Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Kuingia Katika Uzima (I)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 374)

Mwenyezi Mungu, Mkuu wa vitu vyote, hushika madaraka Yake ya kifalme kutoka kwa kiti Chake cha enzi. Yeye hutawala ulimwengu na vitu vyote Naye Anatuongoza katika dunia yote. Mara kwa mara tutakuwa karibu Naye, na kuja mbele Zake kwa utulivu; kamwe hatutakosa wakati mmoja, na kuna mambo ya kujifunza wakati wote. Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi. Usiwe na moyo wa kunung’unika, au Mungu hatatupa neema Yake juu yako. Wakati ugonjwa hutokea ni kwa sababu ya upendo wa Mungu, na nia Yake nzuri kwa hakika inaiunga mkono. Hata wakati mwili wako unavumilia mateso, usichukue ushauri kutoka kwa Shetani. Sifu Mungu katikati ya ugonjwa na furahia Mungu katikati ya sifa yako. Usikate tamaa unapokabiliwa na ugonjwa, endelea kutafuta na kamwe usisalimu amri, na Mungu Ataangaza nuru Yake kwako. Ayubu alikuwa mwaminifu kiasi gani? Mwenyezi Mungu ni daktari mwenye nguvu zote! Kukaa katika ugonjwa ni kuwa mgonjwa, lakini kukaa katika roho ni kuwa mzima. Kama unayo pumzi moja tu, Mungu hatakuacha ufariki.

Uzima wa Kristo Aliyefufuka uko ndani yetu. Kwa kweli tunakosa imani mbele ya Mungu, na hebu Mungu Atie imani ya kweli ndani yetu. Neno la Mungu ni tamu kweli! Neno la Mungu ni dawa yenye nguvu! Tilia aibu mapepo na Shetani! Kama sisi tutafahamu neno la Mungu tutakuwa na msaada na neno Lake litaokoa mioyo yetu kwa haraka! Linaondoa vitu vyote na kuweka yote kwa amani. Imani ni kama daraja moja la gogo la mti, wale ambao hushikilia maisha kwa unyonge watakuwa na ugumu katika kulivuka, lakini wale ambao wako tayari kujitolea wenyewe wanaweza kulivuka bila wasiwasi. Kama mtu ana mawazo ya uoga na ya kuogofya, wao wanadanganywa na Shetani. Ina hofu kwamba tutavuka daraja la imani ili kuingia katika Mungu. Shetani hubuni kila njia iwezekanayo kututumia mawazo yake, tunapaswa daima kuomba kwamba nuru ya Mungu itatuangazia sisi, na ni lazima daima tumtumainie Mungu kututakasa kutoka kwa sumu ya shetani. Daima tutakuwa tukitenda katika roho zetu kuja karibu na Mungu. Tutamruhusu Mungu kuwa na utawala juu ya asili yetu yote.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 6” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 375)

Kuinuka kwa mazingira pande zetu zote huharakisha kurudi nyuma kwetu katika roho. Usitende kwa moyo mgumu, usipuuze kwa vyovyote vile kama Roho Mtakatifu Ana wasiwasi, usijaribu kuwa mjanja na usiwe na ridhaa kupita kiasi na kuridhika kibinafsi au kuzingatia sana matatizo yako mwenyewe; kitu pekee cha kufanya ni kumwabudu Mungu katika roho na kweli. Huwezi kuyaacha maneno ya Mungu nyuma au kuyapa kisogo; lazima uyaelewe kwa makini, rudia kuomba-kusoma kwako, na uelewe maisha ndani ya maneno hayo. Usishiriki katika yale yasiyokuwa na maana kwa kuyabugia pasipo kujipa mwenyewe wakati wa kuyawaza. Je, unategemea maneno ya Mungu kwa kila kitu unachofanya? Usizungumze makubwa kama mtoto na kisha ukuwe katika mvurugo wakati wowote kitu chochote kinazuka. Lazima utumie roho yako kila saa ya kila siku, usipumzike hata kwa muda. Lazima uwe na roho yenye makali. Haidhuru unaweza kukabiliwa na nani au nini, ukikuja mbele ya Mungu utakuwa na njia ya kufuata. Lazima ule na kunywa maneno ya Mungu kila siku, uelewe maneno Yake bila kuwa na uzembe, ufanye juhudi zaidi, upate kabisa kila maelezo na kujiandaa mwenyewe na ukweli kamili ili kuepukana na kutoelewa mapenzi ya Mungu. Ni lazima upanue safu zako za uzoefu na ulenge kupitia maneno ya Mungu. Kupitia uzoefu utakuwa na uwezo wa kuwa yakini zaidi kuhusu Mungu; bila uzoefu, kusema u yakini juu Yake ni maneno tu tupu. Ni lazima tuwe wenye kuelewa haraka! Amka! Usiwe mlegevu tena; ukikabiliana na mambo kwa njia paruparu na wala hautajitahidi kwa maendeleo basi kwa kweli wewe ni kipofu. Ni lazima ulenge kazi ya Roho Mtakatifu, sikiza kwa makini sauti ya Roho Mtakatifu, fungua masikio yako kwa maneno ya Mungu, tunza muda uliobaki na ulipe gharama yoyote. Ukiwa na chuma cha pua, kitumie pahali kinafaa zaidi—kutengeneza chuma thabiti; shikilia mzuri wa ufunguo na ulenge kutenda maneno ya Mungu. Haidhuru jinsi unafanya nje vizuri baada ya kuyaacha maneno ya Mungu, yote ni bila mafanikio. Kutenda kwa maneno matupu haikubaliki kwa Mungu—mabadiliko lazima yaje kwa njia ya mwenendo wako, tabia, imani, ujasiri na utambuzi.

Wakati u karibu sana! Haidhuru mambo ya dunia ni mazuri kiasi kipi, ni lazima yote yaachwe kando. Matatizo mengi na hatari hayawezi kutuogofya sisi, wala anga kuanguka hakutatushinda kabisa. Bila aina hii ya azimio itakuwa ngumu tu sana kwako wewe kuwa mtu yeyote wa umuhimu. Wale ambao ni wadhaifu na ambao kwa uoga hushikilia maisha hawastahili kusimama mbele ya Mungu.

Mwenyezi Mungu ni Mungu wa vitendo. Haidhuru jinsi tu wapumbavu, Yeye bado Atatuonea huruma, mikono Yake hakika itatuokoa sisi na bado Atatufanya kamili. Mradi tuna moyo ambao kwa kweli unamtaka Mungu, mradi tumfuate karibu na wala tusikatishwe tamaa, na tutafute kwa hisia ya haraka, basi kwa hakika Hatachukulia yeyote kati yetu bila haki, kwa hakika Atatufidia sisi kile ambacho tuna ukosefu nacho na Yeye Ataturidhisha—yote hii ni wema wa Mwenyezi Mungu.

Kama mtu ni mlafi na mvivu, anaongoza maisha shibe, legevu na hajali chochote, yeye atapata kuwa ni vigumu kuepuka kupata hasara. Mwenyezi Mungu Hutawala mambo yote na matukio yote! Ili mradi mioyo yetu inamheshimu Yeye wakati wote na tuingie katika roho na kufanya ushirika na Yeye, basi Atatuonyesha mambo yote tunayotafuta na mapenzi Yake kwa hakika yatafichuliwa kwetu; mioyo yetu kisha yatakuwa katika furaha na amani, thabiti kwa uwazi kamili. Ni muhimu kuwa na uwezo wa kutenda kulingana na maneno Yake; kuwa na uwezo wa kuelewa mapenzi Yake na kuishi katika utegemezi wa maneno Yake—hii tu ndiyo kupitia kwa kweli.

Ni kwa kuelewa tu maneno ya Mungu ndipo ukweli wa maneno Yake utaweza kuingia ndani yetu na kuwa maisha yetu. Bila kupitia kwa vitendo vyovyote, unawezaje kuingia kwa uhalisi wa maneno ya Mungu? Kama huwezi kupata maneno ya Mungu kama maisha yako basi tabia yako haitaweza kubadilika.

Kazi ya Roho Mtakatifu sasa inaendelea kwa upesi sana! Kama haufuati kwa karibu na kupokea mafunzo, itakuwa vigumu kuwa sawa na kuendelea kwa kasi kwa Roho Mtakatifu. Harakisha na usababishe mabadiliko ya kimsingi usije ukakanyagwa chini ya miguu na Shetani na kuingia katika ziwa la moto wa jahanamu ambako hakuna kutoroka. Nenda tafuta kadri unavyoweza sasa ili usitelekezwe.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 7” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 376)

Nataka kukukumbusha kwamba huwezi kuwa na wasiwasi hata kidogo juu ya neno Langu na kutokujali kwa aina yoyote hakukubaliki. Unapaswa kulisikiliza na kulitii na kutenda mambo kulingana na nia Zangu. Daima lazima uwe macho na kamwe usiwe na tabia ambayo ni ya kiburi na ya kujidai, na lazima kila wakati unitegemee Mimi ili kutupilia mbali tabia ya zamani ya asili ambayo hukaa ndani yako. Unapaswa daima kuwa na uwezo wa kudumisha hali ya kawaida mbele Yangu, na uwe na tabia thabiti Kuwaza kwako lazima kuwe kwa busara na wazi na hakupaswi kuyumbishwa au kudhibitiwa na mtu yeyote, tukio, au kitu. Unapaswa kuwa mtulivu daima katika uwepo wangu na daima udumishe ukaribu wa kuendelea na kushiriki na Mimi. Utaonyesha ujasiri wa kipekee na kusimama imara katika ushahidi wako Kwangu. Simama na kuzungumza kwa ajili Yangu na usiogope kile ambacho watu wengine wanasema. Zingatia kukidhi nia Zangu na usidhibitiwe na wengine. Kile Ninachokufichulia lazima kifanywe kwa mujibu wa nia Zangu na hakiwezi kucheleweshwa. Je, unajihisi vipi ndani yako? Je! una wasiwasi? Utaelewa. Kwa nini huwezi kusimama kuzungumza kwa ajili yangu na kufikiria juu ya mzigo Wangu? Unaendelea kujihusisha na hila ndogo, lakini ninayaona yote kwa uwazi. Mimi ni msaada wako na kinga yako, na vyote viko mikononi Mwangu, hivyo unaogopa nini? Je, huko sio kuwa na mhemuko sana? Lazima utupilie kando hisia haraka sana; Sifikirii hisia na Ninatenda haki. Ikiwa haina faida kwa kanisa, basi mama yako na baba yako hawana upekee wowote! Nia Zangu zimefichuliwa kwako na hupaswi kuzipuuzia. Badala yake, lazima uweke uangalifu wako wote katika hayo na kutupa kila kitu kando ili kufuata kwa moyo wako wote. Mimi nitakuweka mikononi Mwangu siku zote. Usiwe mwoga na kudhibitiwa na mume au mke wako; utaruhusu mapenzi Yangu kufanywa.

Kuwa na imani! Kuwa na imani! Mimi ni mwenyezi wako. Hiki ni kitu ambacho unaweza ukakitambua kiasi, lakini bado unapaswa kutahadhari. Kwa ajili ya kanisa, mapenzi Yangu, na usimamizi Wangu, lazima ujitoe kikamilifu, na siri zote na miisho yote itaonyeshwa kwako. Hakutakuwa na uchelewaji zaidi na siku zitafikia mwisho. Kwa hiyo utafanya nini? Unawezaje kutafuta kuyafanya maisha yako yakomae kwa kasi zaidi? Je! Utafanyika mwenye manufaa Kwangu haraka kiasi gani? Utafanyaje ili mapenzi Yangu yatekelezwe? Ili kufanya hivyo kunahitaji kutafakari kikamili na ushirika wa kina zaidi na Mimi. Nitegemee Mimi, niamini Mimi, usiwe mzembe kamwe, na uweze kufanya mambo kulingana na mwongozo Wangu. Ukweli lazima utayarishwe vizuri na unapaswa kuula na kuunywa mara kwa mara zaidi. Kila ukweli lazima utekelezwe kabla ya kueleweka vizuri.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 9” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 377)

Haupaswi kuwa na hofu ya hili na lile. Haidhuru wingi wa matatizo na hatari unazokabili, utabaki thabiti mbele Yangu; usizuiliwe na kitu chochote, ili mapenzi Yangu yaweze kufanyika. Huu utakuwa ni wajibu wako, vinginevyo utakabiliana na ghadhabu Yangu na mkono wangu uta..., na utavumilia mateso ya akili yasio na mwisho. Ni lazima uyavumilie yote; kwa ajili Yangu, lazima uwe tayari kuviachilia vitu vyote unavyomiliki na kufanya kila kitu unachoweza kunifuata Mimi, na uwe tayari kutumia kila kitu chako.. Sasa ndio wakati ambao Nitakujaribu: Je, utanipa uaminifu wako? Je, unaweza kunifuata Mimi hadi mwisho wa barabara kwa uaminifu? Usiwe na hofu; kwa msaada Wangu, ni nani angeweza daima kuzuia barabara? Kumbuka hiki! Kumbuka! Kila kitu ambacho hutokea ni kwa kusudi Langu njema na yote yako chini ya uangalifu Wangu. Je, kila neno na tendo lako linaweza kufuata neno Langu? Wakati majaribio ya moto yatakuja juu yako, utapiga magoti na kuomba msaada? Au wewe utajikunyata, bila uwezo wa kusonga mbele?

Lazima uwe na ushujaa Wangu ndani yako na lazima uwe na kanuni wakati unakabiliana na ndugu wasioamini. Lakini kwa ajili Yangu, si lazima pia usikubali kushindwa na nguvu zozote za giza. Tegemea hekima Yangu ili kutembea kwa njia kamili; usiruhusu njama za Shetani kuchukua umiliki. Weka juhudi zako zote katika kuuweka moyo wako mbele Zangu, nami Nitakufariji na kukuletea amani na furaha. Usijitahidi kuwa namna fulani mbele ya watu wengine; Je, si kunifanya Mimi niridhike kuna thamani na uzito zaidi? Kwa kuniridhisha, si utajazwa na amani na furaha ya milele hata zaidi? Mateso yako ya sasa yanaonyesha jinsi baraka zako za baadaye zitakavyokuwa; ni zizisoelezeka. Wewe hujui ukubwa wa baraka ambazo utapata; huwezi hata kuziota. Leo zakuwa halisi, halisi kweli! Hii haiko mbali sana, unaweza kuiona? Kila chemba ya mwisho ya hii iko ndani Yangu na ni jinsi gani kuna ung’avu mbele! Futa machozi yako, na usihisi uchungu au huzuni tena. Vitu vyote vimepangwa na mikono Yangu, na lengo Langu ni kuwafanya ninyi muwe washindi na kuwaleta katika utukufu pamoja na Mimi. Kwa yote yanayokutendekea, unapaswa kushukuru sawasawa na uwe uliyejawa na sifa; hilo litanifanya Niridhike sana.

Maisha ya kuzidi uwezo wa binadamu ya Kristo tayari imeonekana; hakuna kitu chochote unachopaswa kuhofia. Mashetani wako chini ya miguu yetu, na wakati wao hautakuwepo kwa muda muda mrefu zaidi. Amka! Tupilia mbali ulimwengu wa uasherati; jinusuru mwenyewe kutoka dimbwi la kifo! Kuwa mwaminifu Kwangu bila kujali chochote, na usonge mbele kwa ujasiri; Mimi ni mwamba wako wa nguvu, kwa hivyo Nitegemee Mimi!

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 10” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 378)

Ikiwa una tabia ambayo si thabiti, nyepesi kuhamaki kama upepo au mvua, kama huwezi kuendelea kusonga mbele, basi fimbo Yangu haitakuwa mbali na wewe. Unaposhughulikiwa, kadiri hali ilivyo mbaya zaidi, na kadiri unavyoteswa zaidi, ndivyo upendo wako kwa Mungu unavyoongezeka, na unaacha kushikilia dunia. Bila njia nyingine, unakuja Kwangu, na unapata tena nguvu na imani yako. Ilhali, katika hali rahisi, ungeboronga. Ni lazima uingie ndani kwa mtazamo chanya, uwe mwenye vitendo na si baridi. Hutatingisika na yeyote na chochote katika hali yoyote, na huwezi kushawishiwa na maneno ya yeyote. Ni lazima uwe na tabia thabiti, na bila kujali kile watu wanachoweza kusema, utatenda kile unachojua kuwa ukweli mara moja. Lazima daima uwe na maneno Yangu yakifanya kazi ndani yako, bila kujali ni nani unayemkabili; lazima uweze kusimama imara katika ushuhuda wako Kwangu na ufikirie mizigo Yangu. Hupaswi kuchanganyikiwa, ukikubaliana na watu bila kufikiri na bila kuwa na mawazo yako mwenyewe, ila badala yake lazima uwe na ujasiri wa kusimama na kupinga vitu visivyotoka Kwangu. Ukijua kwa dhahiri kwamba jambo si sahihi, ilhali unyamaze, basi wewe si mtu anayetenda ukweli. Ukijua kwamba jambo si sahihi na kisha ugeuze mada, lakini Shetani azuie njia yako—unazungumza bila athari yoyote na huwezi kuvumilia hadi mwisho—basi bado unabeba woga moyoni mwako, na moyo wako bado haujazwi na fikira kutoka kwa Shetani?

Mshindi ni nini? Wanajeshi wazuri wa Kristo lazima wawe jasiri na kunitegemea kuwa wenye nguvu kiroho; lazima wapigane kuwa wapiganaji na wapambane na Shetani hadi kufa. Lazima daima ukae macho, na hii ndiyo maana Nakuomba ushirikiane kwa vitendo na Mimi kila wakati na kujifunza kuja karibu nami. Ikiwa katika wakati wowote na katika hali yoyote, unaweza kubaki kimya mbele Yangu, ukisikiza usemi Wangu na kuzingatia maneno Yangu na matendo, basi hutashawishiwa na kupoteza msimamo wako. Chochote unachopata kutoka ndani Yangu kinaweza kutendwa. Kila neno Langu linaelekezwa kwa hali yako. Yanachoma moyo wako, na hata ukiyakana na kinywa chako, huwezi kuyakana na moyo wako, na ukichunguza maneno Yangu, utahukumiwa. Kwa maneno mengine, maneno Yangu ni ukweli, uhai, njia; hayo ni upanga mkali, ukatao kuwili na yanaweza kumshinda Shetani. Wale wanaoelewa na wana njia ya kutenda maneno Yangu wamebarikiwa, na wale wasioyatenda watahukumiwa pasipo shaka; hili ni jambo la busara sana. Sasa, kadiri ya wale Ninaowahukumu imepanuka. Sitahukumu tu mbele Yangu wale wanaonijua, ila wale wasioniamini na wanaojaribu kadiri wawezavyo kupinga na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu pia watahukumiwa. Wale wote wanaofuata nyayo Zangu mbele Yangu wataona kwamba Mungu ni moto mkali sana! Mungu ni uadhama! Anafanya hukumu Yake, na kuwahukumu kifo. Wale walio kanisani wasiozingatia kufuata kazi ya Roho Mtakatifu, wanaoingilia kazi ya Roho Mtakatifu, wanaojionyesha, walio na nia na malengo yasiyo sahihi, wasioweka jitihada yao katika kula na kunywa maneno ya Mungu, waliokanganyikiwa na wenye shaka, wanaochunguza kazi ya Roho Mtakatifu—maneno ya hukumu yatawajia wakati wowote. Matendo yote ya watu yatafichuliwa. Roho Mtakatifu huchunguza vina vya mioyo ya watu, hivyo usiwe asiyejali; kuwa mwangalifu na utahadhari, usitende bila kufikiri wewe binafsi. Ikiwa matendo yako hayafuati maneno Yangu, basi utahukumiwa. Hakuna haja ya kuiga, ya kuwa mwenye kujifanya, au ya kutoelewa kweli; lazima uje mbele Yangu na kuwasiliana kwa karibu na Mimi mara nyingi.

Chochote utakachochukua kutoka ndani Yangu, kitakupa njia ya kutenda, na utaandamana na nguvu Zangu, utakuwa na uwepo Wangu, na daima utembee katika maneno Yangu, utazidi kila kitu duniani, na kuwa na nguvu ya ufufuo. Ikiwa maneno yako, tabia yako na matendo yako hayana maneno Yangu na uwepo Wangu, ukijitenga kutoka Kwangu na kuishi ndani yako, uishi katika dhana za akili, uishi katika mafundisho na amri, basi hiyo ni ithibati kwamba umeweka akili yako kwa dhambi. Kwa maneno mengine, unaendelea kushikilia nafsi yako nzee na huachi wengine wadhuru nafsi yako kidogo au kuharibu nafsi yako; mtu kama huyu ana ubora duni sana wa tabia na ni mpuuzi sana, na hawezi kuona neema ya Mungu au kutambua baraka za Mungu. Utaweza kuacha Nifanye kazi ndani yako lini ukiendelea kunikwepa! Wakati Nimemaliza kuzungumza, unasikiza lakini hukumbuki, na unakuwa mnyonge hasa shida zako zinapoonyeshwa kweli; hiki ni kimo cha aina gani! Ninaweza kukufanya uwe kamili lini ikiwa daima unahitaji kubembelezwa! Ikiwa unaogopa uvimbe na mikwaruzo, basi unapaswa kuharakisha kuwaonya wengine, “Sitamwacha yeyote anishughulikie, ninaweza kuondoa tabia yangu ya asili na nzee mimi mwenyewe.” Hivyo hakuna mtu atakukosoa au kukugusa, na uko huru kuamini njia yoyote unayotaka bila mtu yeyote kukujali. Je, unaweza kufuata nyayo Zangu hivi? Ni maneno matupu kusema kwamba una hakika kwamba mimi ni Mungu wako na Bwana wako. Ikiwa kweli huna shaka, mambo haya hayatakuwa shida, na utaamini kwamba ni upendo wa Mungu na baraka za Mungu juu yako. Ninapozungumza, ni kwa wana Wangu, na inapaswa kukabiliwa na shukrani na sifa.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 12” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 379)

Watu siku hizi hawawezi kukubali kujiachilia wenyewe, wao siku zote hufikiri kwamba wao ndio sahihi. Wao wamekwama katika dunia yao wenyewe ndogo na hawawi watu sahihi. Wakiendelea kusisitiza kuwa na lengo lisilo sahihi basi hakika watahukumiwa, na kama ni mbaya basi wataondolewa. Lazima uweke juhudi zaidi katika kuwa na ushirika wa kudumu na Mimi na si kuwa na ushirika tu na yeyote umtakaye. Lazima uwe na ufahamu wa watu ambao huwa na ushirika nao na ushirika kuhusu masuala ya kiroho katika maisha, ni hapo tu unapoweza kuruzuku maisha kwa wengine na kufidia mapungufu yao. Hupaswi kuchukua sauti ya kuhubiri nao, ambao kimsingi ni msimamo mbaya kuwa nao. Katika ushirika ni lazima uwe na ufahamu wa mambo ya kiroho. Lazima uwe na hekima na kuwa na uwezo wa kuelewa ni nini kilicho katika mioyo ya watu wengine. Lazima uwe mtu mwafaka kama utawatumikia wengine na lazima ufanye ushirika na kile ulicho nacho.

Jambo la muhimu sasa ni kwako wewe kuwa na uwezo wa kufanya ushirika Nami, kuwasiliana kwa karibu Nami, kula na kunywa peke yako, na kuwa karibu na Mungu. Lazima uelewe haraka mambo ya kiroho na kuwa na uwezo wa kuona kwa njia ya mazingira na mambo yaliyopangwa katika eneo lako. Je, unaweza kuelewa kile Nilicho? Ni muhimu kwamba ule na kunywa kutegemea na kile unachokosa, na kuishi kwa kutegemea neno Langu! Tambua mikono Yangu, na wala usilalamike. Ukifanya hivyo na kujitenga, unaweza kupoteza nafasi ya kupokea neema ya Mungu. Anza kwa kunikaribia Mimi: Je, unakosa nini, unapaswa kunikaribia Mimi na kuuelewa moyo Wangu vipi? Ni vigumu kwa watu kuja karibu na Mimi kwa sababu hawawezi kuiachilia nafsi. Tabia yao daima haiwiani, kuwa moto na kisha baridi, na wao wanajivuna na kuridhika na wao wenyewe wanapopata ladha kidogo ya utamu. Baadhi ya watu bado hawajaamka, ni kiasi gani cha unayoyasema kina kile ulicho? Ni kiasi gani cha hayo ambacho ni kujitetea mwenyewe, au kuiga wengine ama tu kufuata kanuni? Sababu ya wewe kutofahamu au kuelewa kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwa hujui jinsi ya kuwa karibu na Mimi. Kwa nje daima wewe hutafakari juu ya mambo, kutegemea dhana za nafsi na mawazo yako; wewe kwa siri hutafiti na kushiriki katika baadhi ya mipango midogo midogo, na huwezi hata kulileta hilo peupe. Hii inaonyesha kwamba kwa hakika huielewi kazi ya Roho Mtakatifu. Kama kwa hakika unaelewa kwamba jambo halitoki kwa Mungu, kwa nini usithubutu kusimama na kulikataa? Ni wangapi wangeweza kusimama na kuzungumza kwa ajili Yangu? Huonyeshi ujasiri wowote wa mtoto wa kiume.

Kila kitu ambacho kimepangwa sasa ni kwa lengo la kutoa mafunzo kwenu ili kwamba mkue katika maisha yenu, kuzifanya roho zenu ziwe na makali na zenye ncha, kuyafungua macho yenu ya kiroho na kuwafanya mtambue mambo yanayotoka kwa Mungu. Kitokacho kwa Mungu hukuwezesha kuhudumu kwa uwezo na mzigo na kuwa imara katika roho. Mambo ambayo hayatoki Kwangu yote ni matupu; hayakupi kitu, husababisha roho yako kuzama na kukufanya upoteze imani yako na kuweka umbali kati yako na Mimi, yakikufanya ufungiwe katika akili yako mwenyewe. Sasa unaweza kuvuka mipaka ya kila kitu katika ulimwengu wa kawaida unapoishi katika roho, lakini kuishi katika mawazo yako ni kuchukuliwa na Shetani na huu ni mwisho wa njia. Ni rahisi sana sasa: Nitegemee Mimi kwa moyo wako na roho yako mara moja itakuwa imara, utakuwa na njia ya kutenda na Mimi nitakuongoza katika kila hatua. Neno Langu litafichuliwa kwako wakati wote na katika maeneo yote. Bila kujali ni wapi au wakati upi, au mazingira yako ni mabaya namna gani, Mimi nitakuonyesha kwa uwazi na moyo Wangu kufichuliwa kwako ukinitegemea Mimi kwa moyo wako; kwa njia hii utaikimbilia barabara iliyo mbele bila kupoteza njia. Baadhi ya watu hujaribu kupapasa kwa nje, lakini kamwe hawafanyi hivyo kutoka ndani ya roho zao. Mara nyingi hawawezi kuifahamu kazi ya Roho Mtakatifu. Wanapofanya ushirika na watu wengine, wao huchanganyikiwa zaidi tu bila njia ya kufuata na hawajui cha kufanya. Mtu kama huyo hajui kinachomsumbua; anaweza kuwa na mambo mengi na anaweza kuonekana kwa ndani kama amekamilishwa, lakini hilo lina maana yoyote? Je, kweli una njia ya kufuata? Je, umeangaziwa na kunurishwa? Je, una umaizi wowote mpya? Je, umefanya maendeleo au umerudi nyuma? Je, unaweza kujiendeleza na mwanga mpya? Huna utii; utii unaousema mara nyingi si kitu ila maongezi tu. Umeishi kwa kudhihirisha maisha ya utiifu?

Kikwazo cha mtu kujidai, kuridhika, majisifu, na kiburi ni kikubwa jinsi gani? Ni nani wa kulaumiwa usipoweza kuingia katika uhalisi? Lazima ujichunguze mwenyewe kwa makini ili kuona kama wewe ni mtu sahihi. Je, malengo yako hufanywa Nami katika mawazo? Je, maneno na matendo yako husimama mbele Yangu? Mimi huchunguza fikira na mawazo yako yote. Je, si unajihisi mwenye hatia? Unajitwika sura ya bandia ili wengine waone na wewe kwa upole unajifanya kujidai; hili hufanyika ili ujikinge mwenyewe. Wewe hufanya hili ili kuyaficha maovu yako, na hata kutafuta njia za kuusukuma huo uovu kwa mtu mwingine. Ni hila gani hukaa ndani ya moyo wako! Fikiria kila kitu ambacho umesema; haikuwa kwa faida yako kwamba ulikuwa na hofu kwamba roho yako mwenyewe ingepata madhara na hivyo ukamsitiri Shetani na kisha kuwaibia ndugu zako ulaji na unywaji wao kwa nguvu? Una nini la kusema juu yako mwenyewe? Je, unafikiri kwamba wakati mwingine utaweza kulipia kula na kunywa huko ambako Shetani amechukua wakati huu? Hivyo unaona wazi sasa, hiki ni kitu ambacho unaweza kufidia? Je, unaweza kuufidia wakati uliopotea? Lazima kwa bidii mchunguze wenyewe kuona ni kwa nini hapakuwa na kula na kunywa katika mikutano michache iliyopita na ni akina nani ambao walisababisha shida hii. Lazima mfanye ushirika mmoja kwa mmoja mpaka iwe wazi. Watu kama hawa wasipozuiwa bila huruma, akina ndugu hawataelewa, na basi itakuja kutokea tena tu. Macho yenu ya kiroho hayajafunguliwa na wengi wenu sana ni vipofu! Na wale ambao huona ni wa kutojali kuhusu hilo. Hawasimami na kuongea, nao, pia, ni vipofu. Wale ambao huona lakini hawaongei ni mabubu. Kuna wengi hapa ambao wana upungufu.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 13” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 380)

Baadhi ya watu hawaelewi ukweli ni nini, ni nini maisha, njia ni nini, na wao hawaielewi roho. Wao huangalia neno langu kama fomyula tu, na hili ni gumu mno kubadilika. Hawaelewi shukrani ya kweli na sifa ni nini. Baadhi ya watu hawawezi kufahamu mambo muhimu na ya msingi, badala yake, wao hufahamu tu ya upili. Inamaanisha nini kudakiza usimamizi wa Mungu? Inamaanisha nini kubomoa jengo la kanisa? Inamaanisha nini kudakiza kazi ya Roho Mtakatifu? Kikaragosi wa Shetani ni nini? Ukweli huu lazima ueleweke wazi na sio tu kusitiriwa kwa mashaka. Ni kwa nini hakukuwa na kula na kunywa wakati huu? Baadhi ya watu wanaona kuwa wao wanapaswa kumsifu Mungu kwa sauti kubwa leo, lakini ni kwa jinsi gani wamsifu Yeye? Je, wanapaswa kuimba nyimbo na kucheza ngoma ili kumsifu Yeye? Je. njia nyingine hazihesabiki kama sifa? Baadhi ya watu huja kwa mikutano na dhana kwamba sifa za shangwe ndiyo njia ya kumsifu Mungu. Watu wana dhana hizi, na hawatilii maanani kazi ya Roho Mtakatifu, matokeo yake yakiwa kuwa bado kuna madakizo. Hakukuwa na kula na kunywa katika mkutano huu; wote wamesema kwamba wangeweza kuudhukuru mzigo wa Mungu na kutetea ushuhuda wa kanisa. Ni nani ambaye kweli amefikiri kwa makini kuhusu mzigo wa Mungu? Jiulize: Je, wewe ni mtu ambaye ameonyesha nadhari kwa mzigo wa Mungu? Je, unaweza kutenda haki kwa ajili ya Mungu? Je, unaweza kusimama na kuzungumza kwa ajili Yangu? Je, unaweza bila kusita kuweka ukweli katika vitendo? Je, wewe ni jasiri vya kutosha kupambana dhidi ya matendo yote ya Shetani? Je, unaweza kuwa na uwezo wa kuweka hisia zako kando na kufichua Shetani kwa sababu ya ukweli Wangu? Je, unaweza kuyaruhusu mapenzi Yangu yatimizwe ndani yako? Je, umejitolea moyo wako wakati muhimu unapowadia? Je, wewe ni mtu ambaye hufanya mapenzi Yangu? Jiulize na kufikiri juu yake mara kwa mara. Zawadi za shetani zimo ndani yako na wewe ni wa kulaumiwa kwa hayo kwa kuwa huwaelewi watu na umeshindwa kuitambua sumu ya Shetani; unajiongoza mwenyewe kwa kifo. Shetani amekudanganya kabisa kiasi kwamba umekanganyika kabisa; umelewa kwa divai ya uasherati na unayumba mbele na nyuma bila uwezo wa kushikilia maoni dhabiti na bila njia ya kutenda. Huli na kunywa vizuri, wewe hupigana na kugombana ovyo ovyo, hujui mema na mabaya na humfuata yeyote aongozaye—je, una ukweli wowote? Baadhi ya watu hujitetea hata kushiriki katika udanganyifu, wao hufanya ushirika na wengine lakini hilo huwaongoza hadi mwisho wa njia. Je, ni kutoka Kwangu ambapo watu hawa hupata nia zao, malengo, motisha, na chanzo? Je, unafikiri kuwa unaweza kufidia ndugu hawa kwa kula na kunywa kwao kulikochukuliwa? Tafuta watu wachache ili kufanya nao na kuwauliza, na uwaache wajizungumzie wenyewe: Je, wao wamepewa kitu chochote? Au wamekunywa na kuyajaza matumbo na maji machafu na kujawa na takataka na sasa hawana njia ya kufuata? Je, si hilo litabomoa kanisa? Upendo uko wapi kati ya ndugu? Kwa siri, wewe unatafiti ni nani aliye sahihi na asiye sahihi, lakini kwa nini huubebi mzigo kwa ajili ya kanisa? Kwa kawaida wewe hufanya vizuri katika kupiga ukelele wa misemo, lakini mambo yanapotokea katika hali halisi wewe ni una mashaka kuyahusu. Baadhi ya watu huelewa lakini hunung’unika tu kimya kimya wakati wengine huongea yale wanayoyaelewa lakini hakuna mtu mwingine husema neno. Wao hawajui kinachotoka kwa Mungu na ni nini kazi ya Shetani. Ziko wapi hisia zenu za ndani kuhusu maisha? Kabisa hamuifahamu kazi ya Roho Mtakatifu na hamuitambui kazi ya Roho Mtakatifu na ni vigumu kwenu kukubali mambo mapya. Nyinyi hukubali tu mambo ya kidini na ya kidunia, ambayo hupatana na dhana za watu. Kwa hivyo, nyinyi hupambana kitundu. Ni wangapi wanaweza kufahamu kazi ya Roho Mtakatifu? Ni wangapi ambao kwa hakika wamebeba mzigo kwa ajili ya kanisa Je, unaufahamu? Kuimba nyimbo ni njia moja ya kumsifu Mungu, lakini huelewi kwa dhahiri ukweli wa kumsifu Mungu na wewe ni mgumu katika njia unayoitumia kumsifu Yeye. Si hilo ni wazo lako mwenyewe? Daima wewe hushika dhana zako mwenyewe bila kuachilia na huwezi kuzingatia kile Roho Mtakatifu atakachofanya leo, usiweze kuhisi yale ndugu zako wanahisi, na kushindwa kutafuta mapenzi ya Mungu kwa njia ya utulivu. Wewe hufanya mambo kwa upofu na kuimba nyimbo vyema, lakini matokeo yake ni machafuko kamili. Je, hiyo kweli ni kula na kunywa? Je, unaona ni nani hasa anayesababisha madakizo? Kimsingi wewe huishi katika roho, lakini badala yake hushikilia dhana mbalimbali—Hiyo kwa vyovyote vile, inawezaje kuwa kulibebea kanisa mzigo? Lazima muone kwamba kazi ya Roho Mtakatifu inaendelea hata kwa kasi zaidi sasa, kwa hivyo si nyinyi mnakuwa vipofu kama mnashikilia kikiki dhana zenu wenyewe na kupinga kazi ya Roho Mtakatifu? Si hilo ni kama nzi kuruka akigonga kuta na kuvuma pote? Mkiendelea kwa njia hii mtatupwa kando.

Wale ambao wamefanywa kuwa kamili kabla ya maafa ni watiifu kwa Mungu. Wao huishi wakimtegemea Kristo, humshuhudia Kristo, na humtukuza Yeye. Wao ni watoto wa kiume waliofanikiwa na askari wema wa Kristo. Ni muhimu sasa kwamba ujitulize mwenyewe na kuja karibu na Mungu na kufanya ushirika Naye. Kama huwezi kuja karibu na Mungu, una hatari ya kutekwa na Shetani. Kama unaweza kuja karibu na Mimi na kufanya ushirika na Mimi, ukweli wote utafichuliwa kwako, na wewe utakuwa na kiwango cha kufuata kwa maisha yako na vitendo. Kwa sababu wewe ni mmoja ambaye yu karibu na Mimi, neno Langu kamwe halitaondoka kando yako, na hutapotea kutoka kwa neno Langu katika maisha yako; Shetani hatakuwa na njia ya kukudanganya, na badala yake ataona aibu na kutoroka kwa kushindwa. Ukitafuta nje kile kinachokosa ndani yako, kunaweza kuwa na nyakati ambapo unapata baadhi yacho, lakini sehemu kubwa yacho itakuwa sheria na kinaweza kuwa kitu usichohitaji. Lazima ujiachilie mwenyewe na ule na kunywa kutoka kwa neno Langu zaidi na ujue jinsi ya kulitafakari neno Langu. Kama huelewi kitu, njoo karibu Nami na kufanya ushirika na Mimi mara nyingi; kwa njia hii, kile utakachokielewa kitakuwa halisi na cha kweli. Lazima uanze kwa kuwa karibu Nami. Hili ni muhimu! Vinginevyo, hutajua jinsi ya kula na kunywa. Huwezi kula na kunywa wewe mwenyewe—kimo chako kweli ni kidogo mno.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 13” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 381)

Hapana muda wa kupoteza sasa. Roho Mtakatifu hutumia njia nyingi tofauti za kutuongoza katika maneno ya Mungu. Unapaswa kujitayarisha na ukweli wote, kutakaswa, kuwa na undani wa kweli na ushirikiano na Mimi; huruhusiwi nafasi yoyote ya kuchagua. Kazi ya Roho Mtakatifu haina hisia na haijali wewe ni mtu wa aina gani. Mradi tu wewe uko tayari kutafuta na kufuata—si kutoa visingizio, si kubishana juu ya mafanikio yako mwenyewe na hasara lakini kutafuta na njaa na kiu ya haki, basi Nitakupa nuru. Bila kujali jinsi ulivyo mpumbavu na mjinga, Mimi sioni vitu kama hivyo. Naangalia kuona jinsi unavyofanya kazi kwa bidii katika hali ya kujenga. Kama bado unashikilia dhana ya nafsi, kuzungusha duara katika dunia yako ndogo, basi Nafikiri uko katika hatari.… kuchukuliwa kuenda mbinguni ni nini? Inamaanisha nini kutelekezwa? Unapaswa kuishi vipi mbele ya Mungu leo? Unapaswa kushirikiana kikamilifu Nami vipi? Zitupilie mbali dhana zako mwenyewe, jichanganue mwenyewe, ivue barakoa yako, ona dhahiri ubainifu wa tabia yako halisi, jichukie mwenyewe, kuwa na moyo unaotafuta kwa njaa na kiu ya haki, amini kwamba wewe mwenyewe kwa kweli si kitu, kuwa tayari kujiachilia mwenyewe, kuwa na uwezo wa kuacha njia zako zote za kufanya mambo, jitulize mwenyewe mbele Yangu, yafanye maombi zaidi, jiegemeze Kwangu kwa unyofu, nitegemee Mimi, na usiache kuwa karibu na Mimi na kuwa na ushirika na Mimi—hili ni muhimu. Watu mara nyingi hujipata wamenaswa ndani ya nafsi zao wenyewe na hawako mbele ya Mungu.

Kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu kwa kweli ni ngumu kwa watu kuwaza na yote huingia katika uhalisi; kwa kweli haitakufaa kuwa mzembe. Kama moyo wako na mawazo si sahihi, basi hutakuwa na njia. Kutoka mwanzo hadi mwisho ni lazima uwe macho wakati wote na kuhakikisha kuwa umejikinga dhidi ya uzembe. Heri wale ambao daima huwa macho na kusubiri na ambao wako kimya mbele Yangu! Heri wale ambao daima hunitegemea Mimi kwa mioyo yao, ambao huhakikisha wameisikiliza kwa karibu sauti Yangu, ambao huzingatia matendo Yangu na ambao huweka maneno Yangu katika matendo! Wakati kweli hauwezi kuvumilia taahira. Mabaa ya kila namna yataenea, yakifungua midomo yao mikali, yenye damu kuwala nyinyi nyote kama mafuriko. Wanangu! Wakati umefika! Hakuna nafasi zaidi ya kuwaza. Njia pekee itakayowaleta chini ya ulinzi Wangu ni kurudi Kwangu. Ni lazima muwe na nguvu ya tabia ya mwana wa kiume, msiwe wadhaifu au kuvunjika moyo; lazima mfuate unyounyo hatua Zangu, msikatae mwanga mpya na, kwa kuwaambia jinsi ya kula na kunywa, mnapaswa mtii na kula na kunywa vizuri. Je, bado kuna wakati sasa wa kupigana au kushindana na kila mmoja kiholela? Je, mnaweza kufanya vita kama hamli na kushiba na hamjatayarishwa kikamilifu na ukweli? Kama mnataka kuishinda dini, ni lazima mjitayarishe kikamilifu na ukweli. Kuleni na kunywa maneno Yangu zaidi na kutafakari juu ya maneno Yangu zaidi. Lazima mle na kunywa maneno Yangu kwa kujitegemea na kuanza kwa kujongea karibu na Mungu. Acha hili liwe ni onyo kwenu! Lazima mtie maanani! Wale ambao ni werevu lazima kwa haraka wauelewe ukweli! Achilia mambo yote ambayo huna nia ya kuyaacha. Nakwambia kwa mara nyingine tena kwamba mambo haya kwa kweli ni hatari kwa maisha yako na yasiyokuwa na manufaa! Natumaini unaweza kunitegemea Mimi katika matendo yako, vinginevyo njia tu iliyo mbele itakuwa njia ya kifo, na ni wapi basi utakakokwenda kutafuta njia ya maisha? Uondoe moyo wako ambao unapenda kujishughulisha na mambo ya nje! Uondoe moyo wako ambao huwakaidi watu wengine! Kama maisha yako hayawezi kukomaa na umetelekezwa, si wewe basi utakuwa ndiye ambaye amejikwaa mwenyewe? Kazi ya Roho Mtakatifu sasa si kama wewe unavyofikiria. Kama huwezi kuziachilia dhana zako basi utapata hasara kubwa. Kama kazi ingekuwa ni kwa kuambatana na dhana za mtu, je, asili yako ya zamani na dhana zingeweza kufichuka? Je, ungeweza kuwa na uwezo wa kujijua mwenyewe? Labda bado unadhani kuwa huna dhana, lakini wakati huu bado pande zako zote mbalimbali mbaya zitafichuka. Kwa makini jiulize:

Je, wewe ni mtu ambaye hunitii Mimi?

Je, una hiari na tayari kuiachilia nafsi yako na unifuate Mimi?

Je, wewe ni mtu ambaye huutafuta uso Wangu kwa moyo safi?

Je, unajua jinsi ya kujongea karibu na Mimi na kufanya ushirika nami?

Je, unaweza kujituliza mbele Yangu na kutafuta mapenzi Yangu?

Je, wewe huweka katika vitendo maneno ambayo Mimi hukufichulia?

Je, unaweza kudumisha hali ya kawaida mbele Yangu?

Je, una uwezo wa kuona undani wa mipango ya hila ya Shetani? Je, wewe unathubutu kuifichua?

Ni jinsi gani unafanya busara kuhusu mzigo wa Mungu?

Je, wewe ni mtu ambaye hufanya busara kwa mzigo wa Mungu?

Je, wewe huielewaje kazi ya Roho Mtakatifu?

Je, ni jinsi gani wewe huhudumu kwa uratibu katika familia ya Mungu?

Je, wewe huwa na ushuhuda wa nguvu kwa ajili Yangu?

Je, wewe kupiganaje vita vizuri kwa ajili ya ukweli?

Lazima uchukue muda wa kutafakari ukweli huu kabisa. Ukweli ni wa kutosha kuthibitisha kuwa siku i karibu sana. Ni lazima ufanywe mkamilifu kabla ya maafa—hili ni suala la umuhimu mkubwa ambalo lazima litatuliwe haraka! Nataka kuwafanya wakamilifu, lakini Naona kwamba nyinyi kweli kwa kiasi fulani hamjadhibitiwa. Mna ushupavu lakini hamuuweki kwa matumizi bora na bado hamjaelewa mambo yaliyo muhimu zaidi, badala yake yote mnayoelewa ni mambo madogo. Kuna faida gani katika kujadili juu ya mambo haya? Je, si huku ni kupoteza wakati? Mimi huwaonyesha wema kwa njia hii lakini mnashindwa kuonyesha shukrani yoyote na nyinyi hupigana tu miongoni mwenu, hivyo si juhudi Zangu zote zimekuwa bure? Kama mtaendelea kwa njia hii, Sitachukua wakati kuwashawishi muendelee! Nawaambia, isipokuwa mzinduke kwa ukweli, kazi ya Roho Mtakatifu itaondolewa kutoka kwenu! Hamtapewa cha kula zaidi tena, na mnaweza kuamini kama mnavyoona inafaa. Maneno Yangu yamesemwa kwa kirefu; msikilize au la, ni juu yenu. Wakati utakapofika mnapokuwa mmechanganyikiwa na hakuna njia ya kwenda mbele na hamuwezi kuona mwanga wa kweli, mtanilaumu Mimi? Ujinga ulioje! Matokeo yanapaswa kuwa yapi iwapo utajigandamia kikiki na kukataa kujiachilia? Si kazi yenu itakuwa ilikuwa zoezi la bure? Ni sikitiko lililoje kutupwa kando wakati janga linapokumba!

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 382)

Kanisa linajengwa na Shetani anajaribu kwa uwezo wake kulibomoa. Anataka kubomoa ujenzi Wangu kwa njia yoyote iwezekanayo, kwa hivyo, lazima kanisa litakaswe kwa haraka. Lazima kusiwe na makapi au mabaki yoyote maovu; lazima litakaswe ili lisiwe na dosari na libaki takatifu kama awali. Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi. Lazima mtambue mipango ya njama na hila mbalimbali za Shetani, mjue roho, mjue watu na mweze kupambanua watu wa aina zote, masuala na mambo; lazima mle na mnywe maneno Yangu zaidi na, muhimu zaidi, lazima mweze kuyala na kuyanywa nyinyi wenyewe. Jiandaeni wenyewe na ukweli wote, njooni mbele Yangu ili nifungue macho yenu ya kiroho na kuwaruhusu kuona siri zote zilizo rohoni…. Wakati kanisa linaingia awamu yake ya ujenzi, vita vya watakatifu dhidi ya Shetani[a] vinaanza. Vipengele mbalimbali vya Shetani vya kutisha Vinawekwa mbele yenu; je, mnaacha na kurudi nyuma au mnainuka na kuendelea mkinitegemea Mimi? Weka hadharani vipengele vya Shetani vyenye upotovu na viovu, bila hisia wala huruma! Pambana na Shetani hadi kifo! Mimi ni msaada wenu na ni lazima muwe na roho ya mwana wa kiume! Shetani yuko katika hekaheka zake za kifo cha mwisho lakini bado hataweza kuhepa hukumu Yangu. Shetani yuko chini ya miguu Yangu na pia anakanyagwa chini ya miguu yenu—ni ukweli!

Wale wapinga dini wote na wale ambao hubomoa ujenzi wa kanisa hawafai kuvumiliwa hata kidogo na nitawahukumu mara moja. Weka Shetani hadharani, mkanyagie chini ya miguu, muangamize kabisa na usimuachie pa kujificha. Kila aina ya mapepo na vizuka hakika wataonyesha maumbile yao ya kweli mbele Yangu na Nitawatupa wote kuzimu ambamo hawatawahi kuwa huru; wote wako chini ya miguu yetu. Kama unataka kupigana vita vizuri kwa ajili ya ukweli, basi kwanza kabisa, usimpe Shetani nafasi ya kufanya kazi, na ili kufanya hivi mtastahili kuwa na nia moja na muweze kutumika katika kushirikiana, acheni dhana zenu za kibinafsi, maoni, mitazamo na njia za kufanya mambo, tuliza moyo wako ndani Yangu, zingatia sauti ya Roho Mtakatifu, kuwa makini na kazi ya Roho Mtakatifu na uwe na uzoefu wa maneno ya Mungu kwa kina. Lazima uwe na nia moja tu, ambayo ni kwamba mapenzi Yangu yaweze kutendeka. Hupaswi kuwa na nia nyingine. Lazima uangalie Kwangu kwa moyo wako wote, angalia hatua Zangu na Ninavyotenda mambo kwa karibu, na wala usiwe mzembe kabisa. Roho yako lazima iwe amilifu, macho yako yakiwa wazi. Kwa kawaida, wale ambao nia na malengo yao si sahihi, wale ambao wanapenda kuonekana na wengine, wenye hamu ya kutenda mambo, wenye tabia ya kukatiza, walio imara katika mafundisho ya dini, watumishi wa Shetani, nk., watu hawa wanapoinuka wanakuwa ugumu kwa kanisa na kula na kunywa kwa ndugu kunakuwa si kitu; unapompata mtu wa aina hii jifanye kisha mpige marufuku mara moja. Kama muda baada ya muda hawabadiliki basi watateseka sana. Kama wale wanaoendelea katika njia zao kwa ukaidi wanajitetea na kujaribu kufunika dhambi zao, kanisa linapaswa kuwaondoa mara moja na kutowaachia nafasi ya kuendelea. Usipoteze mengi kwa kujaribu kuokoa machache, na uzingatie makubwa.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 17” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

a. Makala ya asili hayana neno “dhidi ya Shetani.”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 383)

Kazi ya Roho Mtakatifu inapoendelea mbele, Mungu kwa mara nyingine tena ametuingiza katika mbinu mpya ya kazi ya Roho Mtakatifu. Matokeo yake, haiepukiki kwamba baadhi ya watu wamenielewa Mimi vibaya na kufanya malalamiko Kwangu. Wengine wamenipinga na kunikataa Mimi, na wamenichunguza Mimi. Hata hivyo, bado Mimi ninasubiri kwa rehema toba yenu na mageuzi. Mabadiliko katika utaratibu wa kazi ya Roho Mtakatifu ni Mungu Mwenyewe kuonekana hadharani. Neno Langu litabaki bila kubadilika! Kwa kuwa ni wewe ninayemwokoa, Mimi sitakutelekeza katikati ya safari. Lakini kuna shaka ndani yenu na nyinyi mnataka kurejea mikono mitupu. Baadhi yenu mmeacha kusonga mbele ilhali wengine wanachunguza na kusubiri. Bado wengine wanashughulika na hali hiyo bila kufanya chochote, huku wengine wanafanya tu uigaji. Nyinyi kwa kweli mmeifanya mioyo yenu kuwa migumu! Mmekichukua nilichokisema Mimi kwenu na kukigeuza kuwa majisifu yenu na majivuno. Tafakarini hili zaidi: Haya ni maneno ya huruma na hukumu tu yanayowashukia. Roho Mtakatifu, anapoona kwamba ninyi kwa kweli ni waasi, moja kwa moja anaanza kunena na kuchambua. Lazima muwe na hofu. Msitende mambo kwa kutojali au kufanya lolote kwa pupa. Msiwe bure, wenye kiburi, au kusisitiza kuwa na njia zenu wenyewe! Inawapasa mzingatie zaidi juu ya kuweka neno Langu katika vitendo, na uishi kwa kuyadhihirisha kokote uendako ili yaweze kukubadilisha kwa kweli kutoka ndani na ili uweze kuwa na tabia Yangu. Ni matokeo kama haya tu ndiyo ya kweli.

Kwa minajili ya kanisa kuweza kujengwa, ni lazima uwe wa kimo fulani, na utafute kwa moyo wote na bila kukoma, pamoja na kupokea mchomo na utakaso wa Roho Mtakatifu na kuwa mtu aliyebadilishwa. Ni katika hali kama hiyo ambapo kanisa linaweza kujengwa. Kazi ya Roho Mtakatifu sasa imewaongozwa nyinyi kuanzisha ujenzi wa kanisa. Kama mkiendelea kutenda mambo kwa njia ilele ya kuchanganyikiwa na uzima kama mlivyofanya zamani, basi hamna matumaini. Lazima mjitayarishe wenyewe na ukweli wote na kuwa na utambuzi wa kiroho, na kutembea njia iliyo kamili kulingana na hekima Yangu. Kwa kanisa kujengwa, ni lazima muwe katika maisha ya roho na siyo tu kuiga kwa juujuu. Maendeleo ya ukuaji katika maisha yenu ni maendeleo sawa na yale ambayo kwayo mmejengwa. Hata hivyo, kumbuka kwamba wale ambao hutegemea vipawa vya kiroho au wale ambao hawawezi kuelewa mambo ya kiroho ama wanakosa hali ya utendaji hawawezi kujengwa, wala wale ambao hawawezi kunikaribia na kuwasiliana na Mimi wakati wote. Wale ambao huyashughulisha mawazo yao na dhana za binadamu au kuishi kwa kufuata mafundisho ya kidini hawawezi kujengwa, na wale ambao huongozwa na hisia zao hawawezi pia. Bila kujali jinsi Mungu anavyokutendea, ni lazima ujiweke chini Yake kabisa. Vinginevyo, huwezi kujengwa. Wale ambao wanajishughulisha na majivuno, kujidai, kiburi, hali ya kuridhika na wanaopenda kujishusha hadhi na kuringa hawawezi kujengwa. Wale ambao hawawezi kuhudumu kwa uratibu na wengine hawawezi kujengwa. Wale wasio na utambuzi wa kiroho, au kwa upofu hufuata yeyote anayeongoza hawawezi kujengwa, na wale ambao hushindwa kuelewa nia Yangu na ambao huishi katika hali ya zamani hawawezi kujengwa. Wale ambao ni wapole mno kufuata mwanga mpya na hawana maono yoyote kama msingi hawawezi kujengwa.

Kanisa linapaswa kujengwa bila kuchelewa, na Mimi nina hangaiko la kusisitiza kwalo. Unapaswa kuanza kwa kuzingatia uhalisi, na kujiunga na mkondo wa ujenzi kwa kujitoa mwenyewe na nguvu yako yote. Vinginevyo, utakataliwa. Ni lazima ukitelekeze kabisa cha kutelekezwa, na kula na kunywa vizuri kistahilicho kuliwa na kunywewa. Ni lazima uishi kwa kudhihirisha uhalisi wa neno Langu, na hupaswi kuzingatia mambo ya juu juu na yasiyo na mpango. Jiulize, ni kiasi gani umechukua katika neno Langu? Ni kiasi kipi wewe huishi kwa kudhihirisha neno Langu? Ni lazima uwe macho na uache kufanya chochote kwa pupa. Vinginevyo, kitakudhuru tu, siyo kusaidia ukuaji wako mwenyewe katika maisha. Ni lazima uelewe ukweli, ujue jinsi ya kuuweka katika vitendo, na uruhusu neno Langu liwe maisha yako kwa ukweli. Huu ndio ukweli wa jambo!

Kwa kuwa ujenzi wa kanisa sasa umefikia wakati muhimu sana, Shetani anapanga mipango na kufanya juu chini kulibomoa. Hampaswi kuwa wavivu lakini endeleeni kwa uangalifu na mfanye utambuzi katika roho. Bila utambuzi kama huo, mtapatwa na hasara kubwa. Hili si jambo dogo. Ni lazima mlifikirie kama suala la umuhimu. Shetani ana uwezo wa kuonekana kwa uongo na kueneza mifano ambayo hubeba tofauti kubwa ya ubora wa yaliyomo. Watu hutenda mambo kipumbavu na kizembe, na wanakosa utambuzi, ambayo ina maana kwamba nyinyi hamuwezi kuwa macho na shwari wakati wote. Mioyo yenu haipatikani popote. Huduma ni heshima na kadhalika hasara. Inaweza kusababisha baraka au balaa. Salia mtulivu mbele Yangu na kuishi kwa mujibu wa neno Langu, na kwa hakika utasalia macho na kutumia utambuzi katika roho. Shetani atakapofika, utaweza kujikinga dhidi yake mara moja, na pia kuhisi kuja kwake; utahisi wasiwasi halisi katika roho yako. Kazi ya sasa ya Shetani hujizoeza kwa mabadiliko ya mielekeo. Watu wanapotenda mambo kwa njia ya kuchanganyikiwa na kukosa hadhari, wao hubaki katika utumwa. Lazima usalie macho wakati wote na kuwa waangalifu sana. Usilete ubishi juu ya mafanikio yako mwenyewe na hasara, au kukokotoa kwa ajili ya faida yako mwenyewe. Badala yake, tafuta mapenzi Yangu kufanyika.

Vitu vinaweza kuonekana kufanana lakini ubora wavyo unaweza kutofautiana. Hali kadhalika, nyinyi mnapaswa kutambua watu binafsi na vilevile roho. Lazima ufanye utambuzi na kudumisha kuwa macho kiroho. Sumu ya Shetani inapoonekana, unapaswa kuitambua mara moja; haiwezi kuepuka mwanga wa hukumu ya Mungu. Lazima uwe makini zaidi kwa kusikiliza kwa karibu sauti ya Roho Mtakatifu katika roho yako; usiwafuate wengine bila kufikiri au kukosea kilicho cha uongo kuwa kitu cha kweli. Usimfuate yeyote anayeongoza, ili usije ukapata hasara kubwa. Je, hilo linakufanya ujihisije? Je, mmeona matokeo yake? Hupaswi kwa nasibu kuingilia huduma au kuingiza maoni yako mwenyewe ndani yake, la sivyo Mimi nitakuangamiza. Lakini baya zaidi, kama wewe ukisalia muasi na kuendelea kusema na kufanya unavyotaka, Mimi nitakutenga! Kanisa halihitaji kulazimisha urafiki na watu zaidi; linawataka wale ambao kwa kweli wanampenda Mungu na kweli huishi kulingana na neno Langu. Unapaswa kuwa na ufahamu wa hali yako mwenyewe halisi. Je, si ni kujidanganya wakati maskini hujifikiria kuwa matajiri? Kwa kanisa kujengwa, lazima ufuate roho. Usiendelee kwa kutenda mambo kwa upofu, lakini kaa katika nafasi yako na kutimiza kazi yako mwenyewe. Hupaswi kupiga hatua nje ya majukumu yako, lakini timiza kazi zozote unazoweza kufanya kwa nguvu zako zote, halafu moyo Wangu utaridhishwa. Si kwamba nyote mtatenda huduma sawa. Badala yake, kila mmoja wenu lazima ufanye wajibu wako mwenyewe na kutoa huduma zenu kwa uratibu na wengine katika kanisa. Huduma zenu hazipaswi kuchepuka kwa upande wowote.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 19” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 384)

Kazi ya Roho Mtakatifu sasa imewaleta katika mbingu mpya na dunia mpya. Kila kitu kinaendelea kufanywa upya, kila kitu ki mikononi Mwangu, kinarudi ulingoni! Kwa dhana zao, watu wanashindwa kulifikiria kwa makini, na kwao haina maana, lakini ni Mimi ambaye niko kazini, na hekima Yangu iko ndani yake. Kwa hiyo mnaweza kukomesha dhana zenu zote na maoni yenu. Mnaweza kujishughulisha na kula na kunywa neno la Mungu katika utii, bila wasiwasi wowote kamwe. Kwa kuwa Nafanya kazi kwa njia hii, Nitachukua jukumu takatifu. Kwa kweli, watu hawana haja ya kuwa namna fulani. Badala yake, ni Mungu anayefanya mambo ya kimiujiza, na kudhihirisha kudura Yake. Watu wasijivune isipokuwa kama wanajivuna kuhusu Mungu. Vinginevyo mtapata hasara. Mungu huwainua masikini kutoka mavumbini, ambako wanyenyekevu wanainuliwa. Mimi nitatumia hekima Yangu katika hali zake zote kulitawala kanisa la watu wote, kutawala mataifa yote na watu wa makabila yote, ili wao wote wawe ndani Yangu, na ili nyote katika kanisa muweze kunitii. Wale ambao hawakutii kabla lazima sasa wawe watiifu mbele Yangu, ni lazima watiiane, wapokeane wao kwa wao, wawe na maisha yanayohusiana, na wapendane, wote wakifaidi kwa weledi wa wenzao katika sehemu ambazo kila mmoja ana udhaifu, wakihudumu kwa uratibu. Kwa njia hii kanisa litajengwa, na Shetani hatakuwa na nafasi ya kuwatumia watu. Ni hapo tu ambapo mpango Wangu wa usimamizi hautakuwa umeshindwa. Acha Niwape kumbusho jingine hapa. Usiruhusu kutoelewana kuzuke ndani yako kwa sababu mtu fulani ni wa namna fulani, au alitenda mambo kwa njia fulani, likikuacha uwe mtu wa kufifia katika roho. Mimi ninavyoona, hili halifai, na ni kitu bure. Je, Yule unayemwamini si Mungu? Siyo mtu fulani. Shughuli si za aina moja. Kuna mwili mmoja. Kila mmoja hufanya kazi yake, kila mmoja kwa nafasi yake na kufanya kadiri ya uwezo wake—kila cheche ya shauku mwako wa mwanga—kutafuta ukomavu katika maisha. Ni hivyo ndivyo nitakavyoridhika.

Ni lazima mjishughulishe tu na kuwa na amani mbele Yangu. Kuweni katika ushirika wa karibu na Mimi, tafuteni pale ambapo hamuelewi, fanyeni maombi, na muusubiri wakati Wangu. Angalia kila kitu kwa dhahiri kutoka kwa roho. Usifanye mambo bila hadhari, ili kuzuia kupotoka. Ni kwa njia hii tu ambapo kula kwako na kunywa kwa maneno yangu kwa kweli kutazaa matunda. Kula na unywe maneno Yangu mara kwa mara, yatafakari niliyoyasema Mimi, zingatia kutenda maneno Yangu, na uishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno Yangu; hili ndilo suala muhimu. Maendeleo ya kujenga kanisa ndiyo pia maendeleo ya ukuaji wa maisha. Maisha yako yakiacha kukua, huwezi kujengwa. Kutegemea uasilia tu, kwa mwili, kwa raghba, kwa michango, kwa sifa, bila kujali jinsi ulivyo mzuri, hutajengwa. Lazima uishi katika maneno ya maisha, ishi ndani ya unurishwaji na kuwa katika hali ya kuangazwa kutoka kwa Roho Mtakatifu, jua hali yako halisi, na uwe mtu aliyebadilika. Lazima uwe na ufahamu huo huo ndani ya roho yako, upate nuru mpya, na uwe na uwezo wa kuendelea sawa na mwanga mpya. Lazima uwe na uwezo wa kupata mawasiliano ya karibu na Mimi bila kukoma, uwe na uwezo wa kutegemeza matendo yako katika maisha ya kila siku kwa maneno Yangu, uwe na uwezo wa kuwashughulikia vizuri watu wa kila aina, matukio, na mambo kwa kutegemeza maneno Yangu, shughuli zote katika maisha ukiwa na maneno Yangu kama kiwango chako na ukiishi kwa kudhihirisha tabia Yangu.

Ikiwa unatamani kuelewa na kuyatunza mapenzi Yangu, lazima uyazingatie maneno Yangu. Usifanye mambo kwa pupa. Yale yote ambayo Mimi sikubaliani nayo yataishia vibaya. Baraka huja tu kwa kile ambacho Mimi nimekikubali. Kama Mimi nikisema, litakuwa. Kama Mimi nikiamuru, litasimama imara. Kabisa lazima ninyi msifanye kile ambacho sijaruhusu Mimi, kuepuka kunikasirisha Mimi. Wakati huo hakutakuwa na wakati wa kujuta.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 21” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 385)

Wakati wa ujenzi wa kanisa pia ni wakati wa mhemuko zaidi wa Shetani. Shetani mara kwa mara husababisha usumbufu na kukatiza kupitia kwa watu wachache, na ni wale ambao hawaijui roho au wale waumini wapya ambao wanatekeleza jukumu la Shetani kwa urahisi zaidi. Mara nyingi kwa sababu watu hawaelewi kazi ya Roho Mtakatifu, wananyoosha mikono yao na kufanya mambo kiholela, kulingana kabisa na wanavyopenda wao wenyewe, njia za kufanya mambo na dhana. Shika ulimi wako—hii inasemwa kwa ajili ya ulinzi wako mwenyewe. Sikiliza na utii vyema. Kanisa na jamii ni tofauti. Huwezi tu kusema kile unachopenda, au kusema chochote unachofikiri. Haitawezekana hapa kwa kuwa hii ni nyumba ya Mungu. Mungu hakubali namna watu wanavyofanya mambo. Lazima ufanye mambo kwa kuifuata Roho, ishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu na kisha wengine watakutazama na kupendezwa nawe. Lazima kwanza utatue matatizo yote ndani yako kwa kumtegemea Mungu. Komesha tabia zako potovu na kuwa na uwezo wa kuelewa kweli hali zako mwenyewe na kujua jinsi unapaswa kufanya mambo; endelea kushiriki chochote ambacho hukielewi. Haikubaliki kwako kutojijua. Kwanza ponya ugonjwa wako mwenyewe, na kwa njia ya kula na kunywa maneno Yangu zaidi, kutafakari maneno Yangu, ishi maisha na fanya mambo kwa mujibu wa maneno Yangu; haijalishi ukiwa nyumbani au mahali pengine, unapaswa kumruhusu Mungu atwae nguvu ndani mwako. Uache mwili na uasili. Daima yaruhusu maneno ya Mungu yawe na mamlaka ndani mwako. Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwamba maisha yako hayabadiliki; utakuja polepole kuhisi kwamba tabia yako imebadilika kiasi kikubwa. Mbeleni ulikuwa na haraka ya kujionyesha mbele ya watu, hukutii yeyote au ulikuwa na nia ya makuu, mwenye kujidai au mwenye majivuno, na utayatupilia mambo haya mbali hatua kwa hatua. Ukitaka kuyatupilia mbali sasa hivi, basi hiyo haiwezekani! Hii ni kwa sababu binafsi yako ya zamani haitawaruhusu wengine kuigusa, imekita mizizi kabisa ndani yako. Hivyo ni lazima ufanye juhudi za kibinafsi, utii kazi ya Roho Mtakatifu vyema na kikamilifu, utumie hiari yako kushirikiana na Mungu na uwe na nia ya kuyaweka maneno yangu katika vitendo. Ukitenda dhambi, Mungu atakufundisha nidhamu. Unaporejelea na kuwa na ufahamu basi yote yatakuwa mema ndani yako kwa mara moja. Kama unazungumza kwa kujipendekeza, basi utafundishwa nidhamu mara moja kwa ndani. Unaona kwamba Mungu hafurahii jambo la aina hiyo, hivyo ukiliacha mara moja, utakuwa na uzoefu wa amani ya ndani. Kuna baadhi ya waumini wapya ambao hawaelewi hisia za maisha ni nini au jinsi ya kuishi ndani ya hisia za maisha. Wakati mwingine unashangaa, ingawa hujasema lolote, kwa nini unahisi kutotulia sana kwa ndani? Wakati kama huu ni wazo lako na akili ambavyo vina makosa. Wakati mwingine unayo maamuzi yako mwenyewe, dhana na maoni yako mwenyewe; wakati mwingine unawaona wengine kuwa wadogo zaidi kukuliko; wakati mwingine unafanya hesabu zako mwenyewe za ubinafsi nawe huombi au kujichunguza. Hii ndiyo sababu unahisi kutotulia ndani. Labda unajua tatizo ni nini, kwa hiyo mara moja unaliita jina la Mungu moyoni mwako, unasogea karibu na Mungu nawe utarejeshwa. Wakati moyo wako umevurugika sana na hautulii, lazima kabisa usifikiri kwamba Mungu anakuruhusu kuongea. Hasa wale ambao ni waumini wapya lazima wamtii Mungu vyema katika suala hili. Hisia ambazo Mungu huweka ndani ya mtu ni amani, furaha, uwazi na udhamini. Mara nyingi watu hawaelewi na watatia fujo mambo na kufanya mambo kiholela—haya yote ni makatizo, na kabisa lazima uizingatie. Kama wewe ni wa kuelekea katika hali hii, unapaswa kwanza kuchukua “dawa za kuzuia,” la sivyo utaleta makatizo na Mungu atakupiga. Usiwe mwenye haki wa kibinafsi; zichukue nguvu za wengine na kuzitumia kusawazisha na mapungufu yako mwenyewe, angalia jinsi wengine wanaishi kwa kutegemea maneno ya Mungu na uone kama maisha, vitendo na hotuba zao ni vya thamani ya kujifunza kutoka kwavyo au la. Ukiwaona wengine kuwa chini yako wewe basi ni mwenye haki binafsi, mwenye majivuno ya kibinafsi na huna manufaa kwa yeyote. La muhimu sasa ni kulenga kuhusu maisha, kula na kunywa zaidi maneno Yangu, upate uzoefu wa maneno Yangu, kuyajua maneno yangu, kuyafanya maneno yangu kwa dhati kuwa maisha yako—hili ni jambo kuu. Je, maisha ya mtu ambaye hawezi kuishi kwa kutegemea maneno ya Mungu yanaweza kukomaa? Hapana, hayawezi. Lazima uishi kwa kutegemea maneno Yangu kila wakati. Katika maisha, lazima maneno Yangu yawe kanuni yako ya vitendo. Yatakusababisha kuhisi kuwa kufanya mambo kwa njia fulani ni kile Mungu anafurahia, na kufanya mambo kwa njia nyingine ni kile Mungu anachochukia; polepole, utakuja kutembea katika njia sahihi. Lazima uelewe ni mambo yapi yanatokana na Mungu ni mambo yapi yanatokana na Shetani. Mambo yanayotokana na Mungu hukusababisha kuwa wazi zaidi kuhusu maono, na hukusababisha kusogea karibu na karibu zaidi na Mungu, ukishiriki upendo na ndugu kwa bidii; unakuwa na uwezo wa kutilia maanani mzigo wa Mungu, na moyo wako umpendao Mungu haupungui; kuna njia mbele yako kuitembea. Mambo ambayo hutokana na Shetani hukusababisha kupoteza maono na vyote ulivyokuwa navyo awali vimetoweka; unajitenga na Mungu, huna upendo kwa ndugu nawe una moyo wa chuki. Unakuwa mwenye kukata tamaa, hutaki tena kuishi maisha ya kanisa, na moyo wako umpendao Mungu hauko tena. Hii ni kazi ya Shetani na pia ni matokeo ambayo yameletwa na kazi ya roho mbaya.

Huu sasa ni wakati muhimu. Lazima muendelee kufanya kazi kwa bidii mpaka dakika ya mwisho kabisa, myaweke wazi macho yenu ya roho ili muweze kutofautisha kati ya mema na mabaya, na mtumie juhudi nyingi muwezavyo kwa ujenzi wa kanisa. Epukeni vikaragosi wa Shetani, misukosuko ya kidini na kazi ya roho mbaya. Litakaseni kanisa, kufanya mapenzi Yangu itendeke bila kupingwa, na katika wakati huu mfupi sana unaotangulia majanga kweli Nitawafanya kuwa kamili haraka iwezekanavyo, na kuwaleta katika utukufu.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 22” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 386)

Unaona kwamba muda ni mfupi sana na kazi ya Roho Mtakatifu inavurumisha mbele, ikikusababisha kupata baraka kubwa hivi, kumpokea Mfalme wa ulimwengu, Mwenyezi Mungu, ambaye ni Jua ling’aalo, Mfalme wa ufalme—hii yote ni neema na huruma Yangu. Kuna nini kinachoweza kuwepo kinachoweza kukutoa kwa upendo Wangu? Tafakari kwa makini, usijaribu kuepa, subiri kwa ustahamilivu mbele Yangu kila wakati na usiwe ukizurura nje daima. Moyo wako lazima ukae karibu na moyo Wangu, na bila kujali kile kinachoweza kukufikia usifanye vitu bila kufikiri au kiholela. Lazima utazame mapenzi Yangu, ufanye chochote Ninachokitaka na kudhamiria kuacha kile ambacho Sikitaki. Ni lazima usitende hisia zako, ila badala yake utende haki kama Mimi; haikubaliki kuwa na hisi za moyoni hata kwa mama na baba yako. Ni lazima uache yote yasiyokubaliana na ukweli na lazima ujitolee na kujitumia kwa ajili Yangu kwa moyo safi unaonipenda Mimi. Usikubali udhibiti wa mtu yeyote, jambo au kitu; alimuradi linapatana na mapenzi Yangu basi lifanye kwa mujibu wa maneno Yangu. Usiogope, kwa kuwa mikono Yangu hukusaidia, na kwa hakika Nitakukinga dhidi ya watu wote wabaya. Unapaswa kuulinda moyo wako, kuwa ndani Yangu nyakati zote, kwa kuwa maisha yako yanaishiwa kwa kutegemea maisha Yangu; ukiniacha basi utanyauka mara moja.

Unapaswa kujua kwamba ni siku za mwisho sasa. Shetani ibilisi, kama simba ambaye ananguruma, anatembea huku na kule, akitafuta watu wa kuwameza. Kila aina ya mapigo yanatokea sasa na kuna aina nyingi tofauti za roho wabaya. Mimi pekee ndiye Mungu wa kweli; Mimi pekee ndiye kimbilio lako. Unaweza tu kujificha sasa katika mahali Pangu pa siri, ndani Yangu tu, na maafa hayatakufika na hakuna janga litakalokuja karibu na hema lako. Ni lazima unikaribie zaidi, ushiriki na Mimi katika mahali pa siri; usishiriki kiholela na watu wengine. Ni lazima uelewe maana katika maneno Yangu—Sisemi kwamba huruhusiwi kushiriki, ni kwamba tu bado sasa huna utambuzi. Katika kipindi hiki, kazi inayofanywa na roho wabaya inaenea kwa haraka. Wanakupa ushirika kupitia kila aina ya watu. Maneno yao yanasikika kuwa mazuri sana, lakini kuna sumu ndani yayo. Ni risasi za kuvutia na kabla ujue yataweka sumu yayo ndani yako. Unapaswa kujua kwamba watu wengi leo si thabiti, kana kwamba wamelewa. Unapokuwa na ugumu na ushiriki na wengine, wanachokuambia ni amri na mafundisho tu, na si kizuri kama kushiriki moja kwa moja na Mimi. Kuja mbele Yangu na umwage kabisa mambo mazee yaliyo ndani yako, fungua moyo wako Kwangu na moyo Wangu hakika utafichuliwa kwako. Moyo wako lazima uwe mwangalifu mbele Yangu. Usiwe mzembe, ila badala yake lazima unikaribie mara kwa mara; hii ni njia ya haraka kabisa ya maisha yako kukua. Ni lazima uishi ndani Yangu na Nitaishi ndani yako na pia Nitatawala kama Mfalme ndani yako, Nikikuongoza katika vitu vyote, na utakuwa na mgao wa ufalme.

Usijidunishe kwa sababu wewe ni mdogo; unapaswa kujitoa Kwangu. Sioni watu wako vipi juu juu au ni wa umri upi. Naona tu iwapo wananipenda kwa kweli au la, na iwapo wanafuata njia Yangu na kutenda ukweli wakipuuza mambo mengine yote. Usijali kuhusu jinsi kesho itakuwa au jinsi siku za baadaye zitakuwa. Alimradi unitegemee kuishi kila siku, basi hakika Nitakuongoza. Usikae kwa fikira kwamba “Maisha yangu ni machanga sana, sielewi chochote,” ambayo ni fikira iliyotumwa na Shetani. Tumia tu moyo wako kunikaribia daima na ufuate nyayo Zangu hadi mwisho wa njia. Unapoyasikia maneno Yangu ya lawama na onyo na kuzinduka, lazima ukimbie mbele mara moja; usiache kunikaribia, kuwa kasi sawa na nyayo za wanakondoo na endelea kuangalia mbele. Mbele Yangu, ni lazima umpende Mungu wako kwa moyo na nafsi yako yote. Jaribu kuyaelewa maneno yangu zaidi katika njia ya kuhudumu. Katika kutenda ukweli lazima usiwe mwenye moyo dhaifu, ila uwe na moyo wenye nguvu, uwe na azimio na ujasiri wa mtoto wa kiume, na kuwa na moyo mgumu. Ikiwa unataka kunipenda, basi lazima uniridhishe na mambo yote Ninayotaka kutimiza ndani yako. Ikiwa unataka kunifuata, basi lazima utelekeze vyote ulivyo navyo, vyote uvipendavyo, utii kwa unyenyekevu mbele Yangu, kuwa na akili ya kawaida na usijishughulishe kutafiti au kufikiria vitu bila mpango maalum; lazima uwe kasi sawa na kazi ya Roho Mtakatifu daima.

Hapa Nakupa ushauri: Ni lazima ushikilie kwa uthabiti na kutenda yote ambayo Nimetia nuru ndani yako!

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 28” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 387)

Amkeni, ndugu! Amkeni, kina dada! Siku Yangu haitakawishwa; wakati ni uhai, na kuushika wakati ni kuokoa uhai! Wakati hauko mbali sana! Mkifanya mitihani ya kuingia katika chuo kikuu na msipite, mnaweza kujaribu tena na mubukue kwa ajili ya mtihani. Hata hivyo, siku Yangu haitakuwa na ucheleweshaji kama huo. Kumbuka! Kumbuka! Ninakuhimiza kwa maneno haya mazuri. Mwisho wa dunia unafunguka mbele ya macho yenu wenyewe, majanga makubwa yanakaribia upesi; Je, maisha yenu ni muhimu au kulala, kula, kunywa, na kuvaa kwenu ndivyo muhimu? Wakati umekuja wa ninyi kufikiria kwa makini mambo haya. Msiwe wenye shaka tena na msiogope kuwa na uhakika!

Ni wa kusikitisha jinsi gani! Jinsi gani walivyo duni! Jinsi gani walivyopofuka! Jinsi gani wanadamu walivyo wakatili! Kwa kweli mnalipuuza neno Langu—je, Ninazungumza nanyi bure? Bado ninyi ni wazembe sana, kwa nini? Kwa nini hivyo? Je, hamjawahi kufikiria kuhusu hilo kabla? Ninasema mambo haya kwa ajili ya nani? Niamini! Mimi ni Mwokozi wenu! Mimi ni Mwenyezi wako! Kesheni! Kesheni! Muda uliopotea hautakuja tena kamwe, kumbuka hili! Hakuna mahali popote duniani ambapo unaweza kununua dawa ambayo itapoza majuto! Kwa hiyo Nitawaambiaje hili? Je, neno Langu halistahili uzingatifu wenu wa makini na kutafakari kwa kurudia? Ninyi ni wazembe sana kwa maneno Yangu na ni msiowajibikia maisha yenu sana; Ninawezaje kustahimili haya? Ninawezaje?

Kwa nini inawachukua muda mrefu sana kuwa na maisha sahihi ya kanisa? Ni kwa sababu mnakosa imani, hamko tayari kulipa gharama, hamtaki kujitoa wenyewe, na hamko radhi kujitumia wenyewe mbele Yangu. Amkeni, wanangu! Niamini, wanangu! Wapendwa Wangu, kwa nini hamuwezi kufikiria yaliyo ndani ya moyo Wangu?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 30” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 388)

Kuhusu shida zinazoibuka kanisani, usiwe na mashaka mengi. Kanisa linapojengwa haiwezekani kuepuka makosa, lakini usiwe na wasiwasi unapokabiliwa na shida hizo; kuwa mtulivu na makini. Sijawaambia hivyo? Omba Kwangu mara nyingi, na Nitakuonyesha kwa wazi nia Zangu. Kanisa ni moyo Wangu na ni lengo Langu la msingi, Nawezaje kutolipenda? Usiogope, mambo kama haya yanapotendeka kanisani, yote yanaruhusiwa na Mimi. Simama na kuzungumza kwa niaba Yangu. Kuwa na imani kwamba mambo na masuala yote yanaruhusiwa na kiti Changu cha enzi na yote yana nia Zangu ndani yayo. Ukiendelea kushiriki kwa hiari kutakuwa na shida, umefikiri kuhusu matokeo? Hii ni aina ya jambo ambalo Shetani atatumia kwa manufaa yake. Kuja mbele Yangu mara nyingi. Nitazungumza kwa uwazi: Kama utafanya kitu bila kuja mbele Yangu, basi usifikiri unaweza kukikamilisha. Ni ninyi ambao mmeniweka katika nafasi hii.

Usivunjike moyo, usiwe dhaifu, Nitakufichulia. Njia ya kwenda kwa ufalme sio laini hivyo, hakuna kitu kilicho rahisi hivyo! Unataka baraka zije kwa urahisi rahisi, sivyo? Leo kila mtu atakuwa na majaribio machungu ya kukumbana nayo, vinginevyo moyo wa upendo ulio nao Kwangu hautakuwa wenye nguvu zaidi na hutakuwa na upendo wa kweli Kwangu. Hata kama ni hali ndogo tu, kila mtu lazima azipitie, ni kwamba tu zinatofautiana kwa kiwango fulani. Hali hiyo ni moja ya baraka Zangu, ni wangapi hupiga magoti mbele Yangu mara kwa mara kuomba baraka Yangu? Watoto wapumbavu! Wewe daima huhisi kwamba maneno machache ya bahati huhesabika kama baraka Yangu, lakini huhisi kuwa uchungu ni moja ya baraka Zangu. Wale wanaoshiriki katika uchungu Wangu bila shaka watashiriki utamu Wangu. Hiyo ni ahadi Yangu na baraka Zangu kwenu. Usisite kula na kunywa na kufurahia. Wakati giza litapotea hapa kutakuwa na nuru. Huwa kuna giza kubwa kabla ya alasiri; baada ya wakati huu kutakuwa na mwangaza zaidi polepole, na baadaye jua litainuka. Usiogope au kuwa mwepesi kutishwa. Leo Ninawaunga mkono wana Wangu na kushika mamlaka Yangu kwa ajili.

Inapofikia shughuli za kanisa, usikwepe jukumu lako. Ukilileta suala hilo mbele Yangu kwa uangalifu sana, utapata njia. Jambo dogo kama hili linapotokea, unakuwa na woga na wasiwasi, hujui la kufanya? Nimesema mara nyingi, “Nikaribie mara kwa mara!” Je, mmeweka vitu Nilivyowaambia mweke katika vitendo kwa uangalifu sana? Mmetafakari neno Langu mara ngapi? Kwa hivyo, hamna utambuzi wowote ulio wazi. Hicho si kitu mlichosababisha? Mnawalaumu wengine, mbona hamjichukii? Mmevuruga vitu na baadaye bado hamko makini sana na bado mko wazembe; mtazingatia neno Langu.

Watiifu na wanyenyekevu watapata baraka nyingi. Kanisani, mtasimama imara katika ushuhuda wenu Kwangu, mshikilie ukweli—haki ni haki na mabaya ni mabaya—wala msichanganye nyeusi na nyeupe. Mtakuwa vitani na Shetani na lazima mumshinde kabisa ili asiinuke kamwe. Lazima mtoe kila kitu kulinda ushuhuda Wangu. Hili litakuwa lengo la matendo yenu, usisahau jambo hili. Lakini sasa, mmepungukiwa katika imani na uwezo wa kutofautisha vitu na ninyi daima hamuwezi kuelewa neno Langu na nia Zangu. Hata hivyo, usiwe na wasiwasi; kila kitu kinaendelea kulingana na hatua Zangu na wasiwasi huzaa shida tu. Shinda kwa muda zaidi mbele Yangu na usitilie maanani chakula na nguo kwa mwili wa asili. Tafuta nia Zangu mara nyingi, na Nitakuonyesha wazi ni nini. Pole pole utapata nia Zangu katika kila kitu, ili kwamba nitakuwa na njia ya kwenda ndani ya kila mtu bila vizuizi. Itauridhisha moyo Wangu na mtapata baraka pamoja na Mimi milele na milele!

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 41” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 389)

Petro alikuwa mwaminifu Kwangu kwa miaka mingi, lakini hakunung’unika wala kuwa na moyo wa kulalamika kamwe, na hata Ayubu hakuwa sawa na yeye. Katika enzi zote, watakatifu wote, pia, hawajamfikia hata kidogo. Yeye hakufuatilia kunijua Mimi tu, lakini pia alipata kunijua wakati ambapo Shetani alikuwa anatekeleza njama zake danganyifu. Hii ilisababisha miaka mingi ya huduma iliyoupendeza nafsi Yangu, na kwa sababu hii Shetani hakumnyonya kamwe. Petro alitumia imani ya Ayubu, ilhali yeye pia alifahamu wazi upungufu wake. Ingawa Ayubu alikuwa na imani kubwa, alikosa ufahamu wa masuala katika ulimwengu wa kiroho, na hivyo alisema maneno mengi ambayo hayakulingana na hali halisi; hii inaonyesha kwamba ufahamu wake bado haukuwa wa kina, na haukuwa na uwezo wa kufanywa kuwa kamilifu. Na hivyo, Petro siku zote alitazamia kufahamu roho, na daima alilenga kuchunguza mienendo ya ulimwengu wa kiroho. Kwa sababu hii, hakuwa tu na uwezo wa kutambua matakwa Yangu kiasi, lakini pia alielewa kidogo juu ya njama danganyifu za Shetani, na hivyo ufahamu wake kuhusu Mimi ulikuwa mkubwa zaidi kuliko mwingine wowote katika enzi zote.

Kutokana na matukio ya Petro si vigumu kuona kwamba mtu akitaka kunijua, lazima awe makini kwa kuzingatia kwa uangalifu katika roho. Sikuombi kwamba utoe kiasi kikubwa Kwangu kwa nje; hili ni la umuhimu wa ziada. Iwapo hunijui, basi imani, upendo na uaminifu wote unaozungumzia ni ndoto tu, ni upuuzi, na wewe hakika utakuwa mtu ambaye ana majivuno makubwa mbele Zangu lakini hajijui mwenyewe, na hivyo wewe utanaswa tena na Shetani na hutaweza kujinasua; utakuwa mwana wa kuteseka milele, na utakuwa mlengwa wa maangamizi. Lakini kama wewe huna hisia na hujali kuhusu maneno Yangu, basi bila shaka unanipinga Mimi. Huu ni ukweli, na ingekuwa vyema utazame kupitia lango la ulimwengu wa kiroho uone roho nyingi na tofautitofauti zilizoadibiwa na Mimi. Ni wapi kati yao hawakukaa tu na hawakujali, na hawakuyakubali maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakuwa na shaka kwa maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakujaribu kuyashika maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakuyatumia maneno Yangu kama silaha ya kujikinga itakayotumiwa kujilinda? Wao hawakutafuta kunijua kwa njia ya maneno Yangu, lakini waliyatumia kama vitu vya kuchezea tu. Katika hili, je, si wao walinipinga moja kwa moja? Nani ni maneno Yangu? Nani ni Roho Wangu? Mara nyingi Mimi nimeyanena maneno haya kwenu, lakini maono yenu yamewahi kuwa ya kiwango cha juu na yenye uwazi? Matukio yenu yamewahi kuwa ya kweli? Nawakumbusha mara nyingine: Iwapo hamyajui maneno Yangu, hamyakubali, na hamyaweki katika matendo, basi bila shaka mtaadibiwa na Mimi! Nyinyi kwa hakika mtakuwa waathirika wa Shetani!

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 8” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 390)

Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze moyo wa Mungu. Hii ni kwa sababu, hata ingawa watu wengi wanalifahamu neno “Mungu” na mafungu ya maneno kama “kazi ya Mungu”, hawamjui Mungu, sembuse kujua kazi ya Mungu. Si ajabu, basi, kwamba wale wote wasiomjua Mungu wamejawa na imani iliyovurugika. Watu hawachukulii imani kwa Mungu kwa uzito kwa kuwa kuamini Mungu ni jambo geni, jambo lisilo la kawaida sana kwao. Kwa njia hii, hawafikii mahitaji ya Mungu. Kwa maneno mengine, ikiwa watu hawamjui Mungu, hawajui kazi Yake, basi hawafai kwa matumizi na Mungu, sembuse kuweza kutimiza hamu ya Mungu. “Imani katika Mungu” inamaanisha kuamini kuwa kuna Mungu; hii ndiyo dhana rahisi zaidi ya imani katika Mungu. Zaidi ya hayo, kuamini kuwa kuna Mungu si sawa na kuamini katika Mungu kwa ukweli; bali, ni aina ya imani sahili ikiwa na vipengee vya uzito vya kidini. Imani ya kweli katika Mungu ina maana kupitia maneno na kazi ya Mungu kwa msingi wa imani kuwa Mungu ndiye mkuu juu ya vitu vyote. Kwa hivyo mtawekwa huru kutokana na tabia yenu ya upotovu, mtatimiza hamu ya Mungu, na mtapata kumjua Mungu. Ni kwa kupitia safari ya aina hii tu ndio mnaweza kusemekana kuwa mnaamini katika Mungu. Ilhali watu mara nyingi huona kuamini katika Mungu kama jambo rahisi sana na la kipuuzi tu. Watu wanaomwami Mungu kwa njia hii wamepoteza maana ya kumwamini Mungu, na ingawa wanaweza kuendelea kuamini mpaka mwisho, hawatawahi kupata idhini ya Mungu, kwa sababu wanatembea katika njia mbaya. Leo, kuna wale ambao bado wanaamini Mungu katika nyaraka, katika mafundisho ya dini yaliyo matupu. Hawana habari kuwa imani yao katika Mungu haina dutu, na hawawezi kupata idhini ya Mungu, na bado wanaomba kupata amani na neema ya kutosha kutoka kwa Mungu. Tunafaa kuweka kituo na kujiuliza wenyewe: Je, kuamini kwa Mungu linaweza kuwa jambo rahisi ya yote duniani? Je, kuamini kwa Mungu hakumaanishi chochote zaidi ya kupokea neema nyingi kutoka kwa Mungu? Je, watu wanaoamini kwa Mungu na hawamjui, na wanaamini kwa Mungu ila wanamuasi; je watu kama hawa wanaweza kutimiza hamu ya Mungu?

Umetoholewa kutoka katika “Dibaji” ya Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 391)

Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu. Wale wanaotumia upendo kwa Mungu kusitawisha maisha yao yasiyopendeza na kujaza utupu katika mioyo yao ni wale ambao wanataka kuishi katika raha, si wale ambao kweli wanatafuta kumpenda Mungu. Upendo wa aina hii ni kinyume na matakwa ya mtu, harakati ya ridhaa ya hisia, na Mungu hahitaji upendo wa aina hii. Upendo wako, basi, ni upendo wa aina gani? Ni kwa ajili gani unampenda Mungu? Je, ni kiasi gani cha upendo wa kweli, ulicho nacho kwa Mungu sasa? Upendo wa watu wengi kati yenu ni kama uliotajwa hapo awali. Upendo wa aina hii unaweza tu kudumisha hali kama ilivyo; hauwezi kufikia uthabiti wa milele, wala kuchukua mizizi katika mtu. Aina hii ya upendo ni ule wa ua ambalo halizai matunda baada ya kuchanuka na hatimaye kunyauka. Kwa maneno mengine, baada ya wewe kumpenda Mungu mara moja kwa jinsi hii na hakuna mtu wa kukuongoza kwa njia ya mbele, basi utaanguka. Kama unaweza tu kumpenda Mungu katika wakati wa kumpenda Mungu na kutofanya mabadiliko katika tabia ya maisha yako baadaye, basi utaendelea kufunikwa na ushawishi wa giza, bila uwezo wa kutoroka, na bila uwezo wa kujinasua kwa kufungwa na kupumbazwa na Shetani. Hakuna mtu kama huyu anayeweza kukubaliwa na Mungu; mwishowe, roho zao, nafsi na mwili bado ni mali ya Shetani. Hili ni bila ya shaka. Wale wote ambao hawawezi kukubaliwa kikamilifu na Mungu watarudi mahali pao pa awali, yaani, kwa Shetani, na watakwenda chini kwa ziwa liwakalo moto wa jahanamu kukubali hatua ya pili ya adhabu kutoka kwa Mungu. Wale wanaokubaliwa na Mungu ni wale ambao wanamkataa shetani na kutoroka kutoka kwa miliki ya Shetani. Watu kama wale watahesabiwa rasmi miongoni mwa watu wa ufalme. Hivi ndivyo watu wa ufalme huja kuwa. Je, uko tayari kuwa mtu wa aina hii? Je, uko tayari kukubaliwa na Mungu? Je, uko tayari kutoroka kutoka miliki ya Shetani na kurudi kwa Mungu? Je, sasa wewe ni mali ya Shetani au umehesabiwa miongoni mwa watu wa ufalme? Mambo hayo lazima yote yawe wazi na hayahitaji maelezo zaidi.

Umetoholewa kutoka katika “Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 392)

Katika nyakati zilizopita, watu wengi walifuatilia kwa jitihada na fikira za mwanadamu na kwa ajili ya matumaini ya mwanadamu. Mambo haya hayatajadiliwa sasa. La muhimu ni kupata njia ya kutenda ambayo itawezesha kila mmoja wenu kudumisha hali ya kawaida mbele ya Mungu na hatimaye kuvunja pingu za ushawishi wa Shetani, ili mpate kuwa wakubalika wa Mungu, na kuishi kwa kudhihirisha duniani matakwa ya Mungu kwenu. Ni haya tu yanayoweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Wengi wanaamini katika Mungu, ila hawajui ni kitu gani Anachotamani Mungu wala ni nini anachotamani Shetani. Wao wanaamini kipumbavu na kuwafuata watu wengine kama vipofu, na kwa hivyo hawajakuwa kamwe na maisha ya kawaida ya Kikristo; hawana uhusiano wa kawaida wa binafsi na watu wengine, sembuse uhusiano wa kawaida ambao mwanadamu anao na Mungu. Kutoka kwa hili inaweza kuonekana kwamba matatizo na makosa ya mtu, na mambo mengine ambayo yanaweza kuzuia mapenzi ya Mungu ni mengi. Hili linatosha kuthibitisha kwamba mwanadamu hajajiandaa kikamilifu kufuata njia iliyo sahihi wala kuwa na uzoefu wa maisha halisi. Kujiandaa kufuata njia iliyo sahihi ni nini? Kujiandaa kufuata njia iliyo sahihi ina maana kwamba unaweza kunyamazisha moyo wako mbele za Mungu wakati wote na wasiliana kwa karibu na Mungu, hatua kwa hatua ukipata kujua ni nini kinachokosa ndani ya mwanadamu na polepole kupata kumfahamu Mungu zaidi. Kwa njia hii, kila siku unapata maono mapya na kupata nuru kiroho; hamu yako inakua, na wewe kutafuta kuingia katika ukweli. Kila siku kuna mwanga mpya na ufahamu mpya. Kupitia njia hii, wewe hatua kwa hatua unavunja ushawishi wa Shetani na kuwa huru, na maisha yako yanakua kwa kiasi kikubwa. Mtu kama huyu ameweka mikakati ya kufuata mwenendo sawa. Tathmini uzoefu wako mwenyewe halisi na kuchunguza njia uliyoichukua katika imani yako kwa Mungu dhidi ya yaliyotajwa hapo juu. Wewe ni yule ambaye amepangwa kufuata mwenendo sawa? Ni katika masuala gani ambapo umejiweka huru kutokana na pingu za shetani na kutokana na ushawishi wa Shetani? Kama bado hujajiandaa kufuata njia iliyo sahihi, uhusiano wako na Shetani bado haujaisha. Kwa jinsi hiyo, ukimbiziaji huu wa upendo kwa Mungu inaweza kusababisha upendo ambao ni sahihi, wa kujitolea, na safi? Unasema kwamba upendo wako kwa Mungu ni wa dhati na imara, bali hujajinasua kutoka kwa pingu za Shetani. Je, wewe si unajaribu kumpumbaza Mungu? Ukitaka kuufikia upendo safi kwa Mungu, kuwa wa Mungu kikamilifu, na kuwa mhesabiwa miongoni mwa watu wa ufalme, basi lazima kwanza ujiandae kufuata njia iliyo sahihi.

Umetoholewa kutoka katika “Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 393)

Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yanayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusisha Mungu katika maisha yake ya kila siku. Hii ni kusema, Mungu ni Mungu, na maisha ni maisha, kama kwamba binadamu hana uhusiano na Mungu katika maisha yake. Hayo ndiyo binadamu wote wanayaamini. Aina hii ya imani kwa Mungu haitaruhusu binadamu kupatwa na kukamilishwa Naye kwa uhakika. Kwa kweli, si kwamba neno la Mungu ni pungufu, badala yake uwezo wa binadamu wa kupokea neno Lake ni duni mno. Inaweza kusemwa karibu binadamu wote hutenda kulingana na nia za Mungu. Badala yake, imani yao kwa Mungu ni kwa mujibu wa nia zao wenyewe, fikra za kidini zilizowekwa, na desturi. Ni wachache wanaopitia mabadiliko baada ya kulikubali neno la Mungu na kuanza kutenda kwa mujibu wa mapenzi Yake. Badala yake, wanaendelea katika imani yao potovu. Wakati mwanadamu anaanza kuamini katika Mungu, anafanya hivyo kwa kuzingatia sheria za kawaida za dini, na anaishi na kuhusiana na wengine kwa misingi ya falsafa yake ya kuishi. Hivyo ndivyo ilivyo kwa watu tisa kati ya kila watu kumi. Ni wachache sana wanaounda mpango mwingine na kuanza mwanzo mpya baada ya kuanza kumwamini Mungu. Hakuna anayeona au kuweka katika vitendo neno la Mungu kama ukweli.

Chukua imani katika Yesu, kwa mfano. Kama mtu alikuwa mwanafunzi katika imani au alikuwa wa imani hiyo kwa muda mrefu, wote walitumia vipaji vyovyote walivyokuwa navyo na kuonyesha ujuzi wowote waliokuwa nao. Mwanadamu aliongeza tu “imani katika Mungu,” maneno haya matatu, katika maisha yake ya kawaida, bado hayakufanya mabadiliko katika tabia yake, na imani yao kwa Mungu haikukua hata kidogo. Ukimbizaji wa mwanadamu wa swala hili haukuwa baridi wala moto. Hakusema kwamba hakuamini, lakini pia hakujitoa kikamilifu kwa Mungu. Hakuwahi kumpenda Mungu kwa kweli wala kumtii Mungu. Imani yake kwa Mungu ilikuwa halali na ya kujifanya, na aligeuka na akapuuza na wala hakuwa na bidii kwa kutenda imani yake. Aliendelea katika hali kama hiyo ya kuchanganyikiwa tangu mwanzo hadi wakati wake wa kufa. Ni nini maana ya hili? Leo, lazima uwe katika njia sahihi kwani unaamini katika Mungu wa vitendo. Kwa kuwa una imani katika Mungu, hupaswi tu kutafuta baraka, lakini pia kutafuta kumpenda Mungu na kumjua Mungu. Kupitia kwa kupata nuru kutoka Kwake na harakati yako mwenyewe, unaweza kula na kunywa neno Lake, kukuza ufahamu wa kweli kuhusu Mungu, na kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu unaotoka moyoni mwako. Kwa maneno mengine, upendo wako kwa Mungu ni wa kweli zaidi, ambapo hakuna yeyote anayeweza kuharibu au kukuzuia kuonyesha upendo wako Kwake. Basi uko kwa njia ya kweli ya imani kwa Mungu. Inathibitisha kwamba wewe unamilikiwa na Mungu, kwani moyo wako umemilikiwa na Mungu na wala huwezi kumilikiwa na kitu kingine. Kutokana na tajriba yako, malipo uliyolipa, na kazi ya Mungu, wewe una uwezo wa kuendeleza upendo usioamriwa kwa Mungu. Kisha unawekwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa neno la Mungu. Ni wakati tu ambao umekuwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza ndipo unaweza kuchukuliwa kuwa umempata Mungu. Katika imani yako kwa Mungu, lazima utafute lengo hili. Huu ni wajibu wa kila mmoja wenu. Hakuna anayelazimika kutosheka na mambo jinsi yalivyo. Hamuwezi kuwa na fikira aina mbili kwa kazi ya Mungu au uichukulie kwa wepesi. Mnapaswa kumfikiria Mungu katika mambo yako yote na wakati wote, na kufanya mambo yote kwa ajili yake. Na wakati mnasema au kufanya mambo, mnapaswa kutilia maanani maslahi ya nyumba ya Mungu kwanza. Ni hii tu ndio inayolingana na mapenzi ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 394)

Kosa kubwa sana la binadamu kuwa na imani katika Mungu ni kwamba imani yake ni ya maneno tu, na Mungu hayupo popote katika maisha yake ya utendaji. Watu wote, kwa kweli, wanaamini kuwepo kwa Mungu, lakini Mungu si sehemu ya maisha yao ya kila siku. Maombi mengi kwa Mungu hutoka katika kinywa cha mtu, lakini Mungu amepewa nafasi ndogo sana katika moyo wake, na hivyo Mungu humjaribu binadamu tena na tena. Kwa vile mtu ni mchafu, Mungu hana budi ila kumjaribu mtu, ili aweze kuona aibu na kisha aje kujitambua mwenyewe katika majaribu. La sivyo, mwanadamu atageuka mwana wa malaika mkuu, na kuzidi kuwa mpotovu. Wakati wa imani ya mtu katika Mungu, nia nyingi na malengo ya kibinafsi hutupwa mbali anavyotakaswa na Mungu bila kukoma. La sivyo, hakuna mwanadamu anayeweza kutumiwa na Mungu, na Mungu hana njia ya kufanya ndani ya mtu kazi anayopaswa kufanya. Mungu kwanza humtakasa mwanadamu. Katika mchakato huu, mtu anaweza kuja kujijua mwenyewe na Mungu huenda akambadilisha mwanadamu. Ni baada ya haya ndipo Mungu anaweza kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kwa njia hii pekee ndio moyo wa binadamu unaweza kumgeukia Mungu kwa ukamilifu. Kwa hivyo, kumwamini Mungu si rahisi jinsi mwanadamu anaweza kuona. Mungu anavyoona, ukiwa tu na ufahamu lakini huna neno Lake kama uhai; ikiwa wewe unazingatia tu maarifa yako mwenyewe lakini huwezi kutenda ukweli au kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, basi hii ni dhihirisho kwamba huna moyo wa upendo kwa Mungu, na inaonyesha kwamba moyo wako si mali ya Mungu. Kuja kumjua Mungu kwa kumwamini; hili ndilo lengo la mwisho na ambalo mwanadamu atatafuta. Lazima ufanye juhudi ya kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ili yaweze kuonekana katika matendo yako. Kama unayo maarifa ya mafundisho ya dini pekee, basi imani yako kwa Mungu itakuwa kazi bure. Kama wewe utatenda pia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake basi imani yako inaweza kuchukuliwa kuwa kamili na kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Katika njia hii, wanadamu wengi wanaweza kusema wana maarifa mengi, lakini katika wakati wao wa kufa, macho yao hujawa machozi, nao hujichukia wenyewe kwa kuharibu maisha yao yote na kuishi maisha yasiyo na mazao hadi uzeeni. Wanaelewa tu mafundisho lakini hawawezi kutia ukweli katika vitendo na kushuhudia kwa Mungu, badala yake wakikimbia huku na kule, wakiwa na kazi kama nyuki; mara wanapochungulia kaburi wao hatimaye huona kwamba hawana ushuhuda wa kweli, kwamba hawamjui Mungu kamwe. Je, si huku ni kuchelewa mno? Kwa nini usichukue nafasi hii na kufuatilia ukweli unaoupenda? Kwa nini usubiri hadi kesho? Iwapo katika maisha huwezi kuteseka kwa ajili ya ukweli au kutafuta kuupata, inaweza kuwa kwamba unataka kujuta katika saa yako ya kufa? Ikiwa hivyo, basi kwa nini umwamini Mungu? Kwa kweli, kuna mambo mengi ambayo mtu, iwapo ataweka juhudi kidogo tu, anaweza kuweka ukweli katika vitendo na hivyo kumridhisha Mungu. Moyo wa binadamu daima umepagawa na mapepo na kwa hivyo hawezi kutenda mambo kwa ajili ya Mungu. Badala yake, yeye daima yumo katika safari ya huku na kule kwa sababu ya mwili, na hafaidiki na chochote mwishowe. Ni kwa sababu hizi ndio mtu hupata matatizo ya mara kwa mara na mateso. Je, haya sio mateso ya Shetani? Je, huu sio ufisadi wa mwili? Hufai kumdanganya Mungu kwa maneno ya mdomo. Badala yake, lazima uchukue hatua inayoonekana. Usijidanganye; ni nini maana katika hilo? Ni faida gani utakayopata kutokana na kuishi kwa ajili ya mwili wako na kufanya bidii kwa ajili ya umaarufu na mali ya dunia?

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 395)

Sasa, mnatakiwa kufuatilia kugeuka kuwa watu wa Mungu, na mtaanza kuingia kote katika njia sahihi. Kuwa watu wa Mungu kuna maana ya kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, mnaanza rasmi kuingia katika mafunzo ya ufalme, na maisha yenu ya baadaye yatakoma kuwa goigoi na hobelahobela kama yalivyokuwa awali; maisha hayo ni yasiyoweza kufikia viwango vinavyotakiwa na Mungu. Kama huhisi umuhimu wowote, basi hili huonyesha kwamba huna hamu ya kujiendeleza mwenyewe, kwamba ukimbizaji wako umekanganywa na kuchanganywa, na wewe ni usiyeweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Kuingia katika mafunzo ya ufalme kuna maana ya kuanza maisha ya watu wa Mungu—uko radhi kuyakubali mafunzo hayo? Uko radhi kuhisi kuthamini kwa umuhimu? Uko radhi kuishi chini ya nidhamu ya Mungu? Uko radhi kuishi chini ya kuadibu kwa Mungu? Wakati ambapo maneno ya Mungu yatakujia na kukujaribu, utafanyaje? Na utafanya nini wakati ambapo utakabiliwa na aina yote ya ukweli? Zamani, kulenga kwako hakukuwa juu ya maisha; leo, lazima uingie katika uhalisi wa maisha, na kufuatilia mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Hili ndilo lazima litimizwe na watu wa ufalme. Wale wote ambao ni watu wa Mungu lazima wawe na uzima, lazima wakubali mafunzo ya ufalme, na kufuatilia mabadiliko katika tabia ya maisha yao. Hili ndilo Mungu huwashurutisha watu wa ufalme.

Masharti ya Mungu kwa watu wa ufalme ni kama yafuatayo:

1. Lazima wakubali maagizo ya Mungu, ambalo ni kusema, lazima wakubali maneno yote yaliyonenwa katika kazi ya Mungu ya siku za mwisho.

2. Lazima waingie katika mafunzo ya ufalme.

3. Lazima wafuatilie kufanya mioyo yao iguswe na Mungu. Wakati ambapo moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na una maisha ya kiroho ya kawaida, utaishi katika eneo la uhuru, ambalo lina maana kuwa utaishi chini ya utunzaji na ulinzi wa upendo wa Mungu. Ukiishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu tu ndipo utakuwa wa Mungu.

4. Lazima wapatwe na Mungu.

5. Lazima wawe dhihirisho la utukufu wa Mungu duniani.

Haya mawazo makuu matano ni maagizo Yangu kwenu. Maneno Yangu yananenwa kwa watu wa Mungu, na kama hutaki kuyakubali maagizo haya, Sitakulazimisha—lakini ukiyakubali kwa kweli, basi utaweza kuyafanya mapenzi ya Mungu. Leo, anzeni kuyakubali maagizo ya Mungu, na kufuatilia kuwa watu wa ufalme na kufikia viwango vinavyohitajika kuwa watu wa ufalme. Hii ndiyo hatua ya kwanza ya kuingia. Kama ungependa kufanya mapenzi ya Mungu kwa ukamilifu, basi lazima uyakubali maagizo haya matano, na kama unaweza kuyatimiza, utaupendeza moyo wa Mungu na kwa hakika utatumiwa sana na Mungu. Kilicho cha maana sana leo ni kuingia katika mafunzo ya ufalme. Kuingia katika mafunzo ya ufalme kunahusisha maisha ya kiroho. Awali, hakukuwa na mazungumzo ya maisha ya kiroho, lakini leo, unapoanza kuingia katika mafunzo ya ufalme, unaingia rasmi katika maisha ya kiroho.

Umetoholewa kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 396)

Maisha ya kiroho ni maisha ya aina gani? Maisha ya kiroho ni yale ambayo kwayo moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na unaweza kuwa mzingatifu wa upendo wa Mungu. Ni yale ambayo kwayo unaishi katika maneno ya Mungu, na hakuna kingine kinachoushughulisha moyo wako, na unaweza kuyafahamu mapenzi ya Mungu leo, na unaongozwa na nuru ya Roho Mtakatifu leo ili kutimiza wajibu wako. Maisha kama hayo kati ya mwanadamu na Mungu ndiyo maisha ya kiroho. Kama huwezi kuifuata nuru ya leo, basi umbali umefunguka katika uhusiano wako na Mungu—huenda hata ukawa umevunjwa—na huna maisha ya kiroho ya kawaida. Uhusiano wa kawaida na Mungu hujengwa juu ya msingi wa kukubali maneno ya Mungu leo. Je, una maisha ya kiroho ya kawaida? Je, una uhusiano wa kawaida na Mungu? Wewe ni mtu anayeifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama unaweza kufuata nuru ya Roho Mtakatifu leo, na unaweza kufahamu mapenzi ya Mungu ndani ya maneno Yake, na kuingia katika maneno haya, basi wewe ni mtu ambaye hufuata mkondo wa Roho Mtakatifu. Kama hufuati mkondo wa Roho Mtakatifu, basi wewe bila shaka ni mtu asiyefuatilia ukweli. Roho Mtakatifu hana nafasi ya kufanya kazi ndani ya wale ambao hawana hamu ya kujiendeleza wenyewe, na kutokana na hayo, watu hao hawawezi kamwe kukusanya nguvu zao, na kila mara wao huwa baridi. Leo, wewe hufuata mkondo wa Roho Mtakatifu? Wewe uko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu? Je, umeibuka kutoka kwa hali baridi? Wale wote ambao huamini katika maneno ya Mungu, ambao huchukulia kazi ya Mungu kama msingi, na hufuata nuru ya Roho Mtakatifu leo—wao wote wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Kama wewe huamini kwamba maneno ya Mungu ni kweli na sahihi kwa dhahiri, na kama wewe huamini maneno ya Mungu bila kujali kile Yeye husema, basi wewe ni mtu ambaye hufuatilia kuingia katika kazi ya Mungu, na kwa njia hii utatimiza mapenzi ya Mungu.

Ili kuingia katika mkondo wa Roho Mtakatifu lazima uwe na uhusiano wa kawaida na Mungu, na lazima kwanza ujiondoshe kwa hali yako baridi. Watu wengine kila mara hufuata walio wengi, na mioyo yao imetangatanga mbali sana na Mungu; watu hao hawana hamu ya kujiendeleza wenyewe, na viwango ambavyo wao hufuatilia ni vya chini sana. Ukimbizaji wa kumpenda Mungu tu na kupatwa na Mungu ndiyo mapenzi ya Mungu. Kuna watu ambao hutumia tu dhamiri yao kulipa mapenzi ya Mungu, lakini hili haliwezi kuridhisha mapenzi ya Mungu; kadri viwango unavyofuatilia vilivyo juu zaidi, ndivyo vitakavyokuwa vinawiana na mapenzi ya Mungu. Kama mtu aliye wa kawaida, na ambaye hufuatilia upendo wa Mungu, kuingia katika ufalme kuwa mmoja wa watu wa Mungu ni siku za usoni zenu za kweli, na maisha ambayo ni yenye thamani na maana sana; hakuna aliyebarikiwa kuliko ninyi. Mbona Nasema hili? Kwa sababu wale wasiomwamini Mungu huishi kwa ajili ya mwili, na wao huishi kwa ajili ya Shetani, lakini leo ninyi huishi kwa ajili ya Mungu, na huishi kutenda mapenzi ya Mungu. Ndiyo maana Nasema maisha yenu ni yenye maana sana. Ni kundi hili tu la watu, ambao wameteuliwa na Mungu, wanaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana sana: Hakuna mwingine duniani anaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya thamani na maana hivyo. Kwa sababu mmeteuliwa na Mungu, na mmekuzwa na Mungu, na, aidha, kwa sababu ya upendo wa Mungu kwenu, mmefahamu uzima wa kweli, na mnajua namna ya kuishi maisha yenye thamani sana. Hili si kwa sababu ukimbizaji wenu ni mzuri, lakini kwa sababu ya neema ya Mungu; ni Mungu aliyefungua macho ya roho zenu, na ni Roho wa Mungu aliyegusa mioyo yenu, kuwapa ninyi bahati nzuri ya kuja mbele Yake. Kama Roho wa Mungu hangekuwa amekupa nuru, basi hungekuwa na uwezo wa kuona kilicho cha kupendeza kuhusu Mungu, wala haingewezekana kwa wewe kumpenda Mungu. Ni kwa sababu kabisa Roho wa Mungu amegusa mioyo ya watu ndiyo mioyo yao imeelekea kwa Mungu. Mara nyingine, wakati ambapo unafurahia maneno ya Mungu, roho yako huguswa, na wewe huhisi kwamba huna budi kumpenda Mungu, kwamba kuna nguvu nyingi ndani yako, na kwamba hakuna chochote usichoweza kuweka kando. Kama wewe unahisi hivi, basi umeguswa na Roho wa Mungu, na moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na utamwomba Mungu na kusema: “Ee Mungu! Sisi kweli tumejaaliwa na kuteuliwa na Wewe. Utukufu Wako hunipa fahari, na inaonekana ya kuleta sifa kuu kwa mimi kuwa mmoja wa watu Wako. Nitatumia chochote na kutoa chochote ili kufanya mapenzi Yako, na nitayatoa maisha yangu yote, na juhudi za maisha yangu yote, Kwako.” Unapoomba hivi, kutakuwa na upendo usioisha na utiifu wa kweli kwa Mungu ndani ya moyo wako. Je, umewahi kuwa na tukio kama hili? Kama watu huguswa mara kwa mara na Roho wa Mungu, basi wako radhi hasa kujitolea wenyewe kwa Mungu katika maombi yao: “Ee Mungu! Ningependa kutazama siku Yako ya utukufu, na ningependa kuishi kwa ajili Yako—hakuna kilicho cha thamani au maana zaidi kuliko kuishi kwa ajili Yako, na sina hamu hata kidogo ya kuishi kwa ajili ya Shetani na mwili. Wewe huniinua kwa kuniwezesha mimi kuishi kwa ajili Yako leo.” Wakati ambapo umeomba kwa njia hii, utahisi kwamba huna budi ila kutoa moyo wako kwa Mungu, kwamba lazima umpate Mungu, na kwamba ungechukia kufa bila kumpata Mungu wakati ambapo uko hai. Baada ya kunena ombi hilo, kutakuwa na nguvu isiyoisha ndani yako, na hutajua hiyo hutoka wapi; ndani ya moyo wako kutakuwa na nguvu bila kikomo, na utakuwa na hisi kwamba Mungu ni wa kupendeza sana, na kwamba Anastahili kupendwa. Huu ndio wakati ambapo utakuwa umeguswa na Mungu. Wale wote ambao wamekuwa na tukio hilo wameguswa na Mungu. Kwa wale ambao mara kwa mara huguswa na Mungu, mabadiliko hutokea ndani ya maisha yao, wao huweza kufanya azimio lao na wako radhi kumpata Mungu kabisa, upendo kwa Mungu ndani yao ni thabiti zaidi, mioyo yao imeelekea kwa Mungu kabisa, wao huwa hawastahi familia, ulimwengu, matatizo, au siku zao za baadaye, na wao huwa radhi kutoa juhudi za maisha yote kwa Mungu. Wale wote ambao wameguswa na Roho wa Mungu ni watu wanaofuatilia ukweli, na ambao huwa na tumaini la kufanywa wakamilifu na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 397)

Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno ya Mungu leo: Kama unafuatilia kuingia katika uzima au kutimiza mapenzi ya Mungu, kila kitu kinapaswa kulenga maneno ya Mungu leo. Kama kile ambacho unawasiliana kwa karibu na kufuatilia hakilengi maneno ya Mungu leo, basi wewe ni mgeni kwa maneno ya Mungu, na umeondolewa kabisa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Kile ambacho Mungu hutaka ni watu ambao huzifuata nyayo Zake. Haijalishi vile ulichoelewa awali ni cha ajabu na safi, Mungu hakitaki, na kama huwezi kuweka kando vitu hivyo, basi vitakuwa kizuizi kikubwa mno kwa kuingia kwako katika siku za baadaye. Wale wote ambao wanaweza kufuata nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Watu wa enzi zilizopita pia walifuata nyayo za Mungu, ilhali hawangeweza kufuata mpaka leo; hii ndiyo baraka ya watu wa siku za mwisho. Wale ambao wanaweza kufuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, na ambao wanaweza kuzifuata nyayo za Mungu, kiasi kwamba wamfuate Mungu popote Awaongozapo—hawa ni watu ambao wamebarikiwa na Mungu. Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu. Leo, wale wote ambao hufuata maneno ya sasa ya Mungu wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu; wale ambao ni wageni kwa maneno ya leo ya Mungu wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na watu hao hawasifiwi na Mungu. Huduma ambayo imetenganishwa na matamshi ya sasa ya Roho Mtakatifu ni huduma ambayo ni ya mwili, na ya dhana, na haiwezi kuwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Kama watu huishi miongoni mwa dhana za kidini, basi hawawezi kufanya lolote lenye kustahili kwa mapenzi ya Mungu, na hata ingawa wao humhudumia Mungu, wao huhudumu katikati ya mawazo na dhana zao, na hawawezi kabisa kuhudumu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Wale ambao hawawezi kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu hawaelewi mapenzi ya Mungu, na wale ambao hawaelewi mapenzi ya Mungu hawawezi kumhudumia Mungu. Mungu hutaka huduma inayoupendeza moyo Wake mwenyewe; Hataki huduma ambayo ni ya dhana na mwili. Kama watu hawawezi kuzifuata hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, basi wao huishi katikati ya dhana. Huduma ya watu hao hukatiza na huvuruga, na huduma ya aina hii huenda kinyume na Mungu. Hivyo wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu hawawezi kumhudumia Mungu; wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu humpinga Mungu bila shaka, na ni wasioweza kulingana na Mungu. “Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu” kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao. Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli. Wale ambao huondoshwa na kazi ya Roho Mtakatifu ni watu wasioweza kufuata kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na ambao huasi dhidi ya kazi ya karibuni zaidi ya Mungu. Kwamba watu hao humpinga Mungu waziwazi ni kwa sababu Mungu amefanya kazi mpya, na kwa sababu picha ya Mungu si sawa na ile iliyo ndani ya dhana zao—kutokana na hilo wao humpinga Mungu waziwazi na kumhukumu Mungu, kusababisha wao kuchukiwa na kukataliwa na Mungu. Kuwa na ufahamu wa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu si jambo rahisi, lakini kama watu wana nia ya kutii kazi ya Mungu kwa kudhamiria na kuitafuta kazi ya Mungu, basi watakuwa na nafasi ya kumwona Mungu, na watakuwa na nafasi ya kupata uongozi mpya zaidi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao hupinga kazi ya Mungu kwa kudhamiria hawawezi kupata nuru ya Roho mtakatifu au uongozi wa Mungu. Hivyo, kama watu wanaweza kupokea kazi ya karibuni zaidi ya Mungu au la hutegemea neema ya Mungu, hutegemea ukimbizaji wao, na hutegemea makusudi yao.

Umetoholewa kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 398)

Wale wote ambao huweza kutii matamshi ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Haijalishi vile walikuwa, au vile Roho Mtakatifu alikuwa akifanya kazi ndani yao—wale ambao wamepata kazi ya karibuni zaidi ni waliobarikiwa zaidi, na wale ambao hawawezi kufuata kazi ya karibuni zaidi huondoshwa. Mungu anataka wale wanaoweza kukubali nuru mpya, na Anataka wale ambao hukubali na kujua kazi Yake ya karibuni zaidi. Kwa nini husemwa kwamba lazima uwe mwanamwali safi? Mwanamwali safi anaweza kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu na kuelewa mambo mapya, na zaidi ya hayo, kuweza kuweka kando dhana za zamani, na kutii kazi ya Mungu leo. Kundi hili la watu, ambao hukubali kazi mpya zaidi ya leo, walijaaliwa na Mungu kabla ya enzi, na ni ambao wamebarikiwa zaidi ya watu wote. Ninyi huisikia sauti ya Mungu moja kwa moja, na kutazama kuonekana kwa Mungu, na hivyo, kotekote mbinguni na duniani, na kotekote katika enzi, hakuna waliobarikiwa kuliko ninyi, hili kundi la watu. Haya yote ni kwa sababu ya kazi ya Mungu, kwa sababu ya majaaliwa na uteuzi wa Mungu, na kwa sababu ya neema ya Mungu; kama Mungu hangeongea na kutamka maneno Yake, hali zenu zingekuwa kama zilivyo leo? Vivi hivi, utukufu wote na sifa ziwe kwa Mungu, kwani haya yote ni kwa sababu Mungu huwainua ninyi. Na mambo haya yakiwa akilini, bado ungeweza kuwa baridi? Nguvu zako bado hazingeweza kuongezeka?

Kwamba wewe huweza kukubali hukumu, kuadibu, kuangamiza, na usafishaji wa maneno ya Mungu, na, aidha, unaweza kukubali maagizo ya Mungu, lilijaaliwa na Mungu mwanzoni mwa wakati, na hivyo lazima usihuzunishwe sana wakati ambapo wewe huadibiwa. Hakuna anayeweza kuondoa kazi ambayo imefanywa ndani yenu, na baraka ambazo zimetolewa ndani yenu, na hakuna anayeweza kuondoa yote ambayo mmepewa ninyi. Watu wa dini hawastahimili mlingano na ninyi. Ninyi hamna ubingwa mkuu katika Biblia, na hamjajizatiti na nadharia za kidini, lakini kwa sababu Mungu amefanya kazi ndani yenu, mmepata zaidi ya yeyote kotekote katika enzi—na kwa hiyo hii ni baraka yenu kuu zaidi. Kwa sababu ya hili, lazima mjitolee hata zaidi kwa Mungu, na hata waaminifu zaidi kwa Mungu. Kwa sababu Mungu hukuinua, lazima utegemeze juhudi zako, na lazima utayarishe kimo chako kukubali maagizo ya Mungu. Lazima usimame imara mahali ambapo Mungu amekupa, ufuatilie kuwa mmoja wa watu wa Mungu, ukubali mafunzo ya ufalme, upatwe na Mungu na hatimaye kuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Je, wewe una maazimio haya? Kama una maazimio hayo, basi hatimaye una hakika ya kupatwa na Mungu, na utakuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Unapaswa kuelewa kwamba agizo kuu ni kupatwa na Mungu na kugeuka kuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Haya ni mapenzi ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 399)

Maneno ya Roho Mtakatifu leo ni nguvu za kazi ya Roho Mtakatifu, na kuendelea kwa Roho Mtakatifu kumpa nuru mwanadamu wakati wa kipindi hiki ni mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu. Na mwelekeo ni upi katika kazi ya Roho Mtakatifu leo? Ni uongozi wa watu ndani ya kazi ya Mungu leo, na ndani ya maisha ya kiroho ya kawaida. Kuna hatua kadhaa za kuingia katika maisha ya kiroho ya kawaida:

1. Kwanza, lazima uumimine moyo wako ndani ya maneno ya Mungu. Lazima usiyafuatilie maneno ya Mungu katika siku za zamani, na lazima usiyasome wala kuyafananisha na maneno ya sasa. Badala yake, lazima uumimine moyo wako kabisa katika maneno ya sasa ya Mungu. Kama kuna watu ambao bado wangependa kuyasoma maneno ya Mungu, vitabu vya kiroho, au maelezo mengine ya mahubiri kutoka kwa siku za zamani, ambao hawafuati maneno ya Roho Mtakatifu leo, basi wao ni wapumbavu zaidi ya watu wote; Mungu huchukia sana watu kama hao. Kama uko radhi kukubali nuru ya Roho Mtakatifu leo, basi mimina moyo wako kabisa katika matamshi ya Mungu leo. Hili ni jambo la kwanza ambalo lazima utimize.

2. Lazima uombe juu ya msingi wa maneno yaliyonenwa na Mungu leo, uingie ndani ya maneno ya Mungu na uwasiliane kwa karibu na Mungu, na ufanye maazimio yako mbele ya Mungu, ni viwango vipi ambavyo ungependa kufuatilia ufanikishaji wake.

3. Lazima ufuatilie kuingia kwa maana sana ndani ya ukweli juu ya msingi wa kazi ya Roho Mtakatifu leo. Usishikilie matamshi na nadharia zilizopitwa na wakati kutoka zamani.

4. Lazima utafute kuguswa na Roho Mtakatifu, na kuingia katika maneno ya Mungu.

5. Lazima ufuatilie kuingia katika njia ambayo Roho Mtakatifu anatembea leo.

Na ni vipi ambavyo wewe hutafuta kuguswa na Roho Mtakatifu? Kilicho muhimu ni kuishi ndani ya maneno ya sasa ya Mungu, na kuomba juu ya msingi wa masharti ya Mungu. Baada ya kuomba kwa njia hii, Roho Mtakatifu kwa kweli atakugusa. Kama hutafuti kwa kutegemea msingi wa maneno yaliyonenwa na Mungu leo, basi hili ni bure. Unapaswa kuomba, na kusema: “Ee Mungu! Mimi hukupinga Wewe, na unanidai Mimi mengi sana; mimi ni mkaidi sana, na siwezi kamwe kukuridhisha Wewe. Ee Mungu, natamani Wewe uniokoe, natamani kukupa Wewe huduma hadi mwisho kabisa, natamani kufa kwa ajili Yako. Wewe hunihukumu na kuniadibu, na sina malalamiko; mimi hukupinga Wewe na nastahili kufa, ili watu wote waweze kutazama tabia Yako yenye haki katika kifo changu.” Wakati ambapo wewe huomba kutoka moyoni mwako kwa njia hii, Mungu atakusikia, na atakuongoza; kama huombi juu ya msingi wa maneno ya Roho Mtakatifu leo, basi hakuna uwezekano wa Roho Mtakatifu kukugusa wewe. Kama wewe huomba kwa kadri ya mapenzi ya Mungu, na kwa kadri ya kile ambacho Mungu hutaka kufanya leo, utasema: “Ee Mungu! Nataka kukubali maagizo Yako na kuwa mwaminifu kwa maagizo Yako, na niko radhi kuyatoa maisha yangu yote kwa utukufu Wako, ili yote nifanyayo yaweze kufikia kiwango cha watu wa Mungu. Moyo wangu na uweze kuguswa na Wewe. Nataka Roho Wako anipe nuru wakati wowote, kusababisha yote nifanyayo yalete aibu kwa Shetani, ili hatimaye nipatwe na Wewe.” Kama wewe huomba kwa njia hii, ukilenga mapenzi ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako bila kuzuilika. Haijalishi maneno ya maombi yako ni mangapi—kilicho muhimu ni kama unaelewa mapenzi ya Mungu au la. Huenda ninyi nyote mmekuwa na tukio lifuatalo: Wakati mwingine, ukiwa unaomba katika kusanyiko, nguvu za kazi ya Roho Mtakatifu hufikia kilele chake, kusababisha nguvu za kila mtu kuongezeka. Watu wengine hulia kwa uchungu na kutoa machozi huku wakiomba, kwa kulemewa na majuto mbele ya Mungu, na watu wengine huonyesha azimio lao, na kuweka nadhiri. Hiyo ndiyo athari ya kutimizwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Leo, ni ya muhimu sana kwamba watu wote wamimine mioyo yao kabisa ndani ya maneno ya Mungu. Usisisitize kwa maneno yaliyonenwa awali; kama bado unashikilia kilichokuja awali, basi Roho Mtakatifu hatafanya kazi ndani yako. Je, waona vile hili ni muhimu?

Je, mnajua njia ambayo Roho Mtakatifu hutembea leo? Mawazo makuu kadhaa hapo juu ni kile kitakachotimizwa na Roho Mtakatifu leo na katika siku za baadaye; ni njia inayofuatwa na Roho Mtakatifu, na kuingia ambako kunapaswa kufuatiliwa na mwanadamu. Katika kuingia kwako maishani, kwa kiasi kidogo sana lazima umimine moyo wako ndani ya maneno ya Mungu, na uweze kukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu; moyo wako lazima uwe na shauku kwa Mungu, lazima ufuatilie kuingia kwa maana sana katika ukweli, na malengo ambayo Mungu hutaka. Wakati ambapo unakuwa na nguvu hizi, basi hilo huonyesha kuwa umeguswa na Mungu, na moyo wako umeanza kuelekea kwa Mungu.

Hatua ya kwanza ya kuingia katika uzima ni kuumimina moyo wako kabisa ndani ya maneno ya Mungu, na hatua ya pili ni kukubali kuguswa na Roho Mtakatifu. Ni nini athari ya kutimizwa kwa kukubali kuguswa na Roho Mtakatifu? Kuweza kuwa na shauku ya, kutafuta, na kuchunguza ukweli wa maana sana, na kuwa na uwezo wa kushirikiana na Mungu katika njia nzuri. Leo, wewe hushirikiana na Mungu, ambalo ni kusema kuna lengo kwa ukimbizaji wako, kwa maombi yako, na kwa mawasiliano yako ya maneno ya Mungu, na wewe hutekeleza wajibu wako kwa mujibu wa masharti ya Mungu—huku pekee ndiko kushirikiana na Mungu. Ukizungumza tu kuhusu kumwacha Mungu atende, lakini usichukue hatua yoyote, wala kuomba au kutafuta, basi hili lingeweza kuitwa ushirikiano? Kama huna chochote kuhusu ushirikiano ndani yako, na umeondolewa mafunzo ya kuingia ambayo yana lengo, basi wewe hushirikiani? Watu wengine husema: “Kila kitu hutegemea majaaliwa ya Mungu, yote hufanywa na Mungu mwenyewe: kama Mungu hangelifanya, basi mwanadamu angewezaje?” Kazi ya Mungu ni ya kawaida, na siyo ya rohoni hata kidogo, na ni kupitia tu kwa utafutaji wako wa utendaji ndiyo Roho Mtakatifu hufanya kazi, kwani Mungu hamlazimishi mwanadamu—lazima umpe Mungu nafasi ya kufanya kazi, na kama hufuatilii au kuingia, na kama hakuna shauku hata kidogo ndani ya moyo wako, basi Mungu hana nafasi ya kufanya kazi. Ni kwa njia ipi ndio unaweza kutafuta kuguswa na Mungu? Kupitia maombi, na kuja karibu na Mungu. Lakini la muhimu zaidi, kumbuka, lazima iwe juu ya msingi wa maneno yanayonenwa na Mungu. Wakati ambapo unaguswa mara kwa mara na Mungu, hutawaliwi kabisa na mwili: Mume, mke, watoto, na pesa—yote ni yasiyoweza kukufunga wewe, na wewe hutamani kufuatilia tu ukweli na kuishi mbele ya Mungu. Wakati huu, utakuwa mtu anayeishi katika eneo la uhuru.

Umetoholewa kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 400)

Mungu ameamua kumfanya mwanadamu mkamilifu, na bila kujali mtazamo ambao Ananena kutoka, yote ni kwa sababu ya kuwafanya watu wawe wakamilifu. Maneno yanenwayo kutoka katika mtazamo wa Roho ni magumu kwa watu kuelewa; hawana namna ya kupata njia ya kutenda, kwa kuwa uwezo wao wa kuelewa ni finyu. Kazi ya Mungu inafikia matokeo tofauti, na katika kuchukua kila hatua ya kazi Ana kusudi Lake. Aidha, ni muhimu kwamba Azungumze kutoka katika mitazamo tofauti, kwa kuwa ni kwa kufanya hivyo tu ndipo Anaweza kumkamilisha mwanadamu. Kama Angetamka sauti Yake kutoka katika mtazamo wa Roho tu, hakungekuwa na njia yoyote ya kukamilisha hatua hii ya kazi ya Mungu. Kutoka katika sauti Anayozungumza nayo, unaweza kuona kwamba Amedhamiria kulifanya kundi hili la watu kamilifu. Kwa hivyo, hatua ya kwanza kwa kila anayetamani kukamilishwa inapasa kuwa ipi? Zaidi ya yote, lazima uijue kazi ya Mungu. Leo, njia mpya imeanza katika kazi ya Mungu; enzi imebadilika, namna ambavyo Mungu hufanya kazi pia imebadilika, na njia ambayo Mungu huzungumza ni tofauti. Leo, sio tu kwamba njia ya kazi Yake imebadilika, lakini pia enzi imebadilika. Sasa ni Enzi ya Ufalme. Pia ni Enzi ya kumpenda Mungu. Ni kionjo cha Enzi ya Ufalme wa Milenia—ambayo pia ni Enzi ya Neno, na ambayo Mungu hutumia njia nyingi za kunena ili kumkamilisha mwanadamu, na Ananena kutoka katika mitazamo tofauti ili kumruzuku mwanadamu. Baada ya kuingia katika Enzi ya Ufalme wa Milenia, Mungu ataanza kutumia maneno kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, Akimruhusu mwanadamu aingie katika uhalisi wa maisha na kumwongoza kwenye njia sahihi. Baada ya kupitia hatua nyingi za kazi ya Mungu, mwanadamu ameona kuwa kazi ya Mungu haibaki vile vile, lakini inageuka na kuongezeka kwa kina bila kukoma. Baada ya uzoefu wa muda mrefu kama huo, kazi imezunguka mara kwa mara, na kubadilika tena na tena, lakini bila kujali kiasi inachobadilika, kamwe haikengeuki kutoka kwa kusudi la Mungu la kufanya kazi kwa mwanadamu. Hata kupitia katika mabadiliko elfu kumi, kamwe haipotei kutoka katika kusudi lake la asili, wala kamwe haijitengi na ukweli au maisha. Mabadiliko katika njia ambayo kazi hufanywa inahusisha mabadiliko katika muundo wa kazi tu, na mtazamo ambao kwao Mungu ananena; hakuna mabadiliko katika kusudi kuu la kazi ya Mungu. Mabadiliko katika toni ya sauti ya Mungu na njia ya kazi Yake hufanywa ili kufikia matokeo. Mabadiliko katika toni ya sauti hayamaanishi mabadiliko katika madhumuni au kanuni ya kazi hiyo. Watu wanamwamini Mungu hasa ili kutafuta uzima; ikiwa unaamini katika Mungu lakini hutafuti uzima au hufuatilii ukweli au maarifa ya Mungu, basi hii siyo imani katika Mungu! Na, je, bado ni jambo lenye uhalisi kutafuta kuingia katika ufalme kuwa mfalme? Kufanikisha upendo wa kweli kwa Mungu kupitia kutafuta uzima—huu pekee ndio uhalisi; ufuatiliaji na utendaji wa ukweli—hivi vyote ni uhalisi. Kusoma maneno ya Mungu, na kuyapitia maneno haya, utakuja kufahamu maarifa ya Mungu katika uzoefu halisi, na hii ndiyo maana ya kufuatilia kweli.

Umetoholewa kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 401)

Sasa ni Enzi ya Ufalme. Ikiwa umeingia katika enzi hii mpya inategemea ikiwa umeingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu, ikiwa maneno Yake yamekuwa uhalisi wa maisha yako. Maneno ya Mungu yanafahamishwa kwa kila mtu ili, mwishowe, watu wote wataishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, na maneno Yake yatampa nuru na kumwangazia kila mtu kutoka ndani. Ikiwa, wakati huu, wewe ni mzembe katika kusoma maneno ya Mungu, na huna shauku ya maneno Yake, basi hili linaonyesha kuwa hali yako ni mbaya. Ikiwa huwezi kuingia katika Enzi ya Neno, basi Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yako; ikiwa umeingia katika enzi hii, Atafanya kazi Yake. Je, unaweza kufanya nini mwanzoni mwa Enzi ya Neno ili upate kazi ya Roho Mtakatifu? Katika enzi hii, na miongoni mwenu, Mungu atatimiza ukweli ufuatao: kwamba kila mtu ataishi kwa kuyadhihirisha maneno ya Mungu, ataweza kuuweka ukweli katika vitendo, na atampenda Mungu kwa dhati; kwamba watu wote watatumia maneno ya Mungu kama msingi na kama uhalisi wao, na watakuwa na mioyo inayomcha Mungu; na kwamba, kupitia kutenda maneno ya Mungu, mwanadamu kisha atashikilia mamlaka ya kifalme pamoja na Mungu. Hii ndiyo kazi inayopaswa kufanikishwa na Mungu. Je, unaweza kuishi bila kusoma maneno ya Mungu? Leo, kuna wengi ambao wanahisi kuwa hawawezi kuishi hata siku moja au mbili bila kusoma maneno Yake. Lazima wayasome maneno Yake kila siku, na ikiwa muda hauruhusu, kuyasikiza kutatosha. Hii ndiyo hisia ambayo Roho Mtakatifu huwapa watu, na ndiyo njia ambayo Anaanza kuwagusa. Yaani, Yeye huwatawala watu kupitia maneno, ili kwamba waweze kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Ikiwa, baada ya siku moja tu bila kula na kunywa maneno ya Mungu, unahisi giza na kiu, na huwezi kustahimili hali hiyo, hili linaonyesha kwamba umeguswa na Roho Mtakatifu, na kwamba Hajakukuacha. Wewe basi, ni mtu aliye kwenye mkondo huu. Hata hivyo, ikiwa baada ya siku moja au mbili bila kula na kunywa maneno ya Mungu, huhisi kitu, ikiwa huna kiu, na hujaguswa hata kidogo, hili linaonyesha kwamba Roho Mtakatifu amekuacha. Hili linamaanisha, basi, kwamba kuna kitu kibaya na hali yako; hujaingia katika Enzi ya Neno, na wewe ni mmoja wa wale ambao wamebaki nyuma. Mungu hutumia maneno kuwatawala watu; unahisi vizuri ukila na kunywa maneno ya Mungu, na usipokula na kunywa maneno ya Mungu, huna njia ya kufuata. Maneno ya Mungu huwa chakula cha watu, na nguvu inayowaendesha. Biblia inasema “Mwanadamu hataishi kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu”. Leo, Mungu ataikamilisha kazi hii, naye Ataukamilisha ukweli huu ndani yenu. Ni vipi kwamba hapo zamani, watu wangeweza kwenda siku nyingi bila kusoma maneno ya Mungu na bado waweze kula na kufanya kazi kama kawaida, lakini hivi sivyo ilivyo leo? Katika enzi hii, Mungu haswa hutumia maneno kutawala vyote. Kupitia katika maneno ya Mungu, mwanadamu anahukumiwa na kukamilishwa, kisha hatimaye kupelekwa katika ufalme. Maneno ya Mungu tu ndiyo yanayoweza kuyaruzuku maisha ya mwanadamu, na ni maneno ya Mungu tu yanayoweza kumpa mwanadamu mwangaza na njia ya kutenda, hasa katika Enzi ya Ufalme. Alimradi hupotei kutoka katika ukweli wa maneno ya Mungu, kula na kunywa maneno Yake kila siku, Mungu ataweza kukufanya mkamilifu.

Umetoholewa kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 402)

Ufuatiliaji wa maisha si jambo ambalo linaweza kuharakishwa; ukuaji wa maisha haufanyiki kwa siku moja au mbili. Kazi ya Mungu ni ya kawaida na ya vitendo, na kuna mchakato ambao lazima ipitie. Ilimchukua Yesu mwenye mwili miaka thelathini na mitatu na nusu kukamilisha kazi Yake ya kusulubiwa—sembuse kazi ya kumtakasa mwanadamu na kuyabadilisha maisha yake, kazi ngumu zaidi? Sio kazi rahisi kumfanya mwanadamu wa kawaida ambaye anamdhihirisha Mungu. Hili ni hivyo hasa kwa watu ambao wamezaliwa katika taifa la joka kubwa jekundu, ambao ni wenye ubora duni wa tabia na wanahitaji muda mrefu wa maneno na kazi ya Mungu. Kwa hivyo usiwe bila subira kutaka kuona matokeo. Lazima uwe mwenye kujitolea katika kula na kunywa maneno ya Mungu, na uweke bidii zaidi katika maneno ya Mungu. Unapomaliza kusoma maneno Yake, lazima uweze kuyaweka katika vitendo halisi, ukikua katika maarifa, ufahamu, utambuzi, na hekima katika maneno ya Mungu. Kupitia katika hili, utabadilika bila kufahamu. Ikiwa unaweza kuchukua kula na kunywa maneno ya Mungu kama kanuni yako, ukiyasoma, ukija kuyajua, kuyapitia, na kuyatenda, utakuwa mkomavu bila kufahamu. Kuna wale ambao wanasema kuwa hawawezi kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo hata baada ya kuyasoma. Haraka yako ni nini? Utakapofikia kimo fulani, utaweza kuyaweka maneno Yake katika vitendo. Je, mtoto wa umri wa miaka minne au mitano anaweza kusema kuwa hawezi kuwasaidia au kuwaheshimu wazazi wake? Unapaswa kujua jinsi kimo chako cha sasa kilivyo kikubwa. Weka katika vitendo kile unachoweza kuweka katika vitendo, na uepukane na kuwa mtu ambaye anasumbua usimamizi wa Mungu. Kula na kunywa maneno ya Mungu tu, na ulichukue hilo kama kanuni yako kuanzia sasa kuendelea. Usijali, kwa wakati huu, kuhusu ikiwa Mungu anaweza kukufanya mkamilifu. Usilichunguze hilo kwa sasa. Kula na kunywa maneno ya Mungu tu yanavyokujia, na Mungu hakika Atakufanya mkamilifu. Hata hivyo, kuna kanuni ambayo kwayo lazima ule na kunywa maneno Yake. Usifanye hivyo tu bila kufikiria. Katika kula na kunywa maneno ya Mungu, kwa upande mmoja, yatafute maneno ambayo unapaswa kuyajua—yaani, yale yanayohusiana na maono—na kwa upande mwingine, tafuta kile unachopaswa kuweka katika vitendo halisi—yaani, kile unachopaswa kuingia ndani. Kipengele kimoja kinahusiana na maarifa, na kingine kinahusiana na kuingia. Mara unapovifahamu vyote viwili—wakati umeshaelewa kile unachopaswa kujua na kile unachopaswa kutenda utajua jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 403)

Kuanzia sasa kuendela, mazungumzo ya maneno ya Mungu yanapaswa kuwa kanuni ambayo kwayo unazungumza. Kwa kawaida, mnapojumuika pamoja, mnapaswa kushiriki katika ushirika kuhusu maneno ya Mungu, mkiyachukua maneno ya Mungu kama maudhui ya mwingiliano wenu, mkiongea juu ya yale mnayojua kuhusu maneno haya, jinsi mnavyoyaweka katika vitendo, na jinsi Roho Mtakatifu afanyavyo kazi. Alimradi unashiriki maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu atakupa nuru. Kufanikisha ulimwengu wa maneno ya Mungu kunahitaji ushirikiano wa mwanadamu. Usipoingia katika hili, Mungu hatakuwa na njia ya kufanya kazi; ukiufunga mdomo wako na usizungumze kuhusu maneno Yake, Hatakuwa na njia ya kukuangazia. Wakati wowote ambapo huna shughuli nyingine, zungumza juu ya maneno ya Mungu, na usijishughulishe na mazungumzo yasiyo na maana! Acha maisha yako yajazwe na maneno ya Mungu—ni hapo tu ndipo utakapokuwa mwumini mwenye kumcha Mungu. Haijalishi ikiwa ushirika wako ni wa juu juu. Bila ujuu juu hakuwezi kuwepo kina kirefu. Lazima kuwe na mchakato. Kupitia mafunzo yako, utafahamu kuangaziwa kwako na Roho Mtakatifu, na jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu kwa matokeo yanayotarajiwa. Baada ya muda wa uchunguzi, utaingia katika ukweli wa maneno ya Mungu. Ni ukiamua kushirikiana tu ndipo utaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu.

Kati ya kanuni za kula na kunywa maneno ya Mungu, moja inahusiana na maarifa, na nyingine inahusiana na kuingia. Ni maneno yapi unayopaswa kujua? Unapaswa kujua maneno yanayohusiana na maono (kama vile, yale yanayohusiana na ni enzi ipi ambayo kazi ya Mungu imeingia sasa, kile ambacho Mungu anataka kufanikisha sasa, kupata mwili ni nini, na kadhalika; haya yote yanahusiana na maono). Je, njia ambayo mwanadamu anapaswa kuingia katika inamaanisha nini? Hii inahusu maneno ya Mungu ambayo mwanadamu anapaswa kutenda na kuingia ndani. Yaliyo hapo juu ni vipengele viwili vya kula na kunywa maneno ya Mungu. Kuanzia sasa, kula na kunywa maneno ya Mungu kwa njia hii. Ukiwa na ufahamu wazi wa maneno Yake kuhusu maono, basi hakuna haja ya kuendelea kusoma kila wakati. Jambo la umuhimu wa msingi ni kula na kunywa maneno zaidi ya kuingia, kama vile kuugeuza moyo wako kwa Mungu, jinsi ya kuutuliza moyo wako mbele za Mungu, na jinsi ya kuunyima mwili. Hivi ni vitu ambavyo unapaswa kuweka katika vitendo. Bila kujua jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu, ushirika wa kweli hauwezekani. Mara tu unapojua jinsi ya kula na kunywa maneno Yake, wakati ambapo umeelewa kile kilicho muhimu, ushirika utakuwa wazi, na suala lolote liibuliwalo, utaweza kushirikiana na kufahamu uhalisi. Ikiwa, wakati unashiriki kuhusu maneno ya Mungu, huna uhalisi wowote, basi hujaelewa kile kilicho cha muhimu, ambalo linaonyesha kuwa hujui jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu. Watu wengine wanaweza kupata kusoma maneno ya Mungu kuwa jambo la kuchosha, ambayo sio hali ya kawaida. Kilicho cha kawaida ni kamwe kutochoka kuyasoma maneno ya Mungu, kuwa na kiu ya maneno hayo kila wakati, na daima kuyaona maneno ya Mungu kuwa mazuri. Hivi ndivyo mtu ambaye ameingia kwa kweli hula na kunywa maneno ya Mungu. Unapohisi kuwa maneno ya Mungu ni ya vitendo sana na ndiyo mwanadamu anapaswa kuingia katika hasa; unapohisi kuwa maneno Yake ni ya msaada mkubwa na yenye faida kwa mwanadamu, na kwamba ni riziki ya maisha ya mwanadamu—ni Roho Mtakatifu anayekupa hisia hii, na Roho Mtakatifu anayekugusa. Hii inathibitisha kuwa Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako na kwamba Mungu hajakuacha. Watu wengine, wakiona kuwa Mungu huzungumza kila wakati, huchoka na maneno Yake, na hufikiria kwamba haina athari wakiyasoma au la—ambayo si hali ya kawaida. Wanakosa moyo ambao unatamani kuingia katika uhalisi, na watu kama hao hawana kiu wala hawaoni umuhimu wa kukamilishwa. Kila unapopata kuwa huna kiu ya maneno ya Mungu, hii inaonyesha kuwa hauko katika hali ya kawaida. Hapo zamani, ikiwa Mungu angekuwa Amekuacha kungeweza kuamuliwa na ikiwa ulikuwa na amani ndani yako, na ikiwa uliona furaha. Sasa cha muhimu ni ikiwa una kiu ya maneno ya Mungu, ikiwa maneno Yake ni uhalisi wako, ikiwa wewe ni mwaminifu, na ikiwa unaweza kumfanyia Mungu yote uwezayo. Kwa maneno mengine, mwanadamu anahukumiwa na uhalisi wa maneno ya Mungu. Mungu huelekeza maneno Yake kwa binadamu wote. Ikiwa uko tayari kuyasoma, Atakupa nuru, lakini ikiwa hauko tayari, Hatafanya hivyo. Mungu huwapa nuru wale ambao wana njaa na kiu ya haki, na Huwapa nuru wale wanaomtafuta. Wengine husema kwamba Mungu hakuwapa nuru hata baada ya kusoma maneno Yake. Lakini uliyasoma maneno haya kwa njia gani? Ukiyasoma maneno Yake kama ambavyo mtu asiye ba shauku, na usiweke umuhimu katika uhalisi, Mungu angewezaje kukupa nuru? Mtu ambaye hayathamini maneno ya Mungu anawezaje kufanywa mkamilifu na Yeye? Ikiwa huyathamini maneno ya Mungu, basi hutakuwa na uhalisi wala ukweli. Ikiwa unayathamini maneno Yake, basi utaweza kuuweka ukweli katika vitendo, na ni hapo tu ndipo utakapomiliki uhalisi. Hii ndiyo maana lazima ule na kunywa maneno ya Mungu wakati wote, iwe una shughuli nyingi au la, hali iwe mbaya au la, na iwe unajaribiwa au la. Kwa jumla, maneno ya Mungu ndiyo msingi wa kuwepo kwa mwanadamu. Hakuna anayeweza kuyaepuka maneno Yake, lakini lazima ale maneno Yake kama anavyokula milo mitatu ya siku. Je, kufanywa mkamilifu na kupatwa na Mungu kunaweza kuwa rahisi vile? Ikiwa wewe unaelewa kwa sasa au la, na ikiwa una utambuzi juu ya kazi ya Mungu au la, lazima ule na kunywa maneno mengi ya Mungu iwezekanavyo. Huku ni kuingia kwa njia ya vitendo. Baada ya kusoma maneno ya Mungu, harakisha kutia katika vitendo kile unachoweza kuingia katika, na uweke kando kwa sasa kile ambacho huwezi. Kunaweza kuwa na maneno mengi ya Mungu ambayo huwezi kuelewa mwanzoni, lakini baada ya miezi miwili au mitatu, pengine hata mwaka, utayaelewa. Je, hili linawezekanaje? Ni kwa sababu Mungu hawezi kuwakamilisha watu kwa siku moja au mbili. Wakati mwingi, unaposoma maneno Yake, huenda usielewe papo hapo. Wakati huo, yanaweza kuonekana kama maandishi tu; lazima uyapitie kwa muda kabla ya kuyaelewa. Mungu akiwa Amezungumza mengi sana, unapaswa kufanya kila uwezalo kula na kunywa maneno Yake, kisha, bila ya wewe kutambua, utakuja kuelewa, na bila wewe kutambua, Roho Mtakatifu atakupa nuru. Roho Mtakatifu anapompa mwanadamu nuru, mara nyingi huwa bila ufahamu wa mwanadamu. Yeye hukupa nuru na kukuongoza unapoona kiu na kutafuta. Kanuni ambayo kwayo Roho Mtakatifu hufanya kazi ina msingi katika maneno ya Mungu ambayo wewe hula na kunywa. Wale wote ambao hawaweki umuhimu katika maneno ya Mungu na daima huwa wenye mtazamo tofauti kwa maneno Yake—wakiamini, katika fikira zao zilizochanganyikiwa, kuwa ni jambo lisilo na athari yoyote wakisoma maneno Yake au la—ni wale ambao hawana uhalisi. Kazi ya Roho Mtakatifu wala utoaji nuru Wake haviwezi kuonekana ndani ya mtu kama huyo. Watu kama hawa wanasairi tu, wanaojifanya na wasio na sifa za kweli, kama Bwana Nanguo wa mfano.[a]

Umetoholewa kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

a. Maandishi ya asili hayana maneno “wa mfano.”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 404)

Maneno ya Mungu yanapotokea, unapaswa kuyapokea mara moja, na kuyala na kuyanywa. Haijalishi wewe unaelewa kiasi gani, mtazamo mmoja ambao lazima ushikilie imara ni kula na kunywa, kujua, na kutebda maneno Yake. Hiki ni kitu ambacho unapaswa kuweza kufanya. Kamwe usijali kuhusu jinsi kimo chako kinavyoweza kuwa kikubwa; lenga tu kula na kunywa maneno Yake. Hiki ndicho mwanadamu anapaswa kushiriki katika. Maisha yako ya kiroho hasa ni kujaribu kuingia katika ukweli wa kula na kunywa maneno ya Mungu na kuyaweka katika vitendo. Sio shughuli yako kulenga juu ya kitu kingine chochote. Viongozi wa kanisa wanapaswa kuwaongoza ndugu zao wote ili wajue jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu. Hili ndilo jukumu la kila kiongozi wa kanisa. Wawe wachanga au wazee, wote wanapaswa kuzingatia kula na kunywa maneno ya Mungu kama jambo lenye umuhimu mkubwa na wanapaswa kuwa na maneno Yake mioyoni mwao. Kuingia katika ukweli huu kunamaanisha kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, watu wengi wanahisi kuwa hawawezi kuishi bila kula na kunywa maneno ya Mungu, na wanahisi kuwa maneno Yake ni mapya bila kujali wakati. Hii inamaanisha kuwa wanaanza kwenda katika njia sahihi. Mungu hutumia maneno kufanya kazi Yake na kumruzuku mwanadamu. Wakati kila mtu anatamani na kuwa na kiu ya maneno ya Mungu, binadamu wataingia katika ulimwengu wa maneno Yake.

Mungu amezungumza mengi sana. Je, ni kiasi gani ambacho wewe umepata kujua? Umeingia kwa kiasi gani? Kama kiongozi wa kanisa hajawaongoza ndugu zake kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu, basi atakuwa hajatimiza wajibu wake, na atakuwa ameshindwa kutekeleza majukumu yake! Kula na kunywa kwako kwa maneno ya Mungu kuwe ni kwa kina au kwa juu juu, bila kujali kiwango chako cha kuelewa, lazima ujue jinsi ya kula na kunywa maneno Yake, lazima uwe makini sana na maneno Yake, na uelewe umuhimu na haja ya kuyala na kuyanywa. Kwa kuwa Mungu amezungumza sana, usipokula na kunywa maneno Yake, au kujaribu kutafuta, au kuyaweka maneno Yake katika vitendo, huku hakuwezi kuitwa kumwamini Mungu. Kwa kuwa unamwamini Mungu, basi lazima uyale na kuyanywa maneno Yake, uyapitie maneno Yake, na uishi kwa kuyadhihirisha maneno Yake. Hii tu ndiyo inayoweza kuitwa imani katika Mungu! Ukisema kwa mdomo wako kwamba unamwamini Mungu lakini huwezi kuyaweka maneno Yake yoyote katika vitendo au kutoa ukweli wowote, huku hakuitwi kumwamini Mungu. Badala yake, ni "kutafuta mkate ili kumaliza njaa." Kuzungumza tu kuhusu ushuhuda mdogo, vitu visivyo na maana, na mambo ya juujuu, bila kuwa hata na ukweli mdogo kabisa: hivi havijumuishi imani katika Mungu, na hujafahamu tu njia sahihi ya kuamini katika Mungu. Kwa nini lazima ule na kunywa maneno mengi ya Mungu iwezekanavyo? Usipokula na kunywa maneno Yake lakini utafute tu kupaa mbinguni, je, huko ni kumwamini Mungu? Je, hatua ya kwanza ambayo mtu amwaminiye Mungu anapaswa kuchukua ni ipi? Ni kwa njia gani ndiyo Mungu humkamilisha mwanadamu? Je, unaweza kukamilishwa bila kula na kunywa maneno ya Mungu? Je, unaweza kuchukuliwa kama mtu wa ufalme bila ya maneno ya Mungu kutumika kama ukweli wako? Je, ni nini hasa maana ya imani katika Mungu? Waumini katika Mungu wanapaswa, angalau, kuwa na tabia njema kwa nje; la muhimu zaidi ni kuwa na maneno ya Mungu. Bila kujali chochote, kamwe huwezi kuyaacha maneno Yake. Kumjua Mungu na kutimiza nia Zake vinafanikishwa kupitia katika maneno Yake. Katika siku zijazo, kila taifa, dhehebu, dini, na sehemu zitashindwa kwa njia ya maneno ya Mungu. Mungu atazungumza moja kwa moja, na watu wote watashikilia maneno ya Mungu mikononi mwao, na kwa njia hii, binadamu watakamilishwa. Ndani na nje, maneno ya Mungu yanapenyeza kotekote: Binadamu watazungumza maneno ya Mungu kwa vinywa vyao, watende kulingana na maneno ya Mungu, na kuweka maneno ya Mungu ndani, wakisalia wamelowa na maneno ya Mungu ndani na nje. Hivi ndivyo binadamu watakamilishwa. Wale wanaotimiza nia za Mungu na wanaweza kumshuhudia, hawa ni watu wanaomiliki maneno ya Mungu kama ukweli wao.

Kuingia katika enzi ya Neno—Enzi ya Ufalme wa Milenia—ni kazi ambayo inatimizwa leo. Kuanzia sasa kuendelea, fanya mazoezi ya ushirika kuhusu maneno ya Mungu. Ni kwa njia ya kula na kunywa na pia kupitia maneno ya Mungu ndiyo utaweza kuishi kwa kuyadhihirisha maneno ya Mungu. Lazima uwe na uzoefu wa vitendo ili uwashawishi wengine. Ikiwa huwezi kuishi kwa kuudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu, hakuna atakayeshawishika! Wale wote wanaotumiwa na Mungu wanaweza kuishi kwa kuudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu. Ikiwa huwezi kutoa ukweli huu na kumshuhudia Mungu, hii inaonyesha kwamba Roho Mtakatifu hajafanya kazi ndani yako, na kwamba wewe hujakamilishwa. Huu ndio umuhimu wa maneno ya Mungu. Je, wewe una moyo wenye kiu ya maneno ya Mungu? Wale ambao wana kiu ya maneno ya Mungu wana kiu ya ukweli, na watu tu kama hawa tu ndio ambao hubarikiwa na Mungu. Katika siku zijazo, kuna maneno mengi zaidi ambayo Mungu atanena kwa dini zote na madhehebu yote. Kwanza Ananena na kutamka sauti Yake kati yenu ili Awakamilishe kabla ya kusonga mbele kunena na kutamka sauti Yake kati ya watu wa Mataifa ili Awashinde. Kupitia katika maneno Yake, wote watashawishika kwa dhati na kikamilifu. Kupitia katika maneno ya Mungu na ufunuo Wake, tabia potovu ya mwanadamu inapungua, anapata kuonekana kwa mwanadamu, na tabia yake ya uasi inapungua. Maneno hayo hufanya kazi kwa mwanadamu kwa mamlaka na humshinda mwanadamu katika nuru ya Mungu. Kazi ambayo Mungu hufanya katika enzi ya sasa, na vile vile mabadiliko ya kazi Yake, yote yanaweza kupatikana ndani ya maneno Yake. Usiposoma maneno Yake, hutaelewa chochote. Kupitia kula kwako na kunywa maneno Yake, na kupitia kushiriki katika ushirika na ndugu na uzoefu wako halisi, utapata ufahamu kamili wa maneno ya Mungu. Ni hapo tu ndipo utaweza kweli kuishi kwa kudhihirisha ukweli wake.

Umetoholewa kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 405)

Nimesema hapo awali kuwa “Wale wote wanaoangazia kuona ishara na maajabu watatelekezwa; wao sio wale watakaofanywa wakamilifu.” Nimenena maneno mengi sana, ilhali mwanadamu hana maarifa hata kidogo ya kazi hii, na, baada ya kufika katika hatua hii, bado mwanadamu anaulizia ishara na maajabu. Je, kuamini kwako kwa Mungu ni harakati ya kuona ishara na maajabu, au ni kwa sababu ya kupata uzima? Yesu pia Alinena maneno mengi, na mengine bado hayajatimika leo. Je unaweza kusema kuwa Yesu sio Mungu? Mungu alishuhudia kuwa Yeye ni Kristo na ni Mwana mpendwa wa Mungu. Je unaweza kukataa haya? Leo, Mungu anazungumza tu maneno, na iwapo huna uwezo wa kufahamu kabisa, basi huwezi kusimama kidete. Je unamwamini kwa sababu Yeye ni Mungu, au unamwamini kwa msingi kwamba maneno Yake yatatimika au la? Je unaamini katika ishara na maajabu, au unaamini katika Mungu? Leo, Haonyeshi ishara na maajabu—je Yeye kweli ni Mungu? Iwapo maneno Anayonena hayatimiki, je Yeye kweli ni Mungu? Je dutu ya Mungu inaamuliwa na iwapo maneno Anenayo yatatimika au hapana? Ni kwa nini watu wengine daima hungoja kutimika kwa maneno ya Mungu kabla ya kumwamini? Je hii si maana kwamba hawamjui? Wote walio na dhana za aina hii ni watu wanaomkana Mungu. Wanatumia dhana kumpima Mungu; maneno ya Mungu yakitimika wanamwamini Mungu, na yasipotimika hawamwamini Mungu; na kila wakati wanatafuta kuona ishara na maajabu. Je wao si Mafarisayo wa wakati wa sasa? Kama unaweza ama huwezi kusimama imara kunategemea iwapo unamjua ama humjui Mungu wa kweli—hili ni muhimu! Jinsi ulivyo ukuu wa uhalisi wa neno la Mungu ndani Yako, ndivyo ulivyo ukubwa wa maarifa yako kuhusu uhakika wa Mungu, na ndivyo utaweza kusimama kidete katika majaribu. Kadri unavyotazamia kuona ishara na maajabu, ndivyo utakavyokosa zaidi kusimama imara, na utaanguka katika majaribu. Ishara na maajabu sio msingi; uhakika wa Mungu tu ndio uzima. Watu wengine hawajui matokeo yanayotokana na kazi ya Mungu. Wanaishi katika mshangao kila siku, wakikosa kutafuta ufahamu wakazi ya Mungu. Harakati zao ni kumfanya Mungu atimize mapenzi yao, na ni baada tu ya haya ndio wawe makini katika imani yao. Wanasema kuwa watautafuta uzima iwapo maneno ya Mungu yatatimika, lakini iwapo maneno ya Mungu hayatatimika, basi hakuna uwezekano wa wao kuutafuta uzima. Mwanadamu anafikiri kuwa imani kwa Mungu ni kutafuta kuona ishara na maajabu na harakati ya kupanda mbinguni na mbingu ya tatu. Hakuna asemaye kuwa imani yake kwa Mungu ni harakati ya kuingia katika ukweli, kutafuta uzima, na kutafuta kupatwa na Mungu. Harakati ya aina hii ina thamani gani? Wale wasiofuata ufahamu wa Mungu na kuridhika kwa Mungu ni watu ambao hawamwamini Mungu, ni watu ambao hukufuru Mungu!

Je sasa mnaelewa imani kwa Mungu ni nini? Je kuamini Mungu ni kuona ishara na maajabu? Je ni kupanda mbinguni? Kuamini Mungu sio rahisi hata kidogo. Zile desturi za kidini lazima zitakaswe; kufuata uponyaji wa wagonjwa na kukemea mapepo, kusisitiza ishara na maajabu, kutamani zaidi neema, amani na furaha ya Mungu, kufuata mandhari na raha za mwili—haya ni matendo ya kidini, na matendo haya ya aina hii ya kidini ni aina ya imani isiyo dhahiri. Leo, imani ya kweli kwa Mungu ni nini? Ni kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha yako na kumjua Mungu kutoka kwa neno Lake ili uufikie upendo wa kweli Kwake. Kuondoa tashwishi: Imani katika Mungu ni ili uweze kumtii Mungu, kumpenda Mungu, na kufanya majukumu ambayo kiumbe wa Mungu anapaswa kufanya. Hili ndilo lengo la kuamini katika Mungu. Lazima upate ufahamu wa upendo wa Mungu, jinsi Mungu anavyostahili heshima, jinsi, katika viumbe Vyake, Mungu anafanya kazi ya wokovu na kuwafanya wakamilifu—hicho ndicho kiasi cha chini zaidi unachopaswa kuwa nacho katika imani yako kwa Mungu. Imani kwa Mungu hasa ni mabadiliko kutoka kwa maisha katika mwili kwenda kwa maisha ya kumpenda Mungu, kutoka maisha ya kiasili kwenda kwa maisha katika nafsi ya Mungu, ni kutoka kumilikiwa na Shetani na kuishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, ni kuweza kupata kumtii Mungu na sio kuutii mwili, ni kukubali Mungu kuupata moyo wako wote, kukubali Mungu akufanye mkamilifu, na kujitoa kutoka kwa tabia potovu ya kishetani. Imani kwa Mungu kimsingi ni kwa kuwezesha nguvu na sifa za Mungu kudhihirishwa kwako, ili uweze kufanya mapenzi ya Mungu, na kutimiza mpango wa Mungu, na uweze kutoa ushuhuda kwa Mungu mbele ya Shetani. Imani kwa Mungu haipaswi kuwa kwa ajili ya kuona ishara na maajabu, wala haipaswi kuwa kwa ajili ya mwili wako mwenyewe. Inapaswa kuwa kwa ajili ya kutafuta kumjua Mungu, na kuweza kumtii Mungu, na kama Petro, kumtii mpaka kifo. Hili ndilo imani hiyo inapaswa kupata. Kula na kunywa neno la Mungu ni kwa ajili ya kumjua Mungu na kumtosheleza Mungu. Kula na kunywa neno la Mungu kunakupa maarifa kubwa ya Mungu, na ndipo tu utakapoweza kumtii. Ukiwa na maarifa ya Mungu tu ndipo unapoweza kumpenda, na hili ndilo lengo ambalo mwanadamu anapaswa kuwa nalo katika imani yake kwa Mungu. Iwapo katika imani yako kwa Mungu, unajaribu kila wakati kuona ishara na maajabu, basi mtazamo wa imani hii kwa Mungu si sahihi. Imani kwa Mungu ni hasa kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha. Ni kuweka tu katika matendo maneno ya Mungu kutoka kwa kinywa Chake na kuyatekeleza mwenyewe ndiko kupatikana kwa lengo la Mungu. Katika kuamini Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kufanywa mkamilifu na Mungu, kuweza kujiwasilisha kwa Mungu, na kumtii Mungu kikamilifu. Iwapo unaweza kumtii Mungu bila kulalamika, kuyajali mapenzi ya Mungu, kupata kimo cha Petro, na kuwa na mtindo wa Petro ilivyozungumziwa na Mungu, basi hapo ndipo utakuwa umefanikiwa katika imani kwa Mungu, na itadhihirisha kuwa umepatwa na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:X. Kuingia Katika Uzima

Inayofuata:Kuingia Katika Uzima (II)

Maudhui Yanayohusiana