71 Ee Mpendwa Wangu, Nakutafuta Wewe

I

Uko wapi, mpendwa wangu?

Unajua jinsi nakukosa Wewe?

Bila mwanga, siku ni ngumu, zimejawa na uchungu.

Katika giza, nakutafuta Wewe.

Sikati tamaa, sipotezi tumaini,

lakini nakutafuta kwa bidii zaidi.

Nangoja kwa hamu kurudi Kwako,

ambapo macho yangu yataona uso wako.

Mungu, mpendwa wangu, mzuri zaidi,

Wewe ni kama mwezi kipaji.

Mungu, mpendwa wangu, Unauvutia moyo wangu.

Sina mpenzi mwingine ila Wewe.

Moyo wangu ni mali Yako.

II

Umenisikia nikikuita,

ukibisha kwenye mlango wa moyo wangu.

Nimesikia sauti Yako na nikafungua mlango,

Ninakaribisha kurudi Kwako.

Matumaini yangu ya miaka mingi yamekuja kuwa,

machozi yamechanganywa na furaha kubwa.

Unaleta ukweli kati ya watu,

Nimeona mwangaza wa kweli ukitokeza.

Mungu, mpendwa wangu, mzuri zaidi,

Wewe ni kama mwezi kipaji.

Mungu, mpendwa wangu, Unauvutia moyo wangu.

Sina mpenzi mwingine ila Wewe.

Moyo wangu ni mali Yako.

III

Ninaishi katika familia Yako,

nikihudhuria sherehe ya Mwanakondoo.

Kila siku ninafurahia maneno Yako,

moyo wangu una furaha isiyo na kifani.

Uniongoze kwa mkono,

niwezeshe nikimbie mbio nyuma Yako.

Nina kiu ya kuwa karibu sana Nawe,

siku zote pamoja na wewe.

Mungu, mpendwa wangu, mzuri zaidi,

Wewe ni kama mwezi kipaji.

Mungu, mpendwa wangu, Unauvutia moyo wangu.

Sina mpenzi mwingine ila Wewe.

Moyo wangu ni mali Yako.

IV

Kupitia hukumu na kuadibu Kwako,

ninaona utakatifu na haki Yako.

Maneno Yako yamenisafisha

na kuniwezesha kuzaliwa upya.

Wanipa ukweli kuwa maisha yangu,

nimefurahia upendo Wako wa kweli.

Nitakupenda, nitakutumikia,

moyo wangu karibu nawe daima.

Mungu, mpendwa wangu, mzuri zaidi,

Wewe ni kama mwezi kipaji.

Mungu, mpendwa wangu, Unauvutia moyo wangu.

Sina mpenzi mwingine ila Wewe.

Moyo wangu ni mali Yako.

Eh, moyo wangu ni mali Yako.

Iliyotangulia: 70 Nisingekuwa Nimeokolewa na Mungu

Inayofuata: 72 Mpenzi Wangu, Tafadhali Nisubiri

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki