313 Popote Uendapo Nitaambatana na Wewe

1

Nimekupa moyo wangu. Sina mpendwa mwingine ila Wewe.

Upendo wangu Kwako ni kijito cha kina, mpendwa wangu.

Natamani kukufuata Wewe maisha yangu yote, hii ni yamini yangu.

Maneno Yako ya uadhama yamenishinda.

Usafishaji wenye uchungu unauvunja moyo wangu.

Nimeona haki Yako. Najua Unapasa kuchiwa.

Mara nyingi, Wewe hunishughulikia kwa ukali.

Ni baada tu ya machozi mengi, ndiyo najua kwamba Wewe ni mzuri zaidi.

Sitaki kingine ila Wewe.

Niko tayari kuyatoa maisha yangu kukupenda Wewe.

Nitakupenda Wewe mpaka mwisho, mpaka mwisho,

na nitakuwa na Wewe milele.

Hata katika uchungu, hata Shetani ingawa Shetani ananizingira,

sitajuta kukupenda. Hivyo kila nilicho nakupa Wewe.

Popote Uendapo, nitaambatana na Wewe.

Na ninatamani, oo, natamani kuungana na Wewe.

Na ninatamani, natamani kuungana na Wewe.

2

Ni nani asiyeweza kukupenda Wewe? Wewe ndiye Unayependeza zaidi.

Upendo wangu kwako ni wa uaminifu na hakuna kinachoweza kupinga.

Upendo wangu ni mti uliopandwa kwa uthabiti kando ya mto.

Hauogopi wakati wa joto. Katika kiangazi haunyauki.

Nateseka kwa ajili ya upendo wangu Kwako. Sina hofu kuhusu kesho.

Iwe ni upepo au dhoruba ya mvua, navumilia yote kwa ajili Yako.

Nastahimili fedheha ili kuwa shahidi Wako.

Natoa kile nilicho nacho kulipiza upendo Wako mkubwa.

Nitakupenda Wewe mpaka mwisho, mpaka mwisho,

na nitakuwa na Wewe milele.

Hata katika uchungu, hata Shetani ingawa Shetani ananizingira,

sitajuta kukupenda. Hivyo kila nilicho nakupa Wewe.

Popote Uendapo, nitaambatana na Wewe.

Na ninatamani, oo, natamani kuungana na Wewe.

Na ninatamani, natamani kuungana na Wewe.

3

Moyo wangu unachomeka ndani yangu. Natamani kukua haraka zaidi,

kukupenda Wewe kwa usafi zaidi na kukupa Wewe kila kitu changu.

Nalia kwa uchungu na kuomba. Siwezi kuvumilia kukuangusha.

Lazima nitume dosari zangu na kuungana na Wewe kataika karamu.

Jinsi gani natamani kukuona, nisiwe mbali nawe tena.

Wakati wa uchungu usioweza kusemwa, nina maneno Yako kunifariji.

Kashfa na kukataliwa, niko tayari kuvumilia vyote hivyo.

Fikira kukuhusu imeuwasha upendo wangu.

Unaweza kuusikia katika sauti ya kuomba.

Hata katika uchungu, hata Shetani ingawa Shetani ananizingira,

sitajuta kukupenda. Hivyo kila nilicho nakupa Wewe.

Popote Uendapo, nitaambatana na Wewe.

Na ninatamani, oo, natamani kuungana na Wewe.

Na ninatamani, natamani kuungana na Wewe.

Natamani kuungana na Wewe.

Iliyotangulia: 312 Kumtamani Mungu

Inayofuata: 314 Nampenda Mungu Sana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki