11 Tumenyakuliwa Hadi Mbele ya Kiti cha Enzi

1 Tumenyakuliwa hadi mbele ya kiti cha enzi, na hili limesababishwa kabisa na neema na rehema za Mungu. Watakatifu wameleta upendo wao wa Mungu mbele na kamwe hawakuyumbayumba kutoka kwa njia yao ya kiroho. Kuwa imara katika imani kwamba Mungu mmoja wa kweli Amekuwa mwili, ya kwamba Yeye ndiye Mkuu wa ulimwengu Ambaye hutawala vitu vyote—hii imethibitishwa na Roho Mtakatifu na ni ushahidi thabiti! Kamwe hauwezi kubadilika! Eh, Mwenyezi Mungu! Leo Umefungua macho yetu ya kiroho, kuwaruhusu vipofu kuona, viwete kutembea, wenye ukoma kuponywa. Umefungua dirisha la mbinguni na tumeona siri za dunia ya kiroho. Maneno Yako matakatifu yametujaza sisi, na Umetuokoa kutoka kwa ubinadamu potovu uletwao na Shetani. Hii ni kazi Yako kuu na rehema Yako kubwa sana. Sisi ni mashahidi Wako!

2 Umekuwa mnyenyekevu na kufichika katika kimya kwa muda mrefu. Wewe umepitia ufufuo na mateso ya msalaba; Wewe umejua furaha na huzuni ya maisha ya binadamu pamoja na mateso na dhiki. Wewe umepitia na kuonja maumivu ya dunia ya binadamu, na Wewe umetelekezwa na enzi. Mungu mwenye mwili ni Mungu Mwenyewe. Wewe umetuokoa kutoka kwa lundo la samadi kwa ajili ya mapenzi ya Mungu na umetushikilia kwa mkono Wako wa kulia; neema Yako imepeanwa huru kwetu sisi. Unafanya juhudi za ukarimu kuingiza maisha Yako ndani yetu; gharama Ulilolipa kwa damu Yako, jasho, na machozi imekuwa katika watakatifu. Sisi ndio matokeo ya juhudi Zako zenye bidii, sisi ndio gharama Unayolipa. Eh, Mwenyezi Mungu! Ni kwa sababu ya upendo Wako na rehema, haki Yako na uadhama, utakatifu Wako na unyenyekevu kwamba watu wote wanapaswa kutii mbele Yako na kukuabudu Wewe daima dawamu.

3 Leo Umefanya kamili makanisa yote—kanisa la Filadelfia—ambayo ni matunda ya miaka 6,000 ya mpango Wako wa usimamizi. Sasa watakatifu kwa unyenyekevu wanaweza kuwa watiifu mbele Yako; wao wameunganishwa pamoja katika roho na kuandama pamoja katika upendo. Wao wameunganishwa kwa chanzo cha chemchemi ya maji. Maji ya uhai ya maisha huenda bila mwisho na husafisha na kutakasa uchafu wote na taka katika kanisa, kwa mara nyingine tena yakitakasa hekalu Lako. Tunamruhusu Mungu Atawale katika roho zetu, kutembea naye na kupata uwezo unaozidi sana wa mwanadamu, kushinda ulimwengu, na roho zetu huruka kwa uhuru na kufikia ufunguliwaji; haya ni matokeo ya Mwenyezi Mungu kuwa Mfalme. Shirikiana na Mungu kwa utendaji, tumikia kwa uratibu na kuwa moja, yakidhi mapenzi ya Mwenyezi Mungu, harakisha kuwa mwili mtakatifu wa kiroho, kanyaga Shetani, na kumaliza hatima yake.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 2” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 10 Ufalme wa Mungu Umeonekana Duniani

Inayofuata: 12 Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp