Hatua Tatu za Kazi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 1)

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. Ni ili kuonyesha hekima Yangu na kudura na wakati uo huo kufichua ubovu wa Shetani usiovumilika. Aidha, ni ili kufundisha viumbe Wangu kubagua kati ya mema na mabaya, kutambua kwamba Mimi ndiye Mtawala wa vitu vyote, kuona wazi kwamba Shetani ni adui wa binadamu, wa chini kuliko wote, yule mwovu, na kujua, kwa uhakika kabisa tofauti kati ya mema na mabaya, ukweli na uwongo, utakatifu na uchafu, kilicho kikuu na kilicho cha aibu. Kwa njia hii, binadamu wasiofahamu wataweza kunishuhudia kwamba si Mimi Ninayewapotosha wanadamu, na kwamba ni Mimi tu—Bwana wa viumbe—Ninayeweza kumwokoa binadamu, Ninayeweza kumpa mwanadamu vitu kwa ajili ya raha yake; na atapata kujua kwamba Mimi Ndimi Mtawala wa vitu vyote na Shetani ni mmoja tu wa viumbe niliowaumba na ambaye baadaye alinigeuka. Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita umegawanywa katika hatua tatu ili kufikia matokeo yafuatayo: kuruhusu viumbe Wangu wawe mashahidi Wangu, kuelewa mapenzi Yangu, na wajue kwamba Mimi Ndimi ukweli. Hivyo, wakati wa awamu ya kwanza ya kazi ya katika Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita, Nilifanya kazi ya sheria, ambayo ilikuwa ndiyo kazi ambayo kwayo Yehova aliwaongoza watu Wake. Hatua ya pili ilianzisha kazi ya Enzi ya Neema katika vijiji vya Yudea. Yesu Anawakilisha kazi yote ya Enzi ya Neema; Alipata mwili na kusulubiwa, na pia Akazindua Enzi ya Neema. Alisulubiwa ili kukamilisha kazi ya ukombozi, ili kumaliza Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema, na hivyo Yeye Aliitwa “Kamanda Mkuu”, “Sadaka ya Dhambi,” “Mkombozi.” Kwa hiyo kazi ya Yesu ilitofautiana katika maudhui na kazi ya Yehova, ingawa zilikuwa sawa katika kanuni. Yehova Alianzisha Enzi ya Sheria, Akaunda msingi wa nyumbani, yaani, mahali pa asili, pa kazi Yake hapa duniani, na Akatoa amri na sheria. Hizi ndizo sehemu mbili za kazi Aliyotekeleza, na zinawakilisha Enzi ya Sheria. Kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema haikuwa kutoa sheria bali kuzitimiza, na hivyo kukaribisha Enzi ya Neema na kuhitimisha Enzi ya Sheria ambayo ilidumu kwa miaka elfu mbili. Alikuwa mwanzilishi, aliyekuja ili kuianzisha Enzi ya Neema, ilhali ukombozi ulibakia msingi wa kazi Yake. Na hivyo mafanikio Yake yalikuwa pia mara mbili: kufungua enzi mpya, na kukamilisha kazi ya ukombozi kupitia kusulubiwa Kwake, nakisha Akaondoka. Na hapo ndipo Enzi ya Sheria ilifikia mwisho wake na Enzi ya Neema ikaanza.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 2)

Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika hatua tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Hatua hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, yaani, ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu ambao wamepotoshwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati uo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani. Hivyo, kama kazi ya wokovu ilivyogawanywa katika hatua tatu, kwa hivyo pia vita dhidi ya Shetani vimegawanywa katika hatua tatu, na vipengele hivi viwili vya kazi ya Mungu vinafanywa sawia. Vita dhidi ya Shetani kwa kweli ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, na kwa kuwa kazi ya wokovu wa wanadamu silo jambo linaloweza kukamilishwa kwa mafanikio katika hatua moja, vita dhidi ya Shetani pia vimegawanywa katika hatua na vipindi, na vita vinapiganwa dhidi ya Shetani kulingana na mahitaji ya mwanadamu na kiwango cha kupotoshwa kwa mwanadamu na Shetani. Pengine, katika mawazo ya mwanadamu, anaamini kuwa katika vita hivi Mungu atajiandaa kupigana na Shetani, katika njia sawa na vile ambavyo majeshi mawili yangepigana. Hili tu ni jambo ambalo akili ya mwanadamu ina uwezo wa kukisia, na ni wazo lisilo dhahiri kupita kiasi na lisiloweza kutendeka, na bado ndilo mwanadamu analiamini. Na kwa sababu Nasema hapa kuwa njia ya wokovu wa mwanadamu ni kupitia vita na Shetani, mwanadamu anawaza ya kwamba hivi ndivyo vita vinavyoendeshwa. Katika kazi ya wokovu wa mwanadamu, hatua tatu zimefanywa, ambayo ni kusema kuwa vita na Shetani vimegawanyika katika hatua tatu kabla ya kushindwa kabisa kwa Shetani. Na bado ukweli wa ndani wa kazi yote ya vita dhidi ya Shetani ni kwamba matokeo yake yanatimizwa kupitia kwa hatua kadhaa za kazi: kumpa mwanadamu neema, na kuwa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, kuzisamehe dhambi za mwanadamu, kumshinda mwanadamu, na kumfanya mwanadamu akamilishwe. Kusema ukweli, vita na Shetani hajiandai kupigana na Shetani, bali ni wokovu wa mwanadamu, kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kubadilishwa kwa tabia ya mwanadamu ili kwamba aweze kumshuhudia Mungu. Hivi ndivyo Shetani anashindwa. Shetani anashindwa kwa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Wakati Shetani ameshindwa, yaani, wakati mwanadamu ameokolewa kabisa, basi Shetani aliyeaibika atafungwa kabisa, na kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kiini cha wokovu wa mwanadamu ni vita dhidi ya Shetani, na vita na Shetani vitajitokeza kimsingi katika wokovu wa mwanadamu. Hatua ya siku za mwisho, ambapo mwanadamu atashindwa, ni hatua ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na pia kazi ya wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Maana ya ndani ya ushindi wa mwanadamu ni kurudi kwa mfano halisi wa Shetani, mtu ambaye amepotoshwa na Shetani, kwa Muumba baada ya ushindi wake, kwa njia ambayo atamwacha Shetani na kurejea kabisa kwa Mungu. Kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni kazi ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na hatua ya mwisho katika kazi ya Mungu ya usimamizi kwa ajili ya kushindwa kwa Shetani. Bila kazi hii, wokovu kamili wa mwanadamu hatimaye haungewezekana, kushindwa kikamilifu kwa Shetani kusingewezekana, na wanadamu kamwe hawangekuwa na uwezo wa kuingia kwenye hatima ya ajabu, ama kuwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, kazi ya wokovu wa mwanadamu haiwezi kukamilishwa kabla vita dhidi ya Shetani havijahitimishwa, kwa kuwa msingi wa kazi ya Mungu ya usimamizi ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Mwanadamu wa kwanza kabisa alikuwa kwa mikono ya Mungu, lakini kwa sababu ya majaribu ya Shetani na upotovu wake, mwanadamu alifungwa na Shetani na kuanguka katika mikono ya yule mwovu. Kwa hivyo, Shetani akakuwa mlengwa wa kushindwa katika kazi ya Mungu ya usimamizi. Kwa sababu Shetani alichukua umiliki wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu ndiye kiini cha usimamizi wote wa Mungu, kama mwanadamu ni wa kuokolewa, basi ni lazima anyakuliwe kutoka mikononi mwa Shetani, yaani mwanadamu ni lazima achukuliwe baada ya kutekwa nyara na Shetani. Hivyo, Shetani lazima ashindwe kupitia mabadiliko ya tabia ya mwanadamu ya zamani, mabadiliko ambayo hurejesha hisia zake za awali, na kwa njia hii, mwanadamu, ambaye ametekwa nyara, anaweza kunyakuliwa kutoka mikononi mwa Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu amewekwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, na baada ya hapo kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 3)

Mungu hana nia mbaya kwa viumbe na anataka tu kumshinda Shetani. Kazi yote Yake—iwe ni kuadibu ama hukumu—inaelekezwa kwa Shetani; inafanyika kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na ina lengo moja: kufanya vita na Shetani mpaka mwisho kabisa! Na Mungu kamwe hatapumzika kabla ya kuwa mshindi dhidi ya Shetani! Atapumzika tu punde atakapomshinda Shetani. Kwa sababu kazi yote ambayo inafanywa na Mungu inaelekezwa kwa Shetani, na kwa sababu wale waliopotoshwa na Shetani wote wanadhibitiwa na milki ya Shetani na wote wanamilikiwa na Shetani, bila kupigana dhidi ya Shetani na kuwa huru dhidi yake, Shetani hangepumzisha kushika kwake kwa watu hawa, na hawangeweza kupatwa. Kama hawangepatwa, ingethibitisha kwamba Shetani hajashindwa, ya kwamba hajatiishwa. Na kwa hivyo, katika miaka 6,000 ya mpango wa usimamizi wa Mungu, katika hatua ya kwanza Yeye alifanya kazi ya sheria, wakati wa hatua ya pili Yeye alifanya kazi ya Enzi ya Neema, yaani, kazi ya kusulubiwa, na wakati wa hatua ya tatu Yeye alifanya kazi ya kumshinda mwanadamu. Kazi hizi zote zinaelekezwa kwa kiwango ambacho Shetani alikuwa amewapotosha wanadamu, yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na hakuna hatua hata moja ambayo si kwa ajili ya kumshinda Shetani. Kiini cha miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi ni vita dhidi ya joka kubwa jekundu, na kazi ya kusimamia watu pia ni kazi ya kumshinda Shetani, na kazi ya kufanya vita na Shetani. Mungu amepigana vita kwa miaka 6,000, na hivyo kufanya kazi kwa miaka 6,000, ili hatimaye kuleta mwanadamu katika ulimwengu mpya. Wakati Shetani atashindwa, mwanadamu atakuwa amewekwa huru kabisa. Je, huu si mwelekeo wa kazi ya Mungu hivi leo? Huu kwa hakika ni mwelekeo wa kazi ya leo: ukombozi kamili na kuwekwa huru kwa mwanadamu, ili kwamba asiwe chini ya sheria yoyote, wala asiwekewe mipaka na vifungu au vikwazo vyovyote. Kazi hii yote inafanywa kwa mujibu wa kimo chenu na kwa mujibu wa mahitaji yenu, kwa maana kuwa nyinyi mnapewa chochote mnachoweza kutimiza. Siyo namna ya “kumpeleka bata kwenye kitulio cha ndege,” ya kuwalazimishia chochote; badala yake, kazi hii yote inafanywa kwa mujibu wa mahitaji yenu ya kweli. Kila hatua ya kazi ni kwa mujibu wa mahitaji halisi na matakwa ya mwanadamu, na ni kwa ajili ya kumshinda Shetani. Kwa kweli, hapo mwanzo hapakuwa na vikwazo kati ya Muumba na viumbe Vyake. Vyote vinasababishwa na Shetani. Mwanadamu amegeuka asiyeweza kuona au kugusa chochote kwa sababu ya usumbufu wa Shetani na upotovu wake. Mwanadamu ndiye mwathiriwa, yule ambaye amedanganywa. Punde tu Shetani anaposhindwa, viumbe watamtazama Muumba, na Muumba ataangalia viumbe na kuweza kuwaongoza binafsi. Haya ndiyo tu maisha ambayo mwanadamu anapaswa kuwa nayo duniani. Na kwa hivyo, kazi ya Mungu kimsingi ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na punde tu Shetani anaposhindwa, mambo yote yatakuwa yametatuliwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 4)

Kazi mzima ya mpangilio wa usimamizi wa Mungu inafanywa binafsi na Mungu mwenyewe. Awamu ya kwanza—uumbaji wa ulimwengu—ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na kama haikuwa hivyo, basi hakuna yeyote ambaye angekuwa na uwezo wa kumuumba mwanadamu; awamu ya pili ilikuwa ukombozi wa wanadamu wote, na pia ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, awamu ya tatu inaenda bila kusemwa: Kuna haja kuu zaidi ya mwisho wa kazi ya Mungu kufanywa na Mungu Mwenyewe. Kazi ya ukombozi, ushindi, kumpata, na kumkamilisha wanadamu wote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe. Kama hangefanya kazi hii Yeye binafsi, basi utambulisho wake hauwezi kuwakilishwa na mwanadamu, au kazi kufanywa na mwanadamu. Ili kumshinda Shetani, ili kumpata mwanadamu, na ili kumpa mwanadamu maisha ya kawaida duniani, Yeye binafsi humwongoza mwanadamu na hufanya kazi binafsi miongoni mwa wanadamu; kwa ajili ya mpangilio mzima wa usimamizi, na kwa kazi yake yote, ni lazima Yeye binafsi afanye kazi hii. Kama mwanadamu anaamini tu kuwa Mungu alikuja kuonekana naye na kumfurahisha, basi imani kama hizo hazina thamani, na hazina umuhimu. Maarifa ya mwanadamu ni ya kijuujuu mno! Ni kwa Mungu kutekeleza kazi Yeye mwenyewe ndivyo Mungu anaweza kufanya kazi yake vizuri na kikamilifu. Mwanadamu hana uwezo wa kuifanya kwa niaba ya Mungu. Kwa kuwa yeye hana utambulisho wa Mungu ama kiini Chake, hana uwezo wa kufanya kazi hii, na hata kama mwanadamu angekuwa na uwezo, haingekuwa na matokeo yoyote. Wakati wa kwanza Mungu kuwa mwili kwa ajili ya ukombozi, ilikuwa ni ili kuwakomboa wanadamu wote kutoka kwa dhambi, ili kufanya mwanadamu aweze kutakaswa na kusamehewa dhambi zake. Kazi ya ushindi pia inafanywa na Mungu binafsi miongoni mwa wanadamu. Kama, katika awamu hii, Mungu angekuwa wa kusema tu ya unabii, basi nabii au mtu ambaye ana kipawa angepatikana wa kuchukua nafasi Yake; kama unabii pekee ungesemwa, mwanadamu angechukua nafasi ya Mungu. Lakini ikiwa mwanadamu binafsi angefanya kazi ya Mungu Mwenyewe na angefanya kazi kwa maisha ya mwanadamu, haingewezekana kwake kufanya kazi hii. Ni lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe binafsi: Ni lazima Mungu binafsi awe mwili ili kufanya kazi hii. Katika Enzi ya Neno, kama unabii pekee ungesemwa, basi Isaya au nabii Eliya wangepatikana wakifanya kazi hii, na hakungekuwepo na haja ya Mungu Mwenyewe kuifanya kazi hii binafsi. Kwa sababu kazi ambayo inafanywa katika awamu hii si tu ya kuongea kuhusu unabii, na kwa sababu ni ya umuhimu mkubwa zaidi kuwa kazi ya maneno inatumiwa kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, kazi hii haiwezi fanywa na mwanadamu, na ni lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe binafsi. Katika Enzi ya Sheria Yehova alifanya sehemu ya kazi ya Mungu, ambapo baadaye alinena baadhi ya maneno na kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa manabii. Hiyo ni kwa sababu mwanadamu angemwakilisha Yehova katika kazi yake, na waonaji wangeweza kutabiri mambo na kutafsiri baadhi ya ndoto kwa niaba Yake. Kazi iliyofanyika hapo mwanzo haikuwa kazi ya kubadilisha tabia ya mwanadamu moja kwa moja, na ilikuwa bila uhusiano na dhambi ya mwanadamu, na mwanadamu alitakiwa tu atii sheria. Kwa hivyo, Yehova hakuwa wa kuwa na mwili na kujifichua Mwenyewe kwa mwanadamu; badala yake Yeye aliongea moja kwa moja na Musa na wengine, akawafanya wao kusema na kufanya kazi kwa niaba yake, na kusababisha wao wafanye kazi moja kwa moja miongoni mwa wanadamu. Awamu ya kwanza ya kazi ya Mungu ilikuwa uongozi wa mwanadamu. Ilikuwa ndio mwanzo wa vita dhidi ya Shetani, lakini vita hivi vilikuwa bado kuanza rasmi. Vita rasmi dhidi ya Shetani vilianza na kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya kwanza, na vimeendelea hadi leo. Tukio la kwanza la vita hivi ni wakati Mungu aliyepata mwili alisulubishwa msalabani. Kusulubiwa kwa Mungu aliyekuwa mwili kulimshinda Shetani, na ilikuwa mafanikio ya awamu ya kwanza katika vita. Wakati Mungu mwenye mwili alianza kufanya kazi kwa mwanadamu moja kwa moja, huu ulikuwa mwanzo rasmi wa kazi ya kumrejesha mwanadamu, na kwa sababu hii ilikuwa kazi ya kubadilisha tabia ya zamani ya mwanadamu, ilikuwa kazi ya kufanya vita na Shetani. Awamu ya kazi iliyofanywa na Yehova hapo mwanzo ilikuwa tu ya uongozi wa maisha ya mwanadamu duniani. Ilikuwa ndio mwanzo wa kazi ya Mungu, na hata ingawa ilikuwa bado haijashirikisha vita vyovyote, au kazi kuu yeyote, ilikuwa imeweka msingi kwa ajili ya kazi ya vita vijavyo. Baadaye, awamu ya pili ya kazi wakati wa Enzi ya Neema ilihusisha kubadilisha tabia ya zamani ya mwanadamu, ambayo ina maana kuwa Mungu Mwenyewe alitengeneza kwa ustadi kazi ya mwanadamu. Hii ilikuwa ni lazima ifanywe na Mungu: ilihitaji kuwa Mungu binafsi awe mwili, na kama hangekuwa mwili, hakuna mwingine angeweza kuchukua nafasi yake katika awamu hii ya kazi, kwa kuwa iliwakilisha kazi ya kupambana dhidi ya Shetani moja kwa moja. Kama mtu angekuwa amefanya kazi hii kwa niaba ya Mungu, wakati mwanadamu alisimama mbele ya Shetani, Shetani hangeweza kutii na haingewezekana kumshinda yeye. Ilibidi iwe Mungu aliyepata mwili aliyekuja kumshinda, kwa kuwa kiini cha Mungu mwenye mwili bado ni Mungu, Yeye bado ni maisha ya mwanadamu, na bado Yeye ni Muumba; chochote kitakachotokea, utambulisho Wake na kiini havitabadilika. Na kwa hivyo, Yeye alivaa mwili na alifanya kazi ili kusababisha kujisalimisha kwa Shetani. Katika awamu ya kazi ya siku za mwisho, kama mwanadamu angefanya kazi hii na angefanywa kusema maneno moja kwa moja, basi hangeweza kusema maneno hayo, na kama unabii ungesemwa, basi haungekuwa na uwezo wa kumshinda mwanadamu. Kwa kuchukua mwili, Mungu huja kumshinda Shetani na kusababisha kujisalimisha kwake kamili. Wakati Yeye atamshinda Shetani kabisa, kumshinda mwanadamu kikamilifu, na kumpata mwanadamu kabisa, awamu hii ya kazi itakamilika na mafanikio kutimizwa. Katika usimamizi wa Mungu, mwanadamu hawezi kuwa naibu wa Mungu na kuwa Mungu wakati hayupo. Hasa, kazi ya kuongoza enzi na kuzindua kazi mpya ina haja kubwa zaidi kufanywa binafsi na Mungu Mwenyewe. Kumpa mwanadamu ufunuo na kwa kumpa yeye unabii kunaweza kufanywa na mwanadamu, lakini kama ni kazi ambayo ni lazima ifanywe na Mungu binafsi, kazi ya vita kati ya Mungu Mwenyewe na Shetani, basi kazi hii haiwezi kufanywa na mwanadamu. Katika awamu ya kwanza, wakati hakukuwepo na vita dhidi ya Shetani, Yehova binafsi aliongoza wana wa Israeli kutumia unabii uliosemwa na manabii. Baadaye, awamu ya pili ya kazi ilikuwa vita na Shetani, na Mungu Mwenyewe binafsi akawa mwili, kuja katika mwili, ili kufanya kazi hii. Chochote ambacho kinahusisha vita na Shetani pia kinahusisha kupata mwili kwa Mungu, ambayo ina maana kuwa vita hivi haviwezi kufanywa na mwanadamu. Kama mwanadamu angekuwa wa kufanya vita, hangeweza kumshinda Shetani. Jinsi gani yeye angekuwa na nguvu ya kupambana dhidi ya Shetani wakati bado yumo chini ya utawala wake? Mwanadamu yumo katikati: Kama wewe utaegemea kuelekea kwa Shetani wewe ni wa Shetani, lakini wewe ukimridhisha Mungu wewe ni wa Mungu. Kama mwanadamu angeweza kuwa mbadala wake Mungu katika kazi ya vita hivi, je, yeye angekuwa na uwezo wa kufanya hivyo? Kama angekuwa na uwezo, je, hangeangamia kitambo sana? Je, yeye si angekuwa ameingia katika ulimwengu wa jahanamu muda mrefu uliopita? Na hivyo, mwanadamu hana uwezo wa kuchukua nafasi ya Mungu katika kazi yake, ambayo ni kusema kwamba mwanadamu hana kiini cha Mungu, na kama ungepambana na Shetani hungeweza kumshinda Shetani. Mwanadamu anaweza tu kufanya baadhi ya kazi; anaweza kushinda baadhi ya watu, lakini hawezi kuwa mbadala wa Mungu katika kazi ya Mungu Mwenyewe. Je, ni jinsi gani mwanadamu atafanya vita na Shetani? Shetani ataweza kukushika mateka kabla hata hujaanza. Ni wakati Mungu Mwenyewe hufanya vita dhidi ya Shetani na mwanadamu kufuata na kutii Mungu katika msingi huu tu ndipo mwanadamu anaweza kupatwa na Mungu na kutoroka kutokana na vifungo vya Shetani. Kile mwanadamu anaweza kufikia kwa hekima yake na uwezo wake mwenyewe ni kidogo sana; hana uwezo wa kufanya mwanadamu akamilike, kumwongoza mwanadamu, na, zaidi ya hayo, kumshinda Shetani. Akili na hekima ya mwanadamu haviwezi kuharibu miradi ya Shetani, hivyo je, ni jinsi gani mwanadamu awezavyo kufanya vita na Shetani?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 5)

Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu ilianza tu baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu pia ilianza tu punde mwanadamu alipopotoshwa. Kwa maneno mengine, usimamizi wa Mungu wa mwanadamu ulianza kutokana na kazi ya kumwokoa mwanadamu, na wala haukutokana na kazi ya kuiumba dunia. Hakungekuwa na kazi ya kumsimamia mwanadamu pasipo kuwepo na tabia potovu ya mwanadamu, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu ina sehemu tatu, badala ya hatua nne, au enzi nne. Hii tu ndio njia sahihi ya kutaja kazi ya Mungu ya usimamizi wa mwanadamu. Enzi ya mwisho itakapofikia kikomo, kazi ya kusimamia mwanadamu itakuwa imekamilika. Hitimisho la kazi ya usimamizi lina maana kuwa kazi ya kuwaokoa wanadamu wote imekamilika kabisa, na kwamba mwanadamu amefika mwisho wa safari yake. Pasipo kazi ya kuwaokoa wanadamu wote, kazi ya usimamizi wa wanadamu haingekuwepo, wala hakungekuwa na hatua tatu za kazi. Ilikuwa ni hasa kwa ajili ya upotovu wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu alihitaji wokovu kwa dharura, ndipo Yehova alikamilisha uumbaji wa dunia na kuanza kazi ya Enzi ya Sheria. Hapo tu ndipo kazi ya kumsimamia mwanadamu ilipoanza, kumaanisha kwamba hapo tu ndipo kazi ya kumwokoa mwanadamu ilipoanza. “Kumsimamia mwanadamu” haimaanishi kuongoza maisha ya mwanadamu aliyeumbwa upya duniani (ambapo ni kusema, mwanadamu ambaye bado hakuwa amepotoshwa). Badala yake, ni wokovu wa mwanadamu ambaye amepotoshwa na Shetani, ambapo ni kusema kwamba, ni kubadilishwa kwa mwanadamu aliyepotoshwa. Hii ndiyo maana ya kumsimamia mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu haihusishi kazi ya kuiumba dunia, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu haijumuishi kazi ya kuumba ulimwengu, na inahusisha tu hatua tatu za kazi zilizo tofauti na uumbaji wa ulimwengu. Ili kuelewa kazi ya kumsimamia mwanadamu, ni muhimu kuwa na ufahamu wa historia ya hatua tatu za kazi—hili ndilo kila mtu anapaswa kulifahamu ili kuokolewa. Kama viumbe wa Mungu, mnapaswa kutambua kuwa mwanadamu aliumbwa na Mungu, na kufahamu chanzo cha upotovu wa mwanadamu, na, vilevile, kufahamu mchakato wa wokovu wa mwanadamu. Iwapo mnafahamu tu jinsi ya kutenda kulingana na mafundisho ili kupata neema ya Mungu, lakini hamna fununu jinsi Mungu anavyomwokoa mwanadamu, au ya chanzo cha upotovu wa mwanadamu, basi hili ndilo mnalokosa kama viumbe wa Mungu. Hupaswi kutoshelezwa tu na kuelewa kwa ukweli unaoweza kuwekwa katika vitendo, huku ukibakia kutojua upeo mpana wa kazi ya usimamizi ya Mungu—kama hivi ndivyo ilivyo, basi wewe ni mwenye kulazimisha kauli sana. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo hadithi ya ndani ya usimamizi wa Mungu wa mwanadamu, ujio wa injili ya dunia nzima, fumbo kubwa zaidi kati ya wanadamu, na pia ni msingi wa kueneza injili. Ukizingatia tu kuelewa ukweli sahili unaohusiana na maisha yako, na usijue lolote kuhusu hili, maajabu makuu zaidi na maono, basi maisha yako si ni sawa na bidhaa yenye kasoro, yasio na maana isipokuwa kuangaliwa?

Ikiwa mwanadamu huzingatia tu matendo, na kuona kazi ya Mungu na hekima ya mwanadamu kama za upili, basi si ni sawa na kufikira mambo yasiyokuwa muhimu huku ukipuuza mambo yaliyo muhimu zaidi? Lile ambalo sharti ulijue, lazima ulijue, na kile unachostahili kuonyesha kwa vitendo, lazima ukionyeshe kwa vitendo. Ni hapo tu ndipo utakapokuwa mtu anayejua kufuata ukweli. Siku yako ya kueneza injili itakapowadia, ikiwa utaweza kusema tu kuwa Mungu ni Mkuu na Mwenye haki, kuwa ni Mungu Mkuu, Mungu ambaye hapana mwanadamu yeyote mkuu anayeweza kujilinganisha naye, na kuwa hakuna aliye juu zaidi wa kumpiku…, kama waweza tu kusema maneno haya yasiyofaa na ovyo, na kabisa huwezi kunena maneno yenye umuhimu zaidi, na yaliyo na kiini, kama huna lolote la kusema kuhusu kumjua Mungu, ama kazi ya Mungu, na zaidi ya hapo, huwezi kuelezea ukweli, au kutoa kile ambacho kinakosekana kwa mwanadamu, basi mtu kama wewe hana uwezo wa kutekeleza wajibu wake vyema. Kumshuhudia Mungu na kueneza injili ya ufalme si jambo rahisi. Lazima kwanza uwe na ukweli, na maono yatakayoeleweka. Unapokuwa na uwazi wa maono na ukweli wa masuala tofauti ya kazi ya Mungu, moyoni mwako unapata kujua kazi ya Mungu, na bila kujali anayoyafanya Mungu—iwe ni hukumu ya haki ama kusafishwa kwa mwanadamu—unamiliki maono makuu kama msingi wako, na unamiliki ukweli sahihi wa kuonyesha kwa matendo, basi utaweza kumfuata Mungu hadi mwisho. Lazima ujue kuwa bila kujali kazi ambayo Yeye anatenda, lengo la kazi ya Mungu halibadiliki, kiini cha kazi Yake hakibadiliki, na mapenzi Yake kwa mwanadamu hayabadiliki. Bila kujali maneno Yake ni makali namna gani, haijalishi mazingira ni mabaya kiasi gani, kanuni za kazi Yake, na nia Yake ya kumwokoa mwanadamu hayatabadilika. Mradi tu si ufunuo wa mwisho wa mwanadamu au hatima ya mwanadamu, na si kazi ya awamu ya mwisho, au kazi ya kutamatisha mpango wote wa usimamizi wa Mungu, na mradi tu ni wakati Anapomfinyanga mwanadamu, basi kiini cha kazi Yake hakitabadilika: Daima kitakuwa wokovu wa mwanadamu. Hili linapaswa kuwa msingi wa imani yenu katika Mungu. Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na matakwa ya mwanadamu. Punde unapofahamu lengo la hatua hizi tatu za kazi, basi utafahamu jinsi ya kuthamini umuhimu wa kila hatua ya kazi, na utatambua jinsi ya kutenda ili kutosheleza shauku ya Mungu. Iwapo utaweza kufikia hatua hii, basi hili, ono kubwa kuliko yote, litakuwa msingi wa imani yako katika Mungu. Unapaswa kufuata sio tu njia rahisi za matendo, ama ukweli wenye undani, lakini unapaswa kuunganisha maono na matendo, ili kwamba kuwe na ukweli unaoweza kuwekwa kwenye vitendo, na maarifa yaliyo na msingi wa maono. Ni hapo tu ndipo utakapokuwa mtu anayefuatilia ukweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 6)

Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu. Wale wasiofahamu hatua tatu za kazi watakosa kuelewa njia mbalimbali na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu; wale wanaoshikilia tu imara mafundisho ya dini yanayosalia kutoka katika hatua moja ya kazi ni watu wanaomwekea Mungu mipaka kwa mafundisho ya dini, na wale ambao imani yao kwa Mungu haina udhahiri na uhakika. Watu kama hao kamwe hawawezi kupokea wokovu wa Mungu. Ni hatua tatu tu za Mungu zinazoweza kuonyesha kabisa ukamilifu wa tabia ya Mungu, na kuonyesha kabisa nia ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu wote, na mchakato mzima wa wokovu wa mwanadamu. Hili ni dhibitisho kuwa Yeye amemshinda Shetani na kumpata mwanadamu, ni dhibitisho la ushindi wa Mungu, na ni maonyesho ya tabia kamili ya Mungu. Wale wanaoelewa hatua moja tu kati ya hatua tatu za kazi ya Mungu wanajua tu sehemu ya tabia ya Mungu. Katika dhana ya mwanadamu, ni rahisi kwa hatua hii moja kuwa mafundisho ya kidini, panakuwa na uwezekano zaidi wa mwanadamu kuweka amri kumhusu Mungu, na mwanadamu anatumia hii sehemu moja ya tabia ya Mungu kama dhihirisho la tabia nzima ya Mungu. Zaidi ya hayo, mawazo mengi ya mwanadamu yanachanganywa ndani yake, hivi kwamba anaweka vikwazo imara kwa tabia, nafsi, na hekima ya Mungu, na pia kanuni za kazi ya Mungu ndani ya vigezo vyenye mipaka, akiamini kwamba ikiwa Mungu alikuwa hivi wakati mmoja, basi Yeye atasalia kuwa vile daima, na kamwe hatabadilika. Ni wale tu wanaojua na kuthamini hatua tatu za kazi ndio wanaoweza kumjua Mungu kabisa na kwa usahihi. Angalau, hawatamfafanua Mungu kama Mungu wa Waisraeli, ama Wayahudi, na hawatamwona kama Mungu atakayesulubiwa msalabani milele kwa ajili ya mwanadamu. Kama unapata kumjua Mungu kutokana na hatua moja ya kazi Yake tu, basi maarifa yako ni kidogo, kidogo sana. Maarifa yako ni sawa na tone moja katika bahari. Kama si hivyo, kwa nini wengi wa walinzi wa kidini wa kale walimtundika Mungu msalabani akiwa hai? Je, si kwa ajili mwanadamu humwekea Mungu mipaka kwenye vigezo fulani? Je, si watu wengi humpinga Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofautitofauti ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye majivuno na wadekezi katika asili yao, na wanatazama kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza masomo ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo zee kudhibitisha kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele ya Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wadogo wasiojua na wasio na habari ya kutosha jinsi na wanajaribu kuonyesha walivyo werevu? Kwa maarifa haba ya Biblia, wanajaribu kupotosha “wasomi”; wa dunia, kwa mafundisho duni ya dini ili kuwafunza watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya ihusu mchakato wao wanavyofikiria, na kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kuona kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Watu hawa hawana mantiki yoyote hata kidogo! Kwa kweli, maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo wanavyokuwa wagumu wa kuhukumu kazi Yake. Zaidi ya hayo, wanazungumzia tu machache kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu leo, lakini si wepesi wa kuhukumu. Kadri watu wanavyojua machache kumhusu Mungu, ndivyo wanavyozidi kuwa wenye majivuno na wenye kujiamini sana, na ndivyo wanavyozidi kutangaza nafsi ya Mungu kwa utundu—ilhali wanazungumzia tu nadharia, na wala hawapeani ushahidi wowote halisi. Watu kama hawa hawana thamani yoyote kabisa. Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru—je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, zaidi ya hayo, wale wasiojua, wenye majivuno ya asili na wasioweza kutawalwa? Hata ikiwa siku itakuja ambapo watu hawa watakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, bado Mungu hatawavumilia. Hawadharau tu wale wanaofanya kazi ya Mungu, bali pia wanamkufuru Mungu Mwenyewe. Watu kama hawa jasiri pasi na hadhari hawatasamehewa, katika enzi hii ama enzi itakayokuja na wataangamia kuzimuni milele! Watu kama hawa wasio na heshima, wenye kujifurahisha, wanajifanya kuwa wanamwamini Mungu, na kadiri wanavyozidi kufanya vile, ndivyo wanavyozidi kukosea amri za utawala wa Mungu. Je, si hao mafidhuli ambao kiasili hawazuiliki, na hawajawahi kumtii yeyote, wote hupitia njia hii? Je, si wao humpinga Mungu siku baada ya siku, Yeye ambaye daima huwa mpya na wala hazeeki?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 7)

Hatua tatu za kazi ni rekodi ya kazi nzima ya Mungu, ni rekodi ya wokovu wa Mungu wa mwanadamu, na si porojo tu. Kama kweli mnataka kutafuta kujua tabia nzima ya Mungu, basi sharti mfahamu hatua tatu za kazi inayofanywa na Mungu, na, zaidi, sharti msiache hatua yoyote. Hiki ndicho kiwango cha chini kinachopaswa kufikiwa na wale wanaotafuta kumjua Mungu. Mwanadamu mwenyewe hawezi kuvumbua maarifa ya Mungu. Si kitu ambacho mwanadamu mwenyewe anaweza kufikiria, wala si matokeo ya fadhila za Roho Mtakatifu kwa mtu mmoja. Badala yake, ni maarifa yanayotokea mwanadamu anapopitia kazi ya Mungu, na ni maarifa ya Mungu yanayotokana tu na mwanadamu kupitia ukweli wa kazi ya Mungu. Maarifa kama haya hayawezi kutimizwa kwa ghafla, wala si jambo linaloweza kufundishwa. Inahusiana kabisa na uzoefu wa kibinafsi. Wokovu wa Mungu wa mwanadamu ndiyo kiini cha hatua hizi tatu za kazi, ilhali katika kazi ya wokovu kumejumuishwa mbinu kadhaa za kufanya kazi na namna ambazo tabia ya Mungu imeonyeshwa. Hili ndilo jambo gumu sana kwa mwanadamu kutambua na kwa mwanadamu kuelewa. Mgawanyiko wa enzi, mabadiliko ya kazi ya Mungu, mabadiliko katika eneo la kazi, mabadiliko ya wanaopokea kazi na kadhalika—haya yote yamejumuishwa katika hatua tatu za kazi. Hususan, tofauti katika njia ya utendakazi wa Roho Mtakatifu, na vilevile mabadiliko katika tabia ya Mungu, picha, jina, utambulisho, au mabadiliko mengine, yote ni sehemu ya hatua tatu za kazi. Sehemu moja ya kazi inaweza tu kuwakilisha sehemu moja, na imewekewa mipaka ndani ya wigo fulani. Haihusiani na mgawanyiko wa enzi, ama mabadiliko ya kazi ya Mungu, wala masuala mengine. Huu ni ukweli ulio waziwazi. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo ukamilifu wa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu lazima ajue kazi ya Mungu, tabia ya Mungu katika kazi ya wokovu, na bila ukweli huu, maarifa yako kumhusu Mungu yatakuwa tu maneno matupu, ni mahubiri ya starehe tu. Maarifa kama haya hayawezi kumshawishi au kumshinda mtu, maarifa kama haya yako nje ya uhalisi, na si ukweli. Yanaweza kuwa mengi, na mazuri kwa masikio, lakini kama hayaambatani na tabia ya asili ya Mungu, basi Mungu hatakusamehe. Hatakosa kuyasifu maarifa yako tu, bali pia atakuadhibu kwa kuwa mwenye dhambi aliyemkufuru. Maneno ya kumjua Mungu hayazungumzwi kwa mzaha. Ingawa unaweza kuwa na ulimi laini wenye maneno matamu, na ingawa maneno yako ni ya werevu kiasi kwamba unaweza kubishana kitu kisichowezekana, bado huna elimu ya kuzungumza kuhusu maarifa ya Mungu. Mungu si mtu ambaye unaweza kuhukumu kwa urahisi, ama kusifu bila mpango, ama kupaka tope bila kujali. Unamsifu mtu yeyote na watu wowote, ilhali unajitahidi kupata maneno sahihi ya kuelezea ukuu wa wema na neema za Mungu—hili ndilo mshindwa yeyote hujifunza. Ingawa kuna wataalam wengi wa lugha wanaoweza kumwelezea Mungu, usahihi wa kile wanachoelezea ni asilimia moja ya ukweli unaozungumzwa na watu wa Mungu na wana misamiati michache tu, ilhali wanamiliki tajriba yenye uzito. Basi inaweza kuonekana kuwa maarifa ya Mungu yapo katika usahihi na uhalisi, na wala si utumiaji mzuri wa maneno au misamiati mingine, na kwamba maarifa ya mwanadamu na maarifa ya Mungu kabisa hayahusiani. Somo la kumjua Mungu liko juu zaidi kuliko sayansi za asili za mwanadamu. Ni somo linaloweza kutimizwa tu na idadi ndogo sana ya watu wanaotafuta kumjua Mungu, na haliwezi kutimizwa na mtu yeyote tu mwenye kipaji. Na kwa hivyo lazima msione kumjua Mungu na kufuatilia ukweli kama kwamba kunaweza kupatikana na mtoto mdogo tu. Pengine umekuwa na mafanikio makuu katika maisha yako ya kifamilia, ama kazi yako, ama katika ndoa yako, lakini inapofika kwenye ukweli, na somo la kumjua Mungu, huna lolote la kujivunia, hujatimiza malengo yoyote. Kutia ukweli kwenye vitendo, inaweza kusemwa, ni jambo gumu kwenu, na kumjua Mungu ni tatizo kuu hata zaidi. Hili ni tatizo lenu, na pia ni tatizo linalokabiliwa na wanadamu wote. Kati ya wale wenye mafanikio katika kumjua Mungu, karibu wote hawajafikia kiwango. Mwanadamu hajui maana ya kumjua Mungu, ama kwa nini ni muhimu kumjua Mungu, ama kiasi kipi kinahesabiwa kama kumjua Mungu. Hili ndilo linalomshangaza mwanadamu, na ni kitendawili kikubwa zaidi kinachokabiliwa na mwanadamu—na hakuna awezaye kujibu swali hili, ama aliye na hiari kujibu hili swali, kwa sababu, hadi leo, hamna katika wanadamu aliyefanikiwa katika kusomea kazi hii. Pengine, kitendawili cha hatua tatu za kazi kitakapotambulishwa kwa mwanadamu, kutakuwepo katika mfululizo kundi la watu wenye vipaji wanaomjua Mungu. Bila shaka, Natumaini kuwa hivyo ndivyo ilivyo, na, hata zaidi, Niko katika harakati ya kutekeleza kazi hii, na Ninatumaini kuona kujitokeza kwa vipaji zaidi kama hivi katika siku za hivi karibuni. Watakuwa wale wanaoshuhudia ukweli wa hatua hizi tatu za kazi, na, bila shaka, watakuwa pia wa kwanza kushuhudia hizi hatua tatu za kazi. Kama kutakuwa na aliye na vipaji hivi, siku ambayo kazi ya Mungu itafikia kikomo, ama kuwe na wawili ama watatu, na kibinafsi wamekubali kufanywa wakamilifu na Mungu mwenye mwili, basi hakuna jambo la kuhuzunisha na kujutia kama hili—ingawa ni katika hali mbaya zaidi tu. Kwa vyovyote vile, Ninatumai kuwa wale wote wanaotafuta kwa kweli wanaweza kupata baraka hii. Tangu mwanzo wa wakati, hakujawahi kuwa na kazi kama hii, hapo awali hakujawahi kuwa na kazi kama hii katika historia ya ukuaji wa mwanadamu. Kama kweli unaweza kuwa mmoja wa wale wa kwanza wanaomjua Mungu, je, si hii itakuwa heshima ya juu kuliko viumbe wote? Je, kuna kiumbe mwingine kati ya wanadamu anayeweza kusifiwa na Mungu zaidi? Kazi kama hii ni ngumu kutekeleza, lakini mwishowe bado itapokea malipo. Bila kujali jinsia yao ama uraia wao, wale wote wenye uwezo wa kufikia maarifa ya Mungu, mwishowe, watapokea heshima kuu ya Mungu, na watakuwa tu wenye kumiliki mamlaka ya Mungu. Hii ndiyo kazi ya leo, na pia ndiyo kazi ya siku za usoni; ni ya mwisho na ya juu zaidi kuwahi kutekelezwa katika miaka 6000 ya kazi, na ni njia ya kufanya kazi inayodhihirisha kila kundi la mwanadamu. Kupitia kazi ya kumfanya wanadamu kumjua Mungu, daraja tofauti za mwanadamu zinadhihirishwa: Wale wanaomjua Mungu wamehitimu kupokea baraka za Mungu na kukubali ahadi zake, wakati wale wasiomjua Mungu hawajahitimu kupokea baraka za Mungu wala kupokea ahadi zake. Wale wanaomjua Mungu ni wandani wa Mungu, na wale wasiomjua Mungu hawawezi kuitwa wandani wa Mungu; wandani wa Mungu wanaweza kupokea baraka zozote za Mungu, lakini wale wasio wandani wa Mungu hawastahili kazi yoyote Yake. Iwe ni dhiki, usafishaji, ama hukumu, yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu hatimaye kufikia maarifa ya Mungu na ili kwamba mwanadamu amtii Mungu. Hii ndiyo athari pekee itakayofikiwa hatimaye. Hakuna lolote katika hatua tatu za kazi lililofichwa, na hii ni faida kwa maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu, na humsaidia mwanadamu kupata maarifa kamili na mengi ya Mungu. Kazi hii yote ni ya kumfaidi mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 8)

Kazi ya Mungu Mwenyewe ni maono ambayo mwanadamu lazima afahamu, kwa kuwa kazi ya Mungu haiwezi kutekelezwa na mwanadamu, wala haimilikiwi na mwanadamu. Hatua tatu za kazi ndizo ukamilifu wa usimamizi wa Mungu, na hakuna ono kuu kuliko hili linalopaswa kufahamika kwa mwanadamu. Kama mwanadamu hafahamu maono haya makuu, basi si rahisi kumjua Mungu, na si rahisi kujua mapenzi ya Mungu, na, zaidi ya hayo, njia ambayo mwanadamu anapitia inazidi kuwa ngumu. Bila maono, mwanadamu hangeweza kufika umbali huu. Ni maono ambayo yamemlinda mwanadamu hadi leo, na ambayo yamempa mwanadamu ulinzi mkuu. Katika siku za usoni, maarifa yenu lazima yawe ya kina, na sharti mfahamu mapenzi Yake yote na umuhimu wa kazi Yake yenye busara katika hatua tatu za kazi. Hiki tu ndicho kimo chenu cha kweli. Hatua ya kazi ya mwisho haisimami peke yake, ila ni sehemu ya yote iliyounganishwa pamoja na hatua mbili za awali, ambayo ni kusema kwamba haiwezekani kukamilisha kazi nzima ya wokovu kwa kufanya kazi ya hatua moja pekee. Ingawa hatua ya mwisho ya kazi inaweza kumwokoa mwanadamu kabisa, hii haimaanishi kwamba ni muhimu tu kutekeleza hatua hii pekee, na kwamba hatua mbili za hapo awali hazihitajiki kumwokoa mwanadamu kutokana na ushawishi wa Shetani. Hakuna hatua moja kati ya zote tatu inayoweza kuwekwa kama maono ya kipekee ambayo lazima yajulishwe mwanadamu, kwa kuwa ukamilifu wa kazi ya wokovu ni hatua tatu za kazi, wala si hatua moja kati ya tatu. Ilimradi kazi ya wokovu bado haijakamilishwa, usimamizi wa Mungu utashindwa kufikia kikomo. Nafsi ya Mungu, tabia, na hekima zimeonyeshwa katika ukamilifu wa kazi ya wokovu, wala hazikufichuliwa kwa mwanadamu hapo mwanzo, lakini zimeonyeshwa hatua kwa hatua katika kazi ya wokovu. Kila hatua ya kazi ya wokovu huonyesha sehemu ya tabia ya Mungu, na sehemu ya nafsi Yake: si kila hatua ya kazi inayoweza moja kwa moja kuonyesha kabisa na kwa ukamilifu nafsi ya Mungu. Kwa hivyo, kazi ya wokovu inaweza tu kuhitimishwa hatua tatu za kazi zitakapokamilika, na kwa hivyo, maarifa ya mwanadamu ya ukamilifu wa Mungu hayawezi kutenganishwa na hatua tatu za kazi ya Mungu. Kile ambacho mwanadamu hupokea kutoka kwa hatua moja ya kazi ni tabia ya Mungu inayoonyeshwa katika sehemu moja ya kazi yake tu. Haiwezi kuwakilisha tabia na nafsi inayoonyeshwa katika hatua ya awali na ijayo. Hii ni kwa sababu kazi ya kumwokoa mwanadamu haiwezi kumalizika mara moja katika kipindi kimoja, ama katika eneo moja, lakini hukuwa kwa kina hatua kwa hatua kulingana na kiwango cha kukua kwa mwanadamu katika wakati na maeneo tofauti. Ni kazi inayofanywa hatua kwa hatua, na haikamilishwi katika hatua moja. Na kwa hiyo, hekima yote ya Mungu imejumuishwa katika hatua tatu, badala ya hatua moja. Nafsi yake yote na hekima yake yote zimewekwa wazi katika hatua hizi tatu, na kila hatua ina nafsi Yake, na ni rekodi ya hekima ya kazi Yake. Mwanadamu anapaswa kujua tabia yote ya Mungu iliyoonyeshwa katika hatua hizi tatu. Nafsi hii ya Mungu ndiyo ina maana zaidi kwa wanadamu wote, na ikiwa watu hawana maarifa haya wanapomwabudu Mungu, basi hawana tofauti na wale wanaoabudu Budha. Kazi ya Mungu kati ya wanadamu haijafichiwa mwanadamu, na inapaswa kujulikana na wale wote wanaomwabudu Mungu. Kwa sababu Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi ya wokovu kati ya wanadamu, mwanadamu anapaswa kujua maonyesho ya kile Anacho na alicho wakati wa hatua hizi tatu za kazi. Hili ndilo ambalo ni lazima lifanywe na mwanadamu. Kile ambacho Mungu anamfichia mwanadamu ni kile ambacho mwanadamu hawezi kutimiza, na kile ambacho mwanadamu hapaswi kujua, ilhali yale Mungu anayomfunulia mwanadamu ni yale ambayo mwanadamu anapaswa kujua na yale ambayo mwanadamu anapaswa kumiliki. Kila moja ya hatua tatu za kazi huendelea juu ya msingi wa hatua iliyopita; haitekelezwi peke yake, tofauti na kazi ya wokovu. Ingawa kuna tofauti kubwa katika enzi na aina ya kazi ambayo inafanywa, katika kiini chake bado ni wokovu wa mwanadamu, na kila hatua ya kazi ya wokovu ina kina kuliko iliyopita.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 9)

Kazi ya Mungu kati ya wanadamu haijafichiwa mwanadamu, na inapaswa kujulikana na wale wote wanaomwabudu Mungu. Kwa sababu Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi ya wokovu kati ya wanadamu, mwanadamu anapaswa kujua maonyesho ya kile Anacho na alicho wakati wa hatua hizi tatu za kazi. Hili ndilo ambalo ni lazima lifanywe na mwanadamu. Kile ambacho Mungu anamfichia mwanadamu ni kile ambacho mwanadamu hawezi kutimiza, na kile ambacho mwanadamu hapaswi kujua, ilhali yale Mungu anayomfunulia mwanadamu ni yale ambayo mwanadamu anapaswa kujua na yale ambayo mwanadamu anapaswa kumiliki. Kila moja ya hatua tatu za kazi huendelea juu ya msingi wa hatua iliyopita; haitekelezwi peke yake, tofauti na kazi ya wokovu. Ingawa kuna tofauti kubwa katika enzi na aina ya kazi ambayo inafanywa, katika kiini chake bado ni wokovu wa mwanadamu, na kila hatua ya kazi ya wokovu ina kina kuliko iliyopita. Kila hatua inaendelea kutoka kwa msingi wa hatua ya mwisho ambayo haiondolewi. Kwa njia hii, katika kazi Yake ambayo daima huwa mpya na kamwe si kuukuu, Mungu mara kwa mara anaonyesha vipengele vya tabia Yake ambavyo havijawahi kuonyeshwa kwa mwanadamu hapo awali, na daima anamfichulia mwanadamu kazi Yake mpya, na nafsi Yake mpya, na hata ikiwa wazoefu wakongwe wa kidini hufanya juu chini kukinzana na hili, na kulipinga waziwazi, Mungu daima hufanya kazi mpya ambayo anakusudia kufanya. Kazi Yake daima hubadilika, na kwa sababu hii, daima inakabiliwa na upinzani wa mwanadamu. Na hivyo, pia, tabia Yake inabadilika daima, na vilevile enzi na wanaopokea kazi Yake. Zaidi ya hayo, kila mara Yeye hufanya kazi ambayo haijawahi kufanywa tena, hata kufanya kazi ambayo huonekana kwa mwanadamu kuhitilafiana na kazi iliyofanywa awali, kuwa kinyume nayo. Mwanadamu anaweza kukubali tu aina moja ya kazi, ama njia moja ya matendo. Ni vigumu kwa wanadamu kukubali kazi ama njia za matendo, ambayo yanakinzana nao, ama yaliyo juu kuwaliko—lakini Roho Mtakatifu daima anafanya kazi mpya, na kwa hivyo kunakuwepo kikundi baada ya kikundi cha wataalamu wa kidini wanaoipinga kazi mpya ya Mungu. Watu hawa wamekuwa wataalamu hasa kwa sababu mwanadamu hana maarifa ya jinsi Mungu huwa mpya wala hazeeki, na zaidi ya hayo, hana maarifa ya kanuni za kazi ya Mungu, na hata zaidi hawana maarifa ya njia nyingi ambazo Mungu humwokoa mwanadamu. Kwa hivyo, mwanadamu kabisa anashindwa kueleza kama ni kazi inayotoka kwa Roho Mtakatifu, au ni kazi ya Mungu Mwenyewe. Watu wengi hushikilia mtazamo ambao, kama inalingana na maneno yanayokuja kabla, basi wanaweza kuikubali, na kama kuna tofauti na kazi ya awali, basi wanaipinga na kuikataa. Leo, je, nyote hamjafuata katika kanuni hizi? Hatua tatu za kazi ya wokovu hazijakuwa na athari kubwa kwenu, na kuna wale wanaoamini kuwa hatua mbili zilizopita za kazi ni mzigo usiohitaji kufahamika. Wanafikiria kuwa hatua hizi hazifai kutangazwa kwa umati na zinafaa kufutwa haraka iwezekanavyo, ili watu wasihisi kwamba wamezidiwa na hatua mbili za awali za zile hatua tatu za kazi. Wengi wanaamini kuwa kupeana ufahamu kuhusu hatua mbili zilizopita ni hatua ya mbali sana, wala haina faida katika kumjua Mungu—hivyo ndivyo mnavyofikiria. Leo, nyote mnaamini kuwa ni haki kutenda vile, lakini siku itawadia ambapo mtagundua umuhimu wa kazi Yangu: Mjue kuwa Sifanyi kazi yoyote ambayo haina umuhimu. Kwa sababu Ninawatangazia hatua tatu za kazi, kwa hivyo lazima ziwe na faida kwenu; kwa sababu hatua hizi tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, kwa hivyo lazima ziwe lengo la kila mmoja duniani. Siku moja, nyote mtagundua umuhimu wa kazi hii. Fahamuni kuwa mnapinga kazi ya Mungu, ama mnatumia dhana zenu kupima kazi ya leo, kwa sababu hamjui kanuni za kazi ya Mungu, na kwa sababu hamchukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa makini kutosha. Upinzani wenu kwa Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kumetokana na dhana zenu na upumbavu wenu wa kiasili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sawa, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kiasili ya kutotii. Baada ya kupata imani yao katika Mungu, watu wengine hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, ilhali wanathubutu kuzungumza hadharani wakitathmini haki na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na pia wanawakemea mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; ubinadamu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote. Je, si siku itawadia ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumwagiza Mungu jinsi atakavyofanya kazi. Je, ni kwa namna gani watu hawa wasio na busara watamjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati anapomtafuta na anapokuwa na uzoefu naye; si katika kumkosoa kwa ghafla ndipo anapokuja kumjua Mungu kwa kupitia kutiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kadiri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao Kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, ubinadamu wako wa zamani, na utu wako, tabia na maadili ndiyo “mtaji” ambao unampingia Mungu, na kadri unavyokuwa mpotovu, ama ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale waliomilikiwa na dhana kali na wenye tabia ya unafiki wamo hata zaidi katika uadui wa Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo. Ikiwa dhana zako hazitarekebishwa, basi daima zitakuwa kinyume na Mungu; daima hutalingana na Mungu, na daima utakuwa mbali na Yeye.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 10)

Hatua tatu za kazi zilifanywa na Mungu mmoja; haya ndiyo maono makubwa zaidi, na ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Hatua tatu za kazi zingefanywa tu na Mungu Mwenyewe, na hapana mwanadamu yeyote ambaye angeweza kufanya kazi kama hii kwa niaba Yake—ambayo ni kusema kuwa ni Mungu Mwenyewe pekee ambaye angeifanya kazi Yake toka mwanzo hadi leo. Ingawa hatua tatu za kazi ya Mungu zimefanywa katika enzi tofauti na maeneo tofauti, na ingawa kazi ya kila moja ni tofauti, yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kati ya maono yote, hili ndilo kuu zaidi ambalo mwanadamu anapaswa kulijua, na ikiwa litaeleweka kabisa na mwanadamu, basi ataweza kusimama imara. Leo, tatizo kuu linalokumba dini na madhehebu kadhaa ni kwamba hazijui kazi ya Roho Mtakatifu, na hazina uwezo wa kutofautisha kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi isiyo ya Roho Mtakatifu—na kwa hivyo hawawezi kueleza kama hatua hii ya kazi, kama hatua mbili za awali, pia zimefanywa na Yehova Mungu. Ingawa watu wanamfuata Mungu, wengi hawawezi kueleza kama ni njia sahihi. Mwanadamu anahofia ikiwa hii ndiyo njia inayoongozwa na Mungu Mwenyewe, na kama Mungu kupata mwili ni jambo la hakika, na watu wengi bado hawana dokezo jinsi ya kupambanua ikifikia maneno kama haya. Wale wanaomfuata Mungu hawawezi kujua njia, na kwa hivyo habari zinazozungumzwa zinaathiri sehemu ndogo tu kati ya watu hawa na hayana uwezo wa kufaa kikamilifu, na kwa hivyo, hili basi linaathiri kuingia kwa maisha kwa watu kama hawa. Ikiwa mwanadamu anaweza kuona katika hatua tatu za kazi kuwa zilitekelezwa na Mungu Mwenyewe wakati tofauti, katika maeneo tofauti, na kwa watu tofauti; ikiwa mwanadamu anaweza kuona kuwa ingawa kazi ni tofauti, yote imefanywa na Mungu mmoja, na kwa kuwa ni kazi ambayo imefanywa na Mungu mmoja, basi lazima iwe sawa, na bila dosari, na kwamba ingawa hailingani na dhana za mwanadamu, hakuna kupinga kuwa ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja—ikiwa mwanadamu anaweza kusema kwa hakika kuwa ni kazi ya Mungu mmoja, basi dhana zake zitakuwa duni, na ambazo hazifai kutajwa. Kwa sababu maono ya mwanadamu hayako wazi, na mwanadamu anamjua tu Yehova kama Mungu, na Yesu kama Bwana, na ana mitazamo miwili kumhusu Mungu mwenye mwili wa leo, watu wengi wamejitoa kwa ajili ya kazi ya Yehova na Yesu, na wamezingirwa na dhana kuhusu kazi ya leo, watu wengi daima huwa na shaka na hawachukulii kazi ya leo kwa makini. Mwanadamu hana uelewa kuhusu hatua mbili za mwisho, ambazo hazikuonekana. Hio ni kwa sababu mwanadamu haelewi uhalisi wa hatua mbili za mwisho za kazi, na wala hakuzishuhudia binafsi. Ni kwa sababu haziwezi kuonekana ndiyo mwanadamu anawaza jinsi anavyopenda; bila kujali atakayodhania, hakuna ukweli wa kudhibitisha, na yeyote wa kurekebisha. Mwanadamu anaruhusu silika yake ya asili itawale, huku akikosa kujali na kuachilia mawazo yake yaende popote, kwa kuwa hakuna ukweli wa kudhibitisha, na kwa hivyo dhana za mwanadamu zinakuwa “ukweli,” bila kujali kama zina dhibitisho. Kwa hivyo mwanadamu anaamini Mungu wake aliyemuwazia akilini mwake, na hamtafuti Mungu wa uhalisi. Ikiwa mtu mmoja ana aina moja ya imani, basi kati ya watu mia moja kuna aina mia moja za imani. Mwanadamu ana imani kama hizi kwa maana hajaona uhalisi wa kazi ya Mungu, kwa sababu amesikia tu kwa masikio yake na hajaona kwa macho yake. Mwanadamu amesikia hekaya na hadithi—lakini amesikia kwa nadra kuhusu maarifa ya ukweli ya kazi ya Mungu. Hivyo ni katika dhana zao ndivyo watu ambao wamekuwa waumini kwa mwaka mmoja tu wanaamini Mungu, na hilo ni kweli pia kwa wale ambao wamemwamini Mungu katika maisha yao yote. Wale ambao hawawezi kuona ukweli daima hawawezi kuepuka imani ambayo wana dhana kwazo kumhusu Mungu. Mwanadamu anaamini kuwa amejiweka huru kutokana na vifungo vya dhana zake za kale, na ameingia eneo jipya. Je, mwanadamu hajui kuwa maarifa ya wale wasioweza kuona uso wa kweli wa Mungu kuwa ni dhana na tetesi? Mwanadamu anafikiria kuwa dhana zake ni sawa, na wala hayana kasoro, na hufikiri kuwa hizi dhana zimetoka kwa Mungu. Leo, mwanadamu anaposhuhudia kazi ya Mungu, anaachilia dhana zilizokuwa zimeongezeka kwa miaka mingi. Mawazo na dhana za awali zilikuwa vizuizi vya kazi ya hatua hii, na inakuwa vigumu kwa mwanadamu kuachana na dhana kama hizo na kupinga mawazo kama yale. Dhana kuhusu kazi hii ya hatua kwa hatua ya wengi wa wale wanaomfuata Mungu hadi leo zimekuwa za kuhuzunisha na watu hawa pole pole wamefanya uadui wa kikaidi na Mungu mwenye mwili hatua kwa hatua, na chanzo cha chuki ni mawazo na dhana za mwanadamu. Ni hasa kwa sababu ukweli haumruhusu mwanadamu kuwa na uhuru wa hiari ya mawazo yake, na, zaidi ya hayo, hauwezi kupingwa na mwanadamu kwa urahisi, na mawazo na dhana za mwanadamu hazistahimili uwepo wa ukweli, na hata zaidi ya hayo, kwa sababu mwanadamu hawezi kufikiria kuhusu usahihi na unyofu wa ukweli, na kwa nia moja tu huachilia mawazo yake, na hutumia dhana yake, kwamba dhana na mawazo ya mwanadamu zimekuwa adui wa kazi ya leo, kazi ambayo haiambatani na dhana za mwanadamu. Hili linaweza kusemwa kuwa kasoro ya dhana za mwanadamu, na wala si dosari ya kazi ya Mungu. Mwanadamu anaweza kufikiria lolote atakalo, lakini hawezi kupinga waziwazi hatua yoyote ya kazi ya Mungu au hata sehemu yoyote; ukweli wa kazi ya Mungu hauwezi kukiukwa na mwanadamu. Unaweza kuruhusu mawazo yako yatawale, na unaweza pia kujumuisha hadithi nzuri kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, lakini kamwe huwezi kupinga ukweli wa kila hatua ya kazi ya Yehova na Yesu; hii ni kanuni, na pia ni amri ya utawala, na mnapaswa kuelewa umuhimu wa masuala haya. Mwanadamu anaamini kuwa hatua hii ya kazi hailingani na dhana za mwanadamu, na hivi sivyo katika hatua mbili zilizopita za kazi. Katika mawazo yake, mwanadamu anaamini kuwa kazi ya hatua mbili zilizopita kwa hakika si sawa na kazi ya leo—lakini je, umewahi kufikiria kuwa kanuni zote za kazi ya Mungu ni sawa, na kuwa kazi Yake huwa vitendo daima, na kuwa, bila kujali enzi, daima kutakuwa na halaiki ya watu wanaokataa na kuupinga ukweli wa kazi Yake? Wale wote ambao leo wanakataa na kuipinga hatua hii ya kazi bila shaka wangempinga Mungu wakati uliopita, kwa kuwa watu kama hawa daima watakuwa adui za Mungu. Watu wanaoujua ukweli wa kazi ya Mungu wataona hatua tatu za kazi kama kazi ya Mungu mmoja, na watatupilia mbali dhana zao. Hawa ni watu wanaomjua Mungu, na watu kama hawa ndio kwa kweli humfuata Mungu. Wakati ambapo usimamizi mzima wa Mungu utakaribia kufika mwisho, Mungu ataweka vitu vyote kulingana na aina. Mwanadamu aliumbwa kwa mikono ya Muumba, na mwishowe lazima kabisa Amrudishe mwanadamu chini ya utawala Wake; huu ndio mwisho wa hatua tatu za kazi. Hatua ya kazi ya siku za mwisho, na hatua mbili zilizopita katika Israeli na Yudea, ni mpango wa Mungu wa usimamizi katika dunia nzima. Hakuna anayeweza kupinga hili, na ni ukweli wa kazi ya Mungu. Ingawa watu hawajapata uzoefu ama kushuhudia nyingi za kazi hizi, ukweli unabaki kuwa ukweli, na hauwezi kukanwa na mwanadamu yeyote. Watu wanaomwamini Mungu katika nchi zote duniani watakubali hatua tatu za kazi. Kama wajua tu hatua moja ya kazi, na huelewi hatua nyingine mbili za kazi, na huelewi kazi ya Mungu katika wakati uliopita, basi huwezi kuongea ukweli wa mpango mzima wa usimamizi wa Mungu, na maarifa yako ya Mungu yameegemea upande mmoja, kwa kuwa katika imani yako katika Mungu humfahamu, ama kumwelewa, na kwa hivyo hustahili kutoa ushuhuda wa Mungu. Bila kujali kama maarifa yako ya sasa ya mambo haya yana kina kirefu ama cha juujuu tu, mwishowe, lazima muwe na maarifa, na ushawishike kabisa, na watu wote wataona uzima wa kazi ya Mungu na kunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Mwishoni mwa kazi hii, madhehebu yote yatakuwa moja, viumbe wote watarejea chini ya utawala wa Muumba, viumbe wote watamwabudu Mungu mmoja wa kweli, na dini zote ovu zitakuwa bure, na hazitaonekana tena.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 11)

Mbona mfululizo huu wa marejeo kwa hatua tatu za kazi? Kupita kwa enzi, maendeleo ya kijamii, na uso wa asili unaobadilika yote hufuata mabadiliko katika hatua tatu za kazi. Mwanadamu hubadilika kwa wakati na kazi ya Mungu, na wala hakui peke yake mwenyewe. Kutajwa kwa hatua tatu za kazi ya Mungu ni kwa ajili ya kuleta viumbe wote, na watu kutoka dini zote, chini ya utawala wa Mungu mmoja. Bila kujali wewe ni wa dini gani, mwishowe nyote mtanyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Ni Mungu Mwenyewe tu anayeweza kufanya kazi hii; haiwezi kufanywa na kiongozi yeyote wa kidini. Kuna dini kadhaa kuu duniani, na kila moja ina kichwa, ama kiongozi, na wafuasi wameenea katika nchi tofauti na maeneo yote duniani; kila nchi, iwe ndogo au kubwa, ina dini tofauti ndani yake. Hata hivyo, bila kujali ni dini ngapi zilizo duniani, watu wote wanaoishi duniani mwishowe wanaishi katika uongozi wa Mungu mmoja, na uwepo wao hauongozwi na viongozi wa kidini au vichwa. Ambayo ni kusema kwamba wanadamu hawaongozwi na kiongozi fulani wa kidini ama kiongozi; badala yake wanadamu wote wanaongozwa na Muumba, aliyeziumba mbingu na nchi, na vitu vyote, na ambaye aliwaumba wanadamu—na huu ni ukweli. Hata ingawa dunia ina dini kadhaa kuu, bila kujali jinsi zilivyo kuu, zote zipo chini ya utawala wa Muumba, na hakuna inayoweza kuzidi wigo wa mamlaka hii. Maendeleo ya wanadamu, maendeleo ya kijamii, maendeleo ya sayansi ya asili—kila moja haitengani na mipango ya Muumba, na kazi hii sio kitu kinachoweza kufanywa na uongozi fulani wa dini. Viongozi wa dini ni viongozi tu wa dini fulani, na hawawezi kuwakilisha Mungu, ama Yule aliyeziumba mbingu na nchi na vitu vyote. Viongozi wa kidini wanaweza kuongoza wale wote walio katika dini yote, lakini hawawezi kuamrisha viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu—huu ni ukweli uliokubalika ulimwenguni. Viongozi wa dini ni viongozi tu, na hawawezi kuwa sawa na Mungu (Muumba). Vitu vyote vi mikononi mwa Muumba, na mwishowe vyote vitarejea mikononi mwa Muumba. Mwanadamu kiasili aliumbwa na Mungu, na haijalishi dini, kila mtu atarejea katika utawala wa Mungu—hili haliwezi kuepukika. Ni Mungu tu Aliye Juu Zaidi kati ya vitu vyote, na mtawala mkuu kati ya viumbe wote lazima pia warejee chini ya utawala Wake. Bila kujali mwanadamu ana hadhi ya juu kiasi gani, hawezi kumfikisha mwanadamu kwenye hatima inayomfaa, wala hakuna anayeweza kuainisha kila kitu kulingana na aina. Yehova mwenyewe alimuumba mwanadamu na kumwainisha kila mmoja kulingana na aina na siku ya mwisho itakapowadia bado Atafanya kazi Yake Mwenyewe, kuanisha kila kitu kulingana na aina—hili haliwezi kufanywa na mwingine isipokuwa Mungu. Hatua tatu za kazi ambazo zilifanywa tangu mwanzo hadi leo zote zilitekelezwa na Mungu Mwenyewe, na zilitekelezwa na Mungu mmoja. Ukweli wa hatua tatu za kazi ni ukweli wa uongozi wa Mungu kwa wanadamu wote, ukweli ambao hakuna anayeweza kuupinga. Mwishoni mwa hatua tatu za kazi, vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina na kurejea chini ya utawala wa Mungu, kwa kuwa duniani kote kuna Mungu mmoja tu, na hakuna dini nyingine. Yule asiyeweza kuiumba dunia hataweza kuiangamiza, ilhali Yule aliyeumba dunia hakika ataiangamiza, na kwa hivyo, kama mtu hana uwezo wa kutamatisha enzi na ni wa kumsaidia mwanadamu kukuza akili zake tu, basi hakika hatakuwa Mungu, na hakika hatakuwa Bwana wa mwanadamu. Hataweza kufanya kazi kuu kama hii; kuna mmoja tu anayeweza kufanya kazi kama hii, na wote wasioweza kufanya hii kazi hakika ni adui wala si Mungu. Dini zote ovu hazilingani na Mungu, na kwa sababu hawalingani na Mungu, wao ni adui za Mungu. Kazi yote inafanywa na huyu Mungu mmoja wa kweli, na ulimwengu mzima unatawaliwa na huyu Mungu mmoja. Bila kujali kama Anafanya kazi Uchina ama Israeli, bila kujali kama kazi inafanywa na Roho ama mwili, yote hufanywa na Mungu Mwenyewe, na haiwezi kufanywa na mwingine yeyote. Ni kabisa kwa sababu Yeye ni Mungu wa wanadamu wote ndiyo kwamba Yeye hufanya kazi kwa njia ya uhuru, pasipo kuwekewa masharti yoyote—na haya ndiyo maono makuu zaidi. Kama kiumbe wa Mungu, kama ungependa kutekeleza jukumu la kiumbe wa Mungu na kuelewa mapenzi ya Mungu, lazima uelewe kazi ya Mungu, lazima uelewe mapenzi ya Mungu kwa viumbe, lazima uelewe mpango Wake wa usimamizi, na lazima uelewe umuhimu wote wa kazi Anayofanya. Wale wasioelewa hivi hawajahitimu kuwa viumbe wa Mungu! Kama kiumbe wa Mungu, kama huelewi ulikotoka, huelewi historia ya mwanadamu na kazi yote iliyofanywa na Mungu, na, hata zaidi, huelewi jinsi mwanadamu ameendelea hadi leo, na huelewi ni nani anayeamuru wanadamu wote, basi huna uwezo wa kutekeleza wajibu wako. Mungu amemwongoza mwanadamu hadi leo, na tangu alipomuumba mwanadamu duniani Hajawahi kumwacha. Roho Mtakatifu daima haachi kufanya kazi, hajawahi kuacha kumwongoza mwanadamu, na hajawahi kumwacha. Lakini mwanadamu hatambui kuwa kuna Mungu, pia hamjui Mungu, na je, kuna jambo la kufedhehesha zaidi kuliko hili kwa viumbe wote wa Mungu? Mungu binafsi humwongoza mwanadamu, lakini mwanadamu haelewi kazi ya Mungu. Wewe ni kiumbe wa Mungu, ilhali huelewi historia yako mwenyewe, na wala hujui ni nani aliyekuongoza katika safari yako, hutambui kazi iliyofanywa na Mungu, na kwa hivyo huwezi kumjua Mungu. Ikiwa hujui sasa, basi hutawahi kuhitimu kutoa ushuhuda kwa Mungu. Leo, Muumba binafsi huwaongoza watu wote kwa mara nyingine, na kuwafanya watu wote kuona hekima Yake, uweza, wokovu, na kustaajabisha Kwake. Ilhali bado hujatambua au kuelewa—na kwa hivyo, je, si wewe ndiwe utakayekosa kupokea wokovu? Wale walio wa Shetani hawaelewi maneno ya Mungu, na wale walio wa Mungu wanaweza kusikia sauti ya Mungu. Wale wote wanaotambua na kuelewa maneno Ninayozungumza ni wale watakaookolewa, na kumshuhudia Mungu; wote wasioelewa maneno Ninayoyazungumza hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu, na ni wale watakaoondolewa. Wale wasioyaelewa mapenzi ya Mungu na hawaitambui kazi ya Mungu hawawezi kupata maarifa ya Mungu, na watu kama hawa hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu. Kama ungependa kumshuhudia Mungu, basi lazima umjue Mungu, na maarifa ya Mungu yanapatikana kwa kupitia kazi ya Mungu. Kwa ufupi, kama ungependa kumjua Mungu, basi lazima ujue kazi ya Mungu: Kufahamu kazi ya Mungu ndilo jambo la umuhimu kabisa. Hatua tatu za kazi zitakapofikia tamati, patafanyika kundi la watu wanaomshuhudia Mungu, kundi la wale wanaomjua Mungu. Watu hawa wote watamjua Mungu na wataweza kuonyesha ukweli kwa matendo. Watakuwa na ubinadamu na hisia, na wote watajua hatua tatu za kazi ya wokovu ya Mungu. Hii ndiyo kazi ambayo itatekelezwa mwishowe, na watu hawa ndio dhihirisho la kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi, na ndio ushuhuda wenye nguvu zaidi kwa kushindwa kwa Shetani. Wale wanaoweza kumshuhudia Mungu wataweza kupokea ahadi na baraka za Mungu, na litakuwa ndilo kundi litakalosalia pale mwisho kabisa, lile linalomiliki mamlaka ya Mungu na lililo na ushuhuda wa Mungu. Pengine wale kati yenu wanaweza wote kuwa sehemu ya kundi hili, ama pengine nusu tu, ama wachache tu—inategemea radhi yenu na ufuatiliaji wenu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 12)

Mpango wa miaka elfu sita umegawa katika hatua tatu za kazi. Hakuna hatua moja pekee itakayowakilisha kazi ya enzi hizo tatu ila inaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya yote. Jina Yehova haliwezi kuwakilisha tabia yote ya Mungu. Ukweli kuwa Alitekeleza kazi katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kuwa Mungu Anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria. Yehova alitengeneza sheria kwa mwanadamu na kutoa amri, Akimuuliza mwanadamu ajenge hekalu na madhabahu; kazi Aliyofanya inawakilisha tu Enzi ya Sheria. Kazi Aliyoifanya haidhibitishi kuwa Mungu ni Mungu Anayemwamuru mwanadamu kufuata sheria, Mungu Aliye hekaluni, ama Mungu Aliye mbele ya madhabahu. Haya hayawezi kusemwa. Kazi chini ya sheria inaweza tu kuwakilisha enzi moja. Kwa hivyo, kama Mungu Alifanya kazi katika Enzi ya Sheria pekee, mwanadamu angemfafanua Mungu na kusema, “Mungu ni Mungu Aliye hekaluni. Ili kumtumikia Mungu, lazima tuvae mavazi ya kikuhani na tuingie hekaluni.” Iwapo kazi katika Enzi ya Neema haingetekelezwa na Enzi ya Sheria ingeendelea mpaka wakati huu wa sasa, mwanadamu hangefahamu kuwa Mungu pia ni mwenye huruma na upendo. Iwapo kazi katika Enzi ya Sheria haingefanywa, na badala yake kazi katika Enzi ya Neema pekee, basi yote ambayo mwanadamu angefahamu ni kwamba Mungu Anakomboa tu mwanadamu na kumsamehe dhambi zake. Wangefahamu tu kuwa Yeye ni mtakatifu na asiye na hatia, kwamba Anaweza kujitoa kafara na kusulubishwa kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu angejua tu kuhusu haya na asiwe na ufahamu wa mambo mengine yoyote. Kwa hivyo kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu. Enzi ya Sheria inawakilisha vipengele vingine, Enzi ya Neema vipengele vingine na enzi hii vipengele vingine. Tabia ya Mungu inaweza tu kuonekana kwa mchanganyiko wa hatua zote tatu. Ni wakati tu mwanadamu anajua hatua hizi tatu ndipo anaweza kuipokea kikamilifu. Hakuna hatua kati ya hizo tatu ambayo inaweza kuachwa. Utaiona tu tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake mara tu utakapozijua hatua hizi tatu za kazi. Ukweli kamba Mungu alikamilisha kazi yake katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kwamba Yeye ni Mungu chini ya sheria tu, na ukweli kamba alikamilisha kazi Yake ya ukombozi haimaanishi kuwa Mungu Atamkomboa mwanadamu milele. Hizi zote ni hitimisho zilizofanywa na mwanadamu kuhusu jambo hilo. Enzi ya Neema ikiwa imefika mwisho, huwezi basi kusema kuwa Mungu ni wa msalaba tu na kuwa msalaba pekee unawakilisha wokovu wa Mungu. Ukifanya hivyo, basi utakuwa unamfasili Mungu. Katika hatua hii, Mungu Anafanya zaidi kazi ya Neno, lakini huwezi kusema kuwa Mungu hajawahi kuwa Mwenye huruma kwa mwanadamu na kwamba yote Aliyoleta ni kuadibu na hukumu. Kazi katika siku za mwisho inaonyesha wazi kazi ya Yehova na ile ya Yesu na mafumbo yote yasioeleweka na mwanadamu. Hii inafanywa ili kuonyesha hatima na mwisho wa binadamu na kukamilisha kazi yote ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Hatua hii ya kazi katika siku za mwisho huleta kila kitu kufika mwisho. Mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu yanapaswa kufunuliwa ili kumpa mwanadamu ufahamu na kuweza kuelewa kwa kina katika mioyo yao. Hapo tu ndipo wanadamu wataweza kuainishwa kulingana na aina. Baada tu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilishwa ndipo mwanadamu atapata kuelewa tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake, kwani usimamizi Wake utakuwa umefika mwisho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 13)

Kazi yote iliyofanyika katika mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita imefika mwisho sasa. Ni baada tu ya kazi hii kubainika wazi kwa wanadamu na kutekelezwa miongoni mwa wanadamu ndipo watakapofahamu tabia ya Mungu na kile alicho na anacho. Kazi za enzi hizi zitakapokamilika, mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu yatakuwa yamebainika, ukweli wote ambao haukuwa unaeleweka utawekwa wazi, na mwanadamu atakuwa ameambiwa njia na hatima ya baadaye. Hii ndio kazi yote inayopaswa kufanyika katika hatua hii. Ingawa njia ambayo mwanadamu hutembea leo pia ni njia ya msalaba na ya kuteseka, kile ambacho mwanadamu wa leo hutenda, hula, hunywa na hufurahia ni tofauti zaidi na yale ya mwanadamu aliyekuwa chini ya sheria na katika Enzi ya Neema. Kinachohitajika kutoka kwa mwanadamu wakati huu sio kama ilivyokuwa kitambo na zaidi sio kama kilichohitajika kutoka kwake katika Enzi ya Sheria. Na ni kipi kilichoulizwa kwa mwanadamu chini ya Sheria Mungu alipokuwa akifanya kazi huko Israeli? Hawakuulizwa chochote zaidi ya kuiheshimu Sabato na Sheria za Yehova. Lakini si hivyo katika wakati huu. Siku ya Sabato, mwanadamu anafanya kazi, hukusanyika na kuomba kama kawaida, na hakuna vizuizi vinavyowekwa. Wale katika Enzi ya Neema ilibidi wabatizwe, na pia zaidi walitarajiwa kufunga, kuvunja mkate, kunywa divai, kufunika vichwa vyao na kuwaoshea wengine miguu yao. Sasa, sheria hizi zimefutwa na mahitaji makuu yanaulizwa kutoka kwa mwanadamu, kwani kazi ya Mungu inazidi kuwa ya kina na kuingia kwa mwanadamu kunafika kiwango cha juu. Zamani, Yesu Aliweka mikono Yake juu ya mwanadamu na kuomba, lakini sasa kwamba kila kitu kimesemwa, kuwekelea mikono kuna maana gani? Maneno pekee yanaweza kupata matokeo. Alipowekelea mikono Yake juu ya mwanadamu hapo awali, ilikuwa ni kwa ajili ya kumbariki na kumponya mwanadamu. Hivyo ndivyo Roho Mtakatifu Alivyofanya kazi wakati huo, lakini sio hivyo wakati huu. Wakati huu, Roho Mtakatifu Anatumia maneno katika kazi Yake ili kupata matokeo. Ameyafanya maneno Yake wazi kwenu, na mnapaswa tu kuyaweka katika matendo. Maneno Yake ni mapenzi Yake na yanaonyesha kazi Atakayofanya. Kupitia katika maneno Yake, utaweza kuelewa mapenzi Yake na yale ambayo Anauliza upate, na unaweza kuyaweka tu maneno Yake katika matendo moja kwa moja bila haja ya kuwekelea mikono. Wengine wanaweza kusema, “Wekelea mikono Yako juu yangu! Wekelea mikono yako juu yangu ili niweze kupokea baraka zako na kushiriki kwako.” Haya yote ni mazoezi yaliyopitwa na wakati na ambayo yanakataliwa katika wakati huu, kwani enzi zimebadilika. Roho Mtakatifu Anafanya kazi kulingana na enzi, sio tu katika mapenzi Yake ama kulingana na masharti. Enzi zimebadilika, na enzi mpya lazima ilete kazi mpya. Huu ni ukweli wa kila hatua ya kazi, na hivyo kazi Yake haiwezi kurudiwa. Katika Enzi ya Neema, Yesu Alifanya nyingi ya kazi hiyo, kama kuponya magonjwa, kukemea mapepo, kuwekelea mikono Yake juu ya wanadamu, na kumbariki mwanadamu. Hata hivyo, kuendelea kufanya hivyo hakutasaidia chochote katika wakati huu. Roho Mtakatifu Alifanya kazi hivyo katika huo wakati, kwani ilikuwa Enzi ya Neema, na mwanadamu alipewa neema ya kutosha ili afurahie. Mwanadamu hakuhitajika kulipa gharama yoyote na angepokea neema mradi tu angekuwa na imani. Kila mtu alitendewa kwa neema kubwa. Sasa, enzi imebadilika, na kazi ya Mungu imeendelea zaidi; kupitia kuadibu na hukumu Yake, uasi wa mwanadamu na vitu vichafu katika mwanadamu vitatupiliwa mbali. Jinsi ilivyokuwa hatua ya wokovu, ilimbidi Mungu kufanya kazi hiyo, Akimwonyesha mwanadamu neema ya kutosha ili mwanadamu afurahie, ili Amkomboe mwanadamu kutoka kwa dhambi, na kwa neema, amsamehe mwanadamu dhambi zake. Hatua hii ya sasa ni ya kufichua udhalimu ulio ndani ya mwanadamu kwa njia ya kuadibu, hukumu, kupigwa na maneno, na vile vile nidhamu na ufunuo wa maneno, ili baadaye binadamu waweze kuokolewa. Hii ni kazi ya undani zaidi kuliko ukombozi. Katika Enzi ya Neema, mwanadamu alifurahia neema ya kutosha na amezoea neema hii, kwa hivyo sio ya kufurahiwa na mwanadamu tena. Kazi kama hii imepitwa na wakati sasa na haitafanyika tena. Sasa, mwanadamu anaokolewa kupitia hukumu ya neno. Baada ya mwanadamu kuhukumiwa, kuadibiwa na kusafishwa, tabia yake basi inabadilika. Je sio kwa sababu ya maneno ambayo Nimenena? Kila hatua ya kazi inafanywa kulingana na maendeleo ya binadamu wote na kwa enzi. Kazi yote ina umuhimu wake; inafanywa kwa ajili ya wokovu wa mwisho, ili binadamu awe na hatima nzuri baadaye, na kwa binadamu kuainishwa kulingana na aina mwishowe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 14)

Kila hatua ya kazi ya Roho Mtakatifu inahitaji kwa sawia ushuhuda kutoka kwa mwanadamu. Kila hatua ya kazi ni vita kati ya Mungu na Shetani, na mlengwa katika vita hivi ni Shetani, huku atakayekamilishwa na kazi hii ni mwanadamu. Kazi ya Mungu kuweza kuzaa au kutozaa matunda kunategemea jinsi ushuhuda wa mwanadamu kwa Mungu ulivyo. Huu ushuhuda ndio Mungu anaohitaji kutoka kwa wale wanaomfuata; ni ushuhuda unaofanywa mbele ya Shetani, na pia unaothibitisha athari za kazi Yake. Usimamizi mzima wa Mungu umegawika katika hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayofaa yanatakiwa kutoka kwa mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu wote huwa ya juu hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,” na kwa njia hii mahitaji ya mwanadamu huwa ya juu hata zaidi, na mahitaji ya mwanadamu kutoa ushuhuda huwa ya juu hata zaidi. Kadiri mwanadamu alivyo na uwezo wa kushirikiana na Mungu kwa kweli, ndivyo anavyozidi kumtukuza Mungu. Ushirikiano wa mwanadamu ndio ushuhuda anaohitajika kuwa nao, na ushuhuda alio nao ndio matendo ya mwanadamu. Na kwa hivyo, kazi ya Mungu iweze au isiweze kuwa na matokeo yanayohitajika, na paweze ama pasiweze kuwa na ushuhuda wa kweli, ni mambo ambayo yameunganishwa yasiyochanganulika na ushirikiano na ushuhuda wa mwanadamu. Wakati kazi itakapokwisha, yaani, wakati usimamizi wote wa Mungu utakapofikia kikomo chake, mwanadamu atahitajika kuwa na ushuhuda wa hali ya juu, na wakati kazi ya Mungu itakapofika mwisho wake, matendo na kuingia kwa mwanadamu vitafikia upeo wake. Wakati wa kale, mwanadamu alihitajika kutii sheria na amri, na alihitajika kuwa mwenye subira na mnyenyekevu. Leo, mwanadamu anahitajika kutii mipango yote ya Mungu na awe na upendo mkuu wa Mungu, na hatimaye bado anahitajika kumpenda Mungu katika taabu. Hatua hizi tatu ndizo Mungu anazozitazamia kutoka kwa mwanadamu, hatua kwa hatua, katika usimamizi Wake wote. Kila hatua ya kazi ya Mungu huzidisha kina kuliko iliyopita, na katika kila hatua, mahitaji kwa mwanadamu ni makubwa kuliko yaliyopita, na kwa njia hii, usimamizi mzima wa Mungu huonekana. Ni hasa kwa sababu mahitaji ya mwanadamu kila mara huwa ya juu kiasi kwamba tabia yake kila mara inafikia viwango anavyovihitaji Mungu, na ni hapo tu ambapo wanadamu wote wanaanza kujiondoa polepole kutoka kwa ushawishi wa Shetani hadi, ambapo kazi ya Mungu itafikia kikomo kabisa, ndio wanadamu wote watakuwa wameokolewa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Wakati huo utakapowadia, kazi ya Mungu itakuwa imefika mwisho wake, na ushirikiano wa mwanadamu na Mungu ili kufikia mabadiliko katika tabia yake hautakuwepo tena, na wanadamu wote wataishi katika nuru ya Mungu, na kuanzia hapo kuendelea, hapatakuwa na uasi au upinzani wowote kwa Mungu. Pia Mungu hatamwekea mwanadamu matakwa, na patakuwepo na ushirikiano wenye upatanifu zaidi kati ya mwanadamu na Mungu, ambao utakuwa maisha ya mwanadamu na Mungu pamoja, maisha ambayo yatafuatia baada ya usimamizi wa Mungu kukamilishwa kabisa, na baada ya mwanadamu kuokolewa kikamilifu kutoka katika mafumbato ya Shetani. Wale ambao hawawezi kutafuata kwa ukaribu nyayo za Mungu hawana uwezo wa kufikia maisha kama hayo. Watakuwa wamejishusha ndani ya giza, ambapo watalia na kusaga meno; hao ndio watu wanaoamini katika Mungu lakini hawamfuati Yeye, wanaoamini katika Mungu lakini hawatii kazi Yake yote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 15)

Katika kazi yote ya usimamizi, kazi muhimu sana ni wokovu kutoka katika ushawishi wa Shetani. Kazi muhimu ni kumshinda kabisa mwanadamu aliyepotoka, na hivyo kurejesha heshima ya awali ya Mungu katika moyo wa mwanadamu, na kumruhusu kufikia maisha ya kawaida, ni sawa na kusema, maisha ya kawaida ya kiumbe wa Mungu. Kazi hii ni muhimu, na ni kiini cha kazi ya usimamizi. Katika hatua tatu za kazi ya wokovu, hatua ya kwanza ya kazi ya Enzi ya Sheria inatofautiana sana na kiini cha kazi ya usimamizi; ilikuwa tu ina kuonekana kwa mbali kwa kazi ya wokovu, na haikuwa mwanzo wa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu kutoka katika utawala wa Shetani. Hatua ya kwanza ya kazi ilifanywa na Roho kwa sababu, chini ya sheria, mwanadamu alijua tu kuzishika sheria, na hakuwa na ukweli zaidi, na kwa sababu kazi katika Enzi ya Sheria haikujihusisha na kubadilisha tabia ya mwanadamu, sembuse haikuwa inajihusisha na kazi ya jinsi ya kumwokoa mwanadamu kutoka katika utawala wa Shetani. Roho wa Mungu alikamilisha hatua hii rahisi ya kazi ambayo haikujihusisha na tabia iliyopotoka ya mwanadamu. Hatua hii ya kazi ilikuwa na uhusiano mdogo na kiini cha usimamizi na haikuwa na uhusiano mkubwa na kazi rasmi ya wokovu wa mwanadamu, na kwa hivyo haikumhitaji Mungu ili aweze kuifanya kazi Yake. Kazi inayofanywa na Roho ni dhahiri na haifahamiki, na ya kutisha kwa kina isiyofikiwa kwa mwanadamu; Roho hafai kikamilifu kwa ajili ya kufanya kazi ya wokovu moja kwa moja, na hafai kikamilifu kwa ajili ya kumpa mwanadamu uzima moja kwa moja. Kinachomfaa zaidi mwanadamu ni kubadilisha kazi ya Roho na kuwa katika hali ambayo inamkaribia mwanadamu, yaani, kile kinachomfaa mwanadamu zaidi ni Mungu kuwa mtu wa kawaida ili kufanya kazi Yake. Hili linahitaji Mungu apate mwili ili kuchukua kazi ya Roho, na kwa mwanadamu, hakuna njia inayofaa zaidi ya Mungu kufanya kazi. Kati ya hatua hizi tatu za kazi, hatua mbili zinafanywa na mwili, na hatua hizi mbili ni awamu muhimu ya kazi ya usimamizi. Kupata mwili huku kuwili kunakamilishana na kuafikiana. Hatua ya kwanza ya Mungu mwenye mwili iliweka msingi kwa ajili ya hatua ya pili, na tunaweza kusema kwamba kupata mwili huku kuwili kwa Mungu kunafanya hatua moja, na zote hazina ulinganifu. Hatua mbili hizi za kazi ya Mungu zinafanywa na Mungu katika utambulisho Wake katika mwili kwa sababu zina umuhimu sana katika kazi nzima ya usimamizi. Inaweza kusemwa kuwa, bila kazi ya Mungu mwenye mwili katika hatua mbili hizi, kazi nzima ya usimamizi ingefikia kikomo kwa ghafla, na kazi ya kumwokoa mwanadamu isingekuwa kitu isipokuwa maneno matupu. Haijalishi kazi hii ni muhimu au si muhimu lakini imejikita katika mahitaji ya mwanadamu, na uhalisi wa upotovu wa mwanadamu, na uzito wa kutotii kwa Shetani na usumbufu wake katika kazi. Mhusika sahihi ni yule anayeifanya kazi ametabiriwa na asili ya kazi inayofanywa na huyo mfanyakazi, na umuhimu wa kazi. Unapokuja umuhimu wa kazi hii, kwa misingi ya mbinu ya kutumia—kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu, au kazi inayofanywa na Mungu mwenye mwili, au kazi inayofanywa kupitia mwanadamu—ya kwanza kuondolewa ni kazi inayofanywa kupitia mwanadamu, na kulingana na asili ya kazi, na asili ya kazi ya Roho dhidi ya ile ya mwili, hatimaye inaamuliwa kwamba kazi inayofanywa na mwili ni ya manufaa zaidi kwa mwanadamu kuliko kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho, na inakuwa na manufaa zaidi. Hili ni wazo la Mungu wakati wa kuamua ama kazi ifanywe na Roho au ifanywe na mwili. Kuna umuhimu na msingi katika kila hatua ya kazi. Siyo fikra tu zisizo na msingi, na wala hazifanywi kiholela; kuna hekima fulani ndani yake. Huo ndio ukweli wa kazi zote za Mungu. Hasa, kuna mpango wa Mungu zaidi katika kazi kubwa kama hiyo kwa kuwa Mungu mwenye mwili akifanya kazi miongoni mwa wanadamu. Na kwa hivyo, hekima ya Mungu na uungu Wake wote unaakisiwa katika kila tendo Lake, fikira, na wazo katika kufanya kazi; huu ndio uungu wa Mungu ambao uko imara na wenye mpangilio. Fikira hizi na mawazo ya kutatiza ni ngumu kwa mwanadamu kuwaza, na mambo magumu kwa mwanadamu kuamini, aidha, magumu kwa mwanadamu kuyafahamu. Kazi inayofanywa na mwanadamu ni kulingana na kanuni ya ujumla, ambayo, kwa mwanadamu, ni ya kuridhisha sana. Lakini ikilinganisha na kazi ya Mungu, kuna tofauti kubwa sana; ingawa matendo ya Mungu ni makuu na kazi ya Mungu ni ya kiwango cha juu sana, nyuma yake kuna mipango na mipangilio midogo ya uhakika ambayo haiwezi kufikirika kwa mwanadamu. Kila hatua ya kazi Yake sio kulingana na kanuni tu, lakini pia inajumuisha vitu vingi ambavyo haviwezi kusemwa kwa lugha ya kibinadamu, na haya ni mambo ambayo hayaonekani kwa mwanadamu. Bila kujali kama ni kazi ya Roho au kazi ya Mungu mwenye mwili, kila kazi inajumuisha mpango wa kazi Yake. Hafanyi kazi bila kuwa na msingi, na hafanyi kazi isiyokuwa na maana. Roho anapofanya kazi moja kwa moja, ni kwa malengo Yake, na Anapokuwa mwanadamu (ambayo ni sawa na kusema, Anapobadilisha ganda Lake la nje) kufanya kazi, ni zaidi hata na lengo Lake. Kwa sababu ipi nyingine kwa urahisi Abadilishe utambulisho Wake vivi hivi tu? Kwa sababu ipi nyingine kwa urahisi Abadilike awe mtu ambaye anachukuliwa kuwa ni duni na kuteswa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 16)

Kazi inayofanywa kwa sasa imesukuma mbele kazi ya Enzi ya Neema; yaani, kazi katika mpango mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita imesonga mbele. Ingawa Enzi ya Neema imeisha, kazi ya Mungu imeendelea mbele. Kwa nini Ninasema mara kwa mara kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria? Hii ina maana kwamba kazi ya siku hii ni mwendelezo wa kazi iliyofanyika katika Enzi ya Neema na maendeleo ya kazi iliyofanyika katika Enzi ya Sheria. Hatua hizi tatu zinaingiliana kwa karibu na kuunganika moja kwa inayofuata kwa karibu. Kwa nini pia Ninasema kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya ile iliyofanywa na Yesu? Tuseme kwamba hatua hii haingejengwa juu ya kazi iliyofanywa na Yesu, ingebidi kusulubiwa kwingine kufanyike katika hatua hii, na kazi ya ukombozi ya hatua iliyopita ingelazimika kufanywa upya tena. Hii isingekuwa na maana yoyote. Kwa hiyo, sio kwamba kazi imekamilika kabisa, bali ni kwamba enzi imesonga mbele, na kiwango cha kazi kimewekwa juu kabisa kuliko kilivyokuwa kabla. Inaweza kusemwa kwamba hatua hii ya kazi imejengwa juu ya msingi wa Enzi ya Sheria na kwenye mwamba wa kazi ya Yesu. Kazi hii inajengwa hatua kwa hatua, na hatua hii sio mwanzo mpya. Ni muungano tu wa hatua tatu za kazi ndio unaweza kuchukuliwa kuwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita. Kazi ya hatua hii inafanywa kwa msingi wa kazi ya Enzi ya Neema. Ikiwa hatua hizi mbili za kazi hazikuhusiana, kwa nini basi kusulubiwa hakurudiwi katika hatua hii? Kwa nini Sibebi dhambi za mwanadamu, lakini badala yake Naja kumhukumu na kumwadibu mwanadamu moja kwa moja? Ikiwa kazi Yangu ya kumhukumu na kumwadibu mwanadamu na kuja Kwangu saa hii si kwa njia ya Roho Mtakatifu na hakukufuata kusulubiwa, basi Nisingekuwa na sifa zinazostahili kumhukumu na kumwadibu mwanadamu. Kazi katika hatua inajenga kabisa juu ya kazi katika hatua iliyotangulia. Hiyo ndiyo maana ni kazi kama hii tu ndiyo inaweza kumleta mwanadamu katika wokovu hatua kwa hatua. Yesu pamoja na Mimi tunatoka kwa Roho Mmoja. Ingawa miili Yetu haina uhusiano, Roho Zetu ni moja; ingawa kile Tunachofanya na kazi Tulizo nazo hazifanani, kwa asili Tunafanana; Miili Yetu ina maumbo tofauti, lakini hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya enzi na mahitaji tofauti ya kazi Yetu; huduma Zetu hazifanani, hivyo kazi Tunayoileta na tabia Tunayoifichua kwa mwanadamu pia ni tofauti. Ndiyo maana kile ambacho mwanadamu anakiona na kukielewa leo hii si kama kile cha wakati uliopita; ni hivyo kwa sababu ya mabadiliko ya enzi. Ingawa jinsia na maumbo ya miili Yao ni tofauti, na kwamba hawakuzaliwa katika familia moja, sembuse katika kipindi kimoja, hata hivyo Roho Zao ni moja. Ingawa miili Yao haina uhusiano wa damu au kimwili kwa namna yoyote ile, haipingiki kwamba Wao ni Mungu kupata mwili katika vipindi viwili tofauti vya nyakati. Ni ukweli usiopingika kwamba Wao ni miili ya nyama ya Mungu, ingawa hawatoki katika ukoo mmoja na hawatumii lugha moja ya binadamu (mmoja alikuwa mwanamume aliyezungumza lugha ya Wayahudi na mwingine ni mwanamke anayezungumza Kichina pekee). Ni kwa sababu hizi ndiyo Wameishi katika nchi tofauti kufanya kazi ambayo inampasa kila mmoja kufanya, na katika nyakati tofauti vilevile. Licha ya ukweli kwamba Wao ni Roho moja, wakiwa na asili inayofanana, hakuna mfanano wa wazi kabisa kati ya ngozi za nje za miili Yao. Wanashiriki tu ubinadamu sawa, lakini sura ya nje ya miili Yao na kuzaliwa Kwao hakufanani. Mambo haya hayana athari katika kazi Zao au maarifa aliyonayo mwanadamu juu Yao, maana, kimsingi, Wao ni Roho moja na hakuna anayeweza kuwatenganisha. Ingawa Hawana uhusiano wa damu, nafsi Zao zote zinaongoza Roho Zao, ambazo zinawapa kazi tofauti katika nyakati tofauti, na miili Yao kwa ukoo tofauti. Roho wa Yehova si baba wa Roho wa Yesu na Roho wa Yesu si mwana wa Roho wa Yehova: Ni Roho moja. Vile vile Kama vile Mungu mwenye mwili wa leo na Yesu. Ingawa Hawahusiani kwa damu, ni Wamoja; hii ni kwa sababu Roho Zao ni moja. Mungu anaweza kufanya kazi ya rehema na wema, vilevile na ile kazi ya hukumu ya haki na kumwadibu mwanadamu, na ile ya kuleta laana kwa mwanadamu; na hatimaye, Anaweza kufanya kazi ya kuuharibu ulimwengu na kuwaadhibu waovu. Je, hafanyi haya yote Mwenyewe? Je, hii si kudura ya Mungu? Aliweza kutangaza sheria kwa ajili ya mwanadamu na kumpa amri, na aliweza pia kuwaongoza Waisraeli wa awali katika kuishi maisha yao duniani na kuwaongoza kujenga hekalu na madhabahu, Akiwatawala Waisraeli wote. Kwa kutegemea mamlaka Yake, Aliishi pamoja na Waisraeli duniani kwa miaka elfu mbili. Waisraeli hawakuthubutu kumwasi; wote walimheshimu Yehova na walifuata amri Zake. Hii ilikuwa Kazi iliyofanywa kwa kutegemea mamlaka Yake na kudura Yake. Kisha, katika Enzi ya Neema, Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu wote walioanguka (sio Waisraeli pekee). Alionyesha rehema na wema kwa mwanadamu. Yesu ambaye mwanadamu alimwona katika Enzi ya Neema Alikuwa amejazwa na wema na siku zote Alikuwa mwenye upendo kwa mwanadamu, maana Alikuwa amekuja kuwakomboa wanadamu kutoka dhambini. Aliweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao hadi pale ambapo kusulubiwa Kwake kuliwakomboa wanadamu kutoka dhambini kabisa. Wakati huo, Mungu alionekana kwa mwanadamu kwa rehema na wema; yaani, Alijitoa sadaka kwa ajili ya mwanadamu na Alisulubiwa kwa ajili ya dhambi za mwanadamu ili kwamba ziweze kusamehewa milele. Alikuwa mwenye rehema, mwenye huruma, mwenye upendo na mstahimilivu. Na wale wote waliomfuata Yesu katika Enzi ya Neema nao pia walitafuta kuwa wastahimilivu na wenye upendo katika mambo yote. Walistahimili mateso kwa muda mrefu, na hawakuwahi kulipiza kisasi hata walipopigwa, kulaaniwa au kupigwa mawe. Lakini haya hayawezi kuwa hivyo tena katika hatua ya mwisho. Vivyo hivyo, hata ingawa Roho Zao zilikuwa moja, kazi ya Yesu na Yehova hazikufanana kabisa. Kazi ya Yehova haikuwa kwa ajili ya kukamilisha enzi bali kuiongoza, kukaribisha maisha ya wanadamu duniani. Hata hivyo, kazi sasa ni kuwashinda wale walio katika mataifa yasiyo ya Wayahudi na ambao wamepotoshwa sana, sio tu watu wateule wa Mungu nchini China, bali ulimwengu mzima na wanadamu wote. Inaweza kuonekana kwako kwamba kazi hii inafanywa Uchina pekee, lakini kwa kweli imekwishaanza kusambaa katika nchi za ughaibuni. Ni kwa nini wageni mara kwa mara wanatafuta njia ya kweli? Hiyo ni kwa sababu Roho tayari amekwishaanza kazi, na maneno yanayonenwa sasa yanaelekezwa kwa watu ulimwenguni kote. Na hili, nusu ya kazi tayari inafanywa. Kutoka kuumbwa kwa dunia hadi sasa, Roho wa Mungu ameendeleza hii kazi kubwa, na aidha Amefanya kazi tofauti katika enzi tofauti, na katika mataifa tofauti. Watu wa kila enzi wanaiona tabia Yake tofauti, ambayo kwa asili inafichuliwa kupitia kazi tofauti Anazozifanya. Yeye ni Mungu, aliye mwingi wa rehema na wema; Yeye ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mwanadamu na mchungaji wa mwanadamu; lakini pia Yeye ni hukumu, kuadibu, na laana kwa mwanadamu. Angeweza kumwongoza mwanadamu kuishi duniani kwa miaka elfu mbili na pia Angeweza kuwaokoa wanadamu waliopotoka kutoka dhambi. Leo, pia Anaweza kuwashinda wanadamu ambao hawamjui na kuwafanya wawe chini ya miliki Yake, ili kwamba wote wajinyenyekeze kwake kikamilifu. Mwishowe, Atachoma yote ambayo si safi na ambayo ni dhalimu ndani ya wanadamu katika ulimwengu mzima, ili kuwaonyesha kwamba Yeye si Mungu wa Rehema, na upendo tu, si Mungu wa hekima, na maajabu tu, si Mungu mtakatifu tu, bali, hata zaidi ni Mungu anayemhukumu mwanadamu. Kwa waovu miongoni mwa wanadamu, Yeye ni mwenye kuchoma, kuhukumu na kuadhibu; kwa wale ambao wanapaswa kukamilishwa, Yeye ni mateso, usafishaji, na majaribu, na vilevile faraja, ruzuku, utoaji wa maneno, kushughulika na kupogoa. Na kwa wale ambao wanaondolewa, Yeye ni adhabu na vilevile malipo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 17)

Baada ya kufanya kazi Yake ya miaka 6,000 hadi leo, Mungu tayari amefichua vitendo Vyake vingi, sababu ya kimsingi ikiwa ni kumshinda Shetani na kuleta wokovu kwa binadamu wote. Anatumia fursa hii kuruhusu kila kitu mbinguni, kila kitu kilicho duniani, kila kitu kinachopatikana baharini pamoja na kila kifaa cha mwisho ambacho Mungu aliumba ulimwenguni kuweza kuona uweza wa Mungu na kushuhudia vitendo vyote vya Mungu. Yeye huchukua fursa ya kumshinda Shetani ili kufichua vitendo Vyake kwa binadamu na kuwaruhusu watu kuweza kumsifu Yeye na kuitukuza hekima Yake kwa kumshinda Shetani. Kila kitu duniani, mbinguni na ndani ya bahari humletea utukufu, huusifu uweza Wake, kinasifu vitendo Vyake vyote na kutamka kwa sauti jina Lake takatifu. Hii ni ithibati ya ushindi Wake dhidi ya Shetani; hii ni ithibati ya Yeye kumshinda Shetani; na la muhimu zaidi, ni ithibati ya wokovu Wake kwa binadamu. Viumbe wote wa Mungu humletea utukufu, humsifu Yeye kwa kumshinda adui Wake na kurudi kwa ushindi na humsifu Yeye kama Mfalme mkubwa mwenye ushindi. Kusudio Lake si kumshinda Shetani tu, na hivyo basi kazi Yake imeendelea kwa miaka 6,000. Anatumia kushindwa kwa Shetani kuwaokoa binadamu; Anakutumia kushindwa kwa Shetani kufichua vitendo Vyake vyote na kufichua utukufu Wake wote. Atapata utukufu, na umati wote wa malaika utaweza kushuhudia utukufu Wake wote. Wajumbe walio mbinguni, wanadamu walio duniani na viumbe wote walio duniani watauona utukufu wa Muumba. Hii ndiyo kazi Aifanyayo. Viumbe vyake kule mbinguni na duniani vyote vitauona utukufu Wake, na Atarudi kwa vifijo na nderemo baada ya kumshinda Shetani kabisa na kumruhusu binadamu amsifu Yeye. Ataweza hivyo basi kutimiza kwa ufanisi vipengele hivi viwili. Mwishowe binadamu wote watashindwa na Yeye, na atamwondoa yeyote yule anayepinga au kuasi, hivi ni kusema, Atawaondoa wale wote wanaomilikiwa na Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 18)

Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya nchi ya Israeli, lakini, Alichagua kikundi cha watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.

Wakati huu, umuhimu, kusudi na awamu za kazi ya Yehova huko Israeli zilikuwa kuanzisha kazi Yake katika dunia nzima, ambayo, ikichukua Israeli kama kituo chake, ilienea polepole hadi kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Hii ni kanuni ambayo kwayo Anafanya kazi katika ulimwengu mzima—kuunda mfano na kisha kuupanua hadi watu wote ulimwenguni watakuwa wamepokea injili Yake. Waisraeli wa kwanza walikuwa wa ukoo wa Nuhu. Watu hawa walikuwa wamejawa tu na pumzi ya Yehova, na walielewa kiasi cha kutosha ili kushughulikia mambo muhimu ya msingi ya maisha, lakini hawakujua Yehova alikuwa Mungu wa aina gani, au mapenzi Yake kwa mwanadamu, sembuse jinsi wanavyopaswa kumcha Bwana wa viumbe vyote. Kuhusu iwapo kulikuwa na sheria na kanuni za kutiiwa,[a] au iwapo kulikuwa na wajibu ambayo viumbe walioumbwa wanapaswa kumfanyia Muumba, wa ukoo wa Adamu hawakujua hata kidogo kuhusu mambo haya. Yote waliyojua ilikuwa kwamba mume anapaswa kutokwa jasho na kufanya kazi ili kukimu familia yake, na kwamba mke anapaswa kumtii mume wake na kuendeleza jamii ya binadamu ambao Yehova alikuwa ameumba. Kwa maneno mengine, watu wa aina hii, ambao walikuwa na pumzi ya Yehova na uzima Wake pekee, hawakujua kabisa kuhusu jinsi ya kufuata sheria za Mungu au jinsi ya kumridhisha Bwana wa viumbe vyote. Walielewa kidogo sana. Kwa hivyo ingawa hakukuwa na kitu kisicho kipotovu au cha udanganyifu mioyoni mwao na wivu na ugomvi viliibuka miongoni mwao mara chache, hata hivyo hawakuwa na maarifa au ufahamu wa Yehova, Bwana wa viumbe vyote. Mababu hawa wa mwanadamu walijua tu kula vitu vya Yehova, na kufurahia vitu vya Yehova, lakini hawakujua kumcha Yehova: hawakujua kwamba Yehova ndiye Yule wanayepaswa kumwabudu kwa kupiga magoti. Kwa hiyo wangeweza kuitwa viumbe Wake vipi? Kama hali ingekuwa hivi, je maneno, “Yehova ndiye Bwana wa viumbe vyote” na “Alimuumba mwanadamu ili mwanadamu aweze kumdhihirisha Yeye, kumtukuza Yeye, na kumwakilisha Yeye”—hayangekuwa yamesemwa bure? Watu ambao hawamchi Yehova wangewezaje kuwa ushuhuda kwa utukufu Wake? Wangewezaje kuwa dhihirisho la utukufu Wake? Je, maneno ya Yehova “Nilimuumba mwanadamu kwa mfano Wangu” si yangekuwa silaha mikononi mwa Shetani basi—yule mwovu? Maneno haya basi hayangekuwa alama ya fedheha kwa Yehova kumuumba mwanadamu? Ili kukamilisha hatua hiyo ya kazi, baada ya kuwaumba wanadamu, Yehova hakuwaagiza au kuwaongoza kutoka wakati wa Adamu hadi ule wa Nuhu. Badala yake, baada ya dunia kuharibiwa na gharika tu ndiyo wakati ambapo Alianza rasmi kuwaongoza Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa Adamu. Kazi na matamshi Yake huko Israeli yaliwapa watu wote wa Israeli mwongozo walipokuwa wakiishi maisha yao katika nchi yote ya Israeli, na kwa njia hii yakaonyesha binadamu kwamba Yehova hakuweza tu kupuliza pumzi ndani ya mwanadamu, ili aweze kuwa na uhai kutoka Kwake na kuinuka kutoka mavumbini kuwa mwanadamu aliyeumbwa, lakini kwamba pia Angeweza kuwachoma wanadamu, na kuwalaani wanadamu, na kutumia fimbo Yake kuwatawala wanadamu. Kwa hivyo, pia waliona kwamba Yehova angeweza kuyaongoza maisha ya mwanadamu duniani, na kuzungumza na kufanya kazi miongoni mwa binadamu kulingana na saa za mchana na za usiku. Alifanya kazi hiyo ili tu viumbe Wake waweze kujua kwamba mwanadamu alitoka kwa mavumbi yaliyochaguliwa na Yeye, na aidha kwamba mwanadamu alikuwa ameumbwa na Yeye. Siyo haya tu, lakini kazi Aliyoanza huko Israeli ilikusudiwa ili kwamba watu na mataifa (ambao kwa kweli hawakuwa wametengwa na Israeli, lakini badala yake walikuwa wameenea kutoka kwa Waisraeli, ilhali bado walikuwa wa ukoo wa Adamu na Hawa) waweze kupokea injili ya Yehova kutoka Israeli, ili viumbe wote walioumbwa ulimwenguni waweze kuwa na uwezo wa kumcha Yehova na kumchukulia kuwa mkuu. Yehova asingeanza kazi Yake huko Israeli, lakini badala yake, baada ya kuwaumba wanadamu, awaache waishi maisha machangamfu duniani, basi katika hali hiyo, kwa sababu ya asili ya maumbile ya mwanadamu (asili inamaanisha kwamba mwanadamu hawezi kamwe kujua vitu ambavyo hawezi kuviona, yaani kwamba hangejua kwamba ilikuwa ni Yehova ambaye aliwaumba wanadamu, sembuse sababu yake kufanya hivyo), hangejua kamwe kwamba ilikuwa Yehova aliyewaumba wanadamu au kwamba Yeye ni Bwana wa viumbe vyote. Kama Yehova angemuumba mwanadamu na kumweka duniani, na kutoshughulika na yeye na kuondoka tu, badala ya kubaki miongoni mwa wanadamu ili kuwaongoza kwa kipindi cha muda, basi katika hali hiyo wanadamu wote wangekuwa wamerudi kuwa bure: hata mbingu na dunia na vitu vyote vingi Alivyoviumba, na wanadamu wote, vingerudi kuwa bure na aidha vingekanyagwa na Shetani. Kwa njia hii matakwa ya Yehova kwamba “Duniani, yaani, miongoni mwa viumbe Vyake, Anapaswa kuwa na mahali pa kusimama, mahali patakatifu” yangevunjwa. Na hivyo, baada ya kuwaumba wanadamu, kwamba Aliweza kubaki miongoni mwao kuwaongoza katika maisha yao, na kuzungumza nao kutoka miongoni mwao, yote haya yalikuwa ili kufanikisha hamu Yake, na kutimiza mpango Wake. Kazi Aliyoifanya huko Israeli ilikusudiwa tu kutekeleza mpango Aliokuwa ameuweka kabla ya kuumba Kwake vitu vyote, na kwa hivyo Yeye kufanya kazi kwanza miongoni mwa Waisraeli na Yeye kuumba vitu vyote hakukutofautiana, lakini yote yalikuwa kwa ajili ya usimamizi Wake, kazi Yake, na utukufu Wake, na pia ili kuimarisha maana ya Yeye kuumba wanadamu. Aliyaongoza maisha ya wanadamu duniani kwa miaka elfu mbili baada ya Nuhu, wakati ambapo Aliwafunza wanadamu kuelewa jinsi ya kumcha Yehova Bwana wa viumbe vyote, jinsi ya kuendesha maisha yao na jinsi ya kuendelea kuishi, na zaidi ya yote, jinsi ya kutenda kama shahidi wa Yehova, kumtii, na kumcha, hata kumsifu kwa muziki kama Daudi na wakuhani wake walivyofanya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi katika Enzi ya Sheria

Tanbihi:

a. Maandishi ya asili hayana maneno “kutiiwa”.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 19)

Kabla ya miaka elfu mbili ambapo Yehova alifanya kazi Yake, mwanadamu hakujua chochote, na karibu wanadamu wote walikuwa wamejipata katika upotovu, hadi, kabla ya uharibifu wa dunia na gharika, walikuwa wamefika kina cha uzinzi na upotovu ambapo mioyo yao haikuwa na Yehova, sembuse njia Yake. Hawakuelewa kamwe kazi ambayo Yehova angefanya; hawakuwa na mantiki, sembuse maarifa, na, kama mashine inayopumua, walikuwa hawamjui mwanadamu, Mungu, dunia, uhai na kadhalika kikamilifu. Duniani walishiriki katika ushawishi mwingi, kama yule nyoka, na walisema mambo mengi ambayo yalimkosea Yehova, lakini kwa sababu hawakujua Yehova hakuwaadibu au kuwafundisha nidhamu. Ni baada ya gharika tu, wakati Nuhu alikuwa na umri wa miaka 601, ndipo Yehova alijitokeza rasmi kwa Nuhu na kumwongoza yeye na familia yake, Akiongoza ndege na wanyama ambao walisalia baada ya gharika pamoja na Nuhu na ukoo wake, hadi mwisho wa Enzi ya Sheria, yote ikiwa ni miaka 2,500. Alikuwa akifanya kazi huko Israeli, yaani, alikuwa akifanya kazi kirasmi, kwa jumla ya miaka 2,000, na Alikuwa akifanya kazi huko Israeli sawia na nje ya Israeli kwa miaka 500, yote ikijumuisha miaka 2,500. Katika kipindi hiki, Aliwaagiza Waisraeli kwamba ili kumhudumia Yehova, iliwapasa kujenga hekalu, kuvaa majoho ya makuhani, na kutembea miguu mitupu kuingia hekaluni kunapopambazuka, viatu vyao visije vikachafua hilo hekalu na moto kushushwa chini kwao kutoka juu ya hekalu na kuwachoma hadi kufa. Walitekeleza wajibu wao na kutii mipango ya Yehova. Walimwomba Yehova hekaluni, na baada ya kupokea ufunuo wa Yehova, yaani, baada ya Yehova kuzungumza, waliuongoza umati na kuufunza kwamba wanapaswa kumcha Yehova—Mungu wao. Na Yehova aliwaambia kwamba ingewapasa kujenga hekalu na madhabahu, na katika wakati uliowekwa na Yehova, yaani, katika siku ya Pasaka, wangepaswa kuwatayarisha ndama na wanakondoo waliozaliwa karibuni kuwaweka juu ya madhabahu kama dhabihu kumhudumia Mungu, ili kuwazuia na kuweka uchaji kwa Yehova mioyoni mwao. Iwapo walitii sheria hii ikawa kipimo cha uaminifu wao kwa Yehova. Yehova pia aliwaagizia siku ya Sabato, siku ya saba ya uumbaji Wake. Akafanya siku baada ya Sabato kuwa siku ya kwanza, siku ya wao kumwabudu Yehova, kumtolea dhabihu, na kumtengenezea Muziki. Katika siku hii, Yehova aliwaita pamoja wakuhani wote ili kugawa dhabihu zilizokuwa juu ya madhabahu kwa ajili ya watu kula, ili wangeweza kufurahia dhabihu zilizokuwa juu ya madhabahu ya Yehova. Naye Yehova alisema kwamba walikuwa wamebarikiwa, kwamba walishiriki sehemu na Yeye, na kwamba walikuwa wateule Wake (ambalo lilikuwa agano la Yehova na Waisraeli). Hii ndiyo maana, hadi siku ya leo, watu wa Israeli bado wanasema kwamba Yehova ni Mungu wao pekee, na si Mungu wa watu wengine.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi katika Enzi ya Sheria

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 20)

Katika Enzi ya Sheria, Yehova aliweka amri nyingi za Musa kupitisha kwa Waisraeli waliomfuata kutoka Misri. Amri hizi walipewa Waisraeli na Yehova, na hazikuwa na uhusiano kwa Wamisri: zilinuiwa kuwazuia Waisraeli. Yeye alizitumia amri kuwatolea madai. Iwapo waliishika Sabato, iwapo waliwaheshimu wazazi wao, iwapo waliziabudu sanamu, na kadhalika: hizi zilikuwa kanuni ambazo kwazo walihukumiwa kuwa wenye dhambi au wenye haki. Miongoni mwao, kuna baadhi walioangamizwa kwa moto wa Yehova, baadhi waliopigwa mawe hadi kufa, na baadhi waliopokea baraka za Yehova, na haya yaliamuliwa kulingana na iwapo walizitii amri hizi au la. Wale ambao hawakuishika Sabato wangepigwa mawe hadi kufa. Wale makuhani ambao hawakuishika Sabato wangeangamizwa na moto wa Yehova. Wale ambao hawakuwaheshimu wazazi wao pia wangepigwa mawe hadi kufa. Yote haya yalikubaliwa na Yehova. Yehova alianzisha amri na sheria Zake ili, Alipokuwa akiwaongoza katika maisha yao, watu wangesikiliza na kuti neno Lake na kutoasi dhidi Yake. Alitumia sheria hizi kuidhibiti jamii ya binadamu iliyokuwa imezaliwa karibuni, ili kuweka vizuri zaidi msingi wa kazi Yake ya baadaye. Na kwa hivyo, kwa msingi wa kazi ambayo Yehova alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya sheria. Ingawa Yehova alisema matamshi mengi na kufanya kazi nyingi, Aliwaongoza watu kwa njia njema tu, akiwafunza watu hawa wasiojua jinsi ya kuwa binadamu, jinsi ya kuishi, jinsi ya kuelewa njia ya Yehova. Kwa kiwango kikubwa sana, kazi Aliyoifanya ilikuwa ili kuwasababisha watu kutii njia Yake na kufuata sheria Zake. Kazi hii ilifanywa kwa watu waliokuwa wamepotoshwa kwa kiasi kidogo; haikuenea kiasi cha kubadili tabia yao au maendeleo katika maisha. Alijishughulisha tu na kutumia sheria kuwazuia na kuwadhibiti watu. Kwa Waisraeli wa wakati huo, Yehova alikuwa Mungu katika hekalu tu, Mungu huko mbinguni. Alikuwa nguzo ya wingu, nguzo ya moto. Yote ambayo Yehova aliwataka wafanye ilikuwa ni kutii kile ambacho watu wa leo wanakijua kama sheria na amri Zake—mtu anaweza pia kusema kanuni—kwa sababu kile ambacho Yehova alifanya hakikunuiwa kuwabadilisha, ila kuwapa vitu zaidi ambavyo mwanadamu anapaswa kuwa navyo, kuwaagiza kutoka kinywani Mwake mwenyewe, kwa sababu baada ya kuumbwa, mwanadamu hakuwa na chochote alichopaswa kumiliki. Na kwa hivyo, Yehova aliwapa watu vitu ambavyo walipaswa kumiliki kwa ajili ya maisha yao duniani, Akiwafanya watu Aliokuwa ameongoza kuwashinda mababu zao, Adamu na Hawa, kwa sababu kile Yehova alichowapa kilishinda kile Alichokuwa amewapa Adamu na Hawa mwanzoni. Bila kujali, kazi ambayo Yehova alifanya huko Israeli ilikuwa tu kuwaongoza binadamu na kuwafanya binadamu wamtambue Muumba wao. Hakuwashinda wala kuwabadilisha, ila Aliwaongoza tu. Hii ndiyo kazi yote ya Yehova katika Enzi ya Sheria. Ndio usuli, masimulizi ya kweli, kiini cha kazi Yake katika nchi nzima ya Israeli, na mwanzo wa kazi Yake ya miaka elfu sita—kuendeleza udhibiti wa wanadamu kwa mkono wa Yehova. Kutokana na hili kulizaliwa kazi zaidi katika mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi katika Enzi ya Sheria

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 21)

Hapo mwanzo, kumwongoza mwanadamu wakati wa Enzi ya Sheria ya Agano la Kale ilikuwa kama kuyaongoza maisha ya mtoto. Wanadamu wa mwanzoni sana walikuwa wazaliwa wapya wa Yehova, ambao walikuwa Waisraeli. Hawakuelewa jinsi ya kumcha Mungu au kuishi duniani. Ambayo ni kusema, Yehova aliwaumba wanadamu, yaani, Yeye aliwaumba Adamu na Hawa, lakini Hakuwapa uwezo wa kuelewa jinsi ya kumcha Yehova au kufuata sheria za Yehova duniani. Bila mwongozo wa moja kwa moja wa Yehova, hakuna ambaye angeweza kulijua hili moja kwa moja, kwani mwanzoni mwanadamu hakuwa na uwezo huo wa kuelewa. Mwanadamu alijua tu kwamba Yehova alikuwa Mungu, na hakuwa na habari ya namna ya kumcha Yeye, nini cha kufanya ili kumcha Yeye, kumcha Yeye na akili gani, na nini cha kutoa katika kumcha Yeye, mwanadamu alijua tu jinsi ya kufurahia kile ambacho kingeweza kufurahiwa kati ya viumbe wa Yehova, lakini mwanadamu hakuwa na fununu ya aina gani ya maisha duniani yalifaa yale ya kiumbe cha Mungu. Bila mtu wa kuwaelekeza, bila mtu wa kuwaongoza binafsi, wanadamu kama hao hawangeweza kamwe kuishi maisha ya kufaa wanadamu, na wangeweza tu kutekwa na Shetani kwa siri. Yehova aliwaumba wanadamu, ambayo ni kusema kwamba Yeye aliumba babu za wanadamu: Hawa na Adamu. Lakini hakuwapa akili zaidi au hekima. Ingawa walikuwa tayari wanaishi duniani, hawakuelewa takriban chochote. Na kwa hiyo, kazi ya Yehova ya kuwaumba wanadamu ilikuwa imefanyika nusu tu, haikuwa imekaribia kukamilika. Alikuwa ameumba tu mfano wa mwanadamu kutoka kwa udongo na kumpa pumzi Yake, lakini Hakuwa amempa mwanadamu radhi ya kutosha kumcha Yeye. Hapo mwanzo, mwanadamu hakuwa na akili ya kumcha Yeye, au kumwogopa Yeye. Mwanadamu alijua tu jinsi ya kuyasikiliza maneno Yake lakini hakujua ujuzi wa msingi wa maisha duniani na sheria za kawaida za maisha. Na kwa hiyo, ingawa Yehova aliumba mwanamume na mwanamke na kumaliza siku saba za shughuli, Hakukamilisha uumbaji wa mwanadamu hata kidogo, kwa maana mwanadamu alikuwa ganda tu, na hakuwa na uhalisi wa kuwa mwanadamu. Mwanadamu alijua tu kwamba ni Yehova aliyeumba wanadamu, lakini mwanadamu hakuwa na fununu ya jinsi ya kutii maneno na sheria za Yehova. Na kwa hiyo, baada ya kuumbwa kwa wanadamu, kazi ya Yehova ilikuwa mbali sana kumalizika. Pia alitakiwa kuwaongoza wanadamu kabisa mbele Yake ili wanadamu waweze kuishi pamoja duniani na kumcha Yeye, na ili wanadamu waweze kwa mwongozo Wake kuingia katika njia sahihi ya maisha ya kawaida ya binadamu duniani baada ya kuongozwa na Yeye. Kwa njia hii tu ndiyo kazi ambayo ilikuwa imeendeshwa kwa kiasi kikubwa kupitia jina la Yehova ilimalizika kabisa; yaani, kwa njia hii tu ndiyo kazi ya Yehova ya kuumba ulimwengu ilihitimishwa kabisa. Na kwa hiyo, kwa vile Alimuumba mwanadamu, Alipaswa kuongoza maisha ya wanadamu duniani kwa miaka elfu kadhaa, ili wanadamu waweze kutii amri na sheria Zake, na kushiriki katika shughuli zote za maisha ya kufaa ya binadamu duniani. Wakati huo tu ndio kazi ya Yehova ilikamilika kabisa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 22)

Kazi ambayo Yesu alifanyika ililingana na mahitaji ya mwanadamu katika enzi hiyo. Kazi Yake ilikuwa ni kuwakomboa wanadamu, kuwasamehe dhambi zao, na kwa hivyo tabia Yake yote ilikuwa ya unyenyekevu, uvumilivu, upendo, ucha Mungu, ustahamilivu, huruma na wema. Aliwabariki wanadamu kwa wingi na kuwaletea neema nyingi, na mambo yote ambayo wangeweza kufurahia, Aliwapa kwa ajili ya furaha yao: amani na furaha, uvumilivu Wake na upendo, huruma Yake na wema. Katika siku hizo, chote alichokutana nacho mwanadamu kilikuwa wingi wa vitu vya kufurahia tu: Moyo wake ulikuwa na amani na uhakikisho, roho yake ilifarijika, na alikuwa anaruzukiwa na Mwokozi Yesu. Sababu iliyomfanya mwanadamu aweze kufaidi mambo haya ni matokeo ya enzi alimoishi. Katika Enzi ya Neema mwanadamu alikuwa amepotoshwa tayari na Shetani, na hivyo kazi ya ukombozi wa wanadamu wote ulihitaji neema nyingi, ustahimili na uvumilivu usio na mwisho, na hata zaidi, sadaka ya kutosha kulipia dhambi za wanadamu, ili kufikia athari yake. Kile wanadamu walichoona katika Enzi ya Neema kilikuwa tu sadaka Yangu ya kulipia dhambi za binadamu, yaani, Yesu. Yote waliyojua ni kwamba Mungu angeweza kuwa mwenye huruma na uvumilivu, na yote waliyoona ni huruma ya Yesu na wema Wake. Hii yote ilikuwa ni kwa sababu wao walizaliwa katika Enzi ya Neema. Na hivyo, kabla ya kuweza kukombolewa, walilazimika kufurahia neema za aina nyingi ambazo Yesu aliwapa; hili pekee ndilo lilikuwa la manufaa kwao. Kwa njia hii, wangeweza kusamehewa dhambi zao kupitia kufurahia kwao neema, na pia wangeweza kuwa na nafasi ya kukombolewa kupitia kufurahia ustahimili wa Yesu na uvumilivu. Ni kwa njia ya ustahimili wa Yesu na uvumilivu pekee ndio walipata haki ya wa kupokea msamaha na kufurahia neema nyingi kutoka kwa Yesu—kama vile Yesu alivyosema: Sijakuja kuwakomboa wenye haki, ila wenye dhambi, kukubali dhambi zao zisamehewe. Kama Yesu angepata mwili wa tabia ya hukumu, laana, na kutovumilia makosa ya mwanadamu, basi mwanadamu kamwe hangeweza kupata nafasi ya kukombolewa, na daima yeye angebaki mwenye dhambi. Hali ingekuwa hivi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Sheria ingeendelea kwa miaka elfu sita. Dhambi za mwanadamu zingeongezeka zaidi na kuwa mbaya zaidi tu, na uumbaji wa binadamu ungekuwa wa bure. Wanadamu wangeweza tu kumtumikia Yehova chini ya sheria, bali dhambi zao zingezidi za wanadamu wa kwanza kuumbwa. Jinsi Yesu alivyowapenda wanadamu zaidi, Akisamehe dhambi zao na kuwapa huruma na wema wa kutosha, ndivyo wanadamu walizidi kuwa na uwezo wa kuokolewa, wa kuitwa wanakondoo waliopotea ambao Yesu Aliwanunua tena kwa gharama kubwa. Shetani hakuweza kuingilia katika kazi hii, kwa sababu Yesu Aliwatunza wafuasi Wake kama mama mwenye upendo anavyotunza mtoto mchanga aliye kifuani pake. Yeye hakuwa na hasira nao au kuwadharau, bali Alikuwa Amejaa faraja; Yeye kamwe hakuwa na ghadhabu miongoni mwao, lakini alistahimili dhambi zao na Akapuuza upumbavu wao na kutofahamu, hata kusema, “Uwasamehe wengine mara sabini mara saba.” Kwa hiyo moyo Wake ulirekebisha mioyo ya wengine. Ilikuwa ni kwa njia hii ndiyo watu walipokea msamaha wa dhambi kupitia uvumilivu Wake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 23)

Ingawa Yesu katika mwili Wake hakuwa na hisia kabisa, Yeye daima Aliwafariji wanafunzi Wake, Aliwapa mahitaji yao, Akawasaidia, na Akawaruzuku. Bila kujali kiwango cha kazi Alichofanya au kiasi gani cha mateso Alivumilia, Yeye kamwe hakuwa na matarajio ya kupita kiasi kwa mwanadamu, lakini kila mara Alikuwa mwenye subira na kuvumilia dhambi zao, kiasi kwamba katika Enzi ya Neema kwa upendo watu walimwita “Mwokozi Yesu anayependeka.” Kwa watu wa wakati huo—kwa watu wote—kile Yesu Alikuwa nacho na kile Alichokuwa, kilikuwa huruma na wema. Yeye kamwe hakukumbuka dhambi za, na hakuwatendea kulingana na dhambi zao. Kwa sababu hiyo ilikuwa enzi tofauti, mara nyingi Alitoa chakula na vinywaji kwa watu ili waweze kula hadi washibe. Yeye Aliwatendea wafuasi Wake wote kwa ukarimu, akaponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kufufua wafu. Ili kwamba watu waweze kumwamini na kuona kwamba yote Aliyofanya yalifanyika kwa bidii na kwa dhati, Yeye Alifika kiwango cha kufufua maiti iliyooza, kuwaonyesha kwamba mikononi Mwake hata wafu wanaweza kuwa hai tena. Kwa njia hii Alivumilia kwa kimya na kufanya kazi Yake ya ukombozi kati yao. Hata kabla Asulubiwe, Yesu Alikuwa tayari Amebeba dhambi za binadamu na kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya wanadamu. Hata kabla Asulubiwe, Alikuwa tayari Amefungua njia ya msalaba ili kuwakomboa wanadamu. Mwishowe Aligongwa misumari msalabani, Alijitoa sadaka Yeye Mwenyewe kwa ajili ya msalaba, na Alitoa huruma Yake yote, wema Wake, na utakatifu kwa wanadamu. Kwa wanadamu daima alikuwa mvumilivu, kamwe Hakutafuta kulipiza kisasi, lakini Aliwasamehe dhambi zao, Akiwasihi watubu, na kuwafundisha kuwa na subira, uvumilivu na upendo, kufuata nyayo Zake na kujitoa wenyewe kwa ajili ya msalaba. Upendo Wake kwa ndugu ulizidi upendo Wake kwa Maria. Kanuni ya kazi Aliyofanya ilikuwa kuwaponya watu na kutoa mapepo, yote kwa ajili ya ukombozi Wake. Haijalishi Alikoenda, Yeye Aliwatendea wote waliomfuata kwa neema. Aliwafanya maskini kuwa tajiri, viwete watembee, vipofu waone na viziwi wasikie; Yeye hata Aliwaalika watu wa hadhi ya chini kabisa, maskini zaidi, wenye dhambi, kula pamoja naye, Akikosa kuwaepuka kamwe ila daima Alikuwa na subira, hata kusema: Wakati mchungaji anampoteza kondoo mmoja kati ya mia, yeye ataondoka na kuwaacha nyuma wale tisini na tisa ili amtafute kondoo mmoja aliyepotea, na anapompata yeye atafurahia sana. Yeye Aliwapenda wafuasi Wake kama kondoo anavyopenda wanakondoo wake. Ingawa walikuwa wajinga na wasio na ufahamu, na walikuwa wenye dhambi katika macho Yake, na zaidi walikuwa washirika wa chini zaidi katika jamii, Aliona hawa wenye dhambi—waliodharauliwa na wengine—kama vipenzi Vyake. Kwa kuwa Aliwapendelea, Alitoa uhai Wake kwa ajili yao, kama mwana kondoo alitolewa madhabahuni. Alitembea kati yao kama mtumishi wao, Akiwaruhusu kumtumia na kumchinja, Alijinyenyekeza kwao bila masharti. Kwa wafuasi Wake Alikuwa Mwokozi Yesu aliyependeka, lakini kwa Mafarisayo, ambao waliwahubiria watu kutoka viweko virefu vya mnara, Hakuonyesha huruma na wema, bali chuki na maudhi. Hakufanya kazi nyingi miongoni mwa Mafarisayo, Akiwahubiria na kuwakemea mara chache tu; Yeye hakutembea miongoni mwao akifanya kazi ya ukombozi, au kufanya ishara na maajabu. Alitoa huruma Yake na wema Wake wote kwa wafuasi Wake, akivumilia kwa ajili ya hawa wenye dhambi mpaka mwisho kabisa, wakati Alipigwa misumari msalabani na akastahimili kila udhalilishaji mpaka Alivyowakomboa wanadamu wote kikamilifu. Hii ndiyo ilikuwa kazi Yake yote.

Bila ukombozi wa Yesu, wanadamu wangeishi milele katika dhambi, na kuwa watoto wa dhambi, kizazi cha mapepo. Kama ingeendelea hivyo, dunia yote ingekuwa mahali pa kulala pa Shetani, maskani yake. Lakini kazi ya ukombozi ilihitaji kuonyesha huruma na wema kwa wanadamu; kupitia kwa njia hiyo tu ndio wanadamu wangeweza kupokea msamaha na mwishowe kupata haki ya kukamilishwa na kumilikiwa kikamilifu. Bila hatua hii ya kazi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeweza kuendelea mbele. Kama Yesu hangesulubiwa, kama Yeye Angewaponya tu watu na kufukuza mapepo, basi watu hawangesamehewa dhambi zao kikamilifu. Katika miaka mitatu na nusu ambayo Yesu Alitumia kufanya kazi Yake hapa duniani alikamilisha tu nusu ya kazi Yake ya ukombozi; kisha, kwa kupigiliwa misumari msalabani na kuwa mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kukabidhiwa kwa yule mwovu, Yeye Alikamilisha kazi ya kusulubiwa na Akaendesha majaaliwa ya wanadamu. Baada ya Yeye kukabidhiwa mikononi mwa Shetani tu, ndipo alipowakomboa wanadamu. Kwa miaka thelathini na mitatu na nusu Aliteseka duniani, Akidhihakiwa, kukashifiwa, na kuachwa, kiasi cha Yeye kukosa mahali pa kulaza kichwa chake, mahali pa kupumzika; kisha Akasulubiwa, huku nafsi Yake yote—mwili mtakatifu na usio na hatia—kupigiliwa misumari msalabani. Alivumilia kila namna ya mateso yaliyoko. Wale waliokuwa madarakani wakamdhihaki na kumcharaza mijeledi, na maaskari hata wakamtemea mate usoni; ilhali Alibaki kimya na kuvumilia mpaka mwisho, Akinyenyekea bila masharti mpaka wakati wa kifo, ambapo Yeye Alikomboa wanadamu wote. Hapo tu ndipo Aliruhusiwa kupumzika. Kazi ambayo Yesu alifanya inawakilisha tu Enzi ya Neema; haiwakilishi Enzi ya Sheria wala si mbadala wa kazi ya siku za mwisho. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, enzi ya pili ambayo wanadamu wamepitia—Enzi ya Ukombozi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 24)

Baada ya kazi ya Yehova, Yesu Alipata mwili ili Afanye kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Kazi Yake haikutekelezwa kivyake, ila ilijengwa juu ya misingi ya kazi ya Yehova. Ilikuwa kazi ya enzi mpya baada ya Mungu kukamilisha Enzi ya Sheria. Vivyo hivyo, baada ya kazi ya Yesu kukamilika, Mungu bado Aliendeleza kazi Yake ya enzi iliyofuata, kwa sababu usimamizi wote wa Mungu huendelea mbele siku zote. Enzi nzee ikipita, itabadilishwa na enzi mpya, na mara tu kazi nzee imekamilika, kazi mpya itaendeleza usimamizi wa Mungu. Kupata mwili huku ni kupata mwili kwa Mungu mara ya pili kufuatia kukamilika kwa kazi ya Yesu. Bila shaka, kupata mwili huku hakufanyiki kivyake, bali ni hatua ya tatu ya kazi baada ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Kila hatua mpya ya kazi ya Mungu kila mara huleta mwanzo mpya na enzi mpya. Vivyo hivyo kuna mabadiliko yanayokubaliana katika tabia ya Mungu, katika njia Yake ya kufanya kazi, katika sehemu Yake ya kufanya kazi, na katika jina Lake. Ndiyo maana basi ni vigumu kwa mwanadamu kukubali kazi ya Mungu katika enzi mpya. Lakini licha ya jinsi anapingwa na mwanadamu, Mungu huendelea kufanya kazi Yake, na daima Yeye huwa Akiongoza wanadamu wote kuendelea mbele. Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alileta Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 25)

Watu wakibaki katika Enzi ya Neema, basi hawatawahi kujiweka huru kutokana na tabia zao za upotovu, sembuse kujua tabia ya asili ya Mungu. Wanadamu wakiishi daima katika wingi wa neema ila hawana njia ya maisha inayowaruhusu kumjua Mungu na kumridhisha Mungu, basi kamwe hawataweza kumpata Mungu kwa kweli hata ingawa wanaamini Kwake. Hiyo ni aina ya imani ya kutia huruma. Wakati umemaliza kusoma kitabu hiki, wakati umepitia matukio yote ya kazi ya Mungu mwenye mwili katika Enzi ya Ufalme, utahisi kwamba matumaini ya miaka mingi hatimaye yametimika. Utahisi kwamba ni sasa tu ndipo umemwona Mungu uso kwa uso; ni sasa tu ndipo umeutazama uso wa Mungu, umesikia matamshi ya Mungu Mwenyewe, umeifahamu hekima ya kazi ya Mungu, na kuhisi kwa kweli jinsi Mungu ni wa kweli na mwenye nguvu. Utafahamu kuwa umepata vitu vingi ambavyo watu wa nyakati zilizopita hawajawahi kuviona wala kuwa navyo. Wakati huu, utajua kwa uhakika ni nini hasa kuamini katika Mungu, na ni nini kupendeza nafsi ya Mungu. Bila shaka, ukikwamilia maoni ya kitambo, na ukatae au ukane ukweli wa kupata mwili kwa Mungu mara ya pili, basi utabaki mkono mtupu na hutapata chochote, na mwishowe utakuwa na hatia ya kumpinga Mungu. Wale wanaotii ukweli na kunyenyekea kwa kazi ya Mungu watakuja chini ya jina la Mungu mwenye mwili wa pili—Mwenyezi. Wataweza kukubali uelekezi binafsi wa Mungu, na watapata ukweli zaidi na wa juu zaidi na watapokea maisha ya kweli ya mwanadamu. Wataona maono ambayo watu wa zamani hawajawahi kuona kamwe: “Na nikapinduka ili kuiona sauti hiyo iliyonizungumzia. Na baada ya kupinduka, nikatazama vinara saba vya taa vilivyokuwa vya dhahabu; Na hapo katikati ya hivyo vinara saba vya taa nilimwona mtu aliyefanana na Mwana wa Adamu, aliyekuwa amevalia nguo iliyofika katika miguu yake, na kifuani alikuwa amefungwa kanda ya dhahabu. Kichwa chake na nywele zilikuwa nyeupe mithili ya sufu, nyeupe mithili ya theluji; na macho yake yalikuwa mithili ya ulimi wa moto; Na miguu yake mithili ya shaba safi, kama kwamba ilikuwa imechomwa ndani ya tanuru; na sauti yake ilikuwa mithili ya sauti ya maji mengi. Na katika mkono wake wa kulia kulikuwa na nyota saba: na alitoa kinywani mwake upanga mkali wenye sehemu mbili za makali: nao uso wake ulikuwa mithili ya jua liangazavyo kupitia nguvu zake yeye” (Ufunuo 1:12-16). Maono haya ni maonyesho ya tabia kamilifu ya Mungu, na maonyesho ya aina hii ya tabia Yake nzima pia ndiyo maonyesho ya kazi ya Mungu Anapopata mwili mara hii. Katika mibubujiko ya kuadibu na hukumu, Mwana wa Adamu Anaonyesha tabia Yake ya asili kupitia kuzungumza kwa maneno, Akiwaruhusu wale wote wanaokubali kuadibu Kwake na hukumu kuuona uso wa kweli wa Mwana wa Adamu, uso ulio mfano wa kuaminika wa Mwana wa Adamu Alivyooneka na Yohana. (Bila shaka, yote haya hayatawaonekania wote wasioikubali kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.) Uso wa kweli wa Mungu hauwezi kuelezwa kikamilifu na maneno ya mwanadamu, na hivyo Mungu Hutumia maonyesho ya tabia Yake asili kuuonyesha uso Wake wa kweli kwa mwanadamu. Ambayo ni kusema wote ambao wamepitia tabia asili ya Mwana wa Adamu wameuona uso wa kweli wa Mwana wa Adamu, kwa kuwa Mungu ni mkuu zaidi na Hawezi kuelezwa kikamilifu na maneno ya mwanadamu. Mara tu mwanadamu amepitia kila hatua ya kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme, basi atapata kujua maana kamili ya maneno ya Yohana alipozungumza kuhusu Mwana wa Adamu kati ya vinara vya taa: “Kichwa chake na nywele zilikuwa nyeupe mithili ya sufu, nyeupe mithili ya theluji; na macho yake yalikuwa mithili ya ulimi wa moto; Na miguu yake mithili ya shaba safi, kama kwamba ilikuwa imechomwa ndani ya tanuru; na sauti yake ilikuwa mithili ya sauti ya maji mengi. Na katika mkono wake wa kulia kulikuwa na nyota saba: na alitoa kinywani mwake upanga mkali wenye sehemu mbili za makali: nao uso wake ulikuwa mithili ya jua liangazavyo kupitia nguvu zake yeye.” Wakati huo, utajua bila shaka yoyote kwamba mwili huu wa kawaida uliozungumza maneno mengi ni kwa hakika Mungu mwenye mwili mara ya pili. Na utahisi ni jinsi gani kwa kweli umebarikiwa, na kujiona mwenyewe kama mwenye bahati kubwa. Je, ungekuwa huna radhi kuikubali baraka hii?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 26)

Kazi katika siku za mwisho ni kunena maneno. Mabadiliko makuu yanaweza kusababishwa kwa watu kupitia katika maneno hayo. Mabadiliko yanayosababishwa sasa kwa watu hawa kwa sababu ya kukubali maneno haya ni makubwa kuliko yale ya watu katika Enzi ya Neema kwa kukubali ishara na maajabu hayo. Kwani, katika Enzi ya Neema, mapepo yaliondoka kutoka kwa mwanadamu kwa kuwekewa mikono na maombi, lakini tabia potovu ndani ya mwanadamu ilibaki. Mwanadamu aliponywa magonjwa na kusamehewa dhambi zake, lakini kazi ya jinsi tabia potovu za kishetani katika mwanadamu haikutupiliwa mbali na bado iko ndani yake. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini hili halikumaanisha kuwa mwanadamu hakuwa na dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia yake potovu ya zamani ya kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivyo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili. Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwema Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na kuonekana kwa kiungu; kama mtu angeishi katika huo msingi, angechukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, ambayo ilimaanisha kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia yoyote ya kubadili tabia yao; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii ni ya kumfanya mwanadamu awea safi kupitia neno, na hivyo kumpa njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendelea na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 27)

Katika kazi ya siku za mwisho, neno ni kubwa zaidi ya udhihirisho wa ishara na maajabu, na mamlaka ya neno yanashinda yale ya ishara na maajabu. Neno linaweka wazi tabia zote potovu katika moyo wa mwanadamu. Huwezi kutambua binafsi wewe mwenyewe. Yatakapofunuliwa kwako kupitia kwa neno, utakuja kujua mwenyewe; hutaweza kuyakataa, na utashawishika kikamilifu. Je haya si mamlaka ya neno? Haya ndiyo matokeo yanayopatikana kwa kazi ya wakati huu ya neno. Kwa hivyo, mwanadamu hawezi kuokolewa kikamilifu kutoka kwa dhambi zake kwa kuponya magonjwa na kukemea mapepo na hawezi kufanywa mkamilifu kabisa kwa udhihirisho wa ishara na maajabu. Mamlaka ya kuponya na kukemea mapepo yanapatia mwanadamu neema tu, lakini mwili wa mwanadamu bado ni wa Shetani na tabia potovu za kishetani zitabaki ndani ya mwanadamu. Kwa maneno mengine, yale ambayo hayajatakaswa bado inahusu dhambi na uchafu. Ni baada tu ya mwanadamu kufanywa safi kupitia kwa maneno ndipo mwanadamu atakapopatwa na Mungu na kutakaswa. Wakati mapepo yalikemewa kutoka kwa mwanadamu na alikombolewa, hii ilimaanisha tu kwamba alipokonywa kutoka kwa mikono ya Shetani na kurudishwa kwa Mungu. Hata hivyo, hajafanywa msafi ama kubadilishwa na Mungu, anabaki kama mpotovu. Ndani ya mwanadamu bado kuna uchafu, pingamizi na uasi; mwanadamu amerudi tu kwa Mungu kupitia kwa ukombozi Wake, lakini mwanadamu hana maarifa hata kidogo kumhusu Mungu na bado anaweza kumpinga na kumsaliti. Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa. Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. Kwa mfano, wakati ambapo watu walijua kwamba walitoka kwa Moabu, walitoa maneno ya malalamiko, hawakutafuta tena uzima, na wakawa hasi kabisa. Je, hili halionyeshi kwamba bado hawawezi kutii kwa ukamilifu kutawaliwa na Mungu? Je, hii siyo tabia ya kishetani ya upotovu kabisa? Ulipokuwa hupitii kuadibu, mikono yako iliinuliwa juu zaidi ya wengine wote, hata ile ya Yesu. Na ulilia kwa sauti kubwa: “Kuwa mwana mpendwa wa Mungu! Kuwa mwandani wa Mungu! Ni heri tufe kuliko kumtii Shetani! Muasi Shetani wa zamani! Liasi joka kuu jekundu! Acha joka kuu jekundu lianguke kabisa kutoka mamlakani! Acha Mungu atufanye kamili!” Vilio vyako vilikuwa vikubwa zaidi ya wengine. Lakini kisha ukaja wakati wa kuadibu na, mara tena, tabia ya upotovu ya watu ilifichuliwa. Kisha, vilio vyao vikakoma, na hawakuwa tena na azimio. Huu ni upotovu wa mwanadamu; unaingia ndani zaidi kuliko dhambi, ulipandwa na Shetani na umekita mizizi ndani zaidi ya mwanadamu. Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea. Mwanadamu alipiga kelele hivyo wakati uliopita kwa sababu mwanadamu hakuwa na ufahamu wa tabia yake potovu ya asili. Huo ndio uchafu ulio ndani ya mwanadamu. Kotekote katika kipindi kirefu hivyo cha hukumu na kuadibu, mwanadamu aliishi katika mazingira ya mvutano. Je, haya yote hayakutimizwa kupitia kwa neno? Wewe pia hukulia kwa sauti ya juu kabla ya majaribio ya watendaji huduma? Ingia katika ufalme! Wale wote ambao wanalikubali jina hili wataingia katika ufalme! Wote watashiriki Mungu! Wakati ambapo majaribio ya watendaji huduma yalikuja, hukulia tena. Mwanzoni, wote walilia, “Mungu! Popote Uniwekapo, nitatii kuongozwa na Wewe.” Baada ya kusoma maneno ya Mungu, “Nani atakuwa Paulo Wangu?” watu walisema, “Niko radhi!” Kisha wakayaona maneno, “Na kuhusu imani ya Ayubu?” Kwa hiyo akasema, “Niko radhi kuichukua imani ya Ayubu. Mungu, tafadhali nijaribu!” Majaribio ya watendaji huduma yalipokuja, walizirai mara moja na kusimama tena kwa nadra sana. Baada ya hilo, uchafu ndani ya moyo wa wao ulipungua polepole. Je, hili halikutimizwa kupitia kwa neno? Kwa hiyo, kile ambacho mmepitia wakati wa sasa ni matokeo ambayo hutimizwa kupitia kwa neno, hata makuu zaidi ya yale ambayo hutimizwa kupitia kwa Yesu kufanya ishara na maajabu. Utukufu wa Mungu na mamlaka ya Mungu Mwenyewe ambayo ninyi huona hayaonekani tu kupitia kwa usulubishaji, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo, lakini zaidi kupitia kwa hukumu ya neno Lake. Hili hukuonyesha wewe kwamba sio tu ufanyaji wa ishara, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo ndiyo mamlaka na nguvu za Mungu, bali kwamba hukumu ya neno la Mungu inaweza kuwakilisha vyema zaidi mamlaka ya Mungu na kufichua uweza Wake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 28)

Katika Enzi ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kuikaribisha enzi mpya, kubadilisha njia ambayo kwayo Yeye hufanya kazi, na kufanya kazi ya enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili Anene kutoka katika mitazamo tofauti, ili mwanadamu aweze kumwona Mungu kweli, ambaye ni Neno kuonekana katika mwili, na angeweza kuona hekima na ajabu Yake. Kazi kama hiyo inafanywa ili kufikia malengo ya kumshinda mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu, na kumwondoa mwanadamu vyema zaidi, ambayo ndiyo maana ya kweli ya matumizi ya maneno kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia katika maneno haya, watu huja kuijua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia katika. Kupitia katika maneno, kazi ambayo Mungu anataka kufanya katika Enzi ya Neno inafanikiwa kwa ukamilifu. Kupitia katika maneno haya, watu wanafunuliwa, kuondolewa, na kujaribiwa. Watu wameyaona maneno ya Mungu, kuyasikia maneno haya, na kutambua uwepo wa maneno haya. Kama matokeo, wameamini katika uwepo wa Mungu, katika kudura na hekima ya Mungu, na pia katika upendo wa Mungu kwa mwanadamu na tamanio Lake la kumwokoa mwanadamu. Neno "maneno" linaweza kuwa rahisi na la kawaida, lakini maneno yanayonenwa kutoka katika kinywa cha Mungu mwenye mwili yanautikisa ulimwengu, kuibadilisha mioyo ya watu, kubadilisha fikira zao na tabia zao za zamani, na kubadilisha jinsi ambavyo ulimwengu wote ulikuwa ukionekana. Katika enzi zote, ni Mungu wa leo tu ndiye Aliyefanya kazi kwa njia hii, na ni Yeye Anayezungumza kwa namna hii na kuja kumwokoa mwanadamu hivi. Kuanzia wakati huu na kuendelea, mwanadamu anaishi chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, akichungwa na kuruzukiwa na maneno Yake. Watu wanaishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, kati ya laana na baraka za maneno ya Mungu, na kuna hata watu wengi zaidi ambao wamekuja kuishi chini ya hukumu na kuadibu kwa maneno Yake. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa sababu ya wokovu wa mwanadamu, kwa sababu ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa sababu ya kubadilisha kuonekana kwa asili kwa ulimwengu wa uumbaji wa zamani. Mungu aliuumba ulimwengu kwa kutumia maneno, Anawaongoza watu ulimwenguni kote kutumia maneno, na Anawashinda na kuwaokoa kutumia maneno. Hatimaye, Atatumia maneno kuutamatisha ulimwengu mzima wa zamani, hivyo kuukamilisha mpango Wake mzima wa usimamizi. Katika Enzi nzima ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kufanya kazi Yake, na kufikia matokeo ya kazi Yake. Hatendi maajabu au kufanya miujiza, lakini hufanya kazi Yake kupitia katika maneno tu. Kwa sababu ya maneno haya, mwanadamu hulishwa na kuruzukiwa, na hupata maarifa na uzoefu wa kweli. Katika Enzi ya Neno, mwanadamu amebarikiwa kwa njia ya pekee. Hapitii uchungu wa mwili na hufurahia tu ruzuku nyingi ya maneno ya Mungu; bila kuhitaji kwenda kutafuta bila kufikiri au kusafiri mbele bila kufikiri, kutoka katikati ya utulivu wake, huiona sura ya Mungu, humsikia Akinena kwa kinywa Chake mwenyewe, hupokea kile ambacho Yeye hutoa, na humtazama Akifanya kazi Yake binafsi. Hivi ni vitu ambavyo watu wa enzi zilizopita hawakuweza kufurahia, na ni baraka ambazo hawangeweza kupokea kamwe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 29)

Wanadamu kwa ajili ya kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumcha kabisa. Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote. Hili ndilo linapaswa kufanywa katika hatua hii ya kazi. Wanadamu watashindwa vipi hasa? Watapata kushindwa kwa kutumia hii kazi ya maneno kumshawishi mwanadamu kwa dhati; kwa kutumia toba, hukumu, kuadibu, na laana isiyo na huruma dhibiti kabisa; na kwa kuweka wazi uasi wa mwanadamu na kwa kuhukumu upinzani wake ili ajue udhalimu wa mwanadamu na uchafu wake, mambo ambayo yatatumiwa kuangazia tabia ya haki ya Mungu. Kwa kiwango kikubwa, ni matumizi ya maneno haya yatakayomshinda mwanadamu na kumshawishi kabisa. Maneno ndiyo njia ya kuwashinda wanadamu na wote wanaokubali ushindi lazima wakubali mapigo na hukumu ya maneno. Mchakato wa sasa wa kunena ni mchakato wa kushinda. Ni kwa njia gani watu wanapaswa hasa kushirikiana? Ni kwa kula na kunywa haya maneno ipasavyo na kuyafahamu. Watu hawawezi kujipatia ushindi wao wenyewe. Ni lazima, kwa kula na kunywa haya matamshi, upate kufahamu uovu na uchafu wako, uasi na udhalimu wako, na uanguke chini mbele ya Mungu. Ikiwa waweza kufahamu mapenzi ya Mungu kisha uyatie katika vitendo, na zaidi, uwe na maono, na ikiwa waweza kuyatii maneno haya kabisa na usitende kulingana na mapenzi yako, basi utakuwa umeshindwa. Na itakuwa ni haya maneno yamekuwezesha kushindwa. Ni kwa nini wanadamu walipoteza ushuhuda? Ni kwa sababu hakuna aliye na imani kwa Mungu au anamshikilia Mungu rohoni mwake. Kuwashinda wanadamu kunamaanisha watu wairudie hii imani. Watu daima wanauegemea ulimwengu, wakiwa na matumaini mengi sana, wakitaka kujua mengi sana kwa ajili ya maisha yao ya usoni, na wakiwa na mahitaji mengi ya kupita kiasi. Wanaifikiria na kuipangia miili yao kila mara wala hawatamani kutafuta njia ya kumwamini Mungu. Nyoyo zao zimetekwa na Shetani, wameacha kumheshimu Mungu, na wanatoa mioyo yao kwa Shetani. Ila mwanadamu aliumbwa na Mungu. Hivyo, mwanadamu amepoteza ushuhuda, kumaanisha amepoteza utukufu wa Mungu. Kusudi la kumshinda mwanadamu ni kuurejesha utukufu wa mwanadamu wa kumheshimu Mungu. Inaweza kusemwa hivi: Kuna watu wengi wasiofuatilia uzima; hata kama kuna wengine, idadi hiyo inaweza kuhesabiwa kwa vidole vya mtu. Watu wanahangaishwa sana kuhusu siku zao za baadaye na hawatilii maanani uzima kwa vyovyote vile. Watu wengine huasi dhidi ya Mungu na kumpinga, humhukumu bila Yeye kufahamu na hawatendi ukweli. Siwajali watu hawa kwa sasa, na Najizuia kushughulikia tabaka hili la wana wa uasi kwa sasa. Katika siku za usoni utaishi gizani, ukilia na kusaga meno yako. Wewe huhisi thamani ya nuru unapoishi ndani yake, lakini utatambua thamani yake mara tu unapoishi katika usiku wa giza. Utasikitika wakati huo. Unahisi sawa sasa, lakini itafika siku ambayo utasikitika. Siku hiyo itakapofika na giza lishuke na nuru isiweko tena, majuto yako yatakuwa yamechelewa. Ni kwa sababu bado huelewi kazi ya sasa ndio unakosa kutunza wakati wako sasa. Mara tu kazi ya ulimwengu mzima ianzapo, kumaanisha wakati ambapo kila kitu Nisemacho leo kimetimia, watu wengi watakuwa wakishikilia vichwa vyao kwa kilio cha uchungu. Je, huko sio kuingia katika giza na kulia na kusaga meno? Watu wote ambao hufuatilia uzima kweli na wamefanywa kuwa kamili watatumiwa, huku wana wote wa uasi ambao hawafai kutumiwa wataingia gizani, bila kupokea kazi yoyote ya Roho Mtakatifu kwa vyovyote vile na kubaki wasioweza kufahamu chochote. Hivyo wataingia katika adhabu kuomboleza na kutokwa na machozi. Kama umejiandaa vyema katika awamu hii ya kazi na maisha yako yamekomaa, basi wewe ni mtu unayefaa kutumiwa. Kama umejiandaa vibaya, basi hata kama umejitayarisha kwa awamu inayofuata ya kazi utakuwa hufai. Wakati huo, hata kama utataka kujiandaa mwenyewe, nafasi itakuwa imepita. Mungu atakuwa ameondoka; utaenda wapi basi kutafuta aina ya nafasi iliyo mbele yako sasa, na utaenda wapi basi kupokea zoezi linalotolewa na Mungu binafsi? Wakati huo, haitakuwa Mungu akinena binafsi au akitoa sauti Yake. Utaweza tu kusoma kinachosemwa leo; utawezaje kuelewa kwa urahisi? Ni vipi ambavyo maisha ya baadaye yataweza kulingana na ya leo? Wakati huo, kulia na kusaga meno kwako hakutakuwa kupitia kifo kilicho hai? Baraka inatolewa kwako sasa lakini hujui namna ya kuifurahia; unaishi katika baraka, lakini hutambui hilo. Hili linaonyesha kwamba umeandikiwa mateso! Wakati huu watu wengine hupinga, wengine huasi, wengine hufanya hili au lile. Mimi hukupuuza tu; usifikiri kwamba Sizifahamu shughuli hizo zenu. Je, Sifahamu kiini chenu? Mbona muendelee kwenda kinyume changu? Huamini katika Mungu ili ufuatilie uzima na baraka kwa ajili yako mwenyewe? Je, si kwa ajili yako mwenyewe ndio una imani? Sasa hivi Nafanya tu kazi ya kushinda na maneno Yangu. Mara tu kazi hii ya kushinda ikihitimishwa, mwisho wako utakuwa dhahiri. Je, Nahitaji kujieleza wazi zaidi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 30)

Kazi ya sasa ya kushinda ni kazi inayokusudiwa kuweka wazi hatima ya mwanadamu itakuwaje. Ni kwa nini Ninasema kuwa kuadibu na hukumu ni hukumu mbele ya kiti cha enzi kikubwa cheupe cha siku za mwisho? Hulioni hili? Ni kwa nini kazi ya kushinda ni hatua ya mwisho? Je, si kudhihirisha kwa usahihi hatima ya kila tabaka la wanadamu? Si kumruhusu kila mtu, katika harakati ya kazi ya kushinda ya kuadibu na hukumu, kuonyesha tabia zake halisi na kisha kuwekwa katika aina yake baadaye? Badala ya kusema kuwa huku ni kuwashinda wanadamu, inaweza bora kusema kuwa huku ni kuonyesha hatima ya kila aina ya mwanadamu. Yaani, huku ni kuhukumu dhambi zao halafu kuonyesha matabaka mbalimbali ya wanadamu, na kwa njia hiyo kubaini kama ni waovu au ni wenye haki. Baada ya kazi ya kushinda, kazi ya kutuza mazuri na kuadhibu maovu inafuata: watu wanaotii kabisa, yaani walioshindwa kabisa, watawekwa katika hatua nyingine ya kusambaza kazi ulimwenguni kote; wasioshindwa watawekwa gizani na watapatwa na majanga. Hivyo, mwanadamu ataainishwa kulingana na aina yake, watenda maovu watawekwa pamoja na maovu, wasiwe na mwanga wa jua tena kamwe, na wenye haki watawekwa pamoja na mazuri, ili kupokea mwangaza na kuishi milele katika mwangaza. Mwisho wa vitu vyote uko karibu; mwisho wa mwanadamu umebainishwa wazi machoni mwake, na vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina yake. Ni vipi basi wanadamu wataepuka kuathiriwa na kuanisha huku? Kufichua mwisho kwa kila jamii ya mwanadamu kutafanywa hatima ya kila kitu ikikaribia, na kutafanywa wakati wa kazi ya kushinda ulimwengu mzima (ikiwemo kazi yote ya kushinda kuanzia kazi ya sasa). Huku kufichua mwisho wa wanadamu kunafanywa mbele ya kiti cha hukumu, katika harakati ya kuadibu, na harakati ya kazi ya kushinda ya siku za mwisho. Kuwaainisha watu kwa kadri ya aina si kuwarudisha watu katika matabaka yao ya asili. Hii ni kwa sababu binadamu alipoumbwa wakati wa uumbaji wa ulimwengu, kulikuwa tu na aina moja ya binadamu, kiume na wa kike. Hakukuwa na aina nyingi tofautitofauti. Ni baada tu ya miaka elfu kadhaa ya upotovu ndio matabaka mbalimbali ya binadamu yameibuka, mengine yakija chini ya miliki ya pepo wachafu, mengine chini ya miliki ya pepo waovu, na mengine, yanayofuatilia njia ya uzima, chini ya miliki ya Mwenyezi. Ni kwa njia hii tu ndio matabaka huibuka polepole miongoni mwa watu na ndio watu hujitenga katika matabaka ndani ya familia kubwa ya mwanadamu. Watu wote huja kuwa na “baba” tofauti; sio ukweli kwamba kila mtu yuko chini ya miliki ya Mwenyezi kabisa, kwa sababu uasi wa watu umezidi sana. Hukumu yenye haki hufichua nafsi ya kweli ya kila aina ya watu, bila kuacha chochote kikiwa kimefichika. Kila mtu huonyesha uso wake wa kweli katika nuru. Wakati huu, mwanadamu hayuko tena alivyokuwa mwanzoni na mfano wa asili wa mababu zake umepotea kitambo, kwa sababu vizazi visivyohesabika vya Adamu na Hawa vimenaswa na Shetani kwa muda mrefu, visijue tena jua la mbinguni, na kwa kuwa watu wamejazwa aina zote za sumu za Shetani. Hivyo, watu wana hatima zao za kufaa. Zaidi ya hayo, ni kwa msingi wa sumu zao zinazotofautiana ndio wanaainishwa kwa kadri ya aina, kumaanisha wanaainishwa kwa kiasi ambacho wanashindwa leo. Hatima ya mwanadamu si kitu kilichoamuliwa kabla tangu uumbaji wa dunia. Hii ni kwa sababu mwanzoni kulikuwa na jamii moja tu, ambayo kwa pamoja iliitwa “wanadamu,” na mwanadamu alikuwa bado hajapotoshwa na Shetani mwanzoni, na wanadamu wote waliishi katika mwangaza wa Mungu, bila giza kuwaandama. Lakini baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, kila jamii na aina ya watu walitapakaa ulimwenguni kote—kila jamii na aina ya watu waliotokana na ukoo mmoja ujulikanao kwa pamoja kama “wanadamu” uliojumuisha mwanamke na mwanamume. Wote walipotoshwa na mababu zao kutoka kwa nia za mababu zao wa kale sana—wanadamu waliojumuisha mwanamke na mwanamume (yaani, Adamu na Hawa wa asili, mababu zao wa kale sana). Wakati huo, watu wa pekee duniani walioongozwa na Yehova walikuwa Waisraeli. Watu wa aina mbalimbali walioibuka kutoka Israeli nzima (yaani kutoka ukoo wa asili) wakati ule walipoteza uongozi wa Yehova. Watu hawa wa mwanzo, wasiofahamu kabisa masuala ya ulimwengu wa wanadamu, walienda na mababu zao kuishi katika maeneo waliyodai kumiliki, mpaka wa leo. Hivyo hawatambui walipotoka vipi kutoka kwa Yehova na jinsi wamepotoshwa mpaka leo na aina yote ya pepo wachafu na roho waovu. Waliopotoshwa zaidi na kutiwa sumu mpaka leo hii, yaani ambao hatimaye hawawezi kukombolewa, hawatakuwa na budi ila tu kufuata mababu zao—pepo wachafu waliowapotosha. Wale wanaoweza kukombolewa hatimaye watakwenda hatima inayostahili wanadamu, yaani sehemu iliyotengwa kwa ajili ya waliokombolewa na walioshindwa. Kila kitu kitafanywa ili kukomboa wanaoweza kukombolewa, ila wale wasiosikia, watu wasioweza kutibika, chaguo lao pekee litakuwa kuwafuata mababu zao katika kuzimu ya kuadibu. Usidhani kuwa hatima yako iliamuliwa kabla tangu mwanzo na imefichuliwa tu sasa. Ikiwa unadhani hivyo, basi, umesahau kuwa katika uumbaji wa mwanzo wa wanadamu, hakukuumbwa jamii tofauti ya Shetani? Je, umesahau kuwa ni aina moja tu ya mwanadamu, yaani Adamu na Hawa, ndiyo iliumbwa (ikiwa na maana kwamba ni mwanamume na mwanamke tu ndio waliumbwa)? Ungalikuwa uzao wa Shetani kutoka mwanzo, je, hilo halingemaanisha kuwa Yehova alipomuumba mwanadamu Alijumuisha jamii ya Shetani? Je, Angefanya jambo kama hilo? Alimuumba mwanadamu kwa ajili ya ushuhuda Wake; Alimuumba mwanadamu kwa ajili ya utukufu Wake. Angeumbaje kwa makusudi jamii ya vizazi vya Shetani ili kumuasi kwa makusudi? Je, Yehova angeweza kufanya hili? Ikiwa hivyo, ni nani angeweza kusema kuwa Yeye ni Mungu Mwenye haki? Nikisema sasa kuwa baadhi yenu mwishowe mtaenda na Shetani, haimaanishi kuwa ulikuwa na Shetani toka mwanzo; ila, inamaanisha umejishusha chini sana hivi kwamba japo Mungu amejaribu kukukomboa, bado umekosa kuupata ukombozi huo. Hakuna budi ila kukuweka katika jamii moja na Shetani. Hii ni kwa sababu huwezi kukombolewa, si kwa sababu Mungu si mwenye haki kwako, yaani, si kwa sababu Mungu kimakusudi alipangia majaliwa yako kama mfano halisi wa Shetani na baadaye kukuweka katika jamii moja na Shetani na kutaka uteseke kwa makusudi. Huo si ukweli wa ndani wa kazi ya kushinda. Ikiwa unaamini hilo, basi ufahamu wako unaegemea upande mmoja sana! Hatua ya mwisho ya kushinda ni ya kukomboa watu na vilevile kufichua mwisho wa kila mtu. Inaweka wazi upotevu wa watu kupitia hukumu na kwa njia hiyo kuwafanya watubu, waamke, na kufuatilia uzima na njia ya haki ya maisha ya mwanadamu. Ni ya kuamsha mioyo ya waliolala na wapumbavu na kuonyesha, kwa njia ya hukumu, uasi wao wa ndani. Hata hivyo, ikiwa watu bado hawawezi kutubu, bado hawawezi kufuata njia ya haki ya maisha ya mwanadamu na hawawezi kuutupa upotovu huu, basi watakuwa vyombo visivyoweza kukombolewa vya kumezwa na Shetani. Hii ndiyo maana ya kushinda—kuwakomboa watu na vilevile kuwaonyesha mwisho wao. Mwisho mzuri, mwisho mbaya—yote yanafichuliwa na kazi ya kushinda. Kama watu watakombolewa au kulaaniwa yote yanafichuliwa wakati wa kazi ya kushinda.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 31)

Siku za mwisho ni wakati ambao vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina zake kupitia kushinda. Kushinda ni kazi ya siku za mwisho; kwa maneno mengine, kuhukumu dhambi za kila mtu ni kazi ya siku za mwisho. La sivyo, watu wangeainishwa vipi? Kazi ya kuainisha inayofanywa miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi ya aina hiyo ulimwenguni kote. Baada ya hii, wale wa kila nchi na watu wote watapitia kazi ya ushindi. Hii inamaanisha kuwa watu wote wataainishwa kimakundi na kufika mbele ya kiti cha hukumu kuhukumiwa. Hakuna mtu na hakuna kitu kitakachoepuka kupitia huku kuadibu na hukumu, na hakuna mtu au kitu kinaweza kukwepa uainishaji huu; kila mtu atawekwa katika jamii. Hii ni kwa sababu mwisho u karibu kwa vitu vyote na mbingu zote na dunia zimefikia hatima yake. Mwanadamu anawezaje kukwepa hatima ya maisha yake? Hivyo, mnaweza kuendelea na matendo yenu ya uasi kwa muda gani zaidi? Je, hamuoni kwamba siku zenu za mwisho ziko karibu sana? Ni vipi ambavyo wale wanaomcha Mungu na kutamani sana Aonekane watakosa kuona siku ya kuonekana kwa haki ya Mungu? Wanawezaje kukosa kupokea thawabu ya mwisho ya wema? Je, wewe ni yule atendaye mema, au yule atendaye maovu? Je, wewe ni yule akubaliye hukumu yenye haki na kisha kutii, au kisha hulaaniwa? Umekuwa ukiishi katika nuru mbele ya kiti cha hukumu, au katika giza jahanamu? Je, wewe mwenyewe si unayejua kwa dhahiri sana kama mwisho wako utakuwa wa thawabu au wa adhabu? Je, wewe si unayejua kwa dhahiri sana na kufahamu kwa kina sana kwamba Mungu ni mwenye haki? Kwa hiyo, kweli, mwenendo wako uko vipi na una moyo wako wa aina gani? Ninapoendelea kukushinda leo, unanihitaji Mimi kwa kweli kukueleza kinagaubaga kama mwenendo wako ni wa uovu au wa mema? Je, umeacha kiasi gani kwa ajili Yangu? Unaniabudu Mimi kwa kina gani? Wewe mwenyewe unajua kwa dhahiri sana ulivyo Kwangu—je, hiyo si kweli? Unapaswa kujua vizuri zaidi kuliko mtu yeyote jinsi utakavyokuwa hatimaye! Kweli Nakwambia, Niliwaumba tu wanadamu, na Nilikuumba wewe, lakini Sikuwakabidhi kwa Shetani; wala kuwafanya kwa makusudi muasi dhidi Yangu au kunipinga Mimi na kwa hivyo kuadhibiwa na Mimi. Hamjapata majanga haya kwa sababu mioyo yenu imekuwa migumu mno na mienendo yenu yenye kustahili dharau mno? Kwa hiyo si kweli kwamba mnaweza kuamua hatima yenu wenyewe? Je, si kweli kwamba mnajua ndani ya mioyo yenu, bora zaidi kuliko yeyote, vile mtaishia? Sababu ya Mimi kuwashinda watu ni kuwafichua, na pia kuhakikisha bora zaidi wokovu wako. Sio kukusababisha ufanye uovu au kwa makusudi kukusababisha uingie katika jahanamu ya uharibifu. Wakati utakapofika, mateso yako yote makuu, kulia kwako na kusaga meno—je, hayo yote hayatakuwa kwa ajili ya dhambi zako? Kwa hiyo, uzuri wako mwenyewe au uovu wako mwenyewe sio hukumu bora zaidi kukuhusu? Je, sio thibitisho bora zaidi ya kile ambacho mwisho wako utakuwa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 32)

Wakati wa siku za mwisho, Mungu Amekuja mahususi kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake. Anazungumza kutokana na mtazamo wa Roho, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, na kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu; Anazungumza kwa namna tofauti, Akitumia njia moja kwa kipindi fulani, na Anatumia njia za kuzungumza ili kubadilisha dhana za mwanadamu na kuondoa taswira ya Mungu yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii ndiyo kazi kuu iliyofanywa na Mungu. Kwa sababu mwanadamu anaamini kwamba Mungu Amekuja kuponya wagonjwa, kutoa mapepo, kufanya miujiza, na kumpatia mwanadamu baraka za vitu, Mungu Anatekeleza hatua hii ya kazi—kazi ya kuadibu na hukumu—ili kuweza kuondoa mambo hayo kutoka katika dhana za mwanadamu, ili mwanadamu aweze kuuelewa uhalisia na ukawaida wa Mungu, na ili kwamba taswira ya Yesu iweze kuondolewa moyoni mwake na kuwekwa taswira mpya ya Mungu. Mara tu taswira ya Mungu ndani ya mwanadamu inapozeeka, basi inakuwa sanamu. Yesu alipokuja na kutekeleza hatua hii ya kazi, Hakuwakilisha Mungu kikamilifu. Alifanya baadhi ya ishara na maajabu, Alizungumza maneno kadhaa, na hatimaye Akasulubishwa, na Aliwakilisha upande mmoja wa Mungu. Hakuweza kuwakilisha yale yote ambayo ni ya Mungu, bali Alimwakilisha Mungu katika kufanya upande mmoja wa kazi ya Mungu. Hiyo ni kwa sababu Mungu ni mkuu, na ni wa ajabu sana, na Haeleweki, na kwa sababu Mungu Anafanya upande mmoja tu wa kazi Yake katika kila enzi. Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu; kufunuliwa kwa tabia potovu ya mwanadamu na kiini cha asili ya mwanadamu; na uondoaji wa fikira za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Alimwongoza Musa kutoka Misri kwa maneno Yake, na Akazungumza maneno fulani kwa Wanaisraeli; wakati huo, sehemu ya matendo ya Mungu yaliwekwa wazi, lakini kwa sababu ubora wa tabia ya mwanadamu ulikuwa finyu na hakuna kitu chochote ambacho kingeweza kufanya maarifa yake kukamilika, Mungu Aliendelea kuzungumza na kufanya kazi. Wakati wa Enzi ya Neema, mwanadamu aliweza kuona tena sehemu ya matendo ya Mungu. Yesu Aliweza kuonyesha ishara na maajabu, kuponya wagonjwa na kutoa mapepo, na kusulubishwa, siku tatu baadaye. Akafufuka na Akawatokea watu Akiwa katika mwili. Kumhusu Mungu, mwanadamu hakujua chochote zaidi ya hiki. Mwanadamu anajua tu kile ambacho Mungu Amemwonyesha, na kama Mungu Asingeonyesha chochote zaidi kwa mwanadamu, basi hicho kingekuwa kiwango cha mwanadamu kumwekea mipaka Mungu. Hivyo, Mungu Anaendelea kufanya kazi, ili maarifa ya mwanadamu juu Yake yaweze kuwa ya kina zaidi, na ili taratibu aweze kuijua hulka ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu anatumia maneno yake kumkamilisha mwanadamu. Tabia yako iliyoharibika imewekwa wazi kwa maneno ya Mungu, na dhana zako za kidini zinaondolewa na uhalisia wa Mungu. Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kutimiza maneno haya kwamba “Neno Lafanyika kuwa mwili, Neno Lakuwa mwili, na Neno Laonekana katika mwili,” na kama huna maarifa ya kina kuhusu hili, basi hutaweza kusimama imara. Wakati wa siku za mwisho, kimsingi Mungu Anakusudia kukamilisha hatua ya kazi ambayo kwayo Neno Anaonekana katika mwili, na hii ni sehemu moja ya mpango wa usimamizi wa Mungu. Hivyo, maarifa yenu yanapaswa kuwa wazi; bila kujali namna ambavyo Mungu Anafanya kazi, Mungu Hamruhusu mwanadamu kumwekea mipaka. Ikiwa Mungu Asingefanya kazi hii wakati wa siku za mwisho, basi maarifa ya mwanadamu juu Yake yasingeweza kwenda popote. Ungeweza kujua tu kwamba Mungu Anaweza kusulubiwa na Anaweza kuiangamiza Sodoma, na kwamba Yesu Anaweza kufufuliwa kutoka katika wafu na kumtokea Petro.... Lakini usingeweza kusema kwamba maneno ya Mungu yanaweza kutimiza yote, na yanaweza kumshinda mwanadamu. Ni kwa njia tu ya kupitia uzoefu wa maneno ya Mungu ndipo unaweza kuzungumza juu ya maarifa hayo, na kadri unapopitia uzoefu wa kazi ya Mungu zaidi, ndivyo maarifa yako yanavyokuwa ya kina zaidi kumhusu Yeye. Ni baada ya hapo tu ndipo utaacha kumwekea Mungu mipaka ndani ya dhana zako binafsi. Mwanadamu anakuja kumjua Mungu kwa kupitia kazi Yake, na hakuna njia nyingine sahihi ya kumjua Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 33)

Katika hatua hii ya mwisho ya kazi, matokeo yanapatikana kupitia kwa neno. Kupitia kwa neno, mwanadamu anaelewa mafumbo mengi na kazi ya Mungu katika vizazi vilivyopita; kupitia kwa neno, mwanadamu anapewa nuru na Roho Mtakatifu; kupitia kwa neno, mwanadamu anapata kuelewa mafumbo ambayo hayajawahi kuelezwa na vizazi vilivyopita, na pia kazi za manabii na, mitume wa enzi zilizopita, na kanuni ambazo walitumia kufanya kazi; kupitia kwa neno, mwanadamu anatambua tabia ya Mungu Mwenyewe, na pia uasi na pingamizi ya mwanadamu, na anakuja kujua dutu yake mwenyewe. Kupitia kwa hatua hizi za kazi na maneno yote yaliyonenwa, mwanadamu anatambua kazi ya Roho Mtakatifu, kazi ya mwili wa Mungu, na zaidi ya hayo, tabia Yake yote. Maarifa yako ya kazi ya usimamizi wa Mungu wa kupita miaka elfu sita ulitwaliwa kupitia kwa neno. Je, maarifa yako hayakuwa ya fikira zako za awali na mafanikio kwa kuyaweka kando pia yalipatikana kupitia neno? Katika hatua ya awali, Yesu Alifanya ishara na maajabu, lakini sio hivyo katika hatua hii. Je si kuelewa kwako kwa nini Mungu hafanyi ishara na maajabu pia kulipatikana kupitia neno? Kwa hivyo, maneno yanenwayo katika hatua hii, yanashinda kazi iliyofanywa na mitume na manabii wa vizazi vilivyopita. Hata unabii uliotabiriwa na manabii haungeweza kupata matokeo haya. Manabii waliongelea unabii pekee, ya kile kitakachotendeka hapo baadaye, lakini sio kazi ambayo Mungu angefanya katika wakati huo. Hawakuongea kuwaongoza wanadamu katika maisha yao, kuwapa wanadamu ukweli ama kumfichulia mwanadamu mafumbo, ama hata kutawaza maisha. Kwa maneno yaliyonenwa katika hatua hii, kuna unabii na ukweli, lakini hasa yanafanya kazi ya kutawaza maisha juu ya mwanadamu. Maneno ya wakati huu sio kama unabii wa manabii. Hii ni hatua ya kazi isiyo ya unabii ila ya maisha ya mwanadamu, kubadili tabia ya maisha ya mwanadamu. Hatua ya kwanza ilikuwa kazi ya Yehova kutengeneza njia ya mwanadamu kuabudu Mungu duniani. Ilikuwa kazi ya kuanzisha kutafuta chanzo cha kazi duniani. Wakati huo, Yehova aliwafunza Waisraeli kuiheshimu Sabato, wawaheshimu wazazi wao na kuishi kwa amani na wengine. Hii ilikuwa kwa sababu watu wa wakati huo hawakuwa ni nini kilichukuliwa kuwa mwanadamu, wala hawakuelewa walivyopaswa kuishi duniani. Ilikuwa lazima Kwake katika hatua ya kwanza ya kazi kuwaongoza wanadamu katika maisha yao. Yote yale Yehova aliwazungumzia hayakuwa yamewahi kujulikana kwa binadamu ama kuwa katika umiliki wao. Wakati huo, Mungu aliwainua manabii wengi kunena unabii, yote kutengenezwa chini ya uongozi wa Yehova. Hii ilikuwa sehemu moja ya kazi ya Mungu. Katika hatua ya kwanza, Mungu hakuwa mwili, hivyo Alizungumza na makabila yote na mataifa kupitia kwa manabii. Yesu alipofanya kazi Yake katika huo wakati, Hakuzungumza sana kama wakati huu wa leo. Kazi hii ya neno katika siku za mwisho haijafanyika katika enzi na vizazi vilivyopita. Ingawa Isaya, Danieli na Yohana walitabiri utabiri mwingi, unabii huo ulikuwa tofauti kabisa na maneno yazungumzwayo sasa. Walichoongelea ulikuwa unabii pekee, lakini maneno ya sasa sio unabii. Iwapo Ningebadilisha Ninayoongea sasa yawe unabii, je mngeweza kuyaelewa? Iwapo yale niliyozungumzia yangehusu mambo baada ya Mimi kuondoka, ungewezaje basi kupata kuelewa? Kazi ya neno haikuwahi kufanyika wakati wa Yesu ama Enzi ya Sheria. Labda wengine wanaweza kusema, “Je Yehova hakuzungumza maneno pia katika wakati wa kazi Yake? Juu yaa kuponya magonjwa, kukemea mapepo na kufanya ishara na maajabu, je Yesu hakuzungumza katika wakati huo?” Kuna tofauti katika vile maneno yananenwa. Ni nini ndiyo ilikuwa dutu ya maneno yaliyonenwa na Yehova? Alikuwa tu Akiwaongoza wanadamu katika maisha yao duniani, ambayo hayakuwa yanahusiana na mambo ya kiroho katika maisha. Ni kwa nini inasemekana kuwa maneno ya Yehova yalitangazwa katika sehemu zote? Neno “kufundisha” linamaanisha kuwaambia waziwazi na kuamrisha moja kwa moja. Hakupa mwanadamu maisha; ila, Alimchukua mwanadamu kwa mkono na kumfunza jinsi ya kumheshimu sana. Hakukuwa na mafumbo. Kazi ya Yehova katika Israeli haikuwa kushughulika na ama kumwadhibu mwanadamu ama kutoa hukumu na kuadibu, ilikuwa kuongoza. Yehova alimwambia Musa awaeleze watu Wake wakusanye mana jangwani. Kila asubuhi kabla ya jua kuchomoza, walikuwa wakusanye mana, iliyotosha tu kuliwa siku hiyo. Mana haingewekwa hadi siku inayofuata, kwani ingeoza. Hakuwakaripia wanadamu au kufichua asili zao, wa Hakufichua mawazo yao na fikira. Hakuwabadilisha watu ila tu aliwaongoza katika maisha yao. Katika wakati huo, watu walikuwa kama watoto; mwanadamu hakuelewa chochote na angefanya hatua za kuelekezwa, na hivyo, Yehova aliamuru tu sheria kuongoza watu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 34)

Mungu huzungumza maneno Yake na kufanya kazi Yake kulingana na enzi tofauti, na katika enzi tofauti, Anazungumza maneno tofauti. Mungu hafuati sheria, ama kurudia kazi ya awali, ama kuhisi hali ya kumbukumbu kwa vitu vilivyopita; ni Mungu ambaye ni mpya kila wakati na hazeeki, na kila siku anazungumza maneno mapya. Unapaswa uyafuate yale ambayo lazima yafuatwe leo; haya ni majukumu na kazi ya mwanadamu. Ni muhimu kwamba utendaji uwekwe katika nuru iliyopo na maneno ya Mungu katika siku ya leo. Mungu hafuati masharti, na Anaweza kuzungumza kutoka kwa mitazamo mingi tofauti ili kufanya wazi hekima Yake na uwezo. Haijalishi ikiwa Anazungumza kutoka kwa mtazamo wa Roho, ama mwanadamu, ama mtu wa tatu—Mungu ni Mungu kila wakati na huwezi kusema kuwa yeye si Mungu kwa sababu ya mtazamo wa mwanadamu ambao Anazungumzia kutoka. Kati ya baadhi ya watu dhana zimetokea kutokana na mitazamo tofauti tofauti ambayo Mungu Anazungumza. Watu hao hawana maarifa ya Mungu, na pia maarifa ya kazi Yake. Iwapo Mungu angezungumza kila wakati kutumia mtazamo mmoja, je mwanadamu hangeweka masharti kuhusu Mungu? Je Mungu Anaweza kukubali mwanadamu kutenda kwa njia hiyo? Haijalishi ni mtazamo gani ambao Mungu Anaongelea, Mungu Ana malengo Yake kwa kila moja. Iwapo Mungu Angeongea kila wakati kwa mtazamo wa Roho, ungeweza kushiriki na Yeye? Hivyo, wakati mwingine Yeye huzungumza kupitia mtu wa tatu ili kukupatia maneno Yake na kukuongoza kwa ukweli. Kila kitu Atendacho Mungu kinafaa. Kwa ufupi, yote yanafanywa na Mungu, na hupaswi kuwa na shaka kuyahusu. Bora tu kwamba Yeye ni Mungu, basi haijalishi kuwa ni mtazamo gani Anaongelea kutoka, Yeye bado ni Mungu. Huu ni ukweli usiobadilika. Njia yoyote Afanyayo kazi, Yeye bado ni Mungu, na dutu Yake haiwezi kubadilika! Petro alimpenda Mungu sana na alikuwa mtu aliyetaka kumridhisha Mungu, lakini Mungu hakumshuhudia kama Bwana ama Kristo, kwani dutu ya kiumbe ni vile ilivyo, na haiwezi badilika. Katika kazi Yake, Mungu hafuati masharti, lakini Anatumia mbinu tofauti kufanya kazi Yake ifanikiwe na kuongeza maarifa ya mwanadamu kumhusu. Kila mbinu Yake ya kazi inamsaidia mwanadamu kumjua, na ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu kamili. Haijalishi ni mbinu gani ya kufanya kazi Yeye hutumia, kila ni ili kumwongeza mwanadamu na kumfanya mtimilifu. Ingawa moja ya mbinu Zake za kazi ilikaa kwa muda mrefu, ni kwa ajili ya kupunguza imani ya mwanadamu Kwake. Hivyo hampaswi kuwa na shaka. Hizi zote ni hatua za kazi ya Mungu, na mnapaswa kuzitii.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 35)

Mungu Amekuja ulimwenguni hasa kuzungumza maneno Yake; unachoshiriki nacho ni neno la Mungu, uonacho ni neno la Mungu, usikiacho ni neno la Mungu, unachokaa nacho ni neno la Mungu, unachopitia ni neno la Mungu, na Mungu aliyepata mwili huyu kimsingi hutumia neno kumfanya mwanadamu kamili. Yeye haonyeshi ishara na maajabu, na hasa hafanyi kazi ambayo Yesu Alifanya hapo awali. Ingawa wao ni Mungu, na wote ni mwili, huduma Zao sio sawa. Yesu Alipokuja, Alifanya pia baadhi ya sehemu ya kazi ya Mungu, na kuongea baadhi ya maneno—lakini ni kazi gani kuu Aliyokamilisha? Alichokamilisha hasa ni kazi ya kusulubishwa. Akawa mfano wa mwili wenye dhambi ili kukamilisha kazi ya kusulubiwa na kuwakomboa wanadamu wote, na ilikuwa kwa ajili ya dhambi zote za binadamu, ndio Alitumika kama sadaka ya dhambi. Hii ndiyo kazi hasa Aliyokamilisha. Hatimaye, Alileta njia ya msalaba ili kuwaongoza wale waliokuja baadaye. Yesu Alipokuja, ilikuwa kimsingi kukamilisha kazi ya ukombozi. Aliwakomboa binadamu wote, na kuleta injili ya ufalme wa mbinguni kwa mwanadamu, na zaidi, Alileta njia ya ufalme wa mbinguni. Kwa sababu hii, waliokuja baada ya yote walisema, “Tunapaswa tutembee njia ya msalaba, na tujitoe kama kafara kwa ajili ya msalaba.” Bila shaka, hapo mwanzo Yesu pia Alifanya kazi nyingine na kuongea baadhi ya maneno ili kumfanya mwanadamu atubu na kukiri dhambi zake. Lakini huduma Yake ilikuwa bado ni kusulubiwa, na miaka mitatu na nusu Aliyotumia kuhubiri njia ilikuwa katika matayarisho ya kusulubiwa kulikokuja baadaye. Mara kadhaa ambazo Yesu Alisali zilikuwa pia ni kwa ajili ya kusulubishwa. Maisha ya mwanadamu wa kawaida Aliyoishi na miaka thelathini na tatu na nusu aliyoishi duniani yalikuwa kimsingi kwa ajili ya kukamilisha kazi ya kusulubishwa, yalikuwa ya kumpa nguvu ya kutekeleza kazi hii, na kwa sababu hii Mungu Alimwaminia kazi ya kusulubiwa. Leo ni kazi gani ambayo Mungu katika mwili atakamilisha? Leo Mungu Amekuwa mwili kimsingi ili kukamilisha kazi ya “Neno kuonekana katika mwili,” kutumia neno kumfanya mwanadamu kamili, na kumfanya mwanadamu kukubali ushughulikiaji wa neno na usafishaji wa neno. Katika maneno Yake, anakufanya kupata kupewa na kupata uzima; katika maneno Yake, unaona kazi Yake na matendo. Mungu Anatumia neno kukuadibu na kukutakasa, na hivyo ukipata ugumu wa maisha, ni pia kwa sababu ya neno la Mungu. Leo, Mungu hafanyi kazi kwa kutumia mambo ya hakika, ila ni kwa maneno. Baada tu ya neno Lake kuja juu yako ndipo Roho Mtakatifu Atafanya kazi ndani yako na kukufanya upate uchungu ama uhisi utamu. Ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukuleta katika hali halisi, na ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukufanya mkamilifu. Kwa hivyo, angalau lazima uelewe hili: Kazi inayofanywa na Mungu katika siku za mwisho kimsingi ni kutumia neno Lake kumfanya kila mwanadamu kamili na kumwongoza mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ni kupitia kwa neno; Hatumii ukweli kuadibu. Kuna wakati ambapo watu wengine humpinga Mungu. Mungu hasababishi ukosefu mkubwa wa starehe kwako, mwili wako hauadibiwi wala wewe kupitia ugumu—lakini pindi tu neno Lake linapokuja juu yako, na kukutakasa, hutaweza kuvumilia. Je si hivyo ndivyo ilivyo? Wakati wa “watendaji huduma” Mungu Alisema mwanadamu atupwe katika shimo lisilo na mwisho. Mwanadamu aliweza kufika kwenye shimo lisilo na mwisho? Kupitia kwa maneno tu kumtakasa mwanadamu, mwanadamu aliingia kwenye shimo lisilo na mwisho. Kwa hivyo, katika siku za mwisho, Mungu anapokuwa mwili, kimsingi Anatumia neno kukamilisha yote na kufanya yote yawe wazi. Katika maneno Yake pekee ndipo unaweza kuona kile Alicho; ni katika maneno Yake pekee ndiyo unaweza kuona kwamba yeye ni Mungu Mwenyewe. Mungu katika mwili Anapokuja duniani, hafanyi kazi nyingine ila kuongea maneno—hivyo basi hakuna haja ya kutumia uhakika; maneno yanatosha. Hii ni kwa sababu Amekuja kimsingi kufanya kazi hii, kumruhusu mwanadamu aone nguvu Zake na ukuu ulio kwenye neno Lake, kumruhusu mwanadamu kuona kupitia kwa maneno Yake jinsi Alivyojificha kwa unyenyekevu, na kumruhusu mwanadamu kujua ukamilifu Wake kupitia kwa maneno Yake. Kila kitu Alicho nacho na kile Alicho kiko katika maneno Yake, hekima Yake na ajabu yako katika maneno Yake. Katika hii ndipo unapofanywa kuona mbinu nyingi ambazo Mungu anatumia kuongea maneno Yake. Kazi ya Mungu nyingi katika wakati huu wote imekuwa kutoa, ufunuo, na kushughulika mwanadamu. Hatoi laana kwa mwanadamu kijuu juu, na hata Akifanya hivyo, ni kupitia kwa neno. Na hivyo, katika enzi hii ya Mungu kuwa mwili, usijaribu kuona Mungu akiponya wagonjwa na kufukuza mapepo tena, usijaribu kila mara kuona ishara—hakuna haja! Ishara hizo haziwezi kumfanya mwanadamu kamili! Kuongea wazi: Leo Mungu wa kweli Mwenyewe wa mwili Anaongea tu, na hatendi. Huu ni ukweli! Anatumia maneno kukufanya mkamilifu, na Anatumia maneno kukulisha na kukunyunyizia. Pia Anatumia maneno kufanya kazi, na Anatumia maneno badala ya uhakika kukufanya ujue ukweli Wake. Kama una uwezo wa kutazama aina hii ya kazi ya Mungu, basi itakuwa vigumu kuwa wa kutoonyesha hisia. Badala ya kulenga vitu vilivyo vibaya, mnapaswa tu kulenga yale yaliyo mazuri—hivyo ni kusema, bila kujali kama maneno ya Mungu yamekamilika au la, ama iwapo kuna majilio ya ukweli ama haupo, Mungu anamfanya mwanadamu kupata uzima kutoka kwa maneno Yake, na hii ndiyo ishara kuu kushinda zote, na hata zaidi, ni ukweli usiopingika. Huu ndio ushahidi bora wa kupata ufahamu kumhusu Mungu, na ni ishara hata kuu kushinda ishara. Maneno haya pekee yanaweza kumfanya mwanadamu kamili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 36)

Pindi tu Enzi ya Ufalme ilipoanza, Mungu alianza kuachilia Maneno Yote. Katika siku za baadaye, maneno haya yataendelea kutimizwa, na katika wakati huo, mwanadamu atakua katika uzima. Matumizi ya neno na Mungu kufichua tabia potovu ya mwanadamu ni ya kweli zaidi, na ni ya lazima zaidi, na Hatumii chochote ila neno kufanya kazi Yake ili kuifanya imani ya mwanadamu iwe kamili, kwani leo ni Enzi ya Neno, na inahitaji imani, uamuzi na ushirikiano wa mwanadamu. Kazi ya Mungu katika mwili wa siku za mwisho ni kutumia neno Lake kutumikia na kukimu mahitaji ya mwanadamu. Ni baada tu ya Mungu katika mwili kumaliza kuongea maneno Yake ndipo yatakapoanza kutimika. Wakati Anapoongea, maneno Yake hayatimiliki, kwani Anapokuwa katika hatua ya mwili, maneno Yake hayawezi kutimika, na hii ni ili mwanadamu aweze kuona kuwa Mungu ni mwili na sio Roho, ili mwanadamu aweze kutazama hali halisi ya Mungu kwa macho yake Mwenyewe. Katika ile siku ambayo kazi Yake imekamilika, wakati ambao maneno yote yanayopaswa kunenwa na Yeye duniani yamenenwa, maneno Yake yataanza kutimika. Sasa sio enzi ya utimizaji wa maneno ya Mungu, kwa kuwa Hajamaliza kuongea maneno Yake. Kwa hivyo ukiona kuwa Mungu bado Ananena maneno yake duniani, usingoje kutimizwa kwa maneno Yake; Mungu Anapokoma kunena maneno Yake, na wakati kazi Yake duniani imekamilika, huo ndio utakuwa wakati ambao maneno Yake yanaanza kutimika. Katika maneno Anayozungumza duniani, kunayo, katika mtazamo mmoja, utoaji wa uzima, na katika mtazamo mwingine, kuna unabii—unabii wa vitu vitakavyokuja, wa vitu vitakavyofanywa, na vya vitu ambavyo bado havijatimizwa. Kulikuwa pia na unabii katika maneno ya Yesu. Katika mtazamo mmoja, Alitoa uzima, na katika mtazamo mwingine Alinena unabii. Leo, hakuna mazungumzo ya kutekeleza maneno na uhakika kwa wakati mmoja, kwani tofauti kati ya yale yanayoweza kuonekana na macho ya mwanadamu na yale yanayotendwa na Mungu ni kubwa mno. Inaweza kusemwa tu kwamba, mara kazi ya Mungu inapokamilika, maneno Yake yatatimika, na mambo ya hakika yatakuja baada ya maneno. Duniani, Mungu katika mwili wa siku za mwisho anafanya huduma ya neno, na kwa kufanya huduma ya neno, Anazungumza maneno pekee, na hajali kuhusu mambo mengine. Mara kazi ya Mungu itakapobadilika, maneno Yake yataanza kutimika. Leo, maneno yanatumiwa kwanza kukufanya mkamilifu; Atakapopokea utukufu katika ulimwengu mzima, utakuwa wakati ambao kazi Yake imekamilika, wakati maneno yote ambayo yanapaswa kuzungumzwa yatakuwa yamezungumzwa, na maneno yote yamekuwa ukweli. Mungu amekuja duniani wakati wa siku za mwisho ili kutekeleza huduma ya neno ili mwanadamu amtambue, na ili mwanadamu aone kile Alicho, na aone hekima Yake na matendo Yake yote ya maajabu kutoka kwa neno Lake. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno kimsingi kushinda watu wote. Baadaye neno Lake litakuja katika kila dini, kikundi, taifa na madhehebu; Mungu hutumia neno kushinda, kuwafanya wanadamu wote waone kuwa neno Lake lina mamlaka na nguvu—na kwa hivyo leo, mnakumbana tu neno la Mungu.

Maneno ambayo Mungu Alizungumza katika enzi hii ni tofauti na yale yaliyozungumzwa katika Enzi ya Sheria, na kwa hivyo, pia yako tofauti na maneno yaliyonenwa katika Enzi ya Neema. Katika Enzi ya Neema, Mungu hakufanya kazi ya neno, lakini Alieleza tu usulubisho ili kuwakomboa binadamu wote. Biblia inaelezea tu ni kwa nini Yesu alikuwa Asulubiwe, na mateso ambayo Alipitia kwenye msalaba, na jinsi mwanadamu anapaswa kusulubiwa kwa ajili ya Mungu. Katika enzi hiyo, kazi yote iliyofanywa na Mungu ilikuwa kuhusu usulubisho. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu katika mwili Anazungumza maneno ili kushinda wale wote wanaomwamini. Huu ni, “Neno kuonekana katika mwili”; Mungu amekuja katika siku za mwisho ili kufanya kazi hii, ambayo ni kusema, Amekuja kutimiza umuhimu wenyewe wa Neno kuonekana katika mwili. Ananena tu maneno, na majilio ya ukweli ni chache. Hii ndiyo dutu kamili ya Neno kuonekana katika mwili, na wakati Mungu katika mwili Anaponena maneno Yake, huku ndiko kuonekana kwa Neno katika Mwili, na ni Neno kuja katika mwili. “Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili.” Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili. Yale yanayofanywa leo, yale yatakayofanywa baadaye, yale yatakayotimizwa na Mungu, hatima ya mwisho mwanadamu, wale watakaookolewa, wale watakaoangamizwa, na mengine mengi—kazi hii ambayo lazima itimizwe mwishowe imesemwa wazi, na yote ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu halisi wa Neno kuonekana kwa mwili. Amri za utawala na katiba ambayo ilipeanwa hapo awali, wale ambao wataangamizwa, wale watakaoingia katika mapumziko—maneno haya lazima yatimizwe. Hii ni kazi iliyotimizwa kimsingi na Mungu katika mwili katika siku za mwisho. Anawafanya watu waelewe kule ambako wale waliopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa na wale wasiopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa, jinsi ambavyo watu Wake na wana Wake watawekwa kwenye vikundi, ni nini kitaifanyikia Uyahudi, ni nini kitaufanyikia Misri—katika siku za usoni, kila mojawapo ya maneno haya yatatimizwa. Hatua za kazi za Mungu zinaharakishwa. Mungu hutumia neno kama mbinu ya kumfichulia mwanadamu kinachopaswa kufanyika katika kila enzi, kinachopaswa kufanywa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho, na huduma Yake ambayo inapaswa kufanywa, na maneno haya ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu hasa wa Neno kuonekana kwa mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 37)

Mungu anafanya kazi Yake katika ulimwengu mzima. Wote wanaoamini katika Yeye lazima walikubali neno Lake, na kula na kunywa neno Lake; hakuna atakayepatwa na Mungu kwa kuona ishara na maajabu yanayoonyeshwa na Mungu. Katika enzi zote, Mungu ametumia neno kila wakati kumfanya mwanadamu mkamilifu. Hivyo hampaswi kuweka mawazo yenu yote kwa ishara na maajabu, ila unapaswa kutafuta kufanywa mkamilifu na Mungu. Katika Enzi ya Sheria ya Agano la Kale, Mungu alinena baadhi ya maneno, na katika Enzi ya Neema, Yesu pia Alinena maneno mengi. Baada ya Yesu kunena maneno haya mengi, mitume na wanafunzi wa baadaye waliwaongoza watu kutenda kulingana na amri zilizotolewa na Yesu na wakapata uzoefu kulingana na maneno na kanuni zilizozungumziwa na Yesu. Katika siku za mwisho, Mungu hasa hutumia neno kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Hatumii ishara na maajabu kumdhulumu mwanadamu, ama kumshawishi mwanadamu; hii haiweki wazi nguvu za Mungu. Iwapo Mungu angeonyesha tu ishara na maajabu, basi hakungekuwa na uwezo wa kuweka wazi ukweli wa Mungu, na hivyo haingewezekana kumfanya mwanadamu mkamilifu. Mungu hamfanyi mwanadamu mkamilifu kwa kutumia ishara na maajabu, ila Anatumia neno kunyunyizia na kumchunga mwanadamu, na baada ya haya kunapatikana utiifu kamili wa mwanadamu na ufahamu wa mwanadamu kuhusu Mungu. Hili ndilo lengo la kazi Anayofanya na maneno Anenayo. Mungu hatumii mbinu ya kuonyesha ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kamili—Anatumia maneno, na Anatumia mbinu nyingi za kazi kumfanya mwanadamu kamili. Iwe ni usafishaji, kushughulikia, upogoaji, ama kupewa maneno, Mungu hunena kutoka taswira nyingi tofauti kumfanya mwanadamu kamili, na kumpa mwanadamu maarifa kuu ya kazi, hekima na ajabu ya Mungu. Mwanadamu anapofanywa mkamilifu katika wakati ambao Mungu Anamaliza enzi katika siku za mwisho, basi atakuwa amehitimu kuona ishara na maajabu. Unapokuja kumjua Mungu na uweze kumtii Mungu bila kujali Anachofanya, hutakuwa tena na mawazo kumhusu Yeye unapoona ishara na maajabu. Kwa sasa, wewe ni mpotovu na huwezi kuwa na utiifu kamili kwa Mungu—je umehitimu kuona ishara na maajabu? Wakati ambao Mungu anaonyesha ishara na maajabu ndio wakati ambao Mungu anamwadhibu mwanadamu, na pia wakati ambao enzi inabadilika, na zaidi, wakati ambapo enzi inatamatika. Wakati ambao kazi ya Mungu inatekelezwa kama kawaida, Haonyeshi ishara na maajabu. Kuonyesha ishara na maajabu ni jambo rahisi mno, lakini hiyo si kanuni ya kazi ya Mungu, wala si lengo la usimamizi wa Mungu wa mwanadamu. Iwapo mwanadamu angeona ishara na maajabu, na kama mwili wa kiroho wa Mungu ungemtokea mwanadamu, je watu wote hawangeweza “kuamini” katika Mungu? Nimesema hapo awali kuwa kikundi cha washindi wanapatwa kutoka Mashariki, washindi ambao wanatoka katika mashaka makubwa. Je maneno haya yana maana gani? Yanamaanisha kuwa watu hao ambao wamepatwa waliamini kwa kweli tu baada ya kupitia hukumu na kuadibu, na kushughulikiwa na kupogolewa, na aina yote ya usafishaji. Imani ya watu kama hao si isiyo dhahiri na dhahania, bali ni ya kweli. Hawajaona ishara na maajabu yoyote, ama miujiza yoyote; hawazungumzi kuhusu barua ngumu kueleweka na kanuni, ama mitazamo ya muhimu sana; badala yake, wana ukweli, na maneno ya Mungu, na maarifa ya kweli kuhusu ukweli wa Mungu. Je kikundi hiki hakina uwezo wa kuweka wazi nguvu za Mungu? Kazi ya Mungu katika siku za mwisho ni ya uhakika. Katika enzi ya Yesu, hakuja kumfanya mwanadamu awe kamili, ila kumkomboa mwanadamu, na hivyo Alionyesha miujiza kadhaa ili kufanya watu wamfuate. Kwani Yeye hasa Alikuja kukamilisha kazi ya kusulubiwa, na kuonyesha ishara haikuwa sehemu ya huduma Yake. Ishara na maajabu hayo yalikuwa ni kazi ambayo yalifanyika ili kufanya kazi Yake iwe na matokeo ya kufaa; hayo yalikuwa tu kazi ya ziada, na hayakuwakilisha kazi ya enzi nzima. Katika Enzi ya Sheria ya Agano la Kale, Mungu pia Alionyesha ishara na maajabu kadhaa—lakini kazi Anayofanya Mungu leo ni kazi halisi, na kwa uhakika hawezi kuonyesha ishara na maajabu sasa. Kama Angeonyesha ishara na maajabu, kazi Yake halisi ingevurugwa, na hangeweza kufanya kazi nyingine zaidi. Iwapo Mungu angesema neno litumiwe kumfanya mwanadamu kuwa kamili, lakini pia Aonyeshe ishara na maajabu, basi mwanadamu kumwamini ama kutomwamini kweli kungeweza kuwekwa wazi? Hivyo, Mungu hafanyi vitu vya aina hiyo. Kuna udini mwingi sana katika mwanadamu; Mungu amekuja katika nyakati za mwisho ili kutoa dhana zote za kidini na vitu visivyo vya kidunia ndani ya mwanadamu, na kumfanya mwanadamu ajue ukweli wa Mungu. Amekuja kutoa picha ya Mungu ambayo ni ya dhahania na bunifu—picha ya Mungu ambaye, kwa maneno mengine, hayupo hata kidogo. Na hivyo, sasa kitu cha pekee kilicho cha thamani ni wewe kuwa na ufahamu kuhusu hali halisi! Ukweli unashinda kila kitu. Unamiliki ukweli kiasi gani leo? Je, kila kitu kinachoonyesha ishara na maajabu ni Mungu? Roho wabaya pia wanaweza kuonyesha ishara na maajabu; je, hawa wote ni Mungu? Katika imani yake kwa Mungu, kile anachotafuta mwanadamu ni ukweli, anachotafuta ni uzima, na sio ishara na maajabu. Hivi ndivyo linavyopaswa kuwa lengo la wote wanaoamini katika Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 38)

Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole. Wokovu haukuwa na maana kuwa mwanadamu alikuwa amepatwa na Yesu kabisa, lakini ni kuwa mwanadamu hakuwa tena mwenye dhambi, na kuwa alikuwa amesamehewa dhambi zake; mradi tu uliamini, wewe kamwe hungekuwa mwenye dhambi. Wakati huo, Yesu alifanya kazi kubwa ambayo haikueleweka kwa wanafunzi Wake, na kusema mengi kwamba watu hawakuelewa. Hii ni kwa sababu, wakati huo, Hakutoa maelezo. Kwa hivyo, miaka kadhaa baada ya Yeye kuondoka, Mathayo aliunda kizazi chake, na wengine pia walifanya kazi kubwa ambayo ilikuwa ya mapenzi ya mwanadamu. Yesu hakuja kumkamilisha na kumpata mwanadamu, lakini kufanya awamu moja ya kazi: kuleta injili ya ufalme wa mbinguni na kukamilisha kazi ya kusulubiwa—na punde tu Yesu Aliposulubishwa, kazi Yake ilifika mwisho kamili. Lakini kwa awamu iliyoko sasa—kazi ya ushindi—maneno mengi zaidi lazima yasemwe, kazi nyingi zaidi lazima ifanywe, na lazima kuwe na hatua nyingi. Hivyo pia ni lazima siri za kazi ya Yesu na Yehova zitafichuliwa, ili wanadamu wote waweze kuwa na ufahamu na uwazi wa imani yao, kwa kuwa hii ni kazi ya siku za mwisho, na siku za mwisho ni mwisho wa kazi ya Mungu, wakati wa kuhitimisha kazi hii. Hii awamu ya kazi itakufafanulia sheria ya Yehova na ukombozi wa Yesu, na ni hasa ili uweze kuelewa kazi nzima ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na kuelewa umuhimu na kiini cha mpango huu wa usimamizi wa miaka elfu sita, na kuelewa kusudi la kazi zote Alizozifanya Yesu na maneno Aliyoyasema, na hata upofu wako wa imani kwenye na katika ibada ya Biblia. Yote haya yatakuwezesha kuelewa kabisa. Wewe utakuja kufahamu kazi anayoifanya Yesu na kazi ya Mungu leo; utaelewa na kushuhudia ukweli wote, uzima, na njia. Katika awamu ya kazi Aliyoifanya Yesu, kwa nini Yesu Aliondoka bila kufanya kazi ya ukamilishaji? Kwa sababu awamu ya kazi ya Yesu haikuwa kazi ya kukamilisha. Wakati Yeye Alisulubishwa msalabani, maneno Yake pia yalifika mwisho; baada ya kusulubiwa kwake, kazi Yake kwa hivyo ilimalizika. Awamu ya sasa ni tofauti. Ni baada tu ya maneno hayo kusemwa hadi mwisho na kazi nzima ya Mungu iwe imehitimika ndipo kazi yake itakapokuwa imemalizika. Wakati wa awamu ya kazi ya Yesu, kulikuwa na maneno mengi yaliyobakia bila kusemwa, au ambayo hayakuwa yameelezwa kikamilifu kwa ufasaha. Waama, Yesu hakujali Alichosema au kile ambacho hakusema, kwa kuwa huduma yake haikuwa huduma ya maneno; na hivyo baada ya Yeye kusulubishwa msalabani Aliondoka. Awamu hiyo ilikuwa hasa kwa ajili ya kusulubiwa, na ni tofauti na awamu ya sasa. Awamu ya kazi hii ni hasa kwa ajili ya kukamilisha, kufumbua, na kuleta kazi yote kwenye hitimisho. Kama maneno hayasemwi hadi tamati yake kabisa, hakutakuwa na mbinu ya kuhitimisha kazi hii, kwa kuwa awamu hii ya kazi yote inafikishwa mwisho na kukamilika kwa kutumia maneno. Wakati huo, Yesu Alifanya kazi kubwa isiyoeleweka na mwanadamu. Akaondoka kimyakimya, na leo bado kunao wengi wasioelewa maneno Yake, ambao ufahamu wao ni potofu lakini bado unaaminika nao kwamba ni sahihi, ambao hawajui kuwa wao si sahihi. Mwishoni, awamu hii ya sasa itafikisha kazi ya Mungu mwisho ulio kamilifu, na kutoa hitimisho Lake. Wote watakuja kufahamu na kujua mpango wa usimamizi wa Mungu. Dhana zilizo ndani ya mwanadamu, nia yake, fahamu yake potofu, dhana zake kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, maoni yake kuhusu watu wa Mataifa mengine na michepuko yake ingine na makosa yake yatarekebishwa. Na mwanadamu ataelewa njia yote ya haki ya uzima, na kazi yote anayofanya Mungu, na ukweli wote. Wakati hayo yatafanyika, awamu hii ya kazi itafikia kikomo. Kazi ya Yehova ilikuwa uumbaji wa ulimwengu, ilikuwa mwanzo; awamu hii ya kazi ni mwisho wa kazi, na ni hitimisho. Hapo mwanzo, kazi ya Mungu ilifanyika miongoni mwa wateule wa Israeli, na ilikuwa mapambazuko ya kipindi kipya katika pahali patakatifu zaidi ya popote. Awamu ya mwisho ya kazi inafanywa katika nchi ambayo ni chafu zaidi ya zote, kuhukumu ulimwengu na kuleta enzi kwenye kikomo. Katika awamu ya kwanza kazi ya Mungu ilifanyika katika maeneo yenye kung’aa kuliko maeneo yote, na awamu ya mwisho inafanyika katika maeneo yaliyo katika giza kuliko maeneo yote, na giza hili litaondolewa, na mwanga kufunguliwa, na watu wote kushindwa. Wakati watu wa maeneo haya yaliyo chafu kuliko yote na yaliyo na giza watakuwa wameshindwa na idadi yote ya watu wametambua kuwa Mungu yupo, na ya kuwa ni Mungu wa kweli, na kila mtu Amemwamini kabisa, basi ukweli huu utatumika kutekeleza kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima. Awamu hii ya kazi ni ya ishara: Punde tu kazi ya kipindi hiki itakapomalizika, kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi itafikia mwisho kabisa. Mara baada ya wale walioko katika maeneo yaliyo na giza kuliko yote watakapokuwa wameshindwa, bila shaka itakuwa hivyo pia kila mahali pengine. Kwa hivyo, kazi ya ushindi tu katika China inabeba ishara ya maana. China inajumuisha nguvu zote za giza, na watu wa China wanawakilisha wale wote ambao ni wa mwili, wa Shetani, na wa mwili na damu. Ni watu wa China ndio wamepotoshwa sana na joka kubwa jekundu, ambao wana upinzani wenye nguvu dhidi ya Mungu, ambao wana ubinadamu ulio mbovu zaidi na ulio mchafu, na kwa hivyo hao ni umbo asili la wanadamu wote wenye matendo maovu. Hii si kusema kwamba nchi nyingine hazina shida kabisa; dhana za mwanadamu ni sawa zote, na ingawa watu wa nchi hizi wanaweza kuwa na uhodari mzuri, ikiwa hawamjui Mungu, basi ni lazima iwe kwamba wanampinga. Kwa nini Wayahudi pia walimpinga na kumwasi Mungu? Kwa nini Mafarisayo pia walimpinga? Kwa nini Yuda alimsaliti Yesu? Wakati huo, wengi wa wanafunzi hawakumjua Yesu. Kwa nini, baada ya Yesu kusulubiwa na kufufuliwa tena, watu bado hawakumwamini? Je, uasi wa mwanadamu sio sawa wote? Ni tu kwamba watu wa China wamefanyika mfano, na watakaposhindwa watakuwa mfano na kielelezo, na watatumika kama kumbukumbu kwa wengine. Kwa nini mimi daima Nimesema yakuwa nyinyi ni kiungo cha mpango wangu wa usimamizi? Ni katika watu wa China ambapo upotovu, uchafu, udhalimu, upinzani, na uasi unadhihirishwa kikamilifu zaidi na kufichuliwa kwa hali zao mbalimbali. Kwa upande mmoja, wao ni wa kimo cha umaskini, na kwa upande mwingine, maisha yao na mawazo yao ni ya nyuma kimaendeleo, na tabia zao, mazingira ya kijamii, familia ya kuzaliwa—yote ni ya umaskini na ya nyuma kimaendeleo kuliko yote. Hadhi yao, pia, ni ya chini. Kazi katika eneo hili ni ya ishara, na baada ya kazi hii ya majaribio hufanywa kwa ukamilifu wake, na kazi yake inayofuata itakwenda vizuri zaidi. Kama awamu hii ya kazi inaweza kukamilika, basi kazi inayofuata itakamilika bila shaka. Mara baada ya awamu ya kazi hii kutimizwa, na mafanikio makubwa kufikiwa kikamilifu, kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima itakua imefikia kikomo kamili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 39)

Enzi ya Neema ilianza na Jina la Yesu. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu. Ushuhuda wa wale waliomwamini Yeye ulitolewa kwa ajili ya Yesu Kristo, na kazi waliyoifanya walifanya pia kwa ajili ya Yesu Kristo. Hitimisho Enzi ya Sheria ya Agano la Kale lilimaanisha kuwa kazi iliyofanywa hasa kutumia jina la Yehova ilikuwa imefikia kikomo. Baada ya hii, jina la Mungu halikuwa Yehova tena; badala yake Yeye Aliitwa Yesu, na kutoka hapa Roho Mtakatifu Alianza kazi hasa kwa kutumia jina la Yesu. Kwa hiyo leo, watu ambao leo bado hula na kunywa maneno ya Yehova, na bado hutumia kazi ya Enzi ya Sheria—je, hufuati masharti bila kufikiria? Je! Hujakwama katika siku za zamani? Leo, unajua kwamba siku za mwisho zimefika. Wakati Yesu atakapokuja, bado Ataitwa Yesu? Yehova aliwaambia watu wa Israeli kwamba Masihi angekuja, lakini alipofika, hakuitwa Masihi bali Yesu. Yesu alisema kwamba Angekuja tena, na kwamba Angekuja kama Alivyoondoka. Haya yalikuwa maneno ya Yesu, lakini je, ulishuhudia jinsi Yesu alivyoondoka? Yesu aliondoka akiwa juu ya wingu jeupe, lakini je, Yeye Mwenyewe angerudi kati ya binadamu juu ya wingu jeupe? Ingekuwa hivyo, je, si bado angeitwa Yesu? Wakati Yesu Atakuja tena, enzi itakuwa tayari imebadilika, je, hivyo bado Ataweza kuitwa Yesu? Je, Mungu Anajulikana tu kwa jina la Yesu? Je, hangeweza kuitwa kwa jina jipya katika enzi mpya? Je, sura ya mtu mmoja na hasa jina moja vinaweza kumwakilisha Mungu katika ukamilifu wake? Katika kila enzi, Mungu Anafanya kazi mpya na huitwa kwa jina jipya; Je, anawezaje kufanya kazi sawa katika enzi tofauti? Itakuwaje Yeye kugandamana na yale ya zamani? Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi? Ni kwa nini Yehova na Yesu ni kitu kimoja, ilhali wanaitwa kwa majina tofauti katika enzi hizi tofauti? Je, si kwa sababu enzi za kazi Yao ni tofauti? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake? Kwa njia hii, lazima Mungu aitwe kwa jina tofauti katika enzi tofauti, lazima Atumie jina kubadilisha enzi na kuwakilisha hiyo enzi, kwa kuwa hakuna jina moja linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe kikamilifu. Na kila jina linaweza tu kuwakilisha kipengele cha wakati cha tabia ya Mungu katika enzi fulani; yote linahitaji kufanya ni kuwakilisha kazi Yake. Kwa hivyo, Mungu Anaweza kuchagua jina lolote ambalo linafaa tabia yake kuwakilisha enzi nzima. Bila kujali iwapo ni enzi ya Yehova, au ni enzi ya Yesu, kila enzi inawakilishwa kwa jina. Baada ya Enzi ya Neema, enzi ya mwisho imewadia na Yesu Amekwisha kuja. Itakuwaje awe bado anaitwa Yesu? Itakuwaje awe bado anachukua umbo la Yesu miongoni mwa watu? Je, umesahau kuwa Yesu Alikuwa tu sura ya Mnazareti? Je, umesahau kuwa Yesu Alikuwa tu mkombozi wa wanadamu? Itakuwaje achukue kazi ya kushinda na kurekebisha mwanadamu katika siku za mwisho? Yesu aliondoka akiwa juu ya wingu jeupe, huu ni ukweli, lakini Angewezaje kurudi juu ya wingu jeupe kati ya wanadamu na bado aitwe Yesu? Ikiwa Yeye kweli alikuja juu ya wingu, si Angetambuliwa na mwanadamu? Je, si watu ulimwenguni kote wangemtambua Yeye? Katika hali hiyo, je, si Yesu peke Yake ndiye angekuwa Mungu? Katika hali hiyo, sura ya Mungu ingekuwa ni sura ya Myahudi, na ingekuwa vilevile milele. Yesu alisema kwamba Angewasili kama Alivyoondoka, lakini unajua maana halisi ya maneno Yake? Je, angeweza kwa kweli kuwaambia ninyi kundi la watu? Unajua tu kwamba Atawasili kama Alivyoondoka juu ya wingu, lakini unajua hasa jinsi Mungu Mwenyewe hufanya kazi Yake? Ikiwa ungeweza kuona kweli, basi maneno ya Yesu yanapaswa kuelezwa vipi? Alisema: Wakati Mwana wa Adamu atakapokuja katika siku za mwisho, Yeye Mwenyewe hatajua, malaika hawatajua, wajumbe wa mbinguni hawatajua, na watu wote hawatajua. Baba tu ndiye atakayejua, yaani, Roho pekee ndiye atajua Hata Mwana wa Adamu Mwenyewe hajui, lakini wewe unaweza kuona na kujua? Ikiwa ungekuwa na uwezo wa kujua na kuona kwa macho yako mwenyewe, je, si maneno haya yatakuwa yalisemwa bure? Na Yesu alisema nini wakati huo? “Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua, wala malaika wa mbinguni, isipokuwa Baba yangu tu. Lakini kama jinsi zilivyokuwa zile siku za Nuhu, ndivyo pia kuja kwa Mwana wa Adamu kutakuwa. … Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu.” Wakati siku hiyo itakapofika, Mwana wa Adamu Mwenyewe hataijua. Mwana wa Adamu inahusu umbo la Mungu lililopata mwili wa Mungu, ambaye atakuwa mtu wa kawaida. Hata Mwana wa Adamu mwenyewe hajui, kwa hiyo wewe ungejuaje? Yesu alisema kwamba Angewasili kama Alivyoondoka. Wakati Atakapowasili, hata Yeye Mwenyewe hajui, kwa hiyo Angekujulisha mapema? Je, unaweza kuona kuwasili kwake? Je, huo sio utani?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 40)

Kila wakati ambao Mungu Atawasili hapa duniani, Yeye Atabadilisha jina lake, jinsia yake, mfano wake, na kazi yake; Yeye harudii kazi yake, na Yeye daima yu mpya na kamwe si wa zamani. Wakati Alikuja hapo awali, Aliitwa Yesu; Je, anaweza bado kuitwa Yesu anapokuja tena wakati huu? Alipokuja hapo awali, Alikuwa wa kiume, Ataweza kuwa wa kiume tena wakati huu? Kazi Yake Alipokuja wakati wa Enzi ya Neema ilikuwa ya kusulubishwa msalabani; Atakapokuja tena, je, bado Atawakomboa wanadamu kutoka kwenye dhambi? Je, bado Atasulubishwa msalabani? Je, huko hakutakuwa kurudia kazi Yake? Je, hukujua kwamba Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani? Kuna wale ambao wanasema kuwa Mungu habadiliki. Hiyo ni sahihi, lakini inaashiria kutobadilika kwa tabia ya Mungu na kiini Chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika. Iwapo utasema kuwa kazi ya Mungu daima inabaki vile vile, basi Angekuwa na uwezo wa kumaliza mpango wake wa usimamizi wa miaka elfu sita? Wewe hujua tu kwamba Mungu habadiliki milele, lakini je, unajua kuwa Mungu ni mpya milele na kamwe si wa zamani? Kama kazi ya Mungu kamwe haikubadilika, basi Angeweza kulea mwanadamu hadi leo? Kama Mungu habadiliki, basi mbona Yeye tayari Amefanya kazi ya nyakati mbili? Kazi yake daima inaendelea mbele, na hivyo pia ndivyo tabia yake inafichuliwa kwa binadamu hatua kwa hatua, na kile ambacho kinafichuliwa ni tabia yake ya asilia. Hapo mwanzo, tabia ya Mungu ilikuwa siri kwa mwanadamu, na kamwe Yeye hadharani hakumfichulia mwanadamu tabia yake, na mwanadamu hakuwa na ufahamu kuhusu Yeye, na hivyo hatua kwa hatua Alitumia kazi Yake kumfichulia mwanadamu tabia Yake, lakini hii haina maana kuwa tabia Yake inabadilika katika kila enzi. Sio kweli kuwa tabia ya Mungu kila wakati inabadilika kwa ajili mapenzi Yake daima hubadilika. Bali, kwa kuwa enzi za kazi Yake ni tofauti, asili ya tabia Yake kwa ujumla hufichuliwa kwa binadamu hatua kwa hatua, ili mwanadamu aweze kumjua Yeye. Lakini hii si kwa njia yoyote ushahidi kuwa Mungu hapo awali hakuwa na tabia fulani na tabia Yake imebadilika hatua kwa hatua kwenye enzi zinazopita—ufahamu kama huo ni wenye kosa. Mungu humfichulia mwanadamu tabia yake fulani ya asili, kile Alicho, kwa mujibu wa enzi zinazopita. Kazi ya enzi moja haiwezi kueleza tabia nzima ya Mungu. Na kwa hivyo, maneno haya “Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani” yanarejelea kazi yake, na maneno haya “Mungu habadiliki” kinarejelea kile ambacho Mungu anacho na alicho kiasili. Bila kujali, huwezi kubaini kazi ya miaka elfu sita kwa mtazamo mmoja, ama kwa kuielezea tu kwa maneno ambayo hayabadiliki. Huo ni ujinga wa mwanadamu. Mungu si wazi kama mwanadamu anavyofikiria, na kazi yake haitasimama katika enzi moja. Yehova, kwa mfano, haliwezi daima kusimamia jina la Mungu; Mungu pia hufanya kazi yake kwa kutumia Jina la Yesu, ambayo ni ishara ya vile ambavyo kazi ya Mungu daima husonga kwenda mbele.

Mungu siku zote huwa Mungu, na kamwe Yeye hatakuwa Shetani; Shetani daima ni Shetani, na yeye hawezi kuwa Mungu. Hekima ya Mungu, ajabu ya Mungu, haki ya Mungu, na adhama ya Mungu kamwe hayatabadilika. Kiini chake na anachomiliki na kile Anacho na alicho kamwe hakitabadilika. Kazi yake, hata hivyo, daima inaendelea mbele, daima inaenda ndani zaidi, kwa kuwa Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani. Katika kila enzi Mungu huchukua jina jipya, katika kila enzi anafanya kazi mpya, na katika kila enzi Yeye huwaruhusu viumbe Wake kuona mapenzi Yake mapya na tabia Yake mpya. Ikiwa watu hawaoni dhihirisho la tabia mpya ya Mungu katika enzi mpya, wao si watamsulubisha msalabani milele? Na kwa kufanya hivyo, si watakuwa wamebaini Mungu? Ikiwa Angepata mwili tu kama mume, watu wangemfafanua kama mume, kama Mungu wa wanaume, na kamwe hawangemwamini kuwa Mungu wa wanawake. Kisha, wanaume wangeamini kwamba Mungu ni wa jinsia sawa na wanaume, kwamba Mungu ni kichwa cha wanaume na je, wanawake? Hii si haki; je, huu sio utendeaji wa upendeleo? Ikiwa ingekuwa hivi, basi wale wote ambao Mungu aliwaokoa wangekuwa wanaume kama Yeye, na hakungekuwa na wokovu wa wanawake. Wakati ambapo Mungu aliumba wanadamu, Alimuumba Adamu na Akamuumba Hawa. Hakumuumba tu Adamu, lakini Aliwafanya wote mume na mke kwa mfano Wake. Mungu sio tu Mungu wa wanaume—Yeye pia ni Mungu wa wanawake. Mungu anafanya kazi mpya katika siku za mwisho. Atafichua tabia Yake zaidi, na haitakuwa huruma na upendo wa wakati wa Yesu. Kwa kuwa Ana kazi mpya, kazi hii mpya itaandamana na tabia mpya. Kwa hiyo kama kazi hii ingefanywa na Roho—kama Mungu hangepata mwili, na badala yake Roho angenena moja kwa moja kupitia radi ili mwanadamu hangekuwa na njia ya kuwasiliana na Yeye, je, mwanadamu angejua tabia yake? Kama Roho tu Angefanya kazi, basi mtu hangekuwa na njia yoyote ya kujua tabia Yake. Watu wanaweza tu kuona tabia ya Mungu kwa macho yao wenyewe wakati Anapopata mwili, wakati ambapo Neno laonekana katika mwili, na Anaonyesha tabia Yake yote kupitia mwili. Mungu kweli huishi kati ya wanadamu. Anaonekana; mwanadamu anaweza kweli kujihusisha na tabia Yake na kile Anacho na Alicho; ni kwa njia hii tu ndiyo mwanadamu anaweza kumjua kweli. Wakati huo huo, Mungu pia Amekamilisha kazi ya Mungu kuwa Mungu wa wanaume na wanawake, na Ametimiza ukamilifu wa kazi Yake katika mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 41)

Kazi ya Mungu kokote katika usimamizi wake ni wazi kabisa: Enzi ya Neema ni Enzi ya Neema, na siku za mwisho ni siku za mwisho. Kuna tofauti baina ya kila enzi, kwa kuwa katika kila enzi Mungu Anafanya kazi ambayo inawakilisha enzi hiyo. Ili kazi ya siku za mwisho iweze kufanywa, lazima kuwe na kuungua, hukumu, kuadibu, ghadhabu, na uharibifu wa kuleta enzi kwenye kikomo. Siku za mwisho zinaashiria enzi ya mwisho. Wakati wa enzi ya mwisho, je, Mungu si Ataleta enzi kwenye kikomo? Na ni kwa njia tu ya kuadibu na hukumu ndio inaweza kuleta enzi kwenye kikomo. Ni kwa njia hii tu ndiyo Anaweza kuitamatisha enzi hiyo. Madhumuni ya Yesu yalikuwa kwamba mwanadamu aweze kuendelea kuwepo, kuishi, na kuweza kuwepo kwa njia bora zaidi. Alimwokoa mwanadamu kutoka kwa dhambi ili mwanadamu akome upotovu wa kudumu na kamwe asiishi katika Kuzimu na jehanamu, na kwa kumwokoa mwanadamu kutoka kwa Kuzimu na jehanamu, Yesu alimwezesha mwanadamu kuendelea kuishi. Sasa, siku za mwisho zimewadia. Mungu atamwangamiza mwanadamu, Atamharibu mwanadamu kabisa, ambayo ina maana kuwa Atageuza uasi wa binadamu. Kwa hivyo, huruma ya Mungu na tabia yake ya hapo zamani ya kupenda haitakuwa na uwezo wa kuhitimisha enzi hiyo, na haitakuwa na uwezo wa kukamilisha usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita. Kila enzi inaonyesha uwakilishi maalum wa tabia ya Mungu, na kila enzi ina kazi ambayo inafaa kufanywa na Mungu. Kwa hivyo, kazi iliyofanywa na Mungu mwenyewe kwa kila enzi ina dhihirisho la tabia Yake ya ukweli, na jina Lake na kazi anaofanya hubadilika na enzi—zote ni mpya. Wakati wa Enzi ya Sheria, kazi ya kumwelekeza mwanadamu ilifanyika katika Jina la Yehova, na awamu ya kwanza ya kazi ilifanyika duniani. Kazi ya awamu hii ilikuwa ni kujenga hekalu na madhabahu, na kutumia sheria kuwaongoza watu wa Israeli na kufanya kazi miongoni mwao. Kwa kuongoza watu wa Israeli, Alizindua kituo cha kazi Yake hapa duniani. Kwa msingi huu, Yeye Alipanua kazi yake nje ya Israeli, ambayo ni kusema kwamba, kuanzia Israeli, Aliendeleza kazi yake nje, ili vizazi vya baadaye walikuja kujua polepole kwamba Yehova Alikuwa Mungu, na kuwa Yehova Alikuwa Ameumba mbingu na nchi na vitu vyote, Alitengeneza viumbe vyote. Yeye Alieneza kazi yake kupitia kwa watu wa Israeli. Nchi ya Israeli ilikuwa ya mahali takatifu pa kwanza pa kazi ya Yehova hapa duniani, na kazi ya Mungu ya hapo mwanzoni ilikuwa kote katika nchi ya Israeli. Hiyo ilikuwa kazi ya Enzi ya Sheria. Wakati wa Enzi ya Neema, Yesu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu. Alichokuwa nacho na Aliyekuwa ni neema, upendo, huruma, uvumilivu, subira, unyenyekevu, huduma, na stahamala, na nyingi ya kazi ambayo Alifanya ilikuwa kwa ajili ya kumwokoa mwanadamu. Tabia Yake ilikuwa ya huruma na upendo, na kwa sababu Yeye Alikuwa na huruma na upendo, ilikuwa sharti asulubishwe msalabani kwa ajili ya mwanadamu, ili kuonyesha kwamba Mungu Alimpenda mwanadamu jinsi anavyojipenda, kwa kiasi kwamba Yeye mwenyewe Alijitoa kama kafara na kwa ukamilifu Wake. Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu, ambalo lina maana kuwa Mungu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu, na ya kwamba Alikuwa Mungu wa rehema na wa upendo. Mungu Alikuwa na mwanadamu. Upendo wake, huruma yake, na wokovu wake uliandamana na kila mtu. Mwanadamu angeweza tu kupata amani na furaha, kupokea baraka zake, kupokea neema yake kubwa na nyingi, na kupokea wokovu wake iwapo mwanadamu angekubali jina lake na akubali uwepo wake. Kupitia kusulubiwa kwa Yesu, wale wote ambao walimfuata Yeye walipokea wokovu na walisamehewa dhambi zao. Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu. Kwa maneno mengine, kazi ya Enzi ya Neema ilifanywa hasa katika Jina la Yesu. Wakati wa Enzi ya Neema, Mungu Aliitwa Yesu. Yeye Alifanya kazi mpya zaidi ya Agano la Kale, na kazi yake ilimalizika kwa kusulubiwa, na ya kwamba huo ulikuwa ukamilifu wa kazi yake. Kwa hivyo, wakati wa Enzi ya Sheria Yehova ndilo lilikuwa jina la Mungu, na katika Enzi ya Neema jina la Yesu lilimwakilisha Mungu. Katika siku za mwisho, jina lake ni Mwenyezi Mungu—mwenye uweza, na yeye hutumia nguvu zake kumwongoza mwanadamu, kumshinda mwanadamu, kumtwaa mwanadamu, na mwishowe, kuhitimisha enzi hiyo. Katika kila enzi, katika awamu yote ya kazi yake, tabia ya Mungu ni dhahiri.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 42)

Je, Jina la Yesu—“Mungu pamoja nasi,”—linaweza kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake? Je, linaweza kueleza Mungu kwa ukamilifu? Kama mwanadamu atasema ya kwamba Mungu Ataitwa tu Yesu, na hawezi kuwa na jina lingine kwa sababu Mungu hawezi kubadilisha tabia yake, basi maneno hayo ni kufuru! Je, unaamini kwamba jina la Yesu, Mungu pamoja nasi, linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu? Mungu Anaweza kuitwa majina mengi, lakini baina ya majina haya mengi, hamna moja ambalo linaweza kujumlisha yote ambayo Mungu Anamiliki, na hamna jina moja ambalo linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu. Na hivyo Mungu Ana majina mengi, lakini majina haya mengi hayawezi kuelezea tabia ya Mungu kikamilifu, kwa kuwa tabia ya Mungu ni tajiri sana, na yanazidi uwezo wa mwanadamu kumjua Yeye. Lugha ya mwanadamu haina uwezo wa kumfafanua Mungu kwa ukamilifu. Mwanadamu ana msamiati finyu tu ambao anaweza kufafanua yote anayojua kuhusu tabia ya Mungu: kubwa, yenye heshima, ya ajabu, isiyoeleweka, kuu, takatifu, yenye haki, yenye hekima, na kadhalika. Maneno mengi sana! Msamiati kama huo finyu hauwezi kuelezea kile kidogo mtu ameshuhudia juu ya tabia ya Mungu. Baadaye, watu wengi waliongeza maneno zaidi ili kueleza vizuri zaidi ari ndani ya mioyo yao: Mungu ni mkuu sana! Mungu ni mtakatifu sana! Mungu ni wa kupendeza sana! Leo, maneno kama haya yamefikia kilele chake, lakini bado mwanadamu hawezi kujieleza wazi wazi. Na kwa hiyo, kwa mwanadamu, Mungu ana majina mengi, lakini Hana jina moja, na hilo ni kwa sababu nafsi ya Mungu ni ya ukarimu sana, na lugha ya mwanadamu haitoshi sana. Neno au jina moja maalum halina uwezo wa kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake. Kwa hivyo, je, Mungu Anaweza kuchukua jina moja lisilobadilika? Mungu ni mkuu sana na mtakatifu sana, kwa hivyo mbona wewe huwezi kumruhusu Yeye abadili jina Lake katika kila enzi mpya? Kwa hivyo, katika kila enzi ambayo Mungu binafsi hufanya kazi yake mwenyewe, Yeye hutumia jina ambalo linafaa enzi hiyo ili kujumlisha kazi ambayo anaifanya. Yeye hutumia hili jina haswa, ambalo linamiliki umuhimu wa wakati, kuwakilisha tabia yake katika enzi hiyo. Mungu hutumia lugha ya mwanadamu kuelezea tabia yake mwenyewe. Hata hivyo, watu wengi ambao wamepata uzoefu wa kiroho na wamemuona Mungu binafsi bado wanahisi kuwa jina moja maalumu haliwezi kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake—ole wetu, hili linasikitisha, hivyo mwanadamu hamwiti Mungu kwa jina lolote, lakini humwita tu “Mungu.” Moyo wa mwanadamu unaonekana kujawa na upendo, lakini pia unaonekana kuzongwa na ukinzani, kwa maana mwanadamu hajui jinsi ya kumueleza Mungu. Kile Mungu alicho ni cha ukarimu sana kiasi kwamba hakuna kabisa njia ya kukieleza. Hakuna jina moja ambalo linaweza kutoa muhtasari wa tabia Ya Mungu, na hakuna jina moja ambalo linaweza kuelezea yote ambayo Mungu anacho na Alicho. Kama mtu ataniuliza, “Ni jina gani hasa unalotumia?” Nitamwambia, “Mungu ni Mungu!” Je, hilo silo jina bora zaidi la Mungu? Je, huko sio kufafanua bora zaidi kuhusu tabia ya Mungu? Hali ikiwa hivi, kwa nini mnatumia juhudi nyingi sana kutafuta jina la Mungu? Kwa nini ufikirie sana, kukaa bila kula na kulala, kwa ajili ya jina? Siku itawadia ambapo Mungu hataitwa Yehova, Yesu, au Masihi—Yeye Ataitwa tu Muumba. Wakati huo, majina yote ambayo Alichukua hapa duniani yatafikia kikomo, kwa kuwa kazi yake hapa duniani itakuwa imefika mwisho, na baada ya hapo Mungu hatakuwa na jina. Wakati mambo yote yatakuja kuwa chini ya utawala wa Muumba, kwa nini umwite kwa jina sahihi ila bado halijakamilika? Je, bado unatafuta jina la Mungu sasa? Je, bado unathubutu kusema kuwa Mungu Anaitwa tu Yehova? Je, bado unathubutu kusema kuwa Mungu Anaweza tu kuitwa Yesu? Je, unaweza kubeba dhambi ya kumkufuru Mungu? Unapaswa kujua kuwa Mungu mwanzoni hakuwa na jina. Yeye Alichukua tu jina moja, au majina mawili, ama majina mengi kwa sababu Alikuwa na kazi ya kufanya na Alikuwa na jukumu la kumsimamia mwanadamu. Jina lolote ambalo anaitwa Yeye, je, si lile analolichagua kwa hiari yake? Je, Yeye atakuhitaji wewe, mmoja wa viumbe wake Wake, kuliamua? Jina ambalo Mungu Anaitwa ni kwa mujibu wa kile ambacho mwanadamu anaweza kufahamu na lugha ya mwanadamu, lakini hili jina haliwezi kujumlishwa na mwanadamu. Wewe unaweza kusema tu kuwa mbinguni kuna Mungu, ya kwamba Yeye anaitwa Mungu, na kwamba Yeye mwenyewe ni Mungu mwenye nguvu nyingi, busara tele, wakuinuliwa sana, wa ajabu kuu, mwenye siri kuu, mwenye uweza mkuu sana, na huwezi kusema mengi zaidi; hayo ndiyo yote unayoyajua. Kwa njia hii, je, jina la Yesu tu linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe? Wakati siku za mwisho zitawadia, ingawa ni Mungu ndiye anafanya kazi yake, ni sharti jina lake libadilike, kwa kuwa ni enzi tofauti.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 43)

Wakati Yesu Alikuja kufanya kazi yake, ilikuwa ni kwa uongozi wa Roho Mtakatifu; Yeye Alitenda vile ambavyo Roho Mtakatifu Alitaka, na haikuwa kwa mujibu wa Enzi ya sheria ya Agano la Kale ama kwa mujibu wa kazi ya Yehova. Ingawa kazi ambayo Yesu Alikuja kufanya haikuambatana na sheria za Yehova ama amri za Yehova, chanzo chao kilikuwa sawa. Kazi ambayo Yesu Alifanya iliwakilisha jina la Yesu, na iliwakilisha Enzi ya Neema; kazi iliyofanywa na Yehova, iliwakilisha Yehova, na iliwakilisha Enzi ya Sheria. Kazi yao ilikuwa kazi ya Roho mmoja katika enzi tofauti. Kazi ambayo Yesu Alifanya ingeweza tu kuwakilisha Enzi ya Neema, na kazi ambayo Yehova Alifanya ingeweza tu kuwakilisha Enzi ya Sheria ya Agano la Kale. Yehova Aliwaongoza tu watu wa Israeli na Misri, na mataifa yote nje ya Israeli. Kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema ya Agano Jipya ilikuwa kazi ya Mungu katika jina la Yesu kwa kuwa Yesu ndiye Aliongoza enzi hii. Iwapo utasema kuwa kazi ya Yesu ilikuwa kwa msingi wa kazi ya Yehova, na kuwa hakufanya kazi yoyote mpya, na kuwa yote Aliyofanya ilikuwa kwa mujibu wa maneno ya Yehova, kulingana na kazi ya Yehova na unabii wa Isaya, basi Yesu hakuwa Mungu Aliyekuwa katika mwili. Kama Alitekeleza kazi yake kwa njia hii, basi Yeye Alikuwa mtume au mfanyikazi wa Enzi ya Sheria. Iwapo ni kama unavyosema, basi Yesu hangeweza kuzindua enzi, wala hangeweza kufanya kazi nyingine. Kwa njia hiyo hiyo, Roho Mtakatifu ni sharti afanye kazi Yake hasa kupitia kwa Yehova, na isipokuwa kupitia kwa Yehova Roho Mtakatifu hangeweza kufanya kazi yoyote mpya. Mwanadamu amekosea kwa kuona kazi ya Yesu kwa njia hii. Kama mwanadamu anaamini kwamba kazi iliyofanywa na Yesu ilifanywa inaambatana na maneno ya Yehova na unabii wa Isaya, basi, je, Yesu Alikuwa Mungu Aliyepata mwili, au Yeye Alikuwa nabii? Kwa mujibu wa mtazamo huu, hakukuwa na Enzi ya Neema, na Yesu hakuwa Mungu Aliyepata mwili, kwa kuwa kazi ambayo Alifanya haingeweza kuwakilisha Enzi ya Neema na ingewakilisha tu Enzi ya Sheria ya Agano la Kale. Kungekuwepo tu na enzi mpya wakati Yesu Alikuja kufanya kazi mpya, Alipozindua enzi mpya, na kupenya katika kazi iliyokuwa imefanyika hapo awali katika nchi ya Israeli, na hakufanya kazi yake kwa mujibu wa kazi iliyofanywa na Yehova huko Israeli, hakuzingatia sheria Yake ya zamani, na hakufuata kanuni zozote, na Alifanya kazi mpya ambayo Alitakiwa kufanya. Mungu Mwenyewe anakuja kuzindua enzi, na Mungu mwenyewe huja kuleta enzi kwenye kikomo. Mwanadamu hana uwezo wa kufanya kazi ya kuanzisha enzi hiyo na kuhitimisha enzi. Kama Yesu hakuleta kazi ya Yehova kwenye kikomo baada ya Yeye kuja, basi hio inadhihirisha ya kwamba Yeye Alikuwa tu mwanadamu, na hakuwakilisha Mungu. Kwa usahihi kwa sababu Yesu Alikuja na kuhitimisha kazi ya Yehova, Akaendeleza kazi ya Yehova na, aidha, Akatekeleza kazi Yake, kazi mpya, inathibitisha kuwa hii ilikuwa enzi mpya, na kwamba Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe. Walifanya kazi katika awamu mbili zinazotofautiana. Awamu moja ilifanyika katika hekalu, na hiyo nyingine ilifanyika nje ya hekalu. Awamu moja ilikuwa ya kuongoza maisha ya mwanadamu kwa mujibu wa sheria, na awamu nyingine ilikuwa ya kutoa kafara ya dhambi. Awamu hizi mbili za kazi bila shaka zilikuwa tofauti; huu ni mgawanyiko wa enzi ya zamani na enzi mpya, na hakuna kosa kusema kuwa hizo ni enzi mbili! Maeneo ya kazi yao yalikuwa tofauti, na kiini cha kazi yao kilikuwa tofauti, na lengo la kazi yao lilikuwa tofauti. Kwa hivyo, enzi hizi zinaweza kugawanywa kwa awamu mbili: Agano la Kale na Jipya, ambayo ni kusema, enzi mpya na ya zamani. Yesu alipokuja hakuenda katika hekalu, ambayo inathibitisha kwamba enzi ya Yehova ilikuwa imeisha. Hakuingia hekaluni kwa sababu kazi ya Yehova katika hekalu ilikuwa imekamilika, na haikuhitajika kufanywa tena, na kwa hiyo kuifanya tena kungekuwa kuirudia. Kwa kuondoka tu hekaluni, kuanza kazi mpya na kuzindua njia mpya nje ya hekalu, ndio Aliweza kuifikisha kazi ya Mungu kwa upeo wake. Kama Hangeenda nje ya hekalu kufanya kazi Yake, kazi ya Mungu haingeweza kamwe kuendelea mbele kupita hekalu, na hakungekuwa na mabadiliko yoyote mapya. Na kwa hiyo, Yesu Alipokuja, Hakuingia hekaluni, na Hakufanya kazi Yake hekaluni. Alifanya kazi Yake nje ya hekalu, na Akafanya kazi Yake kwa uhuru Akiandamana na wanafunzi. Kuondoka kwa Mungu katika hekalu kufanya kazi Yake kulikuwa na maana kwamba Mungu alikuwa na mpango mpya. Kazi Yake ilikuwa ifanyike nje ya hekalu, na ilikuwa iwe kazi mpya ambayo haingezuiliwa kwa njia ya utekelezaji wake. Kuwasili kwa Yesu kulimaliza kazi ya Yehova ya wakati wa Agano la Kale. Ingawa ziliitwa kwa majina mawili tofauti, awamu zote mbili za kazi zilifanywa na Roho mmoja, na kazi ya pili ilikuwa mwendelezo wa kazi ya kwanza. Kwa kuwa jina lilikuwa tofauti, na kiini cha kazi kilikuwa tofauti, basi enzi ilikuwa tofauti. Wakati Yehova Alikuja, hiyo ilikuwa enzi ya Yehova, na wakati Yesu Alikuja, hiyo ilikuwa enzi ya Yesu. Na kwa hivyo, kila wakati Mungu Anapokuja, anaitwa kwa jina moja, Yeye anawakilisha enzi moja, na Yeye anazindua njia mpya; na kwa kila njia mpya, Yeye huchukua jina jipya, ambalo inaonyesha kuwa Mungu daima ni mpya na wala si wa zamani, na ya kwamba kazi yake daima inasonga mbele. Historia inasonga mbele daima, na kazi ya Mungu inasonga mbele daima. Ili mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita ufike upeo wake, lazima uendelee kusonga mbele. Kila siku ni sharti Yeye afanye kazi mpya, kila mwaka lazima Yeye afanye kazi mpya, ni sharti Yeye azindue njia mpya, azindue enzi mpya, aanzishe kazi mpya na kubwa zaidi, na ni sharti alete majina mapya na kazi mpya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 44)

“Yehova” ni jina Nililolichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, nalo linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Linamaanisha Mungu anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. “Yesu” ni Imanueli, nalo linamaanisha sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, naye Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, naye Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya mpango wa usimamizi. Yaani, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wateule wa Uyahudi, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa, na Mungu wa Wayahudi wote. Na hivyo, katika enzi ya sasa, Waisraeli wote, isipokuwa Wayahudi, wanamwabudu Yehova. Wanamtolea kafara kwa madhabahu, na kumtumikia wakiwa wamevalia mavazi ya kikuhani katika hekalu. Wanachotumainia ni kuonekana tena kwa Yehova. Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu. Yeye ni sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Yaani, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema, nalo lilikuwepo kwa ajili ya kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu lilikuwepo ili kuwawezesha watu wa Enzi ya Neema kuzaliwa upya na kuokolewa, nalo ni jina mahsusi la wokovu wa binadamu wote. Kwa hiyo jina Yesu linawakilisha kazi ya ukombozi, nalo linaashiria Enzi ya Neema. Jina Yehova ni jina mahsusi la Wayahudi walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. “Yehova” linawakilisha Enzi ya Sheria, nalo ni jina la heshima kwa Mungu aliyeabudiwa na Wayahudi. “Yesu” linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kuwasili kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anamtarajia Afike katika mfano aliochukua kule Uyahudi, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Ukombozi, nao usingeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, nayo enzi isingekomeshwa. Hiyo ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni kwa ajili ya ukombozi na wokovu wa wanadamu peke yake. Nililichukua jina la Yesu kwa sababu ya watenda dhambi wote katika Enzi ya Neema, nalo si jina ambalo kwalo Nitawaangamiza wanadamu wote. Ingawa Yehova, Yesu, na Masihi yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria tu enzi tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, nayo hayaniwakilishi katika ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza kwa ufasaha tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tofauti tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Na hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina Langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, wala Masihi, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitatamatisha enzi nzima. Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka mwisho wa dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 45)

Mwokozi atakapofika katika siku za mwisho, kama bado angeitwa Yesu, na kuzaliwa mara nyingine katika Uyahudi, na kufanya kazi Yake katika Uyahudi, basi hii ingethibitisha kuwa Niliumba Wayahudi peke yao na kuwakomboa Wayahudi peke yao, na kuwa Sina uhusiano wowote na Mataifa. Je, hii haitakuwa kinyume cha maneno Yangu kwamba “Mimi ni Bwana aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote”? Nilitoka Uyahudi nami Nafanya kazi Yangu kati ya Mataifa kwa sababu Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, ila Mungu wa viumbe vyote. Ninaonekana kati ya Mataifa katika siku za mwisho kwa sababu Mimi si Yehova, Mungu wa Wayahudi tu, lakini, zaidi ya hayo, kwa sababu Mimi ni Muumba wa wateule Wangu wote kati ya Mataifa. Sikuumba Uyahudi, Misri, na Lebanoni pekee, bali pia Niliumba Mataifa yote mbali na Israeli. Na kwa sababu hiyo, Mimi ni Bwana wa viumbe vyote. Nilitumia Uyahudi tu kama hatua ya kwanza ya kazi Yangu, Nikayatumia Uyahudi na Galilaya kama ngome za kazi Yangu ya ukombozi, nami Natumia Mataifa kama msingi ambao Nitatumia kuikamilisha enzi nzima. Nilifanya hatua mbili za kazi katika Uyahudi (hatua mbili za kazi ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema), nami Nimekuwa Nikitekeleza hatua mbili zaidi za kazi (Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme) katika nchi nyingine zote zaidi ya Uyahudi. Nitafanya kazi ya kushinda kati ya Mataifa, na hivyo kuikamilisha enzi. Mwanadamu akiniita Yesu Kristo kila wakati, lakini hajui kuwa Nimeianza enzi mpya katika siku za mwisho na Nimeanza kazi mpya, na mwanadamu akingoja kwa shauku kuwasili kwa Yesu Mwokozi, basi Nitawaita watu kama hao wale wasioniamini. Wao ni watu ambao hawanijui, na imani yao Kwangu ni ya bandia. Je, watu kama hao wanaweza kushuhudia kufika kwa Yesu Mwokozi kutoka mbinguni? Wanachongoja si kufika Kwangu, bali ni kufika kwa Mfalme wa Wayahudi. Hawatamani maangamizo Yangu ya dunia hii nzee yenye uchafu, lakini badala yake wanatamani kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili, ndipo watakapokombolewa; wanamtazamia Yesu kuwakomboa wanadamu wote mara nyingine kutoka nchi hii iliyochafuliwa na isiyo na haki. Watu kama hao watawezaje kuwa wale wanaoikamilisha kazi Yangu katika siku za mwisho? Matamanio ya mwanadamu hayawezi kufikia mapenzi Yangu ama kutimiza kazi Yangu, kwani mwanadamu hutamani au kuthamini tu kazi ambayo Nimeifanya hapo awali, naye hajui kuwa Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mpya siku zote na si mzee kamwe. Mwanadamu anajua tu kuwa Mimi ni Yehova, na Yesu, naye hana fununu kuwa Mimi ni Mwisho, Yule ambaye Atawaangamiza wanadamu. Mwanadamu anachotamani na kujua tu ni kuhusu dhana yake mwenyewe, nayo ni yale tu ambayo anaweza kuyaona kwa macho yake mwenyewe. Hayako sambamba na kazi Ninayoifanya, bali hayatangamani nayo. Kama kazi Yangu ingefanywa kulingana na mawazo ya mwanadamu, basi ingeisha lini? Mwanadamu angeingia katika pumziko lini? Nami Ningewezaje kuingia katika siku ya saba, Sabato? Nafanya kazi kulingana na mpango Wangu, kulingana na lengo Langu, na sio kulingana na nia ya mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Iliyotangulia: Utangulizi

Inayofuata: Kazi na Kuonekana kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp