hufanya si rahisi vile. Bila kujali ni sehemu gani ya kazi ya Mungu unayojali kutaja, yote ni isiyoeleweka kwa mwanadamu. Ikiwa ungeweza kuifahamu, basi kazi ya Mungu ingekuwa isiyo na maana au thamani. Kazi inayofanywa na Mungu ni isiyoeleweka; ni kinyume kabisa na mawazo yako, na kadiri isivyopatana na mawazo yako, ndivyo inavyoonyesha zaidi kwamba kazi ya Mungu ni ya maana; kama ingekuwa inalingana na mawazo yako, basi ingekuwa isiyo maana. Leo, unahisi kwamba kazi ya Mungu ni ya ajabu sana, na kadiri unavyohisi kuwa ni ya ajabu, ndivyo unahisi kwamba Mungu ni asiyeeleweka, na kuona jinsi matendo ya Mungu yalivyo makubwa. Kama Angefanya tu kazi fulani ya juu juu ya kutimiza wajibu kumshinda mwanadamu na Asifanye chochote zaidi baadaye, basi mwanadamu hangeweza kuona umuhimu wa kazi ya Mungu. Ingawa unapokea usafishaji kidogo sasa, ni wa faida kubwa sana kwa ukuaji wako katika maisha; hivyo ni jambo linalohitajika sana wewe kupitia ugumu wa aina hiyo. Leo, unapokea usafishaji kidogo, lakini baadaye utaweza kwa kweli kuyaona matendo ya Mungu, na hatimaye utasema: “Matendo ya Mungu ni ya ajabu mno!” Haya ndiyo yatakuwa maneno moyoni mwako. Baada ya kupitia usafishaji wa Mungu kwa muda (majaribu ya watendaji huduma na wakati wa kuadibu), baadhi ya watu hatimaye walisema: “Kuamini katika Mungu ni jambo gumu kweli!” Ukweli kwamba wao hutumia maneno “jambo gumu kweli”, unaonyesha kwamba matendo ya Mungu ni yasiyoeleweka, kuwa kazi ya Mungu ni yenye umuhimu na thamani kubwa, na kwamba kazi Yake ni yenye kustahili sana kuthaminiwa na mwanadamu. Ikiwa, baada ya Mimi kufanya kazi nyingi hivi, hukuwa na maarifa hata kidogo, basi kazi Yangu ingeweza kuwa na thamani bado? Itakufanya useme: “Huduma kwa Mungu ni ngumu kweli, matendo ya Mungu ni ya ajabu mno, na Mungu kweli ni mwenye hekima! Mungu ni mwenye kupendeza kweli!” Kama, baada ya kupitia kipindi cha uzoefu, una uwezo wa kusema maneno kama haya, basi hii inathibitisha kuwa umepata kazi ya Mungu ndani yako. Siku moja, ukiwa unaeneza injili ughaibuni na mtu akuulize: “Imani yako katika Mungu inaendeleaje?” Utaweza kusema: “Matendo ya Mungu ni ya ajabu kweli!” Mtu huyo atahisi kwamba maneno yako yanazungumza kuhusu matukio halisi uliyopitia. Huku kweli ni kutoa ushahidi. Utasema kuwa kazi ya Mungu imejaa hekima, na kazi Yake ndani yako imekushawishi kwa kweli na kuushinda moyo wako. Wewe daima utampenda kwa maana Yeye anastahili zaidi upendo wa wanadamu! Kama unaweza kuzungumza kwa vitu hivi, basi unaweza kuigusa mioyo ya watu. Haya yote ni kutoa ushahidi. Kama unaweza kuwa shahidi wa ajabu, kuwagusa watu hadi watoe machozi, hiyo inaonyesha kwamba kwa kweli wewe ni mmoja anayempenda Mungu, kwa sababu unaweza kushuhudia kuhusu kumpenda Mungu, na kupitia kwako, matendo ya Mungu yanaweza kushuhudiwa. Kupitia ushuhuda wako, wengine wanafanywa watafute kazi ya Mungu, wapitie kazi ya Mungu, na katika mazingira yoyote wanayopitia, wataweza kusimama imara. Hii pekee ndiyo njia ya kweli ya kuwa shahidi, na hili hasa ndilo linalohitajika kutoka kwako sasa. Unafaa kuona kwamba kazi ya Mungu ni muhimu sana na inastahili kuthaminiwa na watu, kwamba Mungu ni wa thamani mno na mwenye Mengi, Hawezi tu kusema, lakini pia Anaweza kutoa uamuzi juu ya watu, kusafisha mioyo yao, kuwaletea starehe, kuwapata, kuwashinda, na kuwakamilisha. Kutoka katika kupitia kwako utaona kwamba Mungu ni mwenye kupendwa sana. Hivyo unampenda Mungu kiasi gani sasa? Je, unaweza kweli kusema mambo haya kutoka moyoni mwako? Wakati unaweza kuonyesha maneno haya kutoka kwenye kina cha moyo wako, basi utaweza kuwa na ushuhuda. Mara tu uzoefu wako unapofikia kiwango hiki utakuwa na uwezo wa kuwa shahidi wa Mungu, na utakuwa umestahili. Kama huwezi kufika kiwango hiki katika uzoefu wako, basi wewe bado utakuwa mbali sana. Ni jambo la kawaida kwa watu kuonyesha udhaifu katika mchakato wa usafishaji, lakini baada ya usafishaji unapaswa kuweza kusema: “Mungu ni mwenye hekima sana katika kazi Yake!” Kama wewe kweli unaweza kufikia ufahamu wa vitendo wa maneno haya, basi kitakuwa kitu unachokithamini, na uzoefu wako utakuwa wa thamani.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 512)
Je, ni nini unachopaswa kufuatilia sasa? Iwapo unaweza kushuhudia kazi ya Mungu au la, iwapo unaweza kuwa ushuhuda na udhihirisho wa Mungu au la, na iwapo unastahili kutumiwa na Yeye au la—hivi ndivyo vitu unavyopaswa kutafuta. Ni kiasi gani cha kazi ambacho Mungu hakika amefanya kwako? Ni kiasi gani ambacho umeona, ni kiasi gani ambacho umegusa? Umepitia kiasi gani, na kuonja kiasi gani? Bila kujali iwapo Mungu amekujaribu, kukushughulikia, au kukuadhibu, matendo Yake na kazi Yake vimetekelezwa juu yako. Lakini kama muumini katika Mungu na kama mtu ambaye ana nia ya kufuatilia kukamilishwa na Yeye, je, unaweza kushuhudia kazi ya Mungu kwa msingi wa uzoefu wako wa vitendo? Je, Je, unaweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu kupitia kwa uzoefu wako wa vitendo? Je, unaweza kuwakimu wengine kupitia uzoefu wako mwenyewe wa vitendo, na kutumia maisha yako yote kushuhudia kazi ya Mungu? Ili kushuhudia kazi ya Mungu, lazima utegemee uzoefu na maarifa yako, na gharama ambayo umelipa. Unaweza kuyaridhisha mapenzi Yake kwa njia hii pekee. Je, wewe ni mtu ambaye hushuhudia kazi ya Mungu? Je, una matamanio haya? Kama unaweza kulishuhudia jina Lake, na hata zaidi, kazi Yake, na kama unaweza kuishi kwa kudhihirisha sura ambayo Yeye anataka kutoka kwa watu Wake, basi wewe ni shahidi wa Mungu. Je, unashuhudia kwa ajili ya Mungu vipi kwa hakika? Unafanya hivyo kwa kutafuta na kuwa na hamu sana ya kuishi kwa kulidhihirisha neno la Mungu na, kwa kuwa na shahidi kwa maneno yako, kuwaruhusu watu wajue kazi Yake na kuona matendo Yake. Kama kweli unatafuta yote haya, basi Mungu atakukamilisha. Ikiwa yote unayotafuta ni kukamilishwa na Mungu na kubarikiwa mwishoni kabisa, basi mtazamo wa imani yako katika Mungu si safi. Unapaswa kuwa ukifuatilia jinsi ya kuona matendo ya Mungu katika maisha ya kweli, jinsi ya kumridhisha Yeye Anapokufichulia mapenzi Yake, na kutafuta jinsi unavyopaswa kushuhudia maajabu na hekima Yake, na jinsi ya kushuhudia jinsi Anavyokufundisha nidhamu na kukushughulikia. Haya yote ni mambo unayopaswa kuwa ukiyatafakari sasa. Kama upendo wako kwa Mungu ni ili tu uweze kushiriki katika utukufu wa Mungu baada ya Yeye kukukamilisha, basi bado hautoshi na hauwezi kukidhi mahitaji ya Mungu. Unahitaji kuwa na uwezo wa kushuhudia kazi ya Mungu, kutosheleza mahitaji Yake, na kuwa na uzoefu wa kazi ambayo Amefanya kwa watu kwa njia ya utendaji. Iwe ni uchungu, majonzi, au huzuni, lazima upitie vitu hivi vyote katika kutenda kwako. Vitu hivi vinanuiwa kukukamilisha kama Yule anayemshuhudia Mungu. Ni nini hasa kinachokushurutisha sasa kuteseka na kutafuta kukamilishwa? Je, mateso yako ya sasa kweli ni kwa ajili ya kumpenda Mungu na kumshuhudia? Ama ni kwa ajili ya Baraka za mwili na matarajio na kudura yako ya baadaye? Dhamira zako zote, nia, na malengo unayofuatilia lazima yarekebishwe na hayawezi kuongozwa na mapenzi yako mwenyewe. Kama mtu mmoja anatafuta ukamilifu ili apokee baraka na kutawala mamlakani, wakati mtu mwingine anafuatilia ukamilifu ili amridhishe Mungu, awe na ushuhuda wa vitendo wa kazi ya Mungu, je, ni ipi kati ya njia hizi mbili za ufuatiliaji ndiyo ungechagua? Ikiwa utachagua ya kwanza, basi utakuwa mbali sana na viwango vya Mungu. Nilisema wakati mmoja kwamba matendo Yangu yatajulikana wazi katika ulimwengu wote na kwamba Ningetawala kama Mfalme katika ulimwengu. Kwa upande mwingine, kilichoaminiwa kwenu ni kuenda kushuhudia kazi ya Mungu, sio kuwa wafalme na kuonekana ulimwenguni wote. Hebu matendo ya Mungu yajazee ulimwengu na anga. Hebu kila mtu ayaone na ayakiri. Maneno haya yanasemwa kuhusiana na Mungu Mwenyewe, na kile ambacho wanadamu wanapaswa kufanya ni kutoa ushuhuda kwa ajili ya Mungu. Je, unajua kiasi gani kuhusu Mungu sasa? Je, unaweza kutoa ushuhuda kwa Mungu kiasi gani? Je, ni lengo gani la Mungu kumkamilisha mwanadamu? Mara baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, je, unapaswa kuonyeshaje kujali kuelekea mapenzi Yake? Kama uko tayari kukamilishwa na uko tayari kushuhudia kazi ya Mungu kupitia kile unachoishi kwa kudhihirisha, kama una hii nguvu ya msukumo, basi hakuna lililo gumu sana. Wanachohitaji watu sasa ni imani. Kama una hii nguvu ya msukumo, basi ni rahisi kuachilia chochote chenye uhasi, cha kukaa tu, uvivu na mawazo ya mwili, falsafa za kuishi, tabia ya uasi, hisia, na mengineyo.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 513)
Wakati wanapitia majaribu, ni kawaida kwa watu kuwa dhaifu, au kuwa na uhasi ndani yao, au kukosa uwazi juu ya mapenzi ya Mungu au njia yao ya kutenda. Lakini katika hali yoyote, lazima uwe na imani katika kazi ya Mungu, na usimkane Mungu, kama tu Ayubu. Ingawa Ayubu alikuwa dhaifu na aliilaani siku yake ya kuzaliwa, yeye hakukana kwamba vitu vyote katika maisha ya binadamu vilikuwa vimetolewa na Yehova, na kwamba Yehova pia Ndiye anayeyachukua vyote. Haijalishi jinsi alivyojaribiwa, alidumisha imani hii. Katia kupitia kwako, haijalishi ni usafishaji gani unaopitia katika maneno ya Mungu, kile Mungu anahitaji kutoka kwa wanadamu kwa ufupi ni imani yao na upendo wao Kwake. Anachokamilisha kwa kufanya kazi kwa njia hii ni imani, upendo na matarajio ya watu. Mungu hufanya kazi ya ukamilisho kwa watu, nao hawawezi kuiona, hawawezi kuihisi; katika hali kama hizi imani yako inahitajika. Imani ya watu inahitajika wakati ambao kitu hakiwezi kuonekana kwa macho tu, na imani yako inahitajika wakati huwezi kuziachilia dhana zako mwenyewe. Wakati ambapo huna uwazi kuhusu kazi ya Mungu, kinachohitajika kutoka kwako ni kuwa na imani uchukue msimamo imara na kuwa shahidi. Wakati Ayubu alifikia hatua hii, Mungu alimwonekania na kuzungumza naye. Yaani, ni kutoka ndani ya imani yako tu ndipo utaweza kumwona Mungu, na wakati una imani Mungu atakukamilisha. Bila imani, Hawezi kufanya hivyo. Mungu ataweka juu yako chochote ulicho na matumaini ya kupata. Kama huna imani, basi huwezi kukamilishwa na hutakuwa na uwezo wa kuona matendo ya Mungu, sembuse kudura Yake. Wakati una imani kwamba utaona matendo Yake katika uzoefu wako wa utendaji, basi Mungu atakuonekania, na Atakupa nuru na kuongoza kutoka ndani. Bila hiyo imani, Mungu hataweza kufanya hivyo. Kama umepoteza matumaini katika Mungu, utawezaje kupata uzoefu wa kazi Yake? Kwa hiyo, ni wakati tu una imani na huweki mashaka kumhusu Mungu, ni wakati una imani ya kweli Kwake tu bila kujali Anachokifanya ndipo Atakuangazia na kukupa nuru kupitia katika mapito yako, na ni hapo tu ndipo utaweza kuona matendo Yake. Mambo haya yote yanafanikishwa kupitia kwa imani. Imani huja kupitia tu usafishaji, na wakati hakuna usafishaji, imani haiwezi kukua. Je, neno hili “imani”, linarejelea nini? Imani ni kusadiki kwa kweli na moyo wa dhati ambao wanadamu wanapaswa kumiliki wakati wao hawawezi kuona au kugusa kitu, wakati kazi ya Mungu haiambatani na za binadamu, wakati inazidi uwezo wa binadamu. Hii ndiyo imani Ninayozungumzia. Watu wanahitaji imani katika nyakati za shida na usafishaji, na imani ni kitu kinachofuatwa na usafishaji; usafishaji na imani haviwezi kutenganishwa. Haijalishi jinsi Mungu anavyofanya kazi, na haijalishi mazingira uliyomo, unaweza kufuatilia maisha na kutafuta ukweli, na kutafuta maarifa ya kazi ya Mungu, na kuwa na ufahamu wa matendo Yake, na unaweza kutenda kulingana na ukweli. Kufanya hivi ndiko kuwa na imani ya kweli, na kufanya hivyo kunaonyesha kwamba hujapoteza imani katika Mungu. Unaweza tu kuwa na imani ya kweli katika Mungu ikiwa bado unaweza kuendelea kufuatilia ukweli kupitia ukiwa katika usafishaji, ikiwa unaweza kumpenda Mungu kwa kweli na huna na mashaka kumhusu Yeye, ikiwa bila kujali Anachokifanya bado unatenda ukweli kumridhisha Yeye, na ikiwa unaweza kutafuta kwa dhati mapenzi Yake na ujali mapenzi Yake. Zamani, wakati Mungu alisema kwamba ungetawala kama mfalme, ulimpenda, na wakati Alijionyesha hadharani kwako, ulimfuata. Lakini sasa Mungu amejificha, huwezi kumwona, na shida zimekujia—je, hapo unapoteza matumaini kwa Mungu? Hivyo, lazima ufuatilie uzima wakati wote na kutafuta kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Hii inaitwa imani ya kweli, na huu ndio aina ya upendo ulio wa kweli na mzuri zaidi.
Hapo zamani, watu wote walikuja mbele za Mungu kufanya maazimio yao na walisema: “Hata kama hakuna mtu mwingine anayempenda Mungu, ni lazima mimi nimpende.” Lakini sasa, usafishaji unakujia, na kwa sababu hili halilingani na fikira zako, hivyo unapoteza imani katika Mungu. Je, huu ni upendo wa kweli? Umesoma mara nyingi kuhusu matendo ya Ayubu—Je, umesahau kuyahusu? Upendo wa kweli unaweza tu kukua kutoka ndani ya imani. Unakuza upendo wa kweli kwa Mungu kupitia katika usafishaji unaopitia, na ni kupitia kwa imani yako ndiyo unaweza kuyadhukuru mapenzi ya Mungu katika matukio yako ya vitendo, na pia ni kupitia kwa imani yako ndiyo unautelekeza mwili wako mwenyewe na kufuatilia uzima; hili ndilo watu wanapaswa kufanya. Ukifanya hivi, basi utaweza kuona matendo ya Mungu, lakini ukikosa imani, basi hutaweza kuona matendo ya Mungu au kuipitia kazi Yake. Iwapo unataka kutumika na kukamilishwa na Mungu, ni lazima umiliki kila kitu: uwe tayari kuteseka, imani, uvumilivu, utiifu na uwezo wa kupitia kazi ya Mungu, kufahamu mapenzi Yake kujali huzuni Yake, na kadhalika. Kumkamilisha mtu si rahisi, na kila kisa cha usafishaji unachopitia kinahitaji imani na upendo wako. Kama unataka kukamilishwa na Mungu, haitoshi kukimbia tu mbele kwenye njia, wala haitoshi kujitumia tu kwa ajili ya Mungu. Ni lazima umiliki mambo mengi ili uweze kuwa mtu ambaye anakamilishwa na Mungu. Unapokabiliwa na mateso ni lazima uweze kuweka kando masilahi ya mwili na usifanye malalamiko dhidi ya Mungu. Wakati Mungu anajificha kutoka kwako, ni lazima uweze kuwa na imani ya kumfuata Yeye, kudumisha upendo wako wa awali bila kuuruhusu ufifie au kutoweka. Haijalishi anachofanya Mungu, ni lazima utii mpango Wake na uwe tayari kuulaani mwili wako mwenyewe badala ya kulalamika dhidi Yake. Wakati unakabiliwa na majaribu, lazima umridhishe Mungu, ingawa unaweza kulia kwa uchungu au uhisi kusita kuhusu kuacha kitu unachopenda. Huu tu ndio upendo wa kweli na imani. Haijalishi kimo chako halisi ni kipi, ni lazima kwanza umiliki nia ya kupitia ugumu na imani ya kweli, na ni pia lazima uwe na nia ya kuutelekeza mwili. Unapaswa kuwa tayari kuvumilia ugumu wa kibinafasi na kupata hasara kwa maslahi yako binafsi ili kuridhisha mapenzi ya Mungu. Lazima pia uwe na uwezo wa kuhusi majuto kujihusu moyoni mwako: Hapo zamani, hukuweza kumridhisha Mungu, na sasa unaweza kujuta mwenyewe. Ni lazima usipungukiwe katika yoyote ya hali hizi—Ni kupitia katika vitu hivi ndiyo Mungu atakukamilisha. Usipoweza kufikia viwango hivi, basi huwezi kukamilishwa.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 514)
Mtu anayemtumikia Mungu lazima asijue jinsi ya kuteseka kwa ajili Yake; zaidi ya hayo, anapaswa kuelewa kwamba kusudi la kuamini katika Mungu ni kwa ajili ya kufuatilia kumpenda Mungu. Mungu hukutumia si kwa sababu tu ya kukusafisha au kwa sababu ya kukufanya uteseke, lakini badala yake ni Yeye hukutumia ili uweze kujua matendo Yake, kujua umuhimu halisi wa maisha ya binadamu, na hasa, ili uweze kujua kwamba kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Kupata uzoefu wa kazi ya Mungu hakuhusu kufurahia neema Yake, bali kuhusu kuteseka kwa sababu ya upendo wako Kwake. Kwa kuwa unafurahia neema ya Mungu, lazima pia ufurahie kuadibu Kwake; lazima upitie haya yote. Unaweza kupata uzoefu wa nuru ya Mungu ndani yako, na unaweza pia kupitia jinsi Anavyokushughulikia na Anavyokuhukumu. Kwa njia hii, uzoefu wako utakuwa mkamilifu. Mungu ametekeleza kazi Yake ya hukumu na kuadibu kwako. Neno la Mungu limekushughulikia, lakini si hilo yu; pia limekupa nuru, na kukuangazia. Wakati wewe ni hasi na dhaifu, Mungu ana wasiwasi kwa ajili yako. Hizi kazi zote ni za kukufahamisha kwamba kila kitu kuhusu mwanadamu kimo katika udhibiti wa Mungu. Unaweza kufikiri kwamba kuamini katika Mungu ni kuhusu mateso, au kumfanyia mambo ya kila aina; unaweza kufikiri kwamba sababu ya kumwamini Mungu ni ili mwili wako uwe na amani, au ili kwamba kila kitu maishani mwako kiende vizuri, au ili kwamba uweze kuwa na raha na utulivu katika kila kitu. Hata hivyo, hakuna kati ya haya ambayo watu wanapaswa kuhusisha na imani yao katika Mungu. Ukiamini kwa ajili ya sababu hizi, basi mtazamo wako si sahihi na haiwezekani kabisa wewe kukamilishwa. Matendo ya Mungu, tabia ya Mungu ya haki, hekima Yake, maneno Yake, na maajabu Yake na kutoeleweka kwa kina Kwake yote ni mambo ambayo watu wanapaswa kuelewa. Kuwa na ufahamu huu, unapaswa kuutumia kuondoa moyoni mwako madai, matumaini na fikiza za kibinafsi. Ni kwa kuondoa mambo haya tu ndiyo unaweza kukidhi masharti yanayotakiwa na Mungu, na ni kwa kufanua hivi tu ndiyo unaweza kuwa na uzima na kumridhisha Mungu. Kusudi la kumwamini Mungu ni ili kumridhisha na kuishi kwa kudhihirisha tabia ambayo Yeye anahitaji, ili matendo na utukufu Wake viweze kudhihirishwa kupitia kundi hili la watu wasiostahili. Huu ndio mtazamo sahihi wa kuamini katika Mungu, na hili pia ndilo lengo unalopaswa kutafuta. Unapaswa kuwa na mtazamo sahihi kuhusu kuamini katika Mungu na unapaswa kutafuta kupata maneno ya Mungu. Unahitaji kula na kunywa maneno ya Mungu na lazima uwe na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ukweli, na hasa lazima uweze kuona matendo Yake ya vitendo, matendo Yake ya ajabu kotekote katika ulimwengu mzima, pamoja na kazi ya vitendo Yeye hufanya katika mwili. Kupitia katika uzoefu wao wa vitendo, watu wanaweza kufahamu ni jinsi gani hasa Mungu hufanya kazi Yake kwao na mapenzi Yake kwao ni yapi. Kusudi la haya yote ni ili kuondoa tabia potovu ya kishetani ya watu. Baada ya kuondoa uchafu na udhalimu wote ulio ndani mwako, na baada ya kuondoa nia zako mbaya, na baada ya kukuza imani ya kweli kwa Mungu—ni kwa kuwa na imani ya kweli tu ndiyo unaweza kumpenda Mungu kweli. Unaweza tu kweli kumpenda Mungu kwa msingi wa imani yako Kwake. Je, unaweza kufanikisha upendo wa kweli kwa Mungu bila kumwamini? Kwa kuwa unaamini katika Mungu, huwezi kukanganyika kuhusu jambo hilo. Baadhi ya watu hujawa na nguvu mara tu wanapoona kwamba imani katika Mungu itawaletea baraka, lakini kisha hupoteza nguvu zote mara tu wanapoona kwamba wanafaa kupitia kusafishwa. Je, huko ni kuamini katika Mungu? Mwishowe, lazima upate utiifu kamili na mzima mbele ya Mungu katika imani yako. Unaamini katika Mungu lakini bado una madai Kwake, una mawazo mengi ya kidini ambayo huwezi kuyapuuza, maslahi ya kibinafsi huwezi kuacha, na bado unatafuta baraka za mwili na unataka Mungu auokoe mwili wako, kuiokoa nafsi yako—hizi zote ni tabia za watu walio na mtazamo usio sahihi. Hata kama watu wenye imani za kidini wana imani katika Mungu, hawatafuti kubadilisha tabia zao na hawafuatilii maarifa ya Mungu, lakini badala yake wanatafuta tu masilahi ya miili yao. Wengi kati yenu wana imani ambazo ni za kikundi cha kusadiki kidini; hii siyo imani ya kweli katika Mungu. Kuamini katika Mungu, watu lazima wamiliki moyo ulio tayari kuteseka kwa ajili Yake na radhi ya kujitoa wenyewe. Watu wasipokidhi haya masharti mawili, imani yao katika Mungu haihesabiki, na hawataweza kufanikisha mabadiliko katika tabia yao. Ni watu tu wanaotafuta ukweli kwa kweli, wanaotafuta maarifa ya Mungu, na kufuatilia maisha ndio wale ambao kweli wanaamini katika Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 515)
Kusudi la kazi ya usafishaji kimsingi ni ya kukamilisha imani ya watu. Mwishowe, kile kinachofanikishwa ni kwamba unataka kuondoka lakini, wakati huo huo, huwezi; baadhi ya watu bado wanaweza kuwa na imani hata wakati wanaondolewa hata chembe kidogo cha matumaini; na watu hawana tena tumaini kabisa kuhusu matarajio ya siku za zao za usoni. Ni katika wakati huu tu ndipo usafishaji wa Mungu utafikia kikomo. Mwanadamu bado hajafikia hatua ya kuelea kati ya maisha na kifo, na hajaonja mauti, hivyo mchakato wa usafishaji bado haujakamilika. Hata wale ambao walikuwa katika hatua ya watenda huduma hawakuwa wamesafishwa kabisa. Ayubu alipitia usafishaji mkali sana, na hakuwa na kitu cha kutegemea. Watu lazima wapitie usafishaji mpaka ile hatua ambayo hawana matumaini na kitu cha kutegemea—huu tu ndio usafishaji wa kweli. Wakati wa watenda huduma, ikiwa moyo wako daima ulikuwa umetulia mbele ya Mungu, na ikiwa pasipo kujali Alichofanya na pasipo kujali mapenzi Yake kwa ajili yako yalikuwa nini, wewe daima ulitii mipango Yake, basi mwishoni ungeelewa kila kitu ambacho Mungu alikuwa amefanya. Unapitia majaribu ya Ayubu, na wakati uo huo unapitiaa majaribu ya Petro. Wakati Ayubu alijaribiwa, yeye alikuwa shahidi, na mwishowe, Yehova alidhihirishwa kwake. Ni baada tu ya kuwa shahidi ndipo alistahili kuona uso wa Mungu. Kwa nini inasemwa: “Mimi najificha kutoka nchi ya uchafu lakini Najionyesha kwa ufalme mtakatifu”? Hiyo ina maana kwamba wakati tu uko mtakatifu na kuwa shahidi ndipo unaweza kuwa na hadhi ya kuuona uso wa Mungu. Kama huwezi kuwa shahidi kwa ajili Yake, hauna hadhi ya kuuona uso Wake. Ukijiondoa au kufanya malalamiko kwa Mungu ukikabiliwa na usafishaji, hivyo ushindwe kuwa shahidi Wake na uwe kichekesho cha Shetani, basi hutapata sura ya Mungu. Kama wewe ni kama Ayubu, ambaye katikati ya majaribu aliulaani mwili wake na wala hakulalamika dhidi ya Mungu, na aliweza kuuchukia mwili wake bila kulalamika au kutenda dhambi kwa njia ya maneno yake, basi utakuwa shahidi. Unapopitia usafishaji kwa kiasi fulani na bado unaweza kuwa kama Ayubu, mtiifu kabisa mbele ya Mungu na bila mahitaji mengine Kwake au dhana zako mwenyewe, basi Mungu atakuonekania. Sasa Mungu hakuonekanii kwa sababu una nyingi za dhana zako mwenyewe, maoni binafsi, mawazo ya ubinafsi, mahitaji ya binafsi na maslahi ya kimwili, na wewe hustahili kuuona uso Wake. Kama ungemwona Mungu, ungempima kupitia katika mawazo yako mwenyewe na, kwa kufanya hivyo, Angesulubishwa msalabani nawewe. Kama mambo mengi yanakuja kwako ambayo si sambamba na dhana zako lakini bado unaweza kuyaweka kando na kupata ufahamu wa matendo ya Mungu kutoka kwa mambo haya, na katikati ya usafishaji unadhihirisha moyo wako wa upendo kwa Mungu, basi huku ni kuwa shahidi. Kama nyumba yako ina amani, unafurahia starehe za mwili, hakuna mtu anayekutesa, na ndugu na dada zako katika kanisa wanakutii, je, unaweza kuonyesha moyo wako wa upendo kwa Mungu? Je, hali hii inaweza kukusafisha? Ni kwa kupitia katika usafishaji tu ndiyo upendo wako kwa Mungu unaweza kuonyeshwa, na ni kwa mambo yasiyo sambamba na fikira zako kutokea tu ndiyo unaweza kukamilishwa. Akitumia mambo mengi yasiyofaa na mabaya na kwa kutumia kila aina ya maonyesho ya Shetani—matendo yake, lawama yake, usumbufu wake na udanganyifu wake—Mungu hukuonyesha sura mbaya ya Shetani vizuri, na hivyo Anakamilisha uwezo wako wa kumbainisha Shetani, ili uweze kumchukua Shetani na uachane naye.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 516)
Uzoefu wako mwingi wa kushindwa, udhaifu, nyakati zako za uhasi, vyote vinaweza kusemekana kuwa majaribu ya Mungu. Hii ni kwa sababu kila kitu hutoka kwa Mungu, na mambo yote na matukio yako katika mikono Yake. Kama unashindwa au kama wewe ni dhaifu na unajikwaa, yote yako kwa Mungu na vipo katika mfumbato Wake. Kutoka kwa mtazamo wa Mungu, haya ni majaribu yako, na kama huwezi kutambua hivyo, yatageuka majaribu. Kuna aina mbili za hali ambazo watu wanapaswa kutambua: Moja inatoka kwa Roho Mtakatifu, na chanzo cha nyingine huenda ni Shetani. Moja ni hali ambamo Roho Mtakatifu anakuangazia na Anakuruhusu upate kujijua mwenyewe, kuchukia na kuhisi majuto kujihusu mwenyewe na kuweza kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu, kuweka moyo wako katika kumridhisha Yeye. Nyingine ni hali ambamo unajijua mwenyewe, lakini wewe ni hasi na dhaifu. Inaweza kusemwa pia kuwa hii ni hali ya usafishaji wa Mungu, na pia kuwa ni ushawishi wa Shetani. Ukitambua kuwa huu ni wokovu wa Mungu kwako na ukihisi kuwa wewe sasa ni mdeni Wake mkubwa, na kama kuanzia sasa utajaribu kulipa deni Lake na usianguke tena katika upotovu kama huo, kama utaweka juhudi katika kula na kunywa maneno Yake, na kama siku zote unajichukua kama anayekosa, na kuwa na moyo wa hamu, basi haya ni majaribu ya Mungu. Baada ya mateso kumalizika na wewe kwa mara nyingine tena unasonga mbele, Mungu bado atakuongoza, atakuangazia, atakupa nuru, na kukusitawisha. Lakini kama hulitambui na wewe ni hasi, kujiachilia tu kukata tamaa, kama unafikiri hivi, basi kishawishi cha Shetani kimekufikia. Wakati Ayubu alipitia majaribu, Mungu na Shetani walikuwa wanawekeana dau, na Mungu alimruhusu Shetani amtese Ayubu. Hata ingawa ilikuwa ni Mungu aliyekuwa anamjaribu Ayubu, hakika alikuwa ni Shetani ndiye aliyemjia. Kwa Shetani, ilikuwa ni kumjaribu Ayubu, lakini Ayubu alikuwa upande wa Mungu. Kama haingekuwa vile, basi Ayubu angeanguka katika kishawishi. Mara baada ya watu kuanguka katika kishawishi, wao huanguka katika hatari. Kupitia usafishaji inaweza kusemwa kuwa jaribu kutoka kwa Mungu, lakini kama hauko katika hali nzuri inaweza kusemwa kuwa kishawishi kutoka kwa Shetani. Kama hauko na uwazi juu ya maono, Shetani atakushutumu na kukuvuruga katiza mtazamo wa maono. Kabla ya kujua, utaanguka katika majaribu.
Kama hupitii kazi ya Mungu, basi kamwe hutaweza kufanywa mkamilifu. Katika uzoefu wako, lazima pia uingie katika maelezo. Kwa mfano, ni vitu vipi hukuongoza kukuza dhana na nia za kupita kiasi, na ni aina gani za matendo yanayofaa uliyo nayo kushughulikia matatizo haya? Kama unaweza kupitia kazi ya Mungu, hii ina maana kwamba una kimo. Kama unaonekana tu kuwa na nguvu, hiki si kimo halisi na hutaweza kusimama imara hata kidogo. Ni wakati tu unaweza kupitia kazi ya Mungu na uweze kuipitia na kuitafakari wakati wowote na mahali popote, wakati unaweza kuwaacha wachungaji na uishi peke yako ukimtegemea Mungu, na uweze kuona matendo halisi ya Mungu—ni hapo tu ndipo mapenzi ya Mungu yatatimizwa. Sasa hivi, watu wengi hawajui jinsi ya kupitia, na wanapokumbana na suala, hawajui jinsi ya kulishughulikia; hawawezi kuipitia kazi ya Mungu, na hawezi kuishi maisha ya kiroho. Lazima uchukue maneno ya Mungu na kuyafanya ndani ya maisha yako ya utendaji.
Wakati mwingine Mungu hukupa aina fulani ya hisia, hisia inayokusababisha upoteze starehe yako ya ndani kabisa, na unapoteza uwepo wa Mungu, kiasi kwamba unatumbukia gizani. Hii ni aina ya usafishaji. Wakati wowote unapofanya kitu chochote, hicho huenda mrama, au kugonga ukuta. Hii ni nidhamu ya Mungu. Wakati mwingine, unapofanya kitu ambacho si cha utiifu na cha uasi kwa Mungu, huenda hakuna mtu mwingine anajua kukihusu—lakini Mungu anajua. Yeye hatakuachilia, na Atakufundisha nidhamu. Kazi ya Roho Mtakatifu ni yenye kina sana. Kwa makini sana Anatazama kila neno na tendo la watu, kila tendo na mwendo wao, na kila wazo lao na fikira ili watu waweze kupata ufahamu wa ndani wa vitu hivi. Unafanya kitu mara moja na kinaenda mrama, unakifanya kitu tena na bado kinaenda mrama, na hatua kwa hatua utapata kuelewa kazi ya Roho Mtakatifu. Kupitia kufundishwa nidhamu mara nyingi, utajua cha kufanya ili kuwa sambamba na mapenzi ya Mungu na kile kisichoambatana na mapenzi Yake. Mwishowe, utakuwa na majibu sahihi kwa uongozi wa Roho Mtakatifu ndani yako. Wakati mwingine utakuwa muasi na utakemewa na Mungu kutoka ndani. Haya yote hutoka kwa nidhamu ya Mungu. Kama huthamini neno la Mungu, kama unaidharau kazi Yake, Hatashughulika na wewe hata kidogo. Kadiri unavyoyachukulia maneno ya Mungu kwa makini, ndivyo Atakavyokupa nuru zaidi. Sasa hivi, kuna baadhi ya watu katika kanisa ambao wana imani iliyovurugwa na yenye kuchanganyikiwa, na wao hufanya mambo mengi yasiyofaa na kutenda bila nidhamu, na hivyo kazi ya Roho Mtakatifu haiwezi kuonekana wazi ndani yao. Baadhi ya watu huacha nyuma wajibu wao kwa ajili ya kuchuma pesa, kwenda nje kuendesha biashara bila kuwa na nidhamu; mtu wa aina hiyo yuko katika hatari zaidi. Siyo tu kwamba sasa hawana kazi ya Roho Mtakatifu, lakini katika siku zijazo itakuwa vigumu kwa wao kukamilishwa. Kuna watu wengi ambao kwao kazi ya Roho Mtakatifu haiwezi kuonekana na ambao nidhamu ya Mungu haiwezi kuonekana kwao. Wao ni wale ambao hawako wazi juu ya mapenzi ya Mungu na ni wasiojua kazi Yake. Wale ambao wanaweza kusimama imara katikati ya usafishaji, wanaofuata Mungu bila kujali Anachofanya, na angalau wanaweza kusalia, au kutimiza 0.1% ya kile ambacho Petro alitimiza wanafanya vyema, lakini hawana thamani kuhusiana na Mungu kuwatumia. Watu wengi huelewa mambo haraka, wana upendo wa kweli kwa Mungu, na wanaweza kuzidi kiwango cha Petro, na Mungu huwafanyia kazi ya kukamilisha. Nidhamu na nuru huja kwa watu kama hawa, na iwapo kuna jambo ndani yao lisiloambatana na mapenzi ya Mungu, wanaweza kulitupilia mbali mara moja. Watu kama hawa ni dhahabu, fedha na vito—wana thamani ya juu kabisa! Kama Mungu amefanya aina nyingi za kazi lakini bado uko kama mchanga au jiwe, basi huna thamani!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 517)
Kazi ya Mungu katika nchi ya joka kubwa jekundu ni ya ajabu na isiyoeleweka. Yeye atalikamilisha kundi moja la watu na kuondoa wengine, kwani kuna kila aina ya watu kanisani—kuna wale wanaopenda ukweli, na wale wasiopenda; kuna wale wanaopitia kazi ya Mungu, na wale wasiopitia; kuna wale wanaofanya wajibu wao, na wale wasiofanya; kuna wale wanaomshuhudia Mungu, na wale wasiomshuhudia—na wengine wao ni wasioamini na watu waovu, na hakika wataondolewa. Kama hujui vizuri kazi ya Mungu, basi utakuwa hasi; hii ni kwa sababu kazi ya Mungu inaweza tu kuonekana katika watu wachache. Wakati huu, itakuwa wazi ni nani ambao wanampenda Mungu kwa kweli na wasiompenda. Wale ambao kweli wanampenda Mungu wana kazi ya Roho Mtakatifu, huku wale ambao hawampendi kwa kweli watafichuliwa kupitia kila hatua ya kazi Yake. Watakuwa walengwa wa kuondolewa. Watu hawa watafichuliwa katika kipindi cha kazi ya ushindi, na wao ni watu ambao hawana thamani ya kufanywa wakamilifu. Wale ambao wamekamilishwa wamepatwa na Mungu katika ukamilifu wao wote, na wana uwezo wa kumpenda Mungu kama vile alivyokuwa nao Petro. Wale ambao wameshindwa hawana upendo wa hiari, lakini wana upendo usioonyesha hisia, na wao wanalazimika kumpenda Mungu. Upendo wa hiari unakuzwa kwa njia ya uelewa uliopatikana kupitia uzoefu wa vitendo. Upendo huu unachukua moyo wa mtu na unamfanya kujitolea kwa Mungu kwa hiari; maneno ya Mungu yanakuwa msingi wao na wanaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu. Bila shaka haya ni mambo yanayomilikiwa na mtu ambaye amekamilishwa na Mungu. Kama unataka tu kushindwa, basi huwezi kuwa na ushuhuda kwa Mungu; kama Mungu angetimiza tu lengo Lake la wokovu kwa njia ya kuwashinda watu, basi hatua ya watenda huduma ingemaliza kazi. Hata hivyo, kuwashinda watu si lengo la mwisho la Mungu, ambalo ni kuwakamilisha watu. Hivyo badala ya kusema kwamba hatua hii ni kazi ni ya kuwashinda watu, sema kuwa ni kazi ya kukamilisha na kuondoa. Baadhi ya watu hawajashindwa kabisa, na katika harakati ya kuwashinda, kundi la watu watafanywa wakamilifu. Vipande hivi viwili vya kazi vinafanywa kwa pamoja. Watu hawajaondoka hata kwa muda mrefu sana kama huu wa kazi, na hili linaonyesha kuwa lengo la ushindi limekuwa na mafanikio—huu ni ukweli wa kushindwa. Usafishaji si kwa ajili ya kushindwa, lakini ni kwa ajili ya kukamilishwa. Bila usafishaji, watu hawangeweza kukamilishwa. Hivyo usafishaji kweli ni wa thamani! Leo kundi moja la watu linakamilishwa na kupatwa. Baraka kumi zilizotajwa hapo awali zote zililengwa kwa wale ambao wamekamilishwa. Kila kitu kuhusu kubadilisha sura zao duniani kunalenga wale ambao wamekamilishwa. Wale ambao hawajakamilishwa hawastahili kupokea ahadi za Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 518)
Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu. Ingawa ni uamuzi wa watu kama hawa kumfuata Mungu, hawafaidi chochote. Wale wote wasiopata chochote kwenye mkondo huu ndio watakaoondolewa—wao wote hawana kazi. Haijalishi ni hatua gani ya kazi ya Mungu unayopitia, lazima uandamane na maono makuu. Bila maono kama haya, itakuwa vigumu kwako kukubali kila hatua ya kazi mpya, kwa maana mwanadamu hana uwezo wa kuwaza kuhusu kazi mpya ya Mungu, ni kuu kushinda mawazo ya mwanadamu. Kwa hivyo bila mchungaji kumlinda mwanadamu, bila mchungaji kushirikiana na mwanadamu kuhusu maono hayo, mwanadamu hana uwezo kukubali kazi hii mpya. Iwapo mwanadamu hawezi kupokea maono haya, basi hawezi kupata kazi mpya ya Mungu, na iwapo mwanadamu hawezi kutii kazi mpya ya Mungu, basi mwanadamu hana uwezo wa kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na hivyo ufahamu wake wa Mungu ni bure. Kabla mwanadamu atimilize maneno ya Mungu, lazima ayajue maneno ya Mungu, hivyo ni kusema, aelewe mapenzi ya Mungu; ni kwa njia hii tu ndiyo maneno ya Mungu yanaweza kutekelezwa kwa usahihi na kulingana na moyo wa Mungu. Hili lazima liwe na kila mmoja anayetafuta ukweli, na ndiyo njia ambayo lazima kila mmoja anayejaribu kumjua Mungu aipitie. Njia ya kuyajua maneno ya Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na pia njia ya kuijua kazi ya Mungu. Na hivyo, kujua maono hakuashirii tu kuujua ubinadamu wa Mungu mwenye mwili, lakini pia kunajumuisha kujua maneno na kazi ya Mungu. Kutokana na maneno ya Mungu wanadamu wanapata kuelewa mapenzi ya Mungu, na kutokana na maneno ya Mungu wanapata kuelewa tabia ya Mungu na pia kujua kile Mungu alicho. Imani katika Mungu ndiyo hatua ya kwanza katika kumjua Mungu. Harakati ya kusonga kutoka katika imani ya mwanzo katika Mungu mpaka imani kuu kwa Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na harakati ya kuipitia kazi ya Mungu. Iwapo unaamini kwa Mungu kwa ajili tu ya kuamini kwa Mungu, na huamini kwa Mungu kwa ajili ya kumjua Mungu, basi hakuna ukweli katika imani yako, na haiwezi kuwa safi—kuhusu hili hakuna tashwishi. Iwapo, wakati wa harakati anapopata uzoefu wa kazi ya Mungu mwanadamu anapata kumjua Mungu polepole, basi hatua kwa hatua tabia yake itabadilika pia, na imani yake itaongezeka kuwa ya kweli zaidi. Kwa njia hii, wakati mwanadamu anafaulu katika imani yake kwa Mungu, ataweza kumpata Mungu kwa ukamilifu. Mungu alijitoa pakubwa kuingia katika mwili mara ya pili na kufanya kazi Yake binafsi ili mwanadamu apate kumjua Yeye, na ili mwanadamu aweze kumwona. Kumjua Mungu[a] ndiyo matokeo ya mwisho yanayofikiwa katika mwisho wa kazi ya Mungu; ndilo hitaji la mwisho la Mungu kwa mwanadamu. Anafanya hili kwa ajili ya ushuhuda Wake wa mwisho, na ili kwamba mwanadamu mwishowe na kwa kikamilifu aweze kumgeukia Yeye. Mwanadamu anaweza tu kumpenda Mungu kwa kumjua Mungu, na ili ampende Mungu lazima amjue Mungu. Haijalishi vile anavyotafuta, au kile anachotafuta kupata, lazima aweze kupata ufahamu wa Mungu. Ni kwa njia hii tu ndiyo mwanadamu anaweza kumridhisha Mungu. Ni kwa kumjua Mungu tu ndio mwanadamu anaweza kumwamini Mungu kwa ukweli, na ni kwa kumjua Mungu tu ndio anaweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Wale wasiomjua Mungu hawataweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Kumjua Mungu kunahusisha kujua tabia ya Mungu, kuelewa mapenzi ya Mungu, na kujua kile Mungu alicho. Na haijalishi ni kipengee gani cha kumjua Mungu, kila mojawapo kinamhitaji mwanadamu alipe gharama, na kinahitaji nia ya kutii, ambapo bila hivi hakuna atakayeweza kufuata mpaka mwisho. Kazi ya Mungu hailingani na mawazo ya mwanadamu hata kidogo, tabia ya Mungu na kile Mungu alicho ni vitu vigumu sana kwa mwanadamu kufahamu, na yote Anayosema na kufanya Mungu ni makuu sana yasiyoeleweka na mwanadamu; iwapo mwanadamu anatamani kumfuata Mungu, na hana nia ya kumtii Mungu, basi mwanadamu hatafaidi chochote. Tangu kuumbwa kwa dunia mpaka sasa, Mungu Amefanya kazi nyingi ambayo haieleweki na mwanadamu na ambayo mwanadamu amepata ugumu kuikubali, na Mungu amesema mengi yanayofanya mawazo ya mwanadamu magumu kupona. Ilhali Hajawahi kukomesha kazi Yake kwa sababu mwanadamu ana ugumu mwingi; Ameendelea kufanya kazi na kuzungumza, na hata ingawa idadi kubwa ya “wanajeshi” wameangamia njiani, Yeye bado Anaendelea na kazi Yake, na bado anateua kundi baada ya kundi la watu walio tayari kukubali kazi Yake mpya. Yeye hawahurumii wale “mashujaa” walioangamia, na badala yake anawathamini wale wanaoikubali kazi Yake mpya na maneno. Lakini ni kwa sababu gani ndiyo Anafanya kazi kwa njia hii, hatua kwa hatua? Ni kwa nini Yeye kila mara huwaondoa na kuchagua watu wengine? Ni kwa nini Yeye hutumia mbinu za aina hii kila mara? Kusudi la kazi Yake ni ile wanadamu wapate kumjua, na ili waweze kutwaliwa na Yeye. Kanuni ya kazi Yake ni kufanya kazi kwa wale wanaoweza kutii kazi Anayofanya leo, na sio kufanya kazi kwa wale wanaotii kazi Yake ya zamani, na wanaipinga kazi Yake ya leo. Hii ndiyo sababu hasa Amewafuta na kuwaangamiza watu wengi.
Matokeo ya funzo la kumjua Mungu haliwezi kufikiwa kwa siku moja au mbili: Mwanadamu lazima apate uzoefu wa matukio mengi, apitie mateso, na awe na utiifu wa kweli. Kwanza kabisa, anza na kazi na maneno ya Mungu. Lazima uelewe kumjua Mungu kunajumuisha nini, jinsi ya kupata maarifa kuhusu Mungu, na jinsi ya kumwona Mungu katika matukio yako. Hili ndilo kila mtu lazima afanye wakiwa bado hawajamjua Mungu. Hakuna anayeweza kushika kazi na maneno ya Mungu kwa mara moja, na hakuna anayeweza kupata maarifa ya ukamilifu wa Mungu kwa muda mfupi. Kinachohitajika ni harakati mahususi ya matukio, na bila haya hakuna mwanadamu atakayeweza kumjua au kumfuata Mungu kwa kweli. Mungu Anapofanya kazi zaidi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kumjua. Zaidi kazi ya Mungu inavyokinzana na mawazo ya mwanadamu, ndivyo ufahamu wa mwanadamu Kwake unavyofanywa upya na wenye kina kirefu. Iwapo kazi ya Mungu ingebaki milele bila kubadilika, basi mwanadamu angekuwa tu na ufahamu mdogo wa Mungu. Kati ya uumbaji na wakati wa sasa, vitu ambavyo Mungu alifanya wakati wa Enzi ya Sheria, Alichofanya wakati wa Enzi ya Neema, na kile Afanyacho wakati wa Enzi ya Ufalme: lazima ujue vizuri sana maono haya. Lazima mjue kazi ya Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu
Tanbihi:
a. Nakala ya kwanza inasema “Kazi ya kumjua Mungu.”
Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 519)
Mwanadamu hutambua kazi ya Mungu, hupata kujijua mwenyewe, hujitoa katika tabia yake potovu, na kutafuta kukua katika maisha yote kwa ajili ya kumjua Mungu. Ukitafuta kujijua mwenyewe tu na kujishughulisha tu na tabia yako potovu, na huna ufahamu ni kazi gani Mungu Anafanya kwa mwanadamu, kuhusu jinsi wokovu Wake ulivyo mkuu, au jinsi unavyojua kazi ya Mungu na kushuhudia matendo Yake, basi matukio yako hayana maana. Iwapo unafikiri kuwa kuweza kuuweka ukweli katika matendo, na kuwa na uwezo wa kuvumilia kunamaanisha maisha ya mtu yamekua, basi hii ina maana kuwa bado huelewi maana kamili ya Maisha au huelewi kusudi la Mungu la Kufanya kazi ya kumkamilisha mwanadamu. Siku moja, ukiwa katika makanisa ya kidini, miongoni mwa wanachama wa Kanisa la Toba au Kanisa la Uzima, utakutana na watu wengi wenye imani ambao maombi yao yana maono, na wanaohisi kuguzwa na walio na maneno ya kuwaongoza katika kuendelea kwao na maisha. Aidha, kwa mambo mengi wanaweza kuvumilia, na kujitelekeza wenyewe, bila kuongozwa na mwili. Wakati huo, hutaweza kujua tofauti: Utaamini kuwa kila wanachofanya ni sawa, kuwa ni udhihirisho wa kawaida wa maisha, lakini ni jambo la kusikitisha kweli kuwa jina wanaloamini si sahihi. Je imani kama hizi si pumbavu? Ni kwa nini inasemekana kuwa watu wengi hawana maisha? Ni kwa sababu hawamjui Mungu, na hivyo inasemekana kuwa hawana Mungu mioyoni mwao, na hawana uhai. Iwapo imani yako kwa Mungu imefikia kiwango fulani ambapo unaweza kwa kikamilifu kuyafahamu matendo ya Mungu, ukweli wa Mungu, na kila hatua ya kazi ya Mungu, basi umejawa na ukweli. Iwapo hujui kazi na tabia ya Mungu, basi uzoefu wako bado ni wa chini. Jinsi Yesu Aliifanya hatua ile ya kazi Yake, jinsi hatua hii inavyoendelezwa, jinsi Mungu Alifanya kazi Yake katika enzi ya Neema na ni kazi ipi iliyofanywa, ni kazi ipi inafanyika katika hatua hii—iwapo huna ufahamu kamilifu wa mambo haya, basi hutawahi kuondokewa na wasiwasi na utakuwa na shaka. Iwapo, baada ya kipindi cha uzoefu, wewe unaweza kujua kazi inayofanywa na Mungu na kila hatua ya kazi ya Mungu, na unao ufahamu mkuu wa malengo ya maneno ya Mungu, na ni kwa nini maneno mengi yaliyozungumzwa na Yeye hayajatimika bado, basi unaweza kutulia na kuendelea katika safari iliyo mbele yako, ukiwa huru kutokana na wasiwasi na kusafishwa. Mnapaswa kuona kile Mungu anatumia wingi wa kazi Yake. Yeye hutumia maneno Anayozungumza, akimsafisha mwanadamu na kuyabadilisha mawazo ya mwanadamu kupitia maneno mengi tofauti. Mateso yote ambayo mmestahimili, kusafishwa kote ambako mmepitia, kushughulikiwa ambako mmekukubali ndani yenu, kupata nuru ambako mmeona—yote yamefanikishwa kutumia maneno Aliyozungumza Mungu. Ni kwa sababu ya nini ndio mwanadamu anamfuata Mungu. Ni kwa sababu ya maneno ya Mungu! Maneno ya Mungu ni yenye mafumbo makuu, na yanaweza kuuguza moyo wa mwanadamu, kufunua vitu vilivyo ndani ya moyo wa mwanadamu, yanaweza kumfanya ajue vitu vilivyotendeka zamani, na kumruhusu kuona katika siku za usoni. Na kwa hivyo mwanadamu anavumilia mateso kwa sababu ya maneno ya Mungu, na anafanywa mkamilifu kwa sababu ya maneno ya Mungu, na ni baada ya hapo tu ndipo mwanadamu anamfuata Mungu. Anachostahili kufanya mwanadamu katika hatua hii ni kukubali maneno ya Mungu, na haijalishi kama amefanywa mkamilifu, au kusafishwa, kilicho cha muhimu ni maneno ya Mungu; hii ni kazi ya Mungu, na ni maono ambayo mwanadamu lazima ayajue leo hii.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu