5. Unahitaji Kusadiki Vipi Mungu Ili Kuweza Kuokolewa na Kufanywa Kuwa Mtimilifu?
Maneno Husika ya Mungu:
Kwa ufupi, kuichukua njia ya Petro katika imani ya mtu kunamaanisha kuitembea njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kupata kujijua na kubadilisha tabia yako kwa kweli. Ni kwa kuitembea njia ya Petro tu ndipo mtu atakuwa katika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe jinsi hasa ya kuitembea njia ya Petro, na vilevile jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia na vitu vyote vya mwili wake mwenyewe. Yeye lazima ajitolee kwa moyo wote; yaani, lazima ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, alenge kula na kunywa maneno ya Mungu, azingatie kutafuta ukweli na kutafuta madhumuni ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu. Hii ndiyo mbinu ya msingi na muhimu zaidi ya utendaji. Hilo ndilo alilofanya Petro baada ya kumwona Yesu, na ni kwa kutenda kwa njia hii tu ndio mtu anaweza kufanikisha matokeo bora zaidi. Kujitolea kwa moyo wote kwa maneno ya Mungu kimsingi kunajumuisha kutafuta ukweli, kutafuta nia za Mungu ndani ya maneno Yake, kuzingatia kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na kuelewa na kupata ukweli zaidi kutoka katika maneno ya Mungu. Wakati wa kusoma maneno Yake, Petro hakuwa anazingatia kuelewa mafundisho ya dini, sembuse kuzingatia kwa kiasi kidogo kupata maarifa ya teolojia; badala yake, alitilia maanani kuelewa ukweli na kufahamu mapenzi ya Mungu, na vile vile kutimiza ufahamu wa tabia yake na uzuri wake. Petro pia alijaribu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu kutoka katika maneno ya Mungu, na vile vile asili potovu ya mwanadamu na dosari yake halisi hivyo kufikia vipengele vyote vya matakwa ya Mungu kwa mwanadamu ili kumridhisha Yeye. petro alikuwa na vitendo vingi sahihi vilivyofuata maneno ya Mungu; hili lililingana zaidi na mapenzi ya Mungu, na ni njia bora zaidi ambayo mtu angeshirikiana huku akipitia kazi ya Mungu. Wakati ambapo alipitia mamia ya majaribio kutoka kwa Mungu, Petro alijichunguza kabisa dhidi ya kila neno la hukumu ya Mungu kwa mwanadamu, kila neno la ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu, na kila neno la madai Yake kwa mwanadamu, na akajitahidi kuelewa maana ya maneno hayo. Alijaribu kwa bidii kutafakari na kukariri kila neno ambalo Yesu alimwambia, na alitimiza matokeo mazuri sana. Kupitia namna hii ya utendaji, aliweza kutimiza kujifahamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na hakuja tu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu, lakini pia alikuja kuelewa kiini, asili, na dosari mbalimbali za mwanadamu. Hii ndiyo maana ya kujifahamu kwa kweli. Kutoka kwa maneno ya Mungu, Petro hakutimiza tu kujifahamu kwa kweli, lakini kutokana na mambo yaliyoonyeshwa katika maneno ya Mungu—tabia ya Mungu yenye haki, kile Anacho na alicho, mapenzi ya Mungu kwa kazi Yake, mahitaji Yake kwa wanadamu—kutoka kwa maneno haya alikuja kumjua Mungu kabisa. Alikuja kujua tabia ya Mungu, na asili yake; alikuja kujua na kuelewa kile Mungu anacho na Alicho, na vilevile uzuri wa Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu. Ingawa Mungu hakuzungumza wakati huo sana kama Anavyofanya leo, matokeo katika vipengele hivi, hata havyo yalipatikanana Petro. Hili lilikuwa jambo adimu na la thamani. Petro alipitia mamia ya majaribio, lakini hakuteseka bure. Hakuja kujielewa tu kutokana na maneno na kazi ya Mungu, lakini pia alikuja kumjua Mungu. Aidha, alizingatia hasa matakwa ya Mungu kwa wanadamu ndani ya maneno Yake. Bila kujali ni katika hali gani mwanadamu anapaswa kumridhisha Mungu ili kukubaliana na mapenzi ya Mungu, Petro aliweza kufanya juhudi kubwa katika vipengele hivi na kupata uwazi kamili; hili lilikuwa la manufaa kubwa sana kwa kuingia kwake mwenyewe. Haijalishi kile ambacho Mungu alizungumzia, maadamu maneno hayo yangeweza kuwa maisha yake na yalikuwa ya ukweli, Petro aliweza kuyaweka ndani ya moyo wake kuyatafakari na kuyathamini mara kwa mara. Baada ya kuyasikia maneno ya Yesu, aliweza kuathiriwa nayo, ambalo linaonyesha kuwa alikuwa akizingatia hasa maneno ya Mungu, na alitimiza matokeo mwishowe kwa kweli. Yaani, aliweza kuyatia maneno ya Mungu katika vitendo kwa uhuru, kutenda kwa usahihi ukweli na kukubaliana na mapenzi ya Mungu, kutenda kikamilifu kwa mujibu wa nia ya Mungu, na kuacha maoni na mawazo yake mwenyewe. Kwa njia hii, Petro aliingia katika ukweli wa maneno ya Mungu. Huduma ya Petro ililingana na mapenzi ya Mungu hasa kwa sababu alikuwa amefanya hili.
Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo
Ili kutafuta kufanywa mtimilifu na Mungu, mtu lazima kwanza aelewe maana ya kufanywa mtimilifu na Yeye, ni hali gani ambazo mtu anapaswa kumiliki ili kufanywa mtimilifu, na kisha kutafuta njia ya kutenda mara mtu ameelewa mambo kama hayo. Mtu lazima awe na ubora fulani wa tabia ili afanywe mtimilifu na Mungu. Wengi wenu hawana ubora muhimu wa tabia, ambao unahitaji wewe kulipa gharama fulani na jitihada zako za nafsi. Kadiri ubora wako wa tabia unavyozidi kuwa wa chini, ndivyo lazima utie juhudi zaidi za binafsi. Kadiri ufahamu wako wa maneno ya Mungu ulivyo mkuu na kadiri unavyoyatia kwenye matendo, ndivyo unavyoweza kuingia kwenye njia ya kufanywa mtimilifu na Mungu haraka. Kupitia katika maombi, unaweza pia kufanywa mtimilifu katika maombi; pia unaweza kufanywa mtimilifu kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, kuelewa kiini cha maneno hayo, na kuishi kwa kudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu, unaweza kufanywa kuwa mtimilifu. Kupitia uzoefu wa maneno ya Mungu kila siku, unapaswa kujua kile unachokosa ndani yako, na, zaidi ya hayo, unapaswa kujua dosari yako kubwa na upungufu wako, na umwombe na kumsihi Mungu. Kwa kufanya hivyo, utafanywa mtimilifu polepole. Njia za kufanywa mtimilifu: kuomba, kula na kunywa maneno ya Mungu, kuelewa kiini cha maneno ya Mungu, kuingia katika uzoefu wa maneno ya Mungu, kuja kujua kinachokosa ndani yako, kuitii kazi ya Mungu, kuzingatia mzigo wa Mungu na kuunyima mwili kwa kupitia upendo wako kwa Mungu, na kuwa na ushirika wa mara kwa mara na ndugu, ambayo yanaboresha uzoefu wako. Iwe ni maisha ya jumuiya au maisha yako binafsi, na iwe ni makusanyiko makubwa au madogo, yote yanaweza kukuwezesha kupata uzoefu na kupata mafunzo ili moyo wako uwe na utulivu mbele ya Mungu na kurudi kwa Mungu. Haya yote ni mchakato wa kufanywa mtimilifu. Kuyapitia maneno ya Mungu ambayo yamesemwa kunamaanisha kuwa na uwezo wa kwa kweli kuyaonja maneno ya Mungu na kuyaruhusu yaweze kuishi kwa kudhihirishwa ndani yako ili uwe na imani kubwa na upendo kwa Mungu. Kupitia njia hii, utaondoa tabia potovu ya kishetani polepole, utaachana na motisha isiyofaa polepole, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kawaida. Kadiri upendo kwa Mungu ndani yako unavyozidi kuwa mkuu—yaani, kadiri unavyozidi kufanywa mtimilifu na Mungu mara nyingi—ndivyo unayopotoshwa na Shetani kwa kiasi kidogo. Kupitia uzoefu wako wa vitendo, utaingia kwenye njia ya kufanywa mtimilifu polepole. Hivyo, ikiwa unataka kufanywa mtimilifu, kuzingatia mapenzi ya Mungu na kuyapitia maneno ya Mungu hasa ni muhimu sana.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu
Kama unaamini katika utawala wa Mungu, basi lazima uamini kuwa mambo ambayo hutokea kila siku, yawe mema au mabaya, si matukio ya kubahatisha. Sio kwamba mtu fulani ni mkali kwako au anakulenga kwa makusudi; yote kwa kweli husafidiwa na kupangwa na Mungu. Kwa nini Mungu hupanga mambo haya? Sio ili kuzifichua kasoro zako au kukukashifu; kukukashifu si lengo la mwisho. Lengo la mwisho ni kukukamilisha na kukuokoa. Mungu anafanyaje hilo? Kwanza, Anakufanya ufahamu tabia yako potovu, kufahamu asili na hali yako, kasoro zako, na kile unachokosa. Ni kwa kuelewa mambo haya yaliyomo katika moyo wako tu ndiyo utaweza kufuatilia ukweli na kuacha tabia yako potovu hatua kwa hatua. Huku ni Mungu kukupa fursa. Lazima ujue jinsi ya kuitumia fursa hii na usiwe mkaidi kwa Mungu. Hasa unapokabiliwa na watu, matukio, na mambo ambayo Mungu anapanga kando yako, usifikiri kila mara kwamba mambo hayako kama unavyotaka yawe, kila mara ukitaka kutoroka, kila mara ukimlaumu na kumwelewa Mungu visivyo. Huko si kuipitia kazi ya Mungu, na hiyo itafanya iwe vigumu sana kwako kuingia katika uhalisi wa ukweli. Lolote lile ambalo huwezi kulielewa kikamilifu, wakati ambapo una matatizo, lazima ujifunze kutii. Unapaswa kwanza kuja mbele ya Mungu na kuomba zaidi. Kwa njia hiyo, kabla ya wewe kujua kutakuwa na mabadiliko katika hali yako ya ndani na utaweza kutafuta ukweli ili kutatua tatizo lako utaweza kuipitia kazi ya Mungu. Katika kipindi hiki, uhalisi wa ukweli unahemshwa ndani yako, na hivi ndivyo jinsi utakavyoendelea mbele na jinsi mabadiliko katika hali ya maisha yako yatafanyika. Utakapokuwa umepitia mabadiliko haya na kuwa na aina hii ya uhalisi wa ukweli, basi utakuwa na kimo, na kimo huleta uzima. Ikiwa mtu huishi daima kulingana na tabia potovu ya Shetani, basi bila kujali ana shauku au bidii kiasi gani, bado hawezi kufikiriwa kuwa na kimo, au uzima. Mungu hufanya kazi ndani ya kila mtu, na bila kujali mbinu Yake ni ipi, ni watu, vitu au masuala ya aina gani ambayo Yeye hutumia kufanya huduma, au maneno Yake yana sauti ya aina gani, Ana lengo moja tu la mwisho: kukuokoa. Kabla ya kukuokoa, Anahitaji kukubadili, hivyo utakosaje kuteseka kidogo? Ni lazima upate kuteseka. Kuteseka huku kunaweza kuhusisha mambo mengi. Wakati mwingine Mungu huwainua watu, mambo, na vitu ambavyo viko karibu nawe ili kwamba uweze kujitambua, vinginevyo unaweza kushughulikiwa moja kwa moja, kukupogolewa, na kufunuliwa. Kama vile tu mtu aliye juu ya meza ya upasuaji–lazima upitie maumivu kiasi kwa ajili ya matokeo mazuri. Kama kila wakati Mungu anapokupogoa na kukushughulikia na kila wakati Anaibua watu, mambo, na vitu, hilo huchochea hisia zako na kukuongezea nguvu, basi kupitia hayo kwa njia hii ni sahihi, na utakuwa na kimo na utaingia katika uhalisi wa ukweli.
Kimetoholewa kutoka katika “Ili Kupata Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo
Katika imani yake kwa Mungu, Petro alitafuta kumridhisha Mungu katika kila kitu, na alitafuta kutii yote yaliyotoka kwa Mungu. Bila malalamiko hata kidogo, aliweza kukubali kuadibu na hukumu, na vile vile usafishaji, dhiki na kuwa bila kitu maishani, yote ambayo hayangeweza kubadilisha upendo wake kwa Mungu. Je, huu haukuwa upendo mkamilifu kwa Mungu? Je, huku hakukuwa ni kutimiza wajibu wa kiumbe wa Mungu? Kuadibu, hukumu, dhiki—una uwezo wa kufikia utii hadi kifo, na hili ndilo linafaa kutimizwa na kiumbe wa Mungu, huu ni usafi wa upendo kwa Mungu. Kama mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki, basi yeye ni kiumbe wa Mungu mwenye sifa inayostahili, na hakuna kitu kinachokidhi mapenzi ya Muumba bora zaidi ya hiki.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea
Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Ni hapo tu ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe ni Mtu Ambaye Amepata Uzima?
Wale ambao hawana utii kwa Mungu hata kidogo, ambao wanalitambua tu jina la Mungu, na wana ufahamu kiasi juu ya mapenzi na wema wa Mungu lakini hawaenendi sawa na hatua za Roho Mtakatifu na hawatii kazi na maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu—watu kama hao wanaishi katikati ya neema ya Mungu, na hawatachukuliwa na kukamilishwa na Mungu. Mungu huwakamilisha watu kupitia utii wao, kupitia kula kwao, kunywa na kufurahia maneno ya Mungu, na kupitia mateso na usafishaji maishani mwao. Ni kupitia tu imani kama hii ndipo tabia za watu zinaweza kubadilika, baada ya hapo tu ndipo wanaweza kuwa na maarifa ya kweli kuhusu Mungu. Kutoridhika na kuishi katikati ya neema za Mungu, kuwa na kiu ya ukweli, na kutafuta ukweli, na kunuia kuchumwa na Mungu—hii ndio maana ya kumtii Mungu katika hali ya utambuzi; hii ndiyo aina ya imani ambayo Mungu anataka.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu